Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1800 | 1801 | (Page 1802) | 1803 | 1804 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Amina Salum anaratajiwa kuwa mgeni rasimi kesho katika ufungaji wa maonesho ya 41 ya biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Viwanda , Biashara na Uwekezaji kupitia Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara nchini (Tantrade) ilisema kuwa maonesho hayo yataitimishwa na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Amina Salum ambaye atatoa vyeti kwa washindi wa mabanda bora yaliyoshiriki maonesho hayo.

  Taarifa hiyo ilisema kuwa maonesho hayo yatafungwa majira ya saa saba kwa hotoba ya Waziri huyo na kufuatana na viongozi mbalimbali wakiwemo waandaji wa Maonesho hayo.

  Wakati huo katika maonesho hayo wananchi wameendelea kufika katika viwanja vya sabasaba kwa kupata huduma pamoja bidhaa za washiriki.

  Mabanda ambayo yamekuwa na watu katika siku ya maonesho tangu siku kwanza hadi leo ni mabanda Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

  Katibu Mkuu wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji , Profesa Adolf Mkenda akimpa maelekezo Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) ,Mcharo Mrutu katika maonesho ya 41 ya biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji , Profesa Adolf Mkenda akisaini kitabu cha wageni katika maonesho ya 41 ya biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Na Agness Moshi-MAELEZO 
  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imekua mkombozi kwa wagonjwa wa moyo Afrika Mashariki kufuatia kupungua kwa gharama za matibabu ukilinganisha na ilivyokua hapo awali.
  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mbunge wa jimbo la Dokolo nchini Uganda Bi.Cecilia Barbara alipotembelea taasisi hiyo ili kuona na kujifunza jinsi Serikali ya Tanzania inavyotoa huduma za Afya kwa wananchi wake .
  Bi.Cecilia amesema taasisi hii ni msaada mkubwa kwa Afrika Mashariki kwasababu itasaidia kupunguza idadi ya wagonjwa wa moyo wanaopelekwa nchini India au Afrika Kusini kwa matibabu kama ilivyo awali baadala yake watatibiwa Tanzania au nchini kwao.
  “Tunahitaji kubadilishana mawazo kama wana Afrika Mashariki, kwasababu kwa kuja hapa tumegundua tunavifaa na uwezo wa kupunguza gharama za matibabu ya moyo“ Alisema Bi.Cecilia.
  Bi Cecilia amesema kutokana na ubora huduma zinazotolewa na taasisi hii tangu kuanzishwa kwake serikali ya Uganda imekubali kuja kutembelea Tanzania ili kujifunza na kuanzisha mradi kama huu.
  “Hatukujua kama Tanzania kuna mradi mkubwa kama huu na unaofanya kazi nzuri lakini kwa kuja tumejua na tunategemea kuanzisha mradi kama huu japo itatuchukua muda kufikia hatua iliyofikiwa na Tanzania”aliongeza Bi.Cecilia .
   Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza na ujumbe kutoka JICA. Ujumbe huo umetembelea wagonjwa pamoja na miradi mbalimbali  ya kuboresha huduma za afya katika hospitali hiyo leo.
   Wageni kutoka JICA wakiwa katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru. Kutoka kushoto ni Ofisa wa Hospitali Kuu ya Shonan Kamakura, Emiko Shiono,  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JICA Idara ya Afrika, Komori Masakatsu, Mwakilishi wa Afrika nchini Japan, Milanga Mwanatambwe na Meneja wa Tiba, Injinia Katsumasa Shirai.
   Ofisa Mipango, Catherine Shirima (kulia) wa JICA na Yamae Mikuni kutoka Japan wakiwa kwenye mkutano huo leo.
  Wageni hao pamoja na wenyeji wakiwa katika wodi ya wagonjwa Muhimbili leo.         


  0 0
 • 07/12/17--08:47: Ever loving memory
 • Our dearest baba! Kheri Rashid Baghdellah
  We feel saddened and with memories whenever this day arrives - the 13th of  July . We remember the sudden death which was caused by an accident in Arusha at USA River bridge. It's exactly 43 years today since you left us. 
  We still remember your desire for us to be educated and will forever cherish your total investment in our future. You are fondly remembered by all of us…

  0 0


  0 0

  We are excited to bring you some very good news!

