Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109594 articles
Browse latest View live

NSSF YAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI BILIONI 1.5 UPANUZI WA KIWANDA CHA CHAKI SIMIYU

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama(kulia) akimkabidhi hundi ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt.Fredrick Sagamiko.

Na Stella Kalinga, Simiyu

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umekabidhi hundi ya shilingi bilioni 1.5 kwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu, fedha ambazo ni mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha Chaki Wilayani humo na kuongeza uzalishaji.

Hundi hiyo imekabidhiwa kwa Waziri wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama kwa niaba ya Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof.Godius Kahyarara wilayani Maswa mkoani Simiyu.


Akizungumza wakati wa makabidhiano ya hundi hiyo Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof.Godius Kahyarara amepongeza Mkoa wa Simiyu kwa kutekeleza Sera ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda kwa vitendo na kuwataka viongozi wa mkoa huo kutokatishwa tamaa.

Amesema NSSF kama Shirika la Umma linatekeleza sera na maelekezo ya Serikali na wametoa mkopo huo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ili wafanye upanuzi wa kiwanda cha chaki na kuongeza uzalshaji kwa kuwa suala la Viwanda ni la kipaumbele.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof.Godius Kahyarara(kushoto) akimkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama hundi ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa, (kulia) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka.

Waziri wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama amesema kiwanda cha Chaki Maswa kimebeba ujumbe na dhana ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli ya kushikamanisha Uchumi wa Viwanda na Maendeleo ya watu kwa sababu kinatumia malighafi ya hapa nchini.

Aidha, amesema kiwanda hiki kitawanufaisha Watanzania hususani vijana wa Mkoa wa Simiyu ambao watafanya kazi moja moja katika kiwanda na wale wataohusika katika uchimbaji wa malighafi ambayo inapatikana maeneo mengine hapa nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akipokea taarifa ya Upembuzi yakinifu wa panuzi wa kiwanda cha chaki cha Maswa kutoka kwa mtalaam wa Taasisi ya Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF), Deodatus Sagamiko.

“Asilimia 56 ya nguvukazi hapa Tanzania ni vijana na vijana wengi bado hawana ajira lakini kiwanda hiki kitasaidia, kwa kuwa sehemu ya hiyo asilimia 56 wataajiriwa katika kiwanda na wengine watapata ajira huko mkoani Singida ambako malighafi ya kutengenezea chaki inapatikana” amesema.


JUKWAA LA WANAWAKE KIUCHUMI

TANTRADE YAWAKARIBISHA KATIKA MAONYESHO YA 41 YA BIASHAYA YA KIMATAIFA JIJINI DAR

MAGAZETI YA JUMAPILI LEO JUNE 25,2017

MAFUNZO YA SIKU TANO KWA MADAKTARI YALIYOANDALIWA NA WCF YAFUNGWA JIJINI DAR ES SALAAM

0
0

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MAFUNZO ya siku tano kwa madaktari yaliyoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), ili kuwajengea uelewa wa namna ya kufanya tathmini ya ugonjwa na ajali kwa mfanyakazi aliyepata madhara mahala pa kazi yamemalizika kwa washiriki kutunukiwwa vyeti.
Mafunzo hayo yaliyofunhga na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba makao makuu ya Mfuko huo, jingo la GEPF barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam, Juni 23, 2017, yaliwaleta pamoja madaktari 70 kutoka hospitali mbalimbali za umma na binafsi jijini Dar es Salaam.
Mafunzo hayo yaliyogusa maeneo mbalimbali pia yaliwawezesha madaktari hao kujifunza Muongozo mpya unaohusu namna ya kufanya tahmini kabla ya kumlipa fidia stahiki Mfanyakazi aliepata madhara mahala pa kazi.
Akizungumza kwenye ufungaji wa mafunzo hayo,  Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw  Masha Mshomba, alisema kuwa  ni iani ya Mfuko kuwa Madaktari hao wamefaifika na mafunzo hayo na yatawezesha ufanisi katika kjutoa huduma hizo kwa wafanyakazi waliopata magonjwa au kuumia wakati wakiwa kazini.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akimkabidhiDkt.Kezia, cheti cha ushiriki wa mafunzo ya tathmini ya ajali na majeraha kwa mfanyakazi aliyeumia wakati akitekeleza majukumu yake mahala pa kazi,  wakati wa kilele cha mafunzo ya siku tano kwa madaktari kutoka hospitali za umma na binafsi za jijini Dar es Salaam. Jumla ya madaktari 70 kutoka hospitali 35 walishiriki.
 Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge, (kulia),  akifuatilia kwa makini hafla hiyo ya ufungaji wa mafunzo kwa wataalamu hao wa afya. 

