Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1799 | 1800 | (Page 1801) | 1802 | 1803 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Na Robert Hokororo, Kishapu 
   Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 umepokelewa kimkoa kijiji cha Kinampanda kata ya Shagihilu katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga kutoka Simiyu na kuzindua miradi ya maendeleo yenye thamani ya sh. bilioni 3.7. 
  Katika mapokezi hayo Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini alimkabidhi mwenzake wa Shinyanga, Albert Msovela ambaye alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kishapu. 
  Katika mbio hizo jumla ya miradi 12 ilizinduliwa ikiwemo ya kituo cha mafuta wenye thamani ya sh. milioni 337 kutoka kwa mjasiliamali Kija Ng’wani na mashine ya kusindika mafuta ya alizeti na unga wa mahindi sh. 244. 
  Mingine ni mashine ya kukoboa mpunga na kuweka katika madaraja sh. milioni 535.8 na ufugaji ng’ombe sh. milioni 400 ya mjasiliamli Mabela Masolwa pamoja na eneo la viwanda lenye ekari 278 ambao thamani yake ni sh. bilioni 1.1.
  Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela (kushoto) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa mwenzake wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini tayari kwa mbio hizo mkoani Shinyanga.

  Mwenge wa Uhuru ukikimbizwa eneo la Maganzo wilayani Kishapu wakati ukiendelea kizindua miradi ya maendeleo. Kulia mbele ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akitoa hamasa kwa wananchi. 

  Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, Amour Hamad Amour akiweka nafaka ya mahindi katika mashine ya kusaga unga wakati wa uzinduzi wa mradi wa kiwanda kidogo cha kusindika alizeti na kusaga unga wakati wa mbio za Mwenge zilipopita kata ya Mwamalasa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga jana.

  Mwenyekiti wa halmashauari ya Kishapu, Boniphace Butondo akicheza ngoma wakati wa mapokezi ya Mwenge wa         Uhuru kijiji cha Kinampanda.

  Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, Amour Hamad Amour akikagua bidhaa katika banda la wanawake wajasiliamali wilayani Kishapu eneo la mkesha Maganzo. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA


  0 0


  0 0

  Saidi Mwamba Kizota (kushoto) na Hamisi Thobias Gaga
  Na  Haji Sunday  Manara
  Ehhh!! Haya! Na leo naandika tena? Mazoea mengine bana!!  
  Ndio, nimeona niandike ujinga wangu ila safari hi naandika kuhusu suala jepesi la wachezaji kuhama timu kubwa moja kwenda timu kubwa nyingine. Hapa nazungumzia Simba na Yanga, aka mapacha Kulwa na Dotto.

  Kiuhalisia hili jambo halikuanza leo,limeanza miaka Dahal. Na ukienda katika historia, zamani lilikuwa linakera zaid pengine kupita zama zetu, sababu miaka ya nyuma kabisa, wachezaji walikuwa wakihama upande mmoja kwenda mwingine sababu za kishabiki zaid kuliko sasa, ambapo sababu za kimaslahi zmechukua nafasi kubwa.

  Kihistoria mchezaji wa kwanza maarufu kuhama katika  timu hizi ni wajina wangu Haji Omari....Huyu alikuwa sentahafu mahiri sana wa Yanga, lakini akaja kuhamia Sunderland (Simba). Inaarifiwa kwa kitendo chake cha kuhama jinsi kilivyowakera wanayanga,wakaamua kuhakikisha hachezi Simba. Haji akaishia kuuza soda pale Ilala Stadium (Karume).


  Baada ya hapo kulikuwa na mtikisiko mkubwa katika  medani ya kabumbu nchini, baada ya anaetajwa kuwa kiungo bora nchini kuwahi kutokea miaka ya 19960  na mwanzoni mwa 1970 ,Gilbert Mahinya kuihama klabu ya Simba na kujiunga na Yanga. Kiungo huyo inatajwa kuwa alinyan'ganywa hadi fenicha alizonunuliwa na Simba,hali iliopelekea kuacha gumzo kubwa nchini. Gilbert anatajwa na mchezaji wa zamani wa Yanga, Pan, Pamba na timu ya Taifa,Mohamed Rishard Adoph, kuwa ndie half back six bora kuwahi kumuona nchini.

