Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel Catalog



Channel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1806 | 1807 | (Page 1808) | 1809 | 1810 | .... | 3272 | newer

  0 0


  Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Ushauri ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Bw. George Daniel Yambesi (kulia) alipoitambulisha rasmi bodi hiyo jana Jijini Dar es Salaam.
  Wajumbe wakimsikiliza Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo katika picha) jana Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiwatambulisha wajumbe wapya wa bodi ya ushauri waTaasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).
  Wajumbe wakimsikiliza Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo katika picha) jana Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiwatambulisha wajumbe wapya wa bodi ya ushauri waTaasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).
  Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wapya wa wa bodi ya ushauri waTaasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa). (Picha na Lorietha Laurence-WHUSM).

  0 0

  Na Lorietha Laurence -WHSUM.

  Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ameunda kamati ya wajumbe 10 kwa ajili ya kufuatilia undani wa kutopatikana kwa faida kati ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na kampuni ya Star Times kutoka China.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam alisema kuwa kamati hiyo imepewa siku saba kuhakikisha inakuja na taarifa kamili kuhusiana na suala hilo.

  “ nimeipa kamati hii muda wa siku saba ukimalizika siiongezi tena nitatoa labda siku moja mbili kumalizia tu ili inipatie majibu kamili kwa nini kwa miaka yote hiyo hakuna faida”alisema Mwakyembe.

  Aidha Dkt. Mwakyemba anaeleza kuwa uamuzi wa kuunda kamati hiyo ni kutokana na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuonyesha kukerwa na kutokupatikana kwa faida kwenye ushirikiano huo wa TBC na Star Times alipofanya ziara yake mwezi Mei mwaka huu.

  Anazidi kufafanua kuwa Rais alikasirishwa na kitendo cha kampuni hiyo kufanya kazi nchini kwa kipindi cha miaka saba bila faida yoyote na hivyo kuagiza hatua stahiki kuchukuliwa juu ya suala hilo.

  Dkt. Mwakyembe anabainisha kuwa tangu kutolewa kwa kauli ya Rais Mhe. Dkt. Magufuli Wizara na watendaji wake tayari wameshafanya mikutano miwili mmoja Mjini Dodoma na mwingine Jijini Dar es Salaam wakajadili kwa kina sababu zinazopelekea kushindwa kupatikana kwa faida.

  Kabla ya mkutano na waandishi wa habari ,Waziri Dkt. Mwakyembe alitumia takribani saa tatu akijadiliana kwa kina na Mwenyekiti wa Kampuni ya Star Times kutokea nchini China, Xinxing Pang pamoja na wafanyakazi wa wizara akiwamo Katibu Mkuu Profesa Elisante Ole Gabriel na Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt.Hassan Abbas.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Star Times Bw. Xinxing Pang alisema kuwa ana imani kuna uwezekano wa kumalizwa kwa suala hilo kwa kutumia wataalamu wake watakaoangalia sababu za kutokupatikana kwa faida na nini kifanyike katika kuondokana na changamoto hiyo.
  Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiongea na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Katibu Mkuu kutoka Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel na kulia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Star Times Bw. Xinxing Pang.
  Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo katika picha) alipokuwa akieleza msimamo wa Serikali kuhusiana na Kampuni ya Star Times jana Jijini Dar es Salaam. (Picha na Lorietha Laurence.)

  0 0

  CHAMA cha riadha Mkoa wa Singida kimeshauriwa kuangalia uwezekano wa kuzitafutia ufumbuzi baadhi ya changamoto zinazochangia idadi kubwa ya wanawake kutopenda na kisha kutoshiriki kabisa katika mchezo wa riadha.

  Akitoa ushauri huo kwenye viwanja vya michezo vya shule ya msingi Tambukareli,wilayani Manyoni,Mkoani Singida,mmoja wa washiriki wa mashindano hayo,Hamida Nasoro alisisitiza kuwa kutokana na idadi kubwa ya wanawake kutohamasishwa kushiriki katika mashsindano hayo,ndiko kulikochangia mashindano ya mchezo huo wa riadha kuwa na idadi ndogo ya washirki.

