Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109605 articles
Browse latest View live

hoja ya haja: Tujihadhari na wizi wa mitandao

0
0

Kaka issa
Heri ya Mwaka mpya 2013, Naomba kuwakilisha maoni yangu kuhusu hili la wizi wa fedha kwa kutimia mtandao
Kwa muda sasa wa wiki nzima, tumekuwa tukisoma kwenye vombo vya habari wizi wa fedha kwa mtandao au kwa kutumia kadi zinazotolewa na Bank, za ATM Card, Mastercard ama Visa. Kusema ukweli hili suala sijui kama benki za Kitanzania zinaichukua kwa umuhimu uliyonao, ni Hatari kuliko wanavyoichukulia.
Ukweli ni kwamba Benki pekee haziwezi kuhimili mapambano ya Cybercrime, kama kweli tunaelewa na kutambua kwa undani ukubwa wa hili tatizo. Mfano, katikati ya Mwaka 2012, Banki zote Marekani ziliwekwa kwenye ‘high alert’ na vyombo vya usalama kuwa kuna wahalifu wa kimtandao ambao walikuwa wakitaka kuiba fedha kwenye account za wateja wao. Kazi hiyo ilifanywa kwanza na FBI kuitercept uhalifu huo, kabla benki kuchukua hatua.
Hivi ni vita ambavyo vinapiganwa na vyombo vya usalama vya nchi. Cybercrime ni kubwa kuliko mabenki wanavyoifikiria, mwaka jana peke yake, wahalifu wa kimtandao walijaribu kuiba Paundi 2.5 Billion kutoka mabenki mbalimbali Ulaya peke yake achilia nchi zingine kama Asia na America. Ni vita ambavyo Tanzania peke yake hawawezi kuvipigania. Wakati Viongozi wetu wakifanya vikao vya kutaka kuwa kuwadhibit M23, hiyo kazi waichie drones za Obama, na waanze kupambana na Cybercrime ambayo miaka 20 ijayo itatufanya turudi kwenye ukoloni kwasababu tutakuwa tukiwategemea wazungu kutusaidia katika hivo vita.
Elimu ya usalama wa fedha za wateja unahitajika sana tena sana miongoni mwa wafanya kazi wa benki zetu. Usalama wa Banking System pia benki wanatakiwa kuangalia. Mfano, haiwezekani computer ya banki ambayo mfanyakazi wa benki hutumia kuangalia account za wateja, na akimaliza anaingi facebook kuchat. Mara nyingi mtu unaweza kuforwadiwa email ilikwisha pelekwa kwa zaidi ya watu Elfu na ukiangalia imetoka wapi usishangae ukaona john.idd@benkifulani.com.  Huwezi kuingia kwenye website yoyote kwa kutumia mtandao wa Benki. 
Kuna websites ambazo kazi zake ni kuwapatia hawa wahalifu taarifa zote za kila computer itakayoingia kwenye hiyo website. Benki zetu waache ubahiri waanze kuinvest kwenye security technology, na lazima wawe na cyberwatch team masaa 24 siku saba kwa wiki. 
Mambo mengine ni uzembe wa mawazo na kwasababu ajira ni kwa kujuana inakuwa ngumu sana kudhibiti matatizo kwenye mabenki zetu kwasababu hatujui wafanyakazi wanaofanya kazi kwenye maeneo nyeti kama haya wana uaminifu kiasi gani kwa pesa za wateja wao. Na inawekana hatuna huduma ya 'security clearance' kwenye kazi yenye kuhitaji uaminifu wa kiwango hiki.
Naomba kuwakilisha kaka.
Mdau US

WASHIRIKI WA SHINDANO LA GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE WAtimka afrika kusini

