Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110104 articles
Browse latest View live

TRA YAVIFUNGULIA VITUO VITATU VYA MAFUTA DAR ES SALAAM BAADA KUTIMIZA MASHARTI YA KUFUNGA MASHINE ZA KIELEKTRONIKI

$
0
0
Na Kajunason Blog/Cathbert Kajuna. 
 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imevifungulia vituo vya mafuta vipatavyo vitatu jijini Dar es Salaam baada ya kutimiza masharti ya kufunga mashine za kielekitroniki zinazotoa risiti moja kwa moja kutoka kwenye pampu ya mafuta (Automatic EFD).
 Akizungumza mara baada ya kufungua vituo hivyo, Kamishina wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere amewashukuru wamiliki wa vituo hivyo kwa kuonyesha ushirikiano kwa serikali kwa kutimiza masharti waliyopewa ya kufunga mashine hizo na kusisitiza kuwa hakuna kituo kitakachofunguliwa kama hakitatimiza masharti. 
 "Niwaombe wamiliki wa vituo vilivyofungiwa kuwa kwa sasa hakuna kitakachofunguliwa bila kutimiza mashart, timiza masharti tuje tukague na tukufungulie uanze biashara yako," amesema Kamishna Kichere. Amesema vituo vilivyofunguliwa leo ni GBP kilichopo eneo la Majumba Sita, Simba Oil kilichopo eneo la Sitakishari, Ukonga na PETRO kilichopo eneo la Kigamboni. 
 "Kitendo cha kuunganisha mashine hizi na pampu za mafuta ni cha muda mfupi sana na wala hakichukui muda mrefu, angalia huyu tulimfungia siku ya jumanne tarehe 11 Julai na leo Ijumaa Julai 14 ameshafunga mashine na anaanza kufanya biashara bila kugombana na serikali;" amesema Kamishna Kichere. Mpaka sasa vituo zaidi ya 40 vimefungiwa nchi nzima ikiwemo jijini Dar es Salaam kwa kosa la kushindwa kufunga mashine za kielekitroniki zinazotoa risiti moja kwa moja kutoka kwenye pampu ya mafuta (Automatic EFD). 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere akikata utepe katika kituo cha mafuta cha Kigamboni jijini Dar es Salaam baada ya kutimiza masharti ya kufunga mashine za kielekitroniki zinazotoa risiti moja kwa moja kutoka kwenye pampu ya mafuta. Wafanyakazi wakifurahia baada ya kufunguliwa kituo chao.
Mfanyakazi wa kituo cha mafuta cha Kigamboni akitoa risiti mara baada ya kuuza mafuta.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere akikagua risiti mara baada ya kuuza mafuta.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere akiuza mafuta katika kituo cha GBP kilichopo uwanja wa ndege mara  baada ya kukifungulia.Kwa habari zaidi BOFYA HAPA


