Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

IGP SIRRO APOKEA MSAADA WA MAGARI MANNE LEO JIJINI DAR

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro na Meneja Mkuu wa kampuni ya utengenezaji magari ya Haval, Jianguo Liu wakikata utepe kuashiria kukabidhiwa magari manne yaliyotolewa na kampuni hiyo ikiwa ni juhudi zake katika kulisaidia Jeshi la Polisi kupambana na uhalifu nchini. Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi,Oysterbay,jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro akisikiliza maelekezo ya jinsi inavyotumika moja ya magari manne waliyokabidhiwa na Kampuni ya utengenezaji magari ya Haval. Anayemuelekeza ni Meneja wa Kampuni ya Kifaru, Mario Gaspari. Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi, Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro akizungumza wakati wa Hafla ya makabidhiano magari manne yaliyotolewa na Kampuni ya utengenezaji magari ya Haval, ambapo aliishukuru kampuni hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika vita ya kupambana na uhalifu. Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi,Oysterbay,jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Kampuni ya utengenezaji magari ya Haval, Jianguo Liu, akizungumza wakati wa Hafla ya makabidhiano magari manne yaliyotolewa na Kampuni hiyo ambapo aliahidi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika vita ya kupambana na uhalifu nchini.Kushoto aliyesimama ni mkalimani wa lugha ya kichina.Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi, Oysterbay, jijini Dar es Salaam.


DIAMOND PLUTNUMZ, WIZKID, DAVIDO, MR EAZI, JOHN BOYEGA, ABRANTEE & MORE NOMINATED FOR 2017 AFRICAN PRIDE AWARDS

$
0
0
Following its seminal debut ceremony last July, which saw the likes of Wizkid, Fuse ODG, CEO Dancers and Anthony Joshua take home the biggest prizes of the night, having been voted for by over half a million people online, African Pride Awards is back for its second annual award gala and ceremony, proudly brought to you by Africa Unplugged and Therapy Ent.

Leading the award nominations this year are none other than Wizkid once again, Davido, Mr Eazi, Tekno, Yemi Alade, Shatta Wale, Tiwa Savage and Diamond Platnumz, who are all nominated for the ‘Artist Of The Year (Africa)’ award, with the likes of Maleek Berry, Sona, Moelogo, Eugy, Juls and Ms. Banks representing for the UK, in the ‘Artist Of The Year (UK)’ category.

African movie stars Funke Akindele, AY, John Dumelo, Nana Ama McBrown, Nomzamo Mbatha and Abraham Attah, will be vying for the ‘Outstanding Achievement In Film (Africa)’ award, while the likes of John Boyega, Idris Elba, Maria Gomez, Chucky Venn, and Daniel Kaluuya, are up against each other in the ‘Outstanding Achievement In Film (UK)’ award category.

Also nominated are Nqobile, Ezinne Asinugo, Sherri Silver and GOP Dancers in the ‘Dance/Choreography Of The Year’ category, as well as Bella Naija, Iroko TV, Linda Ikeji, Afrobeat360 and Factory 78, in the ‘African Online Entertainment Platform Of The Year’ category, and Abrantee, Twin B, Julie Adenuga, Maya Jama and Manny Norte, in the ‘Radio Personality Of The Year’ category.

African music legend Awilo Longomba will be honoured with the ‘Lifetime Achievement Award’, while ‘Special Recognition Award’ nods will be presented to Ade Adepitan, SBTV, Link Up TV, GRM Daily, John Boyega, Larry Ekundayo, Eddie Kadi and The Compozers, who are also confirmed to be performing at the award ceremony.

Other award categories being announced via the African Pride Awards website include ‘Outstanding Media & PR Agency Of The Year’, ‘Makeup Artist Of The Year’, ‘African Club/Club Night of The Year’, ‘Event Organiser/Promoter Of The Year’, ‘TV Personality Of The Year’, ‘Radio Personality Of The Year’, ‘African TV Station Of The Year’, ‘Comedian Of The Year’ and ‘Outstanding Disk Jockey Of The Year’, just to mention a few.