Miss Tanzania-USA 2017: Venue Announcement

HOTUBA YA RAIS DKT. MAGUFULI KATIKA UZINDUZI WA BARABARA YA MSATA-BAGAMOYO

PSPF YAWATAKIA KHERI YA SIKUKUU YA EID KWA WANACHAMA WAKE NA WATANZANIA WOTE


SHEIKH MKUU, MUFT WA TANZANIA SHEIKH ABUBAKARY BIN ZUBERY ASHIRIKI FUTARI MJINI MOSHI

0
0
Waumini wa Dini ya Kiislamu wakichukua Chakula wakati wa hafla fupi ya Futari iliyoandaliwa na Benki ya Azania na kufanyika ofisi za Bakwata mkoa wa Kilimanjaro.
Sheikh Mkuu Mufti waTanzania, Sheikh Abubakary Bin Zubery akishiriki Futari katika Ofisi za Bakwata mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, jana. 
Sheikh Mkuu Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubery akiwa na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Biashara wa Benki ya Azania, Jackson Lohay wakati wa Futari iliyoandaliwa na Benki hiyo katika Ofisi za Bakwata mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

WAKULIMA WA TANGAWIZI RUVUMA NA TANGA NEEMA YA WANYEMELEA

0
0
Mbunge wa Jimbo la Madaba Mkoani Ruvuma Joseph Mhagama na Mbunge wa Jimbo la Mlalo Mkoani Tanga Mh. Rashidi Shangazi , wazungumzia jitihada wanazozifanya za kuwakwamua wakulima wa zao la Tangawizi.

YALE YALE

Exim Bank Tanzania yafuturisha Wateja Wake Mikoa Mbali Mbali

0
0
 Wateja wa benki ya Exim waliopo Mtwara wakipata futari iliyoandaliwa na benki hiyo katika hoteli ya Tiffany Hotel jana.
 Wateja wa benki ya Exim waliopo Mtwara wakipata futari iliyoandaliwa na benki hiyo katika hoteli ya Tiffany Hotel jana.
 Wateja wa benki ya Exim waliopo Zanzibar wakipata futari iliyoandaliwa na benki hiyo katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort juzi.
 3A2ZSWSAQMeneja mwandamizi wa Exim Bank tawi la Zanzibar, Fred Umiro akizungumza na wateja wa benki hiyo baada ya futari maalum iliyoandaliwa na Exim Bank kwa wateja wao wa Zanzibar iliyofanyika katika hotel ya Zanzibar Beach Resort .

Jiji la Mwanza yatumia Tehama Kuboresha utoaji wa huduma kwa umma

SALA YA EID EL FITR DMV LEO

0
0
Polisi akielekeza Magari sehemu ya maegesho siku ya Jumampili June 25, 2017 siku Waislaam Watanzania wa DMV walipojumuika pamoja na Waislam wenzao kwenye sala ya Eiid el Fitri iliyofanyika kwenye musikiti wa Muslim Community Center uliopo mtaa wa New Hampshire Slver Spring, Maryland.
Watanzania Waislam DMV wakijumuika pamoja na Waislam wenzao DMV kwenye sala ya Eiid el Fitri iliyofanyika kwenye muikiti wa Muslim Community Center uliopo mtaa wa New Hampshire Slver Spring, Maryland.
Watanzania Waislam DMV wakijumuika pamoja na Waislam wenzao DMV kwenye sala ya Eiid el Fitri iliyofanyika kwenye muikiti wa Muslim Community Center uliopo mtaa wa New Hampshire Slver Spring, Maryland.
Sala ya Eid el Fitr ikiendelea.

“MBUNGE MUSSA AWATAKIA WANANCHI WA JIMBO LAKE KUONGEZA UZALISHAJI”

0
0
MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku amewataka wananchi heri ya sikukuu ya Eid El Fitri huku akiwataka kujiandaa na ujio wa fursa ya mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga kwa kuongeza uzalishaji. 

Alhaji Mussa aliyasea hayo wakati akizungumza na mtandano huu ambapo alisema mradi huo ni mkubwa ambao utahusisha watu wengi hivyo wananchi wanapaswa kujipanga ili kuweza kuendana na fursa hiyo muhimu kwa ajili ya kujiongezea kipato halisi.

Alisema lazima wakazi wa mkoa huo watambue kuwa wakati mradi huo ni mkubwa ambao unaweza kuchangia ukuaji wa kipato chao hivyo wajiandae kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo mama ntilie waweze kuendesha shughuli zao kisasa.