WAFANYAKAZI BOHARI KUU ZANZIBAR WAPATIWA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA JANGA LA MOTO

$
0
0
Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar
Sehemu zenye mikusanyiko ya watu zikiwemo Taasisi za Serikali na watu binafsi zinatakiwa kuwa na vifaa vya huduma ya kwanza vya kupambana na janga la moto na watu wenye taaluma ya kutumia vifaa hivyo.
Kaimu Afisa wa mafunzo Inspekta Ibrahim Ali Hassan wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar amesema sheria No. 7 ya mwaka 1999 ya Idara hiyo imewapa uwezo wa kuzifungia sehemu hizo iwapo zitashindwa kuweka vifaa na watu wenye uwezo wa kuzima moto.
Inspecta Ibrahim ametoa maelezo hayo alipokuwa akitoa mafunzo ya kukabiliana na moto kwa wafanyakazi wa Idara ya Bohari Kuu ya dawa Maruhubi.
Amesema lengo la kuwepo sheria hiyo ni kujaribu kuokoa maisha ya wananachi na mali zao wakati wa janga la moto ambalo linasababisha athari kubwa katika jamii.
Hata hivyo amesema bado taasisi nyingi za Serikali na binafsi hazijaona umuhimu wa kuweka vifaa vya huduma ya kwanza vya kuzimia moto na kuwapa mafunzo wafanyakazi wao .
Ameipongeza Wizara ya Afya kwa kujali kuwapatia mafunzo ya kukabiliana na moto wafanyakazi wa vitengo vyake mbali mbali na kuimarisha huduma hiyo katika taasisi zake kila mwaka.
Katika kukabiliana na janga la moto, Inspekta Ibrahim Ali Hassan aliwataka wafanyakazi wa bohari kuu kuacha fadhaa na kutumia njia za kitaalamu kwa kuondosha vitu ambavyo havijaanza kuungua, kuunyima moto hewa na kutia maji kwa moto wa kuni.
Aidha amewashauri wananchi kuanzisha utaratibu wa kuweka chupa ya kuzimia moto katika majumba yao na Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar kinatoa mafunzo ya matumizi sahihi ya kifaa hicho bila malipo.
Amesema binadamu hawezi kuishi bila kutegemea moto na moto ni adui mpenzi wa binadamu hivyo tahadhari inahitajika wakati wote katika kujilinda.
Akizindua mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Idara ya Bohari Kuu ya dawa Zanzibar Zahran Ali Hamad ametaka kila  mfanyakazi wa taasisi hiyo kuwa na uwezo wa kujilinda na moto yeye mwenyewe na mali iliyopo ndani.
Amesema bohari kuu ni taasisi muhimu katika ustawi wa maisha ya wananchi wa Zanzibar na imeweka mkazo kuhusu mafunzo hayo kwa wafanyakazi wote hivyo amewashauri kuyapokea kwa umuhimu wake.
 Mkurugenzi Idara ya Bohari Kuu ya Dawa Zanzibar Zahrani Ali Hamad akifungua mafunzo ya siku moja ya kukabiliana na janga la moto kwa wafanyakazi wa Idara hiyo Ofisini kwao Maruhubi Mjini Zanzibar.
  Kaimu Afisa wa mafunzo Kikosi cha Zimamoto Zanzibar Inspekta Ibrahim Ali Hassan akionyesha utaratibu bora wa kubeba chupa ya gesi kwa ajili ya kuzima moto katika mafunzo ya wafanyakazi wa Bohari Kuu ya dawa Maruhubi.
 Mmoja wa wafanyakazi wa bohari kuu ya dawa Zanzibar Ali Othman Omar (kushoto) akiuliza suala kuhusu matumizi sahihi ya mtungi wa kuzimia moto katika mafunzo hayo.
Fatma Omar Said akiwa katika mafunzo ya vitendo ya kukabiliana na janga la moto katika mafunzo ya wafanyakazi wa Bohari kuu ya dawa Zanzibar yaliyofanyika Maruhubi Mjini Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga.

Profesa Mwandosya ahudhuria Mkutano Mkuu wa 19 wa Umoja wa Mashirika ya Umeme ya Afrika

$
0
0
Kwa mwaliko maalum Waziri mstaafu wa Tanzania  Profes Mark Mwandosya anahudhuria Mkutano Mkuu wa 19 wa Umoja wa Mashirika ya Umeme ya Afrika unaofanyika Livingstone, Zambia. Mkutano Mkuu huo umefunguliwa jumatano tarehe 12 Julai 2017 na Mhe. Edgar Chagwa Lungu,Rais wa Jamhuri ya Zambia.
Katika hotuba yake Rais Lungu amesisitiza umuhimu wa umeme katika maendeleo ya Zambia na aliwaambia Wajumbe kuwa hakuwa tayari kuona Shirika la Umeme la Zambia(ZESCO) likishindwa kutoa huduma stahiki na kushindwa kutekeleza miradi ya maendeleo kutokana na hali mbaya ya kifedha. 
Hivyo basi hivi karibuni ameruhusu ZESCO kuongeza bei ya umeme kwa asilimia 75. Amesema  kitendo hicho ni sawa na kujiua kisiasa lakini yuko tayari kuikosa Ikulu mwaka 2021 kuliko kuiona umeme unakosekana, uchumi unazorota na ZESCO inakufa. 

 Rais wa Zambia Mhe. Edgar Lungu akitoa hotuba ya kufungua Mkutano huo
 Profesa Mark Mwandosya  akitoa mada kuhusu Changamoto za Udhibiti (Regulation) katika Sekta ya Umeme Afrika. 
Profesa Mark Mwandosya akiwa na  Mama Lucy Mwandosya wakimsikiliza Mhe. Rais Lungu.

