Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110108 articles
Browse latest View live

MKUU WA MKOA ATOA MILIONI TATU KWA AJILI YA MRADI WA KUKU KWA WALEVU WA NGOZI

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Bilinith Mahenge ametoa shilingi milioni tatu, ili kusaidia kikundi cha watu wenye ulemavu wa ngozi na macho albino cha wilaya ya songea, kwa ajili ya kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku wa nyama. Akikabidhi kiasi hicho cha fedha mkuu wa mkoa amewaka wanakikundi hao kutimiza malengo ili waweze kuwasaidia hata watu wengine wenye matatizo mbalimbali.hbari kamili hii hapa video yake.

Article 7

Maadhimisho Siku ya Mtoto wa Afrika: Viongozi wa Dini Wakemea Ukatili

$
0
0

VIONGOZI wa Dini wamekemea vitendo vya ukatili kwa watoto na kwani vimekemewa hata katika vitabu vya dini, huku wakimtaka kila mmoja kumlinda mtoto pamoja na kueneza elimu ya malezi. Viongozi hao walioshiriki katika mkutano wa vyombo vya habari ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kwa pamoja waliungana na TAMWA kukemea vitendo vya kikatili wanaofanyiwa watoto, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.

Akizungumza Mwakilishi kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Sheikh Shomari Mchongoma alisema jamii kwa pamoja inapaswa kuungana na kukemea vitendo vya kikatili kwani ni kinyume cha imani zetu. Alisema jambo pekee ambalo linaweza kufanikisha mapambano hayo ni jamii kumrudia mwenyezi Mungu na kukemea vitendo viovu anavyochukizwa navyo.

“…Wakati umefika tuangalie ni namna gani kumkomboa mtoto wetu kwenye wimbi la mateso ya kikatili ambayo wamekuwa wakitendewa baadhi ya watoto wetu. Mtoto anaweza kuwa salama endapo tutaungana na kukemea vitendo hivyo bila kujali tofauti zetu,” alisema Sheikh Mchongoma.

Kwa upande wake, Mwakilishi kutoka Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Bw. Lucas Singili alisema mtoto anaitaji malezi ya pamoja kwa ushirikiano ikiwa ni kuwaweka karibu ili waweze kukua katika malezi mema. Watoto hawapaswi kutengwa wala kufanyiwa vitendo vya kikatili zaidi ya kuwapa msaada kutoka kwa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla ili waweze kuwa raia wema wenye maadili katika taifa la baadaye.
Mwakilishi kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Sheikh Shomari Mchongoma (kushoto) akizungumza katika mkutano wa vyombo vya habari pamoja na viongozi wa dini kutoka BAKWATA, Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) na Mtaalamu wa Saikolojia ya Jamii, John Ambrose kukemea vitendo vya kikatili dhidi ya watoto, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.
Ofisa Miradi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Godfrida Jola (kulia) ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo akizungumza katika mkutano wa vyombo vya habari ulioandaliwa na kushirikisha viongozi wa dini kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kukemea vitendo vya kikatili dhidi ya watoto, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika. Kutoka kushoto ni Sheikh Shomari Mchongoma (BAKWATA), Bw. Lucas Singili (CCT), pamoja na Mtaalamu wa Saikolojia ya Jamii, John Ambrose.
Mwakilishi kutoka Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Bw. Lucas Singili (katikati) akizungumza katika mkutano wa pamoja na viongozi wa dini kutoka BAKWATA, CCT na Mtaalamu wa Saikolojia ya Jamii, John Ambrose kukemea vitendo vya kikatili dhidi ya watoto, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika. Mkutano huo uliandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA). Kulia ni Mtaalamu wa Saikolojia ya Jamii, John Ambrose na Sheikh Shomari Mchongoma wa BAKWATA (kushoto).

AHUKUMIWA KWENDA JELA MIEZI MITATU KWA KUPOST PICHA ZA MAITI MTANDAONI

$
0
0
Askari Polisi nchini Uingereza, wakimtia mbaroni mtuhumiwa mmoja aliyetambulika kwa Jina la Omega Mwaikambo aliyedaiwa kupiga picha ya mwili wa mtu aliyefariki uliokuwemo kwenye mfuko maalum wa kuhifadia maiti inayodhaniwa kuwa ilitokana na ajali ya moto katika jengo la Grenfell Tower iliyotokea hivi karibuni jijini London huko nchini Uingereza kisha kuziweka kwenye mitandao ya kijamii.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo, alifanya hivyo siku ya jumatano asubuhi, alipotoka nje ya nyumba yake na kukuta mfuko huo wenye mwili na kuufungua kisha kuupiga picha na kurekodi video alizoziweka kwenye mtandao wa Facebook huku akiuliza "Je, kuna mtu yeyote anaujua mwili huu ambao uko nje ya ghorofa langu kwa zaidi ya saa mbili?"