  “Mashindano haya tumeonekana wanawake wachache sana labda ni kwa ajili ya changamoto mbali mbali ikiwemo wanawake wengi kutopenda kujishirikisha katika mchezo wa riadha kunakotokana na ukuaji wao wa umri”alisisitiza Hamida.

  Akizungumza na kituo hiki,Hamida hata hivyo hakusita pia kutoa tahadhari kwa wanawake wanaopenda kushiriki katika mchezo huo wa riadha wasijihusishe katika mahusiano ya kimapenzi kwani endapo wataendelea kufanya hivyo,ndoto zao za mafanikio katika mchezo huo zitapotea.
  Hata hivyo Hamida alitumia fursa ya mashindano hayo kuwashauri wanawake wasiopenda kushiriki mchezo huo wajenge utamaduni wa kupenda kushiriki mchezo huo ili waweze kulitangaza soko la mchezo huo kwa wanawake.
  Baadhi ya washiriki wa mashindano ya mchezo wa riadha wa Mkoa wa Singida walioshiriki mashindano hayo yaliyofanyika katika viwanja vya michezo vya shule ya msingi Tambukareli,wilayani hapa.
  Mwanamke mwenye umri wa miaka 48,Zainabu Ramaddhani kutoka wilaya ya Ikungi akishiriki mbio za umbali wa kilomita 21 katika mashindano hayo na kufanikiwa kuchaguliwa kwenda kushiriki mashindano ya kimkoa.(Picha zote Na Jumbe Ismailly).


  0 0


  NA K-VIS BLOG, DODOMA

  NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi, Mhe. Selemani Jafo amejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia Mpango wa uchangiaji wa Hiari, (PSS) na kuhimiza na kjtoa wito kwa waajiri wote nchini kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao katika mifuko ya hifadhi ya jamii kwa wakati kama sheria inavyowataka ili kuepuka usumbufu kwa wanachama wakati wa kupata Mafao yao wanapostaafu. 

  Mhe. Jafo aliyasema hayo wakati akifungua semina ya mafunzo kwa wastaafu watarajiwa mkoani Dodoma Julai 14, 2017.Semina hiyo imelenga kuwajengea uwezo wastaafu hao watajiwa ili kuweza kufanya shughuli za ujasiriamali wakati muda wao wa utumishi wa umma utakapokoma.

  Mhe. Jafo amewanyooshe kidole waajiri wenye tabia ya kutopeleka michango ya wanachama katika mifuko yao kitendo ambacho kinasababisha kero kubwa pindi watumishi hao wanapostaafu na kuanza kuhangaikia Mafao yao kutokana na taarifa za uwasilishaji michango katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kutokamilika.

  “Nitoe rai kwa ndugu zangu watumishi wa umma ambao katika kipindi cha miaka miwili ijayo mtaondoka kwenye utumishi wa umma, yatumieni vema mafunzo haya ili mtakapopata mafao yenu basi tayari mtakuwa na nyenzo ya kuwasaidia kutumia vema fedha mtakazopata kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo, lakini pia kilimo na ufugaji wa kisasa na hatimaye kuyafanya maisha yenu kuwa bora baada ya utumishi wa umma.” Aiasa Mhe. Jafo.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akikabidhiwa fomu ya kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia Mpango wa uchangiaji wa Hiari, (PSS), kutoka kwa Mfkurugenzi wa Uendeshaji, Bi. Neema Muro, (kulia), baada ya kufungua semina ya Mafunzo kwa wastaafu watarajiwa mkoni Dodoma Julai 14, 2017.
  Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, akitoa hotuba yake. "Mfuko umetenga kiasi cha shilingui Bilioni 1.3 kwa ajili ya kulipa mafao watumishi 9,552 wanaotarajiwa kustaafu kati ya mwaka huu wa 2017/2018."
  Naibu Waziri Jafo akitoa hotuba yake.
  Washiriki wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo.


