Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAHIMIZA USHIRIKIANO NA WADAU

$
0
0
 Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Mdemu akitoa maelezo wakati wa Mkutano wa Kazi kati ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wadau  ( hawapo pichani)kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali zilizopo  Mkoani Tabora ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma. Madhumuni ya  Kikao kazi hicho ilikuwa ni  kukutana wa wadau hao kwa lengo la kujadiliana, kubadilishana mawazo na kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali ambazo wadau hao pamoja na  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wanakumbana  nazo wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.  Wadau walioshiriki kikao  hicho ni kutoka Mahakama,  Takukuru, Magereza, Polisi, Wakala wa Barabara, Maliasili, Halmashauri, Mawakili wa Serikali, Wanasheria na  wanajamii. Kushoto kwa   Naibu Mwanasheria Mkuu   Wakili Mfawidhierikali  Kanda ya Tabora Bw. Jackson Bulashi na kulia ni  Kamanda wa Takukuru Tabora  Bw. Fidelis Kalungura
 Sehemu ya  wadau ambao wamekuwa na  mazungumzo na majadiliano na Ujumbe wa  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa  Serikali  ulioongozwa na Naibu  Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bw. Gerson  Mdemu. Majadiliano hayo  yamefanyika katika ukumbi wa  mikutano wa Takukuru Mkoani Tabora siku ya  Ijumaa ( June 16) ikiwa ni sehemu ya  Maadhimisho ya  Wiki ya Utumishi wa Umma.
Wadau kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali, Mahakama, Polisi, Takukuru, Maliasili, Magereza,  Halmashauri,  Wakala wa Barabara,Mawakili wa Serikali na Wanasheria wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa kikao kazi cha majadiliano baina ya  wadau hao  na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa  Serikali ambapo  wameazimia kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali zilizoibuliwa katika kikao hicho na kisha kupeana mrejesho. Kwa taarifa zaidi BOFYA HAPA

New song by AMINI "YA MOYONI"

Live: Mashindano ya Qur-an ya Dunia Yafanyika Diamond Jubilee jijini Dar es salaam

$
0
0

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-an Tanzania Sheikh Othman Ally Kaporo amesema kuwa jumuiya hiyo imetenga kiasi cha dola za kimarekani elfu 25 kwa ajili ya washindi watakaoibuka kwenye mashindano ya kimataifa ya kusoma Qur-an ambayo yanafanyika leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee.


Sheikh Kaporo ameeleza kuwa mashindano hayo ya sita kimataifa tangu waanze kuratibu yanataraji kuzishirikisha nchi 19 ambazo ni Kenya, Uganda, Mali, Nigeria, Algeria, South Africa, Bangladesh, Sudan, Kuwait, Libya, Djibouti, UAE, Russia Federation, USA, Yemen, UK, Dubai, Tanzania Bara na Visiwani (Zanzibar).

FUTARI YA KARIAKOO FAMILY DEVELOPMENT FOUNDATION (KFDF) 2017

$
0
0
 Kisomo wakati wa hafla ya futari ya Kariakoo Family Development Foundation iliyofanyika jana mtaa wa Tandamti na Livingstone na kuhudhiriwa na wanachama, masheikh wa Kariakoo, viongozi wa Saigon Sports Club, wajumbe kutoka Gogo vivu pamoja na watoto wanaolelewa kwenye vituo viwili vya Yatima vya Madina cha Tandale na cha Maalim Bonge kilichopo Jangwani.
 Misaada ilitolewa kwawatoto wanaolelewa kwenye vituo viwili vya Yatima vya Madina cha Tandale na cha Maalim Bonge kilichopo Jangwani
 Picha ya pamoja ya wanachama wa KFDF na watoto wanaolelewa kwenye vituo viwili vya Yatima vya Madina cha Tandale na cha Maalim Bonge kilichopo Jangwani
 Picha ya pamoja ya badhi ya wanachama wa KFDF
  Misaada ilitolewa kwawatoto wanaolelewa kwenye vituo viwili vya Yatima vya Madina cha Tandale na cha Maalim Bonge kilichopo Jangwani.Kwa taarifa kamili na picha zaidi BOFYA HAPA


