Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110153 articles
Browse latest View live

TANZIA: TAARIFA YA KIFO CHA PATRICIA NDENENGO SHANG'A WA MLALAKUA DARAJANI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Familia ya marehemu Mzee Michael Shang'a ya Mikocheni Mlalakua darajani jijini Dar es salaam inasikitika kutangaza kifo cha dada yao Patricia Ndenengo Shang'a kilichitotokea Alhamisi asubuhi hapo nyumbani.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika Jumamosi.
Msiba upo hapo hapo nyumbani Mikocheni Mlalakua darajani. Habari ziwafikie ndugu, jamaa, marafiki na majirani popote pale walipo.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI  PEMA PEPONI-AMEN.

MHENGA WA HARAKA HARAKA HAINA BARAKA JIJINI MBEYA

Meya wa Jiji Isaya Mwita atembelea miradi ya maendeleo

$
0
0
CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI

MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita leo amefanya ziara ya kutembelea miradi ya Maendeleo ya jiji ambapo ameridhishwa na vikundi vinavyo tengeneza mkaa kwa kutumia malighafi ambapo amesema itasaidia kupunguza uchafu uliopo kwenye maeneo mbalimbali na kuliweka jiji katika hali ya usafi.

Ziara hiyo ambayo imehusisha Kamati ya Fedha ya Halmashauri ya Jiji, ilitembelea vikundi vya Maendeleo ya ujasiriamali cha Upendo Smart kilichopo mtaa wa Kilimahewa Kata ya Tandika kinachojihusisha na uzalishaji wa mkaa mbadala ( mkaa poa).

Aidha mbali na kikundi hicho Meya Mwita pia amejionea shuguli za uzalishaji wa mkaa unaofanywa na kikundi cha Maendeleo cha Mwangaza Vikoba kilichopo Pugu stesheni jijini hapa.

Akizungumza na wanakikundi hao, Meya Mwita amesema kuwa vikundi hivyo vinafanya kazi kubwa kutokana na ubunifu walionao jambo ambalo litasaidia kuweka jiji kwenye hali ya usafi. 

Jengo la mradi wa viwanda vidogo vidogo lililopo eneo la Karakana Mwananyamala jijini Dar es Salaam. Awamu ya kwanza ya jingo hilo limepangwa kutumia shilingi milioni 190, ambapo inatarajiwa mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu utakuwa umekamilika kwa asilimia 82.(Picha zote na Christina Mwagala, Ofisi ya Meya wa jiji) 
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita mwenye shati la kijivu akitoa maelekezo kwa maofisa Utumishi wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam leo alipofanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo ya jiji karakana ya Mwananyamala jijini hapa. 
Mhandisi katika Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Swalehe Nyenye akifafanua jambo kwa Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita alipofanya ziara ya kutembelea ujenzi wa viwanda vidogo Karakana ya Mwananyamala. 
Mkurugenzi wa kampuni ya Kuja na Kushoka tool Manufucture Leodard Kushoka akitoa maelezo jinsi namna ambavyo mashine ya kutengenezea nishati ya mkaa kwa kutumia malighafi inavyofanya kazi wakati wa ziara waliofanya kwenye kikundi hicho kilichopo Tandika. Wa kwanza kulia ni Diwani wa Kata ya Segerea Pratrick Asenga. 
Mashine inayotumika kutengeneza nishati ya mkaa 

DC.MNDEME AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA NA KUVIFUNGIA VITUO NANE VYA MAFUTA AKISHIRIKIANA NA TRA DODOMA MJINI

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Mh.Christina Mndeme leo amefanya ukaguzi kwenye vituo vya mafuta ili kuona kama wafanyabiashara ya kuuza mafuta wanafuata sheria na taratibu za utoaji risiti na ulipaji kodi kwa kufunga mashine sahihi ya utoaji risiti iliyofungwa moja kwa moja kwenye pampu au mita ya mafuta. 

