Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1779 | 1780 | (Page 1781) | 1782 | 1783 | .... | 3278 | newer

  0 0


  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank PLC, Dkt. Charles Kimei wakati alipotembelea Banda la CRDB  kwenye Maonyesho ya Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa (sabasaba), yaliyoanza Juni 28 - Julai 8, 2017 ambapo kwa mwaka huu yameongezewa siku tano zaidi na kutarajiwa kumalizika Julai 13, 2017, yaliyozinduliwa na Rais mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Kilwa Road jijini Dar es salaam.
   Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimuuliza jambo Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank PLC, Dkt. Charles Kimei wakati alipotembelea Banda la CRDB  kwenye Maonyesho ya Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa (sabasaba), yaliyoanza Juni 28 - Julai 8, 2017 ambapo kwa mwaka huu yameongezewa siku tano zaidi na kutarajiwa kumalizika Julai 13, 2017, yaliyozinduliwa na Rais mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Kilwa Road jijini Dar es salaam.
   Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank PLC, Dkt. Charles Kimei akieleza jambo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipotembelea Banda la CRDB  kwenye Maonyesho ya Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa (sabasaba), yaliyoanza Juni 28 - Julai 8, 2017 ambapo kwa mwaka huu yameongezewa siku tano zaidi na kutarajiwa kumalizika Julai 13, 2017, yaliyozinduliwa na Rais mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Kilwa Road jijini Dar es salaam.
   Baadhi ya Wafanyakazi wa CRDB Bank PLC wakiendelea kutoa huduma za kibenki kwa wateja waliotembelea Banda lao.
  Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank PLC, Dkt. Charles Kimei akielekeza jambo kwa baadhi ya watendaji wa benki hiyo, katika Banda la CRDB  kwenye Maonyesho ya Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa (sabasaba), yaliyoanza Juni 28 - Julai 8, 2017 ambapo kwa mwaka huu yameongezewa siku tano zaidi na kutarajiwa kumalizika Julai 13, 2017, yaliyozinduliwa na Rais mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Kilwa Road jijini Dar es salaam.


  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk Aloyce Nzuki  akizungumza na baadhi ya watumishi wa wizara hiyo alipotembelea banda la Wizara hiyo Maonyesho ya Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa, yaliyoanza Juni 28 - Julai 8, 2017 ambapo kwa mwaka huu yameongezewa siku tano zaidi na kutarajiwa kumalizika Julai 13, 2017, yaliyozinduliwa rasmi leo jijini Dar es salaam. 

  Afisa Uhusiano wa Bodi ya Utalii Tanzania, Geofrey Tengeneza, akiwa katika mahojiano na Mwandishi wa kituo cha Radio cha Clouds Fm Power Breakfast ndani ya banda hilo akizungumzia juu ya utalii wa ndani
  Sehemu ya Watanzania waliotembelea banda Maliasili na kujionea wanyama mbalimbali ndani ya Zoo ndogo.
  Simba jike na Dume wakionekana ndani ya Zoo iliyopo ndani ya banda la Wizara ya maliasili ndani ya Maonyesho ya Sabasaba
  Mbega wakiwa ndani ya Zoo iliyopo ndani ya banda la Wizara ya maliasili katika Maonyesho ya Sabasaba.

  0 0

  Shirika la ndege la Kitanzania Precision Air limezindua kwa mafanikio safari zake za kwenda Entebbe. Ndege ya uzinduzi wa safari hizo iliondoka Jijini Dar es Salaam majira ya saa 1:10 asubuhi leo kuelekea Entebbe na kuwasili Entebbe majira ya saa 4:50 Asubuhi na kupokewa kwa salamu maalumu ya kumwagiwa maji na magari ya zima moto, ikiwa ni ishara ya kuanza rasmi kwa zama mpya za huduma za Precision Air kati ya Tanzania na Uganda.

  Akizungumzia kuanza rasmi kwa safari hizo Meneja Uratibu na Mahusiano Bw. Hillary Mremi amesema kuwa, kupitia safari za Precision Air Tanzania na Uganda wamehakikishiwa usafiri wa uhakika.

  “Tutakuwa tukifanya safari mara tatu kwa wiki, kila siku ya Jumatatu, Alhamisi na Jumamosi na baadaye kuongeza safari kulingana mahitaji ya soko.” Amekaririwa Bw. Mremi Precision Air iliahirisha safari za Entebbe mnamo mwaka 2013 kupisha maboresho ya mtandao wa wa safari zake katika kuhakikisha inazingatia tija katika shughuli zake.

