Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109973 articles
Browse latest View live

HARBINDER SETHI ADAIWA KUWA NA UVIMBE TUMBONI, KESI YAKE YASHINDWA KUENDELEA YAPIGWA KALENDA

$
0
0




Na Karama Kenyunko-Globu ya Jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeambiwa kuwa, mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Power African Power (T) Limited (PAP) ambaye pia ni mshitakiwa wa kwanza katika kesi ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha, Harbinder Singh Sethi ni mgonjwa sana na anasumbuliwa na uvimbe tumboni.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Wakili wa mshitakiwa, Alexi Balomi ambaye amedai mahakamani hapo kuwa, hali ya mteja wake Seth imekuwa ikibadilika kwa wiki nne sasa na kwamba imezidi kuwa mbaya kwa kuwa hawezi kupata usingizi na hivyo anahitaji uangalizi wa madaktari..

Kabla ya hoja hiyo ya ugonjwa, Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi Mwendesha Mashitaka Mwandamizi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai alidai kuwa kesi hiyo ilikuja kwa kutajwa na upelelezi bado haujakamilika.

Balomi amedai kuwa kutokana na hali mbaya ya mteja wake Seth,wamebahatika kupata nyaraka kadhaa kutoka kwa daktari kwani Hata siku aliyokamatwa alikuwa akienda kwenye matibabu Afrika Kusini alisema huku akitaka kutoa nyaraka hizo.

Hata hivyo, Swai alidai nyaraka ambazo Wakili Balomi anataka kuziwasilisha mahakamani hapo kuhusiana na Sethi hazijakidhi vigezo vya sheria na kwamba alitegemea daktari ambaye anamtibu angefika mahakamani kueleza hali halisi ya ugonjwa husika.

Akijibu hoja hiyo, Hakimu Shaidi amesema suala la ugonjwa siyo la kufumbiwa macho, linapaswa kuchukuliwa kwa uzito na kuelekeza magereza kufanya kila linalowezekana kuhakikisha hali ya mshitakiwa huyo inakuwa nzuri na ikibidi, wawasiliane na wataalam wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kuhakikisha mshitakiwa anapohitajika mahakamani anafika kama inavyotakiwa.

Kesi imeahirishwa hadi Julai 28, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.

Seth anashtakiwa pamoja na James Rugemarila ambaye ni Mkurugenzi wa VIP Engineering na mmiliki mwenza wa zamani wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Ltd (IPTL), ambao wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 12 ya uhujumu uchumi kwa kuisababishia serikali hasara ya dola za Marekani milioni 22. 1 na Sh bilioni 309 pamoja na utakatishaji fedha.

Watumishi wa Mahakama waaswa kushughulikia vitendo vya rushwa.

$
0
0
WAZIRI wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amewaasa watumishi wa mahakama kushughulikia vitendo vya rushwa kwani vinaipatia mahakama taswira hasi na kuzitaka tume za  mahakama na maadili kuchunguza vitendo vya ukiukwaji wa maadili na kuchukua hatua stahiki.

Waziri Kabudi, amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na watumishi wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani juu ya mustakabali wa taasisi hiyo, ikiwa ni mara yake ya  kwanza kufanya ziara tangu alipoteuliwa kuwa Waziri.

Amesema, majaji na mahakimu mara nyingi, wamekuwa wakihusishwa na vitendo vya rushwa hivyo, na kuchangia kuwepo kwa kutokuwa na imani kwa wananchi wanaokuwa na shida ,mbali mbali katika taasisi hizo, hasa wale wenye kesi.

 ‘’Pamoja na mabadiliko makubwa katika mahakama bado kumekuwa na changamoto ya uadilifu hususan vitendo vya rushwa na uwajibikaji ambavyo vimeleta taswira hasi kwa wananchi wanaotafuta haki na kusababisha ushiriki mdogo,’’alisema Profesa Kabudi.

Ameongeza, watendaji wanapaswa kubuni mbinu mbali mbali za kuweza kubadili taswira hiyo kwa kuwachukulia hatua za kinidhamu wanaokiuka maadili na kusogeza huduma kwa wananchi.Kwa mujibu wa Profesa Kabudi, mahakama inanafasi kubwa ya kuchangia maendeleo ya nchi na kwamba jambo wanalopaswa kufanya ni kuimarisha utendaji kazi na kutokomeza rushwa.