Katika ZIARA hiyo Kati ya vituo 9 alivyovitembelea amegundua kituo kimoja tu ndiyo kinafuata sheria na kuchukua hatua ya kuvifungia vituo nane (08).

Kazi hiyo imefanyika kwa kushirikiana na maafisa wa TRA Dodoma Mjini. Tunatekeleza kwa Hapa Kazi Tu, Lipa kodi kwa Maendeleo ya Taifa letu.

Pichani kushoto ni  Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Mh.Christina Mndeme akishirikiana na Ofisa wa TRA kukifungia moja ya kituo cha mafuta mkoani humo kilichobainika kutofuata sheria na taratibu za utoaji risiti na ulipaji kodi kwa kufunga mashine sahihi ya utoaji risiti iliyofungwa moja kwa moja kwenye pampu au mita ya mafuta.
Wasimamizi wa kituo wakipewa maelekezo baada ya kituo chao cha mafuta kufungiwa

MAGAZETI YA IJUMAA LEO JULY 14,2017

WAZIRI MKUU ATEMBELEA MRADI WA KUSAFIRISHA UMEME LINDI

$
0
0
* Asema changamoto ya kukatika umeme Mkoa wa Lindi kuwa historia 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema changamoto ya kukatika umeme katika mkoa wa Lindi kuwa historia baada ya kukamilika kwa mradi wa kusafirisha umeme wa kilovolti 132 Mtwara-Lindi.                             
Amesema hayo leo (Alhamisi, Julai 13, 2017) alipotembelea mradi huo wa kuzalisha umeme unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi. 
Waziri Mkuu amesema kukamilika kwa mradi huo uliogharimu sh. bilioni 16 kutamaliza changamoto ya upatikanaji wa umeme katika mkoa wa Lindi. 
Amesema mkakati wa Serikali ni kuongeza kiwango cha uzalishaji wa umeme ili Watanzania wapate umeme mwingi utakaosambazwa hadi vijijini kwa gharama nafuu. 
“Mikoa wa Lindi ulikuwa na shida kubwa ya kukatika kwa umeme, kukamilika kwa mradi huu ni mkombozi kwetu, tunawakaribisha wawekezaji waje kuwekeza kwa sababu sasa tunanishati ya uhakika.”
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Prof. James Mdoe, wakati alipotembelea mradi wa kuzalisha umeme unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne (katikati) ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Nape Mnauye.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipokea maelezo ya mradi wa kuzalisha umeme unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi kutoka kwa Mhandisi Jafary Msuya, wakati alipotembelea mradi huo unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipokea maelezo ya mradi wa kuzalisha umeme unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi kutoka kwa Mhandisi Ferdinand Mwinje,wakati akikagua mradi huo unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiongea na wananchi, wakati alipotembelea mradi wa kuzalisha umeme wa Mahumbika, unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)​

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AMJULIA HALI MTOTO WA RAIS MSTAAFU KHALFAN KIKWETE

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana amemjulia hali mtoto wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Khalfan Kikwete,  ambaye amelazwa katika wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam. Kulia ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mkewe Salma Kikwete.
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.

TAESA IKISHIRIKIANA NA ILO YAANDAA PROGRAMU ENDELEVU YA MIAKA MITATU YA KUWANOA WANAFUNZI WA VYUO KUWAJENGEA UWEZO WA KUSHIRIKI KATIKA KAZI KWA VITENDO

