Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1802 | 1803 | (Page 1804) | 1805 | 1806 | .... | 3284 | newer

  0 0

  UONGOZI wa timu ya mpira wa miguu ya Everton kutoka nchini Uingereza imeridhishwa na huduma inayotolewa kwa wagonjwa wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ikiwemo mabusha na matende hapa nchini. 
  Hayo yamezungumzwa na mmoja wa viongozi wa Everton Bw. Darren Griffiths ambao ni washiriki katika kuchangia huduma ya magonjwa hayo hapa nchini ambaye ameongozana na timu yake ili kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Gor Mahia kutoka chini Kenya.
  “Tunayo furaha kuona wagonjwa wengi waliokuwa wanaumwa mabusha na metende nchini Tanzania kwa sasa wamepona kabisa na tunahaidi kuwa na Wizara ya afya bega kwa bega katika kutokomeza magonjwa haya” alisema Bw. Darren Griffiths
  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kinga Wizara ya Afya Dkt. Vida Mmbaga amesema kuwa kutokana na ushiriki wa Everton katika kuchangia utoaji wa Huduma ya kutibu ugonjwa huo wamefanikiwa kupata ujuzi wa upasuaji hasa kwa wagonjwa wa mabusha na matende hapa nchini.


  Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Vida Mmbaga akisisitiza juu ya baadhi ya juhudi zilizofanywa na Serikali kupitia Mpango wa taifa wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele mbele ya viongozi kutoka timu ya Everton na mwakilishi kutoka Liverpool katika zoezi lililofanyika leo jijini Dar Es salaam.
  Mratibu wa Mpango wa Taifa wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt Upendo Mwingira akibadilishana Mawazo na Mwakilishi kutoka Liverpool wakati wa tukio la kusaidia waliokuwa wagonjwa wa mabusha na matende liliofanyika mapema leo jijini Dar es salaam. picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii. 
  Mmoja ya Viongozi kutoka timu ya Everton iliyopo ligi kuu nchini Uingereza na aliekuwa mchezaji wa timu hiyo Leon Osman akigawa zawadi kwa waliokuwa wagonjwa wa Matende na Mabusha katika zoezi la kuwasaidia lililofanyika leo jijini Dar Es salaam.
  Picha ya pamoja ya Viongozi kutoka timu ya Everton iliyopo ligi kuu nchini Uingereza, Viongozi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na waliokuwa wagonjwa wa Matende na Mabusha katika zoezi lakuwasaidia lililofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.  0 0


  Waajiri nchini wametakiwa kufanya uhakiki wa kina wa vyeti vya elimu kwa ajira mpya zitakazotolewa ili kuwa na watumishi wa umma wenye sifa zinazostahili katika utumishi wa umma.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) amesema hayo leo katika kikao kazi na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya  Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

  Mhe. Kairuki amesema uhakiki wa kina utasaidia sana kuepukana na kutojirudia tena kwa suala la watumishi wa umma wanaoghushi vyeti.
   “Jana tumetoa vibali vya ajira 10,184 kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Sekretarieti za Mikoa, Wakala za Serikali, pamoja na Taasisi na Mashirika ya Umma ili kujaza nafasi zilizoachwa na watumishi wa umma waliobainika kughushi vyeti vya elimu, hivyo napenda niwasisitize sana waajiri wote kufanya uhakiki wa kina ili tusiwe tena na watumishi wa umma wasiostahili katika orodha ya malipo” Mhe. Kairuki amesema.

  Waziri Kairuki amesisitiza kuwa zoezi la uhakiki ni endelevu ambapo lazima lifanyika pale mtumishi wa umma atakaporudi katika kituo cha kazi kutoka masomoni, na watakaorejea katika utumishi wa umma  baada ya likizo bila malipo au sababu nyingine.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na watumishi wa Wilaya ya Kinondoni (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya  kikazi katika wilaya hiyo leo Jijini Dar es Salaam.

  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally S. Happi akizungumza na watumishi wa umma wa wilaya ya Kinondoni leo (hawapo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) katika Wilaya hiyo kuzungumza na Watumishi wa Umma,  Jijini Dar es Salaam.
  Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni Bibi. Sixtha Kevin Komba akiwasilisha hoja wakati wa kikao kazi  kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) alipofanya ziara ya kikazi katika wilaya ya Kinondoni leo Jijini Dar es Salaam.
  Afisa Utumishi Mwandamizi kutoka Idara ya Ukuzaji Maadili Ofisi ya Rais- Utumishi Bi. Leyla Mavika akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya maadili katika Utumishi wa Umma wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) katika Wilaya ya Kinondoni leo Jijini Dar es Salaam.