NMB yafuturu na watoto yatima zaidi 450 Dar es Saalam

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na wa Kati wa Banki ya NMB, Omary Mtiga akizungumza na zaidi ya watoto 450 waliopo kwenye mfungo mtukufu wa Ramadhani kutoka vituo mbalimbali vya watoto yatima vya jijini Dar es Salaam walipojumuika pamoja katika futari na baadhi ya maofisa wa benki hiyo kwenye Ukumbi wa Shaan Robert. Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na wa Kati wa Banki ya NMB, Omary Mtiga (wa pili kulia) akitoa zawadi kwa watoto walioshiriki katika futari na baadhi ya maofisa wa benki hiyo kwenye Ukumbi wa Shaan Robert. Baadhi ya watoto waliopo kwenye mfungo mtukufu wa Ramadhani kutoka vituo mbalimbali vya watoto yatima vya jijini Dar es Salaam wakiwa katika futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwenye Ukumbi wa Shaan Robert.

"Dunia Sio Yetu" by Mzee Wangaka Ahmad Manyema (RiP)

$
0
0

Mkongwe wa muziki Wangaka Ahmad Manyema amefariki dunia leo katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. Kwa mujibu wa familia mazishi yake yatafanyika kesho Adhuhuri saa saba Mabibo Makutano jijini Dar es salaam.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AONGOZA HARAMBE YA UJENZI WA KANISA PAROKIA YA ZUZU, DODOMA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa niaba ya familia yake akimkabidhi Mchango wa Shilingi Milioni Kumi, Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda Kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Nyumba ya Paroko pamoja na kufanyia Ukarabati wa Kanisa Parokia ya ZUZU Dodoma. Kushoto ni Msaidizi wa Askofu Jimbo la Dodoma Baba Chesco Msaga . Harambe hiyo imefanyika June 17, 2017 katika Makazi ya Waziri Mkuu Mstaafu Pinda yaliyopo ZUZU nje kidogo ya Mjini Dodoma.
Waziri Mkuu Mstaafu,  Mizengo Pinda akiwaonyesha Wageni waalikwa (hawapo pichani) Shilingi Milioni Kumi Mchango aliokabidhiwa na Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa kwa niaba ya Familia yake , Kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Nyumba ya Paroko pamoja na kufanyia Ukarabati wa Kanisa Parokia ya Zinje (ZUZU) Dodoma. Kushoto ni Msaidizi wa Askofu Jimbo la Dodoma Baba Chesco Msaga . Harambe hiyo imefanyika June 17, 2017 katika Makazi ya Waziri Mkuu Mstaafu Pinda yaliyopo ZUZU Nnje kidogo ya mjini Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (Kushoto) akiwa ameongozana na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu Pinda walipo mpokea katika makazi yao yaliyopo Zuzu nje Kidogo ya Mjini Dodoma June 17, 2017, kuhudhuria Misa ya kumbukumbu ya Marehemu Mzee Exavery Pinda Baba Mzazi wa Mizengo Pinda, Pamoja na kuongoza Uchangiaji wa Ujenzi wa Nyumba ya Paroko na Ukarabati wa Kanisa la Parokia ya ZUZU. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

