Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

Mshindi wa Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya NBC akabidhiwa gari lake

$
0
0

Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Andrew Lyimo (katikati), akikabidhi kadi ya gari kwa Rose Richard Getenyi kwa niaba ya mumewe, Lawrence Njozi aliyeshinda zawadi ya gari mpya aina ya Toyota Double Cabin Pick Up baada ya kushiriki katika kampeni ya akaunti ya Malengo ya benki hiyo. Anayeangalia ni Meneja Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza, Dorothea Mabonye. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Andrew Lyimo (katikati), akikabidhi ufunguo wa gari mpya kwa Rose Getenyi kwa niaba ya mumewe, Lawrence Njozi aliyeshinda zawadi ya gari mpya aina ya Toyota Double Cabin Pick Up baada ya kushiriki katika kampeni ya akaunti ya Malengo ya benki hiyo. Anayeangalia ni Meneja Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza, Dorothea Mabonye. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Rose Gitenyi akifurahia kuwasha gari lao Toyota Double Cabin Pick Up jipya ambalo mumewe alijishindia katika kampeni ya akaunti ya Malengo iliyoendeshwa na NBC. Familia ya mteja wa Benki ya NBC Lawrence Njozi aliyeibuka mmoja wa washindi wawili wa kampeni ya Malengo ya benki hiyo na kujishindia gari jipya aina ya Toyota Double Cabin Pick Up wakipozi kwa picha mbele ya gari hilo mara baada ya Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa NBC, Andrew Lyimo (kulia) kumkabidhi mke wa mshindi huyo, Rose Getenyi (wa tano kushoto), jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.     

WILAYA YA UBUNGO YAANZA KUJIPANGA VYEMA KWA MAONESHO YA NANE NANE

$
0
0
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo ndg John Lipesi Kayombo akiwa ameambatana na timu ya wakuu wa idara wa Manispaa ya Ubungo, walitembelea na kujionea maandalizi ya Nanenane katika eneo la Itungi Mkoani Morogoro.

Akiwa katika eneo hilo la Manispaa ya Ubungo, maalum kwa maonesho ya Nanenane,Mkurugenzi na timu yake wamejionea aina mbalimbali za mazao ambayo tayari yamepandwa zikiwemo mboga mboga za kila aina.

Pia Manispaa tayari imetengeneza bwawa la kisasa la samaki aina ya Tilapia, na banda la kisasa la ufugaji ng'ombe ,

Baada ya kuona maandalizi hayo Mkurugenzi ameipongeza idara ya kilimo kwa maandalizi hayo na kuahidi kutoa ushirikiano kwa kuwezesha pale patakapohitaji uwezeshwaji yuko tayari, ili kuhakikisha maonyesho hayo yanafana na kuwa ya tofauti licha ya Ubungo kuwa ni Halmashauri mpya .

Naye kaimu mkuu wa idara ya kilimo na mifugo ,Salimu Msuya amesema wao kama idara wamejipanga vizuri na wanaamini watafanya vizuri katika maonyesho hayo,hivyo wanawakaribisha wananchi wote kutembelea banda la Ubungo siku hiyo ya Nanenane.

Tarehe 8/8/ kila mwaka Tanzania huadhimisha sikukuu ya wakulima.

*Ubungo mpya, Ubungo ya tofauti *

 Mkurugenzi John Kayombo na Timu ya Wakuu wa  Idara wakikagua Ujenzi wa  Bwawa la samaki
 Afisa Kilimo Salim Msuya akitoa Maelekezo kwa timu ya Wakuu was Idara Kuhusu Kilimo cha Mbogamboga kilichofanyika eneo hilo
Mkurugenzi wa  Manispaa ya Ubungo John Kayombo na Wakuu was Idara Wakipata Maelekezo Kutoka ka Afisa wa Kilimo ndugu Salim Msuya

