Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

BINGWA WA UREMBO MAZNAT AFUNGUKA


MASHABIKI WA MUZIKI WAZISUBIRI KOLABO MATATA ZA COKE STUDIO KWA SHAUKU

0
0



Wakati uandaaji wa onyesho la muziki la Coca-Cola Coke Studio msimu wa tano unaendelea jijini Nairobi nchini Kenya linalojumisha kolabo za wanamuziki wa kitanzania kwa kushirikiana na wanamuziki wa nje, washabiki wa muziki nchini wamezisubiri kwa shauku kolabo hizo.
Burudani za onyesho hili ambalo limepata umaarufu mkubwa nchini kutokana na kufuatiliwa na wapenzi wengi wa muziki kupitia luninga litaanza kurushwa mapema mwezi Septemba.
Kwa upande wa Tanzania wasanii ambao wako ndani ya nyumba ni Rayvanny, Izzo Bizness na Nandy.
Katika onyesho la Coke Studio msimu mwa mwaka jana wakali wa muziki nchini ambao walishiriki walikuwa ni Ally Kiba,Vanessa Mdee,Ben Pol na Fid Q ambao walishirikiana na wanamuziki Wangechi, Maurice Kirya, Victoria Kimani na 2Face.
Msanii Rayvanny (katikati) akiwa na wasanii wenzake wakifanya moja ya Mashup hivi karibuni
Mwanamuziki Izzo Business akiwa amepozi ndani ya studio jijini Nairobi

Baadhi ya wasanii nguli waliopo kwenye matayarisho ya Coke Studio msimu wa tano wakiwa katika picha ya pamoja jijini Nairobi hivi karibuni.
Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

Waziri Prof. Mbarawa akagua mradi wa barabara za juu TAZARA jijini Dar es salaam

0
0
Na Joachim Mushi wa TBN
WAZIRI wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa leo ametembelea mradi wa ujenzi wa barabara za juu unaoendelea eneo la Tazara jijini Dar es Salaam na kuridhishwa na kasi ya ujenzi inayoendelea chini ya Kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd ya nchini Japan. 
Akizungumza katika ziara hiyo alisema lengo ni kuangalia maendeleo ya ujenzi wa mradi huo ili kuhakikisha unakamilika mapema kama ulivyopangwa. Prof. Mbarawa alisema ameridhishwa na maendeleo ya mradi huo ambao mara baada ya kukamilika utarahisisha shughuli za usafiri kwa wananchi watumiao barabara hizo mbili za Nyerere na Mandela jijini Dar es Salaam. 
Mradi huo wa ujenzi unatarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba 2018 huku ukitarajiwa kugharimu takribani shilingi bilioni 100, ambapo kati ya fedha hizo shilingi bilioni 93.44 zitatolewa na Japan kupitia Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa (JICA), na Serikali ya Tanzania itatoa shilingi Bilioni 8.3.   
Mhandisi Mkazi wa Kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd inayojenga barabara za juu eneo la Tazara, Kiyokazu Tsuji (kulia) akitoa maelekezo kewa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (katikati) maendeleo ya daraja hilo wakati alipotembelea kuangalia maendeleo ya mradi huo. Kushoto ni Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida akishuhudia. Mhandisi Mkazi wa Kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd inayojenga barabara za juu eneo la Tazara, Kiyokazu Tsuji (kulia) akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (katikati) muonekano wa ramani ya daraja hilo na ujenzi unavyoendelea wakati alipotembelea kuangalia maendeleo ya mradi huo. Kushoto ni Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida akishuhudia.  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kushoto) akipata maelezo juu ya maendeleo ya mradi huo Muonekano wa ujenzi wa barabara za juu unaoendelea eneo la Tazara jijini Dar es Salaam. Muonekano wa ujenzi wa barabara za juu unaoendelea eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.