Speaking about what to expect from the African Pride Awards this year, Abiodun Osibodu, CEO of Africa Unplugged and Therapy Ent says, “We are so proud yet humbled to have honored so many Africans doing incredible things in the diaspora and in Africa at the first ever APA in 2016. This year we will be honouring more people who have excelled within the community and celebrating our culture and heritage in a bigger way”.

Voting is now open to the public, with the first round of voting to end on July 30, and final public voting set to close on August 10. Winners will be announced at the main award gala and ceremony on August 13, 2017.

Vitale Water, ROK TV and Royal London Hotel & Suites are proud to support the 2017 African Pride Awards.

Advanced tickets for the 2017 African Pride Awards are available right now via:

WAZIRI MKUU AAGIZA KUSIMAMIWA KWA UTEKELEZAJI WA SHERIA ZA NCHI ZENYE LENGO LA KUMLINDA MTOTO WA KIKE

British Council  yawaalika watanzania wote wanaopenda kujifunza kiingereza

$
0
0
Na Karama Kenyunko Globu ya jamii.

TAASISI ya Elimu, British Council  inawaalika watanzania wote wanaopenda kujifunza kiingereza kujitokeza kwa wingi kwenye banda lao la sabasaba kwa ajili ya kufanya mtihani na kupunguza garama.

Taasisi hiyo inatumia maonesho ya 41 ya kimataifa ya Biashara  ya  Dar e Salaam (DITF) kutoa mitihani ya kiwango cha lugha ya Kiingereza bure kwa wananchi  wanaohitaji,lengo likiwa ni kujipima ufahamu wao. Meneja wa Maendeleo na Biashara kutoka British Council, Amata Bosco amesema hayo leo katika maonyesho yanayofanyika katika barabara ya Kilwa.
 Mkurugenz wa British Council Nchini, Angela Hennely akizungumza na waandish was habari katika mkutano huo.

Amesema kwa Tanzania kuna uhitaji  mkubwa wa kukuza lugha ambapo watu wengi wamejitokeza katika banda hilo kwa ajili ya kufanya mitihani hiyo yenye kujipima kiwango chao cha Kingereza. 
Amesema  mtihani wa kiwango unaofanyika katika maonesho hayo ni bure unapunguza garama kubwa wa watu wanaopenda kujifunza kiingereza kwa kuwa ukifanyia mtihani huo shuleni kwao unalazimika kulipia sh.48,000.

"kufanyika kwa mitihani hii ya kiwango katika maonesho kutasaidia watanzania walio wengi kuokoa kiwango cha fedha ambacho hukitumia wakati wa kawaida kwa kwenda kusoma katika taasis hiyo", amesema.
"Lengo kubwa la kufanya mtihani huu bure ni  kuhamasiha watu kujiandikisha kwa wingi katika kozi mbalimbali zitolewazo na taasisi hiyo ili kuboresha lugha ya Kiingereza.  Aidha amesema Taaasisi hiyo inawaunganisha watu na Uingereza katika ubunifu na vitu mbalimbali napia kujifunza masuala mbalimbali kutoka nchi hiyo. 

Amata amewaasa, watanzania  wanaopenda kujifunza ama kufundisha  Kiingereza kujitokeza kwa wingi, kufanya mitihani,  katik taasisi hiyo kwani ni  eneo muhimu la kuanzia na kwamba ndio maana wanatumia maonesho hayo maarufu kama sabasaba kwa ajili kuweza kuwafikia walio wengi Zaidi. 

" Mtihani huu wa kiwango wa  Kiingereza unafanyika kila siku ya maonesho na watu wengi wamekuwa wakifika hapa wakiwepo wenye kiwango cha chini, cha katikati na hata kiwango cha juu lakini pia wapo wasiojiamini katika kuzungumza lugha hiyo ambao na wamekuwa wakifika. 