  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akitoa hotuba yake mbele ya maafisa wa Magereza pamoja na watendaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, katika Ukumbi wa Magereza Karanga, Mjini Kilimanjaro Mkoani Kilimanjaro, Julai 14, 2017. Waziri Mhagama alifanya ziara ya kutembelea na kukagua eneo la Mradi wa Ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za ngozi cha karanga kilichopo mkoni Kilimanjaro ambacho kipo chini ya Mfuko wa Pesheni wa PPF kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza nchini. Kiwanda hicho kilikuwa kinazalisha viatu 150 kwa siku na sasa kinatarajiwa kufikia viatu 400 baada ya kukamilika kwa ukarabati.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwira, Katibu mkuu Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji, Prof. Adof Mkenda pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt, Juma Malewa wakiangalia sehemu ya Bidhaa za Ngozi zinazotengenezwa katika Kiwanda cha Viatu cha Magereza Karanga, Mkoani Kilimanjaro, Julai 14, 2017. 
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akichukuliwa kipimo cha mguu kwa ajili ya kutengenezewa Viatu vinavyotengenezwa katika Kiwanda cha Viatu cha Magereza Karanga, Mkoani Kilimanjaro, Julai 14, 2017. 
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakiangalia moja ya mashine za kutengeneza viatu, katika Kiwanda cha Viatu cha Magereza Karanga, Mkoani Kilimanjaro, Julai 14, 2017. Wengine ni Kamishna wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro, Hassan Bakari Mkwiche pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio akitoa taarifa fupi ya uwekezaji uliofanywa na mfuko huo kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza katika ukarabati wa kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Magereza Karanga kilichopo Mkoni Kilimanjaro.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0
 • 07/15/17--05:13: INTRODUCING "ZUZU" BY SAMIR

 • 0 0


  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ajikuta akikesha ofisini kwake pamoja na wananchi takriban 189 wenye Matatizo na Kero za ardhi.

  Mhe. Waziri ametumia takriban saa 20 kusikiliza kero za wananchi ambao waligoma kuondoka ofisini kwake hadi kero zao zitakapopatiwa ufumbuzi. Kazi hiyo ilianza majira ya saa 2 asubuhi hadi saa 9 usiku.

  Hata hivyo wananchi walilazimika kulala Wizarani wakisubiri kuonana na Waziri kutokana na uwepo wa idadi kubwa ya wananchi hao.

  Wananachi wengi wenye matatizo na Kero za ardhi kutoka maeneo ya Bagamoyo, Kibaha, Mkuranga, Kibiti na Dar es salaam kwa ujumla wametumia fursa hii ya kipekee ya kuonana na Waziri mwenye dhamana ya Ardhi na kumuelezea kero zao na hatimaye kupatiwa ufumbuzi papo hapo.

  Wananchi hao wamesifu hatua hii ya Waziri Lukuvi kukutana nao ana kwa ana na kuzitatua kero zao za ardhi kwa kuwa haijawahi kutokea. Nae Bwana Francis Kamara mkazi wa Ilala jijini Dar es salaam amemuomba Waziri aweze kuwaajibisha watumishi ambao wanakwamisha jitihada zake hadi kupelekea yeye kukutana na wananchi moja kwa moja.

  Mwanzoni mwa mwezi Juni 2017 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi alitoa Tangazo la kuwataka wakazi wa kanda ya Dar es Salaam na Pwani ambao wangependa kumuona, wafike katika ofisi yake ya kanda ya Dar es Salaam iliyopo ghorofa ya pili, jengo la Wizara ya Ardhi – Magogoni, Kivukoni ili kujiandikisha majina yao, anuani na namba zao za simu.

  Aidha, Mhe. Waziri atafanya ziara kama hii katika kanda nyingine mara baada ya kukamilisha zoezi hilo katika Kanda ya Dar es Salaam na Pwani.
  Baadhi ya wananchi wa Pwani na Dar es Salaam wakiwa ofisi za Wizara ya ardhi mida ya saa 9 usiku kusubiri kusikilizwa kero zao za ardhi na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi akitatua kero za ardhi za wananchi wa Pwani na Dar es Salaam waliofika ofisini kwake.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi akitatua kero za ardhi za wananchi wa Pwani na Dar es Salaam waliofika ofisini kwake.
  Mkazi wa Goba jijini Dar es salaam Bibi Fatuma Shami akipata ufafanuzi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi kuhusu eneo lake kuvamiwa na kupata miliki pandikizi.
  Mkazi wa Kibaha Mkoa wa Pwani Bibi Mariam Hamis akipata ufafanuzi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi kuhusu eneo lake lililo na Mgogoro.
  Baadhi ya wananchi kutoka Wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani wakimueleza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi kuhusu mgogoro wao wa ardhi katika ofisi za Wizara ya ardhi.
  Watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wa Kanda ya Dare s salaam na Pwani waliokesha na Waziri Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi wakati wa kutatua migogoro ya ardhi kutoka kwa wananchi.


