Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA DKT. JUMA MALEWA AFUNGA RASMI MAFUNZO YA MUZIKI WA BRASS BAND YA JESHI LA MAGEREZA, JIJINI DAR

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akisalimiana na Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Naibu Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana alipowasili kwenye hafla ya kufunga mafunzo ya muziki wa Brass Band ya Jeshi la Magereza kwenye Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 11, 2017(kushoto) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akipokea salaam ya heshima kutoka kwa gwaride maalum katika hafla fupi ya kufunga mafunzo ya muziki wa Brass Band ya Jeshi la Magereza kwenye Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 11, 2017.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akikagua gwaride maalum katika hafla fupi ya ya kufunga mafunzo ya muziki wa Brass Band ya Jeshi la Magereza kwenye Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 11, 2017.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akikagua Gadi ya wahitimu wa mafunzo ya muziki wa Brass Band ya Jeshi la Magereza kwenye Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 11, 2017.


MAMA MERY MAJALIWA ATAKA WAZAZI KUWASOMESHA KWA BIDII WATOTO WA KIKE

$
0
0

Mke wa Waziri Mkuu  Mery  Majaliwa  ametoa Wito kwa Wazizi kupeleka  Watoto wa Kikeke  Shule  ametoa  wito huo katika  mkutano wa hadhara  Uliofanyika  Kiwanja cha  Michezo wilaya ya Liwale July 10, 2017 ,Mama majaliwa  ameongozana na Waziri Mkuu Kassim  Majaliwa  katika ziara ya kikazi  ya siku Nne  Mkoani   Lindi.Pcha na Ofisi ya Waziri Mkuu.
  
Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa  akiangalia Dawa zilizopo katika Stoo ya Dawa Hospital ya  Wilaya ya Liwale July 10, 2017 ,kushoto  kwa  Waziri  Mkuu  ni  Mbunge  wa Wilaya ya Ruangwa(CUF)   Zuberi  Kichauka  na  kulia ni  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Lindi Dr Maulid Majala, Waziri Mkuu Kassim  Majaliwa  yupo  katika ziara ya kikazi  ya siku Nne  Mkoani Lindi

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA MOBILE 360 AFRICA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kusimamia na kuweka mazingira bora yatakayosaidia mamia ya wananchi nchini wanapata huduma za mawasiliano ya simu kwa njia ya kisasa zaidi mjini na vijijini.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati anafungua Mkutano wa mwaka wa Chama cha Makampuni ya Simu Duniani (GSMA MOBILE 360) Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassana amesema anaimani kuwa wadau hao wa makampuni ya simu watajadili kwa kina namna bora ya kufikisha mawasiliano ya kisasa kwa wananchi na kuweka mipango mizuri ya kufikia wananchi wengi zaidi hasa maeneo vijijini ambayo baadhi ya maeneo hayafikiki kutokana na uduni wa miundombinu.

“Ningependa kusema kwamba Tanzania inakubali sana ushirikiano na GSMA na tunatamani kupanua ushirikiano wetu na uwezeshaji kwa Watu wetu kwa njia ya sekta ya simu ili kufikia utekelezaji wa ajenda za Maendeleo endelevu ya Umoja wa Afrika AU na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa 2020”.Amesisitiza Makamu wa Rais.

Ameleeza kuwa kwa sasa Tanzania ni miongoni mwa nchi kadhaa Kusini mwa Bara la Afrika ambayo inafanya vizuri kwa wananchi wake kutuma fedha kwa kutumia simu za mkononi na kusema kuwa hilo ni jambo zuri hasa kutokana na baadhi ya wananchi kutokuwa na akaunti za benki hivyo huduma hiyo huwasaidia kwa kiasi kikubwa kwa kutuma fedha kwa urahisi.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesisitiza umuhimu wa kuimarishwa zaidi kwa huduma za kisasa za kimtandao ili wananchi waweze kunufaika zaidi kwa njia hiyo katika sekta za elimu,afya, kilimo, biashara na masuala ya kijinsia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kukuza matumizi ya teknolojia ya simu ili kufikia maendeleo endelevu ulioandaliwa GSMA Mobile 360 Africa kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Baadhi ya Wageni waalikwa mbalimbali wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kukuza matumizi ya teknolojia ya simu ili kufikia maendeleo endelevu ulioandaliwa GSMA Mobile 360 Africa kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).


NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MALIASILI, DKT. ALOYCE NZUKI AFUNGUA WARSHA YA KUKUSANYA MAONI YA KUBORESHA RASIMU YA SERA MPYA YA MISITU YA MWAKA 2016 KWA WAKAZI WA MIKOA YA KANDA YA KATI MJINI DODOMA

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki akizungumza wakati akifungua warsha iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa wadau wa Mikoa ya Kanda ya Kati kwa ajili ya kukusanya maoni ya kuboresha Rasimu ya Sera Mpya ya Misitu ya mwaka 2016 iliyofanyika mjini Dodoma leo. 
Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Ezeckiel Mwakalukwa akizungumza katika warsha iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa wadau wa Mikoa ya Kanda ya Kati kwa ajili ya kukusanya maoni ya kuboresha Rasimu ya Sera Mpya ya Misitu ya mwaka 2016 iliyofanyika mjini Dodoma leo. 
 Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (kushoto) akipokea vitabu vya Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mpingo Conservation Initiatives, Makala Jasper ambao wamesaidia kuchapisha nakala 1304 za sera hiyo kwa ajili ya kusaidia zoezi linaloendelea la kukusanya maoni ya kuboresha Rasimu ya Sera Mpya ya Misitu ya Mwaka 2016 katika warsha iliyoandaliwa na Wizara hiyo mjini Dodoma leo. Kulia anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezeckiel Mwakalukwa.
 Baadhi wa watumishi wa Wizara ya Maliasili na wadau wa sekta ya Misitu na Nyuki wakiwa kwenye warsha iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ajili ya kukusanya maoni ya kuboresha Rasimu ya Sera Mpya ya Misitu ya mwaka 2016, mjini Dodoma leo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

JWTZ KUKABIDHI MAJENGO WILAYA YA MISENYI

$
0
0

JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA

KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO


Simu ya Upepo  : “N G O M E”        Makao Makuu ya Jeshi,

Simu ya Mdomo: DSM 22150463    Sanduku la Posta 9203,

Telex                   : 41051                      DAR ESSALAAM, 11 Julai, 2017.

Tele Fax              : 2153426

Barua pepe       : ulinzimagazine@yahoo.co.uk

Tovuti                  : www.tpdf.mil.tz


Taarifa kwa Vyombo vya Habari


Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatarajia kukabidhi Majengo ya kituo cha afya Kabyaileishozi,kituo cha malezi ya Wazee cha kilima na shule ya sekondari ya Omumwami yaliyoko wilaya ya Misenyi Mkoani Kagera tarehe 12 Julai 2017 kuanzia saa mbili kamili asubuhi 2:00.


Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu SSera,Uratibu na Bunge Mhe Jenista Mhagama.


Ukiwa mdau wa habari inaombwa kutuma mwakilishi wa chombo chako cha habari ili kufanya coverage la tukio hilo muhimu kwa maendeleo ya Taifa letu.Natanguliza shukrani.


Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Uhusiano

Makao Makuu ya Jeshi, Upanga

S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.


Kwa Mawasiliano zaidi: 0756-716085

NAIBU WAZIRI LUHAGA MPINA AFANYA ZIARA KUKAGUA MAZINGIRA YA MTO MSIMBAZI

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akizungumzana wanahabari katikati ya Mto Msimbazi chini ya Daraja la jangwani baada ya kupima kiwango cha hewa ya Oxygen katika maji ya mto msimbazi na sampuli za maji hayo kupelekwa katika katika maabara ya mkemia mkuu wa serikali kwa vipimo zaidi, ili kujua kama maji hayo yana madhara kwabinadamu, mazingira na viumbe hai wengine.