MASAUNI ADHAMINI MASHINDANO MAKUBWA YA KUHIFADHI QUR-AN, ZANZIBAR NA TANZANIA BARA

$
0
0


Mwanafunzi Khamis Mussaakionyesha jitihada zake katika Mashindano ya kuhifadhi Qur-an katika Jimbo la Kikwajuni, Unguja, Zanzibar, linaloongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, na mdhamini wa mashindano hayo, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani). Mashindano hayo yalishirikisha Madrasa mbalimbali za Jimbo la Kikwajuni pamoja na maeneo mbalimbali ya Zanzibar na Tanzania Bara.
Mgeni rasmi katika Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an, Waziri wa Nchi, Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Abood akimkabidhi zawadi mshindi wa maswali ya papo kwa papo, Ilham Idrisa (kulia). Kushoto ni Mdhamini ya mashindano hayo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni. Watatu kushoto, Mwakilishi wa Jimbo hilo, Nassor Salim Jazeera. Mashindano hayo yaliyoshirikisha Madrasa mbalimbali za Jimbo la Kikwajuni pamoja na maeneo mbalimbali ya Zanzibar na Tanzania Bara, yalifanyika katika Viwanja vya Mnara wa Kisonge mjini Unguja.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauniakizungumza kabla ya mgeni rasmi katika Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an, Waziri wa Nchi, Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Abood(katikati) kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano hayo.Mashindano hayo yaliyoshirikisha Madrasa mbalimbali za Jimbo la Kikwajuni pamoja na maeneo mbalimbali ya Zanzibar na Tanzania Bara, yalifanyika katika Viwanja vya Mnara wa Kisonge mjini Unguja na kudhaminiwa na Mbunge wa Jimbo hilo. Kulia ni Mwakilishi wa Jimbo hilo, Nassor Salim Jazeera
Sehemu ya washiriki katikaMashindano ya Kuhifadhi Qur-an wakimsikiliza mdhamini wa Mashindano hayoNaibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), wakati nalipokua akitoa hotuba yake. Katika hotuba yake Masauni alisema washiriki wameonyesha uwezo mkubwa wa kuhifadhi Qur-an.

MSIICHUKIE SERIKALI ILIYOPO MADARAKANI KWA KUKOSA AJIRA.

$
0
0
Wanafunzi wa shirikisho la vyuo vikuu nchini wa chama cha mapinduzi wanaomaliza masomo yao wametakiwa kuacha kukichukia chama hicho kwa madai ya kukosa ajira kwani kufanya hivyo nikwenda kunyume na ilani ya chama.

Fuatilia LIVE Yanayojiri Bungeni Mjini Dodoma Leo Jumatatu Juni 19. 2017

MUFTI MKUU WA TANZANIA ABUBAKAR ZUBEIR AMEWATAKA WATANZANIA KUPENDEZA KWA KUVAA MAVAZI YANAYOTENGENEZWA TANZANIA

$
0
0
Muft Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir amewataka watanzania na waislamu kwa ujumla kupendeza kwa kuvaa mavazi yanayotengenezwa na kampuni ya mzawa Mussa Bakari ya 'Islamic Fashion Tanzania'. 