0
0


Meneja wa kinywaji cha Guinness.Davis Kambi akiongea.
 Meneja wa kinywaji cha Guinnes, Davis Kambi akipiga picha ya pamoja na washiriki wa shindano la Guinness Football Challenge wakati walipokuwa wakiagwa kwenye mgahawa wa City Sports Lounge Posta ,jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki .Washiriki hao wameondoka usiku wa kuamkia jana kuelekea nchini Afrika Kusini ambako watashiriki katika shindano hilo.
 Meneja wa kinywaji cha Guinnes, Davis Kambi akimkabidhi tiketi za ndege na hati za kusafiria kwa kiongozi wa  washiriki wa shindano la Guinness Football Challenge,Mohamed Kobembe kwenye hafla fupi iliyofanyika mwishoni mwa wiki ndani ya kiota cha maraha cha City Sports Lounge kilichopo katikati ya jiji la Dar.

mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya bia ya serengeti, steve gannon atembelea mjengoni clouds media group.

0
0


Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga 'Joe' pichani kushoto akichanganua jambo kwa Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Steve Gannon mara baada ya kutembezwa studio mpya na ya kisasa kabisa,iliyofungwa mjengoni humo,ambayo inatarajia kuanza kutumika hivi karibuni,Steve Gannon amefanya ziara fupi mwishoni mwa wiki na kutembelea vitengo vyote vya kampuni hiyo na kujionea namna shughuli mbalimbali zinavyofanyika mjengoni humo.
Steve Gannon akitazama picha za wasanii mbalimbali wa nje waliowahi kufika nchini Tanzania na kufanya maonesho yao kadhaa ndani ya ofisi za Prime Time Promotions Ltd.
Mkurugenzi wa mambo ya utafiti na vipindi vya Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akifafanua jambo kwa Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Steve Gannon ambaye nae alikuwa akimsikiliza kwa makini.
Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Steve Gannon akimuuliza jambo mtangazaji wa kipindi cha Power Breakfast,Gerald Hando kuhusiana na mambo mbalimbali ya kikazi,alipotembezwa kwenye studio ya ziada.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga 'Joe' pichani kushoto akifafanua jambo kwa Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Steve Gannon mara baada ya kufanya ziara fupi mwishoni mwa wiki na kutembelea vitengo vyote kampuni hiyo huku akijionea namna shughuli mbalimbali zikifanya mjengoni humo.
Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Steve Gannon akizungumza jambo na baadhi ya wafanyakazi wa kitengo muhimu cha kampuni hiyo cha Masoko.Kwa picha zaidi Bofya JIACHIE BLOG.

BEKO extends its footprints to Tanzania, East Africa

0
0


Prime Minister Mizengo Pinda cuts a ribbon to mark official opening of the first showroom in East Africa to stock BEKO products, a renowned electronic manufacturing brand from Turkey. The showroom which is housed at KIDA Plaza in Mikocheni B, Dar es Salaam is being managed by Modern Holdings (EA) Limited. On his left is Deputy Minister of Trade and Industry, Gregory Teu and on his left is Chairman of Modern Holdings (EA) Limited Anselm Minja followed by Ambassador of Turkey to Tanzania Ali Davutoglu.
Prime Minister Mizengo Pinda shares a light moment with the Deputy Minister of Trade and Industry, Gregory Teu and Chairman of Modern Holdings (EA) Limited Anselm Minja after cutting a ribbon to mark official opening of the first showroom in East Africa which will stock and distribute BEKO products from Turkey. The showroom is which is housed at KIDA Plaza, Mikocheni B in Dar es Salaam will be managed by Modern Holdings (EA) Limited.
Director of sales for BEKO products, responsible Middle East, Africa and Turkic Republic, Murat Buyukerk shows Prime Minister Mizengo Pinda some of the products manufactured by the Turkish company shortly after Pinda launched the first showroom in East Africa which will stock and distribute BEKO products which is housed at KIDA Plaza in Mikocheni B, Dar es Salaam. The showroom is managed by Modern Holdings (EA) Limited. Right is Chairman of Modern Holdings (EA) Limited Anselm Minja.
Lucky winners of a sweepstake which was done during the launch of the first showroom in East Africa which will stock and distribute BEKO products which is housed at KIDA Plaza in Mikocheni B, Dar es Salaam, poses for a group photo with some BEKO officials. Shop it stands for Modern Holdings (EA) Limited becomes the first in the East African region. The showroom is the first in East Africa is managed by Modern Holdings (EA) Limited.
 Director of sales for BEKO products, responsible Middle East, Africa and Turkic Republic, Murat Buyukerk shows Prime Minister Mizengo Pinda some of the products manufactured by the Turkish company shortly after Pinda launched the first showroom in East Africa which will stock and distribute BEKO products which is housed at KIDA Plaza in Mikocheni B, Dar es Salaam. The showroom is managed by Modern Holdings (EA) Limited. Right is Chairman of Modern Holdings (EA) Limited Anselm Minja.