Mto Msimbazi unavyoonekana
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira akiangalia kiasi cha hewa ya Oxygen kilichopo katika maji ya Mto msimbazi akisaidiwa na wataalamu kutoka katika maabara ya mkemia mkuu wa serikali hawapo pichani, katika eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Evelyn Mkoko

TRA YAFANIKIWA KUKUSANYA TRILLIONI 14.4 KWA MWAKA WA FEDHA 2016/17

Stella Manyanya akabidhi bendera kwa wanafuunzi watakaoiwakilisha nchi katika mashindano ya first lbal Robotic Challenges nchini Marekani

$
0
0
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya leo amekabidhi Bendera ya Taifa kwa wanafunzi saba wanaosoma masomo ya sayansi wanaokwenda kuiwakilisha nchi katika mashindano ya First Global Challenges nchini Marekani. Makabidhiano hayo yamefanyika katika shule ya Sekondari ya wasichana Jangwani. 

Katika makabidhiano hayo Mhandisi Manyanya amewataka wanafunzi wote nchini kusoma kwa bidii masomo ya sayansi, teknolojia na ubunifu ili kuhakikisha ndoto ya Tanzania ya kuwa na uchumi wa kati kupitia viwanda na biashara inafanikiwa na kwamba wizara tutaendelea na jukumu lake la kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia ili wanafunzi wote waendelee kufanya vizuri katika masomo ya sayansi.

Shule zilizotoa wanafunzi watakaoshiriki katika mashindano hayo ni pamoja na Jangwani, Azania, Jamhuri, Benjamini Mkapa, Feza na Kisutu.

Naye mratibu wa mashindano hayo kwa upande wa Tanzania ndugu Mkufu Shabani Tindi alisema mashindano haya yameanzishwa na kufadhiliwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la Marekani liitwalo FIRST yenye maana ya for inspiration and recognition of science and technology lenye lengo la kuhamasisha ulimwenguni kote vijana wanaosoma masomo ya sayansi, uhandisi, teknolojia na hesabu kuweza kutatua changamoto mbalimbali ulimwenguni 

Wanafunzi watakaoshiriki wanatarajia kuondoka kesho Juni 12, 2017 na watakuwa nchini Marekani kwa ajilia ya mashindano hayo makubwa kiulimwengu ambapo zaidi ya nchi 170 zitashiriki.

Naye mmoja wa washiriki Raymond Benedict kutoka Shule ya Sekondari Jamhuri amesema yeye wenzake wamejiandaa vizuri katika kuhakikisha wanaiwakilisha nchi katika mashindano hayo vizuri na kwa ufahari.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akikabidhi Bendera ya Taifa kwa wanafunzi watakaoshiriki katika mashindano ya First Global Robotic Challenges nchini Marekani.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya pamoja na baadhi ya wanafunzi watakaoshiriki katika mashindano ya First Global Robotic Challenges wakiwaonyesha wanafunzi wa shule ya wasichana Jangwani (Hawapo pichini) Roboti walioibuni. 
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akipata maelezo kutoka kwa mwanafunzi Raymond Benedict kutoka shule ya sekondari Jamhuri ya namna roboti iliyobuniwa inavyofanya kazi. 


HAFLA YA TUZO ZA SUPERBRANDS AFRIKA MASHARIKI ZAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Wakurugenzi na wawakilishi wa kampuni yaliyopata tuzo ya Superbrands wakiwa na mkurugenzi wa Superbrands Afrika Mashariki, Jawad Jaffer (wa tatu kutoka kushoto).
Mkurugenzi wa Superbrands Afrika Mashariki, Jawad Jaffer akiongea mapema leo katika halfa ya kukabidhi vyeti vya kudhibitisha ubora wa kampuni na bidhaa zinazokubalika Afrika Mashariki iliyofanyika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski, Dar es Salaam. Picha na Kajunason/Cathbert Kajuna.
Wakurugenzi na wawakilishi wa kampuni yaliyopata tuzo ya Superbrands wakimsikiliza mkurungenzi wakati wa hafla ya kutoa vyeti kwa kampuni zenye sifa katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski, Dar es Salaam.