  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimuangalia mhamiaji haramu katika dirisha dogo la chumba cha mahabusu, Kituo cha Polisi Pangani mkoani Tanga. Mhamiaji huyo kutoka nchini Somalia alikamatwa wilayani Pangani katika mwambao wa Bahari ya Hindi. Masauni akiwa mjini Tanga aliwaagiza Maafisa Uhamiaji na Polisi kuongeza kasi ya kutafuta mizizi ya wahamiaji haramu mkoani humo. Kulia ni Mkuu wa Kituo Polisi mjini Pangani, Christina Musyani. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Pangani, mkoani Tanga, Christina Musyani wakati alipokua anamfafanulia masuala ya ulinzi na usalama wilayani humo. Masauni alikikagua kituo hicho pamoja na nyumba za askari polisi ambazo zipo katika hali mbaya zaidi kutokana na kutofanyiwa matengenezo kwa muda mrefu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia) akimsikiliza Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Pangani, mkoani Tanga, Christina Musyani alipokuwa anamuonyesha moja ya nyumba ambazo zipo katika hali mbaya zaidi kutokana na kutofanyiwa matengenezo kwa muda mrefu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akitoka kulikagua Gereza la Wilaya ya Pangani mkoani Tanga. Masauni pia alizungumza na mahabusu wa Gereza hilo kwa kusikiliza kero zao na kuzitolea maamuzi hapo hapo na baadhi kuahidi kuzifanyia kazi kwa haraka zaidi. Kwa nyuma ni Mkuu wa Gereza hilo, Elishinikizo Moshi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea na kufanya ukaguzi katika eneo la mradi wa ujenzi wa gati kwenye Manispaa ya Lindi na kusema kwamba ameridhishwa na utekelezaji wake.

  Pia amewaagiza viongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) mkoa wa Lindi kujenga eneo la kupumzikia abiria kwenye maegesho ya kivuko katika maeneo ya Lindi na Kitunda ili wananchi wa maeneo ya Lindi na Kitunda waanze kupata huduma ya kivuko.

  Waziri Mkuu alitembelea mradi huo jana (Ijumaa, Julai 14, 2017) wakati alipotembelea eneo hilo kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa gati hilo, akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Lindi.

  Alisisitiza kuwa Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuondoa kero ya usafiri kwa wakazi wa maeneo hayo, hivyo ujenzi wa gati hilo uende kwa kasi huku ukizingatia matakwa ya kiufundi na ubora wa hali ya juu.

  “Jengeni sehemu ya kupumzikia abiria katika pande zote mbili, upande wa Lindi na wa Kitunda. Mbali na abiria kupata eneo la kupumzikia pia itarahisisha hata ukataji wa tiketi jambo litakawarahisishia ukusanyaji wa mapato.”

  Pia Waziri Mkuu aliwaomba wananchi waendelee kuiamini na kushirikiana na Serikali katika shughuli mbalimbali za maendeleo na kwamba ahadi zote zilizoahidiwa katika Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) zitatekelezwa.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi kuyafanyia maboresho maeneo ya pwani na kuwa ya kisasa kwa kuondoa majengo yote chakavu ili wananchi waweze kuyatumia kwa ajili ya kupumzikia.

  Alisema ni vema kwa manispaa hiyo kuainisha majengo yote ya zamani yaliyoko katika upande wa pwani yanayotakiwa kuhifadhiwa kwa ajili ya makumbusho ili yaweze kukarabatiwa na yaliyosalia yaondolewe.