Kwa upande wake, Kaimu Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma alisema kuwa wataendelea kutumia sheria kwa ajili ya kuwainua wananchi wengi kwa lengo la kukuza uchumi.

Profesa Juma alisema majaji na mahakimu ni sehemu ya jamii ambao wanapaswa kushiriki kustawisha wanaqnchi ili kutokomeza umasikini.
Akiwasilisha ripoti kuhusu mahakama, Mtendaji Mkuu wa mahakama, Hussein Katanga alisema kuwa idadi ya majaji imeshuka kutoka 100 hadi 80 huku uhitaji wake ukiwa ni kati ya 100 hadi 120.

Katanga alisema majaji 20 wameacha kazi kwa sababu mbalimbali ikiwemo kustaafu na kwamba uhitaji huo unachangia kasi ya kuongezeka kwa ufunguaji mashauri. 

Mfungaji wa Goli la Gor Mahia Awashukuru Mashabiki wa Tanzania

DKT ARNOLD KASHEMBE KATIBU MKUU MPYA WA SIMBA

$
0
0

Kamati ya utendaji ya klabu ya Simba iiliyokutana jana jioni kwenye moja ya kumbi za mikutano za Hoteli ya Serena iliyopo hapa jijini Dar es salaam,imemteua Dr Arnold Kashembe kuwa katibu Mkuu mpya wa klabu. 

Msomi huyo mwenye shahada ya Uzamivu na aliyekuwa Mhadhiri kwenye vyuo mbalimbali barani Ulaya, uteuzi wake unaanza mara moja. 

Pia kamati hyo imepanga kufanya Mkutano wake mkuu wa kawaida tarehe 13-8-2017, huku pia ikitarajiwa kufanya Mkutano Mkuu utakaojadili mabadiliko ya katiba tarehe 20-8-2017.

Mikutano hyo imeitishwa kwa kuzingatia takwa la kikatiba la klabu,linalotaka notisi ya kuitishwa mikutano hiyo,ifanywe sio chini ya siku Thelathini kabla ya mikutano yenyewe. 

Klabu inatarajia kutoa taarifa zaidi juu ya maandalizi na taratibu za mikutano hiyo katika Siku chache zijazo na inaendelea kuwaomba Wanachama na Washabiki wake muendelee kuwa na utulivu,hususan kipindi hiki ambacho baadhi ya viongozi wetu wakiwa kwenye Shauri lao,liliopo Mahakamani.

WAZIRI MKUU AUPONGEZA UONGOZI WA NHC KWA UTENDAJI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameupongeza uongozi wa Shirika la Nyumba (NHC) kwa kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mnolela mkoani Lindi kwa muda mfupi. 

Amesema ujenzi wa zahanati hiyo ya kisasa mwezi Machi, 2017 na sasa tayari kimekamilika, jambo ambalo litarahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa eneo hilo na wa jirani. 

Waziri Mkuu alitoa pongezi hizo jana jioni (Alhamisi, Julai 13, 2017) alipozungumza na wananchi wa kijiji cha Mnolela baada ya kuzindua zahanati hiyo iliyosimamiwa na NHC. 

Alisema ujenzi wa zahanati hiyo ni muendelezo wa mkakati wa Serikali ya awamu ya tano wa kuboresha huduma za afya kwa kusogeza huduma karibu kwa wananchi wake. 

“Rais wetu Dkt. John Magufuli amedhamiria kuwaondolea wananchi changamoto za mbalimbali zikiwemo za huduma za afya, hivyo tuendelee kumuunga mkono.” 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa NHC, Bw. Nehemia Mchechu alisema mradi wa ujenzi wa zahanati hiyo ulisimamiwa na NHC na umegharimu sh. milioni 65.5. 

“Shilingi milioni 15 zilitolewa na Rais. Dkt. Magufuli, sh. milioni 10 zilitolewa na Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye, NHC ilitoa sh. milioni 10 na kiasi kilichosalia ni mchango wa halmashauri.” 

Awali Mbunge wa jimbo la Mtama, Mheshimiwa Nape alimshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa mchango mkubwa alioutoa katika mradi wa ujenzi wa zahanati hiyo. 