WAZIRI MKUU AMUAGIZA MWAKYEMBE AICHUNGUZE BMT

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe alifanyie mapitio Baraza la Michezo Tanzania (BMT) na iwapo hatoridhika na utendaji wake alivunje.

“Ninamuagiza Waziri mwenye dhamana kufanya mapitio na kutathmnini upya utendaji kazi wa Baraza la Michezo Tanzania juu ya usimamizi wake wa michezo nchini na kama hataridhika, anayo mamlaka ya kulivunja Baraza hilo.” 

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Julai 5, 2017) katika hotuba yake ya kuahirisha Mkutano wa Saba wa Bunge mjini Dodoma.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano haitafumbia macho usimamizi mbovu na utawala wa michezo usiojali maslahi ya Taifa. “Serikali imeazimia kuimarisha utendaji kwa vyombo vya michezo nchini ili kila mwenye dhamana awajibike ipasavyo.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameipongeza timu ya vijana walio chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys iliyoshiriki na kutoa upinzani mkubwa kwenye mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika.

Amesema licha ya timu hiyo kumaliza ikiwa na jumla ya pointi 4 sawa na timu iliyoshika nafasi ya pili, ila Vijana hao wameonesha vipaji na uzalendo wa hali ya juu kwa nchi yao.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WATUHUMIWA 4,809 WA DAWA ZA KULEVYA WATIWA MBARONI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema katika kipindi cha miezi minne, Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) imewakamata watuhumiwa 4,809 na kufungua majalada ya kesi 3,222.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Julai 5, 2017), bungeni mjini Dodoma wakati akitoa hoja ya kuahirisha mkutano wa saba wa Bunge la 11. Bunge limeahirishwa hadi Septemba 5, mwaka huu.

“Katika kipindi kifupi tangu Februari, 2017 Mamlaka hii ilipozinduliwa, imefanikiwa kukamata watuhumiwa 4,809 wakiwa na dawa za kulevya aina ya heroine (gramu 327.173); cocaine (kilo 26.977); bangi (kilo 18,334.83); mirungi (kilo 11,306.67) na lita 6,338 za kemikali bashirifu zilikamatwa bandarini,” amesema.

Amesema mamlaka hiyo kwa kushirikiana na Kamati za Ulinzi za Mikoa imefanya operesheni za kuteketeza ekari 569.25 za mashamba ya bangi na ekari 64.5 za mashamba ya mirungi na kazi hiyo inaendelea. Kutokana na hatua hizo, jumla ya majalada ya kesi 3,222 yamefunguliwa.

“Dawa za kulevya zina athari kubwa kwa ustawi wa familia zetu na Taifa kwa ujumla. Hivyo, napenda kurejea wito wangu kwa Watanzania wote kuunga mkono jitihada za Serikali katika mapambano haya kwa kuendelea kutoa taarifa kuhusu watu wote wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Amesema azma ya Serikali ya awamu ya tano ni kutokomeza kabisa mtandao wa dawa za kulevya nchini kwa kuhakikisha kuwa mapambano dhidi ya dawa za kulevya yanakuwa endelevu, yanafanyika kisayansi na yanaleta mafanikio. “Tuungeni mkono kwenye mapambano haya, ili tutokomeze kabisa mtandao huo,” amesisitiza.

WATUHUMIWA 4,809 WA DAWA ZA KULEVYA WAKAMATWA

$
0
0

*Heroine, Cocaine, bangi, mirungi na kemikali bashirifu vyakamatwa
* Mashamba ya bangi ekari 569.25 na mirungi ekari 64.5 yateketezwa


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema katika kipindi cha miezi minne, Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) imewakamata watuhumiwa 4,809 na kufungua majalada ya kesi 3,222.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Julai 5, 2017), bungeni mjini Dodoma wakati akitoa hoja ya kuahirisha mkutano wa saba wa Bunge la 11. Bunge limeahirishwa hadi Septemba 5, mwaka huu.

