Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 175 | 176 | (Page 177) | 178 | 179 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Spika wa Bunge la Oman (Majlis) Mhe. Sheikh Khalid Al Maawal na Ujumbe wake watafanya ziara ya kikazi ya siku sita hapa Nchini kuanzaia kesho Juni 25, 2013 kufuatia mwaliko rasmi wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda uliotolewa kwa niaba yake na Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge walipotembelea Oman Mwezi Februari Mwaka huu.

  Miongoni mwa shughuli zitakazofanyika wakati wa ziara yake hapa Nchini ni uzinduzi rasmi wa Chama cha Urafiki wa Kibunge baina ya Oman na Tanzania (Oman - Tanzania Parliamentary Friendship Group); siku ya tarehe 27 Juni, 2013 katika wa Pius Ukumbi wa Msekwa, Bungeni Dodoma. Hii itakuwa hatua muhimu ya Kuanzisha ushirikiano wa moja kwa moja baina ya Mabunge hayo mawili.

  Spika huyo wa Oman anatarajia kukutana na viongozi mbalimbali wa kitaifa akiwemo Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda, Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda, kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Kamati ya Uongozi ya Bunge na Tume ya Utumishi wa Bunge. Aidha anatarajia kuwa na mazungumzo rasmi na uongozi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam akiwa Dodoma

  Mhe. Sheikh Al Maawal atafanya pia ziara katika Chuo cha Dodoma na kutembelea Jimbo la Kongwa kabla ya kuelekea Arusha ambako atatembelea vivutio vya kitalii vya Ngorongoro na Serengeti. Pamoja na kutembelea vivutio hivyo, Mhe. Sheik Maawal atatembelea pia kisiwa cha Zanzibar ambako atakutana na Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Seif Ali Idd, na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Pandu Ameir Kificho kabla ya kurejea Oman akitokea Zanzibar tarehe 3 Julai, 2013.

  Imetolewa na Idara ya:
  Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa.
  Ofisi ya Bunge
  DODOMA
  25, Juni, 2013

  0 0

  Ambassador Mbelwa Kairuki, Director of the Department of Asia and Australasia in the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation welcomes Ms. Georgina Roberts, Deputy High Commissioner of New Zealand based in Pretoria, South Africa who also covers Tanzania, during their meeting today in Dar es Salaam. 
  Ambassador Mbelwa Kairuki and Ms. Georgina Roberts (left) in a discussion about more areas of cooperation in sectors of agriculture, energy and education. 
  Ms. Georgina Roberts also took time to thank Ambassador Mbelwa Kairuki for taking time to meet, and that her Government was eager to continue working close with Tanzania and explore new areas of cooperation that in turn can generate more experts in areas of technology, energy and agriculture. 
  Also in attendance were Mr. Mkumbwa Ally (left), Acting Head of Government Communication Unit in the Ministry of Foreign Affairs and Mr. Khatibu Makenga, Foreign Service Officer in the Ministry of Foreign Affairs.  
  A group photo of Ambassador Mbelwa Kairuki(2nd right), together with Ms. Georgina Roberts, Deputy High Commissioner of New Zealand, Mr. Mkumbwa Ally (left), Acting Head of Government Communication Unit and Mr. Khatibu Makenga, Foreign Service Officer in the Ministry of Foreign Affairs. All photos by Tagie Daisy Mwakawago of the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation.

  0 0

  Mbunge wa Nkenge, Asumta Mshama (kushoto) akizungumza na Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shellukindo kwenye viwanja vay Buge Mjini Dodoma Juni 25,2013.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Busega, Dr. Titus kamani, Bungeni Mjini Dodoma Juni 25,2013.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 25, 2013.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shellukindo kwenye viwanja vya bunge Mjini Dodoma Juni 25,2013.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na madiwani kutoka jimbo la Chilolo mkoani Iringa kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 25, 2013.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

  UNIVERSAL AUCTION CENTRE Kwa idhini waliyopewa na Ubalozi wa Denmark (SCF Project)  watauza  Magari & Ofisi furniture kwa mnada wa hadhara  tarehe 28 June, 2013 Arusha - Blue plaza building ,ghorofa ya 2 mkabala na Fastjet mtaa wa India, saa 5 asubuhi.  Na Mwanza mnada utafanyika tarehe 29 /06/2013 NSSF building  ghorofa ya kwanza Wing D barabara ya Kenyatta saa 5 asubuhi.