Kiongozi huyo waislamu nchini ametoa kauli hiyo Jijini Dar es Salaam Jumapili wakati akizindua kampuni hiyo ya mavazi ya kiislamu na kueleza kuwa kwa mujibu wa maandiko ya dini hiyo, wameamrishwa kupendeza kwani Mungu ni mzuri na na hupenda vitu vizuri. 
Mufti alifafanua kuwa uislamu huambatana na usafi na usafi huo unaanzia kwenye mavazi, hivyo ni vyema waislamu wakaitumia fursa hiyo kwa kununua mavazi kutoka kwenye kampuni hiyo ya mzawa. 
Pia ameishauri kampuni hiyo kujitangaza zaidi kwani hitaji wa vazi hilo ni mkubwa nchi nzima na sio tu kwa mkoa wa Dar es Salaam, na akawaomba watume muwakilishi kwenye sherehe za Eid El Fitr zinazotaraji kufanyika Mkoani Kilimanjaro kitaifa, ili wakazitangaze bidhaa zao na huko. 
"Ni vyema pia waislamu wakaambizana habari njema za ujio wa Islamic Fashion Tanzania ili wengi waweze kunufaika kwa kupendeza na mavazi yao" alisema Mufti Mkuu. 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya Islamic Fashion Tanzania Mussa Bakari ameeleza kuwa kampuni hiyo imeanza tangu mwaka 2014 ambapo walikuwa wanategemea mavazi hayo kutoka nchi za nje, kutokana na kwa jitihada walizofanya \ sasa wameweza kutengeneza mavazi yao ambapo nusu ya uzalishaji inafanyika Dubai na kumalizikia Tanzania.
Mkurugenzi Mussa Bakari ameongeza kuwa changamoto ya Watanzania kukosa kanzu zenye ubora kwa muda mrefu ndiyo zimewapelekea wao kuanzisha Islamic Fashion Tanzania, ili kuwarahisishia watanzania waliokuwa wanasafiri kwenda nje ya nchi wapate kanzu zenye ubora. Hivyo amewaomba watanzania kumuunga mkono ili aweze kupiga hatua zaidi za kuwahudumia watanzania.

 Muft Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir (kulia) akizungumza jijiini Dar es Salaamn wakati uzindui wa mavazi yanayotengenezwa na kampuni ya mzawa Mussa Bakari ya 'Islamic Fashion Tanzania.  
 Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya Islamic Fashion Tanzania Bw. Mussa Bakari akiwaomba watanzania kumuunga mkono ili aweze kupiga hatua katika uzindui huo.
 Muft Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir (kulia) akizindua mavazi yanayotengenezwa na kampuni ya mzawa Mussa Bakari ya 'slamic Fashion Tanzania  kwa kushirikiana Shehe mkuu wa mkoa wa Dar es salaam,Sheikh Alhad Mussa Salim (katikati) na  Mkurugenzi wa Kampuni hiyo  Bw. Mussa Bakari.
 Sehemu ya viongozi  na  wageni mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo.
 Sehemu ya viongozi na wageni mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo.Picha na Emmanuel Maasaka,Globu ya Jamii.

WAZIRI LUKUVI ATOA ANGALIZO LA MWISHO LA KODI YA PANGO LA ARDHI

BREAKING NEWZZZZ: DAKTARI FEKI ADAKWA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI LEO

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)  leo imemtia mbaroni kijana mmoja aliyekuwa akijifanya daktari.  Mtuhumiwa alikuwa akijitambulisha kwa wagonjwa kwamba anaitwa Dk Abdallah Juma na akijifanya kutoa huduma katika Maabara Kuu. 
Uongozi wa hospitali hiyo umesema kuwa kijana huyo ni daktari feki na si daktari kama alivyokuwa akijitambulisha na kwamba amekamatwa baada ya kuwekewa mtego na askari wa hospitali hiyo. Uongozi wa hospitali hiyo umesema kuwa walinzi walikuwa wakimtilia shaka na kuanza kumfuatilia hadi walipofanikiwa kumkamata. 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa Hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha amesema hospitali imeweka mikakati mbalimbali ya kupambana na wahalifu wakiwamo watu wanaojiita ni madaktari kama huyo ambaye amekamatwa leo.
 Kulia ni daktari feki ambaye amekuwa akijitambulisha kwamba ni Dkt, Abdallah Juma ambaye amekuwa akifanya kazi katika Maabara Kuu, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akiwa chini ya ulinzi baada ya kukamatwa na mmoja wa askari wa Muhimbili (kushoto).
Daktari feki huyo ambaye amekuwa akijitambulisha kwamba ni Dkt. Abdallah Juma akiwa chini ya ulinzi

WAZIRI MKUU AKITETA JAMBO NA WAZIRI JENISTA MHAGAMA

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri , Sera, Bunge, Kazi, Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama,Bungeni Mjini Dodoma Juni 19,2017.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAMBO YA DAR LIVE MBAGALA SIKU YA IDDI MOSI