  0 0

  Shirika la ndege la RwandAir linataraji kuanzisha safari zake za kuelekea mji wa Brussels nchini Belgium kupitia Mjini Kigali nchini Rwanda kutokea Jijini Dar es salaam.

  akizungumzia kuanza kwa safari hizo, Meneja mkazi wa Shirika hilo, Ibrahim Bukenya amesema kuwa safari hizo zitaanza rasmi tarehe 14 Julai 2017 na zitakuwa ni safari za mara tatu kwa wiki na baadae kuwa kila siku. 

  Bukenya amesema Shirika hilo liko kwenye hatua za mwisho kuweka Hub nyingine ya kibiashara kwenye mji wa Cotonou nchini Benin. Pia shirika hilo liko kwenye hatua za mwisho za kuanzisha safari zake mpya za kuelekea  mji wa Guangzhou nchini China.
  Wakati huo huo shirika ndege la RwandAir kwa hapa Tanzania liko kwenye hatua za mwisho za kuanzisha malipo ya ununuzi wa tiketi kwa kutumia mitandao ya simu. 

  Bukenya aliendelea kuwashukuru wateja wote na wadau wao na kwa kuwakumbusha kuwa safari zake kutokea Dar kuelekea Kigali na kuunganisha sehemu nyinginezo kuwa mara mbili kila siku, na kutokea Kilimanjaro kwenda Kigali na kuunganisha sehemu zingine ikiwa ni mara tano kwa wiki, hivyo kila atakaye kusafiri asafiri na Shirika ndege la RwandAir.

  0 0

   Jeneza lenye mwili wa Marehemu Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma ambaye alikuwa Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha 93.7 EFM kupitia kipindi cha Ubaoni, likiwa katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam kunakofanyika misa ya kuaga mwili wake hivi sasa, ambapo baada ya kumalizika kwa misa hiyo, Mwili wa Marehemu utapumzishwa kwenye nyumba yake ya Milele katika Makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es salaam mchana wa leo.
   Sehemu ya Waombolezaji wakiwa katika Viwanja Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam kunakofanyika misa ya kuaga mwili wake hivi sasa, ambapo baada ya kumalizika kwa misa hiyo, Mwili wa Marehemu utapumzishwa kwenye nyumba yake ya Milele katika Makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es salaam mchana wa leo.
  Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Halima Mdee akitoa salamu zake.

  PICHA ZINGINE ZITAWAJIA HAPO BAADAE

  0 0

  Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Kiungo Mshambuliaji wa timu ya Everton ya nchini Uingereza, Wayne Rooney muda mfupi baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere, Jijini Dar es salaam asubuhi ya leo. Timu ya Everton ikiwa na kikosi kamili cha wachezaji 46 pamoja na viongozi na kocha mkuu wa timu hiyo Ronald Koeman, Kimewasili mapema leo tayari wa Mchezo wao na Mabingwa wa SpotiPesa Gor Mahia ya nchini Kenya, unaotarajiwa kuchezwa kesho katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.  
  ORODHA YA WACHEZAJI WA EVERTON
  1 – Jordan Pickford
  2 – Morgan Schneiderlin
  3 – Leighton Baines
  4 – Michael Keane
  5 – Ashley Williams
  6 – Phil Jagielka
  7 – Yannick Bolasie
  8 – Ross Barkley
  9 – Sandro Ramirez
  10 – Wayne Rooney
  11 – Kevin Mirallas
  12 - Aaron Lennon
  16 – James McCarthy
  17 – Idrissa Gana Gueye
  18 – Gareth Barry
  20 – Davy Klaassen
  21 – Muhamed Besic
  22 – Maarten Stekelenburg
  23 – Seamus Coleman
  25 – Ramiro Funes Mori
  26 – Tom Davies
  29 – Dominic Calvert-Lewin
  30 – Mason Holgate
  31 – Ademola Lookman
  33 – Joel Robles
  34 – Oumar Niasse
  38 - Matthew Pennington
  43 - Jonjoe Kenny
  46 - Joe Williams
  Mshambuliaji wa timu ya Everton Wayne Rooney pamoja na wachezaji wenzake wa wakielekea kwenye basi tayari kwa safari ya kuelekea hotelini kwa mapumziko mafupi. 
  Wachezaji wa Everton wakiingia basini.