  GARI NA FANICHA ZITAKAZOUZWA  ARUSHA:

  Office desk/Chairs, Chest drawers, Cupboard, Sign Board, File cabinet, Book shelves, Laptop, Computer set, Printer, Na vingine vingi.


  Idadi

  Aina

  Model

  Mwaka

  Ushuru

  1

  Toyota Prado GX

  5L-E Diesel

  2008

  Haujalipwa


  GARI NA FANICHA ZITAKAZOUZWA  MWANZA:

  Office desk/Chairs, Chest drawers, Cupboard, Sign Board, File cabinet,

  Book helves,Refrigerator,  Laptop, Computer set, Printer, A/c split units nk.


  Idadi

  Aina

  Model

  Mwaka

  Ushuru

  1

  Toyota Prado GX

  5L  Diesel

  2008

  Haujalipwa

  Mali zote zinaweza kukaguliwa Arusha na Mwanza,  tarehe 27 mpaka 28 June,  2013 kuanzia saa 4.00. asubuhi mpaka saa 10.00 jioni.


  MASHARTI YA MNADA:

  1. Mnunuzi  wa fanicha atatakiwa kulipa malipo yote pale pale. Na mnunuzi wa gari atatakiwa kulipa 25% pale pale na salio lilipwe ndani ya siku 14, ukishindwa kulipa kwa muda huu gari litauzwa tena na dhamana haitarudishwa.
  2. Mali zote zitauzwa kama zilivyo.
  3. Mnunuzi atawajibika kulipa ushuru.
  4. Mali yote iliyouzwa itatakiwa kuondolewa siku hiyo hiyo  baada ya kulipia malipo yote pamoja na ushuru.
  5. Kwa maelezo zaidi waone:UNIVERSAL AUCTION CENTRE, NKRUMAH STREET MKABALA NA CO-CABS SIMU NA: 2128027 ; 0754-284 926  DAR ES SALAAM  0 0

  Imeandikwa kwa ushirikiano wa Urban Pulse na Freddy Macha

  Mara ya mwisho Tanzania kusikika kimataifa michezoni ilikuwa 1980 wakimbiaji Filbert Bayi na Suleiman Nyambui walipotwaa medali za Olimpiki, Moscow na timu yetu ya taifa ya mpira iliposhiriki fainali za kombe la Afrika mjini Lagos , Nigeria...
  kids playing football at Academy of Light-oic by Urban PulseWatoto wadogo wakisakata gozi Academy of Light. Samaki mkunje angali mbichi... Kiu ya miaka 30 imezungumziwa na kujadiliwa sana hatimaye tumeanza kuzoea kushangilia wengine. Tumezoea mtazamo huu kiasi ambacho ni rahisi kwa shabiki wa Kitanzania kuijua timu nzima ya wachezaji wa Manchester United au Barcelona kuliko Yanga na Simba. Kati ya sababu kuu za kushindwa huku kila mwaka ni kutowekezea katika matayarisho na kutochangamkia tulicho nacho. Wenzetu wa Hispania, Brazil, Uingereza, Nigeria, Ivory Coast, Kenya nk wanatuzidi moja. Wanajipenda. 
  Ramani ya chuo kitakachojengwa Dar es Salaam 
    Rais akionyeshwa ramani ya mpango wa chuo cha mpira kitakachojengwa Dar es Salaam. Sisi (kama hawa wenzetu) tunao wachezaji wenye vipaji. Tunao pia uchungu kwa nchi yetu; na kama alivyosema Rais Jakaya Kikwete alipoitembelea klabu ya Sunderland AFC Jumapili 16 , Juni, “Watanzania tunapenda michezo.”