Mheshimiwa Nape alisema zahanati hiyo ni mkombozi kwa wakati wa kijiji cha Mnolela na wananchi wengine wanaoishi kwenye maeneo yaliyo jirani na kijiji hicho.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akisalimiana na Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba (NHC),wakati alipofungua Zahanati katika kijiji cha Mnolela, akiwa  njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne (katikati) ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Nape Mnauye Julai 13, 2017.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akikata utepe wakati alipofungua Zahanati katika kijiji cha Mnolela, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne (kutoka kushoto) ni Mbunge wa  Jimbo la Mtama Nape Mnauye, Diwani Kata ya Mnolela Omar Liveta, Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba (NHC) kutoka kulia ni Meneja NHC Lindi Gibson Mwaigomole, Meneja NHC Mtwara Nehemia Msigwa, Mkuu wa Mkoa Lindi Godrey Zambi Julai 13, 2017.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akikagua wakati kifaa katika Zahanati ya Mnolela, baada ya kuifungua, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akizungumza na wananchi wa Mnolela mara baada ya kuifungua Zahanati hiyo iliyopo katika Kijiji cha Mnolela, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA RAIS MSTAAFU WA IRELAND NA BI. GRACA MACHEL

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Rais wa Mstaafu wa Ireland, Mary Robinson ambaye pia ni Mjumbe wa Taasisi inayoshughulika na Amani,Haki za Binadamu na Huduma za Afya, Rais huyo Mstaafu aliongozana na Mjumbe mwingine wa Taasisi hiyo Bi. Graca Machel . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Rais wa Mstaafu wa Ireland, Mary Robinson ambaye pia ni Mjumbe wa Taasisi inayoshughulika na Amani,Haki za Binadamu na Huduma za Afya, Rais huyo Mstaafu aliongozana na Mjumbe mwingine wa Taasisi hiyo Bi. Graca Machel . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na  Rais wa Mstaafu wa Ireland, Mary Robinson pamoja na Bi. Graca Machel ambao ni Wajumbe wa Taasisi inayoshughulika na Amani,Haki za Binadamu na Huduma za Afya, wengine pichani ni Ujumbe ulioongozana na Viongozi hao pamoja na Wasaidizi wa Makamu wa Rais. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mjumbe wa Taasisi inayoshughulika na Amani,Haki za Binadamu na Huduma za Afya, Bi. Graca Machel ambaye aliongozana na  Rais wa Mstaafu wa Ireland, Mary Robinson kumtembelea Makamu wa Rais ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Mstaafu wa Ireland, Mary Robinson (kulia) ambaye pia ni Mjumbe wa Taasisi inayoshughulika na Amani,Haki za Binadamu na Huduma za Afya, kushoto ni Mjumbe wa Taasisi hiyo Bi. Graca Machel mara baada ya kumaliza mazungumzo kwenye ofisi za Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

DISMASI TEN RASMI NI MKUU WA KITENGO CHA HABARI WA YANGA SC

$
0
0
Klabu ya Yanga leo imemtangaza rasmi aliyekuwa afisa habari wa klabu ya soka ya Mbeya City Bwana Dismas Ten kama afisa habari wao baada ya kuingia nae mkataba leo. 

Dismas anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa afisa habari wa klabu hiyo Jerry Murro ambaye mwaka jana 09 Julai 2016 alifungiwa na Shirikisho la soka nchini kujihusisha na soka.

Nafasi hiyo ilikuwa ikikaimiwa na Godlisten Anderson Chicharito kama kaimu afisa habari ambaye sasa ataendelea na nafasi hiyo chini ya Dismas Ten. 

"Tumeamua kuleta mapinduzi kwenye utoaji habari kwenye klabu yetu na naamini kwa muunganiko huu wa Dismas na Chicharito klabu yetu itafanikiwa sana kupitia kitengo iki cha Habari na mawasiliano kama vilabu vingine vikubwa duniani."-Boniface Mkwasa Katibu Mkuu Yanga SC.

SHINDANO LA NGOMA ZA UTAMADUNI KUFANYIKA MJINI DODOMA KESHO


Rooney, Everton Wafurahia Ukarimu wa Watanzania

$
0
0
Timu ya Soka ya Everton inayoshiriki ligi kuu nchini Uiungereza imemaliza ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania na kuelezwa kufurahishwa na namna Watanzania walivyoipokea timu hiyo.

Timu ya Everton iliwasili Tanzania siku ya Jumatano wiki hii ambapo jana ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia kutoka Kenya.

“Imekuwa ni uzoefu mpya kwangu kuja hapa (Tanzania) na nina tumaini sasa Makamu wa Rais atakuwa akiishabikia Everton”, alieleza Wayne Rooney kupitia tovuti ya timu hiyo.