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA DKT. JUMA MALEWA AFUNGA RASMI MAFUNZO YA MUZIKI WA BRASS BAND YA JESHI LA MAGEREZA, JIJINI DAR

$
0
0
MAL4
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akikagua Gadi ya wahitimu wa mafunzo ya muziki wa Brass Band ya Jeshi la Magereza kwenye Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 11, 2017.
MAL5
Wahitimu wa mafunzo ya muziki wa Brass Band ya Jeshi la Magereza wakipita mbele ya jukwaa kwa heshima katika hafla ya kufunga rasmi mafunzo hayo kwenye Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 11, 2017.
MAL6
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakiwa wamesimama kwa heshima kabla ya Wahitimu wa mafunzo ya muziki wa Brass Band ya Jeshi la Magereza kupita mbele ya jukwaa kwa heshima katika hafla ya kufunga rasmi mafunzo hayo.
MAL10
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa tatu toka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu wanawake wa  mafunzo ya muziki wa Brass Band ya Jeshi la Magereza. Walioketi wa pili toka kushoto ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga, (wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaa, Naibu Kamishna wa Magereza Augustine Mboje, (wa tatu toka kulia) ni Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Naibu Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana, (wa pili toka kulia) ni Boharia Mkuu wa Magereza, Naibu Kamishna wa Magereza Uwesu Ngarama na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mafunzo Jeshini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Charles Novart(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

DC- TABORA AONGOZA ZOEZI LA KUWAONDOA WAKULIMA WA MBOGA MBOGA WAVAMIZI WA BWAWA LA IGOMBE.

$
0
0
Na Tiganya Vincent-RS-Tabora

Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Tabora imeendesha oporesheni ya kung’oa mazao mbalimbali ya bustani yaliyokuwa yamepandwa na wavamizi katika maeneo ya vyanzo vya maji na kando kando ya Bwawa la Igome na hivyo kusababisha uzalishaji wa maji kupungua.

Kamati hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mwalimu Queen Mlozi iliendesha zoezi hilo jana mjini hapa baada ya kugunduliwa kuwepo kundi kubwa la watu wanaondeshea kilimo cha mazao mbalimabli ikiwemo matunda na kuhatarisha afya ya watumiaji.

Katika oporesheni hiyo mazao mbalimbali kama vile majani ya maboga, hoho, nyanya na matembele yaliweza kung’olewa.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya zoezi alisema kuwa wavamizi hao wakiendesha shughuli mbalimbali katika vyanzo vya Bwawa hilo ikiwemo kilimo cha mboga mboga na wakati mwingine wamekuwa wakiweka dawa ambazo wakati mwingine dawa hizo zimekuwa zikiingia katika maji hayo ambayo ndio wakazi wengi wa Wilaya ya Tabora wanatumia.

Mwalimu Mlozi aliongeza kuwa endapo maji hayo yasipowekewa dawa vizuri ya kusafisha upo uwezekano wa watumiaji kunywa dawa na kilimo zilizotoririkia majini.Aliongeza kuwa hali ya maji katika Bwawa hilo sio nzuri na endapo wavamizi hao wasipodhibitiwa upo uwezekano mkubwa wa wakazi wa Manispaa ya Tabora kukabiliwa na upungufu wa maji katika miezi ijayo.
 Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mwalimu Queen Mlozi (aliyeshika miche ya nyanya) akiongoza Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo kung’oa na kuwaondoa wakulima wa bustani walivamia kando kando ya Bwawa la Igombe na kusababisha uharibifu wa vyanzo vya maji vya Bwawa hilo. Zoezi hilo lilifanyika jana katika eneo la Bwawa hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mwalimu Queen Mlozi (wa kwanza kushoto) akiongoza Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo kung’oa na kuwaondoa wakulima wa bustani walivamia kando kando ya Bwawa la Igombe na kusababisha uharibifu wa vyanzo vya maji vya Bwawa hilo. Zoezi hilo lilifanyika jana katika eneo la Bwawa hilo.
Picha na Tiganya Vincent-RS  - Tabora.