  Pia Waziri Mkuu alitembelea chuo cha Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) mkoa wa Lindi na kusema kwamba ameridhishwa na utoaji wa elimu chuoni hapo na kuwaagiza viongozi waanzishe mafunzo ya mafuta na gesi ili vijana waweze kupata ujuzi na kuajiriwa kwenye sekta hiyo

  0 0

   Dkt.Hassan Abbasi


  0 0

   Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, akiwasili uwanja wa ndege kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, akitokea Nairobi nchini Kenya kuhudhuria hafla ya ufungaji wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kukabiliana na matishio ya kigaidi na uhalifu mwingine unaovuka mipaka Majeshi ya Polisi ambao ni wanachama wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kwa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO), kushoto ni kamishna wa Polisi Jamii nchini (CP) Mussa Ali Mussa. Picha na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi
   Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro,  akizungumza na Kaimu kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Lucas Mkondya (wa kwanza kushoto), muda mfupi alipowasili nchini akitokea Nairobi nchini Kenya kuhudhuria hafla ya ufungaji wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kukabiliana na matishio ya kigaidi na uhalifu mwingine unaovuka mipaka Majeshi ya Polisi ambao ni wanachama wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kwa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO), kulia ni Kamishna wa Polisi Jamii nchini (CP) Mussa Ali Mussa. Picha na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi

  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro(wa kwanza kulia),akitafakari jambo baada ya kuwasili nchini akitokea Nairobi nchini Kenya kuhudhuria hafla ya ufungaji wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kukabiliana na matishio ya kigaidi na uhalifu mwingine unaovuka mipaka Majeshi ya Polisi ambao ni wanachama wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kwa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO), anayefuata ni Kamishna wa Polisi Jamii nchini (CP) Mussa Ali Mussa na Kaimu kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam (DCP) Lucas Mkondya
   Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya makamanda na washiriki kutoka Majeshi ya Polisi ambao ni wanachama wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kwa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO),  waliohudhuria mafunzo ya kukabiliana na matishio ya kigaidi na uhalifu mwingine unaovuka mipaka, mafunzo yaliyofanyika katika chuo cha Jeshi la Ulinzi la Kenya kilichopo katika eneo la Embakasi, jijini Nairobi
  Baaadhi ya vikosi vya Jeshi la Polisi kutoka nchi wanachama wa Shirikisho la Wakuu kwa Polisi wa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO), walioshiriki katika mafunzo ya kujengewa uwezo wa kukabiliana na matishio ya kigaidi na uhalifu mwingine unaovuka mipaka, mafunzo yaliyofanyika katika chuo cha Jeshi la Ulinzi la Kenya kilichopo katika eneo la Embakasi, jijini Nairobi. 

  0 0


  0 0
 • 07/15/17--07:30: TAARIFA KWA UMMA
 • JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
  IDARA YA UHAMIAJI
       


  KUISHA KWA MUDA WA ZOEZI LA UHAKIKI WA VIBALI VYA UKAAZI KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI (e-VERIFICATION)

  Idara ya Uhamiaji inapenda kuwakumbusha Waajiri, Wakurugenzi wa Makampuni, Taasisi mbalimbali na Wageni wote kuhakikisha wamehakiki vibali vyao kupitia Mfumo wa Uhakiki ambao unapatikana kupitia Tovuti ya Idara ya www.immigration.go.tzkabla ya zoezi la uhakiki kuisha tarehe 19/07/2017.

  Kwa wale ambao kumbukumbu za vibali vyao hazitaonekana katika mfumo wa uhakiki au kuwa na tatizo lolote wanashauriwa kuripoti katika Ofisi za Uhamiaji za Mikoa au kwa Mamlaka husika ndani ya muda uliotolewa.

  Baada ya kuisha kwa muda uliotolewa, Idara itafanya ukaguzi nchi nzima na kuwachukulia hatua za kisheria Wageni binafsi, Waajiri, Wakurugenzi wa Makampuni na Taasisi mbalimbali ambazo wageni wao watabainika kuwa na vibali vya kughushi au vilivyopatikana nje ya utaratibu wa utoaji vibali.

  Idara ya Uhamiaji ilitoa muda wa siku 90 kwa wale wote wenye vibali vya ukaazi kuhakiki vibali vyao; tangu tarehe ya kuzindua mfumo huo tarehe 19 Aprili, 2017.