$
0
0

Pichani kati ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa huduma za ajira, Saneslaus Chandaruba akizungumza jambo mbele ya Wanafunzi wa vyuo mbalimbali,waliohudhuria programu endelevu ya miaka mitatu nchini,iliyohusu jinsi ya kuwajengea Misingi bora wanavyuo ya ufanisi wa kazi katika ushiriki wa kazi kwa vitendo katika ofisi au kampuni tofauti Nchini (intern/ Field work).Programu hiyo imefanyika jijini na kuandaliwa na Wakala wa Huduma za Ajira Tz (TaESA ) kwa kushirikiana na Shirika la kazi la Kimataifa (ILO). Pichani kushoto ni Mkurugenzi wa huduma za ajira Tanzania ( TaESA),Kisa Vivian Kilindu na mwisho kulia ni Mwakilishi kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Paulina Mabuga
Baadhi ya Wanafunzi wa vyuo hao wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakizungumzwa kwenye Programu hiyo endelevu ya miaka mitatu nchini,iliyohusu jinsi ya kuwajengea Misingi bora wanavyuo ya ufanisi wa kazi katika ushiriki wa kazi kwa vitendo katika ofisi au kampuni tofauti Nchini (intern/ Field work).Programu hiyo imefanyika jijini na kuandaliwa na Wakala wa Huduma za Ajira Tz (TaESA ) kwa kushirikiana na Shirika la kazi la Kimataifa (ILO).
Pichani baadhi ya Wanafunzi wa vyuo mbalimbali,waliohudhuria Programu hiyo endelevu ya miaka mitatu nchini,iliyohusu jinsi ya kuwajengea Misingi bora wanavyuo ya ufanisi wa kazi katika ushiriki wa kazi kwa vitendo katika ofisi au kampuni tofauti Nchini (intern/ Field work).Programu hiyo imefanyika jijini na kuandaliwa na Wakala wa Huduma za Ajira Tz (TaESA ) kwa kushirikiana na Shirika la kazi la Kimataifa (ILO)

Ulanga wapongezwa kwa kuibua na kuhamasisha miradi yenye manufaa kwa wananchi.

$
0
0
Na Sekela Mwasubila. Afisa habari Ulanga
Katibu Tawala Msaidizi Bw. Noel Kazimoto ametoa pongezi hizo wakati wa ziara yake ya ukaguzi na uhamasishaji na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo ndani ya wilaya akiwa na viongozi kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI. 
 Bw. Kazimoto aliwapongeza viongozi wa kijiji hicho na watu wote waliochangia ujenzi huo hadi hatua hiyo na kuwakumbusha kusoma mapato na matumizi ya ujenzi huo na kuwashauri kuendelea kubuni miradi yenye manufaa kwa wananchi. 
 Hata hivyo Bw. Kazimoto aliwataka wakuu wa Idara kusimamia miradi yote ndani ya wilaya na kufanya ufuatiliaji katika ngazi za chini ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma stahiki na kwa wakati. 
 Akitoa taarifa ya ujenzi wa ofisi ya kijiji cha Safari Road Afisa Mtendaji wa Kijiji Bi. Sophia Haule amesema kuwa ujenzi huo uliibuliwa na wananchi na viongozi kutokana na kukosekana kwa ofisi ya kijiji na kuwalazimu kupanga ofisi ambayo ni finyu na gharama. 
Aliongeza kuwa ujenzi umefanikiwa kutokana na msaada wa nguvu za wananchi, fedha za Halmashauri na fedha za mfuko wa jimbo ambapo hatua iliyofikia ni umaliziaji na uwekaji wa samani. 
 Ziara ya ufuatiliaji wa miradi imefanyika wilayani Ulanga na mkoa kwa ujumla ikihusisha viongozi kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI na ofisi ya Katibu Tawala Mkoa ambapo kwa wilaya ya Ulanga walitembelea miradi ya ujenzi wa vyoo shule ya Msingi Mahenge Mjini, ujenzi wa soko la Kijiji cha Mahenge, maabara shule ya sekondari Mahenge na ujenzi wa Ofisi ya Kijiji cha Safari Road.

Bibi Beatrice Msomisi kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI akikagua jengo la ofisi ya Kijiji cha Safari Road iliyopo katika kata ya Mahenge Mjini alipofanya ziara ya ukaguzi wa miradi wilayani hivi karibuni.