WIZARA YA MAMBO YA NDANI WAKUTANA KUJADILI MPANGO KAZI NA MPANGO WA UNUNUZI WA BAJETI YA 2017/2018

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango na Bajeti wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Amani Mashaka(katikati), akitoa maelekezo kwa watumishi ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, wakati wa kikao cha Mpango Kazi na Mpango wa Ununuzi wa bajeti ya wizara hiyo.Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Bwalo la Jeshi la Magereza,Ukonga,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mtumishi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Fatuma Mohamed (aliyevaa miwani), akiomba ufafanuzi kutoka kwaKaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango na Bajeti wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Amani Mashaka(aliyesimama kulia) wakati wa Kikao cha Mpango Kazi na Mpango wa Ununuzi wa bajeti ya wizara.Kikao kimefanyika leo katika Ukumbi wa Bwalo la Jeshi la Magereza,Ukonga,jijini Dar es Salaam.
Mratibu Mwandamizi wa Uhamiaji,Colla Kayumba, akizungumza na watumishi wengine wa idara hiyo,Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji,Said Kassim(katikati) na Mkaguzi Msaidizi Sanga Hussein, wakati wa Kikao cha Mpango Kazi na Mpango wa Ununuzi wa bajeti ya wizara.Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Jeshi la Magereza,Ukonga,jijini Dar es Salaam

AFRICA DOMAIN NAME SYSTEM (DNS) TO BE HELD IN DAR ES SALAAM FROM 26th to 28th July, 2017

wAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZINDUA KAMUSI KUU YA KISWAHILI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inatambua umuhimu wa lugha ya Kiswahili kwa ustawi wa Taifa na katika kulinda umoja wa Kitaifa.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatatu, Juni 19, 2017) wakati akizungumza na wabunge, viongozi wa Serikali na wananchi waliohudhuria uzinduzi wa Kamusi Kuu ya Kiswahili uliofanyika kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.

“Serikali inatambua umuhimu wa lugha ya Kiswahili kwa ustawi wa nchi yetu na katika kulinda umoja wa Kitaifa. Hakika lugha ya Kiswahili ndiyo inayotufanya tuwe Watanzania. Hivyo, tunaithamini sana na kwetu hii ni lulu na tunu ya Taifa,” amesema.

Waziri Mkuu amesema uzinduzi wa Kamusi hiyo unaenda sambamba na azma ya Serikali ya kutumia Kiswahili kwenye shughuli zote za kitaifa kama vile mikutano, mijadala, semina na ufundishaji shuleni.

Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kumpongeza Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuhimiza matumizi ya Kiswahili kwenye mikutano na matukio muhimu ya kitaifa, kama vile dhifa za kitaifa anazowaandalia wageni wake kutoka nje ya nchi.

“Hata alipokuwa kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika wa mwaka 2017, Mheshimiwa Rais alitumia Kiswahili kuhutubia mkutano huo. Amekuwa akifanya hivyo, hata kwenye mikutano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Lengo lake ni kuitangaza lugha hii ya Kiswahili,” alisema.

Aliwasihi wazazi kote nchini wahakikishe kuwa watoto wao wanapata kamusi hiyo kama moja ya nyenzo zao za kujifunza lugha ya Kiswahili. “Vilevile, ninashauri, makundi mengine kama vile waheshimiwa wabunge, wanahabari, wakalimani, wafasiri, waandishi na wahariri wa vitabu, maofisa mawasiliano wa kwenye ofisi zetu, muone umuhimu wa kununua Kamusi hii, ili iwasaidie kujiimarisha kwenye matumizi ya Kiswahili fasaha na sanifu,” aliongeza.

Mapema, akizungumza katika hafla hiyo fupi, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe alisema Kiswahili ni lugha ya pili inayotumiwa na watu wengi zaidi barani Afrika lakini pia ni lugha ya 10 kati ya lugha 6,000 zinazozungumzwa na watu wengi duniani.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Dk. Seleman Sewangi alisema kazi ya kuandaa kamusi hiyo ilianza Agosti 12, 2011 na kukamilika mwaka 2015 ambapo toleo la kwanza lilichapishwa.