Pia katika akaunti yake ya mtandao wa tweeter, Rooney aliwashukuru washabikji wa Tanzania kwa kuiunga mkono Everton katika mchezo wao wa kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia kutoka Kenya.

“Great start to the pre-season. Special thanks to the fans supporting us in Tanzania”, aliandika Rooney akitoa shukrani za pekee kwa washabiki wa Tanzania. 


Wayne Rooney (wa tatu kushoto) kushoto akiwa na wachezaji wenzake walipokuwa Jijini Dar es Salaam ambapo timu ya Everton ilicheza na timu ya Gor Mahia katika mchezo wa kirafiki ulichezwa katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

WAFANYAKAZI BOHARI KUU ZANZIBAR WAPATIWA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA JANGA LA MOTO

$
0
0
Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar
Sehemu zenye mikusanyiko ya watu zikiwemo Taasisi za Serikali na watu binafsi zinatakiwa kuwa na vifaa vya huduma ya kwanza vya kupambana na janga la moto na watu wenye taaluma ya kutumia vifaa hivyo.

Kaimu Afisa wa mafunzo Inspekta Ibrahim Ali Hassan wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar amesema sheria No. 7 ya mwaka 1999 ya Idara hiyo imewapa uwezo wa kuzifungia sehemu hizo iwapo zitashindwa kuweka vifaa na watu wenye uwezo wa kuzima moto.

Inspecta Ibrahim ametoa maelezo hayo alipokuwa akitoa mafunzo ya kukabiliana na moto kwa wafanyakazi wa Idara ya Bohari Kuu ya dawa Maruhubi.

Amesema lengo la kuwepo sheria hiyo ni kujaribu kuokoa maisha ya wananachi na mali zao wakati wa janga la moto ambalo linasababisha athari kubwa katika jamii.
Fatma Omar Said akiwa katika mafunzo ya vitendo ya kukabiliana na janga la moto katika mafunzo ya wafanyakazi wa Bohari kuu ya dawa Zanzibar yaliyofanyika Maruhubi Mjini Zanzibar.Picha na Makame Mshenga.
 Mkurugenzi Idara ya Bohari Kuu ya Dawa Zanzibar Zahrani Ali Hamad akifungua mafunzo ya siku moja ya kukabiliana na janga la moto kwa wafanyakazi wa Idara hiyo Ofisini kwao Maruhubi Mjini Zanzibar.
  Kaimu Afisa wa mafunzo Kikosi cha Zimamoto Zanzibar Inspekta Ibrahim Ali Hassan akionyesha utaratibu bora wa kubeba chupa ya gesi kwa ajili ya kuzima moto katika mafunzo ya wafanyakazi wa Bohari Kuu ya dawa Maruhubi.
 Mmoja wa wafanyakazi wa bohari kuu ya dawa Zanzibar Ali Othman Omar (kushoto) akiuliza suala kuhusu matumizi sahihi ya mtungi wa kuzimia moto katika mafunzo hayo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

The Story of Zuriel Oduwole's First Film Class Program Windhoek - NAMIBIA

RC MAKONDA APOKEA KOMPYUTA 50 ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILLION 85 KUTOKA KAMPUNI YA TAMOBA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh.Paul Makonda amepokea Kompyuta 50 zenye thamani ya shilingi Million 85 kutoka kwa kampuni ya ulinzi ya TAMOBA,ikiwa kama namna ya kuunga mkono utendaji kazi mzuri unaofanywa na Ofisi hiyo. 

Upatikanaji wa kompyuta hizo umekuja ikiwa ni sehemu ya shauku na utafutaji wa RC Makonda kwa ajili ya kuongeza tija na ufanisi katika kuwahudumia wananchi wa Dar es Salaam, ambapo itakumbukwa hivi karibuni Mh.Makonda alifanya mkutano na Watumishi wa sekta ya Ardhi wa Manispaa zote na moja ya kero kubwa iliyo bainishwa kuwasumbua wananchi ni namna ya kupata kibali cha ujenzi jambo lililomkera RC Makonda.

Kucheleweshwa kwa huduma ya namna hii kwa wananchi huchochea utoaji Rushwa na ujenzi holela bila vibali unaosababisha Serikali kupoteza kodi ya viwanja na kodi zingine zinazohusiana na ardhi.