YANGA YAMTAMBULISHA AFISA HABARI MPYA

MAPOROMOKO YA LIVINGSTONE NCHINI ZAMBIA

$
0
0
Maporomoko ya maji ya Livingstone huko Zambia kama 
yalivyokutwa  leo na Profesa Mark Mwandosya

Jamii Media na Kongamano la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, ICT

$
0
0
Na Joachim Mushi wa TBN
Kampuni ya Jamii Media ya Tanzania inayoendesha mitandao ya JamiiForums na FikraPevu kwa kushirikiana na CIPESA(The Collaboration on International ICT Policy in East and Southern Africa) iliyo na makao makuu yake nchini Uganda imefanya Kongamano la kuwakutanisha wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) nchini hasa wanaohusika moja kwa moja katika kulinda faragha za wateja wao ili kujadili masuala mbalimbali ya Huduma za Habari na Mawasiliano katika jukumu lao kuwa kiunganishi kati ya mteja na huduma watoazo pamoja na namna ya kulinda usiri wa taarifa za wateja wanaotumia huduma hizo.

Kabla ya kufanyika kwa Kongamano hilo siku ya Jumatano tarehe 12 Julai, Jamii Media ilifanya mafunzo ya siku mbili kuanzia tarehe 10 hadi 11 Julai kwa vijana mbalimbali wakiwemo wanasheria, wanaharakati na wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. Mafunzo hayo yalilenga kujenga uelewa kuhusu sera zinazohusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Usalama wa Data Mtandaoni, Hali ya Uhuru Mitandaoni na Mambo yanayoathiri uhuru Mitandaoni nchini Tanzania.

Katika Kongamano hilo, Mwakilishi wa Jeshi la Polisi Tanzania, Dawson Msongaleli kutoka kitengo cha Makosa ya Mtandaoni alifanya pia Uwasilishaji kuhusu Sheria ya Makosa Mtandaoni na kueleza kuwa Usiri na Usalama wa taarifa za watumiaji wa mtandao ni vitu viwili vinavyokanganya na kwamba inafika wakati ili kutekeleza kimoja inabidi misingi ya kingine ivunjwe.

Aidha, alibainisha kuwa kukosekana kwa kanuni za usimamizi wa Sheria ya Makosa ya Mtandao (The Cyber Crimes Act, 2015) ni changamoto kubwa kwani inapelekea tafsri ya Sheria hiyo kubadilika kulingana na mazingira na mtu anayetafsiri kitu ambacho kinaathiri kazi yao kama watekelezaji wa Sheria na kuahidi kuwa mamlaka zinashughulikia chamgamoto hiyo.

Mara baada ya kumalizika kwa kongamano hilo, Mkurugenzi wa Jamii Media, Bw. Maxence Melo alisema hili ni Kongamano la kwanza la aina hii kufanyika tangu kuanzishwa kwa JamiiForums miaka 11 iliyopita na limekuwa na matokeo chanya baada ya wadau kujadili kwa kina masuala mbalimbali yahusuyo usalama wa watumiaji. Aliongeza kuwa wadau wengi kwenye kongamano hilo wameunga mkono hatua ya uwekaji wa sheria za kusimamia huduma nzima ya matumizi ya mitandao lakini wakashauri ufanywe kwa kutoa fursa za maendeleo na si kuminya ubunifu wala uhuru na usiri wa watumiaji wa huduma hizo.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa kampuni yake itaendelea kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali wa huduma za mawasiliano wakiwemo wamiliki wa blogu na watumiaji wa kawaida wa mitandaonya kijamii ili kuhakikisha wanakuwa na matumizi mazuri ya huduma hiyo ili kupunguza mkanganyiko kwao na kuwapa fursa adhimu ya kunufaika na uwepo wa mitandao hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Mello (wa pili kulia) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumalizika kwa kongamano la wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) nchini Tanzania, lililoandaliwa na Kampuni ya Jamii Media ya Tanzania wamiliki wa mitandao ya Jamii Forums na Fikra Pevu kwa kushirikiana na Kampuni ya CIPESA ya nchini Uganda. Wengine ni Mkurugenzi wa CIPESA, Dk. Wairagala Wakabi (wa kwanza kulia) na Kutoka kushoto ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya Jamii Media, Asha Abinallah na Mkurugenzi wa Jamii Media, Mbaraka Islam. 