WAZIRI MKUU AKABIDHI PIKIPIKI 49 KWA VIJANA WA RUANGWA

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO DKT. PHILIP MPANGO AWAHAKIKISHIA WAMACHINGA KUWEKEWA MAZINGIRA MAZURI YA BIASHARA

Safari ya Mwisho wa Mtangazaji wa EFM Bikira wa Kisukuma Seth Katende

0
0


Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Paul Makonda akiweka shada la maua katika kaburi la Marehemu Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma, ambaye alikuwa Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha 93.7 EFM kupitia kipindi cha Ubaoni,wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika katika Makaburi ya Kinondoni jioni ya leo jijini Dar.Marehemu Seth ameagwa mapema leo katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Bi.Zawadi Kawawa akiweka shada la maua katika kaburi la Marehemu Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma, ambaye alikuwa Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha 93.7 EFM kupitia kipindi cha Ubaoni,wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika katika Makaburi ya Kinondoni jioni ya leo jijini Dar.Marehemu Seth ameagwa mapema leo katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali.
Mkurugenzi wa 93.7 Efm Dar Es Salaam Francis Ciza akiweka shada la maua katika kaburi la mtoto wake Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma, ambaye alikuwa Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha 93.7 EFM kupitia kipindi cha Ubaoni,wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika katika Makaburi ya Kinondoni jioni ya leo jijini Dar.Marehemu Seth ameagwa mapema leo katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali
Baba wa Marehemu,Mzee Katende akiweka shada la maua katika kaburi la mtoto wake Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma, ambaye alikuwa Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha 93.7 EFM kupitia kipindi cha Ubaoni,wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika katika Makaburi ya Kinondoni jioni ya leo jijini Dar.Marehemu Seth ameagwa mapema leo katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali .


Baadhi ya Ndugu jamaa na Marafiki wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kushiriki Mazishi ya Marehemu Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma, ambaye alikuwa Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha 93.7 EFM kupitia kipindi cha Ubaoni,wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika katika Makaburi ya Kinondoni jioni ya leo jijini Dar.Marehemu Seth ameagwa mapema leo katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali.
 

MAGAZETI YA ALHAMIS LEO JULAI 13,2017

MASAUNI APOKEA MSAADA WA VIFAA VYA TEHAMA KWA AJILI YA CHUO CHA UHAMIAJI CHA KIKANDA (TRITA), MJINI MOSHI

0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia), Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI), Dkt. Anna Makakala (kulia) wakipokea moja ya kompyuta kutoka kwa Balozi wa China nchini, Dk. LU Youqing (wapili kushoto) katika hafla ya makabidhiano ya vifaa msaada vya Tehama vyenye thamani ya shilingi milioni 33 vilivyotolewa na Ubalozi huo kwaajili ya kukisaidia Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) kilichopo mjini Moshi. Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho, Maurice Kitinusa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia-waliosimama) akishuhudia Balozi wa China nchini, Dk. LU Youqing (kushoto) na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI), Dkt. Anna Makakala walipokua wakitia saini Mkataba wa Makabidhiano wa msaada wa vifaa vya Tehama vilivyotolewa na Serikali ya China kwa ajili ya Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA), kilichopo mjini Moshi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto), Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI), Dkt. Anna Makakala (kushoto), Balozi wa China nchini, Dk. LU Youqing (aliyevaa saa) pamoja na maafisa wengine wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Tehama, Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA), Mkaguzi wa Uhamiaji, Zawadi Chazuka alipokua anawaonyesha kifaa cha kuangalia alama au maandishi ambayo hayawezi onekana kwa macho ya kawaida mpaka kifaa hicho kitumike. Ubalozi wa China ulitoa msaada wa vifaa vya Tehama vyenye thamani ya shilingi milioni 33 kwa ajili ya matumizi ya chuo hicho kilichopo mjini Moshi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati waliokaa), Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI), Dkt. Anna Makakala (watatu kushoto), Balozi wa China nchini, Dk. LU Youqing (watatu kulia), Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mtafungwa wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa Uhamiaji na Ujumbe kutoka China mara baada ya Balozi wa China kutoa msaada wa vifaa vya Tehama kwa ajili ya matumizi ya Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) kilichopo mjini Moshi. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akipokelewa na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI), Dkt. Anna Makakala, wakati kiongozi huyo alipokua anawasili Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA), mjini Moshi kwa ajili ya kukabidhiwa vifaa vya Tehama vilivyotolewa na Ubalozi wa China nchini kwa ajili ya matumizi ya chuo hicho.



