Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110029 articles
Browse latest View live

UNESCO YATOA TAHADHARI ONGEZEKO LA JANGWA

$
0
0
Nchi yetu. Nyumba zetu. Mustakabali wetu. Hii lazima iwe kauli mbiu yetu leo - hasa katika mapambano dhidi ya kuenea kwa jangwa. Mchango wa mabadiliko ya mazingira katika uhamiaji na makazi ya watu uko wazi duniani kote. Idadi kubwa ya 'wakimbizi wa mazingira' sasa huwasilishwa kama moja ya matokeo makubwa ya mabadiliko ya hali ya hewa na kuenea kwa jangwa. 

Na hili hii inategemewa kundelea kuongezeka. Kufikia 2030, Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Kuenea kwa Jangwa imeonya kuwa, kufikia mwaka 2030 watu wapatao milioni 135 wako katika hatari ya kuhama makazi yao kwa sababu ya kuenea kwa jangwa, na watu milioni 60 wanatarajiwa kuhama kutoka Kusini mwa jangwa la Sahara kuelekea Afrika ya Kaskazini na Ulaya. 

Utabiri huu unaonyesha kuwa sehemu zilizo kame na zile zilizo kame zaidi huathirika zaidi na kuenea kwa jangwa na kuhama kwa watu. Watu wanaokaa vijijini amabao hutegemea ufugaji wa wanyama, kilimo na maliasili watakuwa katika hatari zaidi ya kuwa wahanga wa athari hizo, ambazo hujumuisha umaskini, kudorora kwa elimu, ukosefu wa uwekezaji, umbali kutoka huduma muhimu, na kutengwa.

 Ni lazima tukabiliane na hali hii na hii inamaanisha kufanya kazi katika ngazi mbili: Kwanza, ni lazima tusimamie ardhi kwa usahihi,hii ni muhimu katika kuzuia kuenea kwa jangwa na katika kulinda kiwango chake cha uzalishaji. 

Hifadhi ya Bayongahewa ya Las Bardenas Reales ya UNESCO iliyoko nchini Hispania inaonyesha kwamba usimamizi wa ardhi kame unaotumia taarifa sahihi, kwa kuzingatia kupishana kati ya matumizi ya malisho, ukulima na vipindi ya bila ya kuilima ardhi hupelekea si tu kusitisha kuwepo hali ya kuenea kwa jangwa lakini pia huleta uwezekano wa kurejesha ardhi kama ilivyokua awali. 

Hii ndio sababu Programu ya Kimataifa ya UNESCO ya Nishati-Maji imejikita katika kujenga uwezo na kutoa mwongozo wa sera na zana za kushughulikia ukame, kuenea kw jangwa na changamoto zinazotikana na hayo, hasa kuhusiana na usimamizi wa rasilimali maji, kwa njia ya Mtandao wa Kimataifa unaohusika na Maji na Maendeleo ya Taarifa ya Ardhi Kame (G- WADI). 

Pili, inatupasa kuimarisha ustahimilivu wa watu walio katika mazingira hatarishi kwa kuwawezesha kuwa na njia mbadala za kujipatia kipato ili tuweze kuuharibu mduara wa kuenea kwa jangwa na madhara yake ya kijamii na kiuchumi ambayo mara nyingi husababisha watu kuyahama makazi yao. Katika kutafuta na kuendeleza elimu na kujenga uwezo katika sayansi, teknolojia na uhandisi, kwa wasichana na wavulana katika nchi zilizo katika hatari zaidi, 

Programu ya Sayansi ya Msingi ya Kimataifa ya UNESCO inafanya kazi ya kujenga fursa mpya za ajira kwa vijana, kupunguza utegemezi wa rasilimali zinazotegema hali ya hewa, ili kuwapatia watu maisha yenye ustahimivu katika makazi yao. 