CHUO CHA UTALII TANZANIA CHA WAKARIBISHA WATANZANIA KUJIUNGA NA CHUO HICHO

$
0
0
 Kaimu Mkuu wa Chuo cha Utalii Tanzania ,Rosada Msoma  akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya kozi mbalimbali zinazotolewa na chuo  cha Utalii nchini,mapema leo jijini Dar.Bi Rosada amewakaribisha watu mbalimbali kujiunga na kozi mbalimbali zitolewazo na chuo hicho.
 Baadhi ya watendaji wa Chuo cha utalii walioshiriki mkutano huo na waandishi wa habari juu ya kozi mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho,mapema leo jijini dar.
Waandishi wa habari walioshiriki mkutano huo wa  Waandishi wa Habari uliohusu juu ya kozi mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho

KUMBILAMOTO AMALIZA AHAADI ZAKE KATIKA KATA YA VINGUNGUTI

$
0
0
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto akihutubia wakazi wa Vingunguti wakati wa mkutano wake wa Hadhara wa kutekeleza ahadi alizoaahidi katika kata hiyo.
 wakazi wa Vingunguti  wakiwa katika mkutano huo wa Diwani wao Omary Kumbilamoto
 Diwani wa viti Maalum wa Chama cha Wananchi CUF  kata ya Upanga, Riziki Shahari akikabidhi jezi kwa timu ya mtaa wa kwa kombo
 Bondia wa Ubingwa wa kati wa zamani ,Rashid Matumla akikabidhi mpira kwa Veterani wa Vingunguti.

JAFO AWATAKA WAHANDISI KUSIMAMA IMARA KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI

$
0
0
NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amewataka wahandisi wa Halmashauri nchini kutumia taaluma zao ipasavyo katika usimamizi wa miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu katika halmashauri zao.

Jafo aliyasema hayo leo alipokuwa katika ziara maalum ya ukaguzi wa miradi ya barabara na madaraja katika Halmashauri ya wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.

Katika ziara hiyo, Jafo alikagua ujenzi wa barabara ya Lami ya kilometa moja katika mji wa Bahi inayojengwa na Ofisi ya Rais Tamisemi kupitia mfuko wa barabara.

Jafo alisema maagizo ya kuzingatia ubora wa barabara inayo jengwa ili iweze kudumu kwa muda ulio kusudiwa.Katika ukaguzi wa madaraja, Jafo alikagua ujenzi wa madaraja mawili ya Nkulugano na Chipanga pia daraja la barabara ya Chipanga- Kigwe yanayojengwa kwa mradi maalum wa kuondoa vikwazo kwa ufadhili wa fedha za DFID.

Jafo alimpongeza mhandisi wa halmashauri ya Bahi Eng. Geofrey Mkinga kwa usimamizi mzuri wa kazi hizo zinazoendelea.Akihitimisha ziara yake, Naibu Waziri Jafo aliwataka wahandisi wa halmashauri zote hapa nchini kusimamia ubora wa kazi za ujenzi kwa umakini na kuweka mbele maslahi ya Taifa.

Madaraja hayo mawili yanatarajiwa kukamilika mwezi oktoba mwaka huu na yatakuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wanaotumia barabara hizo.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Bahi Omary Badwel ameishukuru sana serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk.John Magufuli kwa kuwa madaraja hayo yalikuwa ni kikwazo kikubwa sana kwa maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua ujenzi wa daraja la Chipanga.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua daraja la Nkulugano ambalo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 95.
 Sehemu ya daraja hilo 
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua ujenzi wa barabara ya lami mji Bahi huku akitoa maelekezo kwa wataalam kuhakikisha ujenzi huo unazingatia viwango ili kudumu kwa muda mrefu. 

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA UJENZI WA DARAJA MTO LUKULEDI