Taarifa ya Msiba Wa Mtanzania Prof Henslay Kabisama Nchini Marekani

0
0
WaTanzania nchini Marekani wanaomboleza msiba wa Profesa Henslay Kabisama aliyefariki huko California mwishoni mwa mwezi June
Mjane wa Marehemu pamoja na wadau kadhaa waliungana na Mubelwa Bandio katika kipindi cha NJE-NDANI kuongelea mipango ya mazishi ilipofikia sasa.

Unaweza kushiriki kusaidia gharama za kuusafirisha mwili kupitia akaunti HII ya GoFundME
Karibu uwasikilize

Barclays Bank launches a bonus savings account campaign

0
0

Double your deposit and earn double interest up 10% with Bonus Savings Account .Tanzanian’s can now earn up to 10% interest when they double their savings with Barclays.

Speaking at the launch, which took place at the bank’s Head Office, Barclays Liability Manager, Innocent Chonya said “After carefully analysing the saving patterns of Tanzanian’s, we found out that many of our customers do not open savings accounts for multiple reasons, one being low interest rates.

Following our research, we decided to develop an offering that will help address our customers concerns. Customers who currently have a Bonus Savings account need to double their existing balances to qualify to earn double the interest that they were originally receiving.

For new customers, they simply need to visit any of our branches, open a bonus savings account, and make a deposit of their choosing and they will qualify to receive double the interest up to 10%”

Barclays Bonus Savings account provides customers the opportunity of earning the highest interest rate in the country for a saving product that is not a fixed deposit product. This savings account allows you to earn a bonus interest payment in addition to the ordinary interest if you do not withdraw more than once within a given quarter.

He continued, “At Barclays, we believe in delivering products that meet the need of our customers and the ever changing economic landscape of the country. Our customers are why we exist as a bank, and it’s therefore our duty to ensure that we offer them with solutions that help them achieve their saving goals. Let your money start working for you, open a Bonus Savings account with Barclays today!.”

 Barclays bank Tanzania Marketing and Communications Manager, Joe Bendera (left) and banks Liability Product Manager, Innocent Chonya launch the bank's bonus savings account campaign in Dar es Salaam yesterday to enable customers to earn a bonus up to 10% interest on their savings.  
 Barclays bank Tanzania Liability Product Manager, Innocent Chonya (centre), and banks marketing and Communications Manager, Joe Bendera (on his left) during a media conference to launch the Barclays bonus savings account campaign in Dar es Salaam yesterday.

Jamii Media, CIPESA Wakutanisha Wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, ICT

0
0

 KAMPUNI ya Jamii Media ya Tanzania wamiliki wa mitandao ya Jamii Forums na Fikra Pevu kwa kushirikiana na Kampuni ya CIPESA ya nchini Uganda imefanya kongamano la kuwakutanisha wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) nchini Tanzania ikiwa ni kujadili masuala mbalimbali ya huduma za habari na mawasiliano pamoja na kuangalia namna ya kulinda usiri wa taarifa za wateja wanaotumia huduma hizo. 

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kongamano hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Mello alisema kongamano hilo limekuwa na matokeo chana baada ya wadau kujadili masuala mbalimbali ya ICT lengo likiwa kuboresha zaidi huduma hiyo na usalama kwa watumiaji. Alisema wadau wengi kwenye kongamano hilo wameunga mkono hatua ya uwekaji wa sheria za kusimamia huduma nzima ya ICT lakini wakashauri ufanywe kwa kutoa fursa za maendeleo na si kuminya ubunifu wala uhuru na usiri wa watumiaji wa huduma za ICT. 