  Mheshimiwa Rais mwenyewe, aliwaeleza wanahabari waliomhoji kwamba zamani alikuwa mchezaji wa mpira wa kikapu. Ni vizuri kuwa na kiongozi mpenda michezo. Na mwaliko Rais aliopewa na mwenyekiti wa klabu ya Sunderland AFC , Ellis Short umeotesha si tu mbegu ; sharti tuanze kuchangamkia tulicho nacho. Mpenda kwao hutunzwa. Jamani, eh, tuichangamkie dili. Dili yenyewe ni ipi?Ramani ya Mpango wa chuo kitakachojengwa Dar es Salaam 
    Rais Kikwete akitembezwa viwanja vya Academy of Light. Mkono wake wa kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara klabu ya Sunderland AFC, Gary Hutchinson na kulia kwake, Profesa Anna Tubaijuka, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Rais na msafara wake uliomhusisha pia Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara, walielezwa kuwa kampuni ya kimataifa ya umeme –Symbion Power- itaanza mara moja kujenga chuo (Sports Academy) cha kufundishia mpira jijini Dar es Salaam. Afisa Mkuu wa Symbion, Bw. Paul Hinks alisema punde ujenzi utakapomalizika, Sunderland AFC itaanza utaalamu na uzoefu wake kwa kutoa mafunzo ya mchezo huu unaopendwa Tanzania. Kazi hii ina hatua mbili. Ya kwanza Dar es Salaam, ya pili, kujenga na kuendeleza mpira Tanzania ili kuufikisha hatua ya juu, aliahidi Hinks.


  0 0
 • 06/26/13--22:08: IN MEMORIAM
 • A MEMORIAL MASS TO CELEBRATE THE LIVES OF OUR LOVING PARENTS, MR & MRS NGALAWA, WILL BE HELD AT KYELA ANGLICAN CHURCH ON FRIDAY, 5 JULY 2013. YOU ARE ALL INVITED.

  MOM & DAD, YOU ARE SORELY MISSED BY YOUR DAUGHTERS, SONS, RELATIVES, NEIGHBORS, AND FRIENDS. WE WILL FOREVER REMEMBER YOU BOTH. MAY YOUR SOULS CONTINUE TO REST IN PEACE!

  0 0

  Nelson Mandela is on life support, according to a South African tribal chief.

  In South Africa's Eastern Cape province, where Mandela grew up, a traditional leader said the time was near for Mandela, who is also known by his clan name, Madiba.

  'I am of the view that if Madiba is no longer enjoying life, and is on life support systems, and is not appreciating what is happening around him, I think the good Lord should take the decision to put him out of his suffering,' said the tribal chief, Phathekile Holomisa.

  'I did speak to two of his family members, and of course, they are in a lot of pain, and wish that a miracle might happen, that he recovers again, and he becomes his old self again,' he said.
  'But at the same time they are aware there is a limit to what miracles you can have.'

  A South African newspaper has also reported the anti-Apartheid icon is on life support, citing numerous sources close to the family.

  The Citizen newspaper says Mandela has a team of doctors supporting him at a Pretoria hospital.

  One source was quoted as saying that Mr Mandela's family had the option to switch off the ventilator.

  South African President Jacob Zuma cancelled a trip to neighbouring Mozambique, intensifying speculation about the deterioration of Mandela's life. 

  Zuma made his decision not to leave the country after visiting the 94-year-old late yesterday in the Pretoria hospital where he has been receiving treatment for a lung infection for nearly three weeks.

  'Clearly the issue of seriousness has been such that President Jacob Zuma has cancelled his trip,' presidential spokesman Mac Maharaj told Talk Radio 702.

  He declined to comment on reports that Mandela was on life support, saying: 'I cannot confirm any clinical details.'


  Read more: http://www.dailymail.co.uk/news/article-2348862/Nelson-Mandela-life-support-family-option-switch-claim-South-African-sources.html#ixzz2XOIM7XQF 

  0 0

  UONGOZI WA MAHAKAMA YA TANZANIA UNAPENDA KUWAJULISHA WADAU WA SHERIA NA WANANCHI WOTE KWA UJUMLA KUWA, MAHAKAMA NI MOJA KATI YA WASHIRIKI KATIKA MAONYESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA ALMAARUFU KAMA ‘SABASABA.’

  KATIKA MAONYESHO HAYA MAHAKAMA YA TANZANIA INAKUSUDIA KUTOA ELIMU JUU YA TARATIBU MBALIMBALI ZA KIMAHAKAMA, PAMOJA NA KUSIKILIZA NA KUTOLEA SULUHISHO MALALAMIKO YA WANANCHI WATAKAOPATA FURSA YA KUTEMBELEA BANDA LA MAHAKAMA.

  HUDUMA HIZO ZINATOLEWA KWENYE BANDA LA MAHAKAMA, LINALOPATIKANA KATIKA UKUMBI WA BENJAMIN MKAPA ULIOPO NDANI YA VIWANJA VYA SABASABA.