MHE. BALOZI WILSON MASILINGI KATIKA FUTARI YA PAMOJA YA WANA DMV, MAREKANI

$
0
0
Mwambata wa Jeshi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Canada, Col. Aldoph Mutta (kushoto) akimlaki Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi siku ya Jumamosi June 17, 2017 siku Mhe. Balozi alipokua mgeni rasmi kwenye futari ya pamoja inayoandaliwa na Jumuiya ya Waislam DMV (TAMCO) Silver Spring, Maryland.
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi akipokewa na mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislam DMV (TAMCO) ustaadh Ally Mohamed mara tu alipowasili na kujumuika na wanajumuiya hao waislam wa DMV na marafiki zao katika futari ya pamoja iliyofanyika siku ya Jumamosi June 17, 2017 Silver Spring, Maryland.
.
Kutoka kushoto ni Mwambata wa Jeshi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Canada, Col. Aldoph Mutta, mkuu wa idhaa ya Kiswahili Voice of America (VOA) Dr. Hmza Mwamoyo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi na The Maryland House of Delegates Legislative District 41 Baltimore City Mhe. Bilal Ali ambaye nae alialikwa na Jumuiya hiyo kwenye futari ya pamoja DMV.
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi na The Maryland House of Delegates Legislative District 41 Baltimore City Mhe. Bilal Ali wakiongozwa na  mkuu wa idhaa ya Kiswahili Voice of America (VOA) Dr. Hmza Mwamoyo kwenye futari ya pamoja iliyofanyika siku ya Jumamosi June 17, 2017 Silver Spring, Maryland.


WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AONGOZA MAZISHI YA MABAKI YA MWILI WA MAREHEMU YUSTINO NDUGAI, KONGWA MKOANI DODOMA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi mbele ya Jeneza lililowekwa mabaki ya mwili wa Marehemu Yustino Ndugai, Baba Mzazi wa Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai. Marehemu Yustino alifariki Mwaka 1992 na Mabaki yake yamezikwa upya June 17 , 2017 katika makaburi ya familia ya Ndugai Kijiji cha Chimoloto Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa akiweka Shada la Maua katika kaburi la mabaki ya mwili wa Marehemu Yustino Ndugai, Baba Mzazi wa Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai, yaliyozikwa  upya June 17 , 2017 katika makaburi ya familia ya Ndugai Kijiji cha Chimoloto Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.

WARIOBA :Msaidieni Rais tushinde Vita ya Rasilimali za nchi, Suala la Makinikia sio la Chama wala Siasa ni la Watanzania wote

$
0
0
Na Judith Mhina .


Wananchi hawahitaji mgawanyiko wa uongozi na malumbano wanataka maendeleo.Msaidieni Rais tushinde Vita ya Rasilimali za nchi
Suala la Makinikia sio la Chama wala Siasa ni la Watanzania wote

Hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli alipokea ripoti ya Kamati ya kwanza na ya pili ya uchunguzi wa makontena 277 ya mchanga wa madini (makinikia) yaliyokuwa njiani kusafirishwa nje ya nchi na uchunguzi ulifanyika na kulibaini ndani ya mchanga huo kuna dhahabu na madini mengine kwa asilimia kubwa.

Aidha, Mhe Rais amechukua hatua mbalimbali kulingana na ushauri wa kamati husika, pamoja na maamuzi yake kama Rais. Kutokana na sakata la hilo, Idara ya Habari-MAELEZO imepata fursa ya kufanya mahojiano na Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mstaafu Mheshimiwa, Jaji Joseph Sinde Warioba katika ofisi zake zilizopo Osterbay Jijini Dar-es-salaam.

SWALI: Ninanukuu maneno ya Baba wa Tafa, Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere kuhusu raslimali za nchi na hususan madini alisema: “Madini yetu tuliyonayo ni vema kuyaacha mpaka Watanzania watakapokuwa na ufahamu wa kutosha wataamua kuyachimba” mwisho wa kunukuu nini maana yake?

JIBU: Mara baada ya Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 Hayati, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipokea nchi kama Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanganyika huru akiwa hana wataalamu zaidi ya madaktari 2 na yeye mwenyewe ambaye alikuwa msomi kutoka chuo Kikuu cha Edinburg Uingereza. Kwa hali hiyo, Mwalimu alikuwa sahihi usingeweza kuruhusu rasilimali za nchi mfano madini kuchibwa na wageni kutoka nje maana yake Watanganyika wangekuwa watazamaji tu bila kufaidika na lolote.

Mwalimu alihakikisha anawekeza katika elimu ambayo ilikuwa bure kuanzia msingi hadi chuo kikuu elimu ndio msingi wa kuondoa Ujinga Umasikini na Maradhi. Alitambua Watanganyika wakielimika na kupata utaalamu wa madini ikiwani pamoja na uchimbaji watakuja kuyachimba na kufaidika.