Alisema wadau wengi katika kongamano hilo walihoji kitendo cha Sheria ya Makosa ya Mtandao (The Cyber Crimes Act, 2015) kuanza kutumika bila ya uwepo wa kanuni jambo ambalo limewapa ugumu hata watekelezaji na wasimamizi wa sheria husika. Mkurugenzi huyo aliongeza Jamii Media itaendelea kusaidia kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali wa huduma za mawasiliano wakiwemo bloggers ili kuona wanakuwa na uelewa na matumizi mazuri ya mitandao yao kupunguza mkanganyiko kwa wanufaika. Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Mello (wa pili kulia) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumalizika kwa kongamano la wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) nchini Tanzania, lililoandaliwa na Kampuni ya Jamii Media ya Tanzania wamiliki wa mitandao ya Jamii Forums na Fikra Pevu kwa kushirikiana na Kampuni ya CIPESA ya nchini Uganda. Wengine ni Mkurugenzi wa CIPESA, Dk. Wairagala Wakabi (wa kwanza kulia) na Mkurugenzi wa Jamii Media, Mbaraka Islam (kushoto). Kongamano hilo lilifanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Mmoja wa washiriki katika kongamano hilo, Joseph Ngwegwe-mdau wa ICT akijadili jambo katika mjadala wa wadau wa ICT, wengine ni Robert Madziva- Maxcom Africa (kulia) na Chambi Chachage wakiwa katika mjadala huo. Mmoja wa washiriki katika kongamano hilo, Catherinerose Barretto (wa kwanza kulia) akizungumza katika mjadala na wadau wa ICT kwenye kongamano hilo. Kutoka kushoto ni Chambi Chachage-Udadisi Blog, Joseph Ngwegwe-mdau wa ICT pamoja na Robert Madziva- Maxcom Africa wakiwa katika mjadala huo. Meneja Mkuu wa Kampuni ya Jamii Media, Asha Abinallah akizungumza na washiriki wa kongamano la wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) nchini Tanzania.
Maria Sarungi (kushoto) Mkurugenzi Uzalishaji kutoka 'Compass Communications Ltd' akiongoza majadiliano kwenye kongamano hilo. Mmoja wa washiriki katika kongamano hilo, Catherinerose Barretto (wa kwanza kulia) akizungumza katika mjadala na wadau wa ICT kwenye kongamano hilo. Kushoto ni Robert Madziva- Maxcom Africa wakifuatilia mjadala huo.

ALIYEKUWA KAMADA WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI (DCP) MOHAMED MPINGA RPC MPYA MKOA WA MBEYA

0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Saimon Sirro,  amefanya mabadiliko ya Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani pamoja na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya.
 
Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Naibu Kamishna wa Polisi  Mohamed Mpinga anaenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu.
 
Aidha,  Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya (DCP) Dhahiri Kidavashari amehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi.
 
Uhamisho huo ni wa kawaida katika kuboresha utendaji wa kazi za Polisi kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.
 
 Imetolewa na:
Barnabas D. Mwakalukwa – ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.

BREAKING NYUUUUZZZ:MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU YAWAACHIA HURU MASAMAKI NA WENZAKE WATANO

0
0

Karama Kenyunko-Globu ya Jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuachia huru aliyekuwa Kamishna wa TRA, Tiagi Masamaki na Wenzake watano waliokuwa wakishtakiwa na makosa ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya sh. Bilioni 12.7.

Washtakiwa hao wameachiwa na Hakimu Mkazi Huruma Shahidi baada ya upande wa mashtaka uliokuwa ukiongozwa na wakili wa Serikali Mwandamizi, Timon Vitalis kuiomba mahakama kufanya hivyo chini ya kifungu cha 91(1) ya makosa ya jinai (CPA)  kuwa DPP hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa hao.

"Mheshimiwa Hakimu kesi hii leo imekuja kwa ajili ya kutajwa, hata hivyo tuna maombi, DPP amewasilisha Nolle Prosque, hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa", amesema Wakili wa Serikali Timon Vitalis.
Hakimu Shahidi alikubaliana na ombi hilo na kuwaachia huru washtakiwa.

Mbali na Masamaki, washtakiwa wengine waliokuwa katika kesi hiyo  iliyotokana na sakata la makontena 329 ni Meneja Kitengo cha Huduma za Ushuru  TRA, Habib Mponezya  (45) na Meneja Msimamizi na Ufuatiliaji wa Forodha, Burton  Mponezya (51).