  0 0

  Mhandisi Mkazi wa Kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd inayojenga barabara za juu eneo la Tazara, Kiyokazu Tsuji (kulia) akitoa maelekezo kewa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (katikati) maendeleo ya daraja hilo wakati alipotembelea kuangalia maendeleo ya mradi huo. Kushoto ni Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida akishuhudia.

   WAZIRI wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa leo amevamia mradi wa ujenzi wa barabara za juu unaoendelea eneo la Tazara jijini Dar es Salaam na kuridhishwa na kasi ya ujenzi inayoendelea chini ya Kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd ya nchini Japan. 

  Akizungumza katika ziara hiyo alisema lengo ni kuangalia maendeleo ya ujenzi wa mradi huo ili kuhakikisha unakamilika mapema kama ulivyopangwa. Prof. Mbarawa alisema ameridhishwa na maendeleo ya mradi huo ambao mara baada ya kukamilika utarahisisha shughuli za usafiri kwa wananchi watumiao barabara hizo mbili za Nyerere na Mandela jijini Dar es Salaam. 

  Mradi huo wa ujenzi unatarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba 2018 huku ukitarajiwa kugharimu takribani shilingi bilioni 100, ambapo kati ya fedha hizo shilingi bilioni 93.44 zitatolewa na Japan kupitia Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa (JICA), na Serikali ya Tanzania itatoa shilingi Bilioni 8.3. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kushoto) akipata maelezo juu ya maendeleo ya mradi huo. Muonekano wa ujenzi wa barabara za juu unaoendelea eneo la Tazara jijini Dar es Salaam. Muonekano wa ujenzi wa barabara za juu unaoendelea eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua vifaa ndani ya gari la kubebea wagonjwa baada ya kukabidhi gari mbili za kisasa za kubebea wagonjwa,katika hospitali ya  Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017.

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara katika hospitali ya wilaya ya Ruangwa na amekabidhi magari mawili ya kubebea wagonjwa. Amesema kati ya magari hayo moja ni kwa ajili ya hospitali hiyo ya wilaya na la pili litapelekwa katika kituo cha afya cha Mandawa.

  Waziri Mkuu amekabidhi magari hayo leo (Jumatano, Julai 12, 2017), alipotembelea hospitali hiyo, ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi Mkoani Lindi. Amesema magari hayo ni muendelezo wa mkakati wa Serikali ya awamu ya tano wa kuboresha huduma za afya kwa wananchi wake.

   “Rais wetu Dkt. John Magufuli amedhamiria kuwaondolea wananchi kero mbalimbali zinazowakabili zikiwemo za huduma za afya, hivyo tuendelee kumuunga mkono.”
   
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimjulia hali mtoto Nasib Robert,(kushoto) ni mama wa mtoto Veronica Chilala,wakati alipo tembelea wodi ya watoto katika hospitali ya  Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017.

  Waziri Mkuu amesema magari hayo ya kisasa yatasaidia kurahisisha usafiri kwa  wagonjwa wanaohitaji matibabu ya dharura katika hospitali kubwa. Kabla ya kukabidhi magari hayo, Waziri Mkuu alitembelea wodi ya  akina  mama na ya  watoto waliolazwa katika hospitali hiyo na amesema kwamba ameridhishwa na hali ya utoaji huduma.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Mheshimiwa Rashid Nakumbya amesema magari hayo ni faraja kwao kwa kuwa walikuwa na changamoto ya usafiri kwa wagonjwa wa dharura.