“Mkoa wa Tanga hasa kwenye Jimbo langu la Tanga mjini kutatekelezwa mradi mkubwa wa mradi wa boma la mafuta ghafi kutoka hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga hiyo wananchi wangu wajiandae kwa kuongeza uwajibika na uzalishaji ambao utakuwa na tija kwao “Alisema.

“Lakini pia niwaambie wenzetu madereva wa tax, mafundi wajiandae kikamilifu kuona namna ya kuboresha huduma zao kwani ujio wa mradi huo utalifanya Jiji la Tanga kuwa na watu wengi kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi ili kuweza kupata mafanikio “Alisema.

Aidha pia mbunge huyo aliwataka waumini ya dini ya kislaam kuendelea kutenda mema hata baada ya kumalizika mwezi mtukufu wa ramadhani ikiwemo kuwajali wengine.

Mbunge huyo pia aliwataka wananchi wa Jimbo hilo kuhakikisha wana sheherekea vema sikukuu ya Iddi Salama kwa kuwa makini hasa wakati watoto wao wanapokwenda kutembelea wawe na wasaidizi.


Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka wazidi kushika kasi jijini Dar es salaam

0
0

Na Mathew Kwembe

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Mhandisi Ronald Rwakatare ameeleza kuwa mradi huo umepata mafanikio makubwa katika kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es salaam hususani katika barabara ya Morogoro.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea kituo kikuu cha Kimara mwisho ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma, Mhandisi Rwakatare alisema kuwa katika kipindi hicho cha mpito, Mabasi yaendayo haraka yameweza kusafirisha watu 200,000 kila siku kutoka watu 50,000 iliyokuwa ikisafirisha mwaka jana, wakati mradi unaanza.

Mhandisi Rwakatare alieleza kuwa Mradi huo umeweza kuokoa muda wa wananchi ambao kabla ya mradi kuanza walikuwa wakitumia usafiri mwingine uliokuwa ukichukua kutoka masaa mawili, wakati sasa wanatumia dakika 45 tu kwa safari ya kutoka Kimara hadi Posta kwa kutumia mabasi yaendayo haraka.

Alifafanua kuwa huduma hiyo mbali na kuwapunguzia mzigo wa nauli watumiaji wa kawaida wa mabasi ya daladala, mradi wa mabasi yaendayo haraka imeokoa gharama ya usafiri kwa wenye magari binafsi ambapo wengi wao wamekuwa wakiutumia zaidi usafiri huo.

Akizungumzia kuhusu maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma Mhandisi Rwakatare alisema kwa wakala umeona ni vyema kutumia maadhimisho hayo kusikiliza kero na maoni ya wananchi hasa watumiaji wa huduma hiyo ili kuona namna nzuri ya kuiboresha.

“Watumishi wa Wakala wa Mabasi yaendayo haraka wamekuwepo katika vituo vya Gerezani na Kimara mwisho kwa siku hizi mbili ili kusikiliza kero na maoni kutoka kwa wananchi wetu, na tunafurahi kuona huduma hii ikizidi kushika kasi, hasa kwa kuzingatia kuwa tupo katika kipindi cha mpito,” alisema.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Mhandisi Ronald Rwakatare akiwasili katika Kituo Kikuu cha Mabasi Yaendayo Haraka cha Kimara Mwisho. Mhandisi Rwakatare alipokewa na Kaimu Meneja Usafirishaji wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dkt Philemon Mzee (kushoto).
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Mhandisi Ronald Rwakatare akipita sehemu ya ukaguzi wa tiketi na kadi zitumiwazo na Mabasi Yaendayo Haraka. Mhandisi Rwakatare alipata fursa ya kutembelea vitengo mbalimbali vya Kituo Kikuu cha Kimara mwisho na kujionea huduma za usafiri zinavyofanyika katika kituo hicho.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Mhandisi Ronald Rwakatare akizungumza na mmoja wa abiria wa Mabasi yaendayo haraka katika Kituo Kikuu cha Mabasi hayo katika eneo la Kimara Mwisho.
Sehemu ya daraja linalotumiwa na wananchi pindi wanapoingia na kutoka katika Kituo Kikuu cha Mabasi Yaendayo Haraka kilichopo Kimara Mwisho. Daraja hili ni miongoni mwa miundombinu iliyojengwa na Serikali kwa ushirikiano na Benki ya Dunia.



DC MTATURU AWAASA WAISLAMU KUENDELEZA TABIA NJEMA

0
0
MKUU wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida Miraji Mtaturu amewafuturisha waislamu wa wilaya hiyo huku akiwaasa kuendeleza tabia njema kwa mujibu wa kitabu cha Mwenyezi Mungu Quran hata baada ya mwezi Mtukufu wa Ramadhan kumalizika.