Wakuu wa Idara wa Halmashauri Ya wilaya ya Ulanga wakiwasikiliza kwa umakini watumishi kutoka Ofisi ya Katibu Tawala Morogoro na Ofisi ya Rais TAMISEMI

GOR MAHIA WASHUKURU MASHABIKI WA TANZANIA KWA KUWASHANGILIA

Mbunge wa Morogoro Mjini akabidhi milioni 20 za Biko kwa mshindi wao

$
0
0
MBUNGE wa Morogoro Mjini, Mheshimiwa Abdulaziz Abood, leo mjini hapa, amemkabidhi mshindi wa Sh Milioni 20 wa Bahati Nasibu ya Biko, Elizabeth Damian, aliyetangazwa mshindi katika droo ya 22 ya bahati nasibu hiyo inayojulikana pia kama ‘Ijue Nguvu ya Buku’ iliyofanyika juzi Jumatano, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika makabidhiano ya Sh Milioni 20 mjini Morogoro jana, Mbunge Abdulaziz, alisema bahati nasibu ni mchezo unaoweza kutoa fursa nzuri kiuchumi, huku akimtaka mshindi huyo azitumie vizuri pesa zake ili ziweze kumnufaisha kiuchumi.

Alisema kwamba jinsi mchezo wa Biko unavyochezeshwa ni sehemu muafaka ya kuhakikisha kwamba kila mtu anatumia vyema fursa ya kupiga hatua kiuchumi kwa namna moja ama nyingine, hivyo wananchi wake wa Morogoro na Watanzania wote kwa ujumla waendelee kucheza ili wavune fedha za ushindi.

“Wakati nawapongeza Biko kwa kubuni michezo hii inayotoa mamilioni kwenu washindi, lakini pia nakupongeza wewe mwananchi wangu wa Morogoro kwa kuwa kati ya wachezaji wenye bahati kubwa kiasi cha leo kukabidhiwa Sh Milioni 20,” Alisema.

Akizungumzia ushindi wake, Elizabeth aliyekabidhiwa fedha zake katika benki ya NMB, mjini Morogoro, alisema hakuamini kama angeweza kuibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 20 kutoka Biko, jambo linalomfanya furaha yake isielezeke.

“Kwa kweli siamini kama leo nimekabidhiwa fedha zangu kiasi cha Sh Milioni 20 nilizopata kutoka kwa Biko, hivyo nawakumbusha Watanzania wenzangu kucheza kwa wingi bahati nasibu hii maana ushindi upo nje nje na fedha zangu nitazitumia vizuri kwa mambo mengi kama vile biashara na ujenzi wa nyumba,” Alisema.
Mbunge wa Morogoro Mjini, Mheshimiwa Abdulaziz Abood, kushoto akimkabidhi hundi ya Sh Milioni 20 mshindi wa Biko Morogoro saa chache kabla ya kukabidhiwa fedha taslimu katika benki ya NMB, mjini hapa jana. Anayeshuhudia ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven wa pili kutoka kulia.
Mbunge wa Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood wa tatu kutoka kulia akimkabidhi jumla ya Sh Milioni 20 mshindi wa Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku, mshindi wa Morogoro Mjini, Elizabeth Damian wa pili kutoka kushoto. Wa kwanza kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven wakati wanamkabidhi mshindi huyo katika Tawi la benki ya NMB Morogoro jana.
Mshindi wa Shilingi Milioni 20 wa Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku', Elizabeth Damian baada ya kukabidhiwa jana mjini Morogoro.