Msanii Lady Jay dee atangaza utalii wa ndani kwa kupanda mlima Kilimanjaro

0
0
Msanii wa muziki Judith Wambura maarufu kama Lady Jay Dee akiwa ameshikwa mikono kusaidiwa kushuka kutoka mlima Kilimanjaro aliko panda Jaanuary 8 mwaka huu na mumewe Gadner G Habash kwa lengo la kutangaza utalii wa ndani.
Mhifadhi mkuu wa mlima Kilimanjaro Erastus Lufungulo akimuongoza msanii Lady Jay Dee mara baada ya kushuka kutoka mlima Kilimanjaro,shoto mwa Jay dee ni mpiga picha wa JayDee,Bw Justine Bayo.
Mhifadhi mkuu (KINAPA)Erastus Lufungulo akimkabidhi cheti cha uthibitisho wa kufika kileleni msanii Lady Jay Dee.
Mhifadhi mkuu (KINAPA)Erastus Lufungulo akimkabidhi Gadner Habash cheti cha uthibitisho wa kufika kileleni Gadner G Habash.
Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya mlima Kilimanjaro (KINAPA), Erastus Lufungulo akimkabidhi cheti Bw. Justin Bayo baada ya kufanikiwa kufika katika kilele cha Uhuru.
Msanii Lady Jay Dee,mumewe Gadner na mpiga picha wao Justine wakimsikiliza kwa makini mhifadhi mkuu wa Mlima Kilimanjaro Erastus Lufunguro(hayupo pichani).
Mume wa msanii Lady Jay Dee aliyekuwa ameambatana nae katika safari hiyo ya siku tano Gadner G Habash akizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani) mara baada ya kushuka katika lango kuu la Marangu.
Msanii Lady Jay dee akizungumza na wanahabari( hawapo pichani) mara baada ya kufanikiwa kushuka salama kutoka mlima Kilimanjaro.
Mhifadhi mkuu (KINAPA)Erastus Lufungulo akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumpoekea msanii Lady Jay Dee mara baada ya kushuka kutoka mlima Kilimanjaro.

Vacancy- Financial Controller

0
0

Global Skill Consulting and Education on behalf of our client a fast growing start up company based in Arusha,  is seeking a Financial Controller for the Arusha office.

Job description
The controller will manage accounting systems, financial controls, accounts payable, accounts receivable, and journal entries. They will also assist in a successful audit. They will need to make journal entries themselves, but will be expected to build an accounting team around them as the company grows. The company uses a web-based accounting software called Xero.

The ideal candidate must be a quick learner who can adapt to this tool. The ideal candidate must also be comfortable working by themselves and making decisions - this is not an environment where there will always be someone telling them exactly what to do. The candidate must have fluent English, as this is a English-language office. The candidate must be smart, ambitious, trustworthy, ethical, and willing to grow with the company.

They must also have experience managing a commercial P&L statement. They must be a team player and enjoy working as part of a small, dedicated team that does whatever it takes to get the job done

Education Requirement
·         Bachelor's degree program in accounting, finance, business administration/management.
·         Individual with CPA will be given a preference
·         Minimum  of 3-5 years of experience
·         Exemplary communication skills in both oral and written aspects

If you are  qualified send your resume by Email to apply@globalskill.co.tz indicating the job title as a subject

BREAKING NYUZZZZ: WANAFUNZI WA VYUO VYA IFM NA MWALIMU NYERERE KIGAMBONI WAANDAMANA HIVI SASA

0
0
TAARIFA ILIYOIFIKIA GLOBU YA JAMII MUDA HUU INAELEZA KUWA,WANAFUNZI WA VYUO VYA IFM NA KILE CHA MWALIMU NYERERE KULE KIGAMBONI,WANAANDAMANA HIVI SASA KUELEKEA WIZARA YA ULINZI HUKU WAKIIMBA KUWA "WAMECHOKA KUIBIWA" IKIWA NI KUTOKANA NA MATUKIO YA KUIBIWA MARA KWA MARA.

