Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109595 articles
Browse latest View live

MICHUZI TV: ALLY MAYAI TEMBELE NA MTEMI RAMADHAN WACHUKUA FOMU KUWANIA UONGOZI TFF


UZINDUZI WA KAMUSI KUU MPYA YA KISWAHILI KUTASAIDIA WATANZANIA KUJUA KISWAHILI FASAHA - MAMA SALMA KIKWETE

HAKIKISHENI MTWARA INAPATA MAJI KWA ASILIMIA 100 – PROF. MKUMBO

0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo ameiagiza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Mtwara (MTUWASA) ifanye bidii na kuhakikisha Mtwara inapata maji kwa asilimia 100, ikizingatiwa ni mji ulio na viwanda vikubwa, ili kuunga mkono Sera ya Viwanda inayotekelezwa na Serikali.

Prof. Mkumbo alisema hayo katika ziara yake ya kikazi aliyoifanya mkoani Mtwara, alipokuwa akitembelea mamlaka hiyo kwa nia ya kujua utendaji kazi wake na mipango ya utekelezaji wa miradi yake.

“MTUWASA imeshika nafasi ya 8 kati ya mamlaka 25 nchini mwaka huu kulingana na ripoti ya EWURA, ni moja ya mamlaka zinazofanya vizuri. Hivyo, hamna budi kutoka asilimia 60 ya huduma mnayotoa sasa na kufikisha asilimia 100, ili kuendana na mahitaji ya wananchi pamoja na viwanda vikubwa vilivyopo mjini hapa”, alisema Katibu Mkuu.

Prof. Mkumbo alisisitiza kuwa ili kuendana na Sera ya Viwanda huduma ya maji haina budi kuwa ya uhakika na endelevu, na MTUWASA inabidi wahakikishe Serikali inafanikiwa kufikia lengo hilo kama watoa huduma wa maji.

Aidha, aliwaasa wananchi wa Mtwara kuhakikisha wanatunza vyanzo vya maji, kwani pamoja na juhudi za Serikali za kuwekeza katika miradi mikubwa ya maji, itakuwa ngumu kufanikisha lengo la kutoa huduma ya uhakika na endelevu ya majisafi na salama kama vyanzo vya maji havitatunzwa na kuwa endelevu.

Naye Mkuregenzi Mtendaji wa Mamlaka ya ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Mtwara (MTUWASA), Inj. Mashaka Sitta alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha mamlaka hiyo inakuwa bora nchini ndani ya miaka miwili; baadhi ya mipango yao ikiwa ni kutunza vyanzo vya maji, kuongeza mitandao ya miundombinu ya maji, kuongeza uzalishaji na wateja ili kufikia lengo hilo.

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu alitembelea pia Ofisi za Bonde la Mto Ruvuma na Pwani ya Kusini na kukutana na baadhi ya watendaji wake na kuzungumza nao kuhusu usimamizi na maendeleo ya rasilimali za maji katika bonde hilo na kukamilisha ziara yake ya siku mbili katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo akipokea maelezo kutoka kwa Mkuregenzi Mtendaji wa Mamlaka ya ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Mtwara (MTUWASA), Inj. Mashaka Sitta alipotembelea chanzo cha maji cha Mtawanya, mkoani Mtwara pamoja na Inj. Najib Asumbwile kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo akiwa kwenye Mtambo wa Maji wa Kusafishia Maji, mkoani Mtwara.
 Sehemu ya Mtambo wa Kusafishia Maji, mkoani Mtwara.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo akikagua sehemu ya majengo mapya ya Ofisi za Bonde la Mto Ruvuma na Pwani ya Kusini ambayo ujenzi wake unaendelea, akiwa na Afisa Bonde, Msiru Msengi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo akizungumza kwenye ofisi ya Katibu Tawala Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maji mkoa wa Mtwara.