SWALI:Tanzania ni kati ya nchi zilizobarikiwa kuwa na raslimali nyingi za kila aina kuanzia madini, gesi, wanyamapori na hifadhi, misitu, milima, maporomoko ya maji, mabonde maziwa makubwa kwa madogo, bahari ya hindi na raslimali za mazao ya uvuvi, nchi yenye ardhi ya kutosha watanzania wenye uwezo wa kufanyakazi kwa ufanisi . Unadhani nini tatizo letu, nini cha kufanya?

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BENKI YA DTB, EFM RADIO WATOA MSADA WA MADAWA TAASISI YA MIFUPA MOI

$
0
0
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said.

BENKI ya DTB kwa kushirikiana na EFM Radio kupitia kipindi chake cha “Bustani ya Watoto”, wametoa msada wa madawa mbalimbali kwa Taasisi ya Mifupa MOT iliyoko Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam, leo Juni 18, 2017.

Akikabidhi madawa hayo, Afisa Uhusiano wa EFM Radio, Bi.Jesca Mwanyika alisema, EFM kupitia kipindi chake cha watoto cha “Bustani ya Watoto” iliamua kuwashirikisha DTB ili kuona ni namna gani wanaweza kusaidia watoto waliolazwa kwenye Taasisi ya MOI hususan wale wenye matatizo ya kichwa kikubwa na mgongo wazi.

“Sisi kama EFM Radio tuna kipindi cha watoto cha Bustani ya Watoto, tumeona kwa vile tunashughulika na watoto, na kwa vile siku chache zilizopita Dunia iliadhimisha siku ya mtoto wa Afrika Duniani, basi tumeona tutoe kiasi hiki cha madawa kuwasaidia watoto hawa wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi waliolazwa hapa MOI.”Alisema Bi. Jesca.

Akizungumza kwa niaba ya DTB, Afisa Masoko wa benki hiyo, Bw.Baguma Ambari alisema, Benki kama taasisi inayotoa huduma kwa wananchi, inao wajibu mkubwa kutoa sehemu ya faida yake kusaidia jamii na hivyo imefurahishwa kuungana na EFM Radio katika kutoa msada huo wa madawa ambao anaamini utasaidia katika kuwahudumia watoto hao wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa MOI, Dkt.Respicious Boniface, (kulia), akipokea sehemu ya msada wa madawa kutoka kwa Meneja wa Benki ya DTB Tawi la Morocco jengo la Airtel, jijini Dar es Salaam, Bi.Sheena .Y. Sinare, kwenye jengo jipya la MOI, leo Juni 18, 2017. DTB kwa kushirikiana na EFM Radio, wametoa msada wa madawa mbalimbali yenye thamani ya shilingi milioni 4 ili kusaidia watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi wanaopatiwa matibabu kwenye taasisi hiyo
 Dkt. Boniface, akipokea sehemu ya msada wa madawa kutoka kwa Afisa Uhusiano wa EFM Radio, Jesca Mwanyika kwenye jengo jipya la MOI jijini Dar es Salaam leo Juni 19, 2017. EFM kwa kushirikiana na Benki ya DTB wametoa msada huo wa madawa yenye thamani ya shilingi milioni 4 ili kusaidia watoto wenye matataizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi wanaopatiwa matibabu kwenye taasisi hiyo
 Mtayarishaji wa kipindi cha "Bustani ya Watoto" kinachopeperushwa na EFM, ambaye ndiye chachu ya kutolewa kwa msada huo, Bi. Flora Amon maarufu kama  Aunt FIFI, akikabidhi sehemu ya msada huo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Precious Boniface

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Mkulima wa Handeni Tanga ajinyakulia Sh Milioni 20 za Biko

$
0
0

MAMBO yamezidi kunoga katika bahati nasibu ya ‘SMS’ ya Biko, ‘Ijue Nguvu ya Buku’, baada ya mkulima kutoka wilayani Handeni, mkoani Tanga, Yahaya Ally Khamis, kuibuka kidedea kwa kuzoa Jumla ya Sh Milioni 20 kutoka kwenye bahati nasibu hiyo inayozidi kushika kasi nchini Tanzania, ikiwa ni droo yake ya 15 tangu kuanzishwa kwake.