HALI HIYO IMEFIKIA BAADA YA KUONA MATUKIO YA NAMNA HIYO YAMEZIDI KUSHIKA KASI HUKU WAKIONA JESHI LA POLISI HALICHUKUI HATUA YEYOTE KWA WEZI HAO.

RIPOTA WA GLOBU YA JAMII YUPO ENEO LA TUKIO HIVI SASA NA TUTAENDELEA KUJUZANA KINACHOENDELEA KATIKA MAANDAMANO HAYO NA PICHA KIBAO ZITAFUATA.

WAPIGANAJI WALIPOKUTANA JIJINI DAR


WAGOMBEA TFF KUPATA FOMU KWENYE MTANDAO

0
0

Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inawaarifu wadau wote kuwa fomu za maombi ya uongozi wa TFF na Tanzania Premier League Board (TPL Board) zinapatikana pia kwenye tovuti ya TFF.

Wote wanaopenda kugombea uongozi katika vyombo hivyo wanaarifiwa kuwa wanaweza kupata fomu hizo kwenye tovuti ya TFF (www.tff.or.tz) na wanatakiwa kulipia fomu hizo katika akaunti ya TFF namba 01J1019956700 iliyoko CRDB tawi la Holland House.

Fomu zikiambatanishwa na risiti ya malipo (receipt) au malipo ya benki (deposit slip) zirejeshwe kwa Katibu Mkuu wa TFF kwa mkono au kwa barua pepe (email) ambayo ni tfftz@yahoo.com kabla ya saa 10 kamili alasiri ya Januari 18 mwaka huu.

Kwa wagombea wanaorejesha fomu kwa mkono kuna fomu ya orodha (register) ambayo wanatakiwa kusaini wakati wanakabidhi.

Kamati ya Uchaguzi
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

NSSF KAHAMA YATOA ELIMU KUHUSU MAFAO MBALIMBALI WANAYOYATOA KWA WAFANYAKAZI WA MGODI WA DHAHABU WA AFRICAN BARRICK GOLD (ABG) BULYANHULU

0
0
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa (NSSF) Kahama, Omari Mziya (kulia), akikabidhi hundi ya Milioni 2/- kwa Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa African Barrick Gold (ABG) Bulyanhulu, Dennis Hoof ikiwa ni moja ya udhamini ya mfuko huo katika kufanikisha Siku ya Wanafamilia ya mgodi huo, iliyofanyika mgodini wilayani Kahama juzi. NSSF pia ilitoa jumla ya T-shirts 200.
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa (NSSF) Kahama, Omari Mziya akizungumza kabla ya kukabidhi hundi.
Afisa Mwandamizi wa NSSF Kahama, Lusajo Enest (kushoto), akitoa elimu kuhusu mafao mbalimbali yanayotolewa na mfuko huo kwa wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu wakati wa Siku ya Wanafamilia.

QChilla: Walionishusha walichangia kutumia na madawa ya kulevya

0
0
Q Chilla amesema kuingia kwake kwenye matumizi ya madawa ya kulevya ilisababishwa na baadhi ya watu kuchangia kumrudisha chini na kujikuta yuko peke yake katika mitihani aliyokuwa akipitia.

Huku akikataa kuwataja kwa majina alisema watu hao walihakikisha kila anachokifanya hakifanikiwi na kujikuta katika wakati mgumu. Akiongea na Fina Mango kwenye kipindi cha Makutano, Qchilla amesema alishindwa kujua amemkosea nani au nani amuombe msamaha.