  “Tunatambua na kuthamini jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano katika halmashauri yetu na Taifa kwa ujumla, nasi tutayatumia magari haya kama ilivyokusudiwa.”
   
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipo kabidhi gari mbili za kisasa za kubebea wagonjwa,katika hospitali ya  Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017.

  Awali, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa, Dkt. Regan Rajuu amesema hali ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika hospitali hiyo umeongezeka kutoka asilimia 80 Desemba, 2016 na kufikia asilimia 90 Juni 2017.

  Pia Waziri Mkuu alitembelea shule ya Sekondari ya Kassim Majaliwa iliyoanza kujengwa Desemba, 23, 2016 kwa michango ya Halmashauri, fedha za mfuko wa jimbo pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo.

  Kaimu Mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Emmanuel Sechawe alisema msingi wa kuanzisha shule hiyo ulitokana na uwepo wa wanafunzi 319 waliofaulu darasa la saba mwaka 2016 kukosa nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza katika shule zilizopo.

  Mbali na kutembelea shule hiyo, pia Waziri Mkuu alifanya ukaguzi wa maendeleo ya mradi wa ujenzi wa gereza la wilaya ya Ruangwa, ambalo litakapokamilika litapunguza msongamano wa wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Nachingwea.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua gari ya kubebea wagonjwa wakati alipokabidhi gari mbili za kisasa za kubebea wagonjwa,katika hospitali ya  Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wakati alipo tembelea hospitali ya  Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017.

  0 0

  BENKI ya NMB imedhamini mashindano ya mchezo wa Golf yaliyoandaliwa na Club ya Gymkhana ya jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa club hiyo. 


  Michuano hiyo mikali na ya kipekee iliyopambanisha wachezaji wa mchezo wa golf kutoka club mbalimbali ilifanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam na washindi mbalimbali wa mchezo huo kujishindia tuzo baada ya kuibuka kidedea hatua mbalimbali. 

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe ndiye mgeni rasmi aliyewaongoza wageni mbalimbali waalikwa kwenye hafla ya kuwakabidhi tuzo washindi kabla ya kuyapongeza makampuni mbalimbali ikiwemo Benki ya NMB iliyofanikisha michuano hiyo. Menaja Mahusiano ya Wateja wa NMB, Gibson Mlaseko akimkabidhi tuzo ya ushindi wa mchezo wa Golf, Bi. Tayana William katika michuano ya mchezo huo maalumu kwaajili ya kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Clabu ya Gymkhana ya jijini Dar es Salaam. Benki ya NMB ilidhamini mashindano hayo yaliyofanyika kwa siku mbili na kushirikisha wanamichezo mbalimbali.

  Katika hafla hiyo ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mchezo wa golf, NMB ilipata fursa ya kukabidhi tuzo sita kwa washindi mbalimbali, wakiwemo; Samwel Mosha, Chiku Eliasy, Tayana William, Eric Tango, Vicky Elias pamoja na Mohamed Rahim aliyetwaa tuzo ya mshindi wa Jumla wa mchezo huo. Hata hivyo, katika hafla hiyo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe pia aliikabidhi Benki ya NMB na makampuni mbalimbali tuzo ya shukrani iliyotolewa na Uongozi wa Club ya Gymkhana ya jijini Dar es Salaam kutambua mchango wa benki hiyo na taasisi zingine katika mafanikio ya mchezo wa Golf.

  Meneja Mahusiano ya Wateja wa NMB, Gibson Mlaseko akimkabidhi tuzo ya ushindi wa mchezo wa Golf, Samwel Mosha katika michuano ya mchezo huo maalumu kwaajili ya kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Clabu ya Gymkhana ya jijini Dar es Salaam. Benki ya NMB ilidhamini mashindano hayo yaliyofanyika kwa siku mbili na kushirikisha wanamichezo mbalimbali.