SUMAYE AKILI KATIKA UONGOZI WAKE KUWA VIWANDA VILIKUFA

$
0
0
 Waziri Mkuu Mstaafu ,Fredrick Sumaye akizungumza na Waandishi wa habari juu ya utendaji kazi wa serikali ya awamu ya tano na kujikosoa yeye kuwa  katika utawala wake Viwanda vilikufa hivyo anashangaa kuona Rais Magufuli akiviamsha kama uyoga.
 Sehemu ya Viongozi wa kanda ya Pwani wa CHADEMA wakifuatilia mkutano huo wa Waandishi wa habari
 Sehemu ya Waandishi wa habari walioshiriki mkutano huo na Waandishi wa habari

 Katibu wa CHADEMA kanda ya Pwani Juma Mabina akizungumza katika mkutano wake na Waandishi wa habri jijini Dar es Salaam leo
Sehemu ya Waandishi wa habari walioshiriki mkutano huo na Waandishi wa habari.

NMB YATETA JAMBO NA WALIMU KATIKA SIKU YA WALIMU MKOA WA DAR ES SALAAM

$
0
0
Meneja wa benki ya NMB kanda ya Dar es Salaam ,Vicky Bishibo akizungumza na walimu wakati wa mkutano wa siku ya walimu katika mkoa wa Dar es Salaam na benki hiyo uliofanyika mapema leo Sinza,jijini Dar.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini(TCU), Prof Eleuther Mwageni akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Walimu na Benki ya NMB wakati wa mkutano mkuu wa siku ya walimu na benki hiyo jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi Mkuu wa wateja wadogo wadogo na wakati wa NMB,Abdulmajid Nsekela akizungumza na walimu juu ya huduma mpya za NMB ambazo zinaweza kuwasaidia katika kujiongeza kipato na kulea familia kwa uraisi.
 Sehemu ya walimu walioshiriki mkutano huo ambao uliweza kuwakutanisha walimu kutoka Wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam.

TAKUKURU YAMTIA MBARONI DIWANI WA CHADEMA KATA YA MSIGANI KWA TUHUMA ZA RUSHWA

$
0
0
--
Diwani Kata ya Msigani, Ubungo, Israel Mushi ( 48 ) na Mrasimu ramani wa Manispaa ya Ubungo, Francis Mwanjela Peter ( 28 ) wamekamatwa na Tasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),wilaya ya Kinondoni kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa  Sh.5,000,000/=.

kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa  TAKUKURU wilaya ya  Kinondoni Teddy Mjangira, amesema kuwa Watuhumiwa walikamatwa Julai 12, 2017 baada ya kupokea kiasi hicho cha fedha toka kwa mwananchi ambaye jina lake limehifadhiwa na ambaye mbali na kutoa kiasi hicho cha pesa alitakiwa  na watuhumiwa kuwapa  rushwa ya Sh.10,000,000/=

Inadawaiwa Watuhumiwa walishawishi na kupokea rushwa ili waweze kutoa ushawishi kwa wajumbe wa kamati ya mipango miji  inashughulikia maombi ya kubadilisha michoro, kubadilisha matumizi ya kiwanja na kupitisha kibali cha ujenzi katika Manispaa ya Ubungo.

Uchunguzi wa tuhuma unaendelea na Watuhumiwa ambao wanatuhumiwa kutenda makosa kinyume na kifungu namba 15 cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007 wamepewa dhamana.

Mkuu wa TAKUKURU (M) Kinondoni Bi.T. MNJAGIRA anawaasa Viongozi wote wa Umma, Wanasiasa na Watumishi wote wa Serikali, kuheshimu nyadhifa zao na kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria bila kujihusisha na vitendo vya Rushwa. Pia, anatoa wito kwa  Wananchi wote kuendelea kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU kwa kuwafichua wale wote wanaojihusisha na  vitendo vya rushwa ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria, Kwa kufanya hivyo, tutakuwa tumezuia vitendo hivyo visiendelee kujitokeza katika Jamii
 