  Mstahiki Meya Manispaa ya Kinondoni Mhe. Benjamini Sitta (kulia) akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) baada ya kupokea hoja za watumishi wa Umma wa Wilaya ya Kinondoni leo Jijini Dar es Salaam. Pichani- Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb)  na kushoto ni Mkurugenzi Manispaa ya Kinondoni Bw. Aron Kagurumjuli. Picha na: Genofeva Matemu - MAELEZO.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0


  0 0

  Guess who is Going to Hit the  Tanzania National Spelling Bee Competition 2017(TNSBC).
  We  provide a platform where learning is made fun and spiced up with a little healthy competition.
  Register your child or recommend a school through www.coconutfoundation.or.tz  Instagram @spellingbeetz Twitter @spellingbeetz
  We Inspire, We Empower  0 0


  0 0

   Maafisa wa Eminence Group wakimsikiliza mdau wa sekta ya mawasiliano aliyetembelea banda la Huawei katika katika kongamano la makampuni yaliyo katika sekta ya mawasiliano Afrika (Mobile 360 Conference 2017) ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Huawei Technologies Tanzania Bw Gao Mengdong wa pili kutoka kulia katika picha ya pamoja na maafisa kutoka Eminence Group katika kongamano la makampuni yaliyo katika sekta ya mawasiliano Afrika (Mobile 360 Conference 2017)

  0 0

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba aliyevaa suti nyeusi akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye  baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege Mjini Dodoma, kwa ajili ya kufungua Kikao cha Makamanda wa Jeshi hilo mapema leo asubuhi
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akiangalia kikundi cha ngoma mara baada ya kuwasili uwanjani hapo mapema leo asubuhi. 
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akiwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye wapili toka kulia, Kamishna wa Utawala na Fedha Michael Shija na Kamishna wa Utawala na Rasilimali watu Billy Mwakatage wakiimba wimbo wa Taifa mara baada ya kuingia kwenye ukumbi wa Mikutano wa LAPF kinapofanyika Kikao cha Makamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mapema leo asubuhi. 

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akisoma hotuba ya ufunguzi wa Kikao cha Makamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mapema leo asubuhi. 
   Sehemu ya Makamanda wa Mikoa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi mapema leo asubuhi. 


  0 0


  0 0
  0 0

   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Job Ndugai (kulia) akimkabidhi picha ya jengo la Bunge Rais Mstaafu wa Ireland ambae pia ni Mjumbe wa  “The Elders” Taasisi inayoshughulika na Amani, Haki za Binadamu na Huduma za Afya, Mhe. Mary Robinson katika tukio lililofanyika leo katika Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma.
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  (kulia)akizungumza wakati ugeni kutoka “The Elders” Taasisi inayoshughulika na Amani, Haki za Binadamu na Huduma za Afya ilipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, katikati ni Rais Mstaafu wa Ireland ambae pia ni Mjumbe kutoka Taasisi hiyo Mhe. Mary Robinson na kushoto ni Mjumbe wa Taasisi hiyo Mama Graca Michel
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimsikiliza Mjumbe wa  “The Elders” Taasisi inayoshughulika na Amani, Haki za Binadamu na Huduma za Afya Mama Graca Machel (kushoto) katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, katikati ni Rais Mstaafu wa Ireland ambae pia ni Mjumbe kutoka Taasisi hiyo Mhe. Mary Robinson 
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  akimsikiliza Rais Mstaafu wa Ireland (katikati) ambae pia ni Mjumbe wa “The Elders” Taasisi inayoshughulika na Amani, Haki za Binadamu na Huduma za Afya, Mhe. Mary Robinson, kulia ni Mjumbe wa Taasisi hiyo Mama  Graca Machel (kushoto) katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