  Precision Air ndilo Shirika pekee la ndege linalotambuliwa na IATA ambalo linafanya safari za moja kwa moja kati ya Tanzania na Uganda. Inatarajiwa safari hizi za Precision zitaimarisha mahusuano ya kiuchumi na kidiplomasia kati ya Tanzania na Uganda, hasa ikizingatiwa kuwepo kwa miradi mbali mbali ya pamoja kama ule wa bomba la mafuta litakalo anzia nchini Uganda hadi Tanzania.Ni miradi kama hiyo inayotarijiwa kunufaika na safari za Precision Air kwa kufanikisha miradi hiyo kwa wakati.

  Precision Air ilianzishwa mnamo mwaka 1993 kama shirika binafsi la ndege za kukodi,Shirika la ndege la Precision Air limeendelea kukua na kuwa moja ya mashirika ya ndege ya nayoheshimika Africa Mashariki na Africa kwa ujumla.Kwa sasa Shirika hilo linafanya safari za ndani na nje kuelekea sehemu takribani 11. Iktokea Dar es Salaam (makao makuu) Precision Air inasafiri kuelekea Arusha, Bukoba, Kigoma, Kilimanjaro, Musoma, Mtwara, Mwanza, Tabora, Zanzibar na Nairobi.

  0 0


  0 0

  Serikali ya Ufaransa imetoa mchango wa EUR 250,000 kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) ili wakimbizi wanaoishi nchini Tanzania wapate msaada zaidi wa fedha taslimu. Mchango huu unafuatia ule wa EUR 750,000 za mwaka jana, huu ukiwa uthibitisho wa utayari wa Serikali ya Ufaransa katika kuimarisha njia za kuleta usalama wa chakula na ujumuishi.

  Mwezi Desemba 2016, WFP ilianza kutoa TSh 20,000 (Dola za Marekani 9.00) kila mwezi kwa wakimbizi 10,000 kama sehemu ya programu ya majaribio inayotekelezwa kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR). Mchango wa Ufaransa unaiwezesha WFP kuendeleza programu ya fedha taslimu kwa wakimbizi 10,000 kwa miezi miwili ya nyongeza.

  Kupitia programu hii, wakimbizi wanapata mgao wa mafuta ya mbogamboga yaliyoongezewa virutubisho na mchanganyiko maalumu wa uji, wakati ambapo badala ya mgao wa mahindi, kunde na chumvi wakimbizi wanapewa fedha taslimu. Kabla ya kuzinduliwa kwa programu ya fedha taslimu, wakimbizi walikuwa wakipewa tu msaada wa chakula kutoka WFP.

  Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni, asilimia 98 ya kaya zinazoshiriki katika mpango huu zinapendelea fedha taslimu badala ya migao ya chakula, wakati ambapo asilimia 83 walisema utaratibu huu umeongeza ubora wa milo yao na uchaguzi mpana wa aina ya vyakula.

  “Msaada wa Ufaransa kwa mradi huu ni muhimu,” alisema Bi. Malika Berak, Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania. “Mfumo huu utawezesha kuwa na utoaji msaada wa chakula wenye ufanisi, unaoheshimu soko la bidhaa la mahalia na litakaloacha alama nzuri kwa mazingira.”


  Msaada wa fedha taslimu una manufaa ya nyongeza katika kuunda soko imara kwa wakulima na wafanya biashara wa mahalia, na wakati huo huo ukiwapatia wakimbizi na wanufaikaji wengine uhuru wa kuchagua nini wanunue, wapike na kuzilisha familia zao.

  “Kufuatia ubunifu katika njia za utumaji fedha taslimu, msaada wa fedha taslimu umeonekana siyo tu kuwa ndio unaopendelewa zaidi kwa wakimbizi kupokelea msaada wa chakula, bali pia kama njia yenye ufanisi inayokuza uchumi wa mahalia,” alisema Michael Dunford, Mwakilishi Mkazi wa WFP Tanzania. “Utumaji wa fedha taslimu na ongezeko la shughuli za kiuchumi kunaweza kusaidia kuimarisha miundombinu ya mahalia, kama vile huduma za fedha, huduma za masoko, na pia upatikanaji wa mitandao ya intaneti na simu.”

  Katika miaka ya karibuni, WFP imekuwa ikiongeza kiasi cha msaada inaotoa kwa njia ya fedha taslimu na vocha. Kote ulimwenguni, asilimia 29 ya wanufaikaji wa WFP wanapokea msaada wa chakula kwa njia ya utumaji wa fedha taslimu.