Katika siku hii, ni lazima tutambue kuwa hali ya kuenea kwa jangwa ni jambo la kimataifa ambalo linalomtishia kila mtu na ni lazima lishughulikiwe kwa pamoja ili kujenga mustakabali endelevu na imara kwa wote. Ujumbe kutoka kwa Bi. Irina Bokova, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO katika Maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Kuenea kwa Jangwa na Ukame Duniani, 17 Juni 2017.

DKT. MABODI: CCM INAFANYA SIASA ZA USHINDANI WA SERA ZA MAENDELEO.

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar , Abdulla Juma Saadalla “ Mabodi” amesema CCM itaendelea kufanya ushindani wa sera za maendeleo zitakazowanufaisha wananchi wa makundi yote mijini na vijijini.

Kauli hiyo ameitoa wakati akifungua Mafunzo ya Wanawake na Uongozi kwa wanachama na viongozi wa UWT Mkoa wa Mjini huko Amani Zanzibar, Dkt. Mabodi alisema wananchi wa visiwa vya Zanzibar kwa sasa wanachohitaji ni siasa za ushindani wa kisera katika kukuza kipato cha mwananchi mmoja mmoja hadi taifa kwa ujumla.

Dkt. Mabodi alisema taifa lolote linalotamani kuendelea kiuchumi ni lazima wananchi wake wakubali kwa vitendo dhana ya siasa za ustaarabu katika kudumisha amani na utulivu wa nchi ili kufanya kazi za kujiongezea kipato na kukuza uchumi wa nchi.

Aidha Naibu Katibu Mkuu huyo alisema ushindi wa CCM katika chaguzi mbali mbali za dola unatokana na nguvu za Wanawake wa UWT katika kuunga mkono harakati mbali mbali za kisiasa hadi kuhakikisha chama kinaingia madarakani.

“ kila mtu ndani ya Chama Chetu anajua na kutambua mchango wa Wanawake katika medali za kisiasa, wao ndio wamekuwa mstari wa mbele kwa kila kitu ikiwemo kujitokeza kwa wingi kupiga kura halali za kuiletea ushindi CCM.

Pia nakuahidini kwamba nitaendelea kuwa nanyi bega kwa bega kwa lengo la kuimarisha chama na jumuiza zake sambamba na kuwaletea wananchi maendeleo ya kudumu.”, alisema Dkt. Mabodi.

Majeruhi wa shule ya Lucky Vincent ya arusha kurejea nchini Agosti

$
0
0
 Watoto watatu walionusurika katika ajali iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva wa Shule ya Lucky Vincent ya mjini Arusha, huenda wakaruhusiwa kurejea nchini baada ya miezi miwili.
Taarifa hiyo imetolewa na Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu katika mtandao wake wa kijamii wa Facebook.
Pia, Nyalandu ameandika katika mtandao huo kuwa watoto hao; Doreen Mshanga, Saidia Ismael na Wilson Tarimo wanategemewa kutembea tena.
Hata hivyo, kwa sasa Doreen, atahamishiwa katika kituo maalumu kwa ajili ya matibabu ya uti wa mgongo cha Madonna katika mji wa Lincoln, Nebraska.
“Katika watoto wote hao watatu, Doreen ni muujiza mkubwa zaidi,” amesema Nyalandu.

MAGIC FM BAMIZA TOP 20 COUNT DOWN JUNE 17TH 2017

MBUNGE VITI MAALUMU MKOA WA SHINYANGA MHE.LUCY MAYENGA AKICHANGIA BUNGENI

MHADHIRI MAARUFU WA KENYA PROFESA PLO LUMUMBA AKIONGEA JIJINI DAR ES SALAAM

Sheikh Shariff Kusoma Dua maalum Dar es salam jumamosi ijayo

$
0
0
Sheikh Shariff Majini siku ya Jumamosi tarehe 24-06-2017 sawa na Ramadhani 29 ataendesha Dua nzito kwa ajili ya kuuaga mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika ukumbi wa Star Light Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam.

