Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1780 | 1781 | (Page 1782) | 1783 | 1784 | .... | 3278 | newer

  0 0


  0 0

  Na,Jumbe Ismailly SINGIDA July,03,2017 Nyalandu 


  MBUNGE wa Jimbo la Singida Kaskazini,Lazaro Nyalandu ametangaza donge nono kwa timu itakayokuwa bingwa wa mashindano ya kombe la Mbunge huyo,maarufu kwa jina la “NYALANDU CUP” linalotarajia kuanza mwezi wa nane mwaka huu.

  Kombe hilo litakaloanza mwezi ujao,litashirikisha timu za mpira wa miguu kwa wanaume na mpira wa miguu kwa wanawake na kilele cha mashindano ya kombe hilo kitafanyika katika Kijiji cha Ngamu,kilichopo katika Kata ya Mwasauya.

  Akitangaza msimamo wake huo mbele ya Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2017,Amour Hamad Amour,Nyalandu alisema kwamba tangu alipochaguliwa kuwa mwakilisha wa wananchi wa jimbo hilo la Singida Kaskazini hajawahi kuandaa ligi ya aina yake kama hiyo inayotarajiwa kuanza kuchezwa katika jimbo zima.

  “Nilimwambia Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru nafikiri nilikuwa namnong’oneza kwamba mwenge ukipita na hii itakuwa ni mara ya kwanza tangu nimekuwa Mbunge halafu kuchezesha mambo hii ya mechi”alifafanua ‘Mimi nafanyaaga maskolashipu,wasome sekondari,wafanye nini,mambo ya maji nafikiri sasa hivi tutaenda kwa zote, kwa hiyo ningependa kuanzisha ligi ambayo itafanyika ya mpira wa miguu lakini nataka iende sambamba na ligi ya wanawake” alisisitiza Mbunge Nyalandu.

  Kwa mujibu wa Mbunge huyo kutakuwa na ligi ya wanaume na itafungwa pamoja na ligi ambayo itakuwa ni ya wanawake na ligi hiyo watashirikiana kuitangaza,kuiunda na kuiandaa na serikali ya wilaya hiyo pamoja na Halmashauri hiyo kwa ujumla.
  Mchezaji wa timu ya Mtinko Fc,Yusufu Samsoni (mwenye jesi yenye rangi ya bluu) alipomtoka mchezaji wa timu ya Msange Fc,Yasini Athumani na kwenda kuifungia timu yake bao la pili na la ushindi.
  Baadhi ya wachezaji wa timu ya Msange FC wakifanya mazoezi katika uwanja wa michezo wa shule ya msingi Mtinko kabla ya kuanza kwa mchezo huo ambao matokeo yalikuwa Mtinko FC 2 na Msange FC 1.(Picha zote Na Jumbe Ismailly).


  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  SINGIDA United inaingia kambini kesho kwa ajili kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu Vodacom  huku ikizitahadharisha timu za Simba na Yanga kuwa hawana undugu nao na kama kuna wanaodhani hivyo wanaota ndoto za mchana kwani wataujua ukweli baada ya kuanza msimu mpya wa ligi utaoanza mwezi Agosti.

  Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa klabu hiyo Festo Sanga mbele ya Waandishi wa Habari na kuondoa utata ulioanza kujitokeza kuhusu baadhi ya viongozi kuwa na mapenzi na timu hizo kongwe nchini.

  Kumekuwa na dhana kuwa Singida inaweza kuwa undugu na karibu na Yanga kwakua kiongozi wake mkuu Waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba, kocha mkuu wa timu hiyo Mholanzi Hans Pluijm na msaidizi wake Fred Minziro wote wakiwa ni wapenzi wakubwa wa mabingwa hao wa ligi kuu msimu uliopita.

  "Inawezekana kuna viongozi wana mapenzi na timu za Simba na Yanga ila Singida United haitambui hilo, na mkitaka kuamini kauli yangu subirini ligi ianze ndiyo mtaona kitakacho tokea," alisema Sanga.