  Tangu kutokea kwa machafuko nchini Burundi mwaka 2015, karibu Warundi 250,000 wametafuta hifadhi nchini Tanzania, ambayo hivi sasa imewapa hifadhi wakimbizi 315,000, wengi wao wakiwa wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

  Hadi mwisho wa mwaka, WFP inalenga kupanua programu yake ya utoaji fedha taslimu ili kuwafikia wakimbizi 80,000. WFP inahitaji jumla ya Dola za Marekani milioni 6.8 kwa mwezi ili kuendelea kutoa msaada wa fedha taslimu na chakula kwa wakimbizi nchini Tanzania.

  0 0
 • 07/03/17--10:00: Article 1


 • 0 0


  0 0


  0 0

  Mkurugeni mtendaji wa kampuni ya Global Packaging Ndg Joseph Wasonga(wa pili kulia) akiwapa maelezo wakurugenzi wa TIB juu ya bidhaa zinazotengenezwa na kampuni hiyo. Wa kwanza kushoto ndugu Frank Nyabundege Mkurugenzi mkuu wa wa TIB Corporate Bank . Wa pili kushoto Charles Singili –Mkurugenzi Mkuu wa TIB Development Bank na wa mwisho kulia ni Bi Theresia Soka mkuu wa kitengo cha masoko – TIB Corporate Bank Ltd. Kiwanda cha Global Packaging ni miongoni mwa wateja ambao wamenufaika na mikopo inayotolewa na benki ya TIB. Kiwanda hiki ni miongoni mwa viwanda vya kisasa ambavyo vinazalisha vifungashio mbali mbali.
  Wafanyakazi wa TIB Group (TIB Development Bank Ltd, TIB Corporate Bank na TIB Rasilimali Ltd) wakiwa tayari kutoa huduma kwenye viwanja vya Maonyesho - Saba Saba.
  Wafanya kazi wa TIB Corporate Bank Ltd katika picha ya pamoja, wakiwa taya ri kuwahudumia wananchi mbalimbali watakao tembelea banda lao katika maonyesho hayo.

  0 0

  New York City - July 3rd, 2017 — After weeks of a closely guarded audition process, 2014 Big Brother Africa-Hotshots winner Idris Sultan is cast in the upcoming American motion picture ‘Ballin...On the Other Side of the World,' to be directed by Harvey White, an American music director and editor turn filmmaker who’s worked with Chris Brown, Mariah Carey, Lady Gaga and Tamia to name a few. As a film editor, he’s worked on films such as 'Think Like A Man 2,''The Wedding Ringer,' and ‘King of The Dance Hall,’ with Whoopi Goldberg.

  Written by Torino Von Jones, the story is about a young Kenyan boy (Kunjani), whose parents are victims of a violent crime. One day on the schoolyard, the thirteen year old is noticed by an American priest who sees him playing basketball and believes he has potential for greatness in the NBA. The two develop a friendship and a mentorship begins. (King) to be played by Sultan, is a very charming, but an extremely dangerous gangster who has another idea and wants Kunjani to join his gang of criminals and will stop at nothing to make it happen.

  Last seen in the Tanzanian film ‘Kiumeni,’ which marked his feature film debut, Idris will be in Zanzibar next week for ZIFF (Zanzibar International Film Festival) to screen ‘Kiumeni’ during ZIFF’s Swahili Day on July 14th, with the producer and star Ernest Napoleon. Earlier this year, Mr. Napoleon made history when he was appointed president of the American production and distribution company D Street Media Group based in New York City, with offices in Berlin, Buenos Aires and Cape Town.

  D Street’s CEO and executive producer Dexter Davis became aware of Idris from a private screening of ‘Kiumeni’ in the United States and thought he would be great for one of the leading roles. “Idris Sultan has what it takes to become an international star and our upcoming film ‘Ballin…On the Other Side of the World’ is a perfect fit. We’re considering Mr. Sultan for other movies as well, said Davis. The team is now looking forward to casting the American and Kenyan parts and can’t wait to do a major talent search for the actors in Kenya and other East African countries including Tanzania if necessary.”

  The story takes place in New York City and a major city in Africa. The producers are deciding which African country the production will be filmed and looking at the beginning of the new year to start shooting. The film’s budget is set at $5 Million U.S. dollars and will also star two American A-list actors to play the priest and his best friend. ‘Ballin’ is another example of D Street’s commitment to put African talent and Africa on display in productions for the international market. The company is also behind the action-packed heist film ‘The Blue Mauritius,’ which is shooting in Cape Town and seeing South African star Pearl Thusi team up with Eric Dane (Grey’s Anatomy) and John Rhys-Davies (Lord of the Rings,) and many more international stars from around the world.