$
0
0
*Asema watu wengi wamekufa wakikatiza katika eneo hilo
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea mradi wa ujenzi wa daraja la mto Lukuledi lenye urefu wa kilomita 30.45 linalounganisha mikoa ya Lindi na Mtwara na na kusema kwamba ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wake.
Amesema ujenzi wa daraja hilo unatakaogharimu sh. bilioni 5.4 ni mkombozi kwa wananchi wa mikoa hiyo hasa wa wilaya za Ruangwa na Masasi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakishirikiana katika masuala mbalimbali yakiwemo kilimo na huduma za kijamii. 
Waziri Mkuu amesema hayo leo Jumanne, Julai 11, 2017  alipotembelea mradi huo wa ujenzi wa daraja hilo katika kijiji cha Nandanga alipowasili wilayani Ruangwa akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi.
“Watu wengi wamepoteza maisha kwa kuliwa na mamba walipokuwa wakikatiza katika eneo hilo. Ujenzi wa daraja hili ni muhimu, watu wengi wa Ruangwa wanavuka kufuata matibabu katika hospitali ya Ndanda, wilayani Masasi na wakazi wa Ndanda wanavuka kufanya shughuli za kilimo wilayani Ruangwa.”
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipata maelezo ya mradi wa daraja la Nandaga, linalo unganisha Wilaya ya Ruangwa na Wilaya ya Masasi, kutoka kwa Mhandisi Josam Mlaki, kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) . 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua mradi wa daraja la Nandaga, linalo unganisha Wilaya ya Ruangwa na Wilaya ya Masasi, kutoka kwa Mhandisi Josam Mlaki, kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


UJENZI WA BARABARA ZA JUU UBUNGO WASHIKA KASI

$
0
0

 Mafundi ujenzi wakiwa eneo la mradi mahali ambapo patatumika kuanza kazi ya kucanganaya zege kwa ajili ya kwenda kumiminwa kwenye barabara  za juu
 Sehemu ya nyumba zilizobomolewa kupisha mradi wa barabara za juu katika eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam

Mafundi wakiwa kazini katika mradi huo wa barabara za juu



Maandalizi  katika eneo la ubungo Tanesco mahali ambapo panawekwa nguzo za barabara za juu yaani Fly Over  katika makutano ya barabara ya Morogoro na Sam Nujoma Ubungo jijini Dar es Salaam. 
Picha na Humphrey Shayo, Globu ya Jamii

MASAUNI AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO YA WIZARA YAKE MJINI BABATI, AHITIMISHA ZIARA YAKE MKOANI MANYARA LEO

$
0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wa pili kulia) akionyeshwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Afande Francis Massawe (kulia), jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Polisi mkoani humo ambalo limekwama ujenzi wake  mjini Babati mkoani humo. Mhe Masauni amemaliza ziara yake ya siku mbili mkoani humo kwa kutembelea ofisi mbalimbali zilizopo ndani ya Wizara yake.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akimsikiliza Afisa Uhamiaji Mkoa wa Manyara, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Juliette Sagamiko (kushoto) alipokua anatoa maelezo kuhusu Jengo la Makao Makuu ya Uhamiaji mkoani humo (linaloonekana nyuma ya viongozi hao), ambalo lipo katika hatua ya mwisho kukamilika lakini limekwama kuendelea na ujenzi wake. Katikati ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Afande Francis Massawe. 
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akipokea salamu ya heshima kutoka kwa Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Manyara. Watatu kulia ni Kamanda wa Jeshi hilo, mkoani humo, Heriel Kimaro. Masauni amemaliza ziara yake ya siku mbili mkoani humo kwa kutembelea ofisi mbalimbali zilizopo ndani ya Wizara yake. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Afande Francis Massawe, wakati alipokua akitoa taarifa fupi ya utendaji wa Jeshi hilo ofisini kwake mkoani humo.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mjue Mtunza Muda wa Old Moshi Sekondary School Anayetumia Hisia kutambua muda