  NJOO UPATE ELIMU YA SHERIA PAMOJA NA KUTOA MAONI YAKO WEWE MWANANCHI ILI KUBORESHA HUDUMA YA UTOAJI HAKI NCHINI. 

   WOTE MNAKARIBISHWA.

  IMETOLEWA NA:

  KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO,
  MAHAKAMA YA RUFANI (T).

  0 0

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi. 
   Mkaazi wa majengo mjini Moshi aliyefahamika kwa jina la Frank Ngowi usiku wa kuamkia leo amaenusurika kifo baada ya kugongwa na gari aina ya Hiace (daladala) lenye namba za usajili T352 AFM ikifanya safari zake kati ya Kiboriloni na katikati ya mji wa Moshi.
  Ajali hiyo imetokea jana majira ya saa 3 usiku eneo la majengo polisi jirani kabisa na zahanati ya Kishamba. Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo walisema kuwa dereva wa daladala hiyo ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja alionekana amelewakupita kiasi. 
   Mashuhuda walidai dereva huyo baada ya kugundua amesababisha ajali alikimbia na kuelekea maeneo ya majengo sekondari ambapo waendesha bodaboda walimkimbiza na kufanikiwa kumkamata na kumrudisha mpaka kwenye eneo la ajali. 
   Askari polisi walifanikiwa kufika eneo la tukio na kumchukua dereva wa gari hilo pamoja na majeruhi kwa ajili ya hatua za awali.
   Huu ndio usafiri aliokuwa akiutumia Bw Ngowi.
   Hii ndio daladala iliyosababisha ajali na dereva wake akakimbia. Hata hivyo jitihada zilifanyika na kufanikiwa kukamatwa na kurudishwa katika eneo la ajali..
   Majeruhi wa ajali Frank Ngowi aliyegongwa na daladala wakati akiendesha baiskeli akionesha majeraha baada ya kupata ajali.
   Askari polisi wanawasili eneo la tukio 

  Baada ya dereva wa Hiace kukimbia vijana walimkimbiza na kumrudisha kwenye eneo la ajali. Picha na Dixon Busagaga

  0 0

   Wapita njia na abiria wa treni ya Mwakyembe wakiwa wamekwama kwa muda asubuhi hii Tabata Relini jijini Dar es salaam leo kabla ya mafundi kurekebishwa mambo na safari kuelekea mjini kuendelea
   Hakuna kwenda 


  0 0
 • 06/26/13--22:33: Article 17


 • 0 0
 • 06/26/13--23:00: mkataa kwao mtumwa

 • 0 0

  Bondia wa Ngumi Za Kulipwa wa Tanzania Francis Cheka atazichapa Na Bondia wa Marekani Derrick Findley katika Kuwania taji la Ubingwa wa Dunia Uzito wa Kati wa Shirikisho la Ngumi Duniani.
  Pambano Hilo la kusisimua limepangwa kufanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam tarehe 30 Mwezi wa Nane. 
  Pia kutakuwa na Pambano lingine la utangulizi la kugombea ubingwa wa Afrika uzito wa kati (WBF super middle weight African title) Kati ya mabondia wenye upinzani mkali nchini Tanzania ,Mada Maugo vs Thomas Mashari. Lady Jayde(Binti Machozi) atatumbuiza live. Katika usiku huo utaokuwa wa aina yake.


  0 0

  Sasa tunaamini unafahamu kuwa Night of the Legends aka usiku wa malegendari isumba lounge zamani jollies club ndiyo gumzo mjini. Sasa basi the magic continues, this friday kama kawaida melegendari tunakutana tunapata oldies, old scul kali, raga, soca rumba, chacha na nyingine nyingi. J'mosi hii kama kawaida moto unaendelea, ma gentleman 50 wataofika kabla ya saa 6 usiku watapata vol mpya kabisa The Legend is Back Nonstop cd, wadada 50 kupata a very cold glass of wine mlangoni. Entry 10k, doors open 9pm. Karibu"
  DJ JD in action...