  0 0

  Na Karama Kenyunko.

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewasomea upya mashtaka, washtakiwa Harbinder  Singh Sethi na James Burchard  Rugema rila kwa kuwaongezea mashtaka na kufanya idadi yao kufikia 12.

  Mapema mwezi uliopita, washtakiwa hao walipandishwa kizimbani hapo baada ya kusomewa mashtaka sita kabla ya leo kuwa 12.

  Katika mashtaka hayo ambayo ni ya uhujumu uchumi yapo pia matano ya utakatishaji wa fedha na kuisababishia Serikali hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

  Mashtaka hayo ni, kula njama, kujihusisha na mtandao wa uhalifu , kughushi,  kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu kuisababishia Serikali Hasara na kutakatisha fedha.

  Washtakiwa wamesomewa mshtaka yao mapya na wakili wa Serikali, Shedrack Kimaro mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

  Katika shtaka la kwanza inadaiwa, Rugemarila Mkurugenzi wa VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL na Sethi ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa PAP,    kati ya oktoba 18 ,2011 na Machi 19 , 2014 jiji Dar es Salaam walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

  Imedaiwa kuwa, Oktoba 18,2011na Machi 19,2014 washtakiwa hao wakishirikiana na watumishi wa umma walitekeleza mtandao huo wa uhalifu kwa lengo la kujipatia faida.

   Aidha katika shtaka la tatu linalomkabili  Sethi peke yake imedaiwa, Oktoba 10,2011 katika mtaa wa Ohio Ilala, akiwa na nia ya ulaghai alighushi fomu namba 14 a ya usajili wa makampuni  na kuonyesha yeye ni mtanzania anayeishi Kitalu namba 887 Mtaa wa Mrikau Masaki wakati akijua ni uongo.

  Seth pia anadaiwa kutoa nyaraka ya kughushi ambayo ni fomu namba 14a ya usajili wa kampuni kwa ofisa msajiri wa kampuni,Seka Kasera kwa njia ya kuonesha kwamba yeye ni mtanzania na Mkazi wa Mtaa wa Mrikau.
   Mtuhumiwa James Burchard  Rugemarila akirejeshwa rumande 
  Mtuhumiwa Harbinder  Singh Sethi wakirejeshwa rumande.


  0 0


  Na Teresia Mhagama, DSM

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani amepiga marufuku uagizaji wa nguzo za umeme, nyaya na transfoma nje ya nchi na kuliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha kuwa linanunua vifaa husika kutoka kwa wazalishaji wa ndani.

  Dkt. Kalemani aliyasema hayo wakati wa kikao chake na watendaji wa TANESCO, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na wazalishaji wa nguzo za umeme, transfoma na nyaya za umeme kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.

  Alisema kuwa kikao hicho kililenga kukutanisha pande mbili yaani REA, TANESCO na wazalishaji wa vifaa vya umeme ili kufahamu mahitaji halisi ya vifaa vya umeme na kampuni zinazotengeneza vifaa hivyo, kuieleza Serikali kama wanao uwezo wa kuzalisha vifaa husika kwa kuzingatia ubora unaohitajika.

  “Tumedhamiria kusambaza umeme kwa kasi mijini na vijijini hivyo tunahitaji kufahamu uwezo wenu wa uzalishaji, tuelezeni hali halisi na kama kuna changamoto tuzijadili hapa na kufikia suluhisho kwani msimamo wa Serikali ni kutumia vifaa vya umeme vinavyozalishwa ndani ya nchi,” alisema Dkt. Kalemani.

  Aliongeza kuwa ingawa Serikali imeamua kutumia vifaa vya umeme vinavyozalishwa ndani ya nchi, kampuni husika zinapaswa kuzalisha vifaa vyenye ubora ili kuiondolea TANESCO gharama ya kubadilisha miundombinu ya umeme mara kwa mara na kwamba vifaa husika viuzwe kwa gharama itakayofaidisha pande zote mbili.

  Kwa upande wa mahitaji ya Transfoma, kampuni ya TANELEC, inayozalisha transfoma hizo ilieleza kuwa ina uwezo wa kutengeneza transfoma 10,000 zenye ukubwa tofauti kwa mwaka huku mahitaji ya REA na TANESCO yakiwa ni transfoma 8000 kwa mwaka hivyo watakidhi mahitaji ya hapa nchini.