  Singida itaingia kambini kesho jijini Mwanza kwa ajili ya kambi kujiandaa na msimu mpya wa ligi mwezi ujao ambapo imepanga kutafuta mechi za kirafiki kutoka nchi za Kenya, Uganda na Rwanda.

  Wakati huo huo Sanga alisema wamefanikiwa kununua basi la klabu hiyo aina ya Dragon lenye thamani ya shilingi milioni 350 watakalo litumia kusafiri sehemu mbalimbali kuanzia sasa.
  " Tumefanikiwa kununua basi kwa ajili ya safari zetu za timu ndani na nje ya nchi kuanzia sasa," alisema Sanga.

    Muonekano wa gari la Singida United linaloratajiwa kutumiwa na wachezaji wa timu hiyo katika msimu mpya wa ligi kuu.

  Meneja wa klabu ya Singida United Festo Sanga akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kulitambulisha basi lao jipya litakalotumika kwa safari za ndani za timu ya Singida United.


  0 0


  Na Mwashungi Tahir-Maelezo Zanzibar 03-07-2017

  Wananchi wa Tanzania wanaoishi Marekani wanadiaspora wakishirikiana na Madaktari bingwa wapo nchini kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu ya maradhi mbalimbali yanayowasumbua wananchi.

  Zoezi la kutoa huduma hizo za matibabu bure linafanyika kwa muda wa siku tatu katika Hospitali ya Mnazi mmoja.

  Akizungumza na waandishi wa habari huko katika kitengo cha maradhi ya ngozi kwenye hospitali kuu ya Mnazi mmoja, Mwanadiaspora Idi Seif Sandaly amesema wameamua kuja nchini hapa kutoa huduma hizo ili kuwasaidia wananchi wenye matatizo mbalimbali.

  “Tumekuja Zanzibar kwa lengo la kuwasaidia wananchi ambao wana maradhi mbali mbali na kuwapatia matibabu kwa kupitia jumuiya yetu ya marekani Health Education Development kwa kutibu maradhi ya ngozi , sukari na pressure pamoja na maradhi ya akinamama.” Amesema Mwanadiaspora huyo.
  Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la kutoa huduma za Elimu ya afya Nchini Marekani Bi. Asha Mustafa Nyang’anyi akizungumza na wandishi wa habari kuhusu ujio wao hapa Zanzibar.
  Bwana. Amiri Muhammed Amiri akimuonesha fangas Daktari bingwa wa ngozi Mamotheo alipokuwa akitoa matibabu katika hospitali ya Mnazi mmoja Mjini Zanzibar. 
  Baba wa mtoto Abdulmajid akiwaonesha madaktari bingwa wa maradhi ya ngozi namna mwanawe alivyodhurika kwa kufanya mabaka mwilini katika hospitali ya Mnazimmoja mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga.


  0 0

  NA CHRISTINA MWAGALA ,OFISI YA MEYA WA JIJI

  MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amesema watanzania hawajafikia hatua ya kubaguana kwa kiitikadi ya vyama, Dini, Kabila badala yake wote wanapaswa kutangaza hali ya Umoja, Upendo na Mshikamano katika nchi yao.

  Meya Mwita alitoa kauli hiyo jijini hapa jana, wakati wa harambee ya uchangiaji wa ujenzi wa Kanisa la kisasa la Tanzania Assemblies Of God (TAG) lililopo Kivule ,Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini hapa ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuwa watanzania wanapaswa kuwa wamoja ili nchi iendelee kuwa na amani.

  Alisema yapo mambo mbalimbali ambayo yanajitokeza ndani ya nchi ambapo kama watanzania , kwakushirikiana na viongozi wa dini kwa pamaoja wanapaswa kusimama na kuliombea Taifa ili kuendelea kudumisha amani iliyopo.

  " Tangu nimezaliwa sijawahi kushuhudia vita, machafuko katika nchi yetu, kikubwa huwa naona amani iliyotawala, Upendo, na umoja , sasa nawasishi sana ndugu zangu tuendelee kuwa wamoja tusibaguane, kwa namna yoyote ile , ili nchi yetu iendelee kuwa na amani" alisema Meya Mwita.