  Na Dotto Mwaibale
  VIONGOZI wa dini wametakiwa kutumia taaluma waliyonayo kumsaidia Rais Dk. John Magufuli kuliletea taifa maendeleo na kuondokana na umaskini nchini.
  Mwito huo umetolewa na muhubiri wa kimataifa 'Mama Afrika' Dk.Nicku Kyungu wakati akihubiri katika kongamano la kimataifa la viongozi wa dini lililofanyika Kanisa la Naoith Pentekoste Church Makuburi jijini Dar es Salaam leo.
  Alisema viongozi wa dini waliopo katika makanisa wanataaluma mbalimbali hivyo mbali ya kuhubiri neno la mungu wanapaswa kutumia taaluma walizonazo kumsaidia Rais katika maendeleo ya nchi jambo litakalosaidia nchi kuondokana na umaskini na adui ujinga.
  Dk.Kyungu alisema katika imani Tanzania sasa imetoka katika uchanga na sasa inakwenda mbele na hilo ni jambo la kujivunia.
  Alisema nchi ya Tanzania imebarikiwa tangu uongozi wa baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamini Mkapa, Jakaya Kikwete na sasa Dk. John Magufuli.
  "Ili ni jambo la kujivunia kwa nchi kuwa na amani tangu wakati huo hadi leo hii na ndio maana tumeona ni vizuri tukafanya maombi ya shukrani ya kuliombea taifa na Rais wetu yatakayofanyika Jumamosi Uwanja wa Uhurua jijini Dar es Salaam kuanzia asubuhi" alisema Dk. Kyungu.
   Muhubiri wa kimataifa 'Mama Afrika' Dk.Nicku Kyungu  akihubiri katika kongamano la kitaifa la viongozi wa dini lililofanyika Kanisa la Naoith Pentekoste Church Makuburi  Ubungo jijini Dar es Salaam leo.

   Mchungaji Dk. William Kopwe wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania  (KKKT) Dodoma, akifundisha katika kongamano hilo.
   Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maombi hayo, Askofu Mkuu wa Naoith Pentekoste Church, Dk.David Mwasota akizungumza katika kongamano hilo.

   Mchungaji Timoth Joseph kutoka Nigeria alifundisha somo la watu kuwa waaminifu katika kila jambo. 

  0 0

  Naibu waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani amesema daraja la Mto Momba lenye urefu wa mita 75 litakalounganisha Mkoa wa Rukwa na Songwe litaanza kujengwa  mapema mwaka huu.

  Eng. Ngonyani ametoa kauli hiyo mara baada ya kukagua barabara ya Kasansa hadi Kilyamatundu na eneo litakapojengwa daraja la Momba na kusema kuwa Serikali imeshampata Mkandarasi atakajenga daraja hilo.

  “Serikali imeshatoa kiasi cha sh. Bilioni tatu  fedha hizo zimetusaidia kutangaza zabuni na kumpata mkandarasi, tayari Mkandarasi wa ujenzi huu ameshapatikana na mkataba wa makubaliano ya ujenzi umeshakamilika hivyo mkandarasi atausaini rasmi hivi karibuni,” amesema Eng. Ngonyani.

  Aidha, Eng.Ngonyani amemtaka Meneja Wa Wakala wa barabara (TANROADS) Mkoa wa Rukwa kuhakikisha anatoa ajira kwa wakazi waliopo kata ya Kipeta ambapo ujenzi wa daraja hilo utafanyika.

  Naye Mbunge wa Jimbo la Kwela Mhe. Ignas Malocha ameishukuru Serikali ya awamu ya tano ya Mhe. Dkt. John Magufuli kwa kutekeleza ahadi ya ujenzi wa daraja hilo ambalo kukamilika kwake kutawaletea maendeleo wakazi hao kwa vile litaufungua Mkoa wa Rukwa na kuunganisha na Songwe na Katavi.

  “Kukamilika kwa ujenzi wa daraja hili kutarahisisha usafirishaji wa mazao ya biashara kutoka mkoa wetu kwenda mikoa mingine inayopakana na mkoa huu na kuokoa maisha ya wananchi ambapo awali walikuwa wa wakiliwa na mamba na wengine kusombwa na maji wakati kuvuka kwenye mto huu,” amesisitiza Malocha.

   Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akielekea kukagua sehemu ambapo litajengwa Daraja la Momba litakalounganisha Mkoa wa Rukwa na Songwe .Kulia ni Meneja wa Wakala wa barabara  (TANROADS)Mkoa wa Rukwa  Eng. Msuka Mkina na Wa pili kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Kwela Mhe. Ignas Malocha.