Mtuhumiwa huyo ambaye anaishi eneo la jirani kabisa na jengo la Grenfell Tower lililopatwa na janga la kuteketea kwa moto alipandishwa kizimbani jana Juni 16, 2017 katika Mahakama ya Hakimu Westminster na kusomewa mashtaka yake na kuhukumiwa kwenda jela kwa miazi mitatu kwa kutenda kosa hilo. 

mali mpya maalumu kwa sikukuu ya Eid el Fitr kwa kila rika

NEWS ALERT: MWANAMICHEZO ALHAJ SHAABAN MINTANGA HAJULIKANI ALIPO, NDUGU WANAMTAFUTA

$
0
0

MWANAMICHEZO ALHAJ SHAABAN MINTANGA HAJULIKANI ALIPO, AMEPOTEA, SIKU YA TATU LEO TANGU AONDOKE NYUMBANI HAJARUDI. 

KWA YEYOTE ATAKAEMUONA AU KUPATA TAARIFA ANITAFUTE KWA SIMU ZIFUATAZO.... 067528439107166633260719168547

ASANTENI -

FAMILIA YA MZEE KIBINDA, KAWE DSM...


Facebook,Instagram, Messenger, Imo,Viber, Twitter, LinkeldIn, (Skype: baraka.sunga1) you will see  Baraka Sunga or Whatsapp no / call +255756298029

AZANIA BENKI YAPATA FUTARI PAMOJA NA WATEJA WAKE

$
0
0
 Mkurugenzi mkuu wa Benki ya Azania ,Charles  Itembe akizungumza na wateja na wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa futari iliyoandaliwa na benki yake katika ofisi za Aznia Benki Mawasiliano Tower.
  Mkurugenzi mkuu wa Benki ya Azania ,Charles  Itembe, akisalimiana na watoto wa kituo cha Yatima cha Vingunguti wakati wa wakati wa futari iliyoandaliwa na benki yake katika ofisi za Azania Benki Mawasiliano Tower.
 Mkuu wa kitengo cha Maendeleo ya Biashara Benki ya Azania , Othman Jibrea akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watoto wa Kituo cha watoto yatima kutoka Vingunguti
 Watoto wa kituo cha Watoto Yatima Vingunguti wakipata futari  wakati wa futari iliyoandaliwa na benki yake katika ofisi za Azania Benki Mawasiliano Tower,jijini Dar.

CCM Mwanza yawapiga mkwara watakaotumia rushwa kwenye uchaguzi

$
0
0
Na Baltazar Mashaka, Mwanza

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wa Mkoa wa Mwanza Bw. Raymond Mwangwala amesema kuwa uchaguzi wa chama hicho wa mwaka huu umelenga kuwapata viongozi bora watakaokivusha kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2019 na Uchaguzi Mkuu wa 2020.

Ameonya kuwa wana CCM watakaobainika kutumia rushwa ili wachaguliwe na watakaopokea rushwa hiyo wote watashughulikiwa kwa taratibu zilizowekwa.

Bw. Mwangwala alitoa kauli hiyo juma hili wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, ambapo aliomba ushirikiano wa wanahabari hao katika utekelezaji wa majukumu yake.

Alisema CCM mpya ya “hapa kazi tu” haitamchekea mtu yeyote mwenye kupanga kukiharibu chama hicho kwa namna anayotaka na haitakuwa tayari kupokea mamluki wanaojiunga nayo kwa maslahi binafsi badala ya wananchi na wana CCM.

Katibu huyo alieleza kuwa ili wapatikane viongozi waadilifu watakaoinua mapato ya CCM na kukisaidia chama hicho tawala kwenye uchaguzi wa 2020, wanachama wenye sifa na uwezo wakachukue fomu ili wapigiwe kura kwani ndio watakaokifikisha kwenye uchaguzi huo na kukiwezesha kupata kura za ushindi za urais, ubunge na udiwani.

Bw. Mwangwala alisisitiza kuwa watakaotumia rushwa hawatapitishwa kugombea nafasi wanazoomba kwani wanatakiwa viongozi wa kusimama na kuielezea CCM badala ya mamluki.

Hata hivyo katibu huyo alisema chama hicho kinafanya uhakiki wa mali zake kuanzia ngazi ya matawi, wilaya hadi mkoa ili zitambulike na kufahamu mapato yake yalikuwa yanatumikaje.

“Zipo mali watu walikuwa wakizutumia vibaya kutokana an mikataba mibovu iliyopo, watakaobainika kwenye zoezi la uahkiki watashughulikiwa na wapo waliodiriki kuziuza mali hizo na kuzigeuza shamba la bibi,
“Tunataka tujue mali zetu zilipo na zingine zilizotelekezwa tuzijue na mapato yake yanatumikaje.Ifikapo Julai mwaka huu zote ziwe na hati,”alisema. 
Katibu wa CCM wa Mkoa wa Mwanza Bw. Raymond Mwangwala akizungumza na wanahabari ofisini kwake katikati ya juma hili.