  "Baba wataifa Hayati Mwalim Julius Nyerere enzi ya uhali wake alikuwa akisisitiza sana kulinda amani ya nchi yetu, na sisi ambao tupo hai hadi sasa , mambo ya vyama, Udini, Ukabila tuweke pembeni tusimame kama Taifa moja.

  Awali akijibu risala iliyoandaliwa na uongozi wa kanisa hilo, Meya Mwita aliahidi kuchangia katika ujenzi huo mifuko 100 ya Simenti na kiasi cha Fedha shilingi 500,000 huku aliwataka waumini wa kanisa hilo kujitolea ili kufanikisha ujenzi huo.

  Risala hiyo ilieleza kujenga kanisa la kisasa lenye uwezo wa kuchukua waumini 600 ambapo jumla ya shilingi milioni 95 zinahitajika ili kukamilisha ujenzi huo.

  0 0


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


  MASHINDANO ya Sprite BBall Kings yameendelea tena juzi katika uwanja wa chuo kikuu cha Dar es salaam, ikiwa ni hatua ya robo fainali ya mashindano hayo.

  Mchezo wa kwanza uliwakutanisha timu za Mchenga na The fighter na timu ya Mchenga kuibuka na ushindi wa vikapu 109 dhidi ya 41 za The fighter .

  Mechi ya pili iliwakutanisha Flying dribblers ambaye alitoka na ushindi wa vikapu 91 dhidi ya Osterbay aliyepata vikapu 82, TMT wakaumana na Dream chaser na kufanikiwa kushinda kwa vikapu 96 dhidi ya vikapu 73.

  Mechi ya nne iliyowakutanisha Kurasini Heat na Kigamboni Heroes ilimalizika kwa vikapu 64 vya Kurasini Heat dhidi ya 59 vya Kigamboni Heroes. 

  Mratibu wa Mashindano hayo ya Sprite BBall Kings Basilisa Biseko amesema kuwa baada ya kumalizika kwa mechi za Robo fainali na kupatikana kwa timu nne zitakazoendelea kwenye hatua ya nusu fainali kutachezeshwa kwa droo maalumu kwa ajili ya kuzipanga timu zitakazochuana kwenye hatua ya nusu fainali ya mashindano haya ya Sprite BBall Kings kwa mwaka 2017.

  "Timu zilizopata alama nyingi katika michezo ya wiki hii ndizo zilizofanikiwa kuendelea katika hatua ya nusu fainali ya mashindano ya Sprite Bball kings 2017 "amesema Basilisa.

  Michuano hiyo inayodhaminiwa na Sprite kwa kushirikiana na East Africa Tv na Redio huku mshindi akitarajiwa kuondoka na kitita cha shiling milion 15.

  Timu ya The fighter (jezi nyeupe) ikisalimiana na timu ya Mchenga (jezi nyeusi) wakati wa mchezo wa hatua ya robo fainali ya shindano la Sprite Bball Kings uliomalizika kwa timu ya Mchenga kushinda kwa vikapu 109 dhidi ya vikapu 41
  Mchezaji wa timu ya The Fighter akiambaa na mpira wakati wa mchezo wa hatua ya robo fainali dhidi ya Mchenga  wa mashindano ya Sprite Bball Kings uliomalizika kwa timu ya Mchenga kuibuka na ushindi wa vikapu 109 dhidi ya 41.
  Mchezaji wa timu ya kikapu ya TMT  akipiga pigo la adhabu kwa upande wa timu yake wakati wa mchezo wa hatua ya robo fainali dhidi ya Dream Chaser  wa mashindano ya Sprite Bball Kings uliomalizika kwa timu ya TMT  kuibuka na ushindi wa vikapu 96 dhidi ya 73.
   Timu ya Dream Chaser  (jezi nyeupe) na TMT (Jezi buluu) wakikaguliwa na waamuzi wa mchezo huo kabla ya  kuanza kwa mchezo wa hatua ya robo fainali ya shindano la Sprite Bball Kings.