Bahati nasibu hiyo imechezeshwa leo jijini Dar es Salaam na Balozi wa Biko, Kajala Masanja kwa kushirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humud Abdulhussein.

Akizungumza katika droo hiyo, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba bahati nasibu yao imezidi kupanua mbawa zake kwa kutua wilayani Handeni, mkoani Tanga kwa mshindi wao Yahaya ambaye ana umri wa miaka 50 anayejishughulisha na kilimo.

Alisema ni faraja yao kuona mchezo wao umekuwa ukitoa washindi katika sehemu mbalimbali za Tanzania, akiamini kuwa ni mwendelezo wa kuhakikisha kwamba kila mtu anaibuka na mamilioni ya Biko.

“Tunafarijika sana kuona mkulima wa Handeni Tanga naye ameibuka na mamilionin ya Biko, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linaweza kumpatia utajiri mkubwa kwa kuzitumia fedha hizi kwa umakini katika shughuli zake za ukulima, ukizingatia kuwa amepatikana kwa kucheza Biko ambao ni mchezo rahisi kwa kuingiza namba ya kampuni 505050 na ile ya kumbukumbu ambayo ni 2456, huku kiasi cha kucheza kikianzia Sh 1000 na kuendelea.


Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini Tanzania, Humud Abdulhussein kushoto, akiagana na Balozi wa Biko, Kajala Masanja mara baada ya kumaliza kuchezesha droo ya 15 leo jijini Dar es Salaam, ambapo mkulima wa wilayani Handeni, mkoani Tanga, Yahaya Ally Khamis aliibuka kidedea kwa kuzoa jumla ya Sh Milioni 20.

Balozi wa Biko Kajala Masanja akichezesha droo ya 15 ya Bahati Nasibu ya Biko ambayo donge nono la Sh Milioni 20 liliangukia kwa mkulima wa wilayani Handeni, mkoani Tanga, Yahaya Ally Khamis baada ya kuchezeshwa droo hiyo jana, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humud Abdulhussein.


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

TGGA YAENDESHA KAMBI YA MAFUNZO YA MTOTO WA KIKE KUJIAMINI, KUJITAMBUA NA KUWA JASIRI

$
0
0


Na Richard Mwaikenda

MAFUNZO ya kujiamini na kujitambua kwa mtoto wa kike yamepamba moto katika kambi maalumu inayoendelea eneo la Mombasa, Ilala, Dar es Salaam.

Kambi hiyo iliyoandaliwa na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), inashirikisha walimu na viongozi wa chama hicho kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Akizungumza na mwandishi wetu aliyetembelea kambi hiyo leo,Kamishna wa TGGA,Mkoa wa Tanga, Modesta Mshata alisema kuwa lengo la kambi hiyo ni kuwajengea uwezo walimu na viongozi wa kujiamini na kujitambua.

"Tunata mtoto wa kike popote alipo ajiamini, ajitambue na kuwa jasiri ikiwemo pia kumudu maisha kwa kushirikiana vyema na jamii inayomzunguka."Alisema Mshata.

Pia alisema kuwa, lengo ni kumfundisha mtoto wa kike kuwa mama na kiongozi bora wa familia na taifa kwa ujumla. Washiriki 36 wa kambi hiyo ya siku tano wanatoka Kondoa, Dodoma, Tanga, Lindi, Rukwa na Dar es Salaam pamoja na nchi za Uganda, Rwanda na Madagascar.