Hata hivyo anasema anawashukuru watu wake karibu waliokuwa wakisikitishwa na hali aliyokuwa nayo na kuamua kumshauri aache kutumia madawa hayo.

Alipoulizwa anawashauri vipi wasanii ambao wametumbukia kwenye matumizi hayo alisema njia pekee ni kukubali kuwa wana tatizo na kuishika dini.

Pia aliipongeza hatua ya rais Kikwete kumsaidia Ray C ambaye pia alikuwa aliingia katika wimbi hilo akitolea mfano wa rais Nelson Mandela aliejaribu kumsaidia mwanamuziki Brenda Fassie na Rais Obama aliemsaidia marehemu Whitney Houston na kusisitiza wasanii wote ambao ni waathirika wa madawa ya kulevya kujitokeza ili wasaidiwe na jamii.

Q Chilla amesema kwa sasa anafanya muziki akilenga soko la kimatafifa zaidi akiwatolea mfano PSquare na kusema tatizo la wanamuziki wengi kuishia kusikika nchini tu ni kujiwekea mipaka na kulenga soko la ndani tu na kumalizia hana mpango wa kutoa album badala yake ataendelea kutoa nyimbo kali.

Kusikiliza au Ku-download mahojiano yote na Qchilla bofya hapa: https://soundcloud.com/makutano-na-fina-mango/makutano-show-mahojiano-na-1
QChilla akiongea katika kipindi cha Makutano Magic FM
Fina Mango akimsikiliza QChilla wakati akijibu moja ya maswali katika kipindi.
Muendeshaji wa kipindi cha Makutano Fina Mango akiwa na QChilla na mwanae Nuru baada ya kipindi.

ngoma azipendazo ankal - Kizazi kipya

0
0
Japo kabaki mpweke baada ya kuondokewa na Freddy Ndala Kasheba, Mzee Mzima Kikumbi Mwanza Mpango a.k.a King Kikii bado anaendeleza libeneke. Sikiliza hicho 'Kitambaa Cheupe'

ngoma azipendazo ankal - enzi hizo

0
0
Bi Kidude na ngoma yake ya 'Muhogo Wa Jang 'Ombe' wa enzi na enzi bado anadai

ngoma azipendazo ankal - kizazi kipya

0
0
Ngoma ya Beyoncé ya 'Run The World (Girls)' ni moto!

Digital Video Editing Training - CoiCT


Taarifa ya kupata nyufa kwa kioo cha ndege ya ATCL

0
0
  ATC kioo chenye crake
 Ndege ya ATCL ikiwa imetua uwanja wa Kigoma baada ya kioo chake kupata nyufa na kulazimika kutua,hii ni tofauti na taarifa zilioneshwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa ndege hiyo iliharibika vibaya sehemu yake ya mbele pamoja na mabawa yake.

====  ======= ====== =======

Taarifa ya kupata nyufa kwa kioo cha ndege ya ATCL. 