Aidha amesema kuwa wananchi wamekuwa wakipata kero mbalimbali ikiwemo ile ya kupewa kibali na manispaa kisha wakaja watu wa zima moto wakakuzuia kuendelea kwa ujenzi sababu hawana taarifa, huku wakati mwingine ukimalizana na watu Zimamoto wanakuja watu wa OSHA nao wanakuzuia usiendelee na ujenzi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda ( kushoto) akikabidhiwa Kompyuta  50 zenye thamani ya shilingi Million 85 na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Joseph Kimisha, kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TAMOBA Balozi Mstaafu Francis Mndolwa.

Baadhi ya Kompyuta hizo.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda (wakwanza kulia) akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya kukabidhiwa Computer 50 zenye thamani ya shilingi Million 85 na kampuni ya ulinzi ya TAMOBA kama sehemu ya kuunga mkono utendaji kazi mzuri

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TAMOBA Balozi Mstaafu Francis Mndolwa kizungumza mchache katika hafla hiyo leo jijini Dar es Salaam.


AZAM YAENDELEA NA MAKAMUZI YA MAANDALIZI YA LIGI KUU MSIMU UJAO

$
0
0

Kikosi cha timu ya Azam kimeanza mazoezi ikiwa  ni maalumu kabisa katika kipindi hiki cha maandalizi ya msimu ujao, ambapo Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba, amepanga kutengeneza kikosi kikali kitakachoweza kufanya makubwa katika siku za usoni.

Kikosi hicho leo kimeshafanya mazoezi mara mbili, saa 1.00 asubuhi na 3.30 asubuhi na kitamalizia mazoezi mwisho saa 11.00 jioni ndani ya viunga vya Azam Complex, Chamazi.

Cioaba amesema faida kubwa ya kufanya mazoezi makali hivi sasa ni kuwajenga wachezaji kwenye maeneo mbalimbali, kiufundi uwanjani, stamina na ustahimilivu kwenye kupambana.

Baada ya kumaliza programu hiyo ya mazoezi, Azam FC itasafiri Julai 20, mwaka huu kuelekea kwenye mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, ikienda kucheza mechi tatu za kirafiki, ya kwanza ikiwa ya mwaliko dhidi ya Mbeya City, itakayofanyika Julai 22 katika siku watakayokuwa wakisherehekea Mbeya City Day.

Mechi nyingine za kirafiki itacheza na timu mbili zilizopanda daraja. Njombe Mji Julai 24 mwaka huu mjini Njombe na ikimaliza ziara hiyo kwa kukipiga na Lipuli ya Iringa Julai 26 kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam Julai 27.

 Wachezaji wa Azam wakiwa katika mazoezi leo asubuhi ikiwa ni katika maandalizi ya msimu ujao chini ya  Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba na Iddy Cheche. 


Wachezaji wa Azam wakiwa katika mazoezi ya viungo leo asubuhi ikiwa ni katika maandalizi ya msimu ujao chini ya  Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba. 


Mbarawa afanya ziara JNIA

$
0
0
 Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uhamiaji Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Bw. Flugence Andrew (kulia) akitoa maelezo ya utaratibu unaotumika kulipia viza kwa Mhe. Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano leo alipofanya ziara kwenye jengo la abiria la kiwanja hicho. 
 Afisa wa Benki ya NMB, Bi. Leah Rutayungurwa  (aliyendani ya dirisha) leo akimmsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof Makame Mbarawa aliyetaka kujua muda anaohudumiwa abiria mmoja wakati akilipia viza kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (TBII-JNIA).
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa leo akiwa katika mfumo wa kupokelea mizigo kwa abiria wanaowasili kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere alipofanya ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali. Mwenye kizibao ni Kaimu Mkurugenzi wa kiwanja hicho, Bw. Joseph Nyahende.
Mhe. Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (TBII-JNIA), mwenye kizibao akielezea jambo katika meza ya ukaguzi wa tiketi za abiria wanaosafiri. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (kulia) akifurahia jambo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Phillip Mpango (kushoto)  na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Susan Kolimba na Katibu Mkuu  sekta ya Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho (mwenye mkoba mweusi) leo walipokutana kwenye Jengo la Watu Mashuhuri la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA MFUMO WA HCIMS ILI UWEZE KUTUMIKA NA WATUMISHI WENGI ZAIDI

$
0
0
Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inaendelea kusanifu na kuboresha Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCIMS) ili uweze kutumika kutoa taarifa za msingi kwa watumishi  wa umma wengi zaidi kwa lengo la kuleta mabadiliko ya utendaji kazi katika sekta ya umma nchini.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) amesema hayo leo katika kikao kazi na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya  Kinondoni – Kata ya Kawe, jijini Dar es Salaam.