Washiriki wa Kambi ya Mafunzo ya kuwajengea uwezo wanawake wakiimba  wimbo wa Taifa baada ya kujifunza jinsi ya kufunga kamba vifundo na kupandisha bendera ya Taifa katika kambi ya siku tano iliyoandaliwa na Tanzania Girl Guides Association (TGGA), Mombasa, Dar es Salaam
Wakiimba wimbo wa Taifa

Walimu na viongozi wa chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), wakijenga mahema kwa ajili ya kambi ya kumjengea uwezo mtoto wa kike yaliyoandaliwa na TGGA, Mombasa, Dar es Salaam jana. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Wakijifunza kufunga vifundo kwenye mti.

SINGIDA UNITED YA MSAJILI MFUNGAJI BORA WA RWANDA

$
0
0
Singida United ya Msainisha mkataba wa miaka miwili mfungaji bora kutoka nchini Rwanda Danny Usengimwana, ambaye anachezea timu ya Polisi fc pamoja na timu ya Taifa ya Rwanda.

KIJANA ABDULMJID MUJAHID KUTOKA YEMEN AMEIBUKA MSHINDI WA MASHINDANO YA KIMATAIFA YA QUR-AN

$
0
0
KIJANA Abdulmjid Mujahid kutoka Yemen ameibuka mshindi wa mashindano ya kimataifa ya Qur-an yaliyozishindanisha nchi kumi ambapo mshindi  amezawadiwa dola 5000 za kimarekani huku ubalozi wa Kuwait ukimzawadia dola 500, mshindi wa pili wa mashindano hayo ni Omary Abdallah kutoka Tanzania ambaye nae amezawadiwa dola 4000 na dola 300 kutoka ubalozi wa Kuwait.

Mashindano hayo yameshirikisha nchi kumi zikiwemo Uganda, Mali, Tanzania Bara, Yemen, Russia, Uingereza, Libya, Bangladesh, Marekani na Jumuiya ya Falme za kiarabu (United Arab Emirates).
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd akimkabidhi hundi ya dola za Kimareni 5,000 mshindi kwanza wa mashindano ya kimataifa ya Qur-an Abdulmjid Mujahid kutoka Yemen leo jijini Dar es Salaam. 

Pia Mashindano hayo yameudhuriwa na viongozi mbalimbali yakiongozwa na makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddy, na mlezi wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-an Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi, Muft Mkuu wa Tanzania Abubakar Zuber, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum, mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete na mgeni maalum kutoka Saudi Arabia Abdallah Basfar ambaye ni msomaji Qur-an wa kimataifa.

Akihutubia katika mashindano hayo Makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Ally Seif Iddy ameeleza kuwa vijana wamekosa adabu na matendo ya ulawiti, mauaji kwa watoto wachanga, unyanyasaji, mauaji ya wenye ulemavu wa ngozi yamekuwa yakiripotiwa, huku akieleza kuwa aamini kama Mwenyezi Mungu anayaridhia matendo haya, hivyo tabia za watanzania na waislamu ziendane na maamrisho ya Qur-an.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd akimkabidhi hundi ya dola za Kimareni 4,000 mshindi pili wa mashindano ya kimataifa ya Qur-an wa Tanzania,Omary Abdallah leo jijini Dar es Salaam. 

Pia Makamu wa Rais Balozi Seif Ally Iddy ameongeza kuwa mbora ni mwenye kujifunza Qur-an na akawafundisha wengine Mwenyezi Mungu amewanasihi waislamu katika kitabu chake kitukufu.

Rais mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ally Hassan Mwinyi awapongeza wanafunzi wa kiislamu wanaojifunza Qur-an kwani kufanya hivyo ni kuiendea jamii njema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-an Tanzania Sheikh Othman Ally Kaporo amewataka wadau wa masuala ya Qur-an kuhakikisha Qur-an inakaa katika nyoyo za vijana ili jamii iweze kuwa bora na kuheshimiana wakubwa kwa wadogo.
Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ally Hassan Mwinyi, akipokea tuzo ya heshima kutoka Muft wa Tanzania Abubakar Zuber iliyotolewa na Jumuiya ya kuhifadhisha Qur-an Tanzania katika mashindano ya kimataifa ya kusoma Qur-an yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo.PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA, GLOBU YA JAMII.