  0 0

  Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge, akimwonyesha Mtambo Mpya wa kisasa wa Kusukuma maji wa Ruvu Chini unaomilikiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA), mgeni wake Waziri wa Maji na Umwagilia wa Misri Dk. Mohamed Abdel ATY (wapili kulia), baada ya kuwasili jana katika eneo la kusuku maji la Ruvu chini na kujionea maji yanavyoingizwa katika mtambo huo kutoka mtoni.(kushoto ni ) Mkurugenzi wa Sekta ya Maji na Umwaghiliaji wa Misri Dk. Ahmed BahaaEl Deen na kulia ni Mkurugenzi wa DAWASCO, Cyprian Luhemeja.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge, akiwa na mgeni wake Waziri wa Maji na Umwagilia wa Misri Dk. Mohamed Abdel ATY (wapili kulia), baada ya kuwasili jana katika eneo la kusuku maji la Ruvu chini na kujionea maji yanavyoingizwa katika mtambo huo kutoka mtoni.(kushoto ni ) Mkurugenzi wa Sekta ya Maji na Umwaghiliaji wa Misri Dk. Ahmed BahaaEl Deen na kulia ni Mkurugenzi wa DAWASCO, Cyprian Luhemeja.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge, akimwonyesha Mtambo Mpya wa kisasa wa Kusukuma maji wa Ruvu Chini unaomilikiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA), mgeni wake Waziri wa Maji na Umwagilia wa Misri Dk. Mohamed Abdel ATY (wapili kulia), baada ya kuwasili jana katika eneo la kusuku maji la Ruvu chini na kujionea maji yanavyoingizwa katika mtambo huo kutoka mtoni.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge, akiondoka katika eneola Ruvu chini pamoja na mgeni wake Waziri wa Maji na Umwagilia wa Misri Dk. Mohamed Abdel ATY (wapili kulia), baada ya kumaliza kukagua katika eneo la kusukuma maji la Ruvu chini na kujionea maji yanavyoingizwa katika mtambo huo kutoka mtoni.

  0 0


  Mwanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akipitia taarifa ya michango yake, baada ya kukabidhiwa na Maafisa wa Mfuko huo, alipotembelea banda la PSPF kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, leo Julai 12, 2017. Wakati wa maonesho hayo yakitarajiwa kufikia kilele kesho Alhamisi Julai 13, 2017, zaidi ya watu 500 wametembeela banda la Mfuko huo hadi mchana huu na kati ya hao asilimia 70 walifika kujiunga na Mpango wa uchangiaji wa Hiari, (PSS), unaomuwezesha mwananchi yeyote ambaye anafanya kazi za kumuingizia kipato kuwa mwanachama. Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi, alisema na kuongeza faida za mwanachama kujiunga na PSS, ni pamoja na kupata bima ya afya. (NA K-VIS BLOG/Khalfan Said)
  Afisa Msaidizi wa Uendeshaji wa PSPF, Bw.Mussa Mfaki, (kulia), akimkabidhi kadi ya kujiunga na PSPF kupitia Mpango wa uchangiaji wa Hiari, PSS, Bi.Damare B. Nampwani, leo Julai 12, 2017.
  Mwananchi akijaza fomu ya lujiunga na PSPF kupitia Mpango wa PSS, huku Mwanasheria kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti MHifadhi ya Jamii, (SSRA), Bi.Imani Masebu, (kulia), na Mhandisi Ally Shanjirwa, (katikati), wakishuhudia.
  Afisa Uhusiano wa PSPF, Bi. Coleta Mnyamani, (kulia), akimkabidhi kadi ya uanachama ya PSPF, Afisa wa Polisi wa Usalama Barabarani, Salvatory A. Chacky.
  Hiki ndio kikosi kazi cha PSPF ambacho kwa takriban wiki moja na nusu kimekuwa kikitoa huduma kamambe kwenye banda la Mfuko huo kwenye jengo la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, ambako kumekuwa na maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam. Kutoka kushoto waliosimama ni Isack Kimaro, Mussa Mfaki, Chaula Miteko, Mhandisi Ally Shanjirwa, Abdul Njaidi, Noah Amri,Win-God, Bw.Msina. Waliokaa kutoka kushoto, ni Bi. Coleta Mnyamani, Bi. Mariam Saleh, Bi. Irine Musetti na Bi. Asmahan H.Haji.