$
0
0
Na Geofrey Chambua 
Hapa duniani kuna mambo mengi sana. Yapo ya kawaida na pia yapo ya kustaajabisha. Yanastaajabisha pale mtu binafsi unavyoona kwamba iko juu ya uwezo wako na wengine na kukufanya mhusika uone kama ni maajabu vile.
Nataka kusema ni kwa uwezo wa Mwenyenzi Mungu, kwa sababu binadamu anaweza kufanya kitu zaidi ya ufikiri wa binadamu mwenzake. ​Mmoja wa watu wa aina hiyo anaitwa Ramadhan Yasin Isuja (pichani) ambaye ni mwanafunzi wa Kidato cha Tatu Shule ya Sekondari Moshi (Zamani Old Moshi) mkoani Kilimanjaro.
Huyu kijana hakika ana kipaji cha pekee, kwani yeye ni MTUNZA MUDA wa shule mwenye ulemavu wa macho, lakini ana uwezo wa kukutajia SAA na DAKIKA bila kuangalia SAA. 
Na si hivyo tu, hata saa yenyewe wala SIMU hana maungoni mwake Sidhani kama utaamini kirahisi kama ambayo nami sijaamini maajabu hayo hata sasa lakini ndio ukweli halisi ambao nimeushuhuda bila kusimuliwa na mtu kwa kumuuliza majira zaidi ya mara tatu naye akinijibu bila kukosea hata chembe.
Licha ya kuwa mtunza muda wa Shule, Kijana Ramadhani pia ana uwezo wa kutaja ratiba ya shule nzima, yaani kila darasa na kipindi chake na hili tulilithibitisha wenyewe.
Ramadhani ni mzaliwa wa pili kwenye famlia ya watoto watano, na anasema wazazi wake walikua wakifanya kwa Wahindi na sasa mmojawapo anauza nguo, biashara ambayo ndiyo inayomsomesha kwa sasa. 
Katika ziara yangu niliambatana na Mkurugenzi wa Ubunifu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Dr Mafunda ambaye naye alichukua kumbukumbu kadhaa kwa tafakuri zaidi
Inline image 1Ramadhan Yasin Isuja mlemavu wa macho ambaye ni  mtunza muda (timekeeper) wa shule ya Sekondari Moshi (zamani Old Moshi) mkoani Kilimanjaro.
Inline image 2
Dr Dugushilu Mafunda (kulia) akiwa na kijana  Ramadhan Isuja na wanafunzi wenzie shuleni hapo

Inline image 4
Dr Dugushilu Mafunda akiwa anatajiwa noti na thamani yake na Ramadhan Isuja 

Inline image 3
​Dr Dugushilu Mafunda (Aluminae 1978) akipata ushahidi zaidi kwa wenzie na Ramadhan. Kulia ni Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule Hiyo Bwana Koshuma ...Wenye Imani haba huenda itakuwa vtema waende kumuona Shuleni Hapo..

WATUMISHI WA UMMA WALIOGHUSHI VYETI KUCHUKULIWA HATUA ZA KINIDHAMU

$
0
0
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) amesema Watumishi wa  Umma walioghushi vyeti watachukuliwa hatua za kinidhamu.
Mhe. Kairuki alisema hayo katika kikao kazi na watumishi na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke,Tarafa ya Mbagala mapema leo.

Mhe. Kairuki alisisitiza kuwa wote  walioghushi vyeti hawapo kazini na wameshafutwa katika orodha ya malipo ya Serikali (payroll) na kuelekeza waajiri kuwafuta wote wasiostahili kuwepo katika orodha ya malipo na wasimsubiri hadi afike katika maeneo ya kazi ili kutekekeza hilo.

“Baada ya zoezi la uhakiki kukamilika, hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa walioghushi vyeti kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na miongozo iliyopo katika Utumishi wa Umma” Kairuki alisema.

Aidha, aliwataka waajiri kuhakikisha wanahakiki taarifa za watumishi wapya wanapoajiriwa na wale wanaohamia ili kujiridhisha kama wana vyeti safi.

“Ni wajibu wa kila Mwajiri kuhakikisha kuwa Vyeti vya kila mwajiriwa mpya vinathibitishwa na Mamlaka husika kabla ya kumwajiri na hatimaye kumuingiza kwenye Orodha za Malipo ya Mishahara (Payroll) kupitia kwenye Mfumo wa HCMIS na Mifumo mingine ya mishahara ya kitaasisi.”

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Angellah J. Kairuki akizungumza na viongozi na watumishi wa umma wa tarafa ya Mbagala Wilaya ya Temeke alipofanya ziara katika tarafa hiyo kwa ajili ya kusikiliza kero za watumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Tawala Wilaya ya Temeke Bw. Hashim Komba

 Afisa Elimu Kata ya Mbagala Kuu Bibi. Mindi Kuchilingulo akichangia mada wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Angellah J. Kairuki kusikiliza kero za watumishi wa umma leo katika tarafa ya Mbagala Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam.