WATUMUSHI OFISI YA MWANASHERIA MKUU WAZINGATIE MAADILI YA UTUMISHI

0
0
Naibu Mwanasheria wa Serikali Bw. Gerson Mdemu akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake wa kazi na watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Tabora wakati wa wiki ya Utumishi wa Umma. Katika Mkutano huo Naibu  Mwanasheria Mkuu, amesisitiza watumishi wa Ofisi yake kuzingatia misingi na maadili ya  Utumishi.  Kushoto kwa Naibu Mwanasheria Mkuu ni Wakili wa Serikali Mfawidhi Bw. Jackson Bulashi na kulia ni  Bw. Benny Kabungo Mkurugenzi wa Utumishi na Raslimali  Watu.

Sehemu ya  Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria  Mkuu wa Serikali Tabora wakimsikiliza Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali  wakati wa kikao  kazi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho wa wiki ya  Utumishi wa Umma. Katika kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma Ofisi ya  Mwanasheria Mkuu ( 16-23) ilitenga siku mbili za kukutana na wadau na watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu.

WAZIRI MWAKYEMBE AKIZUNGUMZIA UMUHIMU WA KAMUSI KUU MPYA YA KISWAHILI

KILA SHULE ITAKAYOHITAJI USAJILI LAZIMA IWE NA VIWANJA VYA MICHEZO - SIMBACHAWENE

0
0
Serikali imesema ni marufuku kwa shule ambayo itakuwa haina viwanja vya michezo kupatiwa kibali cha kufungua shule ikiwa ni utekelezaji wa Sheria ya Elimu namba 25 ya mwaka 1978.


Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Masindano ya kwashule za msingi nchini UMITASHUMTA mkoani Mwanza, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMO) Mh. George Simbachawene, amemuagiza Kamishna wa Elimu nchini, kutozipatia vibali shule zinazo hitaji kufunguliwa endapo zitakuwa hazina viwanja vya michezo.


Simbachawene, amesema kutokana na sheria ya Elimu namba 25 ya mwaka 1978, ambayo inataka kila shule inapofunguliwa lazima iwe na viwanja visivyo pungua vitano hivyo nilazima hili lizingatiwe, “nichukue nafasi hii kumuagiza kamishna wa Elimu kuanzia sasa asisajili shule yeyote ile ambayo itakuwa haina Viwanja vya michezo, kwani bila kufanya hivyo azma yetu yakuinua michezo nchini haiwezi kutimia” alisema.

Mbali na kutoa maagizo hayo waziri Simbachawene, ameziagiza pia halmashauri na wilaya kote nchini kutenga sehemu ya mapato yao ya ndani kwaajili ya kitengo cha michezo, huku akizihimiza kuweka katika bajeti ijayo ya serikali fedha kwenye vifungu vinavyo husiana na michezo na kuonya kuwa endapo Halmashauri itashindwa kufanya hivyo basi yeye kama waziri mwenye dhamana hatakubali ipite. 

Baadhi ya Viongozi wa Serikali wakiongozwa na Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI George Simbachawene, wakionekana wenye furaha wakati wa Uzinduzi wa UMITASHUMTA 2017.
Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI George Simbachawene, akisalimiana na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Projestus Rubanzibwa alipofika kufungua rasmi Mashindano hayo.
Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI George Simbachawene akipeana mkono na Katibu Mkuu Baraza la Michezo la Taifa Mohamed Kiganja  wakati wa Uzinduzi wa UMITASHUMTA 2017.
RUBANZIBWA-- Mh. George Simbachawene, akisalimiana na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Projestus Rubanzibwa alipofika kufungua rasmi Mashindano hayo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WAGOMBEA 62 WAJITOKEZA KUCHUKUA FOMU TFF, KESHO MWISHO SAA 10

0
0
MCHAKATO WA UCHUKUAJI FOMU TFF

Wakati kesho Jumanne Juni 20, 2017 itakuwa mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), wagombea 62 tayari wamejitokeza.

Wanafamilia hao ni wale waliojitokeza kuanzia Ijumaa iliyopita Juni 16, mwaka huu wakiongozwa na Jamal Malinzi aliyekuwa wa kwanza kuchukua fimu kati ya wagombea tisa walioomba nafasi hiyo.