WANANCHI WAJAA KWENYE VITUO VYA MAFUTA VINAVYOTOA RISITI ZA TRA

$
0
0
 Baadhi ya Madereva Bodaboda wakiwa katika foleni ya  kituo cha Mafuta cha Total kilichopo Shekilango mara baada ya kukosa mafuta katika vituo vingine ambavyo vimefungwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kwa kosa la kutotoa risiti kwa wateja hivyo kuikosesha serikali mapato
 Foleni ya Magari inavyoonekana kwa nje ya kituo cha Mafuta cha TOTAl Shekilango jijini Dar es Salaam kutokana na baadhi ya vituo kufungwa kwa makosa ya kutotoa risiti za TRA
 Baadhi ya madereva wa Bodaboda wakiwa  wamekata tamaa mara baada ya kuona kuwa foleni kuwa kubwa
Madereva bodaboda wakiwa katika foleni ya kuweka mafuta

HEART WARMER


BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 14.07.2017

THE KILIMANJARO CONNECTION (KC) RADIO YA WADAU IKITANGAZA MUBASHARA TOKA HOUSTON, TEXAS, MAREKANi

$
0
0

 Dj Rex wa KC Radio. Hii ni  Radio ya wadau inayotangaza mubashara kutoka Houston, Texas, Marekani. Ni moto wa kuotea mbali. ukitaka kuwapata zaidi hebu BOFYA HAPA

MJADALA WA ESCROW

MAGAZETI YA JUMAMOSI LEO JULAI 15,2017

KIWANJA CHA NDEGE TABORA CHATAKIWA KUJIENDESHA

$
0
0

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ameutaka uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kuweka mikakati endelevu ili kuwezesha kiwanja cha ndege cha Tabora kujisimamia na kujiendesha kutokana na miundombinu bora na ya kisasa inayoendelea kujengwa kiwanjani hapo.

Amezungumza hayo jana mkoani humo, mara baada ya kuanza ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine Waziri Prof. Mbarawa amekagua na kujionea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kiwanja hicho ambapo mpaka sasa ujenzi wake umefikia asilimia 96 na umegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 27.

“Hivi sasa huduma ya usafiri wa ndege katika kiwanja hichi unaridhisha, hivyo ongezeni ubunifu ili kuvutia abiria wengi na kuwezesha kiwanja kujiendesha”, amesema Prof. Mbarawa.

Amesisitiza kuwa gharama za usafiri wa anga zitaendelea kupungua kadri huduma na ubora zitavyokuwa zinaendelea kuongezeka ili kuwezesha abiria wengi zaidi kutumia usafiri huo na hivyo kuwezesha pato la Taifa kuongezeka.
Meneja wa Mradi wa ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Tabora Eng. Neema Joseph, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, kuhusu maendeleo ya ujenzi yaliyofikiwa kiwanjani hapo, wakati akikagua ujenzi wake, mkoani humo jana.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Mradi wa ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Tabora Eng. Neema Joseph, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi ya kiwanja hicho uwanjani hapo, jana.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Kaya-Ceytun JV Eng. Ifran Sakrak (kushoto), wakati alipokuwa akikagua maendeleo ya ujenzi ya kiwanja cha ndege cha Tabora, jana.
Muonekano wa Taa za kuongozea ndege wakati wa kutua zilizojengewa katika Kiwanja cha Ndege cha Tabora.
Muonekano wa Mtambo wa kisasa wa kuongoza ndege unaonesha mwelekeo na umbali wa zaidi ya Kilomita 200 uliopo katika kiwanja cha ndege cha Tabora.

SOMA ZAIDI HAPA

VIJIJI 347 KUPATA UMEME WA REA AWAMU YA TATU MKOANI SIMIYU

$
0
0

Na Stella Kalinga, Simiyu

Jumla ya Vijiji 347 Mkoani Simiyu vinatarajia kupata Umeme kupitia Mradi wa Umeme Vijijini (REA) awamu ya Tatu ambao utatekelezwa katika kipindi cha miezi 24 kuanzia mwezi Julai 2017.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt.Medard Kalemani wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Umeme Vijijini (REA) Awamu ya Tatu na utambulisho wa Mkandarasi wa mradi katika Kijiji cha Nangale, Kata ya Ndolelezi Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu.