 Katibu Tawala Wilaya ya Temeke Bw. Hashim Komba akifafanua jambo wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Angellah J. Kairuki kusikiliza kero za watumishi wa umma leo katika tarafa ya Mbagala Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mhe. Waziri Angellah Kairuki

 Mkurugenzi Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma Bw. Issa Ng’imba akielezea shughuli zinazofanywa na idara yake wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Angellah J. Kairuki kusikiliza kero za watumishi wa umma leo katika tarafa ya Mbagala Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watumishi wa umma kutoka tarafa ya Mbagala Wilaya ya Temeke wakifuatilia hoja zilizokua zikiendelea wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Angellah J. Kairuki kusikiliza kero za watumishi wa umma leo katika tarafa ya Mbagala Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam. Picha na Genofeva Matemu - Maelezo. 
                                                    Taarifa kamili BOFYA HAPA

JIJI LA POTSDAM NCHINI UJERUMANI NA SHEHIA YA KIKWAJUNI JUU ZASAINI HATI YA MAKUBALIANO YA MAHUSIANO MEMA

$
0
0
Na Faki Mjaka - MAELEZO,  Zanzibar
Mji wa Drewits uliopo Jiji la Potsdam nchini Ujerumani kwa kushirikiana na Shehia ya Kikwajuni Juu wamesaini hati ya makubaliano ya Mradi wa mahusiano mema baina ya Jiji la Potsdam na Kikwajuni Mjini Zanzibar.
 Miongoni mwa Vipengele vya makubaliano hayo ni kuijenga miundombinu ya Majumba ya Mjerumani Kikwajuni ili kuhakikisha muonekano wake inafanana na Mji wa Drewits wa Potsdam Ujerumani. 
 Akizungumza katika Hafla hiyo Meya wa Jiji la Potsdam Jann Jakobs amesema amefurahi kuona mambo mbalimbali yameanza kutekelezwa kabla ya utiaji saini jambo ambalo linaonesha matumaini mazuri. 
Miongoni mwa mambo ambayo yameanza kutekelezwa ni pamoja na upandaji Miti inayozunguka Uwanja wa Mnazi mmoja na Mtaro wa kutirishia Maji machafu katika eneo hilo. Meya huyo amesema atahakikisha mradi huo unafikia malengo yake kwa ajili ya maslahi mapana ya Watu wa Ujerumani na Zanzibar kwa ujumla.
 Mstahiki Meya wa Jiji la Potsdam nchini Ujerumani Mhe. Jann Jakobs akikagua Mti alioupanda Mwaka 2014 alipotembelea Zanzibar mwaka huo.
 Mstahiki Meya wa Jiji la Potsdam nchini Ujerumani  Mhe. Jann Jakobs na Ujumbe wake wakipita katika Maeneo ya Kikwajuni kwa Mjerumaini kabla ya hafla ya kusaini hati ya Makubaliano ya Mradi wa Mahusiano mema baina ya Jiji la Potsdam na Kikwajuni Mjini Zanzibar.
 Baadhi ya wananchi wa Shehiya ya Kikwajuni Juu wakisalimiana na Mstahiki Meya wa Jiji la Potsdam Ujerumani Mhe. Jann Jakobs mara baada ya kutembelea maeneo ya Kikwajuni kwa Mjerumani. 
 Sheha wa Shehiya ya Kikwajuni juu Mzee Juma Saadat Haji na  Kati Anton Mkurugenzi wa Nyumba za kulelea Watoto wa Drewtz wakisaini hati ya Makubaliano ya Mradi wa Mahusiano mema Baina ya Mji wa Drewits na Kikwajuni Mjini Zanzibar kulia yao ni  Mstahiki Meya wa Jiji la Potsdam Ujerumani Mhe. Jann Jakobs 
Picha ya Pamoja ya Wananchi wa Kikwajuni na Ujumbe kutoka Jiji la Potsdam mara baada ya kusaini hati ya Makubaliano ya Mradi wa Mahusiano mema Baina ya Mji wa Drewits na Kikwajuni Mjini Zanzibar Picha na Makame Mshenga.
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images