Msimamizi Mkuu Kitengo cha Ushuru wa Forodha  ICD Azam, Eliachi  Mrema (31),  Mchambuzi  Mwandamizi  wa Masuala ya Biashara  TRA,  Hamis Omary (48), Meneja wa Oparesheni  za Usalama na Ulinzi  ICD, Raymond Adolf Louis (39) na Meneja wa Azam ICD, Ashrafu Khan (59) na Haroun Mpande (28) wa kitengo cha Mawasiliano ya Kompyuta ICT TRA.
Hata hivyo, DPP amewafutia mashtaka watuhumiwa watano tu ambao ni,Tiagi Masamaki, Eliachi Mrema, Habibu Mponezya, Burton Mponezya na Ashraf Khan.

Hata hivyo, Raymond Louis, Haruni Mpande na Khakis Ally Omari wameendelea kushikiliwa na kusomewa mashtaka mapya pamoja na watuhumiwa wapya, Khalid Yusuph Hassan na Benson Vitalis Malembo.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo imemuachia huru aliyekuwa Kamishna wa TRA, Tiagi Masamaki (pichani kulia) na Wenzake watano waliokuwa wakishtakiwa na makosa ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya sh. Bilioni 12.7.
-----  ------  --------

MBUNGE WA CHADEMA AWAOMBA WANANCHI WALIOMBEE TAIFA AMANI

0
0
MBUNGE viti Maalumu Chadema, Mheshimiwa Upendo Peneza amewaomba wananchi waliombee Taifa liendelee kuwa na amani pamoja na kuwaombea viongozi wa kisiasa wawe na uvumilivu ili wazidi kusonga mbele kimaendeleo.

Aliyasema hayo jana (Jumatano, Julai 12, 2017), katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa shule ya msingi Likangara wilayani Ruangwa wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mkoani Lindi.

“Wananchi wa Ruangwa nawatakia maisha mema ili mzidi kusonga mbele, tuombee amani ya nchi yetu na mtuombee viongozi tuwe na uvumilivu wa kisiasa.”

Mbali na Mheshimiwa Upendo, pia mkutano huo uliudhuriwa na wabunge wengine ambao ni Mheshimiwa Hassan Masala (Nachingwea), Mheshimiwa Zubery Kuchauka (Liwale), Mheshimiwa Hassan Kaunje (Lindi Mjini) na Mheshimiwa Hamida Abdalaah (Viti Maalumu).

Kwa pamoja wabunge hao walisema lengo la kushiriki kwenye ziara hiyo ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya awamu ya Tano katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi aliwataka wananchi wa mkoa huo kuhakikisha wanaendelea kudumisha na kuilinda amani iliyoko kwa sababu ndiyo inayowawezesha kufanya shughuli zao za kimaendeleo.

Alisema licha ya kuwepo kwa matukio machache ya uhalifu yanayojitokeza katika baadhi ya maeneo vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na mikoa jirani limejizatiti kukabiliana na wahalifu wa aina yoyote kwa mtu mmoja mmoja au vikundi.

MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU YASHINDWA KUSIKILIZA KESI YA AGNES MASOGANGE

0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisitu imekwama kusikiliza kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili video Queen, Agnes Gerald 'Masogange' kwa sababu ana tatizo la kiafya.

Hayo yameelezwa leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya wakili wa serikali, Costantine Kakula kueleza shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kusikilizwa.

Hata hivyo, wakili wa Masogane, Ruben Simwanza alimueleza Hakimu kwamba mteja wake anaumwa hivyo anaomba kesi iahirishwe.

Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 25, 2017 kwa ajili ya kuanza kusikilizwa

HALMASHAURI YA IGUNGA KUWACHUKULIA HATUA WATUMISHI WANAOSABABISHA HOJA ZA CAG

0
0
HALMASHAURI ya wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora imesema haitasita kuwachukulia hatua za kisheria watumishi wote watakaokwamisha upatikanaji wa majibu ya hoja za ukaguzi kwa muda waliokubaliana na hivyo kusababisha Halmashauri hiyo kupata hati ya mashaka au hati chafu.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora,Peter Onesmo alitoa tahadhari hiyo kwenye mkutano maalumu wa baraza la madiwani wa Halmashauri kupitia hoja za ukaguzi wa CAG kwa mwaka 2015/2016 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri uliopo mjini Igunga.