“Mradi wa REA awamu ya tatu utapeleka Umeme katika vijiji vyote vya Mkoa wa Simiyu hilo la kwanza, pili mradi huu utapeleka Umeme katika vitongoji vyote hata vijiji ambavyo vilipelekewa Umeme lakini baadhi ya vitongoji vyake bado havina umeme, sasa katika awamu hii navyo vinapelekewa” amesema Kalemani. 

Ameongeza kuwa Umeme wa REA awamu ya tatu pamoja na kuwanufaisha wananchi katika makazi yao kwenye vijiji vyote 347 vilivyosalia pia utapelekwa katika Taasisi za Umma zikiwepo shule, vituo vya kutolea huduma za afya, visima na mitambo ya miradi ya maji pamoja na nyumba za ibada( makanisa na misikiti).
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe.Dkt.Medard Kalemani akizindua Mradi wa Umeme Vijijini (REA)Awamu ya Tatu Mkoani Simiyu katika Kijiji cha Nangale wilayani Itilima (kushoto) Mkuu wa mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka.
Mmoja wa Wazee 10 waliopewa kifaa cha Umeme kiitwacho UMETA katika Kata ya Ndolelezi Wilayani Itilima na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe.Dkt.Medard Kalemani akitoa shukrani wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Umeme Vijijini (REA)Awamu ya Tatu Mkoani Simiyu uliofanyika katika Kijiji cha Nangale wilaya ya Itilima.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe.Dkt.Medard Kalemani akizungumza na wannachi wa Wilaya ya Itilima wakati wa Uzinduzi waMradi wa Umeme Vijijini (REA) Awamu ya Tatu Mkoani Simiyu uliofanyika katika Kijiji cha Nangale wilaya ya Itilima.

TRA YAANZA KUVIFUNGULIA VITUO VINAVYOTIMIZA MASHARTI YA KUFUNGA MASHINE ZA KIELEKTRONIKI

$
0
0

Na Kajunason Blog/Cathbert Kajuna. 

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imevifungulia vituo vya mafuta vipatavyo vitatu jijini Dar es Salaam baada ya kutimiza masharti ya kufunga mashine za kielekitroniki zinazotoa risiti moja kwa moja kutoka kwenye pampu ya mafuta (Automatic EFD).

Akizungumza mara baada ya kufungua vituo hivyo, Kamishina wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere amewashukuru wamiliki wa vituo hivyo kwa kuonyesha ushirikiano kwa serikali kwa kutimiza masharti waliyopewa ya kufunga mashine hizo na kusisitiza kuwa hakuna kituo kitakachofunguliwa kama hakitatimiza masharti. 

"Niwaombe wamiliki wa vituo vilivyofungiwa kuwa kwa sasa hakuna kitakachofunguliwa bila kutimiza mashart, timiza masharti tuje tukague na tukufungulie uanze biashara yako," amesema Kamishna Kichere. 

Amesema vituo vilivyofunguliwa leo ni GBP kilichopo eneo la Majumba Sita, Simba Oil kilichopo eneo la Sitakishari, Ukonga na PETRO kilichopo eneo la Kigamboni. 

"Kitendo cha kuunganisha mashine hizi na pampu za mafuta ni cha muda mfupi sana na wala hakichukui muda mrefu, angalia huyu tulimfungia siku ya jumanne tarehe 11 Julai na leo Ijumaa Julai 14 ameshafunga mashine na anaanza kufanya biashara bila kugombana na serikali;" amesema Kamishna Kichere. 