  Peter Msechu just released a brand new song titled “YAKAWA” under the management of African Music Connects (AMC). 

  YAKAWA  is a Swahili song with captivating lyrics, with a sweet African/Bongo flavor beat - a very catchy tune with production done by TEAZ.
  Peter Msechu, now signed under African Music Connects,  is a former nominee of several prestigious awards namely “National Spotlight - Bongo Star Search (2009)", a runner-up in the Tusker Project Fame 2010 and 2011 as well as a Nominee of Afrima 2013.

  AMC is a creative, multidisciplined digital music management, distribution, and marketing team based in Dar es Salaam. 
  Feel free to share with your contacts.
  #PeterMsechu #YAKAWA #AfricanMusicConnects #AMC

  0 0

   Basi lililobeba wachezaji wa Timu ya Everton ya nchini Uingereza likiwasili katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazoezi leo.
    Mchezaji Wayne Rooney wa Timu ya Everton FC ya nchini Uingereza akielekea kufanya mazoezi na wenzie katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salam leo.
   Wachezaji wa Timu ya Everton FC ya nchini Uingereza wakiingia katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.
   Wachezaji wa Timu ya Everton FC ya nchini Uingereza wakifanya mazoezi katika dinba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.
   Wachezaji wa Timu ya Everton FC ya nchini Uingereza wakifanya mazoezi katika dinba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.  0 0

  Na Dotto Mwaibale
  KAMPENI ya Castle lite unlocks inahamasisha washiriki kuhudhuria kwa wingi katika tamasha kubwa la muziki ambalo halijawahi kushuhudiwa Tanzania.
  Wito huo umetolewa na Meneja wa mahusiano ya wateja wa kampuni ya Tanzania Brewaries Limited (TBL) kwa Afrika Mashariki, George kavishe katika taarika yake kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo, ambapo alitumia fursa kuwataja wadhamini na wabia wa kampeni hiyo. 
  “Kwa mara nyingine tena tunawakumbusha wapenzi wa muziki, hasa walioko katika jiji la Dar es salaam na maeneo ya karibu kujiandikisha kwa wingi kwani tukio hilo la aina yake linakaribia” alisema Kavishe, akiongeza kuwa washiriki watapata fursa adimu sana ya kufurahia bonanza lamuziki litakalo tayarishwa na brand ya kipekee ya bia, Castle Lite hivi karibuni.
  Akitangaza washirika, kavishe alipongeza mchango wao, akisema kwamba wametekeleza jukumu kubwa katika mafanikio ambayo kampeni hiyo imefikia mpaka sasa.
  Alitaja wadhamini kama vile Tigo Tanzania (mshirika  rasmi wa mawasiliano ya Simu), Clauds FM (Mshirika kama chombo cha habari), CFAO Motors  (Mshirika katika usafirishaji), Marlborona Serena Hotel Dar es Salaam (Mshirika katika malazi).
  “Tunawashukuru sana washirika wetu kwa kukamilisha juhudi zetu katika kuelekea kwenye tamasha la nne la muzikiambalo linahakika kuwa litakuwa ni chanzo cha mabadiliko makubwa katika tasnia ya muziki wa wandani”, Kavishe amesema kuhusu Bonanza kubwa ambalo limepangwa kufanyika tarehe 22 mwezihuu wa julai katika ukumbi wa Leader’s Club hapa Dar es salaam. 
   Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Idara ya Kuunganisha Wateja Afrika Mashariki, George Kavishe (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu kuhamasisha washiriki kuhudhuria kwa wingi katika tamasha kubwa la muziki ambalo halijawahi kushuhudiwa Tanzania. Kutoka kushoto ni Mratibu wa Malipo wa kwa Tigo Pesa, Newton David na Meneja Masoko wa TBLKitengo cha Bia Laini Afrika Mashariki, Amou Majok.


