Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109604 articles
Browse latest View live

Makamu wa Rais,Dkt. Bilal afunga Mafunzo ya Uofisa na Ukaguzi wa Jeshi la Polisi,Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini jijini Dar leo

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal akikagua Gwaride Maalum lililoandaliwa na Wahitimu wa kozi ya Uofisa na Ukaguzi wa Jeshi la Polisi leo katika Chuo cha Taaluma ya Polisi, Kurasini, Jijini Dar Es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal akimvisha Cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Mhitimu wa Kozi ya Ukaguzi wa Polisi INSP. Leah Cheyeki kwa niaba ya Wahitimu wenzake kutokana na kufanya vizuri katika Mafunzo hayo. Sherehe za kuhitimisha Mafunzo hayo zimefanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi leo Kurasini, Jijini Dar es Salaam.
Wahitimu wa kozi ya Uofisa na Ukaguzi wa Polisi wakipita mbele ya Mgeni Rasmi kwa mwendo wa haraka Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayupo pichani. Sherehe za kuhitimisha Mafunzo hayo zimefanyika leo katika Chuo cha Taaluma ya Polisi, Kurasini, Jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Judo kikionesha Onesho Maalum la namna ya kupambana na Mhalifu ambaye hataki kutii amri halali ya Polisi. Sherehe za kufunga Mafunzo ya Kozi ya Uofisa na Ukaguzi wa Polisi zimefanyika Chuo cha Taaluma ya Polisi, Kurasini, Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dkt. Emmanuel John Nchimbi(wa pili kutoka kushoto mwenye suit nyeusi)akiwa na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama ambao wamehudhuria Sherehe hizo za ufungaji Mafunzo ya Kozi ya Uofisa na Ukaguzi wa Polisi(katikati) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja.
Baadhi ya Wananchi waliohudhuria Sherehe za Ufungaji Mafunzo ya Kozi ya Uofisa na Ukaguzi wa Polisi katika Chuo cha Taaluma ya Polisi, Kurasini Jijini Dar es Salaam(Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Wadau wa Haki za Wanyama Mnasemaje kwa hili?

0
0
Mbwa akiwa amepakiwa juu ya Carrier ya gari maeneo ya Msamvu roundabout, Morogoro. Wadau wa Haki za Wanyama mnasemaje? By Mdau

OMMY DIMPOZ KUWASHA MOTO AMERICA NA CANADA

Vyombo vya habari vyatajwa kama mdau muhimu kwa maendeleo ya kilimo

0
0
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Vyombo vya habari nchini vimetakiwa kutumia nafasi na taaluma maalum iliyonayo kuhakikisha kuwa umaskini unapigwa vita kupitia sekta ya kilimo.
Wito huu umetolewa wakati wa semina ya mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusiana na uandishi wa habari za biashara na uchumi.
Pia semina hiyo ililenga kuwapa uwezo na uelewa wa kuandika kuhusu matokeo ya utafiti kuhusu ripoti inayojulikana kama AgFiMS Tanzania 2011 Demand Side Technical Report.
Ripoti hiyo ilifanywa na Financial Sector Deepening Trust Tanzania (FSDT).
Mkuu wa kitengo, Huduma za Kifedha sekta ya kilimo, FSDT, Bw. Mwallu Mwachang’a alisema jana jijini Dar es Salaam kwamba vyombo vya habari vina nafasi ya pekee kutafuta, kuchambua na kusambaza habari kuhusiana na maswala ya fedha na kilimo kuliko taaluma nyingine yoyote na kwamba ni vyema kama wakitumia nafasi hiyo kuendeleza sekta ya kilimo na hivyo nchi nzima kwa ujumla.
“Waandishi wana nafasi muhimu na kipekee katika kuripoti maswala ya mahitaji ya fedha katika sekta ya kilimo…nia yetu ni kuwawezesha kufanya hivyo,” alisema.
Mmoja wa wawezeshaji katika mafunzo hayo toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Humphrey Moshi alisema huu ni muda muafaka kwa waandishi wa habari nchini kutumia taaluma yao kuokoa sekta ya kilimo, hasa upatikanaji wa fedha kwa wakulima.
“Fursa za fedha kwa sekta ya kilimo inayoajiri watu wengi hasa vijijini bado ni changamoto kubwa, hili ni tatizo na waandishi wana nafasi kushughulikia changamoto hii,” alisema Prof. Moshi.      
Mkurugenzi wa maswala ya ufundi, FSDT, Mr. Sosthenes Kewe alisema moja ya vikwazo vinavyowakabili wakulima wadogo na wanaojihusisha na biashara ya kilimo ni ukosefu wa fedha kwa kuwa vyombo vya fedha bado vinawaona kama watu wasiokua na sifa kupata mikopo.
“Hili limesababisha vyombo hivi vya fedha kutokua na huduma zinazolenga maendeleo ya kilimo kwa kiwango kinachotakiwa,” alisema.
Moja ya madhumuni ya ripoti ya AgFiMS Tanzania 2011 ilikua ni kusaidia maendeleo ya huduma za fedha kuchochea biashara katika kilimo na kufikisha huduma hizo kwa wakulima.
Kwa mujibu wa wataalamu, maendeleo ya kilimo ni njia bora ya kupunguza umaskini.  Asilimia 75 ya maskini katika nchi zinazoendelea wanaishi vijijini na asilimia 85 ya watu hao wanategemea kilimo kuendesha maisha yao.
FSDT inalenga kuhamasisha watu katika kada na maeneo mbalimbali nchini kukubalika na kushiriki kwa kiwango kinachoridhisha katika mfumo rasmi wa kifedha.