Fomu hizo zinachukuliwa na kurejeshwa katika ofisi za TTF, Karume jijini Dar es Salaam na Uchaguzi wa TFF utakafanyika Agosti 12, mwaka huu mkoani Dodoma.

Mbali ya Malinzi, wengine waliochukua fomu hizo ni Imani Madega, Wallace Karia, Fredrick Masolwa, Athumani Nyamlani, Fredrick Mwakalebela na Ally Mayay wakati waliojitokeza kuwania Makamu wa Rais wako Mulamu Nghambi, Michael Wambura, Geofrey Nyange, Mtemi Ramadhani na Robert Selasela.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YATEMBELEA HALMASHAURI YA WILAYA YA WANGING’OMBE KUHIMIZA UWAJIBIKAJI

0
0
 Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Ibrahim Mahumi akitoa ufafanuzi kuhusu taratibu zinazohusu  menejimenti ya  Rasilimaliwatu serikalini kwa viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe katika Ofisi za  Halmashauri hiyo  ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2017. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe Bi. Amina Kiwanuka.
 Viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakizungumza masuala ya kiutumishi na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo  ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2017.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NEWS ALERT: adakwa akitaka kuingiza simu katika gereza la mahabusu la Keko jijini Dar es salaam.

0
0
Jeshi  la Magereza jana Jumapili limemkamata kijana mmoja aitwaye Ramadhani Nombo akiwa na simu tano alizozificha kwenye mapande ya nyama aliyokuwa ameletea ndugu zake walio mahabusu katika gereza la mahabusu la Keko jijini Dar es salaam.


Kwa mujibu wa taarifa za jeshi hilo, hivi sasa vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kabla ya kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo.


“Kutokana na umakini wa askari wetu mara alipofika na kuomba kuwaone ndugu zake walio mahabusu na kuwapa chakula walibaini kwamba ndani yake kuna simu” imesema taarifa hiyo. Haikutajwa nyama na hizo simu alikuwa anapalekewa  mahabusu gani hapo gerezani.

Taarifa zinasema kimsingi kijana huyo amevunja Kifungu cha 86 (1) cha Sheria ya Magereza sura ya 56 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002 ambayo inakataza mtu yeyote kuingiza magerezani kitu chochote kisichoruhusiwa.
Kifungu hicho kinatamka bayana kwamba endapo ikithibitika mtu yeyote amekamatwa na kuingiza kitu chochote ambacho hakiruhusiwi kuingizwa gerezani, atahukumiwa kifungo kisichozidi miezi sita (6) gerezani au faini au vyote kwa pamoja.

 Mtuhumiwa Ramadhani Nombo akiwa amebeba mapande ya nyama ambayo yanatuhumiwa kuwa na simu tano ndani yake 

BREAKING NEWZZZZ :TAKUKURU YAWAPANDISHA KIZIMBANI VIGOGO WA ESCROW NA IPTL KWA KESI YA UHUJUMU UCHUMI.

0
0
Taasisi ya kupambana na kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU),imewafikisha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu watu wawili James Rugemalira (Pichani kushoto) na Harbinder Seth Sigh (Pichani kulia) kwa tuhuma ya kesi ya Uhujumu Uchumi.
Akizungumza mapema leo mchana jijini Dar Es Salaam,Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU), Valentino Mlowola amesema kuwa Mmiliki wa VIP Engineering and Marketing, James Rugemalira na Mmiliki wa Kampuni ya IPTL, Habirnder Seth wamefikishwa mahakama ya Kisutu leo mchana kwa kosa la kuhujumu uchumi pamoja na makoasa mengine yanayofanana na hayo.
Mlowola amesema kuwa watuhumiwa hao wameshafikishwa mahakamani kwa kosa la kuhujumu uchumi pamoja na makosa yanayofanana na hayo,akaongeza kusema kuwa TAKUKURU wamechunguza shauri hilo kwa muda mrefu na sasa imefika wakati kuwapeleka mahakamani watuhumiwa hao kujibu mashtaka yao.
Mlowola ametoa Wito kwa wananchi kutambua kuwa serikali ina nia njema na dhati kabisa ya kuwapa Maisha bora Watanzania,hivyo hakuna budi wale wote wanaotuhumiwa kwa makosa mbali mbali watafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
Kabla ya vigogo hawa wawili kufikishwa mahakamani leo, baadhi ya watumishi wa TANESCO tayari walishtakiwa kufuatia tuhuma za kupokea fedha kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engeneering and Marketing ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Ltd (IPTL), James Rugemalira.
Kwa picha zaidi na habari kamili BOFYA HAPA