“Katika kipindi kifupi tangu Februari, 2017 Mamlaka hii ilipozinduliwa, imefanikiwa kukamata watuhumiwa 4,809 wakiwa na dawa za kulevya aina ya heroine (gramu 327.173); cocaine (kilo 26.977); bangi (kilo 18,334.83); mirungi (kilo 11,306.67) na lita 6,338 za kemikali bashirifu zilikamatwa bandarini,” amesema.

Amesema mamlaka hiyo kwa kushirikiana na Kamati za Ulinzi za Mikoa imefanya operesheni za kuteketeza ekari 569.25 za mashamba ya bangi na ekari 64.5 za mashamba ya mirungi na kazi hiyo inaendelea. Kutokana na hatua hizo, jumla ya majalada ya kesi 3,222 yamefunguliwa.

“Dawa za kulevya zina athari kubwa kwa ustawi wa familia zetu na Taifa kwa ujumla. Hivyo, napenda kurejea wito wangu kwa Watanzania wote kuunga mkono jitihada za Serikali katika mapambano haya kwa kuendelea kutoa taarifa kuhusu watu wote wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Amesema azma ya Serikali ya awamu ya tano ni kutokomeza kabisa mtandao wa dawa za kulevya nchini kwa kuhakikisha kuwa mapambano dhidi ya dawa za kulevya yanakuwa endelevu, yanafanyika kisayansi na yanaleta mafanikio. “Tuungeni mkono kwenye mapambano haya, ili tutokomeze kabisa mtandao huo,” amesisitiza.


IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
40480 - DODOMA.
JUMATANO, JULAI 5, 2017.

SERIKALI YAKEMEA UBOMOAJI WA MAJENGO YA KALE NCHINI

$
0
0
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo amesema apendezi kabisa kuona shughuli za Ujenzi wa Majengo mapya zinaadhiri majengo ya kale bila sababu za msingi au kuridhiwa na Serikali.

 

Akizungumza kwa niaba ya waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Dr Harson Mwakyembe, katika ufunguzi wa jengo la OLD BOMA lililopo jijini Dar es Salaam Naibu katibu Mkuu wa wizara hiyo Mh Nuru Milano amesema Sera ya Mambo ya kale ya mwaka 2007 inaimiza utunzaji wa majengo ya kale yenye zaidi ya miaka miamoja ili vizazi vilivyopo na vijavyo viweze kujifunza historia hii muhimu ya nchi yetu. 
Akitoa salama za Umoja wa nchi za Ulaya  Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya hapa nchini Mh Roeland Van De Geer wanesema Umoja huo unajisikia furaha kushiriki katika uhifadhi wa uridhi wa histori ya Tanzania hasa kwa kupitia majengo ya kale na kuahidi kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali katika uhifadhi huo. 
Nae Rais wa Wasanifu majengo nchini Mwandisi Henry. L.M. Mwoleka amewashau wananchi na taarisis mbali mbali kuacha kabisa kubomoa majengo ya kihistoria nchini ili kuendelea kuhifadhi majengo haya kama alama ya historia ya nchi yetu. 
Akitoa salama za shukrani Mea wa Jiji la Dar es Saalam Mh Isaya Mwita ameushukuru Umoja wa Nchi za Ulaya na wadau mbali mbali kwa kufadhili ukarabati wa jengo hilo la Kale na kuendelea kutoa wito kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kushiriki kikamilifu katika utunzaji wa Utamaduni huu wa Kihistoria kwani kwakufanya hivyo jiji la Dar es Salaam litaingiza mapato mengi kupitia Utalii.
 Naibu katibu Mkuu wa wizara hiyo Mh Nuru Milano (kulia) na Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya hapa nchini Mh Roeland Van De Geer wakifungua rasmi jengo la Kihistoria la Old Boma lililopo jiji Dar es Salaam.