  Imetolewa na;
  KITENGO CHA UHUSIANO,
  MAKAO MAKUU, IDARA YA UHAMIAJI,



  14 JULAI, 2017.

  0 0

   Mwanafunzi Francis Thomas aliyemaliza kidato cha Sita katika shule ya Wavulana ya Feza akiwa amebebwa juu na wanafunzi wenzie wa shule hiyo mara baada ya kuibuka Mwanafunzi bora kitaifa katika Masomo ya Arts na Biashara katika matokeo yaliyotangazwa na baraza la mitihani leo

    Mwanafunzi Francis Thomas aliyemaliza kidato cha Sita katika shule ya Wavulana ya Feza  akiwa katika picha ya pamoja na Wazazi wake Thomas Samky na Victoria Samky walipofika shuleni hapo
   Wanafunzi waliofanya vizuri na kuwamo katika 10 bora ya wasichana waliofanya vizuri kitaifa ,Kabhabhira Bukuru na Atuganile Cairo  wakiwa katika picha ya pamoja wenye furaha mara baada ya kuwasili shule ya Wasichana Feza mara baada ya matokeo kutoka ambapo Atganile amekuwa wa tatu kitaifa katika Masomo ya Sayansi na Kabhabhira amekuwa wa Saba katika masomo hayo.
   Wanafunzi waliofanya vizuri na kuwamo katika 10 bora ya wasichana waliofanya vizuri kitaifa Kabhabhira Bukuru na Atuganile Cairo wakilakiwa na walimu wao mara baada ya kuwasili shule ya Wasichana feza walipokuwa wanasoma mara baada ya matokeo ya kidato cha Sita kutoka
   Mwanafunzi aliyefanya vizuri na kuwa wa tatu  katika 10 bora ya wasichana waliofanya vizuri kitaifa ,  Atuganile Cairo akiwa na Mama yake Mzazi  akimpongeza kwa kufanya vizuri katika mtihani huo wa kidato cha Sita

   Wanafunzi waliofanya vizuri na kuwamo katika 10 bora ya wasichana waliofanya vizuri kitaifa Kabhabhira Bukuru na Atuganile Cairo  wakisalimiana na Mwalimu mkuu wa Shule ya Wasichana fedha ,Ibrahim Rashid pamoja na baba yake Atuganile, Jimmy Cairo

  0 0

   Wachezaji wa JKT NA Mabibo  wakipena mikono katika mchezo wa Ligi ya mchezo wa Kikapu mkoa wa Dar es Salaam RBA katika uwanja wa Gymkhana Dar es Salaam
   Mchezaji wa Mabibo akijaribu kutupa mpira nje ya D katika mchezo wao wa Ligi ya Mchezo wa Kikapu iliyofanyika ya mkoa wa Dar es Salaam RBA iliyofanyika katika uwanja wa Gymkhana Dar es Salaam
   Mchezaji wa timu ya JKT akitupa mpira nje ya D katika mchezo wao wa Ligi ya Mchezo wa Kikapu iliyofanyika ya mkoa wa Dar es Salaam RBA iliyofanyika katika uwanja wa Gymkhana Dar es Salaam
   Mchezaji wa JKT na Mabibo wakiwania mpira katika mchezo wao wa Ligi ya Mchezo wa Kikapu iliyofanyika ya mkoa wa Dar es Salaam RBA iliyofanyika katika uwanja wa Gymkhana Dar es Salaam
   Mchezo wa Mabibo akijaribu kuwatoka wachezaji wa JKT katika  mchezo wao wa Ligi ya Mchezo wa Kikapu iliyofanyika ya mkoa wa Dar es Salaam RBA iliyofanyika katika uwanja wa Gymkhana Dar es Salaam
    Mchezo wa Mabibo kijaribu kutupa mpira nje ya D katika mchezo wao wa Ligi ya Mchezo wa Kikapu iliyofanyika ya mkoa wa Dar es Salaam RBA iliyofanyika katika uwanja wa Gymkhana Dar es Salaam
   Mchezaji wa JKT akipiga  Danki kwenye ngome ya Mabibo k katika mchezo wao wa Ligi ya Mchezo wa Kikapu iliyofanyika ya mkoa wa Dar es Salaam RBA iliyofanyika katika uwanja wa Gymkhana Dar es Salaam