Mpaka sasa vituo zaidi ya 40 vimefungiwa nchi nzima ikiwemo jijini Dar es Salaam kwa kosa la kushindwa kufunga mashine za kielekitroniki zinazotoa risiti moja kwa moja kutoka kwenye pampu ya mafuta (Automatic EFD).  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere akikata utepe katika kituo cha mafuta cha Kigamboni jijini Dar es Salaam baada ya kutimiza masharti ya kufunga mashine za kielekitroniki zinazotoa risiti moja kwa moja kutoka kwenye pampu ya mafuta. 
Mfanyakazi wa kituo cha mafuta cha Kigamboni akitoa risiti mara baada ya kuuza mafuta. 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere akikagua risiti mara baada ya kuuza mafuta.

 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere akiuza mafuta katika kituo cha GBP kilichopo uwanja wa ndege mara baada ya kukifungulia. 

SERIKALI IPO KATIKA HATUA ZA MWISHO KUHIDHINISHA BILIONI 1.6 KUTOKA MFUKO WA GEPF KWAAJILI YA KUJENGA KINU CHA KUYEYUSHIA VYUMA KATIKA KIWANDA CHA (KMTC)-WAZIRI MHAGAMA

$
0
0

Serikali ipo katika hatua za mwisho katika kuhidhinisha bilioni 1.6 kutoka katika mfuko wa hifadhi za jamii GEPF kwaajili ya kujenga kinu cha kuyeyushia vyuma katika kiwanda cha kutengeneza vipuri na mashine cha Kilimanjaro Machine Tools Limited (KMTC).

Akizungumza jana katika kiwanda hicho mara baada ya kutembelea Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh.Jenista Joakim Mhagama,alisema kuwa fedha hizo zitatumika kwaajili ya kuboresha kiwanda hicho kwa lengo la kufufua kwa kuwa kiwanda hicho kinabeba dhana nzima ya maendeleo ya uchumi wa viwanda kwenye nchi ya Tanzania

Alisema kuwa mfuko wa GEPF baada ya kupokea maagizo kutoka kwa Rais akihimiza Serikali ya viwanda ,wameweza kujiridhisha kuwa wanauwezo wa kuwekeza katika kiwanda hicho cha kutengeneza vipuri na mashine cha Kilimanjaro Machine Tools (KMTC)

Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh.Jenista Joakim Mhagama,wa pili kulia jana alipata fursa ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza vipuri na mashine cha Kilimanjaro Machine Tools Limited (KMTC),wa tatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh.Anna Mghwira na wa kwanza kulia ni Meneja mkuu Kilimanjaro Machine Tools Eng.Adriano  Nyaluke akitoa taarifa za uzalishaji wa kiwanda hicho(Picha na Pamela Mollel Arusha).
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh.Jenista Joakim Mhagama akiteta jambo na wakurugenzi wa mifuko ya jamii jana katika ziara yake katika kiwanda cha kutengeneza vipuri na mashine cha Kilimanjaro Machine Tools Limited (KMTC),Kulia ni Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa pensheni wa GEPF Mh..Daud Msangi ,kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa Pensheni wa PPF Mh. William Erio.
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh.Jenista Joakim Mhagam akiwa anatoa maelekezo katika kiwanda hicho ambapo alisema kuboreshwa kwa kiwanda hicho kitasaidia ajira kwa vijana
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh.Jenista Joakim Mhagam akiangalia baadhi ya vyuma vilivyo zalishwa katika kiwanda hicho.


The Desk & Chair Foundation yatoa msaada kwa mtoto Mlemavu

$
0
0

Na Baltazar Mashaka, Mwanza.

Familia ya mtoto Malale Mihayo (12) yenye makazi yake katika Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga imeishukuru Taasisi ya The Desk & Chair Foundation (TD&CF) Tawi la Tanzania kwa msaada wa baiskeli (Wheel Chair ) kwa ajili ya mtoto wao mwenye tatizo la Cerebral Polse (mtindio wa ubongo).

Akizungumza na mtandao huu baada ya kukabidhiwa baiskeli hiyo mama mzazi wa mtoto huyo Elizabert Tungu alisema  itampunguzia adha ya kumbeba mwanaye huyo ambaye hana uwezo wa kufanya chochote kutokana na tatizo alilonalo.

“ Mwanangu alizaliwa  mwaka 2008 akiwa mzima wa afya, alipata tatizo hili baadaye akiwa na umri  wa miaka 3 na nusu.Nilimpeleka kutibiwa hospitali huko Arusha na Moshi madaktari wakanieleza anasumbuliwa na tatizo la uti wa mgongo, licha ya kutibiwa hakupata nafuu.Nawashukuru Desk & Chair kwa msaada huu,”alisema.