Mhe. Kairuki amesema Mfumo wa HCIMS awali ulikuwa unapatikana Ofisi ya Rais–Utumishi pekee, lakini baadae ukakasimishwa kwa Maafisa Utumishi lakini sasa lengo ni kuwafikia watumishi wa umma waweze kuona taarifa zao ili kupata taarifa sahihi na za uhakika katika kanzidata. 

Amesema Tovuti ya Watumishi, Watumishi Portal, imeanzishwa maalum ili watumishi wa umma wajisajili kupitia tovuti ya Ofisi ya Rais-Utumishi yenye anuani www.utumishi.go.tz na kuona taarifa zao za msingi.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na viongozi na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni-Kata ya Kawe (hawapo pichani) leo alipofanya ziara ya kikazi  katika Kata hiyo ili kupokea maoni, ushauri na kusikiliza kero za watumishi wa umma Jijini Dar es Salaam. 
 Mhudumu wa Afya kutoka Hospitali ya Magomeni Bi. Rukia Mkapa akitoa malalamiko yake wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) wakati wa kikao kazi na watumishi wa Kata ya Kawe kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mwalimu Paschal Mugayana kutoka shule ya Sekondari ya Njechele  akitoa malalamiko yake wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) wakati wa kikao kazi na watumishi wa umma wa Kata ya Kawe kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.


 Sehemu ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni-Kata ya Kawe wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) wakati wa kikao kazi na watumishi hao kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.



TANAPA YATOA TUZO YA HESHIMA YA UTUNZAJI WA SOKWE KWA DKT. JANE GOODALL

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii. 

Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Shirika la Hifadhi za Tanzania TANAPA, limempatia tuzo nne za Heshima, mwanasayansi na mtafiti wa kimataifa Dkt. Jane Goodall. Dkt. Jane amekabidhiwa tuzo mapema leo na Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Magembe ambazo ni kinyago cha Sokwe, Kitenge, cheti cha heshima na ngao. 

Tuzo hiyo ya heshima imetolewa maalumu kwa kutambua mchango wake katika masuala ya utafiti na uhifadhi wa Sokwe kwenye hifadhi ya taifa ya Gombe ambao ameufanya kwa zaidi ya miaka 60. Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji tuzo hizo, Waziri wa Magembe amesema, Tanzania ni nchi ya kwanza ya uhifadhi katika bara Africa. 

Katika hifadhi zetu za taifa za wanyama mbali mbali ambazo ziko 16, ziko pia, hifadhi za taifa mbili, Gombe na Mahale ambazo wanyama wanaohifadhiwa humo kwa sehemu kubwa ni Sokwe ambapo hata katika dunia hizo mbili ndio hifadhi nzuri kupita zote. 

Amesema, Kazi kubwa iliyofanywa na mtafiti huyo imeiwezesha jamii kugundua kuwa, Sokwe, wanajitambua na kushirikiana. Wao kama wanyama, wana hisia zao kama viumbe na kama binadamu. 

Amesema, kabla ya utafiti huo wa Sokwe, na katika ulimwengu wa sayansi binadamu ndio waliokuwa wa wanahisiwa kuwa ndio wenye hisia na kushirikiana kama viumbe wenye akili sana kumbe hata Sokwe kwani wao pia wanatumia nyenzo katika maisha yao. 