“Na kama taarifa hiyo itakuja kwamba hatua hazijachukuliwa hatutasita kuwachukulia hatua wale ambao wametusababisha tuvuke ile tarehe tuliyoweka utekelezaji hatujauweka,kwa hiyo kama mtu atakuwa anajitakia hayo basi afike tu huko apime”alisisitiza Mwenyekiti huyo.

Aidha Mwenyekiti huyo hata hivyo alifafanua kuwa maagizo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa huo kwamba watumishi wote wale watakaosababisha Halmashauri kuingia katika mahali kusikostahili,ni lazima watachukuliwa hatua za kisheria.

Akifungua mkutano huo maalumu,Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Agrey Mwanry alisisitiza kwamba watu pekee wenye mamlaka na madaraka ya kufanya maamuzi katika Halmashauri ya wilaya ya Igunga ni watu wanaoitwa Baraza la madiwani kutokana na wao kuwa ndiyo wawakilishi wa wananchi.

“Kwa nini leo kuna districk Commisioner na Region Commishiner hapa,Regional Comisioner na district Comisioner wanakuja hapa kama wawakilishi wa Rais kwa maneno mengine ni wawakilishi wa serikali,kwa nini kwa sababu Halmashauri ya wilaya ya Igunga inapokea ruzuku ya serikali”alifafanua Mwananry.

Hata hivyo Mkaguzi wa nje,Mohamed Msangi aliweka bayana kwamba bado utekelezaji wa maoni ya CAG siyo wa kuridhisha kwani kati ya hoja 120 zilizotolewa kwa hesabu za mwaka 2015/2016 zikijumulisha na hoja za miaka ya nyuma,ni hoja 72 tu zilizopatiwa majinu ya kuridhisha na kufungwa na hivyo hoja 48 sawa na asilimia 40 zimeendelea kusalia.
Ni Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo wakati wa mkutano maalumu wa Baraza hilo kupitia taarifa CAG.(Picha Na.Jumbe Ismailly)  

TRA YAVIFUNGIA VITUO VYA MAFUTA VISIVYOTUMIA MASHINE ZA KIELEKTRONIKI JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Cathbert Kajuna-Kajunason Blog

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imevifungia vituo zaidi ya 10 jijini Dar es Salaam kwa kosa la kuendesha biashara bila mashine ya Kielektroniki. 

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa zoezi la kufungia vituo mbalimbali, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere amesema kuwa kwa sasa zoezi hilo linaendelea nchi nzima ili kuumbua vituo vyote vinavyokwepa kulipa kodi.

 "Tuliwapa muda wafunge mashine hizo mpaka mwaka jana 2016 mwishoni lakini mpaka sasa hawajatekeleza agizo hilo hivyo hatuna budi kuvifunga hivyo vituo mpaka pale watakapotekeleza matakwa ya serikali," amesema Kamshna Kichere. 

Kwa upande wa Kamishna wa Mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya amesema wakati umefika kwa wafanyabiashara kufuata makubaliano wanayokuwa wakiwafanya na TRA ili kuepuka usumbufu unaojitokeza kwa sasa. Ameongeza kuwa sheria kali zitachukuliwa kwa wafanyabiashara wote ambao vituo vyao vya mafuta vimefungwa na wakakaidi. Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere (mwenye miwani kulia) akimuhoji msimamizi wa kituo cha GBP cha Sinza Mori jijini Dar es Salaam mara baada ya kufika kwa ajili ya zoezi la kukifungia kituo hicho kwa kukosa kuwa na mashine za kielektroniki. Wengine ni wafanyakazi wa TRA walioambatana nae.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere (aliyenyoosha mkono) akiwahimiza vijana wake wafunge kituo hicho.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere (kushoto) akiwa na  Kamishna wa Mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (kulia) wakitoa msisitizo.