Alisema kamusi hiyo imekusanya maneno mengi makuu (vidahizo) kuliko kamusi zilizotangulia na kwamba ya sasa ina maneno hayo 45,500.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha Kamusi Kuu ya Kiswahili baada ya kuizindua kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Juni 19, 2017. Kulia ni Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu. Kushoto ni Balozi wa Kiswahili Afrika, Mama Salma Kikwete. Wapili kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipozindua Kamusi Kuu ya Kiswahili kwenye ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma Juni 19, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Kamusi Kuu ya Kiswahili kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Juni 19, 2017 (kushoto) ni Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu nakala ya Kamusi Kuu ya Kiswahili baada ya kuzindua kamusi hiyo kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, Juni 19, 2017.

Tume ya Jaji Mshibe yaanza kuwasilisha mapendekezo ya miswada mitatu ya sheria

$
0
0
NA HAJI NASSOR, PEMBA

TUME ya kurekebisha sheria Zanzibar, imeanza zoezi la kuwasilisha miswada mitatu ya sheria ikiwemo ya uharibifu wa mazao, kwa wadau mbali mbali kisiwani Pemba, baada ya kukusanya maoni ya marekebisho ya sheria hizo, miezi iliopita.

Awali tume hiyo chini ya Mwenyekiti Jaji Mshibe Ali Bakari na Katibu wake Asma Jidawi, walipita kwa wadau mbali mbali wakiwemo masheha, wanasheria, wakulima na wananchi wengine kukusanya maoni, ili kuzifanyia marekebisho sheria hizo kongwe.

Akiwasilisha mswada ya sheria ya Uharibifu wa mazao, mwanasheria kutoka Tume hiyo Tajo Ameri alisema, kwa sasa baada ya maoni ya wananchi, sheria inayokuja inatmbua uharibifu wa mazao mbali mbali, badala ya ile ya zamani kuwa na mazao aina mbili pekee.

Alisema, jengine ambalo limo kwenye mswada huo ni kuingizwa kwa mazao hata yanayotoka nje ya Zanzibar, ambapo mawali sheria hiyo ya uharibifu wa mazao, ilitambua yale yanayozaliwa nchini pekee.

“Tulipita Unguja na Pemba kwa wadau mbali mbali, ili kukusanya maoni juu ya sheria ya uharibifu wa mazao, na sasa tunayarejesha tena kwenu ili kuona kama mliotueleza ndio”,alifafanua.

Kwa upande wake, mwanasheria wa Tume hiyo Miwta Khamis Haji, alisema, suala la usajili wa nyaraka limekuwa ni jambo la lazima kwa mali, kama vile mashamba na nyumba, ili kuondoa udanganyifu unaoweza kujitokeza.

Mapema Katibu wa Tume hiyo ya Kurekebisha Sheria Zanzibar, Asma Jidawi, alisema miongoni mwa kazi kubwa ya tume hiyo, ni kuzifanyia marekebisho sheria au vifungu ambavyo vinaonekana kupitwa na wakati.

Hata hivyo aliwataka wananchi na wadau wengine, kuendelea kutoa maeoni yao kwa sheria mbali mbali, ambazo tume hiyo huzifanyia marekebisho.

Baadhi ya masheha waliohudhuria mkutano huo, walisema elimu ya usajili wa mali, nyaraka na ardhi inahitajika ili wananchi wapate elimu ya kutekeleza sheria.

Shehe wa shehia ya Mgelema Omar Idd Zaina, alisema bado migogoro ya ardhi hujitokeza kwa baadhi ya wamiliki kutokana na kukosa uwelewa juu ya umuhimu wa kusajili ardhi zao.