OFISA MTENDAJI MBARONI KWA RUSHWA YA SH 200,000

$
0
0
NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA .

OFISA Mtendaji wa Mtaa wa Mtakuja Kata ya Kishiri James Mwansyemela (39) amekamatwa kwa tuhuma za kushawishi na kupokea rushwa ya shilingi 200,000 kinyume cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa kifungu cha 15 (1a) akijifanya Mhandisi wa Jiji la Mwanza .

Mtuhumiwa huyo alikamatwa Juni 13 mwaka huu na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza baada ya kuomba na kupokea rushwa hiyo kutoka kwa mfanyabiashara mmoja wa Mkolani jijini Mwanza ili asimwondoe kwenye eneo analofanyia biashara akidai ni hifadhi ya barabara.

Mkuu wa TAKUKURU wa Mkoa wa Mwanza Ernest Makale akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana alisema Mwansyemela alijifanya Mhandisi wa Jiji la Mwanza na alijitambulisha kwa mfanyabiashara huyo kwa jina la Alex.

Alisema baada ya kujitambulisha alimwambia ampe sh. milioni 1,000,000 amfanyie mpango wa kibali cha kuendelea kufanya biashara zake kwenye eneo hilo la hifadhi ya barabara waakti akifahamu kuwa kosa kisheria kwa mujibu wa kifungu cha 15 (1a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya Namba 11/ 2007.

“Mwansyemela alianza kuomba rushwa ya shilingi milioni 1,000,000 na baadaye kutoa punguzo na kufikia makubaliano ya sh.200,000.Siku ya tukio alimtuma Mtendaji wa Kata ya Mkolani Godfrey Mwangonda (35) akampokelee kwa niaba yake na ndipo akadondokea mikononi mwa maofisa wa TAKUKURU lakini ndiye aliyefanikisha mtuhumiwa kukamatwa,” alisema Makale.

Alisema sambamba na fedha alizopokea kama rushwa kutoka TAKUKURU pia alikutwa na kiasi cha fedha zingine sh. 1,050,000 ambazo alishindwa kuzitolea maelezo alikozipata wala kufahamu kiasi cha fedha alichokuwa nacho.

Kwa mujibu wa Makale mtuhumiwa huyo alidai fedha hizo alilipwa na Barnabas Nibengo wa Mbogo Mining and General Supply ltd ambaye alikana kumpatia fedha kabla ya kubadili maelezo kuwa alipewa na mkewe ili akununue chakula cha kuku, lakini mkewe naye alikana.

“ Uchunguzi wetu fedha hizo ni rushwa kutoka kwa wananchi wengine waliotapeliwa kwani ni bayana kuwa ingawa ni mtumishi wa umma ni tapeli ambaye hafai kwenye utumishi wa umma.Kumbukumbu zinaonyesha amewahi kushitakiwa mahakamani kwa makosa ya namana hiyo,” alisema Makale .

Alieleza kuwa uchunguzi na upekuzi uliofanywa na maofisa wa TAKUKURU nyumbani kwa mtuhumiwa walimkuta akiwa na hati ya mashitaka ya kujipatgia fedha kwa njia ya udanganyifu na mashitaka ya wizi akiwa mtumishi wa umma katika kesi namba moja ya mwaka 2016.

Pia maofisa hao wa TAKUKURU wanaendelea na uchunguzi wa elimu ya mtuhumiwa huyo ingawa ana vyeti vya ufaulu mzuri kwa kidato cha nne na sita alishindwa kutoa maelezo sahihi ya elimu yake na hajui alihitimu shule gani ya sekondari wala masomo aliyosoma zaidi ya kudai alichukua mchepuo wa HGE.

Mkuu huyo wa TAKUKURU alieleza zaidi kuwa watamfikisha mahakamani leo (Ijumaa), na kueleza kuwa wananchi wengi wamekumbwa na matapeli na vitendo vya rushwa kutokana na kutafuta njia za mkato kupata ufumbuzi wa matatizo yao.

Aliongeza kuwa wananchi ni wadau wa mapambano dhidi ya rushwa, hivyo watoe ushirikiano na taarifa za vitendo hivyo TAKUKURU ili wahusika wawajibishwe kwa mujibu wa sheria, kwani serikali ipo kwa ajili yao ingawa baadhi ya watumishi wasio waadilifu wanaharibu taswira nzuri ya utumishi serikalini.

NISHUSHE IDD MOSI... WASANII WATAKAOLIAMSHA DUDE, DAR LIVE

$
0
0
Mashabiki wakiwa ndani ya Dar Live.


SIKU zikiwa zinahesabika kuelekea Usiku wa Nishushe Dar Live utakaofanyika Sikukuu ya Idd Mosi ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo MbagalaZakhem jijini Dar, wakali kibao watakaoliamsha dude siku hiyo wamefungukia makamuzi watakayotoa. 