  Mratibu wa Malipo wa kwa Tigo Pesa, Newton David (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
  Ofisa Masoko kutoka Kampuni ya CFAO Motors Ltd, Angelina Ndege akizungumza katika mkutano huo kuhusu kudhamini tamasha hilo.
  Wasanii wa hapa nchini watakaotoa burudani katika tamasha hilo. Kutoka kulia ni Vanessa Mdee, Nahreel Mkono na Aika Marealle.


  0 0  Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Paul Makonda akiweka shada la maua katika kaburi la Marehemu Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma, ambaye alikuwa Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha 93.7 EFM kupitia kipindi cha Ubaoni,wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika katika Makaburi ya Kinondoni jioni ya leo jijini Dar.Marehemu Seth ameagwa mapema leo katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali
  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Bi.Zawadi Kawawa akiweka shada la maua katika kaburi la Marehemu Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma, ambaye alikuwa Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha 93.7 EFM kupitia kipindi cha Ubaoni,wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika katika Makaburi ya Kinondoni jioni ya leo jijini Dar.Marehemu Seth ameagwa mapema leo katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali.
  Mkurugenzi wa 93.7 Efm Dar Es Salaam Francis Ciza akiweka shada la maua katika kaburi la mtoto wake Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma, ambaye alikuwa Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha 93.7 EFM kupitia kipindi cha Ubaoni,wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika katika Makaburi ya Kinondoni jioni ya leo jijini Dar.Marehemu Seth ameagwa mapema leo katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali
  Baba wa Marehemu,Mzee Katende akiweka shada la maua katika kaburi la mtoto wake Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma, ambaye alikuwa Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha 93.7 EFM kupitia kipindi cha Ubaoni,wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika katika Makaburi ya Kinondoni jioni ya leo jijini Dar.Marehemu Seth ameagwa mapema leo katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali .


  Baadhi ya Ndugu jamaa na Marafiki wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kushiriki Mazishi ya Marehemu Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma, ambaye alikuwa Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha 93.7 EFM kupitia kipindi cha Ubaoni,wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika katika Makaburi ya Kinondoni jioni ya leo jijini Dar.Marehemu Seth ameagwa mapema leo katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali.
   

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akizungumza na Waziri  wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa nchi ya Lesotho Mhe. Lesogo Makgothi (kushoto) ambaye alifika ofisini kwa Makamu wa Rais kuwasilisha Ujumbe Maalum wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutoka kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo ambapo Makamu wa Rais aliupokea kwa niaba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais-Ikulu, Dar Es Salaam)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akimsikiliza Waziri  wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa nchi ya Lesotho Mhe. Lesogo Makgothi (kushoto) ambaye alifika ofisini kwa Makamu wa Rais kuwasilisha Ujumbe Maalum wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutoka kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo ambapo Makamu wa Rais aliupokea kwa niaba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais-Ikulu, Dar Es Salaam)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akipokea Ujumbe Maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutoka kwa Waziri Mkuu wa nchi ya Lesotho na kukabidhiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa nchi ya Lesotho Mhe. Lesogo Makgothi (kushoto) ofisini kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais-Ikulu, Dar Es Salaam)

  0 0

  Na Abraham Ntambara. 
  MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wasichana ambo ni wanachama wa chama cha Tanzania Girl Guides Association (TGGA) kuzingatia mafunzo wanayopatiwa kwa ajili ya maisha yao ya baadaye. 
   Kauli hiyo aliitoa leo jijini Dar es Salaam wakati akikabidhiwa kijiti cha kuwa mlezi wa chama hicho kutoka kwa Mama Salma Kikwete anayesitaafu nafasi hiyo aliyoihudumu kwa zaidi ya miaka 12.
   “Niwatake tu watoto wangu kutochukulia kwa mzaha mafunzo mnayopatiwa kwani ni tija kwa maendeleo ya Taifa,” alisema Makamu wa Rais. 
  Aidha aliwaahidi wanachama kutowaangusha katika kutekeleza majukumu ya kukilea chama hicho ambapo alimpongeza Mama Salma Kikwete kwa kuweza kukiongoza vizuri kwa mafanikio makubwa licha ya kuwa na majukumu mengine. 
  Mama Salma Kikwete akisalimiana na Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi
  Salma Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba
  Mama Salma Kikwete akisalimiana na Kamishna wa TGGA