Dua hiyo ni maalum hasa kwa kina mama na itaafanyika kuanzia asubuhi saa mbili mpaka saa sita mchana ili kutoa fursa kwa wataohudhuria kuwahi kuandaa futari.
Mara baada ya kumalizika kwa Dua, Sheikh ataenda Jijini Arusha kwa mwaliko maalum wa Baraza la Eid siku ya Eid Pili. Baraza la Eid litafanyika katika viwanja vilivyopo jirani na soko la Kilombero na Stand ya Hiace Jijini Arusha.
Sheikh atarejea Dar es salaam mara tu baada ya kumalizika kwa Baraza la Eid.

KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCO DKT. TITO MWINUKA AWAHAKIKISHIA WATANZANIA MRADI WA UMEME WA GESI ASILIA WA KINYEREZI II UNAENDELEA KWA KASI

$
0
0
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA la Umeme Nchini, (TANESCO), limewahakikishia watanzania kuwa mradi wa umeme wa gesi wa Kinyerezi II unaendelea kwa kasi kubwa na utakamilika kama ilivyopangwa.
Hakikisho hilo limetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito E. Mwinuka, wakati wa ziara yake ya kutembelea mradi wa umeme wa gesi wa Kinyerezi II jijini Dar es Salaam, ambao unatarajiwa kutoa Megawati 240 za umeme.
“Niwahakikishie watanzania kuwa ifikapo Agosti mwakani (2018), mradi wa umeme Kinyerezi II utakamilika na hivyo tutaongeza Megawati 240 kwenye gridi ya Taifa.” Alisema Dkt. Mwinuka wakati akitoa majumuisho ya ziara yake.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito E. Mwinuka (katikati), akiongozana na  Meneja wa mradi wa upanuzi wa Kinyerezi I, Mhandisi   Simon Jilima,(kushoto) na Meneja Mwandamizi wa Miradi wa TANESCO, Mhandisi Gregory Chegere, wakitembelea kukagua maendeleao ya ujenzi wa mradi wa Kinyerezi II na ule wa upanuzi wa Kinyerezi I jijini Dar es Salaam, leo Juni 17, 2017.

Sehemu ya mitambo hiyo
 DKT. Mwinuka, (kulia), Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia miradi, Mhandisi Khalid James, (katikati) na Meenja Mradi wa Kinyerezi II, Mhandisi Stephen A.S.Manda, wakijadiliana jambo
 Mitambo ikiteremshwa eneo la ujenzi
 Mkurugenzi wa Business Times, Imma Mbuguni, (kulia) akizungumza jambo na Mhandisi, Khalid James.
Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