Katika usiku huo, pazia la burudani litafunguliwa rasmi mapema kuanzia saa 8:00 asubuhi ambapo burudani ya watoto itatolewa chini ya kundi la sarakasi na kudensi la Wakali Dancers pamoja na Kundi la Muziki wa Asili la Makhirikhiri kutoka Tanzania. Wakizungumza na Mikito Nusunusu kwa nyakati tofauti, wakali hao watakaoongozwa na R.O.M.A Mkatoliki walisema kuwa wataliamsha dude mwanzo mwisho sambamba na kutoa sapraizi kibao jukwaani. ROMA “Kwa muda mrefu sijafanya shoo tangu nipate matatizo hapa kati. Mara ya mwisho nilifanya shoo Dar Live nikiwa na Darassa ilikuwa Usiku wa Michano (Mkesha wa Mwaka Mpya) na waliofika waliona na ambao hawakufika walisimuliwa. Safari hii nisingependa ikupite hii. Nimepona na nipo fiti hivyo mje kwa wingi kushuhudia shoo yangu ya kwanza tangu mwaka huu uanze nikikinukisha kwa ngoma kali kuanzia Viva Roma Viva, K, Ivan, Kaa Tayari na nyingine kibao.”

TANGAZO LA SHUKRANI - MAREHEM MAMA ESTER NAPENDA MFINANGA

$
0
0

                       ESTER NAPENDA MFINANGA
(1952 – 2017)


Kwa niaba ya wanandugu wote Ndugu Boniface A. Mfinanga wa Chanjale, Kisangara Mwanga Kilimanjaro anayo heshima kubwa kutoa shukrani za dhati kabisa kwa ndugu, jamaa na marafiki ambao walishiriki kwa namna moja au nyingine katika kufanikisha mazishi ya mama yao mpendwa, ESTER NAPENDA MFINANGA aliyefariki dunia siku ya tarehe 13/4/2017 Neema Roman Catholic Health Centre Mwanga na kuzikwa kijijini kwao Chanjale, Kisangara, Mwanga, Kilimanjaro tarehe 17/4/2017


Kwa vile mlioungana nasi kwa kutufariji wakati wa kipindi chote cha msiba huu mkubwa ni wengi na ni vigumu kuwataja wote kwa majina, kama familia tunapenda kwa heshima kubwa kutoa shukrani za jumla tukiwaomba wote mkubali kuzipokea kwa moyo ule ule kama mlivyotuunga mkono. Mmetufariji sana, mmekesha nasi, mmeshinda nasi, nyote mmekuwa kimbilio salama kwetu wakati wa kipindi hiki kigumu. Mlionyesha upendo wa kweli kwetu kama familia na kwa mama yetu mpendwa.



Tunapenda kutoa shukurani za kipekee kwa  marafiki na wanandugu ambao michango yao itabakia kwa familia na nyoyo za watoto wa marehemu tukianza na Ndugu wote, majirani na marafiki wa karibu  kutoka Mwanga, Kisangara, Lembeni, Kifaru, Kiruru, Kilomeni, Soffe, Kisangara juu, Same, Pongwe Tanga, Bukoba, Moshi, Arusha, Mwanza na Dar es Salaam, kweli michango yenu kamwe haitasahaulika.




Familia pia inapenda kuwashukuru Baba askofu mstahafu Jacob Koda, Baba Paroko wa Parokia ya Chanjale Samwel Lawena, Padre Peter Mvungi, Padre Valence Sewangi, na Padre Anthony Mmari kwa kutuongozea misa takatifu ya kumpumzisha mama yetu mpendwa katika nyumba yake ya milele.


Familia vile vile inapenda kutoa shukrani za dhati kabisa kwa Dr Avelin Kimario na  Dr Swai  pamoja na manesi Prisca Silayo, Prediganda Kimario, Lightness Mduma, Donatila Msuya na Vaileth Mdee  wa NEEMA ROMAN CATHOLIC HEALTH CENTRE Mwanga, Kilimanjaro  kwa juhudi zao za dhati kabisa za kutaka kuokoa maisha ya mama yetu mpendwa.



Aidha, tunatoa shukrani kwa wafanyakazi na uongozi wa TANAPA Arusha, MSD Tanga na Bukoba, South African High Commission Dar es Salaam Mission, Murhandzwa Ltd, Tanganyika Arms Ltd, Ndugu Marwa Issa wa Kiliflora Ltd, Ndugu Gabin Msuya na wafanyakazi wote wa MSUYA AUTO GARAGE Mwanga, Wanajumuiya wa Mashahidi wa Uganda kanisa la Kristo Mfalme Moshi, Wanajumuiya ya Mt. Petro parokia ya Mwanga, Magrooup yote ya WhatsApp ya wanandugu na marafiki kwa michango yenu  iliyotufariji, tutaendelea kukumbuka ukarimu wenu daima. 