 Mkurugenzi Mkuu wa kituo cha Uridti wa Ubunifu Majengo Bi Aida Mulokozi  akitoa malezo ya onesho maalum lililopondani ya jengo la OLD BOMA, pembeni yake ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mh Isaya Mwita na wageni wengine wakimsikiliza kwa makini. 

 Wageni mbali mbali walioudhuria sherehe hizo za ufunguzi wakiangalia onesho maalum lililopondani ya jengo la OLD BOMA
Muonekano wa Jengo la kale la OLD BOMA lililopo eneo la Posta jijini  Dar es Salaam. 


AMREF YAFANYA MKUTANO NA WADAU KATIKA MAHADHIMISHO YA MIAKA 60

$
0
0
 Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabiti Kombo akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa wadau wa Amref  Uliofanyika jijini Dar es Salaam leo
 Mkurugenzi wa Amref Nchini, Bi. Florence Temu  akizungumza wakati wa mkutano huo wa wadau uliofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam


 Mtendaji Mkuu wa kurugenzi wa Amref Africa  Bw. Githinji Gitahi akizungumza kwa ufupi Historia ya Amref Hapa nchini na Mafanikio yake katika sekta ya Afya
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulisubisya akizungumzia namna gani Amref imesaidiakatika sekta ya Afya nchini
 sehemu ya wadau walioshiriki mkutano wa wadau wa Amref  katika Hotel Serena Jijini Dar es Salaam
  sehemu ya wadau walioshiriki mkutano wa wadau wa Amref  katika Hotel Serena Jijini Dar es Salaam
Picha ya Pamoja ya wadau wa Amref na Mgeni Rasmi Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mamhoud Thabiti Kombo

SERIKALI YAPUNGUZA TOZO YA ARDHI KWA ASILIMIA 5

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuanzia mwaka huu wa fedha, Serikali imepunguza gharama za malipo ya awali ya thamani ya ardhi iliyopimwa kutoka asilimia 7.5 hadi asilimia 2.5.

“Serikali inaendelea kupunguza gharama za umilikaji wa ardhi nchini na katika mwaka wa fedha 2017/2018, imepunguza tozo ya awali ya ardhi iliyopimwa (premium) kutoka asilimia 7.5 ya thamani ya ardhi hadi asilimia 2.5 tu. Natoa wito kwa wananchi kuchangamkia punguzo hili na kujitokeza kupimiwa na kumilikishwa ardhi,” amesisitiza.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Julai 5, 2017), bungeni mjini Dodoma wakati akitoa hoja ya kuahirisha mkutano wa saba wa Bunge la 11. Bunge limeahirishwa hadi Septemba 5, mwaka huu.

Amesema Serikali itahakikisha kuwa kila kipande cha ardhi ya Tanzania kinapimwa ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015. “Serikali imeweka mkakati na mpango kazi wa kuwezesha kufikia lengo la kupanga matumizi bora ya ardhi katika vijiji 1,500 na wilaya tano kila mwaka.”

Amesema Serikali itaendelea kuimarisha Ofisi za Ardhi za Kanda kwa kupeleka wataalam wa kada mbalimbali na kuwawezesha kwa kuwapatia vitendea kazi stahiki. “Kazi ya upimaji wa ardhi haiwezi kufanikiwa bila ya rasilmali watu.Lengo letu ni kuwawezesha wananchi kupata huduma mbalimbali za ardhi katika kanda badala ya kufuata huduma hizo makao makuu ya wizara,” amesema.

Amewasihi watumishi watakaohamishiwa katika ofisi za kanda pamoja na wale waliopo katika Halmashauri, wafanye kazi kwa ushirikiano na watekeleze majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia sekta ya ardhi na kutoa huduma kwa wananchi bila ubaguzi wa aina yoyote.


IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
40480 - DODOMA.
JUMATANO, JULAI 5, 2017.

HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB), WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI WA KUAHIRISHA MKUTANO WA SABA WA BUNGE LA KUMI NA MOJA LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TAREHE 05 JULAI, 2017

$
0
0
UTANGULIZI:                        


1.           Mheshimiwa Spika, leo tumefika mwisho wa Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 ulioanza Jumanne ya tarehe 4 Aprili, 2017. Tunayo kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kuifikia siku hii, tena baada ya kuwa tumetimiza wajibu wetu wa Kikatiba kikamilifu na kwa umahiri mkubwa. Huu ulikuwa ni Mkutano muhimu sana kwa nchi yetu kutokana na jukumu kubwa la kujadili na kupitisha bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 ulioanza tangu tarehe 1 Julai, 2017. Bajeti hii ambayo ni nzuri na ya kihistoria ni ya pili tu kati ya takribani Bajeti tano za Serikali ya Awamu ya Tano zitakazoandaliwa hadi kifikia Mwaka wa Fedha 2020/2021.


2.           Mheshimiwa Spika, wakati Bunge lako likiendelea, tarehe 13 Aprili, 2017 tulipokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za vifo vya askari polisi wetu 8 waliopoteza maisha wakiwa wanalitumikia Taifa kwa kuuawa na kundi la wahalifu katika eneo la Jaribu Mpakani, Wilayani Kibiti mkoani Pwani. Askari hao waliopoteza maisha ni Inspekta Msaidizi Peter Kiguu, Koplo Francis, PC Haruna, PC Jackson, PC Zakaria, PC Siwale, PC Maswi na PC Ayoub. Pia, hivi karibuni mwezi Juni, 2017 Askari wetu wawili wa Kikosi cha Usalama Barabarani walivamiwa na kupigwa risasi na majambazi katika Kijiji cha Bungu “B” kilichopo Wilayani Kibiti. Aidha, wananchi wetu wengi wamepoteza maisha kutokana na uhalifu unaofanywa na majambazi waliopo katika maeneo ya Kibiti, Rufiji na Mkuranga.

MAHAKAMA YAMFUATA MANJI HOSPITALI, ASOMOMEWA MASHTAKA YA UHUJUMU UCHUMI

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imelazimika kuhamishia shughuli zake katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa muda kumsomea mfanyabiashara Yusufali Manji (41), mashitaka ya uhujumu uchumi yanayomkabili.

Manji amesomewa mashtaka hayo katika Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo Hospitalini hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mhe. Huduma Shaidi.

Katika kesi hiyo, Manji anashitakiwa pamoja na wenzake watatu, Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Quality Group Ltd, Deogratius Kisinda (28), Mtunza stoo, Abdallah Sangey (46) na Thobias Fwere (43)  mkazi wa Chanika, ambapo wote watatu wamesomewa mashtaka yao katika Mahakama hiyo kabla haijahamia hospitali ya Muhimbili kuanzia muda wa saa Tisa alasiri na kumalizika saa 16:41 (saa kumi na dakika arobaini na moja).

Mahakama ilifikia uamuzi wa kuhamia Muhimbili baada ya Manji kuwa amelazwa Hospitalini hapo akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo na kulazimika kusomewa mashtaka yake akiwa kitandani.

Akisoma mashtaka hayo, wakili Mwandamizi wa Serikali, Tulumanywa Majigo amedai kwamba Juni 30, mwaka huu huko Chang’ombe A wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, washitakiwa wote kwa pamoja, walikutwa na askari polisi wakiwa na mabalo 35 ya vitambaa vinavyotumika kutengenezea  sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) vyenye thamani ya milioni 192.5.
Imedaiwa kuwa, Julai Mosi mwaka huu, maeneo hayo hayo, washitakiwa  wote walikutwa na askari polisi wakiwa na mabalo nane ya vitambaa vinavyotumika kutengenezea sare za JWTZ vyenye thamani ya milioni 44.