Nae Sheha wa shehia ya Uweleni Abdalla Omar Mjawiri, aliipongeza Tume hiyo, kutokana na kuwarejeshea maoni yao walioyakusanya wakati zikifanyia marekebisho sheria za uharibifu wa mazao, usajili wa nyaraka na sheria ya endelevu ya ardhi.

Tayari Tume ya Kurekebisha sheria Zanzibar imeshazifanyia marekebisho sheria 17 ikiwemo sheria ya ushahidi, sheria ya wanyama, vileo na sheria ya usafirishaji baharini.

NEWS ALERT: MAKAMU MWENYEKITI WA BAVICHA TAIFA PATRICK OLE SOSOPI AKAMATWA NA POLISI IRINGA

$
0
0
JESHI la polisi mkoa wa Iringa linamshikilia makamu mwenyekiti wa baraza la vijana la chama cha Demokrasi na maendeleo (BAVICHA ) Taifa Patrick Ole Sosopi (pichani) kwa tuhuma za kufanya mikutano ya hadhara bila kuwa na kibali cha jeshi la polisi . 
Akithibitisha hilo, Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Iringa John Kauga amesema kwamba  Sosopi alikamatwa leo asubuhi na kuwa bado jeshi hilo linaendelea kumshikilia kwa mahojiano kabla ya kufikishwa mahakamani kwa kosa la kufanya mikutano bila kibali cha jeshi hilo kwenye vijiji viwili vya Kinyika na Mlowa jimbo la Ismani wilaya ya Iringa mkoani hapa . 
 
Alisema kuwa makamu mwenyekiti huyo wa Bavicha alipewa kibali ya kufanya mikutano ya ndani ambayo inaruhusiwa ila hakufanya hivyo na badala yake kufanya mikutano ya nje kinyume na taratibu na kuwa mikutano hiyo ilifanyika kati ya tarehe 16 na 17 mwaka huu . 

Tunaendelea kumshikilia Sosopi kutokana na kosa la kuvunja sheria kwa kufanya mikutano ya hadhara pasipo kuwa na kibali cha polisi kimsingi mikutano yote ya hadhara kwa vyama vya siasa ilipigwa marufuku na mikutano inayoruhusiwa na ile ya ndani pekee ila yeye aliomba kibali cha kufanya mikutano ya ndani ila hakuweza kufanya hivyo na badala yake alifanya mikutano ya hadhara nje “ 
Hata hivyo kaimu kamanda huyo hakusema ni lini makamu mwenyekiti huyo wa BAVICHA Taifa atafikishwa mahakamani.

Hatua ya kukamatwa kwa Sosopi imekuja zikiwa zimepita wiki mbili toka aliposhikiliwa na kuachiwa kwa dhamana jeshi la polisi la polisi kwa tuhuma za kufanya mkutano katika eneo la wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Kijiji cha Nyakavangala.
Huko  alikamatwa kwa agizo la mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela kwa madai ya kufanya mkutano huo  kutoa maneno ya uchochezi kwa wachimbaji hao

POLEPOLE AFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE KUTOKA KITUO CHA DEMOKRASIA YA VYAMA VINGI CHA UHOLANZI, OFISI NDOGO YA MAKAO MAKUU YA CCM, DAR ES SALAAM, LEO