  0 0


  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mjini Zanzibar Abdulrahman Khatib kulia akitiliana saini na Mstahiki Meya wa Postdam Ujarumani Jan Jacob kuhusiana na mkataba wa mashirikiano kati ya Baraza la manispaa ya mjini na Jiji la Postdam la Ujerumani katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni Mjini Zanzibar.

  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mjini Zanzibar Abdulrahman Khatib kulia wakibadilishana hati baada ya kitiliana saini na Mstahiki Meya wa Postdam Ujarumani Jan Jacob kuhusiana na mkataba wa mashirikiano kati ya Baraza la manispaa ya mjini na Jiji la Postdam la Ujerumani katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni Mjini Zanzibar.
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mjini Zanzibar Abdulrahman Khatib kulia akiwa pamoja na Mstahiki Meya wa Jiji la Postdam Ujarumani wakionesha hati walizotiliana saini kuhusiana na mkataba wa mashirikiano kati ya Baraza la manispaa ya mjini na Jiji la Postdam la Ujerumani katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni Mjini Zanzibar.
  PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.


  0 0

  Benki ya Ecobank Tanzania leo imeingia katika ushirikiano rasmi na TICTS, ambapo wateja wa kampuni hiyo wataweza kufanya malipo yao kwa haraka na ufanisi zaidi kupitia tawi lolote la Ecobank. 

  Benki hii imeanzisha mfumo ambao utawawezesha wateja wa TICTS kufanya malipo yao papo kwa hapo kupititia mfumo huu rahisi. Huduma hiyo itakuwa inapatikana kwa wateja wa Ecobank na wasio wateja wa benki hii.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaaam leo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank, Raphael Benedict alisema benki hiyo inataka kuhakikisha huduma ya uagizaji na utoaji mizigo bandarini katika Bandari ya Dar es Salaam inakuwa rahisi zaidi na ya haraka zaidi kwa wateja wa TICTS.

  Benedict aliongeza kuwa ili kuwezesha jambo hilo, Ecobank Tawi la PSPF ambalo linapatikana karibu na geti la ofisi za TICTS, limeogeza muda wa huduma zake na sasa litakuwa likifunguliwa saa 8:00 asubuhi hadi saa 4:00 usiku kwa siku za kazi, na saa 3:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni kwa siku ya Jumamosi.