ZANTEL YASHIRIKI KATIKA MKUTANO WA MOBILE 360 AFRICA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Meneja wa Kitengo cha chapa na Mawasiliano Zantel, Rukia Mtingwa (kushoto) akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wakuu wa vitengo vya mawasiliano kutoka kampuni mbalimbali Afrika Mashariki wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kukuza matumizi ya teknolojia ya simu ili kufikia maendeleo endelevu ulioandaliwa GSMA Mobile 360 Africa kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jana jijini Dar es salaam. Katikati ni Meneja wa Mawasiliano wa Tigo Tanzania Woinde Sishael na Kulia ni Meneja Ushirikiano wa Masoko wa Africa-GSMA, Adreni Mhuhura.
Meneja wa Kitengo cha chapa na Mawasiliano Zantel, Rukia Mtingwa (kulia) akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wakuu wa vitengo vya mawasiliano kutoka kampuni mbalimbali Afrika Mashariki wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kukuza matumizi ya teknolojia ya simu ili kufikia maendeleo endelevu ulioandaliwa GSMA Mobile 360 Africa kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jana jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mwakilishi kutoka Idara ya Mambo ya nje na biashara Australia Dan Woods.
Meneja wa Kitengo cha chapa na Mawasiliano Zantel, Rukia Mtingwa (katikati) akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wakuu wa vitengo vya mawasiliano kutoka kampuni mbalimbali Afrika Mashariki wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kukuza matumizi ya teknolojia ya simu ili kufikia maendeleo endelevu ulioandaliwa GSMA Mobile 360 Africa kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jana jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mwakilishi kutoka Idara ya Mambo ya nje na biashara Australia Dan Woods na Kulia ni Meneja Mawasiliano wa Safaricom Eunice Mumma.
Mwakilishi kutoka Idara ya Mambo ya nje na biashara Australia Dan Woods akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wakuu wa vitengo vya mawasiliano kutoka kampuni mbalimbali Afrika Mashariki wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kukuza matumizi ya teknolojia ya simu ili kufikia maendeleo endelevu ulioandaliwa GSMA Mobile 360 Africa kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jana jijini Dar es salaam Pamoja nae ni Meneja wa Kitengo cha chapa na Mawasiliano Zantel, Rukia Mtingwa. 

MAONESHO YA KIMATAIFA YA 41 (SABA SABA) YAFUNGWA RASMI LEO JIJINI DAR

$
0
0
 Waziri wa  Biashara, Viwanda na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (MB) Mhe. Balozi Amina Salum Ali akizungumza wakati wa kuyafunga maonesho ya Kimataifa ya 41 ya Biashara ya Dar es Salaam leo Katika Viwanja vya JK Nyerere ,Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa  Biashara, Viwanda na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (MB) Mhe. Balozi Amina Salum Ali akifurahia zawadi ya begi lililotengenezwa kwa bidhaa za ngozi ya Tanzania.
 Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji (Biashara na uwekezaji) Prof. Adolf Mkenda akizungumza wakati wa hafla ya kufunga maonesho ya Kimataifa ya 41 ya Biashara ya Dar es Salaam Leo Katika Viwanja vya JK Nyerere ,Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bw. Edwin Rutageruka akitoa maelezo mafupi kuhusu maonesho ya Kimataifa ya 41 ya Biashara ya Dar es Salaam.
 .Kikundi cha kwaya ya TOT kikitumbuiza wakati wa hafla ya kufunga maonesho ya Kimataifa ya 41 ya Biashara ya Dar es Salaam Leo Katika Viwanja vya JK Nyerere ,Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.

Serikali kupitia upya mikataba ya uwanja wa ndege pamoja na kufumua uongozi uliopo.

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

SERIKALI imesema kuwa itapitia mikataba yote katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere pamoja na kufanya mabadiliko ya uongozi huo kutokana na kufanya kazi kwa mazoea.

Hayo ameyasema leo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa wakati alipotembelea uwanja wa ndege huo baada ya kuwepo kwa taarifa ya wasafiri wakichukua muda mrefu kutoka uwanjani hapo.

