Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1751 | 1752 | (Page 1753) | 1754 | 1755 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii. 

  Mwenyekiti wa Cha Soka Mkoa wa Mara (FAM) Michael Wambura amechukua fomu ya kugombea nafasi ya makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF). 

  Wambura anakuwa kiongozi wa kwanza kuchukua fomu kugombea nafasi ya makamu wa rais wa TFF . Michael Wambura aliwahi kuteuliwa katika kamati ya utendaji ya Simba na aliyekuwa Rais wa klabu hiyo Ismail Aden Rage.

  Wambura amewahi kuwa katibu mkuu wa Simba na ndiye alikuwa mtu wa kwanza kumshinda Rage katika nafasi ya ukatibu mkuu wa Chama cha Soka Tanzania (FAT)
  Mwenyekiti wa Cha Soka Mkoa wa Mara (FAM) Michael Wambura akionesha fomu ya kugombea nafasi ya makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF)


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amepongezwa kwa kazi za kizalendo anazoendelea kuzifanya kwa maslahi mapana ya Taifa .

  Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO), Mhandisi John Jeremiah amesema wanaunga mkono jinsi suala la mchanga wa madini (makinikia) linavyoshughulikiwa na Serikali ikiwa ni moja ya hatua za kuleta mageuzi ya kweli na kujenga Tanzania mpya.

  “Tofauti na wale wanasiasa wanaobeza juhudi za Rais Mgufuli sisi wana DARUSO tunapenda kumuhakikishia kuwa tuko pamoja nae kifikra, kimikakati na kimaombi na tunaamini kuwa fedha iliyopaswa kulipwa na ACACIA kwa Tanzania tangu 1998 hadi 2017 zitalipwa mara moja”Alisisitiza Jeremiah.

  Aliongeza kuwa ripoti ya kamati iliyoongozwa na Profesa Michael Ossoro imebainisha kuwa fedha zilizopotea zingeweza hudumia bajeti ya miaka mitatu hivyo juhudi za kulinda rasilimali za Taifa zinapaswa kuungwa mkono na kila mtanzania 

  “DARUSO tunapenda kukumbusha kuwa vita hii sio ya chama chochote cha siasa bali ni vita ya watanzania wote kwa hivyo tusimame na kuungana na Mhe. Rais wetu Dkt. Magufuli kwenye mapambano haya.” Alisisitiza Mhandisi Jeremiah

  Mwandisi Jeremiah amesema kuwa kiwango hicho cha fedha kingetosha kuhudumia huduma za kijamii hivyo kuwapa Watanzania unafuu wa maisha.  

  “Tunapenda kumpongeza Mhe. Rais kwa muelekeo mzuri wa juhudi zake za kizalendo zilizomfanya Mwenyekti Mtendaji wa Kampuni ya (Afica) Barrick Gold Mining Professor John Thornton kuja Tanzania kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huu”.Alisisitiza Mwandisi Jeremiah.
   Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) Mhandisi John Jilili(katikati) akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano uliolenga kupongeza juhudi za kuleta ukombozi wa kiuchumi zinazofanywa na Rais Dkt. John Magufuli. Kulia ni Makamu wa Rais wa Serikali hiyo bi Anastazia Anthony na kushoto ni Waziri wa michezo,Haiba na Burudani Bw. Mabina David. 
  Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano huo.
    (Picha na frank Mvungi-MAELEZO)

  0 0

   Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah akiongoza kikao cha Menejimenti ya Utumishi wa Bunge kilichofanyika leo Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
  Wajumbe wa kikao cha Menejimenti ya Utumishi wa Bunge wakimsikiliza Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika leo Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
  (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba (katikati) akiongea na waandishi wa habari juu ya Maadhimisho ya Siku ya Kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na Ukame. Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa hazina Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora na Bw. Timothy Mande Afisa Misitu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora (kushoto) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utoaji wa tamko la kuadhimisha siku ya kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame, mkutano huo umefanyika leo katika ukumbi wa hazina Dodoma

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Mjini Marina Joel Thomas akifungua mafunzo ya waandishi wa habari  juu ya maradhi ya kipindupindu yaliyoandaliwa na Idara ya Kinga katika Ukumbi wa  RCH Kidongochekundu Mjini Zanzibar.
   Afisa  Afya Juma Mohd Juma akitoa maelezo ya historia ya kipindupindu duniani na hatimae kuingia Zanzibar katika miaka ya 1976 na kurejea kila baada ya kipindi.
   Mwandishi wa habari wa Redio Coconut Tabia Makame akitoa mchango katika mafunzo ya waandishi wa habari ulioandaliwa na Idara ya Kinga na Elimu ya Afya kuhusu maradhi ya kipindupindu.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

  Upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Kamishna Mkuu Mstaafu wa TRA, Harry Kitilya na wenzake umeieleza mahakama kuwa wamepokea awamu ya kwanza ya vielelezo kutoka nchini Uingereza.