Serikali yaipongeza Tulia Trust kwa kusomesha vijana mafunzo ya Sanaa Bagamoyo

$
0
0
Serikali yaipongeza Tulia Trust kwa kusomesha vijana mafunzo ya Sanaa Bagamoyo Serikali kupitia Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo imepongeza juhudi za Taasisi ya Kijamii ya Tulia Trust kwa kuwezesha kusomesha vijana 20 masomo ya Sanaa na Utamaduni katika taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) huku akiziomba taasisi za wadau wengine kuiga mfano huo. 
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya masomo kwa vijana hao 20 waliodhaminiwa na Tulia Trust, Kaim Mkurugenzi Idara ya Sanaa Bi. Leah Kilimbi,ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Wizara hiyo,amewataka vijana hao kuwa Mabalozi wazuri ili wakawafundishe na wengine kile walichojifunza hapo. 
“Sisi kama Serikali, tunafarijika sana kwa namna wadau wanavyosaidiana nasi katika kuleta maendeleo katika Nyanja mbalimbali. Taasisi ya Tulia Trust imeonyesha nia na tunaipongeza sana kwani imesaidia vijana wetu kujifunza Sanaa, Utamaduni na kila aina ya mafunzo. Tunaamini huko waendako watakuwa mabalozi wazuri sana pia wadau wengine waige mfano huu” alieleza Bi. Leah Kilimbi. 
Kaimu Mtendaji Mkuu wa TaSUBa, Gabriel Kiiza akizungumza katika tukio hilo la ukabidhiwaji wa vyeti kwa vijana hao 20 waliofadhiliwa kwa msaada wa Tulia Trust. Tukio limefanyika chuoni hicho Juni 16.2017, Mjini Bagamoyo.
Balozi wa Tulia Trust Hassan Ngoma akizungumza katika tukio hilo la ukabidhiwaji wa vyeti kwa vijana hao 20 waliofadhiliwa kwa msaad wa Tulia Trust. Tukio limefanyika chuoni hicho Juni 16.2017, Mjini Bagamoyo.
Baadhi ya vijana hao wakiwa katika maonesho yao maalum ikiwemo ya upigaji wa ngoma na kucheza wakati wa kuhitimu mafunzo yao
Vijana hao wakikabidhi risala yao kwa uongozi wa Tulia Trust.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNE 18,2017

Tanzania Day Journey with Mboni Show

KANDA YA KATI (DODOMA) YAVUKA MALENGO MAKUSANYO YA KODI YA PANGO LA ARDHI

$
0
0
Kanda ya kati (Dodoma) imekusanya kiasi cha Tshs. 1,426,273,033.70 ya Makusanyo ya Kodi ya Pango la Ardhi, sawa na 204% ya malengo na hivyo kuvuka malengo iliyopangiwa. Kamishna Msaidizi wa Ardhi, kanda ya kati Dodoma; Hezekiel Kitillya ameeleza wakati akizungumza na Waandishi wa Habari. 

Kamishna Kitillya alisema; tathimini iliyofanyika ni ya mpaka 31 Mei, 2017. Malengo ya Makusanyo yaliyokuwa yamepangwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17 - 30 Juni, 2017 yalikuwa ni kukusanya kodi ya Tshs. Bilioni111.77, ambapo kati ya kanda nane za ardhi zilizopo nchini, kanda ya kati ilipangiwa kukusanyaTshs. Milioni 700.

Vile vile,  baadhi ya Halmashauri tayari zimeshavuka malengo ya makusanyo zilizowekewa, kama vile Manispaa ya Dodoma,  malengo yalikuwa Tshs. 200,000,000/= na makusanyo yakawa;  Tshs.678,804,841.40, Manispaa ya Singida, malengo yalikuwa Tshs. 200,000,000/= na makusanyo yakawa Tshs.308,392,069.17 na Halmashauri ya Manyoni, malengo yalikuwaTshs. 100,000,000/= na makusanyo yakawa Tshs. 117,200,000.00. Pia Halmashauri nyingine za Wilaya ya Itigi, Chamwino, Bahi; nazo zimeshavuka malengo na nyingine zilizobaki zikikaribia kufikia malengo.

Akieleza moja ya mkakati muhimu ambao umewezesha kanda yake kuvuka malengo ni pamoja na kusambaza hati za madai Demand notes. Alisema; “Halmashauri zote zilielekezwa kuandaa na kusambaza hati za madai kwa wadaiwa wakubwa sugu”.

Akizungumzia moja ya changamoto Kuu inayokabili zoezi la Makusanyo; Alisema ni Wananchi kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu tofauti ya Kodi ya Pango la Ardhi na Kodi ya Majengo, ambapo Wananchi wengi hudhani wakishajenga nyumba na kuanza kulipa kodi ya jengo, hawapaswi tena kulipa kodi ya pango la Ardhi.