Ameongeza kuwa tafiti anazofanya zimekusanya takwimu zenye maana kubwa sana katika uhifadhi wa Sokwe na pia katika uhifadhi wa wanyama pori. "Kwa mchango wake huu alioutoa, kidunia, kimataifa lakini kwa Tanzania kutoa mchango huu, tumeamua kumtunukia tuzo katika uhifadhi wa wanyamapori na zaidi Sokwe" amesema Waziri Maghembe. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia), akimkabidhi Tuzo ya Uhifadhi Wanyama aina ya Sokwe, Dkt. Jane Goodall, aliyekuwa akifanya utafiti wa Wanyama hao kwa miaka 60 katika hifadhi mbalimbali na baadaye kujikita katika Hifadhi ya Gombe. Picha zote na Kajunason Blog/Cathbert Kajuna. Dkt. Jane Goodall akionyesha cheti chake cha kutambua mchango wake katika Uhifadhi Wanyama aina ya Sokwe. Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe, akimkabidhi Tuzo ya Uhifadhi Wanyama aina ya Sokwe, Dkt. Jane Goodall, aliyekuwa akifanya utafiti wa Wanyama hao kwa miaka 60 katika hifadhi mbalimbali na baadaye kujikita katika Hifadhi ya Gombe. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tanapa, George Waitara na Bi. Gertude Mongella. 
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe Profesa Maghembe akizungumza wakati wa hafla ugawaji wa tuzo kwa Dk. Jane Goodall ambaye ametoa mchango mkubwa kwenye sekta ya uhifadhi na kubainisha tabia za sokwe ambazo watu wengi hawazijui. Profesa Maghembe aliongeza kuwa mtafiti huyo ambaye ni raia wa Uingereza amebainisha katika tafiti zake kwamba sokwe wana fikiri na wana hisia kama walivyo binadamu. Picha zote na Kajunason Blog/Cathbert Kajuna.  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Alan Kijazi akitoa machache wakati wa hafla ya ugawaji wa tuzo kwa Dk. Jane Goodall ambaye ni muhifadhi Wanyama aina ya Sokwe aliyekuwa akifanya utafiti wa Wanyama hao kwa miaka 60. 

VOA Swahili has uploaded Zulia Jekundu S1 Ep 131: Madonna, Migos, Rob Kardashian, na Blue Ivy

Dkt. Mwakyembe: Everton Yaipaisha Tanzania Kimataifa

TANAPA YAMPATIA DKT. JANE GOODALL TUZO MAALUM YA UTAFITI WA MIAKA 60 YA MAISHA YA SOKWE TANZANIA

$
0
0
Na Richard Mwaikenda
Dkt. Jane Goodal ambaye ni raia wa Uingereza alianza utafiti katika Hifadhi ya Gombe mnamo miaka ya 60 akiwa na umri wa miaka 26.
Katika utafiti wake amegundua mambo mengi ikiwemo jinsi Sokwe wanavyojitambua, kuwa na hisia na jinsi wanavyoishi kwa ushirikiano kama walivyo binadamu.
Akizungumza katika hafla hiyo Dkt Goodal anasema wakati anaanza kufanya utafiti ilikuwa vigumu Sokwe hao kumkaribia kwani walikuwa wanamuogopa na ilikuwa ni mara ya kwanza kwao kumuona mtu mweupe, lakini alifanya jitihada hadi wakamzoea na kuanza kumsogelea na kumuona mtu wao wa karibu.
Anasema alitumia mbinu mbalimbali kama vile kuwapatia ndizi na vyakula vingine hadi wakamzoea.
Wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Chuo cha Utalii katikati ya jiji la Dar es Salaam, viongozi na wageni waalikwa walipata wasaa wa kuangalia picha mbalimbali za matukio ya sokwe wakiwa na Jane Goodall.
Katika utafiti wake amefanikiwa kuanzisha chuo na kutunga vitabu pamoja na video zinazoelezea maisha yake na Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma.
Katika hafla hiyo walihudhuria Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, Mwenyekiti wa Bodi ya Tanapa, Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali George Waitara, Mwanasiasa Mkongwe Getrude Mongela, Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Goodall, Mhe. Lembeli pamoja na mabalozi mbalimbali  na waalikwa wengine. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kushoto) akimkabidhi  Dk. Jane Goodall tuzo maalumu kwa kutambua mchango wake wa utafiti wa miaka 60 wa maisha ya Sokwe  pamoja na uhifadhi wa wanyama wengine kwenye hifadhi ya Gombe, mkoani Kigoma  katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Tuzo hiyo iliandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa). Habari zaidi zitaletwa punde. (NA  RICHARD MWAIKENDA-KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
Dk. Jane Goodall akikabidhiwa cheti cha kutambua mchango wake kwa Tanzania kwa kuhifadhi Sokwe na wanayama wengine
 Dkt. Jane Goodall akipatiwa pia zawadi ya kinyago cha Sokwe
 Dkt. Jane Goodall akikabidhiwa picha ya Sokwe
 Mama Mongela akimvisha Dkt. Jane Goodall zawadi ya vitenge.

MASANJA MKANDAMIZAJI IN DALLAS, TEXAS, THIS SATURDAY

Viewing all 109973 articles
Browse latest View live




Latest Images