Rais Wa Sri Lanka Manida Rajapaksa awasili nchini leo

0
0
Mtoto Faith Warioba anayesoma katika shule ya awali ya Montessori jijini Dar es Salaam akimlaki kwa maua Rais Mahinda Rajapaksa wa Srilanka muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ziara ya kikazi nchini huku Rais Dkt.Jakaya Kikwete akishuhudia.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Mahinda Rajapaksa wa Srilanka muda mfupi baada ya kuweasili nchini kwa ziara ya kikazi leo asubuhi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.Kushoto ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik.
Rais wa Srilanka Mhe.Mahinda Rajapaksa akisalimia na Msaidizi wa Rais Masuala ya Kidiplomasia,Balozi Liberata Mulamula wakati Rais Kikwete alipokuwa akiwatambulisha baadhi ya viongozi na wasaidizi wake kwa mgeni wake muda mfupi baada ya kuwasili nchini kwa ziara ya kikazi leo asubuhi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais wa Srilanka Mhe.Mahinda Rajapaksa wakipokea heshima za urais muda mfupi baada ya mgeni huyo kuwasili katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Rais Wa Sri Lanka Me.Mahinda Rajapaksa akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo asubuhi kwa ziara ya kikazi nchini.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Mahinda Rajapaksa wa Sri Lanka wakiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za utamaduni vilivyokuwa vikitumbuiza katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati wa shamrashamra za kumpokea mgeni huyo wakati alipowasili leo asubuhi kwa ziara ya kikazi nchini.(picha na Freddy Maro).

Taarifa za uwepo wa taasisi ya kifedha kwa ajili ya mikopo iliyoandaliwa na Serikali si za kweli,ogopa matapeli

TANGAZO KWA MADAKTARI ,WAFAMASIA , MAAFISA AFYA MAZINGIRA NA MAAFISA WATEKNOLOJIA MAABARA WALIOPANGIWA VITUO VYA KAZI WAKIWABADO WAKO KWENYE MAFUNZO KWA VITENDO

Rais Kikwete akutana na Kiongozi wa Shirika la UNDP,Bi. Helen Clark,Pia akutana na Spika wa bunge la Oman ikulu jijini Dar leo

0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha na kufanya mazungumzo na Kiongozi wa Shirika la UNDP(UNDP Administrator) Bi. Helen Clark ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Kiongozi wa Shirika la UNDP(UNDP Administrator) Bi. Helen Clark ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Spika wa bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Al Mawaali ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wajumbe waliofuatana na Spika wa Bunge la Oman ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Spika wa Bunge la Oman Mhe.Sheikh Khalid Bin Hilal Al Mawaali ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Oman Mhe.Sheikh Khalid Bin Hilal Al Mawaali na ujumbe wake ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.kulia ni Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai.
(picha na Freddy Maro).

Plot for sale

t's Cocktail Party "The Last One Standing" @ Napoleon With DVJ Infinity

KUMBUKUMBU

0
0
MAREHEMU KATALINA STACHUMA SEMSENA
1945-2000

Imetimia miaka 13 tangu ututoke ghafla usiku wa tarehe 28 Juni 2000 wakati bado tulikuwa tunakuhitaji. Ingawaje kimwili umetutoka, kiroho bado tunakukumbuka.