   Meneja wa Wakala wa barabara(TANROADS), Mkoa wa Rukwa  Eng. Msuka Mkina (aliyenyoosha kidole) akimwonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa tatu kulia) eneo lipakapojengwa Daraja la Momba wakati alipokagua sehemu ambapo litajengwa Daraja hilo litakalounganisha Mkoa wa Rukwa na Songwe.

   Muonekano wa Sehemu ambapo daraja la Mto Momba litakapojengwa. Daraja hilo litakalounganisha Mkoa wa Rukwa na Songwe.

   Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Kulia) akitoa maelezo kwa wananchi wa kijiji cha Kilyamatundu kata ya Kipeta Mkoani Rukwa kuhusu  ujenzi wa daraja la Mto Momba litakalounganisha Mkoa wa Rukwa na Songwe.

  Wananchi wa kijiji cha Kilyamatundu kata ya Kipeta Mkoani Rukwa wakifurahi mara baada ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (hayupo picha) kutoa tamko la kupatikana kwa Mkandarasi atakayejenga daraja la Mto Momba litakalounganisha Mkoa wa Rukwa na Songwe.


  0 0

   Mtoto Lameck Charles (9) pamoja na mdogo wake Fredrick Charles (8) ni wanafunzi  wa shule ya Msingi Inteki wakiwa wanaonyesha mchezo wa sarakasi ndani ya stendi ndogo ya jijini Arusha  ikiwa ni sehemu ya kazi ambayo wanaifanya kipindi wakiwa likizo. 
  Watoto hawa ambao  walikutwa na kamera yetu walisema kuwa wamekuwa wakitumia kipaji hicho walichojifunza kutoka kwa kaka yao kujipatia fedha ya kununulia vitu vidogo vidogo pindi pale wanaporejea shuleni.
  Pembeni ni baadhi ya wananchi wakiwa wanawashuhudia watoto hao wakiendelea kuonyesha vipaji vyao. Wengi walipohojiwa walisema iko haja kwa wazazikutambua na kuendeleza vipaji vya watoto wao badala ya kuwaachia wanahangaika wenyewe. 
  Picha na Woinde Shizza, Arusha


  0 0


  Na Jumia Travel Tanzania
  Jumia kwa mara ya pili mfululizo imeorodheshwa na Taasisi ya Kiteknolojia ya Massachusetts (MIT) ya nchini Marekani kuwa ni miongoni mwa makampuni 50 bora yanayotumia teknolojia katika biashara ili kurahisisha utoaji na upatikanaji wa huduma.
  Kwenye orodha hiyo ambayo hujumuishwa makampuni makubwa ya kiteknolojia duniani kama vile Apple, Amazon, Facebook na Alibaba, Jumia kwa mwaka huu wa 2017 imetajwa kushika nafasi ya 44 kutokea nafasi ya 47 iliyoishika mwaka 2016.
  MIT imeiatambua Jumia ambayo ilianzishwa mwaka 2012 ikijulikana kama Africa Internet Group (AIG) kwamba ni miongoni mwa makampuni ya awali kuchipukia barani Afrika, ikiwa na thamani ya dola za Kimarekani bilioni moja kutoka dola za Kimarekani milioni 327 ambapo ilimjuisha Goldman Sachs kama mmojawapo wa wawekezaji wake.
  Ikiwa inajishughulisha na utoaji wa huduma mtandaoni kwenye maeneo kama vile manunuzi ya bidhaa, usafiri, chakula, makazi na magari ambazo zote zinatumia jina la Jumia, kampuni hiyo inapambana na changamoto za kufanya biashara kwa njia ya mtandao barani Afrika zikiwemo barabara zisizopitika kwa urahisi, wateja wasiotabirika, kukosekana kwa mtandao wa intaneti kwenye baadhi ya maeneo ambapo lengo kubwa ni kuwashawishi watu wa tabaka la kati kufanya matumizi.