  Samia akiangalia kazi mbalimbali zinazofanywa na Girl Guides
  Aliyekuwa Mlezi wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Mama Salma Kikwete (kushoto) akimkabidhi  Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan bendera ikiwa ni ishara ya kumpatia ulezi wa chama hicho katika hafla iliyofanyika, kwenye viwanja vya Jumba la Makumbusho Dar es Salaam leo
  Mama salma akimkabidhi Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mpango mkakati wa TGGA
  Samia Suluhu Hasan akimkabidhi Mlezi mstaafu wa TGGA zawadi ya saa aliyopewa zawadi na uongozi wa TGGA kwa ajili ya kumbukumbu.

  0 0

  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na mshambuliaji na nahodha wa Timu ya Taifa ya Unigereza na mchezaji mpya wa klabu ya Everton Wayne Rooney katika hafla ya chakula cha usiku aliyowaandalia wageni hao usiku huu ambao kesho wanacheza na Gor Mahia ya Kenya katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

  0 0


  Benny Mwaipaja, WFM-Dar es Salaam
  Zikiwa zimebaki siku tatu kati ya siku 15 zilizoongezwa na Serikali kwa wananchi kulipa kodi ya majengo bila adhabu, baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wameiomba Serikali iongeze muda mwingine zaidi ili watu wote waweze kulipa kodi hiyo bila adhabu kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza wakati wa zoezi hilo.
  Wananchi hao wamemweleza Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango alipofanya ziara za kushitukiza katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA-Mtaa wa Kipata-eneo la Mnazi Mmoja na Mbagala mkoani Dar es Salaam
  Wamesema kuwa mwamko wa wananchi kulipa kodi ni mkubwa hali iliyosababisha foleni kubwa kila mahali nchini kutokana na uhaba wa watumishi wa TRA pamoja na vitendeakazi muhimu kama vile kompyuta na mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFDs).
  Waziri wa Fedha na Mipango Dokta Philip Mpango amewataka Watanzania kuwa watulivu na kuendelea kulipa kodi hiyo huku akiahidi kutatua changamoto ya uhaba wa watumishi pamoja na vitendeakazi ili kuwaondolea adha wananchi waliojitokeza kwa moyo kulipa kodi mbalimbali ikiwemo ya majengo.
   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akiongea na wananchi waliojitokeza kulipa kodi ya majengo katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)-Ilala Mtaa wa Kipata, na kuwapongeza kwa kuitikia wito huo kwa wingi na kuwaeleza kuwa kwa kulipa kodi kutasaidia upatikanaji wa huduma muhimu kama maji, barabara, umeme  na dawa hospitalini.
   Wananchi waliofika katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Ilala Mtaa wa Kipata, wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) akiwaelezea namna atakavyoboresha huduma kwa walipa kodi za majengo kwa kuwapa kipaumbele walemavu, wazee, wagonjwa na wasiojiweza. Tukio hili litaenda sambamba na kuwawekea sehemu maalumu ya kukaa wakati wakisubiri huduma.
   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) akipokea shukrani na pongezi kutoka kwa Bi. Rose Muyalo, kwa utendaji makini wa Serikali ya Awamu ya Tano na kwa kupatiwa huduma bora kutoka kwa wafanyakazi wa TRA.
   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) akiongea na wananchi waliofika katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Ilala Mtaa wa Kipata kulipa kodi za majengo na kuelezea furaha yake namna walivyoitikia wito huo.


  0 0  0 0


  Na Greyson Mwase, Geita

  Naibu  Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, ametoa siku 13 kwa mameneja wote wa Shirika la Umeme  Tanzania (TANESCO) kuhakikisha wananchi wote waliolipa ada kwa ajili ya kuunganishiwa huduma ya umeme wanaunganishiwa mapema na kuondokana na adha ya kuwepo gizani.
  Dkt. Kalemani alitoa agizo hilo katika kijiji cha Nyijundu wilayani Nyang’hwale mkoani Geita wakati akizindua Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu kwa mkoa wa Geita pamoja na kumtambulisha mkandarasi atakayetekeleza mradi kwa mkoa huo.