uhuru marathon

BALOZI KHAMIS KAGASHEKI AKUTANA NA WACHEZAJI WA SEATLLE SOUNDERS KATIKA HOTELI YA SERENA JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na ujumbe wa wachezaji na waandishi wa habari kutoka timu ya seattle Sounders ya Nchini Marekani wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Bodi ya Utalii ya Tanzania TTB kwenye hoteli ya serena jijini Dar es salaam jana kwa ajili ya ugeni huo, Bodi ya Utalii ilisaini mkataba wa kutangaza utalii wa Tanzania katika kiwanja cha timu hiyo katika ziara iliyofanywa na Waziri wa Maliasili Balozi Khamis Kagasheki nchini humo katika msafara huo unaoongozwa na mchezaji wa mpira wa American Football Kevin Griffin ambaye pia ni Fan Development Marketing wa Sunders FC, wachezaji hao walitembelea mbuga za Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Mbuga ya Tarangire ambapo walipata muda wa kujionea vivutio vilivyomo katika hifadhi hizo na kupiga picha.
Balozi Khamis Kagasheki akimsikiliza mmiliki wa timu ya Africa Lyon Rahim Kangezi ambaye ndiye mwenyeji wa wageni hao wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa kwenye hoteli ya Serena Dar es salaam jana, kushoto ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Razalo Nyalandu.
Ugeni huo ukipata chakula cha jioni katika hoteli ya Serena jana usiku kutoka kulia ni Kevin Griffin mchezaji wa mpira wa American Footballn Kasey Keller mchezaji maarufu wa mpira wa miguu vilabu mbalimbali Ulaya na Marekani na mchezaji wa timu ya Taifa ya MarekaniKristen Addings kutoka Taasisi ya Washington Global Hearthna David Glass Mtaalam Video na Majarida
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Lazaro Nyalandu katika hafla hiyo kushoto ni Ibrahim Mussa Mkurugenzi wa Utalii Wizara ya Maliasili na Utalii
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Dr. Aloyce Nzuki akizungumza na Devotha Mdachi Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi hiyo wakati wa hafla hiyo, katikati ni Mmiliki wa timu ya Africa Lyon Rahim Kangezi.
Devotha Mdachi Mkurugenzi wa Masoko Bodi ya Utalii Tanzania TTB akimkaribisha Mh. Waziri Balozi Khamis Kagasheki na wageni kutoka Seatlle Sounders kwa ajili ya kujitambulisha na kupata chakula cha jioni kilichoandaliwa na bodi hiyo.
Kevin Griffin ambaye ndiyo kiongozi wa msafara huo akimshukuru Mh Waziri na Uongozi wa Bodi ya Utalii TTB kwa ushirikiano waliouanzisha katika kutangaza utalii wa Tanzania nchini Canada.
Kasey Keller akizungumza katika hafla hiyo.

Kasey Keller akimkabidhi zawadi ya Saa Mh. Lazaro Nyalandu Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii.
Kasey Keller akimkabidhi zawadi ya saa Ibrahim Musa Mkurugenzi wa Utalii katika Wizara ya Maliasili na Utalii.

Mh. Waziri Balozi Khamis Kagashiki akiongozana na Mchezaji wa Seatlle Sounders Marc Burch kuelekea katika meza ya chakula.
Mh. Lazaro Nyalandu Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji na waandishi wa habari kutoka Seatlle Sounders nchini Marekani pamoja na uongozi wa Bodi ya Utalii na Wizara ya Maliasili na Utalii.

PARTY YA KUMUAGA BALOZI MAAJAR DC

MWANRI AMALIZA ZIARA YAKE YA SIKU SABA MKOANI RUKWA, ASEMA HALMASHAURI ZITAKAZOPATA HATI CHAFU KUTOPATA RUZUKU SERIKALINI

0
0

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ndugu Agrey Mwanri akitoa maelekezo mbalimbali kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa katika majumuisho ya ziara yake iliyodumu kwa muda wa siku saba Mkoani Rukwa ambapo alitembelea miradi zaidi ya 22 ambayo baadhi yake aliiwekea mawe ya msingi. Katika hotuba yake hiyo alitoa maagizo mbalimbali ambayo yote yalikuwa yakilenga kwenye utawala bora, matumizi bora ya fedha za Serikali katika miradi pamoja utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010. Katika hotuba yake iliyodumu kwa zaidi ya saa tatu alizionya halmashauri zote nchini zitakazopata hati chafu kuwa hazitapata fedha ya ruzuku ya miradi ya maendeleo (LGCDG-Local Government Capital Development Grant) ikiwa ni kutoa funzo kwa watendaji wa halmashauri pamoja na kupandisha hasira za madiwani ili waweze kuisimamia vizuru halmashauri husika. 
Mama Grace Mwanri, mke wa Naibu Waziri wa TAMISEMI Agrey Mwanri akitoa ushuhuda kuhusu utendaji wa mumewe "Anavyoongea na kutenda mume wangu ndivyo alivyo hata nyumbani na si kwamba anafanya hivyo kupata sifa wala umaarufu kwani mara zote huwa hapendi mambo ya kipuuzipuuzi" alisema mama Mwanri.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Viewing all 109605 articles
Browse latest View live




Latest Images