Mbarawa amesema kuwa watu wanapoingia kutoka nje ya nchi wanaanza kusoma Tanzania ilivyo ikiwemo na uwanja wan degu kukaa kwa muda mrefu kutokana na mifumo ya watu kushindwa kujipanga.

Amesema kuwa mikataba katika uwanja huo wameingia wale watu waliofanya mikataba hawakuangalia masilahi ya nchi ndio maana mapato yanakuwa kidogo tofauti na ilivyo katika uhalisia.

Aidha amesema kuwa watakaa kikao kimoja kati ya watoa huduma katika uwanja wa mwalimu Julius Nyerere wakiwemo Idara ya Uhamiaji pamoja na benki ambako ndio inafanya watu wakae muda mrefu.

Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Salim Msangi amesema kuwa wanazifanyia kazi changamoto ambazo Wazari amezianisha licha ya kuwa na miundombinu finyu.

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuangalia utoaji huduma katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Salim Msangi akizungumza na waandishi wa habari juu Uboreshaji wa Huduma katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere leo.
Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akipata maelezo KaimuMkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Josepp Nyahende alipofanya ziara katika uwanja huo leo .
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akipata maelezo Afisa Maidizi wa Ushuru uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Hezron Gibe jinsi wanafanya kazi katika uwanja huo.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akipewa maelezo na watoa huduma Ushuru uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere leo .

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA WIZARA YA ARDHI,NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

MASAUNI AWATAKA MAAFISA UHAMIAJI, POLISI KUONGEZA KASI KUCHUNGUZA NA KUWAKAMATA WAHAMIAJI HARAMU TANGA

$
0
0


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akizungumza na Viongozi wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara yake, mkoani Tanga wakati kiongozi huyo alipofanya ziara yake kikazi mkoani humo. Katika mazungumzo yao, Masauni aliwahasa viongozi hao kuhakikisha wanafanya kazi kwa kujituma zaidi na kuwahakikishia kero zote walizompa atahakikisha anazifanyia kazi. Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Benedict Wakulyamba.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kushoto) akimsikiliza  Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela (katikati) alipokua anatoa taarifa ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo, kabla ya kiongozi huyo kuanza ziara yake mkoani humo. Katika mazungumzo yao, Masauni aliwataka Maafisa Uhamiaji pamoja na Polisi kuongeza kasi ya kutafuta mizizi ya wahamiaji haramu mkoani humo. Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Benedict Wakuliamba. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akitoka kulikagua jengo la Ofisi ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Tanga ambalo linahitaji matengenezo ili kulirudisha katika hali yake ya kawaida. Hata hivyo, Masauni alimuagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba (kulia) kuhakikisha jengo hilo linatengenezwa haraka iwezekavyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimfafanulia jambo Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela (katikati) na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Zena Saidi, kabla ya kiongozi huyo kuanza ziara yake mkoani humo. Katika mazungumzo yao ambayo yalifanyika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa huyo, Masauni aliwataka maafisa uhamiaji pamoja na Polisi kuongeza kasi ya kutafuta mizizi ya wahamiaji haramu mkoani humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

WAZIRI MWIGULU AFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU BALOZI WA MAREKANI NCHINI TANZANIA

$
0
0


Naibu Balozi wa Marekani nchini, Dk. Inmi Patterson, akizungumza na Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, alipomtembelea Waziri huyo kujadili Masuala ya Ulinzi na Usalama, jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Siasa na Uchumi wa Ubalozi huo,Marilyn Gayton na kushoto ni Katibu wa Waziri,Nelson Kaminyoge. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba, akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Balozi wa Marekani nchini, Dk. Inmi Patterson(kulia), baada ya kumaliza mazungumzo yaliyohusu Masuala ya Ulinzi na Usalama.Kikao hicho kimefanyika leo jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Viewing all 110153 articles
Browse latest View live




Latest Images