  Kwa upande wa kampuni inayotengeneza nyaya za umeme ya East African Cables, ilieleza kuwa ina uwezo wa kutengeza nyaya za urefu wa kilomita 14,000 zenye uwezo wa msongo wa kati (medium voltage) kwa mwaka huku mahitaji ya TANESCO na REA yakiwa ni kilomita 10,100.

  Kampuni hiyo pia ilieleza kuwa ina uwezo wa kutengeneza nyaya za umeme za urefu wa kilomita 38,000 zenye uwezo wa msongo wa chini (low voltage) huku mahitaji ya REA na TANESCO yakiwa ni kilomita 31,000 kwa mwaka hivyo itaweza kukidhi mahitaji ya nyaya hizo nchini.

  Kuhusu uwezo wa wazalishaji wa nguzo nchini, kampuni zilizohudhuria kikao hicho zilieleza kuwa zina uwezo wa kuzalisha nguzo takribani 1,200,000 kwa mwaka huku mahitaji ya TANESCO na REA yakiwa ni nguzo 1,000,000 kwa mwaka.

  Dkt. Kalemani alitoa wito kwa kampuni hizo za Tanzania kuhakikisha kuwa wanatekeleza mahitaji ndani ya wakati na viwango vinavyokubalika ili kuweza kuhakikisha kuwa Sekta ndogo ya Umeme inaivusha nchi kwenda uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

   Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (wa kwanza kushoto) akiwa katika kikao na watendaji wa TANESCO, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na wazalishaji wa nguzo za umeme, transfoma na nyaya za umeme kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.
   Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo ( wa kwanza kushoto) akiwa katika kikao na  watendaji wa TANESCO, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na wazalishaji wa nguzo za umeme, transfoma na nyaya za umeme kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni  Kaimu Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga (wa pili kushoto),  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Dkt. Gideon Kaunda (wa tatu kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa  TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka.

  Baadhi ya wazalishaji wa nguzo za umeme, transfoma na nyaya za umeme wakiwa katika kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam ambacho kiliongozwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani).


  0 0

   Afisa Teknohama wa Islamic Benki ya PBZ ,Rahma Ali akizungumza na mmoja wateja waliofika katika banda lao la Maonyesho lililopo katika Viwanja vya Maonyesho ya Sabasaba  ambapo benki hiyo inawezesha kufungua akaunti ya Islamic benki na kuwezesha kupata mkopo usiokuwa na riba.
   Afisa Mahusiano wa PBZ -Bank LTD ,Aisha  Ali Mohd akizungumza na mmoja wa wadau waliofika katika banda la PBZ kupata maelekezo namna ya kufungua Akaunti kwenye benki hiyo

   Afisa  Masoko  PBZ Bank, Anas  Rashid Ramadhani akizungumza na wateja juu ya huduma za mikopo na ufungaji wa akaunti katika benki hiyo pamoja na ununuzi wa Viwanja kwa njia ya mkopo ambao utalipwa ndani ya miaka 10 wakati wa Maonyesho ya Sabasaba
   Wafanyakazi wa PBZ ,Hamyer Said na Biubwe Vuai wakimuelekeza mteja aliyefika katika banda hilo faida za Islamic Bank
   Salehe Abdalah akizungumza na mmoja wa wateja waliofika katika banda la Benki ya watu wa Zanzibar PBZ kutaka kufungua akaunti wkati wa Maonesho ya Sabasaba.

  0 0

  Na Ripota wa Globu ya Jamii,

  SERIKALI imetoa wito kwa taasisi za elimu ya afya na mashirika mbalimbali yanayofanya tafiti za afya hapa nchini kuhakikisha tafiti hizo zinafika kwa wadau na wananchi kwa ujumla ili zilete tija zaidi kwa jamii badala ya kuzifungia kwenye ofisi zao.

  Wito huo wa serikali ulitolewa mwisho wa wiki jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Elimu ya juu, Wizara ya Elimu, Sayansi, teknolojia na mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylvia Temu alipomuwakilisha Katibu Mkuu Wizara hiyo, Dk. Leonard Akwilapo kwenye hafla ya kuhitimisha Mkutano wa tano wa kisayansi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS).