Akizungumza na waislamu hao baada ya kupata futuru wilayani humo Mtaturu alisema katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan watu wametenda mema yanayopaswa kuendeleza hata baada ya mwezi huo.

“Wakati tupo kwenye mfungo huu tupo kwenye darasa la tabia njema hivyo nawashauri hata baada ya mfungo huu tuyaendeleze,”alisema Mtaturu.Alisema serikali inafarijika pale inapoona wananchi wake wakifuata imani za dini zao na hivyo kuwa raia wema na nchi kuendelea kuwa na amani.

“Tunamaliza kukamilisha moja ya nguzo tano za uislamu panapo majaaliwa ya Mwenyezi Mungu,nawaombeni isiwe mwisho wa kufanya mema bali iwe ni mwendelezo katika siku zetu zote za maisha yetu,”alisisitiza Mtaturu.Mtaturu aliwatakia maandalizi mema ya sikukuu ya Eid El Fitri huku akiwaasa kusherehekea kwa amani,utulivu na upendo na kukumbuka kutoa Zaka kwa watu wasio na uwezo.

Alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumuombea Rais Dokta John Magufuli kutokana na kazi kubwa anayoifanya katika kuendeleza dhamira yake ya kulinda rasilimali za nchi ili ziwanufaishe watanzania wote hasa wale wanyonge.

Kwa upande wake Sheikh wa wilaya hiyo Abdi Seleman akitoa neno la shukrani alimshukuru mkuu wa wilaya huyo kwa kuwafuturisha na kusema hiyo ni mara ya kwanza toka wilaya hiyo ianzishwe kwa mkuu wa wilaya kuwaalika futari.

“Kwa sadaka yako hii kwetu tunamuomba Mwenyezi Mungu akulipe kila la kheri,na inshallah huu usiwe mwisho bali uwe mwanzo wa kufanya hivi,”alisema Sheikh Seleman.

Nae Kadhi wa mkoa wa Singida Ramadhan Kaoja alimshukuru mkuu wa wilaya huyo na kusema hiyo ni dalili za kiongozi bora kwa kuwa karibu na jamii lakini pia ni sehemu ya kukamilisha imani yake ambapo kwa mwezi huu wa Ramadhan kwa kufuturisha anapata thawabu nyingi sana.

SALAAM ZA EID KUTOKA KWA SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

ZIWA KITANGILI LAFUNGWA KWA MWAKA MMOJA KULINDA UOTO WA ASILI

0
0
KAMATI za ulinzi na usalama za wilaya za Igunga,Meatu,Kishapau pamoja na Iramba zimelifunga ziwa kitangili kwa muda wa mwaka mmoja kuanzia julai,01,mwaka huu hadi Julai,01,2018 ili kulinusuru ziwa hilo lisitoweke,kulinda raslimali zilizopo na kulinda uoto wa asili ili uweze kurejea kutokana na uvuvi haramu unaoendelea katika ziwa hilo.


Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Iramba,Emmanueli Luhahula alitoa kauli hiyo kwenye mkutano wa baraza la Kawaida la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo,uliopo mjini Kiomboi.

“Lakini pia Mwenyekiti nieleze suala la ziwa Kitangili ni mwendelezo ule ule wa Mkoa wetu kuwa jangwa na sisi tuliokabidhiwa wilaya tumefanya kikao cha kamati za ulinzi na usalama wilaya nne,wilaya ya Igunga,Meatu,Kishapu na Iraamba ambao wote tunafaidika na ziwa Kitangili”alifafanua Mwenyekiti huyo.

“Utakumbuka wewe mwenyewe Mwenyekiti ulifadhili kamati hii kwenda kujadili mara ya kwanza tukiwa na baadhi ya madiwani,lakini baadaye tulikubaliana kuu zenyewe zinazosimamia ulinzi tukakutane”alisisitiza Luhahula.

Kwa mujibu wa Luhahula baada ya kukutana Mkoani Shinyanga kutokana na hali halisi ya ziwa kitangili na kutokana na tathimini ya wataalamu iliyoletwa kuhusu ziwa hilo ikieleza kwamba likiachwa jinsi lilivyo kwa kipindi cha miaka kumi ziwa hilo litakuwa limetoweka.
Baadhi ya wakuu wa idara wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo wakati wa mkutano wa kawaida wa baraza la madiwani uliofanyika mjini Kiomboi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba,Mkoani Singida,Simon Tyosela(wa kwanza kutoka kulia) akiongoza mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya hiyo.(Picha zote Na.Jumbe Ismailly).

Article 6

Viewing all 109594 articles
Browse latest View live




Latest Images