  0 0


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amewapongeza wana kijiji cha Ghalunyangu kilichopo kata ya Makuro Wilayani Singida kwa uzalendo wa kujitolea nguvu kazi ya kuchimba mtaro wenye urefu wa mita 670 katika mradi wa maji kijijini hapo.
  Dkt Nchimbi ametoa pongezi hizo mara baada ya kushuhudia mtaro huo utakaopitisha maji kutoka katika chanzo cha maji hadi katika tenki la ukubwa wa lita elfu 10 na kuelekea katika vituo vitatu vya kuchotea maji ikiwa ni jitihada za kufanikisha ukarabati wa mradi wa maji kijijini hapo.
  Amesema “nguvu ya kuchimba mtaro huu haitaenda bure, tuna uhakika maji yatafika katika vituo hivyo vitatu kwa kuanzia ili kuwaepusha kuendelea kuchota maji katika bomba moja lililopo eneo la chanzo cha maji”.
  Dkt Nchimbi ameongeza kuwa, “uzalendo huu usiishie kwenye kuchimba mtaro tu, nawaomba mtoe ushauri na mapendekezo ili ukarabati wa mradi huu uwe wa ufanisi mkubwa, na hata mkiona mambo yanaenda ndivyo sivyo toeni taarifa mapema, lakini nina imani na halmashauri ya Singida, itatekeleza kwa ufanisi mradi huu kwa manufaa yenu wana Ghalunyangu”.
  Aidha amewataka wana kijiji hao kuwa walinzi wa miundo mbinu ya mradi huo pamoja na kutunza chanzo cha maji hasa kwa kuongeza eneo la hifadhi ya chanzo cha maji kutoka mita 60 mpaka mita 100 na kupanda miti ya kutosha katika chanzo hicho.

   Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akizungumza na fundi anayejenga mnara wa kuweka tanki la maji la lita elfu 10 katika kijiji cha Ghalunyangu, Wilayani Singida.
   Mhandisi wa Maji Mkoa wa Singida Mhandisi Lydia Joseph (aliyeinama) akikagua mabomba yatakayotumika kupeleka maji kwenye vituo vitatu vya kuchotea maji katika kijiji cha Ghalunyangu, Wilayani Singida.
   Wanakijiji cha Ghalunyangu wakichota maji katika bomba pekee lililopo katika chanzo cha maji na maradi wa maji kijijini hapo. Fedha za malipo kwa matokeo zimeelekezwa kijijini hapo ili kujenga vituo vitatu vya kuchotea maji kwa kuanzia ikiwa vituo vingine vitajengwa hapo baadaye.
   Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akizungumza na wana kijiji cha Ghalunyangu, Wilayani Singida waliokusanyika katika chanzo cha maji na eneo ulipo mradi wa maji kijjini hapo.
  Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0


  0 0


  Mshabiki wa Manchester United aliyevamia uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kwenda kumkumbatia Wayne Rooney wakati Everton ya Uingereza  ikichuana na Gor Mahia ya Kenya. Uwanja mzima ulishangilia.
  Mpira umekwisha kwa Everton kushinda bao 2-1, magoli yakifungwa na Rooney dakika ya 35 kabla  Tuyisenge wa Gor Mahia kusawazisha dakika mbili baadaye. Goli la ushindi la Everton limepatikana dakika ya 82 kupitia kwa mshambuliaji Kieran Dowell. 

  Askari polisi wakimdaka mshabiki wa Manchester United aliyevamia uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kwenda kumkumbatia Wayne Rooney wakati Everton ya Uingereza  ikichuana na Gor Mahia ya Kenya - ikiwa ni baada ya kuandika katika Instagram ujumbe unaosadikiwa kuwa wake kwamba atafanya tendo hilo. 

  Mshabiki huyo akisindikizwa na polisi.  0 0

   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Lindi SACAP. Rajab Nyange, wakati alipo tembelea na kukagua ujenzi wa Gereza la Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Lindi SACAP. Rajab Nyange, wakati akikagua ujenzi wa Gereza la Wilaya Ruangwa,  akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea pikipiki aina ya SANLG kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Alan Lin katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini,  akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Wauza Pikipiki na spea Taifa Martin Mbwana katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini,  akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi pikipiki kwa niaba ya waendesha bodaboda 49 wa Wilaya ya Ruangwa waliokabidhiwa pikipiki Juma Selemani, katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini,  akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na waendesha bodaboda waliokabidhiwa pikipiki 49 kwa mkopo, katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini,  akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.
  Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 1802 | 1803 | (Page 1804) | 1805 | 1806 | .... | 3284 | newer