  “Kwa sasa tunaelekea kwenye uchumi wa viwanda na miongoni mwa sekta muhimu ambazo pia zinatarajia wawekezaji ni pamoja na sekta ya afya hivyo basi muelekeo na mapendekezo ya tafiti za afya ndio zitakazoweza kuwasaidia wadau na serikali kufahamu aina ya ukwekezaji huo pamoja na maeneo gani yanafaa kulingana na mahitaji. Tafiti hizi zikifungiwa kwenye makabati tafsiri yake ni kwamba hata hii mikutano itakosa tija pia.’’ alisisitiza.

  Aliongeza kuwa Serikali kwa kiasi kikubwa inajitahidi kutumia tafiti hizo katika kuandaa sera mbalimbali zinazohusiana na masuala ya afya huku akitoa pongezi kwa uongozi wa chuo hicho kwa kuendelea kuandaa wataalamu wanaoandaa tafiti hizo kwa weledi na ufanisi mkubwa.

  “Zaidi umuhimu wa mkutano huu ni pale unapowakutanisha wataalamu wa afya tena katika ngazi tofauti wakiwemo wale waliobobea pamoja na wanafunzi na hivyo kuwa kama jukwaa kwa wao kuweza kubadilishana ujuzi. Jumla ya tafiti 160 tofauti za afya zimewasilishwa kupitia mkutano huu ambapo tafiti 70 kati ya hizo zilijadiliwa kwa kina na wataalamu hawa,’’ aliongeza.

  Awali, akizungumza kwenye hafla hiyo Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa MUHAS, Prof. Appolinary Kamuhabwa alisema nyingi kati ya tafiti zilizowasilishwa kwenye mkutano huo wa siku mbili zilijikita katika vipaumbele vya taifa yakiwemo masuala ya HIV/AIDS, kifua kikuu, afya ya uzazi na mtoto, magonjwa yasiyo ya kuambukiza, ajali pamoja na magonjwa ya kitropiki yaliyosahaulika.

  “Ndio maana tunaishukuru sana serikali ya Sweden kupitia Shirika la Sida ambao kwa kushirikiana na wadau wengine wamewezesha mkutano huu muhimu.,’’ alisema Prof Kamuhabwa huku akibainisha kuwa chuo hicho kimejipanga kuhakikisha tafiti hizo zinawafikia walengwa ikiwemo Serikali, mashirika na taasisi mbalimbali pamoja na wananchi kwa ujumla.
   Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Tano wa Sayansi ya Afya waChuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS) Dk. Irene Kida akitoa majumuisho ya Mkutano huo mbele ya Mkurugenzi wa Elimu ya juu, Wizara ya Elimu, Sayansi, teknolojia na mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylvia Temu (wa tatu kushoto meza kuu) wakati wa hafla fupi ya kuhitimisha mkutano huo uliofanyika kwa mwishoni mwa wiki  jijini Dar es Salaam. Wengine ni pamoja na walimu na uongozi wa chuo hicho akiwemo Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa MUHAS, Prof. Appolinary Kamuhabwa ( wa pili kushoto)
  Mkurugenzi wa Elimu ya juu, Wizara ya Elimu, Sayansi, teknolojia na mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylvia Temu (wa pili kushoto) akisikiliza maelezo kuhusiana na dawa za asili zinazoandaliwa na kitengo cha tiba asili katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS) alipotembelea maonyesho ya shughuli zinazofanywa na MUHAS mara baada ya kuhitimisha Mkutano wa tano wa kisayansi ulioandaliwa na chuo hicho jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Wanaoshuhudia ni pamoja na viongozi wa Chuo hicho akiwemo  na Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa MUHAS, Prof. Appolinary Kamuhabwa (kushoto)


  0 0

  Mkutano wa 29 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) amefunguliwa rasmi Jijini Addis Ababa- Ethiopia ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anawakilishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo 

  Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi na Serikali unaofanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika Jijini Addis Ababa- Ethiopia na utajikita katika kujadili masuala mbalimbali yanayohusu umoja huo ikiwemo hali ya ulinzi na usalama katika Bara la Afrika hasa kwenye nchi za Sudan Kusini, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo- DRC na Libya.

  Aidha, Viongozi hao watajadili hali ya usalama kwenye baadhi ya nchi ambazo ziliathiriwa na kundi la Boko Haram za Nigeria, Niger, Chad na Cameroon.

  Wakuu hao wa Nchi na Serikali wa AU pia watajadili kwa kina kuhusu uanzishwaji wa eneo huru la kibiashara katika bara la Afrika kwa ajili ya kuliendeleza Bara hilo kwa ajili ya kukuza biashara baina ya nchi wanachama, uwekezaji, kuondoa vikwazo vya kibiashara pamoja na kupunguza utegemezi kwa masoko ya nje.