  0 0

  DSC03460Dr. Mary Mwanjelwa mbunge wa Mbeya (viti maalum) mgeni rasmi katika wa mkutano wa Je Nifanyeje ulioandaliwa na VOA kwa ushirikiano na USAID akifungua rasmi mkutano huo wa vijana katika ukumbi wa African Dreamer Dodoma Jumatano. DSC03455Katika meza kuu kutoka kushoto ni Mariam Salum Msahaba (Zanzbar), Josephine Johnson Genzabuke (Kigoma),Ritta Motto Kabati (Iringa), Faida Mohamed Bakari (Kusini Pemba) IMG_2784Washiriki wa "Town Hall meeting". IMG_2770Washiriki wakifuatilia mkutano. IMG_2777Washiriki wakiwa na mgeni rasmi. IMG_2788Mshiriki Sebastian ambaye ni mwanafunzi wa CBE akitoa pointi. IMG_2776Washiriki wa mkutano huo kushoto Panelist Dr.Ilyu Mohamed na Advocate Jp mshauri wa EABTM. IMG_2778Kutoka kushoto Mariam Salum Msahaba (Zanzbar),Faida Mohamed Bakari (Kusini Pemba),Dr. Mary Mwanjelwa Mbeya, Rose Mwakitwange,Ritta Motto Kabati (Iringa) na Rais wa wanafunzi wa CBE Dodoma. Nikitoa saini kwa washiriki wa semina. IMG_2805Timu ya Je Nifanyeje Tanzania kutoka kushoto Adeodatus Kakorozya, Mwanaharusi Pongwa na Mensiah . IMG_2790Washiriki wa mkutano wakiwa kwenye majadiliano. IMG_2799Wasaa wa kung'aa na baadhi ya washiriki wa mkutano wanafunzi wa CBE Dodoma. Kwa picha zaidi bofya
  IMG_2798IMG_2816

  0 0


  WANACHAMA wa chama cha mapinduzi Kata ya mipingo Kijiji cha Matapwa wilaya Lindi Jimbo la mchinga wakicheza kwa furaha baada kuwapokea wanachama zaidi ya 120 waliohama chama cha wananchi cuf na kujiunga na chama hicho tukio limesababisha tawi la chama cha wananchi kubaki na mwenyekiti na katibu wake.
  Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Lindi Alli Mtopa akimkabidhi kadi ya CCM miongoni mwa wanachama 120 wa kijiji cha Matapwa jimbo la mchinga hadija Saidi aliyehama chama cha wananchi cuf na kujiunga na chama hicho.
  Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Lindi Alli Mohamed Mtopa akimkabidhi kadi ya CCM Fatuma hamisi mkazi wa kijiji cha Matapwa jimbo la mchinga aliyeyehama chama cha wananchi cuf na kujiunga na chama hicho.

  Na Abdulaziz video

  WANACHAMA wa chama cha wananchi (Cuf ) tawi la Matapwa Jimbo la Mchinga wamekiama chama hicho na kuamia chama cha mapinduzi huku wakiliacha tawi ili likibaki na wanachama wawili akiwemo mwenyekiti na katibu yake.

  Tukio hilo limetokea jana kwenye mkutano wa adhara uliitishwa na mbunge wa jimbo la mchinga saidi mtanda wakati alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika jimbo.

  Akizungumza kabla ya kugawa kadi kwa wanachama zaidi ya 120 wa tawi hilo lililokuwa ngome ya cuf katika jimbo Hilo la Mchinga kiongozi mwandamizi wa chama cha mapinduzi taifa Tambwe Hiza aliwataka wananchi wa kata hiyo kuachana na siasa za kichochezi zinazo sababisha uvunjifu wa amani badala yake wafanye kazi za kujiletea maendeleo yao.

  Tambwe alisema hakuna chama kinachotawala duniani ambacho kinagawa fedha kwa wananchi wake kwa ajili ya kuendesha maisha yao ya kila siku bali ilani, na sera mzuri kama za ccm ndizo zinawafanya wananchi wao kuwa na maendeleo ikiwemo upataji wa huduma muhimu za kijamii kama vile. Maji, elimu, miundombinu pamoja na huduma za Afya.

  Aidha Tambwe aliwaomba wananachi wa jimbo hilo ambao hawajajiunga na chama hicho kujiunga haraka na kuachana vyama vyenye itikadi za kibaguzi, kidini na kueleza kuwa chama Ccm ndicho chama pekee nchini chenye sera mzuri na mwelekeo wa kuwaletea maendeleo wananchi yake.