Bi. Tungu mwenye familia ya watoto sita alisema alimpeleka kwa waganga wa tiba za jadi nako hakupata nafuu na hivyo akalazimika kurejea nyumbani ambapo mwanaye huyo aliendelea kukakamaa viungo vya mwili wake na kupoteza uwezo wa kukaa wala kutembea.
  Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation Tawi la Tanzania Sibtain Meghjee kulia, akimkabidhi Elizabert Tungu baiskeli (Wheel chair) kwa ajili ya  mwanaye Malale Mihayo (aliyekaa) ambaye ana tatizo la mtindio wa ubongo.Kushoto ni Abass Meghjee mmoja wa wafadhili na kiongozi wa taasisi hiyo yenye makao makuu nchini Uingereza. 

 Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foudation Tawi la Tanzania Sibtain Meghjee akimsaidia kumsukuma Malale Mihayo mkazi wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga baada ya kumkabidhi msaada wa baiskeli (Wheel chair) itakayomsaidia kwa usafiri. Mtoto huyo ana tatizo la mtindio wa ubongo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RC SHINYANGA ATEMBELEA KIWANDA CHA MAFUTA YA MCHELE KIZUMBI SHINYANGA

$
0
0
Ijumaa Julai 15,2017,Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack ametembelea kiwanda cha kutengeneza mafuta ya mchele kinachomilikiwa na kampuni ya Mwekezaji kutoka nchi ya China Jielong Holding kilichopo katika kijiji cha Nhelegani kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga.

Mkuu huyo wa mkoa aliyekuwa ameambatana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga na maafisa mbalimbali mkoa huo amejionea jinsi kampuni hiyo ilivyodhamiria kuzalisha mafuta ya kupikia yanatokana na mapumba laini ya mpunga “Mchele”. 

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Telack alisema kiwanda hicho ni cha pekee nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla na kitasaidia wamiliki wa mashine za kukobolea mpunga pamoja na wakulima kunufaika na zao la mpunga kwani wataweza kuuza mapumba kwa ajili ya kutumika kama malighafi kuzalishia mafuta hayo. 

“Niwapongeze wawekezaji hawa kwa ubunifu huu wa kiwanda cha aina yake, serikali ya mkoa wa Shinyanga inaunga mkono jitihada za kuhakikisha tunakuwa na uchumi wa viwanda,tushirikiana kuwahamasisha wananchi kulima mpunga kwa wingi na wale wenye mpunga basi wauze mapumba yao ili wajipatie kipato”,alieleza Telack. 

“Naamini watu wenye mashine za kukobolea mpunga wataongeza kipato kwa kuuza mabaki ya mpunga kwa ajili ya kuendeshea kiwanda hiki ambacho pia kinazalisha nishati ya umeme kwa kutumia mapumba”,alieleza Telack. 
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack (kulia) akitembelea kiwanda cha kutengeneza mafuta ya mchele kinachomilikiwa na kampuni ya Mwekezaji kutoka nchi ya China Jielong Holding kilichopo katika kijiji cha Nhelegani kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga.Kulia kwake ni Mkalimani katika kampuni hiyo Joseph Warioba akifuatiwa na Mwenyekiti wa kampuni Jielong Holding,Qi Qi Shuwei.Wengine ni wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga na maafisa kutoka mkoa huo. 
Qi Shuwei akiongoza msafara wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga kuangalia uzalishaji wa bidhaa mbalimbali zinazotokana na mazao yanayolimwa na wakulima. 
Mkalimani katika kiwanda cha Jielong Holding,Joseph Warioba akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack kuhusu malighafi mbalimbali zinazotumika katika kiwanda hicho cha kutengeneza mafuta ya alizeti,pamba,mchele na sabuni. 
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akingalia shughuli ya uzalishaji mafuta ya alizeti inavyofanyika.