Introducing "someone else" by sauti from east

MICHUZITV: KAMANDA MKONDYA AELEZEA KILICHOWAFANYA POLISI KUWATAWANYA WALEMAVU DAR ES SALAAM

MICHUZI TV: TIC KUTOA SEMINA KWA WAFANYA BIASHARA JIJINI DAR ES SALAAM

MFUMO WA USAJILI NCHINI KUBORESHWA

0
0
 Serikali ya Tanzania inafanya maboresho ya Mfumo wa Usajili uliopo na kuanzisha mfumo utakaofanya kazi vizuri usajili wa matukio muhimu ya binadamu na takwimu nchini unaofanywa na Wakala wa  Usajili, Ufilisi na Udhamini - RITA 
Waziri wa Katiba na  Sheria Prof.  Palamagamba  Kabudi  amesema hayo mjini Dodoma wakati akifungua mkutano wa wadau wanaojadili mfumo huo. Amesema maboresho ya mfumo huo yanatekelezwa kupitia Mkakati wa Kitaifa wa usajili wa Matukio muhimu ya binadamu na takwimu (Civil Registration and Vital STATISTICS-CVRS. 
Prof Kabudi amesema Mfumo huo unalenga kutatua changamoto mbalimbali ambazo zimefanya hali ya usajili wa Matukio muhimu ya binadamu kutokuwa ya kuridhisha nchini. Ameongeza kuwa ana imani kuwa utekelezaji wa mkakati huo itakuwa njia sahihi itakayowezesha kumuona kila mwananchi katika picha ya taifa.
Mkutano huo wa wadau wa usajili wa Matukio muhimu ya mwanadamu nchini umeandaliwa na RITA
Waziri Prof. Kabudi akipata picha na washiriki baada ya kufungua mkutano wa wadau wanaojadili mfumo huo. Amesema maboresho ya mfumo huo yanatekelezwa kupitia Mkakati wa Kitaifa wa usajili wa Matukio muhimu ya binadamu na takwimu (Civil Registration and Vital STATISTICS-CVRS. 

ofisa wa TRA kugombea urais wa TFF

0
0
MBIO za kuwania uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), zimezidi kushika kasi baada ya Ofisa wa juu Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shija Richard kujitosa kuwania urais wa shirikisho hilo.
Shija ambaye ni Meneja ndani ya Mamlaka ya Mapato Tanzania, amechukua fomu hiyo leo Jumatatu katika ofisi za TFF Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, ingawa hakuzungumza lolote kwa maelezo kuwa muda wa kampeni bado. 
“Ni kweli nimechukua fomu kuwania urais wa TFF, wengi mtataka kujua mengi kuhusu mimi na kwa nini nimejitosa katika nafasi hii, tuvute subira wakati wa kampeni ukifika nitazungumza, ila kwa leo itoshe kuuthibitishia umma kwamba nimechukua fomu ya urais,” alisema Shija. 
Mgombea huyo ana Shahada ya Uzamili katika masuala ya Sheria za Kodi na Utawala kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, pia ana Stashahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Fedha kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dar es Salaam na Stashahada ya Juu ya Uhasibu kutoka Chuo Kikuu cha Uhasibu Arusha (IAA). 
Pia Shija amehudhuria mafunzo mbalimbali ya uandishi wa habari na ameandikia magazeti mbalimbali hapa nchini kuanzia mwaka 1997.
 Mgombea huyo aliwahi kuitumikia Taasisi ya Kuzuia na Kupambaana na Rushwa (TAKUKURU) kabla ya kujiunga na Mamlaka ya Mapato Tanzania. Kwa sasa ni Mhazini Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA), akiwa pia amepata kuongoza klabu mbalimbali za mpira wa miguu kwa ngazi tofauti. 
Mwaka 2008 alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya Chama cha Soka wilayani Chato (CDFA), ambapo alisimamia usajili wa chama hicho kuelekea kwenye uchaguzi ambao hata hivyo hakugombea. Pia Shija amepata kuwa Katibu Mkuu wa Klabu ya Michezo ya Bukoba Veteran iliyopo mkoani Kagera. 
Ofisa wa juu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shija Richard akitoka ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Uwanja wa Karume Dar es Salaam muda mfupi baada ya kuchukua fomu kuwania urais wa shirikisho hilo.