Aidha, Kamishna Kitillya ametoa wito kwa Wananchi kuhamasika kulipa Kodi ya Pango la Ardhi kwa mujibu wa Sheria na kwa Maendeleo ya Taifa.  Aliongeza kuwa; “Sasa Kodi ya Pango la Ardhi imeboreshwa kwa kumuwezesha mwananchi kutambua kiasi anachodaiwa na kufanya malipo hayo kieletroniki, kwa kutumia Tovuti ya Wizara au simu kwa tigo pesa au m-pesa, tofauti na ilivyokuwa awali ambapo Mwananchi alilazimika kufika katika vituo vya malipo, katika Halmashauri yake”.

Kanda yakati (Dodoma) inahudumia mikoa miwili (2) Dodoma na Singida yenye jumla ya Halmashauri kuminatano (15).

Kamishna wa Ardhi msaidizi – Kanda ya Kati (Dodoma); Hezekiel Kitillya akizungumza na  A Fm Radio -  92.9 – Dodoma;  kuhusu Tathimini ya Malipo ya Kodi ya Pango la Ardhi ya Kanda na Maboresho ya ulipaji wa Kodi hiyo kwa njia ya Kielektroniki.

 Mwananchi akifurahia kupata elimu na kupatiwa kipeperushi kwa elimu zaidi kuhusu Kodi ya pango la Ardhi katika mojawapo ya Saloon za kusuka, mjini Dodoma.

 Vipeperushi vya kuelimisha jamii kuhusu  Kodi ya Pango la Ardhi vikigaiwa kwa Wananchi katika Stand ya Mabasi mjini Dodoma

  Vipeperushi vya kuelimisha jamii kuhusu  Kodi ya Pango la Ardhi vikigaiwa kwa Wananchi katika Stand ya Mabasi mjini Dodoma
Kamishna wa Ardhi msaidizi – Kanda ya Kati (Dodoma); Hezekiel Kitillya akizungumza na  Waandishi wa habari kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi yake, Tathimini ya Malipo ya Kodi ya Pango la Ardhi ya Kanda na Maboresho ya ulipaji wa Kodi hiyo kwa njia ya Kielektroniki. Kushoto kwake ni Mwanasheria na Afisa Ardhi mwandamizi; Jane Kapongo na kulia kwake ni Msajili wa Hati katika kanda hiyo; Geoffrey Mauya.

JK akutana na Mwadhama Policarp Kadinali Pengo

$
0
0
Akiwa njiani kwenda Toronto, Canada kuhudhuria Mkutano wa 31 wa Shirikisho la Kimataifa la Wakunga Duniani, Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtembelea na kumjulia hali Mwadhama Policarp Kadinali Pengo akiwa hotelini Dubai njiani kurejea Dar es Salaam akitokea matibabuni. Rais Mstaafu amefurahishwa na kumuona Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo katika siha njema na amemtakia safari njema na maisha marefu.

Vijana Wakumbushwa Umuhimu wa Kulipa Kodi

$
0
0
Mwalimu wa Elimu ya Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Bw. Gabriel Mwangosi akielezea jambo wakati wa Mdahalo wa Vijana kuhusu Nguvu ya Kodi, ulioandaliwa na Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa TYVA Taifa Bw. Suleiman Makwita na Muongoza mada Bi. Nuria Mshare. Kauli mbiu ya mdahalo huo ni “Nguvu ya Kodi” Kodi kwa Huduma Bora za Jamii.
Mwenyekiti wa Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) Bw. Suleiman Makwita akifafanua jambo wakati wa mdahalo hukusu kodi ulioandaliwa na asasi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Muongozaji wa mdahalo huo Bi. Nuria Mshare na Mwalimu wa Elimu ya Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Bw. Gabriel Mwangosi.
Muongozaji wa Mdahalo wa Vijana kuhusu umuhimu wa kodi uliondaliwa na  Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) Bi. Nuria Mshare akifafanua jambo wakati wa mdahalo huo leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa TYVA, Bw. Suleiman Makwita na Mwalimu wa Elimu ya Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Bw. Gabriel Mwangosi. Kauli mbiu ya mdahalo huo ni “Nguvu ya Kodi” Kodi kwa Huduma Bora za Jamii.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