  0 0


  Msafara wa wachezaji, makocha na walezi wa timu ya vijana ya FC Vito ya Lindi, umetua salama jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya kukabidhiwa bendera ya Taifa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

  FC Vito inatarajia kuondoka nchini Julai 5, kwenda Helsinki, Finland kushiriki michuano ya vijana ya Helsinki Cup 2017, michuano ya nne kwa ukubwa barani Ulaya kwa vijana

  Kikosi hicho kitakabidhiwa Bendera ya Taifa hapo kesho katika Ukumbi wa Mikutano uliopo Ubalozi wa Finland makutano ya mitaa ya Mirambo na Garden Avenue jijini Dar es Salaam....

  Mgeni rasmi wa hafla hiyo, ambaye ndiye atakayekabaidhi bendera ya taifa ni Katibu Mkuu wa BMT, Mohammed Kiganja...
  0 0
  Mtafiti Mkuu Kiongozi Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu Tanzania (NIMR) Leonard Mboera akizungumza kwenye mkutano wao wa Watafiti,uliohusu Utafiti kuhusu taarifa za vifo vinavyotokea katika hospitali za Tanzania,uliofanyika katika taasisi hiyo mapema leo mchana,ambapo watafiti mbalimbali walihudhuria na kuwasilicha mada zao sambamba na kuzijadili kwa pamoja.

  Katika mkutano huo,Dkt Leonard alisema kuwa wamefanya utafiti wa kuangali eneo kubwa na vyanzo na sababu za vyanzo katika hospitali zetu hapa nchini,alisema kuwa katika utafiti huo vya wameufanya kwa kujumuisha hospitali ya Taifa Muhimbili,hospitali tatu za rufaa,hospitali maalum ambazo ni Kibong'oto,Mirembe,taasisi ya saratani ya ocean road,taasisi ya MOI na pia wakajumlisha hospitali zote za mikoa na asilimia kumi ya hospitali za Wilaya.

  Dkt Leonard alisema kuwa dhumuni la kufanya utafiti huo ni kuangalia upatikanaji wa takwimu za vifo katika hospitali hizo na pili kuangalia ni magonnjwa gani ambayo yanasababisha vifo hospitalini "na zoezi hilo lilianza Julai 20016 na ukusanyaji wa takwimu ulikamilika mwezi Novemba,2016 ,baada ya hapo tukawa tunafanya uchanganuzi",alisema Dkt Leonard.

  Alisema kuwa walichobaini katika uchanganuzi huo katika makundi ya magonjwa kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO),Magonjwa ya kuambukiza,maradhi yanawakuta Wakina mama wakati wa uja uzito na maradhi yanayohusiana na Lishe ndio yanayoongoza (kundi kubwa) kwa kuwa na asilimia 57,kundi kubwa, na Magonjwa yasiambukizwa ni asilimia 30 (kundi la kati) na kuna kundi dogo la Maradhi linalosabishwa na ajali ambalo linachukua asilimia 15.

  kutokana hali hiyo Magonjwa yasio ambukiza yameanza kuchukua nafasi,lakini kwa upande mwingine ugonjwa wa Malaria ndio una oongoza kuleta vifo katika hospitali zetu.

  Baadhi ya Watafiti waliokutana leo katika mkutano wao,ambao ulibeba dhima ya 'Utafiti kuhusu taarifa za vifo vinavyotokea katika hospitali za Tanzania'.

  0 0


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Viongozi wa Dini mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiombewa sala na Viongozi mbalimbali wa dini kutoka Kanda ya ziwa mara baada ya kuwasili mkoani Mwanza. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa katikati ya jiji la Mwanza waliokusanyika kumpokea.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinunua Karanga kutoka kwa Mmachinga anayefanya biashara katikati ya jiji la Mwanza.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Wachezaji wa Buhongwa Fc mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Nyamagana. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono washabiki wa mpira wa miguu wakati akitoka katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza. PICHA NA IKULU  0 0