  Alisema kuwa, ni haki ya mwananchi  aliyelipia gharama za kuunganishiwa umeme kupatiwa huduma ndani  ya siku saba kama sheria inavyofafanua na kuwataka mameneja kuhakikisha wananchi wote waliokuwa wamelipia huduma za kuunganishiwa  umeme kupata huduma hiyo kabla ya  Julai 25, mwaka huu.

  Katika hatua nyingine, Dkt. Kalemani aliwataka mameneja  wa TANESCO  kusogeza huduma karibu na wananchi badala ya wananchi kusafiri  umbali mrefu  kwa gharama kubwa kufuata  huduma za umeme.

  Alisema serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuinua  uchumi wa viwanda kwa kuhakikisha nishati ya umeme ya uhakika inapatikana hususan katika maeneo ya vijijini ili wananchi waweze kujiajiri kupitia viwanda vidogo  vidogo kama mashine za kusaga na kukoboa nafaka, kuchomelea vyuma na kusindika matunda.
   Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akielezea  hali ya upatikanaji wa umeme katika mkoa huo  mbele ya Naibu  Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) kwenye uzinduzi huo.

   Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na Mbunge wa Bukombe,  Dotto Biteko akifafanua jambo kwenye uzinduzi huo.

   Naibu  Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akitoa maelekezo  kwa wakandarasi na watendaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) (hawapo pichani) kwenye uzinduzi huo.

   Sehemu ya wakandarasi na watendaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wakipokea maelekezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) kwenye uzinduzi huo.

   Naibu  Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akitoa sehemu ya  vifaa maalum vya Umeme Tayari (UMETA) kama zawadi kwa  sehemu ya wazee wa kijiji cha Nyijundu wilayani Nyang’hwale kwenye uzinduzi huo.

  0 0


  0 0

  Na Ramadhani Juma

  Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa

   WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI George Simbachawene ameahidi kumfikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Magufuli ombi la kuitangaza Manispaa ya Dodoma kuwa Jiji kwani inakidhi vigizo na kwamba sasa ni wakati muafaka wa kupewa hadhi hiyo.
  Alitoa ahadi hiyo jana wakati akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Dodoma katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Dodoma ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku moja katika Manispaa hiyo, iliyojumuisha pia ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo.

  Aidha, amewataka watumishi wa iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao (CDA) kumshukuru Rais kwa uamuzi wa kuivunja Mamlaka hiyo kwa sababu hatua hiyo imeondoa mkanganyiko uliokuwepo katika kuhudumia wananchi hususani katika sekta ya ardhi na mipango miji ambako Manispaa ya Dodoma pia ilikuwa na jukumu hilo.

  Pia aliwaeleza watumishi hao wapatao 260 kuwa, sasa watapata fursa pana zaidi ya kuitumikia nchi yao katika mikoa mbalimbali watakayopangiwa kuendelea kutumikia wananchi kwani wao ni watumishi wa umma na wana haki na wajibu wa kufanya kazi sehemu yeyote nchini.   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI George Simbachawene (wa pili kushoto) akiingia katika Ofisi za Mhandisi wa Halmashauri ya  Manispaa ya Dodoma kukagua magari na mitambo iliyorithiwa na Manispaa hiyo kutoka kwa iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) wakati wa ziara ya siku moja ya  Waziri huyo katika Manispaa hiyo jana. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Christine Mndeme na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Mhandisi Lusako Kilembe.
  Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Mhandisi Lusako Kilembe (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI George Simbachawene wakati wa ziara ya siku moja ya  Waziri huyo katika Manispaa hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Christine Mndeme. PICHA KWA HISANI YA BERN PATRICK WA GAZETI LA MWANANCHI.

  0 0


  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr. A. P Makakala, akitiliana saini Makubaliano na Dkt. Lu Youqing, Balozi wa China nchini kuhusu  Msaada wa Vifaa vya TEHEMA vya thamani ya Shilingi 33 Milioni kwa Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda Moshi,  toka Serikali ya Watu wa China kupitia Ubalozi wake nchini, Mjini Moshi. Nyuma Katikati ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe, Mhandisi Hamad Massauni akishuhudia tukio hilo.

   Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe, Mhandisi Hamad Massauni aliyesimama nyuma katikati,  akishuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Makabidhiano ya ya msaada uliotolewa kwa Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda, Moshi na Serikali ya Watu wa China uliofanywa na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. A.P Makakala na Balozi wa China nchini, Mhe.Balozi Lu Youqing, Mjini Moshi.

  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr. A. P Makakala, akielezea matumizi ya moja ya vyumba vya Maktaba ya Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda cha Moshi kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe, Mhandisi Hamad Massauni na , Mhe.Balozi Lu Youqing, kabla ya tukio la kupokea Msaada wa Vifaa vya TEHEMA vya thamani ya Shilingi 33 Milioni  toka Serikali ya Watu wa China, Mjini Moshi.

  0 0

  Na Dotto Mwaibale
  KAMPUNI ya Simu za Mkononi ya Tigo kwa kushirikiana na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA),Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto ( UNICEF) na GSMA wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke jijini Dar es Salaam kuona zoezi la usajili wa watoto walio chini ya miaka mitano jinsi wanavyopata vyeti vya kuzaliwa kupitia mpango maalumu unaosimamiwa na taasisi hizo.
  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo,  Meneja wa masuala ya kijamii wa Tigo, Halima Okash alisema Tigo kama mdhamini wa mpango huo wa upatikanaji kwa urahisi wa vyeti hivyo kwa njia ya mtandao , kama kampuni ya mawasiliano wameamua kushirikiana na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) bega kwa bega kuhakikisha watoto wanapata vyeti vyao kwa urahisi na hadi sasa zaidi ya watoto milioni 1.6 wamepata vyeti kwenye mikoa saba nchini. 
  Kwa upande wake Meneja Masoko na  Mawasiliano wa Rita,  Josephat Kimaro amesema kwa sasa wamesaji watoto mikoa saba na kuwa wamejipanga kuendelea mikoa ya kusini ambapo amewataka wazazi wajitokeze kupata vyeti vya kuzaliwa vya watoto wao. 
  Alitaja mikoa waliyokwisha fanya usajili huo kuwa ni Shinyanga, Mbeya , Njombe, Mwanza, Iringa, Geita na Temeke.
   Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Kampuni ya Millicom, Mohamed Dabour (katikati), akimkabidhi cheti cha kuzaliwa mmoja wa akina mama aliyempeleka mtoto wake kumsajili katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke Dar es Salaam leo. Mpango huo unasimamiwa na Kamuni ya simu za mkononi ya Tigo, Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA),Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto ( UNICEF) na GSMA. Kutoka kulia waliosimama ni Mtaalamu wa Masuala ya Watoto kutoka Unicef, Bhashar Mishra na Makamu wa Rais wa Mambo ya Nje wa Kampuni ya Millicom, Rachel Samren. 

   Mtaalamu wa Masuala ya Watoto kutoka UNICEF, Bhashar Mishra (kulia) akiteta jambo na maofisa waliopo katika mpango huo. Kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael.
   Ofisa Mwandamizi wa Rita, Beatrice Mboya (kulia), akielekeza jinsi vyeti vya watoto vinavyosajiliwa kwa njia ya mtandao.
  Meneja Huduma za Jamii wa Tigo, Halima Okash akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tigo ilivyodhamini mpango huo.  0 0


  Sehemu ya watumishi wa umma wa Wilaya ya Kigamboni walioshiriki katika ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki leo katika Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam

   Mganga Mkuu wa Wilaya yaKigamboni Dkt. Bakari Mbwana akitoa hoja wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki kuzungumza na watumishi wa umma na kutatua kero zao leo katika Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam
   Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa akitoa taarifa fupi ya watumishi wa wilaya yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (kulia) alipofanya ziara ya kikazi katika wilaya hiyo leo Jijini Dar es Salaam
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki akizungumza na watumishi wa umma wa Wilaya ya Kigamboni (hawapo pichani) wakati wa ziara ya kikazi katika wilaya hiyo leo Jijini Dar es Salaam


  0 0


older | 1 | .... | 1800 | 1801 | (Page 1802) | 1803 | 1804 | .... | 3284 | newer