Aidha imedaiwa kuwa, Juni 30, washitakiwa hao walikutwa wakiwa na mhuri wa JWTZ ambao uliandikwa ‘’Mkuu wa Kikosi 121  Kikosi cha JWTZ’’ bila kuwa na uhalali,  kitendo kinachohatarisha usalama wa nchi.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

RAIS DKT. MAGUFULI ALIPOZUNGUMZA NA WANANCHI WA MKOA WA GEITA WAKATI AKIELEKEA CHATO JANA JIONI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpungia mkono Mama mmoja mlemavu mkazi wa Buseresere mara baada ya kumaliza kuhutubia mamia ya wakazi wa Katoro na Buseresere waliojitokeza pembezoni mwa barabara katika eneo hilo kumsalimia wakati akielekea Chato Mkoani Geita jana jioni
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Bwanga njia panda ya kuelekea Makao makuu ya Wilaya ya Chato jana jioni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Katoro na Buseresere mara baada ya kusimama wakati akielekea Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Geita mjini wakati akielekea Chato.
Wananchi wa Geita waliokuwa na Shauku ya kumuona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakiwa wamepanda juu ya magari pembezoni mwa barabara ya Usagara-Sengerema-Geita jana jioni

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mama Rosemary Lucas ambaye alikuwa akiwasilisha kero yake ya kuvunjiwa nyumba Sengerema mkoani Mwanza.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela akichukua maelezo ya mama huyo Rosemary Lucas aliyevunjiwa nyumba yake Sengerema mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kada wa zamani wa CHADEMA Hamis Tabasamu ambaye alikuwa akionesha Kadi yake mpya ya CCM mara baada ya kuhamia. Kadi hiyo alikabidhiwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza katika Wilaya ya Sengerema.PICHA NA IKULU

MICHUZI TV: RAIS DKT. MAGUFULIA AWAASA WANAFUNZI, AWATAKA WASOME NA KUACHANA NA MAMBO YASIYOFAA

HOSPITALI YA SHALBY YA NCHINI INDIA YAADHIMISHA MIAKA 15 YA KUBORESHA AFYA ZA WANANCHI NCHINI.

$
0
0
Hospitali ya nchini India ya Shalby imesherekea miaka 15 ya huduma mbalimbali wanazozitoa za kiafya Afrika huku ikiahidi kuendeleza mashirikiano ili kuboresha afya za Watanzania. 
Hayo yamesemwa na daktari bingwa wa mifupa na upasuaji wa magoti kutoka India ambaye pia ni Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wa hospitali ya Shalby  Dk Vikram Shah wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 
 Dk Shah amesema timu ya madaktari bingwa kutoka katika hospitali imekuwa ikija Afrika na kufanya kambi za upasuaji mbalimbali ikiwapo upasuaji wa magoti na nyonga. Amesifu ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na India na kusisitiza kuendelea kusaidiana katika shughuli zao ili kuboresha afya na maisha ya wananchi wa pande zote mbili. 
 “Tanzania na India zimekuwa na uhusiano wa muda mrefu na kambi za kimatibabu mbalimbali zinazofanywa na madktari wa Shalby nchini na Afrika kwa ujumla ni kithibitisho cha utu na upendo baina ya India na Tanzania na Afrika kwa ujumla,” alisema Dk Shah. 
 Dk Shah ambaye anaaminika kuwa daktari aliefanya upasuaji wa kubadilisha magoti mara nyingi zaidi, ambapo mpaka sasa ashafanya upasuaji zaidi ya 85,000, alisema teknolojia ina mchango mkubwa katika kuboresha huduma za afya na kuahidi kuboresha zaidi mashirikiano na Tanzania.
Dk Vikram Shah akitoa hotuba kwa wageni waliohudhuria halfa hiyo
Daktari bingwa wa mifupa na upasuaji wa magoti ambaye pia ni Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Shalby kutoka nchini India, Dk Vikram Shah akifurahia jambo na  Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Phili Mangula (katikati) pamoja na Dk Edmund Mndolwa (kushoto) katika halfa ya kusherekea miaka 15 ya huduma za hospitali hiyo barani Africa iliyofanyika jijini Dar es Salaam, hivi karibuni


Baadhi ya wshiriki waliohudhuria hafla hiyo.
Picha na Emmauel Massaka,Globu ya Jamii.