SIMU KUTOKA LONDON: Baba wa Sam Mwanyika Akifafanua Ushindi wa Mwanae


Introducing 'Bang by Benjamin Mambo Jambo

“RAIS AMETUNGUA VICHAKA” MWIGULU NCHEMBA

$
0
0
Ikiwa zimepita siku chache tangu Rais Magufuli kuzuia watu kuwahusisha marais wawili wastaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete na Benjamin Mkapa katika sakata la mchanga wa dhahabu maarufu kama makinikia kwani katika ripoti zote mbili hakuna sehemu ambayo imewataja wastaafu kuhusika. 

 Waziri wa Mambo ya ndani na Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi Mkoani Singida, Mwigulu Nchemba amesema Wezi hao walitafuta kichaka cha kutaja viongozi waliostafu ili kuzia serikali iache kufatilia sakata hilo, “Viongozi wetu hawajawai kuwa maagernt wa wale wanao tuibiwa maagernt tumewabaini ni wale wanao watetea wezi.” Tumekusogezea Video ya Habari hiyo.

RAIS AMETUNGUA VICHAKA VYOTE - MWIGULU NCHEMBA

$
0
0
Ikiwa zimepita siku chache tangu Rais Magufuli kuzuia watu kuwahusisha marais wawili wastaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete na Benjamin Mkapa katika sakata la mchanga wa dhahabu maarufu kama makinikia kwani katika ripoti zote mbili hakuna sehemu ambayo imewataja wastaafu kuhusika. Waziri wa Mambo ya ndani na Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi Mkoani Singida, Mwigulu Nchemba amesema Wezi hao walitafuta kichaka cha kutaja viongozi waliostafu ili kuzia serikali iache kufatilia sakata hilo, “Viongozi wetu hawajawai kuwa maagernt wa wale wanao tuibiwa maagernt tumewabaini ni wale wanao watetea wezi.” Tumekusogezea Video ya Habari hiyo.

Balozi wa Tanzania nchini Italia Mh. George Kahema Madafa akabidhi hati za utambulisho kwa Rais wa Italia Mh. Sergio Mattarella

$
0
0
Mh. Balozi George Kahema Madafa katika tukio la kukabidhi hati za utambulisho kwa Rais Wa Jamhuri ya Italia Mh. Sergio Mattarella kwenye Ikulu ya Rais jijini Roma hapo tarehe 18.05.2017. Mh. Balozi Madafa aliambatana na maafisa wawili wa Ubalozi wa Tanzania nchini Italia pamoja na mkewe Bi. Esther Bhoke Madafa.
 Balozi wa Tanzania nchini Italia Mh. George Kahema Madafa akabidhi hati za utambulisho kwa Rais wa Italia Mh. Sergio Mattarella katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Roma
Balozi wa Tanzania nchini Italia Mh. George Kahema Madafa akapeana mikono na Rais wa Italia Mh. Sergio Mattarella baada ya kukabidhi hati zake za utambulisho katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Roma
 Balozi wa Tanzania nchini Italia Mh. George Kahema Madafa katika mazungumzo na Rais wa Italia Mh. Sergio Mattarella na maofisa wake baada ya kukabidhi hati zake za utambulisho katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Roma
Balozi wa Tanzania nchini Italia Mh. George Kahema Madafa akiagana na Rais wa Italia Mh. Sergio Mattarella baada ya kukabidhi hati zake za utambulisho katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Roma.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA



Kumbukumbu ya Mr.Henry Michael Wimile

$
0
0
Its is  9 years today since you departed from our lives. We miss you too much. All your children(Hellen, Harris and Hope), your lovely  wife (Happiness Wimile) and friends and relatives. We love you
Viewing all 110029 articles
Browse latest View live




Latest Images