  0 0

   Rais wa Samsung Africa ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Bw. Yoo Young Kim akizungumza na wasambazaji pamoja na wadau mbalimbli juu ya mchango wao endelevu na akitumaini maendeleo bora ya kibiashara kwa siku za usoni katika hafla iliyo fanyika jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Samsung Africa Mashariki, Bw. John Park (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi mtendaji wa kampuni Pyramid consumers, Bw. Abraham Okora cheti cha kumtambulisha rasmi kama msambazaji wa bidhaa za majumbani za samsung Tanzania
   Meneja wa Samsung nchini Tanzania,Rayton Kwembe akifafanua mbele ya wadau mambo mbalimbali ya vifaa vya kampuni hiyo.
  Kikundi cha Safari Theatre kikitoa burudanza katika hafla hiyo.
  Picha na Emmanuel Massaka  
     

  0 0

  BODI ya Usajili wa Wakandarasi Nchini (CRB), imewatahadharisha wananchi, watu  wenye miradi ya ujenzi pamoja na wakandarasi nchini kuwa makini na watu wanaotumia jina la bodi hiyo na kufanya utapeli.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msajili wa bodi hiyo, Rhoben Nkori, bodi imewataka wananchi na wakandarasi wawe wanatoa taarifa katika ofisi za bodi za Makao Makuu Dar es Salaam na Kanda zake ili kuwakamata na kuwafikisha mahahani watu wa aina hiyo.

  “CRB ina ofisi za kanda ambazo zinafanya kazi nchi nzima, kanda hizo ni Kanda ya mashariki – Dar es salaam, Kanda ya kaskazini  Arusha, Kanda ya kusini Mbeya,  Kanda ya ziwa Mwanza

  na Kanda ya kati  Dodoma, watumie ofisi hizi wasirubuniwe na matapeli,” alisema Nkori.

  Aidha, alisema watumishi wa CRB wamekuwa wakienda kwenye ukaguzi wakiwa na vitambulisho vya bodi hiyo na vizibao vyenye nembo ya CRB vinayowatambulisha kuwa wanatoka bodi hiyo.

  Alisema kuna watu ambao wamekuwa wakijiita wawakilishi wa Bodi hiyo na kufanya shughuli za bodi hiyo kwa njia ya utapeli na kuchukua rushwa kwa wakandarasi na wenye miradi.

  Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa jana na  CRB, watu hao wamekuwa wakijitambumbulisha kama wawakilishi wa bodi hiyo ambao huwa wanakwenda kukagua miradi mbalimbali ya ujenzi maeneo mbalimbali.

  Alisema watu hao hutembelea sehemu zenye miradi na kuwatisha watu wanaofanya shughuli za ujenzi na kuwaomba rushwa ili wasiwashtaki wanapobaini kasoro kwenye miradi yao.

  Aidha, alisema watu hao wamekuwa wakiwaandikia barua watu wenye miradi ya ujenzi wajieleze kwanini wasichukuliwe hatua na bodi kwa kufanyakazi zao bila kuzingatia masharti ya ujenzi kama vile kuweka vibao vya kuonyesha mkandarasi anayejenga.

  “Sisi CRB hatuwatambui watu hao na tunawaomba wananchi na watu wenye miradi ya ujenzi wawe makini na wakiwa na tatizo waende kwenye ofisi za kanda zetu ambazo tumezitaja kama kuna watu anahisi wanataka kumtapeli awasiliane na bodi ili tumkamate na kumfikisha mahakamani,” alisema

  Gazeti hili lilifanikiwa kupata nakala ya barua yenye nembo ya CRB iliyoandikwa na mmoja wa matapeli hao kwenda kwa mmoja wa wateja akidai kutaka ufafanuzi wa baadhi ya mambo kwenye mradi wake wa ujenzi unaoendelea.

   Kwenye barua hiyo kwenda kwa mteja tapeli huyo  aliandika hivi “ I need the following drawings, architectural drawing, structural drawing and Building permit and sign board.