Vile vile familia inawashukuru sana majirani wa Mwanga, Chanjale, Kisangara kwa kushiriki na kushughulika kwa heshima zote katika msiba wa Mama yetu mpendwa.



Mwisho Tunawashukuru wote mlioweza kufika nyumbani Chanjale, Kisangara Mwanga na kumhifadhi Mama yetu mpendwa ESTER NAPENDA MFINANGA katika nyumba yake ya milele. Hatuna cha kuwalipa, Mungu atawalipa zaidi na zaidi.



Mama utakumbukwa daima na wanafamilia wote, Kaka na dada zako, shangazi, na wanao woote hususani Boniface, Bona, Yukunda, Bruno, Dorice, Luciana, Anastazia (Team Napenda)na wajukuu wako woote hususani Nice, Ester, Anatoly, Primi, Laris na Emmilyne


Quotes from Mom

1. “MUWASAMEHE MADHAMBI YAO NA MUWAPENDE”

                               2. “MGURANE”


BWANA ALITOA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE

AMEN



DIWANI WA KIVUKONI AUNGA MKONO JESHI LA POLISI KWA PIKIPIKI

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Diwani wa Kata ya Kivukoni, Henry Massaba ametoa pikipiki mbili kwa Jeshi la Polisi Wilaya ya Kati zenye thamani ya sh. Milioni Tano ili ziweze kutumika kwa masuala ya usalama kwa wananchi wa kata hiyo Kivukoni.

Akizungumza wakati wa kukabidhi pikipiki hizo , Massamba amesema kuwa kumeibuka wizi wa kutumia pikipiki hivyo hata polisi wanatakiwa kutumia pikipiki kwa ajili ya kuwakimbiza wahalifu hao.

Massamba amesema kuwa wahalifu wamekuwa na njia tofauti za kufanya uhalifu na kuamua kutumia pikipipiki kwa kutambua hawawezi kukamatwa kutokana na polisi kwa muda mwingi wanatumia magari.

Aidha amesema kuwa ataendelea kushirikiana na jeshi la polisi kwa namna juu ya kuhamasisha masuala ya ulinzi ili wananachi waishi kwa amani pamoja na mali zao.

Nae Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kati , Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Amon Kakwale amesema kuwa msaada huo ni mkubwa na kuwataka watu wengine waendelee kuliunga mkono jeshi la polisi.

Kakwale amesema kuwa Diwani wa Kata ya Kivukoni amejitoa kwa ajili ya wananchi kuweza kupata usalama.
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kati , Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Amon Kakwale akizungumza wakati hafla ya kukabidhiwa pikipiki mbili zilizotolewa na Diwani wa Kata ya Kivukoni leo jijini Dar es Salaam.
Diwani wa Kata ya Kivukoni, Henry Massaba akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi pikipiki kwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kati katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Diwani wa Kata ya Kivukoni, Henry Massaba akikabidhi msaada wa Pikipiki Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kati Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Amon Kakwale katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu Polisi wa Wilaya ya Kati pamoja na wananchi wa kata ya kivukoni wakiwa katika hafla ya kukabidhiana Pikipiki iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

NOAH NA BAJAJ ZAGONGANA KATIKATI YA BARABARA YA MWENDO KASI

$
0
0
 Basi la Mwendo kasi likilazimika kupita upande mwingine wa barabara yake baada ya gari ndogo aina ya Toyota Noah kugongana na Bajaj katika ya barabara hiyo eneo la Kinondoni kwa Mwanambona jijini Dar es salaam. Tukio hilo limetokea mchana wa leo, huku ikielezwa kuwa chanzo ni Bajaj hiyo iliyokuwa ikitokea njia ya Kinondoni Makaburini na kutaka kukatisha ghafla kuelekea upande wa Morocco.


Wakati mwendo kasi likiendelea kutaabika kupita, mwenye Noah na Mwenye Bajaj wakiendelea kupatana juu ya nini cha kufanya.

BIASHARA YA KUBEBA MKAA KWA NJIA YA BAISKELI YASHAMIRI CHANIKA

$
0
0
 Mfanyabiashara ya Mkaa akipandisha na Baiskeli iliyobeba mkaa katika eneo la pugu Sekondari akitokea maeneo ya Chanika  akifata soko  eneo la Gongolamboto Dar es Salaam.
 Mfanyabiashara ya Mkaa akipandisha eneo la Kigogo Fresh Pugu  akitokea Chanika  na kufata masoko katika eneo la Gongo la Mboto, mchuuzi huyo hutembea zaidi ya kilometa kumi kutokea katika maeneo ya misitu hadi kufika mjini akiwa na mzigo huo
 Mfanyabiashara ya Mkaa akivuta pumzi katika eneo la Chanika baada ya kutembea kwa muda mrefu akifuata soko katika eneo la Gongo la mboto Jijini Dar es Salaam
Baiskeli zikiwa zimepiga kambi katika kituo chao eneo la Kigogo Fresh nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam

MSHINDI WA WA MASHINDANO YA QUR-AN KUPEWA DOLA 25,000 ZA KIMAREKANI

$
0
0
Na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii

Jumuiya ya Kuhifadhi Qur-an Tanzania imeandaa  mashindano ya kimataifa ya kusoma Qur-an yanayotarajia kufanyika kesho siku ya Jumapili katika ukumbi wa Diamond Jubilee,ambapo Mgeni rasmi anatarajai kuwa Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddy. 