Naibu Waziri Dk. Kigwangalla aagiza uboreshaji wa huduma za Afya Tunduru

$
0
0
Naibu waziri wizara ya Afya, Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto Dk. Hamisi Kigwangalla ametoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tunduru kuhakisha wanaboresha huduma za Afya katika Wilaya hiyo hasa kituo cha Afya Mkasale ambacho kimebainika kuwa na huduma mbovu huku pia kikiwa na uchakavu kwenye majengo yake hali ambayo inaweza kuhatarisha usalama na afya za watumishi na wagonjwa wanaohudumiwa hapo.

Akiwa katika ziara ya kikazi ya ukagazi wa utekelezajiwa agizo la uboreshaji wa vituo vya afya katika kila Kata nchini lilitolewa Desemba 2016, Dk. Kigwangalla akikagua kituo hicho cha Mkasale , aliweza kujionea mazingira hayo ambapo licha ya kupewa taarifa alitaka mara moja Uongozi wa Halmashahuri

hiyo kushughulikia suala ndani ya miezi mitatu ikiwemo Mkandarasi wa Maji kuhakikisha anaingiza mifumo ya maji ndani ya kituo hicho, pia aliagiza uongozi wa kijiji kushiriki katika kufanya usafi wa mazingira yanayozunguka kituo hicho cha Mkasale.

Awali akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Tunduru baada ya ziara hiyo ya kukagua vituo vya Afya na Hospitali ya Wilaya, Dk Kigwangalla amesema Serikali inaendelea na uboreshaji wa huduma za afya na kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma zenye ubora na kwa wakati na lengo la serikali ya awamu ya tano ni kupunguza kwa asilimia kubwa changamoto zinazoikabili wilaya ikiwa ni pamoja na kupunguza vifo vya kinamama wajawazito na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano, kukamilisha maboma yote ya vituo vya afya, zahanati na hospitali ambazo hazijakamilika, na kuhakikisha kuwa vifaa tiba na dawa zinapatikana za kutosha.

“Hata hivyo nawasihi wananchi tumuunge mkono Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kwa vita aliyoianzisha ya kulinda rasilimali za nchi yetu, kwani taifa limekuwa likiibiwa kwa muda mrefu sana ila umefika muda kuhakikisha kuwa rasimali za nchi zinatunzwa na kulindwa kwa ajili ya vizazi vijavyo.” Alieleza Dk. Kigwangalla wakati akiwahutubia wananchi hao.
Naibu waziri wizara ya Afya, Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto Dk. Hamisi Kigwangalla akilakiwa na wananchi wa Kijiji cha Mkasale wilayani Tunduru, Mkoani Ruvuma wakati wa ziara yake hiyo 
Naibu waziri wizara ya Afya, Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto Dk. Hamisi Kigwangalla akimsabahi mmoja wa watoto waliofika na wazazi wake wakati wa kumpokea katika Kijiji cha Mkasale wilayani Tunduru, Mkoani Ruvuma wakati wa ziara yake hiyo.
Naibu waziri wizara ya Afya, Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza katika mkutano huo wa wazi kwa wananchi wa Halmashauri ya Tunduru, Mkoani Ruvuma.



NAIBU WAZIRI NISHATI DKT MEDARD KALEMANI AZINDUA MRADI WA REA MKOA WA SIMIYU

$
0
0
 Naibu waziri wa Nishati na Madini Dkt Medard Kalemani akizindua mradi wa Umeme vijijini REA jana Nangale wilaya ya Itilima mkoani Simiyu akiwa ameambatana na viongozi wa mkoa huo.
 Naibu waziri wa Nishati na Madini Dkt Medard Kalemani akiwasalimia wabunge wa mkoa wa Simiyu wakati wa uzinduzi mradi wa Umeme vijijini REA jana.

 Wabunge  mkoa wa Simiyu  wakicheza na Naibu waziri wa Nishati na Madini Dkt Medard Kalemani wakati wa uzinduzi mradi wa Umeme vijijini REA jana  ikiwa ni katika kuhakikisha umeme unapatikana nchi nzima na kwa bei nafuu.
  Wananchi  wakiwa wanafuatilia uzinduzi wa mradi wa Umeme vijijini REA jana wakati ulipozinduliwa na Naibu waziri wa Nishati na Madini Dkt Medard Kalemani ikiwa ni katika kuhakikisha umeme unapatikana nchi nzima na kwa bei nafuu.
Viewing all 110104 articles
Browse latest View live




Latest Images