  Mambo mengine yatakayojadiliwa na Viongozi hao ni bajeti ya Umoja huo, mpango mkuu kuhusu hatua za kivitendo za kuzuia mapigano katika Afrika kufikia mwaka 2020, maboresho katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na maboresho ya kitaasisi katika AU.

  Kwa upande wa Tanzania, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan anaongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo ambao unahudhuriwa pia na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Augustine Mahiga na Waziri wa Kazi,Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maudline Cyrus Castico pamoja na Watendaji wengine wa Serikali. Kauli Mbiu ya Mkutano wa mwaka huu ni Kuimarisha Mgawanyiko wa Idadi ya Watu Kupitia Uwekezaji katika Vijana. (Harnessing Demographic Divident Through Investments in the Youth)
  Picha ya pamoja 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amemwakilisha Rais wa John Pombe Magufuli katika mkutano wa AU katika Makao makuu ya Umoja huo Addis Ababa- Ethiopia.Mkutano umefunguliwa hii Leo Jijini Addis Ababa- Ethiopia.
  Mkutano wa AU katika Makao makuu ya Umoja huo Addis Ababa- Ethiopia uliofunguliwa leo hii eo Jijini Addis Ababa- Ethiopia ukiendelea

  0 0

  Albano Midelo ni Mwandishi wa kitabu cha Neema ya Mafuta na Gesi Tanzania, Azungumzia sababu za kuandika kitabu hicho ambacho kimeanza kuzaa matunda kutokana nay ale aliyoyaandika, Je amepata mafanikio gani katika uandishi wa kitabu hicho ? pia azungumzia vitabu vingine anavyoviandaa kuviingiza sokoni.

  0 0  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira na Uongozi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.

  Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) wakiwa katika mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika ukumbi wa Ikulu MJini Unguja leo
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Maji na Nishati Zanzibar(ZURA) Ng,Haji Kali alipokuwa akitoa mchango na kuelezea maendeleo waliofikia katika Mamlaka hiyo walipokuwa na Kikao cha siku moja cha Uongozi wa Wizara ya Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira na Uongozi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) akiwa Mwenyekiti wa Kikao hicho kilichofanyuika leo Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 03/07/2017.
   

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Luckness Amlima amewakamata wanunuzi wawili wa mazao kutoka manispaa ya Songea kwa kununua mazao katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo katika kijiji cha Namahoka bila kibali kutoka Halmashauri hiyo.

  Wanunuzi hao waliokamatwa ni Omari Fundi na Salumu pili wote kutoka manispaa ya Songea wakinunua mpunga eneo la kilimo cha umwagiliaji katika kijiji cha Namahoka wilayani humo.

  Akiwakamata wanunuzi hao Mkuu wa wilaya huyo aliwataka wafanyabiashara hao kuonesha vibali vya kununua mpunga katika eneo hilo ambapo walishindwa kutoa vibali hivyo na ndipo aliamuru washikwe mpaka walipe ushuru pamoja na faini kwa kutofuata utaratibu .

  Aidha katika hatua nyingine mkuu wa wilaya huyo aliwataka wakulima katika eneo hilo kutumia fulsa ya kilimo cha umwagiliaji kujipatia kipato na kubadilisha maisha yao na kuacha kuwanufaisha wafanyabiashara ambao wanawanyonya kila mara.

  “Sitakubali Serikali imetumia fedha nyingi kujenga miundombinu ya umwagiliaji kwa ajili ya kuwawezesha wakulima walime zao la mpunga kwa vipindi viwili kwa mwaka lakini wafanyabiashara wanajipenyeza kuwakopesha wananchi fedha kwa riba kubwa na kuwafanya wananchi hao kubaki katika hali zao za umaskini na kuwanufaisha wafanyabiashara alisema mkuu wa wilaya huyo.

  Omari Silimu (Mamboya ) mkulima katika eneo hilo alimwambia mkuu wa wilaya huyo kuwa ni kweli kuwa wafanyabiashara hao wanawanyonya wakulima kwa kuwakopesha pesa shilingi elfu ishirini mpaka thelathini wakati wa kupanda kwa ahadi ya kulipa mpunga kiasi cha kilo 120 baada ya mavuno ambapo wakati huu wa mavuno kiasi hicho cha mpunga ni shilingi 120,000.