Akizungumza mbele ya Waandishi wa habari,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhi Qur-an Tanzania Sheikh Othman Ally Kaporo amesema kuwa jumuiya hiyo imetenga kiasi cha dola za kimarekani elfu 25 kwa ajili ya washindi watakaoibuka kwenye mashindano hayo.

Sheikh Kaporo amesema kuwa mashindano hayo ya sita Kimataifa tangu waanze kuratibu, yanatarajia kuzishirikisha nchi 18 ambazo ni Kenya, Uganda, Mali, Nigeria, Algeria, South Africa, Bangladesh, Sudan, Kuwait, Libya, Djibouti, UAE, Russia Federation, USA, Yemen, UK, Dubai, Tanzania Bara na Visiwani (Zanzibar). Muhamedi Saidi 

Amesema kuwa matarajio yao yalikuwa ni ushiriki wa nchi 35 lakini baadhi yao ziliomba udhuru wa kutohudhuria kutokana na sababu zilizonje ya uwezo wao.

Sheikh Kaporo amesema mgeni wa heshima katika mashindano hayo atakuwa Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddy akiambatana na mlezi wa Jumuiya hiyo Alhaj Ally Hassan Mwinyi Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sheikh Kaporo ametoa wito kwa watanzania kuhudhuria mashindano hayo na kujitokeza kwa wingi ukizingatia huu ni mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo katika kumi la mwisho iliteremka Qur-an tukufu hivyo ni vyema wakahudhuria ili waweze kupata ujira kutoka kwa mola wao (Allah).

Mshiriki wa Tanzania Omary Abdallah Salum, ambaye amewaomba watanzania kuwaombea dua kwa wingi ili waweze kupata ushindi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-an Tanzania, Sheikh Othman Ally Kaporo (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam,kuhusiana na  mashindano ya kimataifa ya kusoma Qur-an ambayo yanayotaraji kufanyika siku ya Jumapili katika ukumbi wa Diamond Jubilee. kulia ni Katibu wa Kamati ya maandalizi ya mashindano hayo.


NMB yafuturisha baadhi ya wateja wake Mjini Pemba

$
0
0
Mkuu wa Mkoa Pemba Kusini Mhe. Mwanajuma Majidi Abdalallah (Kulia) akipokea zawadi maalumu kwa ajili ya Ramadhani kutoka kwa Meneja wa NMB kanda ya Dar es salaam, Bi. Vicky Bishubo (kushoto) mara baada ya kumalizika kwa tafrija ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwaajili ya Wateja wake walio kwenye mfungo Mtukufu wa Ramadhani Mjini Pemba. Hafla hii ya Futari ilifanyika mwishoni mwa wiki Mjini Pemba- Zanzibar. Meneja Mwandamizi wa kitengo cha wateja Binafsi wa NMB - Omari Mtiga (Kulia) akimkabidhi Afisa Tawala Mkoa wa Pemba, Bwana Yussuf Mohammed Ali zawadi maalumu kwa ajili ya Ramadhani iliyotolewa na Meneja wa NMB kanda ya Dar es salaam, Bi. Vicky Bishubo (hayupo pichani) mara baada ya kumalizika kwa tafrija ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa ajili ya wateja wake walio kwenye mfungo Mtukufu wa Ramadhani Mjini Pemba. Sehemu ya wageni waalikwa ambao walihudhuria tafrija ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwaajili ya Wateja wake walio kwenye mfungo Mtukufu wa Ramadhani. Hafla hii ya Futari ilifanyika Mjini Pemba-Zanzibar. Maofisa wa Benki ya NMB wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mku wa Mkoa Pemba Kusini, Mhe. Mwanajuma Majidi Abdalallah (Wa nne kutoka kushoto) mara baada ya kumalizika kwa tafrija ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwaajili ya Wateja wake walio kwenye mfungo Mtukufu wa Ramadhani Mjini Pemba. Hafla hii ya Futari ilifanyika mwishoni mwa wiki Mjini Pemba. Maofisa wa Benki ya NMB wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mku wa Mkoa Pemba Kusini, Mhe. Mwanajuma Majidi Abdalallah (Wa nne kutoka kushoto) mara baada ya kumalizika kwa tafrija ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwaajili ya Wateja wake walio kwenye mfungo Mtukufu wa Ramadhani Mjini Pemba. Hafla hii ya Futari ilifanyika mwishoni mwa wiki Mjini Pemba.