MSTAHIKI MEYA WA JIJI ISAYA MWITA NA MEYA WA KINONDONI BENJAMINI SITTA WATEMBELA BANDA LA NHC

$
0
0
 Meya wa Jiji la Dares Salaam ,Isaya Mwita akiwasili katika banda la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Katika maonyesho ya 41 ya Sabsaba
 Meneja Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Joseph Haule akitoa maelezo kwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Manispaa ya Kinondoni ,Benjamini Sitta.

Meya wa  Manispaa ya Kinondoni ,Benjamini Sitta. akisaini kitabu cha Wageni kwenye banda la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

IGP SIRRO APOKEA MSAADA WA MAGARI MANNE LEO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro na Meneja Mkuu wa kampuni ya utengenezaji magari ya Haval, Bw. Jianguo Liu wakikata utepe kuashiria kukabidhiwa magari manne yaliyotolewa na kampuni hiyo ikiwa ni juhudi zake katika kulisaidia Jeshi la Polisi kupambana na uhalifu nchini. Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi,Oysterbay,jijini Dar es Salaam
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro   akisikiliza maelekezo ya jinsi linavyotumika moja ya magari manne waliyokabidhiwa na Kampuni ya utengenezaji magari ya Haval. Anayemuelekeza ni Meneja wa Kampuni ya Kifaru Bw. Mario Gaspari. Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi, Oysterbay, jijini Dar es Salaam
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro   akizungumza wakati wa Hafla ya makabidhiano magari manne yaliyotolewa na Kampuni ya utengenezaji magari ya Haval, ambapo aliishukuru kampuni hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika vita ya kupambana na uhalifu. Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi,Oysterbay,jijini Dar es Salaam
 Meneja wa Kampuni ya utengenezaji magari ya Haval, Jianguo Liu, akizungumza wakati wa Hafla ya makabidhiano magari manne yaliyotolewa na Kampuni hiyo ambapo aliahidi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika vita ya kupambana na uhalifu nchini.Kushoto aliyesimama ni mkalimani wa lugha ya kichina.Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi, Oysterbay, jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro (wanne kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Kampuni ya utengenezaji magari ya Haval, Jianguo Liu(watatu kushoto), baada ya makabidhiano ya magari manne kutoka kwa kampuni hiyo ikiwa ni mchango wao katika kulisaidia Jeshi la Polisi kupambana na uhalifu nchini.Wengine ni viongozi wa juu wa jeshi na viongozi wa kampuni ya Haval.Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi,Oysterbay, jijini Dar es Salaam. 
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

MRISHO MPOTO ATANGAZWA KUWA BALOZI WA PROPERTY INTERNATIONAL

$
0
0
 Mrisho Mpoto akiwa ameshika tuzo ya Property International mara baada ya kutangazwa kuwa balozi wa kampuni ya Property International katika maonyesho ya kimataifa ya Biashara
 Mtendaji Mkuu wa Property International Abdulkarim Haleem  akitoa maelezo kwa Mrisho Mpoto mara baada ya kumtangaza kuwa balozi wa kampuni hiyo
Mrisho Mpoto akipata maelezo kutoka kwa wakurugenzi wa kampuni ya Property

WAZIRI MKUU AAGIZA KUFANYIWA TATHIMINI KWA BARAZA LA MICHEZO TANZANIA

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, PROF. JUMANNE MAGHEMBE ATEUA WAJUMBE WA BODI YA MAMLAKA YA HIFADHI YA ENEO LA NGORONGORO

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images