  Mhasibu wa mapato Mji mdogo Lusewa alisema kuwa wafanyabiashara hao walikubali kulipa ushuru pamoja na faini kwa kukiuka utaratibu wa ununuzi wa mazao katika halmashauri hiyo na kuwataka wakulima wanaowakaribisha wafanyabiashara kwenye maeneo ya kilimo kwa njia za kinyemera nao watahesabika na kuunganishwa na wafanyabiashara katika kulipa ushuru na faini.
  Mkuu wa wilaya aliyevaa kitenge akiwafokea akinamama wanaokubali kuzurumiwa nguvu zao kwa kupewa shilingi elfu thelathini wakati wa kupanda mpunga na kulipa mpunga kiasi cha kilo 120 kila elfu thelathini ambapo kwa sasa wangeweza kupata shilingi 120,000 badala ya shilingi 30,000( Na mpiga picha Yeremias Ngerangera)

  0 0

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja, wakati alipotembelea banda la maonesho la benki hiyo wakati wa Sherehe ya Vyama vya Ushirika yaliyofanyika kitaifa mwishoni mwa wiki mjini Dodoma, Waziri Mkuu ameiagiza benki hiyo kuhakikisha inafikisha huduma za bima ya matibabu na Bima ya Mazao kwa vyama vilivyoko vijijini. Pamoja nao katika picha ni Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Charles Tizeba.

  0 0

  Naibu Mhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) anayeshughulikia huduma za jamii, Asangye Bangu amewataka watanzania kuanza kuhamasika kutembelea hifadhi ya wanyama ya Ngorongoro ili kujionea mambo mbalimbali yanayopatikana ndani ya hifadhi hiyo.

  Bangu amesema hayo akiwa katika banda la balozi wa hifadhi hiyo Mrisho Mpoto lililopo katika viwanja maonesho ya biashara vya Babasaba jijini Dar es salaam.

  “Hii ni fursa ya pekee kwa watanzania kuanza kuhamisika na kwenda kuangalia maajabu ya hifadhi ya Ngorongoro, kusema kweli tunakosa uhondo kabisa. Kwa sababu wewe jiulize mzungu anapanda ndege na kutumia gharama kubwa kuja Ngorongoro wakati sisi wenyewe tupo karibu hapa tunashindwa kuwapeleka watoto wetu kijifunza mambo mbalimbali,” alisema Bangu.

  Alisema Ngorongoro Crater ni mbuga ya wanyama mfano wa bakuli kubwa lililoundwa miaka 25 elfu iliyopita baada ya milima miwili Makaroti na Satiman kulipuka na kutoa tope lenye moto. Tope hili ndilo lilikuwa na tabaka tatu za udongo na kuumba bonde lililofanana na bakuli kubwa ambalo wenyeji wa kabila la Kimasai walilipa jina la Ngorongoro Kaldera.

  “Kijiji cha Malanja ni cha pekee katika bonde la Ngorongoro katikati ya Milima ya Makaroti ambao ni mkubwa na Satiman ambao ni mdogo. Wenyeji wa kijiji hicho huendesha Maisha yao kama kawaida ya kufuga mifugo yao ndani ya mbuga wakichanganyika na wanyama pori,” alisema

  Pia katika bonde hilo kuna mto mmoja ambao unatoka Olmot Crater, Ziwa Magadi ambalo wakati wa kiangazi hukauka na kutoa vumbi aina ya majivu ambayo wenyeji wa Kimasai hutumia kuwalisha Ng’ombe kama dawa ya kudhibiti magonjwa.

  Alisema huwezi kuitaja Hifadhi ya Ngorongoro Crater bila kuwataja wanyama wakubwa wajulikanao kama “Big Five”, ambao ni Faru, Tembo, Chui, Nyati na Simba.

  “Kinachovutia zaidi ni kuona wanyama wote, wakali na wapole jinsi wanavyoishi kwa pamoja hadi pale tu wanapokuwa na njaa ndio hubadilikianana. Penye kundi la Nyumbu, Faru, Punda milia, Ngiri, Nguruwe na kadhalika utawakuta pia Simba pembeni wamelala wakipunga upepo baada ya kupata mlo wa mchana. Hii ni kuonyesha kwa jinsi gani wanaishi kama familia moja na wako katika nyumba moja,” alisema B

  Bangu aliwataka watanzania kuacha kusimuliwa kuhusu ufahari wa Ngorongoro bali watembelee mbuga hiyo kwaajili ya kujionea wenyewe

older | 1 | .... | 1779 | 1780 | (Page 1781) | 1782 | 1783 | .... | 3278 | newer