MAKAMU WA RAIS AWATAKA VIJANA WASOMI KUCHANGAMKIA FURSA ZA AJIRA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa awamu ya pili ya fursa za ajira kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kati ya Tanzania na China ambapo makampuni ya China yatatoa ajira kwa wasomi wa Tanzania . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Baadhi ya vijana wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakizungumzwaa kwenye ufunguzi wa awamu ya pili ya fursa za ajira kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kati ya Tanzania na China ambapo makampuni ya China yatatoa ajira kwa wasomi wa Tanzani, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alikuwa mgeni rasmi. 
Sehemu ya Vijana waliojitokeza kwenye ufunguzi wa awamu ya pili ya fursa za ajira kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kati ya Tanzania na China ambapo makampuni ya China yatatoa ajira kwa wasomi wa Tanzani, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alikuwa mgeni rasmi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa awamu ya pili ya fursa za ajira kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kati ya Tanzania na China ambapo makampuni ya China yatatoa ajira kwa wasomi wa Tanzania . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Balozi wa China nchini Dkt.Lu Youqing akizungumza kwenye ufunguzi wa awamu ya pili ya fursa za ajira kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kati ya Tanzania na China ambapo makampuni ya China yatatoa ajira kwa wasomi wa Tanzani, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alikuwa mgeni rasmi.
Sehemu ya Vijana waliojitokeza kwenye ufunguzi wa awamu ya pili ya fursa za ajira kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kati ya Tanzania na China ambapo makampuni ya China yatatoa ajira kwa wasomi wa Tanzani, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alikuwa mgeni rasmi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na balozi wa China nchini Dkt.Lu Youqing ,MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala na viongozi wengine wa Serikali na wa Chama cha Wafanyabiashara wa China nchini Tazania mara baada ya ufunguzi wa awamu ya pili ya fursa za ajira  kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kati ya Tanzania na China ambapo makampuni ya China yatatoa ajira kwa wasomi wa Tanzania.

MBUNGE WA KIBAHA MJINI KOKA, AIKABIDHI SERIKALI VIFAA VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA VYENYE THAMANI YA ZAIDI YA SH.MILIONI 400

$
0
0
Akizungumza katika hafla hiyo, Mbunge Koka, alisema kuwa alifanikiwa kupata msaada wa vifaa hivyo kutoka kwa rafiki zake waishio nchini Marekani, wakati alipokwenda katika shughuli zake za kibiashara, ambapo walimhakikishia kupata vifaa hivyo kwa kuchangia gharama za usafirishaji hadi kuingia nchini.

Baada ya uhakika huo Koke alitumia gharama zake kuwasafirisha baadhi ya wataalamu (Wazungu) kutoka nchini Marekani na kuja nchini hadi Mji wa Kibaha kwa lengo la kukagua na kujiridhisha juu ya uhitaji wa vifaa hivyo vya kutolea huduma za afya, ambapo alitumia jumla ya Sh. milioni 12.

Aidha alisema kuwa vifaa hivyo vilichelewa kutokana na uhitaji kutoka mataifa mengine yaliyokuwa yakipata matatizo na magonjwa ya mlipuko, na hivyo kampuni hiyo ya Project Cure, kulazimika kughairisha kusafirisha kuja nchini na kutoa kipaumbele kwa mataifa hayo yaliyokuwa yakipata matatizo kwanza.

Mbali na Mbunge kuchangia kiasi cha Sh. milioni 12, pia Halmashauri ya Mji wa Kibaha pia ilichangia kiasi cha Sh milioni 32, zilizosaidia kusafirisha vifaa hivyo kutoka nchini Marekani hadi kuwasili nchini. Vifaa hivyo vilivyokabidhiwa hii leo vina thamani ya zaidi ya Sh. milioni 400.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala (wa tano kushoto) akipokea karatasi yenye orodha ya Vifaa vya kutolea huduma za Afya kutoka kwa Mbunge wa Kibaha Mjini, Silyvestry Koka (kushoto kwake) wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo vyenye thamani zaidi ya Sh. milioni 400 iliyofanyika kwenye Kituo cha Afya Mkoani, mjini Kibaha, leo mchana. Kulia kwa Waziri ni MKuu wa Wilaya ya Kibaha, Asumta Mshama. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO).
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala, akikagua sehemu ya vifaa hivyo wakati akikabidhiwa na Mbunge wa Kibaha Mjini, Silyvestry Koka (kulia kwake).
Mbunge wa Kibaha mjini, Silyvestry Koka, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Vifaa vya kutolea huduma za Afya, iliyofanyika kwenye Kituo cha Afya cha Mkoani mjini Kibaha. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mjini, Asumta Mshama.