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 19.06.2017

MAGAZETI YA LEO JUMANNE JUNE 20,2017

LEO NI SIKU YA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAKIMBIZI DUNIANI

0
0
 
Mkimbizi akiwasili nchini Tanzania kutoka Burundi baada ya kukimbia machafuko

BALOZI MIGIRO AMTUNUKU KIJANA ALIYESHINDA PICHA ZA KIMATAIFA

0
0
Baadhi yetu huwaita wenye hali hii “taahira” – neno la asili ya Kiarabu  lenye maana “mtu asiye sawa” (wazimu, chizi, bwege, nk).  Sahihi ni “mtindio ubongo” – kwa Kiingereza “Down Syndrome”....

Baadhi ya taswira zake ni : kufikiri na kuzungumza taratibu, kigugumizi,  mwili mfupi,  utofauti wa tambo la kichwa,vidole vya mikono na miguu,nk.
Balozi Migiro akimvika Samwel Mwanyika bendera ya taifa, alipowakaribisha na familia ofisini kwake, Ijumaa 16, Juni 2017.

Mbali na kuwanyanyapaa,  jamii zetu Afrika bado hazitambui umuhimu wa kuendeleza wenye ulemavu.


Mwaka huu kijana wa miaka 18, Samwel Mwanyika, mwenye “Mtindio Ubongo “  (Down Syndrome) alikuwa mshindi wa kimataifa wa upigaji picha.


Balozi wetu Uingereza Mheshimiwa Asha-RoseMigiro akaeleza:

“Wametoka vijana wengi kwenye nchi  zilizoendelea, wengine wamemzidi umri...tena wenzetu huwa na mipango maalum ya kuwapa mbinu mbalimbali,...sasa huyu wa familia ya kawaida tu ya Kitanzania ambapo bado hatujaweka miundo mbinu kama walivyoweka huku,  picha yake imeshinda...”


Mwasisi wa kujitolea  wa shirika la Mtindio Ubongo (Pearl of People with Down Syndrome) , Mony Teri Pettite  na wazazi wake Samwel, Philip Mwanyika na Sophie Mshangama, walikutana na Balozi  Migiro na kupongezwa Ijumaa iliyopita. Afisa Utawala Ubalozini, Rose Kitandula , pia alikuwepo.

Picha na Habari za Freddy Macha 

Samwel Mwanyika na picha iliyonyakua tuzo la kimataifa la Stephen Thomas, mjini London.
Balozi Migiro, na Afisa Utawala Ubalozi London wakiwa na Samwel Mwanyika na mwenzake mwenye “Mtindio Ubongo” (Down Syndrome), Penina Haika Petitte.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA RAIS MSTAAFU WA NIGERIA MHE. OLUSEGUN OBASANJO IKULU DAR ES SALAAM

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimlaki Rais Mstaafu wa Nigeria Mhe. Olusegun Obasanjo aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 20, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na  Rais Mstaafu wa Nigeria Mhe. Olusegun Obasanjo aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 20, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsindikiza Rais Mstaafu wa Nigeria Mhe. Olusegun Obasanjo baada ya kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 20, 2017

PICHA NA IKULU
Viewing all 109595 articles
Browse latest View live




Latest Images