  Hayo yameelezwa Leo na wakili wa Serikali, Christopher Msigwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

  Msigwa ameiambia mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa wanatarajia awamu ya pili ya vielelezo kuwasili nchini Tanzania wakati wowote kuanzia sasa.

  Hata hivyo wakili wa utetezi, Mwanahamisi Adam ameuomba upande wa mashtaka kueleza muda muafaka ambao utatumika kwa vielelezo hivyo kufika nchini.

  Aidha Hakimu Mkeha amewaambia upande wa mashtaka huo muda wowote wanaoutaja wahakikishe unaangukia ndani ya siku 14 na ikishindikana basi Juni 30 mwaka huu waeleze vielelezo hivyo vitafika ndani ya siku ngapi.

  Miezi miwili iliyopita upande wa mashtaka uliieleza mahakama kuwa upalelezi dhidi ya kesi hiyo uliokuwa unafanywa ndani ya nchi umekamilika na kuwa bado wanasubiri upepelelezi unaofanywa nje ya nchi.

  Mbali na Kitilya washtakiwa wengine ni Miss Tanzania, 1996, Shose Sinare na Sioi Graham Solomon.Wanadaiwa kutenda makosa nane likiwemo la utakatishaji wa fedha wa kiasi cha USD milioni sita.

  Mbali na shtaka la utakatishaji wa fedha, watuhumiwa hao wanakabiliwa na tuhuma za kula njama, kutoa nyaraka za uongo na kughushi.

  Wanadaiwa kutenda makosa hayo katika tarehe tofauti kati ya Machi2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa Mkopo wa USD 550 wa Serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard ya Uingereza

  0 0  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe Paul Makonda amekutana na Masheikh na Viongozi wa Misikitini zaidi ya Mia sita (600) ya Mkoa wa Dar es salaam.

  Hatua hii ni muendelezo wa Mikutano yake na Makundi ya watu mbalimbali, ambapo katika kuenzi mwezi wa Mfungo wa Ramadhani.

  Mhe Makonda ametoa vitu mbalimbali kama SADAKA KWA KILA KIONGOZI vifuatavyo kwa kila Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam :-
  1. Mchele Kg 25
  2. Ngano Kg 25
  3. Sukari Kg 25
  4. Mafuta ya kupikia Lita 20

  Akizungumza na Masheikh na  Viongozi wa Dini ya KIISLAMU, Mhe Makonda kwanza amewapongeza kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali pamoja na kumuunga mkono Mhe, Rais, Dot. John Pombe Magufuli kwa jinsi ambavyo anatekeleza utendaji wake wa kazi kwa kuhakikisha anaipeleka Tanzania kwenye nchi ya Uchumi na kipato cha kati kupitia mapinduzi ya VIWANDA.

  Mhe Makonda pia, amewaomba viongozi wa Dini kuutumia mwezi huu mtukufu wa Ramadhani kuhubiri AMANI, UTULIVU NA KUVUMILIANA katika kila mambo wanayofanya waumini wao.

  Katika hatua nyingi, Mhe Makonda amefanikiwa KUWASHAWISHI wafanyabiashara haswa wa SUPERMARKET Mkoa wa Dar es salaam kufanya kazi mpaka saa sita za usiku, ili kutoa fursa kwa wananchi kujipatia mahitaji yao muhimu kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani.

  Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
  Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
  16/06/2017

  0 0

  Na Mwandishi Wetu 

  Mwanasiasa mkongwe nchini Augustine Lyatonga Mrema amesema Rais John Pombe Magufuli ameweka historia ya mapambano ya uchumi nchini kutokana na namna ambavyo analishughulikia suala la madini.

  Bwana Mrema amesema kuwa kitendo cha Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Cooperation Profesa John Thornton kusafiri usiku kucha kuja kuonana na Rais Magufuli na kukubali kuilipa Tanzania fedha zote ilizokoseshwa na Kampuni Acacia ni kielelezo kuwa sio tu kuwa ujumbe wake umefika lakini zaidi inadhihirisha kuwa madai yake dhidi ya kampuni hiyo ya uchimbaji madini ni ya msingi.