  “Hapo anamaanisha kuwa mteja huyo amuonyeshe mchoro wa jengo, kibali cha ujenzi na kibao ambacho kisheria kinapaswa kuwekwa sehemu ya ujenzi kikionyesha jina la mteja, mkandarasi, mhandisi mshauri na  mkandarasi”alisema

  0 0

  Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Lucy Mayenga jana alikabidhi gari la wagonjwa Mkuu wa wilaya Shinyanga mjini Mhe. Josephine Matiro  katika sherehe fupi iliyofanyika mjini humo. Sambamba na gari hilo pia Mhe. Mayenga alitoa Shilingi  milioni 17 ambapo milioni 15 ni  mchango wake wa ujenzi wa chumba cha upasuaji na milioni mbili  kwa ajili ya kifaa cha maabara katika kituo cha Afya cha Kambarage.
   Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Lucy Mayenga akionesha funguo la gari la wagonjwa kabla ya kuikabidhi kwa Mkuu wa wilaya Shinyanga mjini Mhe. Josephine Matiro (kulia)  katika sherehe fupi iliyofanyika mjini humo
    Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Lucy Mayenga akisindikizwa kwa nderemo na wananchi waliojawa na furaha baada ya kukabidhi gari la wagonjwa  kwa Mkuu wa wilaya Shinyanga mjini Mhe. Josephine Matiro (kulia)  katika sherehe fupi iliyofanyika mjini humo
  La wagonjwa ambalo   Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Lucy Mayenga amemkabidhi  Mkuu wa wilaya Shinyanga mjini Mhe. Josephine Matiro.

  0 0

  SHINDANO la ngoma za utamaduni liitwalo ‘Mavunde na utamaduni wetu’ limefanyika leo mjini Dodoma likiwa na lengo la kuenzi, kulinda na kuhifadhi utamaduni wa watu wa Dodoma.

  Shindano hilo limeandaliwa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde na lilihusisha vikundi vya ngoma za asili ya Dodoma 7.Vikundi hivyo ni Simba dume, changamoto, Noti mtemi, Neema Yerusalem, Chipukizi, Finga Vikonje na Imani Makulu.

  Akizungumza katika shindano hilo, Mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, amesema uwepo wa shindano hilo ni utekelezaji wa ahadi yake ambayo aliitoa wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu 2015 na kumpongeza Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kuhamishia shughuli za serikali Dodoma, kupiga vita Rushwa na Ubadhirifu na Kulinda Maliasili za Taifa kwa manufaa ya watanzania wote.

  “Tamaduni zetu zilikuwa zimeanza kusahaulika watu hawakuona tena umuhimu wa ngoma za jadi na hii ni kutokana na utandawazi na kuwa watu wa mjini sana tumesahau tumetoka wapi,”amesema Mavunde.
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Anthony Mavunde akizungumza katika Shindano la Mavunde na Utamaduni wetu lililofanyika mjini Dodoma.
  Chifu wa Dodoma mjini Lazaro Chihoma akizungumza katika Shindano la Mavunde na Utamaduni wetu, mjini Dodoma 
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Anthony Mavunde akiwa na viongozi mbalimbali katika Shindano la Mavunde na Utamaduni wetu. 
  Umati wa wakazi wa Dodoma waliohudhuria shindano la Mavunde na Utamaduni wetu.
  Vikundi mbalimbali vya ngoma vilivyoshiriki katika Shindano la Mavunde na Utamaduni wetu.


  0 0

  *Ukubwa: Sqm 1215
  *Kipo Mita 800 kutoka Barabara kubwa iendayo Bagamoyo
  *Kiwanja kimepimwa, kina hati na Kipo katika eneo lililopangwa na kuendelezwa vizuri
  *Bei: Tshs. 40,000,000 (negotiable), na malipo yanaweza kufanywa kwa awamu

  *Mawasiliano: +255 713 576464 (ikiwa haipatikani acha msg ya whatsapp)
  Email: roseodessa@yahoo.com


older | 1 | .... | 1806 | 1807 | (Page 1808) | 1809 | 1810 | .... | 3272 | newer