Huku Muft Mkuu wa Tanzania Abubakari  amesema ni vyema watu wakajifunza Qur-an kwasababu ni dawa ya kila tatizo, endapo waja wataifuata kwa mafunzo yaliyoamrishwa na kuacha yaliyokatazwa, kwani Qur-an imekataza kuuana, kuchukiana, kuvuruga amani.


TAIFA LA WATU WAADILIFU HUANZIA KWENYE FAMILIA - WAZIRI MKUU

SPIKA NDUGAI AONGOZA WABUNGE KATIKA HARAMBEE YA UJENZI WA JENGO LA JUMUIYA YA KIKRISTO TANZANIA TUKIO LILILOFANYIKA LEO MJINI DODOMA.

$
0
0


Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza jambo kabla ya kuanza harambee kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Jumuiya ya kikristo Tanzania, tukio lililofanyika leo Mjini Dodoma. kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Mizengo Pinda na katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya kikristo Tanzania, Askofu Dkt. Alex Malasusa 
Waziri Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Mizengo Pinda (wa pili kushoto) akizungumza jambo baada ya kumalizika kwa harambee kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Jumuiya ya kikristo Tanzania, kulia ni Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah, kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya kikristo Tanzania, Askofu Dkt. Alex Malasusa na wa pili kulia ni Ndg. Elton Mapesa Mwakilishi wa Harambee kutoka External Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya kikristo Tanzania, Askofu Dkt. Alex Malasusa kabla ya kuanza harambee kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Jumuiya ya kikristo Tanzania, katika tukio lililofanyika leo Mjini Dodoma, Spika Ndugai pia ni Mgeni rasmi na aliongoza Wabunge katika harambee hiyo. 
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kulia)akiongoza Wabunge Mbali mbali kucheza nyimbo ya injili kama njia moja wapo ya kuhamasisha uchangiaji kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Jumuiya ya kikristo Tanzania, tukio lililofanyika leo Mjini Dodoma 

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JUNE 19,2017

Hamidu City Park ya Kigamboni Yawaandalia futari Waislamu, ndugu jamaa na marafiki

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni,Hashim Mgandilwaakimshukuru Bw. Hamodu H. Mvungi mara baada ya kushiriki katika futari hiyo pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria.
Bw. Hamidu H. Mvungi miliki wa kijiji cha Hamidu City Park, Mikwambe Kibada Kigamboni chenye nyumba 1500 akizungumza na wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria katika futari aliyowaandalia wageni wake wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mh .Hashim Mgandilwa ambapo aliwashukuru wageni waalikwa hao kwa kujumuika naye katika futari hiyo katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan, huku akiwatambulisha makazi hayo yenye nyumba za kuuza ambapo ameshirikiana na mabenki mbalimbali na kukopesha kwa watu wanaohitaji nyumba katika kijiji hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni,Hashim Mgandilwa na Mwenyeji wake Bw. Hamidu Mvungi wakiongoza wageni waalikwa katika futari hiyo.
Baadhi ya wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria katika futari hiyo wakichukua chakula.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni,Hashim Mgandilwa katikati , Mwenyeji wake Bw. Hamidu Mvungi pamoja na wageni wake wakipata futari.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Rahel Mhando pamoja na wageni mbalimbali waalikwa wakishiriki katika futari hiyo iliyoandaliwa na Bw. Hamidu Mvungi nyumbano kwake Kigamboni.

WAZIRI MAGHEMBE AZINDUA MRADI WA UHIFADHI NA MAENDELEO YA IKOLOJIA YA PORI LA AKIBA LA SELOUS (SECAD) ULIOFADHILIWA NA SERIKALI YA UJERUMANI

$
0
0
NA HAMZA TEMBA - WMU

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe kwa kushirikiana na Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Egon Konchanke amezindua Mradi wa Uhifadhi na Maendeleo ya Ikolojia ya Pori la Akiba la Selous SECAD (Selous Ecosytem Conservation and Development Program) ambao umefadhiliwa na Serikali ya Ujerumani kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania, mradi huo utatekelezwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, WWF (World Wildlife Fund) na FZS (Frankfurt Zoological Society).