  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Raphael Benedict (kulia)  akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam kuhusu ushirikiano wa Benki hiyo na TICTS ambapo wateja wa kampuni hiyo wataweza kufanya malipo yao kwa haraka na ufanisi zaidi kupitia tawi lolote la Ecobank hapa nchini ambapo katika kufanikisha jambo hilo benki imefungua Tawi lake katika jengo la PSPF linalopakana na geti la ofisi za TICTS, huku muda wa huduma ukiongezwa kuanzia saa 8:00 asubuhi hadi saa 4:00 usiku kwa siku za kazi, na saa 3:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni kwa siku ya Jumamosi. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa TICTS Jared H. Zerbe na kushoto ni Katibu Mkuu wa Tanzania Freight Forwarders Association (TAFFA), Tony Swai. 
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Raphael Benedict (kulia)  na Mkurugenzi Mkuu wa TICTS Jared H. Zerbe wakisaini mkataba wa makubaliano wa kushirikiana katika kuhakikisha wateja wa TICTS wanafanya malipo yao kwa haraka na ufanisi zaidi kupitia tawi lolote la Ecobank hapa nchini. Mkataba huo ulisainiwa jana katika tawi la Ecobank lililopo PSPF Towers jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia kushoto ni Katibu Mkuu wa Tanzania Freight Forwarders Association (TAFFA), Tony Swai.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Raphael Benedict (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa TICTS Jared H. Zerbe (katikati) wakipeana mkono baada ya kutia saini ya mkataba wa makubaliano wa kushirikiana katika kuhakikisha wateja wa TICTS wanafanya malipo yao kwa haraka na ufanisi zaidi kupitia tawi lolote la Ecobank hapa nchini. Mkataba huo ulisainiwa jana katika tawi la Ecobank lililopo PSPF Towers jijini Dar es salaam. Wanaoshuhudia (kulia) ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa fedha wa Ecobank Africa, Isaac Kamuta, Katibu Mkuu wa Tanzania Freight Forwarders Association (TAFFA), Tony Swai (wa pili kushoto), na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni ya TICTS, Donald Talawa (kushoto). 
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Raphael Benedict (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa TICTS Jared H. Zerbe (katikati) wakibadilisha mikataba ya makubaliano ya kushirikiana katika kuhakikisha wateja wa TICTS wanafanya malipo yao kwa haraka na ufanisi zaidi kupitia tawi lolote la Ecobank hapa nchini. Mikataba hiyo ilisainiwa jana katika tawi la Ecobank lililopo PSPF Towers jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia kushoto ni Katibu Mkuu wa Tanzania Freight Forwarders Association (TAFFA), Tony Swai. 


  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA  0 0   Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Kujanakushoka Tools Manufactures Group Bw. Leonard Kushoka (kushoto) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitambulisha mashine ya kuzalisha mkaa mbadala utokanao na takataka, kulia ni mmoja ya wafanyakazi wa kampuni hiyo Bi. Zainabu Mtiga.
  blu2
  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Kujanakushoka Tools Manufactures Group Bw. Leonard Kushoka wakati akitambulisha mashine ya kuzalisha mkaa mbadala utokanao na takataka mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
  blu3
  Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Kujanakushoka Tools Manufactures Group Bw. Leonard Kushoka akielekeza waandishi wa habari (hawapo pichani) namna mashine inavozibadili takataka na kuwa nishati ya mkaa mbadala.

  0 0  0 0  Abiria wakiwa wamevalia maboya maalumu ya kujiokolea ndani ya Boti ya MV. Mkongo inayosimamiwa na Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA). Boti hiyo inatoa huduma za usafiri katika mto Rufiji kati ya Utete na Mkongo wilayani Rufiji Mkoani Pwani.
  Boti za raia zilizokua zikitumika kuvusha abiria katika Mto Rufiji kati ya Utete na Mkongo kabla ya ujio wa Boti ya MV. Mkongo kuletwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) zikiwa zimepakia abiria tayari kwa kuanza kuwavusha.
  Boti za raia zilizokua zikitumika kuvusha abiria katika Mto Rufiji kati ya Utete na Mkongo kabla ya ujio wa Boti ya MV. Mkongo kuletwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) zikiwa zimepakia abiria tayari kwa kuanza kuwavusha.
  Mkuu wa Kivuko cha Magogoni/Kigamboni Mhandisi Lukombe King’ombe akizungumza na waandishi wa Habari wa TBC1 waliotembelea kivuko hicho leo asubuhi na kufanya nae mahojiano ya moja kwa moja kupitia kipindi cha Jambo Tanzania.