$
0
0

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akimsalimia Meneja Mradi wa kushawishi Siasa Shirikishi katika kuimarisha vyama vya Siasa hapa nchini, hasa katika ushiriki wa Wanawake na Vijana katika masuala ya Siasa, unaoendeshwa na Kituo cha Demokrasia ya Vyama Vingi cha Uholanzi (NIMD) kwa kushirikiana na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Arjan Van Der Waal, wakati alipokutana na ujumbe wa Meneja huyo na Mwakilishi wa NIMD Kanda ya Afrika Dk. Augustine Magolowondo (kulia), katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM,Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Watatu kulia ni Mwenyeji wa ugeni huo, Daniel Loyc kutoka TCD.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akimsalimia Mwakilishi wa Kituo cha Demokrasia ya Vyama Vingi cha Uholanzi (NIMD) Kanda ya Afrika Dk. Augustine Magolowondo kutoka Malawi, alipopokea na kufanya mazungumzo na ugeni huo kutoka NIMD, leo
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akiwakaribisha kuketi kwa ajili ya kuendelea na mazungumzo.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akizungumza na ujumbea kutoka Kituo cha Demokrasia ya Vyama Vingi cha Uholanzi (NIMD) katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Katika Mazungumzo hayo, Polepole aliitaka NIMD kuja kufanya kazi nchini kwa lengo la kuinua hadhi ya siasa nchini badala ya kubomoa. "Hatutarajii NIMD ije kufanya mambo hasi, mradi usilenge kuondoa madarakani Chama tawala, bali uwe chachu katika kuhamasisha uungaji mkono mambo mazuri yanayofanywa na Rais Dk. John Magufuli kama haya ya kulinda rasilimali za nchi", alisema Polepole. MAELEZO/PICHA NA BASHIR NKOROMO

MAALIM SEIF AJUMUIKA KATIKA FUTARI NA WAKAAZI WA TEMEKE

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF , Maalim Seif Sharif Hamad akiwa amejumuika na wakazi wa Temeke katika swala ya Magharibi  iliyofanyika nyumbani kwa Mbunge wa Temeke Abdalah Mtolea ambapo alipata kujumuika katika futari na wakazi wa eneo hilo iliyoandaliwa na Mbunge huyo

Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala  Mstahiki Omary Kumbilamoto  akiwa katika safu ya kuswali swala ya Magharibi nyumbani kwa Mbunge wa Temeke Abdalaha Mtolea wakati wa futari iliyoandaliwa na Mbunge huyo
Umati wa watu uliofika katika  futari iliyoandaliwa na mbunge wa Temeke Mhe. Abdallah Mtolea
Mbunge wa Temeke Abdalah Mtolea akitoa neno la Shukrani kwa watu waliojumuika katika futari aliyo iandaa nyumbani kwake Buza Kanisani Temeke jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF , Maalim Seif Sharif Hamad akitoa neno kwa wakazi wa Temeke jijini Dar es Salaam mara baada ya futari iliyoanfdaliwa na mbunge wa jimbo hilo Abdalah Mtolea.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

RAIS DKT MAGUFULI KUAZA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU TATU MKOANI PWANI

SPRITE BBALL KINGS YAINGIA HATUA YA MTOANO, DROO KUCHEZWA LEO USIKU

$
0
0
 Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


MASHINDANO ya Sprite BBall Kings yameendelea tena juzi kwa michezo mitano kupigwa katika uwanja wa Habours Club Mivinjeni na kufanikisha kupatikana kwa timu zitakazoungana na zingine za wiki iliyopita.

Hiyo ni raundi ya pili ya mashindano hayo ikiwa ni muendelezo wa michezo ya mtoano iliyoanza takribani wiki tatu zilizopita ili kumpata bingwa wa Sprite BBall Kings 2017

Mchezo wa kwanza uliwakutanisha timu za Mchenga na Ukongana timu ya Mchenga kuibuka na ushindi wa vikapu 115 dhidi ya 63 za Ukonga.

Mechi ya pili iliwakutanisha Ardhi ambaye alitoka na ushindi wa vikapu 60 dhidi ya Heroes B aliyepata vikapu 42, Flying D wakaumana na UDSM na kufanikiwa kushinda kwa vikapu 68 dhidi ya vikapu 45.

Mechi ya nne iliwakutanisha Kigamboni na St Montfort na ulimalizika kwa vikapu 71 vya Kigamboni dhidi ya 40 vya Montfort huku mechi ya mwisho ikiwa ni DMI aliyetoka na vikapu 41 dhidi ya 74 vya Oysterbay na kuhitiMisha michezo ya raundi ya pili ya Sprite Bball Kings.