Unakumbukwa na mume wako Mzee ATTILIO LUSINDE MWANG’INGO watoto wako AUDA, Eng. ROMANUS, RITHA, BENJAMIN, DR. GETRUDE, SALOME, DOROTHY , Eng. LILIAN na wajukuu wako Tawela, Antony, Nora, Adam, Eric, Catherine na Silvanus, wakwe zako Mh. Msiska(Mbunge), Lorna, Mary, Eng. Elisante na ndugu wote wa ukoo wa Ng’ingo na Msena..

Tunakukumbuka siku zote kwa upendo wako, mawazo yako yaliyojaa busara, ukarimu na malezi bora. Tulikupenda lakini Mungu alikupenda zaidi.

Tunamwomba Mwenyezi Mungu aiweke roho yako mahali pema peponi Amina.  

President Kikwete talks about U.S President Obama Visit to Tanzania

Gearing up for Global 2013 today in dar es salaam

0
0
Final Countdown to Global 2013 

Activities  geared up towards the start of today's Global 2013. Briefings were held throughout the day with Dialogue Resource Group Members and  their Tanzanian counterparts. One  of the highlights of the day's events was a much anticipated reunion of Smart 29'ers from eight countries including Tanzania, Uganda and Zambia among others.  Today there will be a live webcast covering the opening ceremony of the Global 2013 Smart Partnership Dialogue, at 17:00 EAT. We are looking forward to welcoming Smart Partners across the globe to the Dialogue, both in person and virtually.

Although some of you can't be with us in Dar es Salaam The Smart Communication Team will make sure you don't miss any of the action. You will be able to catch " As it Happens" live updates through www.cptm.org/Global2013.htm 

WAtanzania washiriki Keene Ndola trade fair 2013

0
0
 Baadhi ya mabanda ya maonesho ya Watanzania katika Keene Ndola Trade Fair 2013 mjini Ndola, Zambia

mkataa kwao mtumwa


miondoko ya kumeremeta kwenye mnuso

sunday shomary wa idhaa ya kiswahili ya VOA atinga Dodoma

TEKNOLOJIA YA TELEPRESENCE YAANZA NCHINI

0
0

Telepresence refers to a set of technologies which allow a person to feel as if they were present, to give the appearance of being present, or to have an effect, via telerobotics, at a place other than their true location. Telepresence requires that the users' senses be provided with such stimuli as to give the feeling of being in that other location. Additionally, users may be given the ability to affect the remote location.
In this case, the user's position, movements, actions, voice, etc. may be sensed, transmitted and duplicated in the remote location to bring about this effect. Therefore information may be traveling in both directions between the user and the remote location. A popular application is found in telepresence videoconferencing, the highest possible level of videotelephony.
Telepresence via video deploys greater technical sophistication and improved fidelity of both sight and sound than in traditional videoconferencing. Technical advancements in mobile collaboration have also extended the capabilities of videoconferencing beyond the boardroom for use with hand-held mobile devices, enabling collaboration independent of location.

For more CLICK HERE

JK AFANYA UKAGUZI WA MWISHO WA MAANDALIZI YA MKUTANO WA SMART PARTNERSHIP UNAOFUNGULIWA LEO JIONI

0
0
 Rais Jakaya Kikwete akiwa katika banda la HUAWEI wanakoonesha teknolojia ya kisasa ya TELEPRESENCE ambayo imeshaanza kutumika nchini
 Rais Kikwete akisalimiana na wadau wa IT wa eDucation
 Akiwa katika banda la Malaysia
 Akikagua sehemu ya kukaa viongozi.

MMOJA KATI YA WASHINDI 5 WA PROMOSHENI YA CHEKA NAO AKABIDHIWA KITITA CHAKE

0
0
Meneja wa Vodacom kanda ya Nyanda za juu kusini Bw. Elisha Tengeni (kulia)akimkabidhi Tsh milioni 2 Mshindi wa droo kubwa ya Promosheni ya Cheka Nao Bw. Isaya Sengo-mkazi wa makunguru Mbeya,ambae ni mshindi ,kati ya washindi 5 waliojishindia shilingi Milioni 2 kila mmoja,baada ya kuzitoa kwenye M PESA alizotumiwa toka makao makuu ya Vodacom kwa ushindi wake kwenye Promosheni hiyo inayowawezesha wateja kuongea na mitandao yote bila mipaka kwa bei nafuu.Ili wateja kujiunga na promosheni hiyo wanatakiwa kupiga *149*01#.

Viewing all 109604 articles
Browse latest View live




Latest Images