  0 0


  Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki, akikagua timu wakati wa uzinduzi wa michuano ya Airtel Rising Stars katika mkoa wa kisoka wa Temeke ambapo Faru Boys football ilichuana na timu ya Mapambano katika mechi ya ufunguzi.
  Beki wa timu ya Faru Boys Nassoro Dibagula (kushoto) akitoa mpira katika eneo la hatari mbele ya Abdalah Juma wa Mapambano katika mechi ya ufunguzi wa michuanoa ya vijana wenye umri chini ya miaka17 ya Airtel Rising Star,. Mkoa wa Temeke, uliofanyika kwenye uwanja wa Twalipo jijini Dar es Salaam Juni 25, 2013. Faru Boys ilishinda 1-0.

  Timu ya Mbaspo Academy ilifanya mauaji juzi Jumanne kwa kubamiza bila huruma timu ya Mbeya Sekondari 6-0 katika mashindano yanayoendelea ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa. Mechi hiyo ilichezwa kwenye kiwanja cha Magereza mkoani Mbeya.

  Washindi walifungua kitabu chao cha magoli katika dakika ya sita kupitia kwa mshambuliaji wao mahili Jackson Mwaibale aliyefunga magoli manne peke yake. Mshambuliaji huyo kinda aliifungikia tena timu yake magoli matatu katika dakika za 16, 20 na 74. Wanafunzi wa shule ya sekondari Mbeya waliokuja kushangilia timu yao walijikuta kwenye hali ya kukata tamaa baada ya timu yao kuwanyong’onyesha na wapinzani wao Mbaspo.

  Peter Noah, mshambuliaji mwingine hatari wa timu ya Mbaspo, aliifungia tena timu yake katika dakika ya 30. Alikua ni yeye tena katika dakika ya 68 alipoitimisha kalamu ya magoli baada ya kuwapita walinzi wa Mbeya Sekondari na kumuacha golikipa akiduwaa baada mpira kutinga wavuni.

  Kwa upande mwingine timu ya Faru Boys football walipata ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya wapinzania wao Mapambano katika mechi ya ufunguzi ya ARS, katika mkoa wa Temeke uliofanyika katika uwanja wa Twalipo jumanne jioni jijini Dar es Salaam.

  Timu zote zilianza mchezo kwa kasi na babada ya kosa kosa za hapa na pale hatimaye Yohana Joseph ilifanikiwa kuitoa kimasomaso timu yake alipounganisha krosi kutoka upande wa kushoto ambayo iliingia moja kwa moja wavuni. Goli hili lilipokelewa kwa furaha na washabiki wa Faru.

  Mchezo mwingine wa Another Airtel Rising Stars, mkoa wa Ilala, ilichezwa kwenye kiwanja cha soka cha shule ya sekondari ya Benjamin William Mkapa ambapo timu ya Amana Shooting ilishinda 2-0 dhidi ya Msimamo Youth Academy. Magoli hayo yalipatikana kupitia kwa Isiaka Mohamed dakika ya 22 na Ally Shaban dakika ya 68.

  Mkoa wa Mwanza ulitarajia kuzindua mechi zake za ARS ngazi ya mkoa leo, Juni 26 wakati Morogoro na Mbeya walitarajiwa kuendeleza na mechi za mashindano hayo leo, Juni 26, 2013.

  Wakati huo huo, mkoa wa kisoka wa Kinondoni umetangaza kombaini yao ya wachezaji 15 watakaowakilisha mkoa huo kwenye mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa yatakayofanyika wenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 2 hadi 7.

  Wachezaji hao ni Hamza Mohamed, Hamza Abdallah, Twalib Athuman, Fred Bakari, Hazzad Jumanne, Salim James, Abubakary Mohamed, Willy Kalolo, Didas Proches, Mustafa Yusuf, Rashid Khalifan, James Msuva, Isiaka Lukana, Ally Amin na Shabani Idd.

  0 0

  Vimwana wa Redd's Miss Temeke 2013,wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa kutangaza kuanza kwa kambi yao pamoja na Mazoezi katika Ukumbu wa TCC,Chang'ombe jijini Dar.Shindano la Redd's Miss Temeke 2013,linatarajiwa kufanyika Julai 5,2013 kwenye Ukumbi wa TCC,Chang'ombe jijini Dar es Salaam.Jumla ya Warembo 15 watachuana siku hiyo.

  0 0
 • 06/27/13--02:11: MAPITIO YA MAGAZETI LEO

 • 0 0


older | 1 | .... | 175 | 176 | (Page 177) | 178 | 179 | .... | 3272 | newer