Mratibu wa Mashindano hayo ya Sprite BBall Kings Basilisa Biseko amesema kuwa baada ya kumalizika kwa mechi za wiki hii kutachezeshwa kwa droo maalumu kwa ajili ha kuzipanga timu zitakazochuana kwenye hatua ya mtoano ya raundi ya tatu ya Sprite BBall Kings 2017.

"Timu zilizopata alama nyingi katika michezo ya wiki iliyopita na katika michezo ya ju ndiyo watakaofanikiwa kuingia hatua inayofuata ya michuano ya Sprite BBall Kings na kutakuwa na droo ya moja kwa moja itakayorushwa hewani kupanga timu zitakazoumana,"amesema Basilisa.

Michuano hiyo inayodhaminiwa na Sprite kwa kushirikiana na East Africa Tv na Redio huku mshindi akitarajiwa kuondoka na kitita cha shiling milion 15. 

Timu ya Mchenga (Njano) wakiumama katika hatua ya pili ya michuano ya Sprite BBalla Kings dhidi ya Ukonga katika mechi iliyopigwa Harbours Club Mivinjeni na Mchenga kutoka na ushindi wa vikapu 115 dhidi ya 63. 

Timu ya Kigamboni Heroes (wekundu) wakisalimiana na St Montfort kabla ya mchezo wao wa hatua ya pili ya Sprite BBall Kings uliofanyika katika uwanja wa Harbours Club Mivinjeni na Kigamboni kuibuka na ushindi wa vikapu 71 dhidi ya 40
 Mohamed Yusuph mchezaji wa Mchenga akipiga pigo la adhabu kwa timu yake katika mchezo wa hatua ya pili ya michuano ya Sprite Bball Kings uliomalizika kwa Mchenga kupata ushindi wa vikapu 115 dhidi ya 63 vya Ukonga.

SPRITE BBALL KINGS YAINGIA HATUA YA MTOANO, DROO KUCHEZWA LEO USIKU

$
0
0
 Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MASHINDANO ya Sprite BBall Kings yameendelea tena juzi kwa michezo mitano kupigwa katika uwanja wa Habours Club Mivinjeni na kufanikisha kupatikana kwa timu zitakazoungana na zingine za wiki iliyopita.
Hiyo ni raundi ya pili ya mashindano hayo ikiwa ni muendelezo wa michezo ya mtoano iliyoanza takribani wiki tatu zilizopita ili kumpata bingwa wa Sprite BBall Kings 2017.
Mchezo wa kwanza uliwakutanisha timu za Mchenga na Ukongana timu ya Mchenga kuibuka na ushindi wa vikapu 115 dhidi ya 63 za Ukonga.
Mechi ya pili iliwakutanisha Ardhi ambaye alitoka na ushindi wa vikapu 60 dhidi ya Heroes B aliyepata vikapu 42, Flying D wakaumana na UDSM na kufanikiwa kushinda kwa vikapu 68 dhidi ya vikapu 45.
Mechi ya nne iliwakutanisha Kigamboni na St Montfort na ulimalizika kwa vikapu 71 vya Kigamboni dhidi ya 40 vya Montfort huku mechi ya mwisho ikiwa ni DMI aliyetoka na vikapu

Timu ya Mchenga (Njano) wakiumama katika hatua ya pili ya michuano ya Sprite BBalla Kings dhidi ya Ukonga katika mechi iliyopigwa Harbours Club Mivinjeni na Mchenga kutoka na ushindi wa vikapu 115 dhidi ya 63. 

Timu ya Kigamboni Heroes (wekundu) wakisalimiana na St Montfort kabla ya mchezo wao wa hatua ya pili ya Sprite BBall Kings uliofanyika katika uwanja wa Harbours Club Mivinjeni na Kigamboni kuibuka na ushindi wa vikapu 71 dhidi ya 40
 Mohamed Yusuph mchezaji wa Mchenga akipiga pigo la adhabu kwa timu yake katika mchezo wa hatua ya pili ya michuano ya Sprite Bball Kings uliomalizika kwa Mchenga kupata ushindi wa vikapu 115 dhidi ya 63 vya Ukonga. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images