Prof. Mkenda aziasa taasisi za viwango kufanya kazi pamoja

0
0
Serikali imeziasa taasisi za umma zinazoshughulikia viwango nchini kufanya kazi kwa ushirikiano ili kupunguza urasimu na kujiruidia kwa majukumu vitu ambavyo vinapelekea kukuza gharama za uwekezaji nchini.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano uliowakutanisha watendaji wakuu wa mashirika ya viwango nchini jana Jijini Dar es Salaam kujadili uboreshaji wa namna ya kufikia viwango vya bidhaa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof Adolf Mkenda amesema kuboresha na kurahisisha mazingira ya uwekezaji ndio kipaumbele cha sertiukali.

Mkutano huo ambao uliandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) unatokana na mikutano ya wadau iliyofanyika awali kwenye mikoa ya Arusha, Mtwara na Dar es Salaam chini ya ufadhili wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) ambapo wadau mbalimbali walipata fursa ya kutoa maoni juu ya uboreshaji wa sekta ya viwango nchini.

“Taasisi za serikali za viwango zinafanya kazi nzuri, lakini kuna urudiwaji wa majukumu ambao unafanya mazingira ya uwekezaji kua magumu,” alisema Prof Mkenda.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo kwenye mkutano uliowakutanisha watendaji na wakuu wa mashirika ya viwango nchini ambapo aliwataka kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuchochea uwekezaji. Kushoto ni Mkurugenzi wa Upimaji na Ugenzi wa TBS na kulia ni Meneja wa Viwango wa TBS, Bi Mary Meela. Mkutano huo ulifanyika jana Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watendaji wakuu wa mashirika ya viwango nchini wakiwa kwenye mkutano uliofanyika jijini Dar Es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda (wa pili kushoto)akibadilishana mawazo baadhi ya wakurugenzi mara baada ya kufungua mkutano uliowakutanisha watendaji na wakuu wa mashirika ya viwango nchini ambapo aliwataka kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuchochea uwekezaji. Kushoto ni Mkurugenzi wa Upimaji na Ugenzi wa TBS na wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Bw. Godfrey Simbeye. Mkutano huo ulifanyika jana Jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KWA KUSHIRIKIANA NA TAASISI YA MADAKTARI AFRIKA YA NCHINI MAREKANI WAFANYA MATIBABU YA MOYO KWA WAGONJWA KWA KUWEKA KIFAA MAALUM

0
0
 Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Tulizo Shemu  na mwenzake kutoka Taasisi ya Madaktari Afrika  ya Nchini Marekani Mathew Sackett wakimwekea mgonjwa kifaa maalum cha kurekebisha  mapigo ya moyo ili yawe sawa (kwa jina la kitaalamu Pacemaker) kifaa hicho huwekewa wagonjwa ambao mapigo yao ya moyo yako chini sana. Tangu kuanza kwa kambi maalum ya matibabu ya moyo jumla ya wagonjwa nane wameshawekewa Pacemaker na wengine wanne wanatarajia kuwekewa leo na kesho.  
 Wataalamu wa Magonjwa ya  Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  na wenzao wa Taasisi ya Madaktari Afrika  ya Nchini Marekani wakimwekea mgonjwa kifaa maalum cha kurekebisha  mapigo ya moyo ili yawe sawa (kwa jina la kitaalamu Pacemaker) kifaa hicho huwekewa wagonjwa ambao mapigo yao ya moyo yako chini sana.Picha na JKCI.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

UZINDUZI REA AWAMU YA TATU MWANZA, WAFANA

0
0
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani (katikati) akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu kwa mkoa wa Mwanza.
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani akielezea mikakati ya serikali ya kupeleka umeme katika vijiji na vitongoji vyote mkoani Mwanza kupitia  Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu kwenye uzinduzi huo.
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akielezea hali ya umeme katika mkoa huo kwenye uzinduzi huo.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani (wa tano kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (wa sita kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wabunge, watendaji kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la  Umeme  Tanzania (TANESCO) na viongozi wengine wa kitaifa mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi huo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live




Latest Images