  0 0

  Kampuni ya simu za mkononi Airtel kwa kushirikiana na Dar Teknohama Business Incubator (DTBi) leo imezindua maabara ya Kompyuta ijulikanayo kama  ‘Airtel Fursa Lab’ katika shule ya msingi Kijitonyama iliyopo  Wilaya ya Kinondoni jijini kwa lengo la kuwawezesha vijana kupata ujuzi wa masomo.   
  Akizungumza katika uzinduzi huo, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Profesa Faustine Kamuzora amesema kuwa kuweka nguvu ya pamoja kama hiyo kutawezesha kuchochea mapinduzi ya vijana wa kitanzania katika sekta ya habari na mawasiliano.  
  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel, Betrice Singano amesema kuwa Airtel imejipanga kujenga vijana wenye ujuzi na weledi wakiwa bado watoto wadogo kutumia teknolojia ya mawasiliano ya simu pamoja na Tehama katika kukuza ujuzi.    
  Naye Mkurugenzi Mkuu wa Atamia ya Teknohama ya Dar es salaam ( DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Eng. George MulaMula amesema kuwa Tanzania inachangamoto kubwa katika kutoa mafunzo kwa vitendo, hivyo maabara hiyo itachochea kasi ya ubunifu katika Teknolojia itakayoleta tija katika taifa
   Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Profesa Faustine Kamuzora akizungumza katika uzinduzi maabara ya Kompyuta ijulikanayo kama  ‘Airtel Fursa Lab’ katika shule ya msingi Kijitonyama iliyopo  Wilaya ya Kinondoni leo jijini Dar es Salaam.kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Atamia ya Teknohama ya Dar es salaam ( DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Eng. George MulaMula na kulia NI Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel, Betrice Singano
   Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Betrice Singano akizungumza  juu ya huduama ya maabara ya kompyuta inavyofanya kazi  kwa wanafunzi ijulikanayo kama  ‘Airtel Fursa Lab’ hafla iliyofanyika  katika shule ya msingi Kijitonyama iliyopo  Wilaya ya Kinondoni leo jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi Mkuu wa Atamia ya Teknohama ya Dar es salaam ( DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Eng. George MulaMula akizungumza katika hafla ya uzinduzi maabara ya Kompyuta ijulikanayo kama  ‘Airtel Fursa Lab’ katika shule ya msingi Kijitonyama iliyopo  Wilaya ya Kinondoni leo jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Profesa  Faustine Kamuzora kwakushirikiana Mkurugenzi Mkuu wa Atamia ya Teknohama ya Dar es salaam ( DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Eng. George MulaMula pamoja na Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel, Betrice Singano wakikata utepe kuashiria uzinduzi  wa maabara ya Kompyuta ijulikanayo kama  ‘Airtel Fursa Lab’ katika shule ya msingi Kijitonyama iliyopo  Wilaya ya Kinondoni leo jijini Dar es Salaam
   Sehemu ya walimu na wanafunzi
   Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Profesa  Faustine Kamuzora akiwa na  Mkurugenzi Mkuu wa Atamia ya Teknohama ya Dar es salaam ( DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Eng. George MulaMula pamoja na Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel, Betrice Singano wakipata maelezo ya maabara ya Kompyuta ijulikanayo kama  ‘Airtel Fursa Lab’ katika shule ya msingi Kijitonyama iliyopo  Wilaya ya Kinondoni leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.

  0 0
  0 0  Octavian Nshiu Makamu wa Rais Viwanda Shirika la TCCIA akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa shirika hilo katika banda lao kwenye maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaa,
  Baadhi ya wadau wa TCCIA wanaoshughulika na mavazi ya viwandani na ujenzi wakiwa katika banda lao kwenye maonyesho ya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam

  0 0


  0 0

   Mwenyekiti wa bodi ya Bodi ya Utalii Tanzania ,Jaji Thomas Mihayo  akizungumza na wadau wa mikutano wakati wa ufunguzi Semina Maalum ya wadau hao kuhusu utalii wa mikutano hapa nchini ambao utaweza  kusaidia mapato ya sekta ya utalii na Taifa kwa ujumla.
   Mwenyekiti wa Bodi ya AICC, Balozi Dkt  Ladislaus Komba  akizungumza katika Semina ya wadau wa mikutano juu ya utalii wa mikutano ambao utaweza kukuza utalii nchini  na mapato ya mwekezaji mmoja mmoja kupitia mikutano hiyo
   Washiriki wa mkutano huo kutoka bodi ya utali nchini TTB wakifatilia kwa ukaribu yanayozunmzwa katika mkutano huo
   Mkurugenzi wa Mikutano kutoka AICC,Mkunde Senyangwa akizungumza na wadau walioshiriki Semina hiyo juu ya umuhimu wa utalii wa mikutano nchini
   Sehemu ya wadau walioshiriki mkutano huo wakisilikiliza mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa
   Mkufunzi kutoka kampuni ya Business Tourism  ya Afrika Kusini ,Rick Taylor akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya nchi nyingi zilivyofanikiwa kupitia Utaliihuo wa Mikutano
  Wajumbe wa mkutano huo wakizungumza jambo na  Mwenyekiti wa bodi ya Bodi ya Utalii Tanzania ,Jaji Thomas Mihayo

  0 0


  0 0

  Msanii wa muziki wa asili ambaye pia ni Balozi wa Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA), Mrisho Mpoto ametangaza deal kwa waimbaji pamoja na wapiga ala za muziki kujitokeza kwa wingi Sabasaba jijini Dar es salaam katika banda la maonyesho la Hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya kupata wasanii wapya watakao unda bendi mpya ya hifadhi hiyo.
  Akiongea wa wadau waliojitokeza kwa wingi katika banda hilo, Mrisho Mpoto ambaye ni balozi wa hifadhi hiyo, alisema vijana hao wanatakiwa kujua kuimba pamoja na mambo mbalimbali yanayohusu Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na vitu vinavyopatikana.
  “Hii fursa kwa waimbaji wa muziki pamoja na wapiga ala za muziki, tunatakiwa kuanzisha bendi ya muziki ‘Ngorongoro Band’, kuandaa nyimbo maalum ambazo zitakuwa zinawaelimisha watanzania juu ya ufahari wa hifadhi hii. Kuandaa wimbo ambazo zitawafanya watanzania kuijua zaidi mbuga zao , masuala ya utalii pamoja na vitu mbalimbali vilivyomo ndani yake,” alisema Mpoto.
  Katika hatua nyingine Mrisho amesema anashukuru wadau mbalimbali wanajitokeza kwa wingi katika banda la Ngorongoro kwaajili ya kujifunza mambo mbalimbali kuhusu hifadhi ya Ngorongoro pamoja na wanyama wanaopatika.
  “Kuwema kweli mambo yamekuwa mazuri sana katika banda letu, watu wanakuja kwa wingi sana kwa sababu sisi tunatoa burudani na elimu, burudani na elimu, kuna bendi hapa In African ambio inatoa burudani kila siku, kuna mastaa mbalimbali wanakuja kutoa burudani kama mlivyowana akina Stara Thomas, Solid Ground, Steve B&B na wengine wengi ambao wanakuja na kuondoka. Kwa hiyo kikubwa zaidi kwetu ni burudani na elimu,” alisema Mpoto.
  Aliongeza, “Pia tumekuwa na kipengele cha elimu kuhusu wanyama kila siku na baada ya haps tunawaita watoto waeleze vitu ambavyo wanajifunza kila siku na tumekuwa tukitoa zawadi ya mpaka tsh milioni moja kwa siku na tumeona matunda kabisa watoto wanakuja hapa hawajuhi chochote lakini wakiondoka hapa wanaweza kueleza vitu mbalimbali ambavyo vinapatika katika hifadhi ya Ngorongoro,”
  Mshairi huyo amewataka watanzania kwa ujumla kutembelea banda hili pamoja na watoto wao ili wapate kujifunza mambo mbalimbali kuhusu Hifadhi ya Ngorongoro.

  0 0


  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

  WAAJIRI na wafanyakazi wamejitokeza kwa wingi kupata elimu kuhusu kazi za Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwenye banda la Mfuko huo lililoko kwenye hema kubwa la Jakaya Kikwete kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kunakofanyika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam.

  Maonesho hayo ya kila mwaka huwaleta pamoja wafanyabiashara ya makampuni makubwa ya kimataifa kutoka nje na dnani ya nchi, lakini pia kunakuwepo na mkusanyiko mkubwa wa wafanyakazi wa umma na binafsi wanaotoa huduma mbalimbali kwa watu wanofika kutembeela maonesho hayo.