  0 0

   Wakazi wa jijini Dar es Salaam waliotembelea Banda la Jeshi la Magereza, wakiangalia nafaka mbalimbali zinazolimwa katika mashamba ya Magereza nchini kwenye Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa, yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere,Barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
   Askari wa Jeshi la Magereza, Happy Kweka, akiwaonyesha vitambaa vinavyotengenezwa na jeshi hilo wakazi waliotembelea Banda la jeshi hilo katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea   katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere,Barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.
   Wakazi wa jijini Dar es Salaam waliotembelea Banda la Jeshi la Magereza, wakiangalia vikapu vinavyotengenezwa katika viwanda vya ufumaji vya Magereza nchini kwenye Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa, yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere,Barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.Kulia ni askari wa  jeshi hilo,Issah Ramadhan


  0 0


  0 0

  Kampuni ya Mantrac Tanzania imezindua mpango maalum wa kukodisha na kumiliki mitambo kwa kulipa kidogo kidogo ili kuwarahisishia wateja mzigo wa kulipa fedha kununua mtambo kwa mara moja.

  Hii inamaanisha kuwa wafanyabiashara na wakandarasi wataweza kukodisha mitambo kutoka katika kampuni ya Mantrac Tanzania kwa bei nafuu na kuanzia miezi sita na kuendelea anakuwa mmiliki kamili wa mtambo huo.Hayo yamesemwa na mkuu wa kitengo cha mipango na masoko Bw Valence Pantaleo. 

  Alisema katika kipindi chote cha kukodisha, kampuni ya Mantrac Tanzania inagharamia matengenezo ya mtambo huo kadiri ya mwongozo wa kampuni ya CAT.Mpango wa kukodisha na kumiliki ni maalum ambao unamwezesha mkandarasi au mfanyabiashara kupata manufaa lukuki ya kutumia mitambo inayotumia tekinolojia ya kisasa kabisa ya kampuni ya CAT bila ya kununua mtambo huo mwanzo wa mradi.

  Mpango huu unatoa unafuu mkubwa sana na huweza kupunguza sana gharama za uendeshaji kwa mkandarasi au mfanyabiashara.Kampuni ya Mantrac Tanzania inamhakikishia mteja mitambo na tekinolojia madhubuti ya Catepillar yenye historia pana ya kutengeneza na kuuza mitambo ya kisasa inayotumia katika miradi mikubwa ya kujenga miundombinu.
  Miradi hii mikubwa ya miundombinu ni pamoja na ujenzi wa barabara, reli, majengo, madaraja, kwenye madini na kilimo.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  Meneja Masoko wa Mantrac  Bw Valence Pantaleo.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  WATANI wa jadi Simba na Yanga watakutana Agosti 23 katika mchezo wa ngao ya hisani ikiashiria ufunguzi msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom 2017/18.

  Pazia rasmi la ligi hiyo litafunguliwa Agosti 26 ambapo mechi saba zitachezwa katika viwanja mbalimbali nchini ambapo itamalizika Mei 20 mwakani kwa kupatikana bingwa mpya.

  Ofisa Habari wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) amewaambia Waandishi wa Habari kuwa mchezo huo wenye kuvuta hisia za mashabiki wengi ndani na nje ya nchi utafanyika kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

  "Mchezo wa ngao ya hisani kati ya Simba na Yanga utafanyika Agosti 23 kwenye uwanja wa Taifa ukiashiria kuanza kwa msimu mpya wa ligi 2017/18 na wiki moja mbele itaanza rasmi," alisema Lucas.

  Aidha Lucas amesema miamba hiyo itakutana tena Oktoba 14 katika mchezo wa kwanza wa msimu kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa.

  Ratiba ya michezo katika wiki ya kwanza ya ligi hiyo.

  Agosti 26
  Ndanda vs Azam FC
  Mwadui FC vs Singida United
  Mtibwa Sugar vs Stand United
  Simba vs Ruvu Shooting
  Kagera vs Mbao FC
  Njombe Mji vs Prisons
  Mbeya City vs Majimaji

  Agosti 27
  Yanga vs Lipuli.older | 1 | .... | 1799 | 1800 | (Page 1801) | 1802 | 1803 | .... | 3285 | newer