Akizungumza katika hafla iliyofanyika jana, Matambwe na Tagalala Selous, Mkoani Morogoro, Waziri Maghembe alisema Serikali ya Ujerumani kupitia benki ya KFW imechangia Euro Mil. 18 (sawa na Shilingi Bil. 45.124) katika mradi huo wa miaka mitano huku mashirika ya WWF (World Wildlife Fund) na FZS (Frankfurt Zoological Society) yakichangia Euro laki 4 kila moja (sawa na Shilingi bil. 2.005) katika mradi huo. Pamoja na uzinduzi huo alizindua pia Mpango Kazi wa Dharura wa kuendeleza pori hilo.


"Mradi huu ni muhimu sana kwakua utasaidia kuongeza nguvu kwenye jitihada zetu za kuendeleza na kuimarisha hifadhi ya pori hili la Selous ikiwemo upatikanaji wa vitendea kazi muhimu pamoja na kutuongezea nguvu kwenye mapambano dhidi ya ujangili", alisema Prof. Maghembe.


Alisema jitihada ambazo Serikali imeshazifanya katika pori hilo ni pamoja na kuimarisha doria za ndege zenye rubani na zisizo na rubani (drones), kutoa mafunzo ya jeshi usu kwa askari, kuongeza maaskari pamoja na vitendea kazi ambapo katika mwaka ujao wa fedha Serikali itatoa magari mengine 15 kusaidia pori hilo.


"Pamoja na jitihada hizo tunawekeza dola za kimarekani Milioni 156 (sawa na Shilingi bilioni 349.441) kwa ajili ya kuboresha pori hili (Selous), Ruaha, Mikumi, Rungwa na Kitulo kuhakikisha watalii wanatembelea maeneo haya na kuondoa kile kikwazo cha wao kutotembelea hifadhi za kusini, hiyo inaenda sambamba na kuimarishwa kwa shirika la ndege la Serikali la Air Tanzania na kuondoa changamoto iliyokuwepo ya usafiri wa anga", alisema Prof. Maghembe. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizindua Mradi wa Uhifadhi na Maendeleo wa Ikolojia ya Pori la Akiba la Selous (SECAD) ambao umefadhiliwa na Serikali ya Ujerumani kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania katika hafla iliyofanyika jana Matambwe, Selous Mkoani Morogoro. Wanaoshudia kulia kwake ni Balozi wa Ujerumani, Egon Konchanke, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili, Meja Jenerali Gaudence Milanzi na Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Prof. Faustin Kamuzora.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori wa Wizara hiyo, Prof. Alexander Songorwa Mpango Kazi wa Dharura wa Kuendeleza Pori la Akiba la Selous baada ya kuuzindua sambamba na mradi wa Uhifadhi na Maendeleo ya Ikolojia ya Pori la Akiba la Selous (SECAD). Kulia kwake ni Balozi wa Ujerumani, Egon Konchanke, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi, Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Prof. Faustin Kamuzora, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, Martin Loibooki na Muwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Dkt. Dembe. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) na  Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Egon Konchanke wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa magari sita aina ya Land Cruiser ambayo ni sehemu ya Mradi aliouzindua wa Uhifadhi na Maendeleo ya Ikolojia ya Pori la Akiba la Selous (SECAD).
 Magari sita aina ya Land Cruiser yaliyotolewa na Serikali ya Ujerumani kama sehemu ya mradi wa SECAD.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Mghembe (kushoto) akipokea zawadi ya picha yenye ujumbe wa Mashujaa wa Kuokoa Selous kutoka kwa Mkurugenzi wa Afrika wa WWF Ujerumani, Philipp Goltenboth (kulia). Anaeshuhudia katikati ni Mkurugenzi Mkaazi wa WWF Tanzania, Dkt. Amani Ngusaru.
Taswira mwanana ya baadhi ya Twiga ndani ya Pori la Akiba la Selous.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images