  Mfuko wa Fidia kwa wWafanyakazi, (WCF) imetumia fursa hiyo kutoa elimu kwa waajiri na wafanyakazi ambao walifika kwenye banda la Mfuko huo na kupatiwa maelezo ya kina kuhusu kazi za Mfuko kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wake Bw. Masha Mshomba, wakurugenzi na wakuu wa idara pia.

  “WCF ni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ulioanzishwa kwa mujibu wa sheria namba 5 ya Fidia kwa Wafanyakazi kifungu namba 263 ya mwaka 2015.” Bw. Mshomba aliyasema hayo akiwa kwenye banda hilo ambapo waajiri na wafanyakazi walifika kupata elimu zaidi ya kuhusu Mfuko huo.

  Bw. Mshomba aliendelea kufafanua kuwa, kwa mujibu wa sheria iliyoanzasha Mfuko huo, tofauti na Mifuko mingine ya Hifadhio ya Jamii, ambapo mwajiri na mfanyakazi hutoa michango ya kila mwezi, kwa upande wa WCF, ni mwajiri pekee ndiye anawajipika kumchangia mfanyakazi wake kila mwezi na mfanyakazi hawajibiki kutoa mchango wowote.

   Aidha Bw. Mshomba alieleza kuwa, dhumuni kuu la kuanzishwa kwa Mfuko huo ni kutoa Mafao ya kutosha na stahili  kwa Mfanyakazi aliyepatwa na maradhi au majeraha yaliyotokana na kazi anazozifanya Mfanyakazi huyo.
   Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCD), Dkt. Abdulsalaam Omar, akimfafanulia mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo lililoko kwenye hema kubwa la Jakaya Kikwete, kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam 2017, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kuhusu hatua ambazo mfanyakazi anapaswa kuchukua baada ya kupata maradhi au kuumia wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi kabla ya kupatiwa Fidia na WCF.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akizungumza wakati akiwa kwenye banda la Mfuko huo.

   Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Mfuko huo, Bi. Laura Kunenge, (kulia), akizungumza na Posta Masta Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Deo Kwiyukwa, wakati alipotembelea banda hilo.
    Mkurugenzi wa Huduma zaTiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCD), Dkt. Abdulsalaam Omar, akimfafanulia mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo lililoko kwenye hema kubwa la Jakaya Kikwete, kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam 2017, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kuhusu hatua ambazo mfanyakazi anapaswa kuchukua baada ya kupata maradhi au kuumia wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi kabla ya kupatiwa Fidia na WCF.
   Wafanyakazi hawa wakipatiwa maelezo mbalimbali yahusuyo huduma zitolewazo na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), walipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Meneja Masoko wa Benki ya Access Bank ,Sijaona Simon akizungumza na Mmoja wa Wateja waliotembelea Banda la benki hiyo hili kuweza kujipatia huduma mbalimbali zinazotolewa ikiwemo mikopo na akaunti ya malengo Maalum.
   Afisa Mikopo wa Access Bank , Marggoreth Riziki  akizungumza na mmoja  wateja juu ya huduma zinazotolewa na benki hiyo ikiwemo mikopo kwa wajasiliamali wadogo
   Afisa Mikopo wa Access Bank , Godbless Exaud  akizungumza na mmoja  wateja juu ya huduma zinazotolewa na benki hiyo ikiwemo mikopo kwa wajasiliamali wadogo.


  0 0

  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasilano Shirika la Ndege la ATCL Bi. Lilian Fungamtama akifurahia jambo na wananchi waliotembelea banda la shirika hilo lililopo katika banda la Maliasili katika maonesho ya biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, Maonyesho hayo yanaandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Nje TANTRADE na kufanyika kila mwaka mwezi Julai.
  Baadhi ya wananchi mbalimbali wakitembelea banda la Shirika la Ndege la ATCL katika viwanja vya maonesho vya J.K.Nyerere Barabara ya Kilwa.

older | 1 | .... | 1780 | 1781 | (Page 1782) | 1783 | 1784 | .... | 3278 | newer