DC MJEMA AWAONYA WALE WANAOSABABISHA MIGOGORO YA ARDHI MBONDOLE

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akizungumza na Waandishi wa Habari na kuwatahadharisha wale wote ambao wamekua wakichochea migogoro ya Ardhi katika Mtaa wa Mbondole kwa Muhaya eneo la Msongola jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya amesema atawachukulia hatua za kisheria wale wote wanaotoa taharifa za uongo kuwa hukumu ya kubomolewa eneo hilo limetoka hivyo watu hao wanatakiwa waondoke wakati hukumu hiyo inataraji kutoka tarehe 28 June 2017.

aidha ametoa wito kwa wakazi wa Mbondole kuwa wapole na kuacha kufata maneno ya Matapeli ambao wamekuwa wakiwadanganya kuwa eneo hilo hukumu imetoka na kutaja kuwa mtu anayewatisha wanatakiwa wamwambie awaonyeshe hukumu iliyo tayari hivyo kama ana hukumu wamlete ofisini kwake hili taratibu za kisheria zifuatwe.
Sehemu ya mji Mbondole kwa Muhaya ambayo mtu mmoja amejitokeza na kusema eneo hilo lake na kuwadanganya kuwa hukumu ya mahakama imetoka hivyo wanatakiwa waondoke
Wananchi wa Mbondole wakiwa wameshika mabango na kuandamana kupinga kubomolewa nyumba zao mara baada ya kutolewa taharifa ya uongo kuwa hukumu ya kubomolewa imetoka

Wakazi wa Mbondole wakiwa wameshika bango kuandamana kupinga kubomolewa nyumba zao mara baada ya kutolewa taarifa ya uongo kuwa hukumu ya kubomolewa imetoka mahakamni hivyo waondoke eneo hilo
Sehemu ya Wananchi wa Mbondole ambao walikusanyika na kuandamana kupinga kubomolewa nyumba zao mara baada ya kutolewa taharifa ya uongo kuwa hukumu ya kubomolewa imetoka mahakamani hili waondoke katika eneo hilo

"NEXT EINSTEIN" YAZINDUA WIKI YA SAYANSI AFRIKA TANZANIA

$
0
0

Na Dotto Mwaibale

KONGAMANO la Next Einsten (NEF) ambalo ni mpango wa Taasisi ya kuendeleza Hisabati na Sayansi Afrika (AIMS) kwa kushirikiana na Taasisi ya Robert Bosch Stiftung leo imetangaza uzinduzi wa wiki ya sayansi Afrika kupitia kongamano la NEF jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika uzinduzi wa kongamano hilo jijini Dar es Salaam jana, Balozi wa NEF, Aneth David ambaye ni mwanataaluma wa sayansi na mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), alisema kongamano hilo wanataaluma wa ndani, mabingwa wa sayansi na teknolojia wataongoza kwenye tukio hilo.

"Kongamano la Next Einsten la wiki ya sayansi Afrika ni wiki la kwanza la sayansi kuratibiwa ndani ya Afrika" alisema David.

Alisema lengo la msingi la kongamano hilo ni kuendeleza wanasayansi na wanateknolojia wa kesho kwa kuwahusisha watoto na vijana katika shughuli za kisayansi kama vile kujumuika pamoja na kushiriki maonesho.

"Shughuli zetu pia zitaonesha matokeo chanya ya sayansi kwa jamii nzima kwa kuwakutanisha wadau muhimu kutoka sekta zote na kuchochea uwekezaji katika tafiti na maendeleo pamoja na kujadiliana njia nzuri za kuwavutia na kuendeleza vijana hususan wasichana na wanawake katika nyanja ya sayansi" alisema Rais wa AIMS ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa NEF, Thierry Zomahoun.

Alisema wiki ya Sayansi Afrika inayofanyika hapa nchini itashuhudia vipindi vya kusisimua kama vile kuhusisha wanafunzi katika kujifunza kwa vitendo somo la kemia, Teknolojia na Uhandi kwa kutumia vifaa shirikishi vya sayansi ambapo pia wanafunzi watashiriki katika shughuli za vitendo na mashindano ya miradi ya sayansi na baadaye kufuatia na sherehe ya kutoa tuzo kwa washindi.

Kongamano hilo linafanyika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Seminari ya Al-Murtaza Upanga jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa masomo ya Sayansi, Fadhil Leonard akiwaelekeza wanafunzi wa Shule ya Msingi namna ya kutengeneza gari linalojiendesha bila ya kuwa na dereva wakati wa hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Sayansi Afrika Tanzania iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Al-Murtaza Upanga jijini Dar es Salaam leo. 
Mtaalamu wa masomo ya Sayansi kutoka Shule ya Ilboru Arusha, Vedasto Biyaka akiwaelekeza wanafunzi wa Shule ya Msingi namna ya kutengeneza magari hayo.
Wanafunzi wakipata maelekezo ya kutengeneza magari hayo kutoka kwa mtaalamu wa masomo ya sayansi, Gibson Kawago kutoka Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT).

Viewing all 110108 articles
Browse latest View live




Latest Images