  “Ni kiongozi gani barani Afrika aliyethubutu kuishutumu kampuni ya nje kama alivyofanya Rais Magufuli halafu viongozi wake wakasafiri kuonana na kiongozi huyo kutaka suluhu kama alivyofanya Mwenyekiti huyo wa Barrick kwa Tanzania?”alihoji Bwana Mrema.

  Mwanasiasa huyo aliungana na wito wa Rais Magufuli wa kuwataka baadhi ya watu wanaowahusisha viongozi wastaafu na taarifa za Tume za Rais za kuchunguza Makinikia.

  “Si vizuri na kwamba si sheria kwa mtu yeyote kuwatukana au kuwashambulia marais wastaafu kama ilivyo kwa Rais aliye maradakani na sheria inatoa dhabu kali kwa wanaofanya hivyo” alieleza bwana Mrema.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya, akizungumza wakati wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kamati Ndogo ya Usalama wa Raia ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, leo jijini Dar es Salaam.

  Na Mwandishi Wetu.

  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya, amewaomba washiriki wa Mkutano wa Kamati Ndogo ya Usalama wa Raia ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kuhakikisha wanapambana kupunguza vitendo vya ujangili, biashara ya magendo, biashara ya binadamu, uhamiaji haramu kwani vitendo hivyo vinarudisha nyuma maendeleo ya nchi zilizopo katika jumuiya hiyo, hivyo kupelekea kurudi nyuma kwa shughuli za maendeleo na uchumi.

  Balozi Simba aliyasema hayo alipozungumza katika Mkutano huo uliojadili masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama katika maeneo ya nchi wanachama wa jumuiya hiyo, uliohusu masuala ya uhamiaji, ukimbizi, mbuga na wanyamapori katika maeneo ya nchi wanachama wa jumuiya ya SADC, leo jijini Dar es Salaam.

  “Hatuwezi kuendelea kiuchumi katika nchi zetu za wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, kama matendo ya ujangili,biashara ya binadamu, masuala ya wakimbizi, uhamiaji haramu hayajatafutiwa ufumbuzi, kwani haya yatazorotesha shughuli za kiuchumi ikiwepo utalii, hivyo ni bora tukayafanyia kazi maeneo hayo,” alisema Balozi Simba.

  Akizungumza wakati wa uchangiaji mada katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Jorge Cardoso, alisema uhalifu katika mipaka ya nchi wanachama ikiwemo uwindaji haramu wa pembe za ndovu, uhamiaji haramu,biashara ya binadamu na madawa ya kulevya lazima vidhibitiwe kwani vikiachwa mbeleni vitahatarisha Amani na utulivu uliopo katika nchi wanachama.

  “Amani na utulivu katika nchi wanachama ni kichocheo cha mabadiliko ili kupiga hatua za kimaendeleo kwenda mbele na kushirikiana kukuza uchumi katika nchi wanachama wa SADC, hivyo yatupasa wote kwa pamoja kuunga mkono harakati za kukomesha vitendo vya uhalifu katika nchi na mipaka yetu,” alisema Cardoso.

  Aidha washiriki wa mkutano huo kutoka katika nchi za Tanzania, Afrika Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Swaziland, Malawi, Zimbabwe kwa pamoja walikubaliana kupitia Kamati za Ulinzi na Usalama katika nchi zao kudhibiti matendo yote yanayohatarisha amani na utulivu.
  Mkurugenzi wa Masuala ya Siasa,Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Jorge Cardoso, akizungumza wakati wa Mkutano wa Kamati Ndogo ya Usalama wa Raia ya Jumuiya hiyo,uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere,leo jijini Dar es Salaam.
  Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya, akiongoza Mkutano wa Kamati Ndogo ya Usalama wa Raia ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika,Kulia ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini, Dk. Anna Makakala.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere,leo jijini Dar es Salaam.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye ,akichangia hoja wakati wa Mkutano wa Kamati Ndogo ya Usalama wa Raia ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika(SADC),uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere,leo jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Mdemu akitoa maelezo wakati wa Mkutano wa Kazi kati ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wadau ( hawapo pichani)kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali zilizopo Mkoani Tabora ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma. Madhumuni ya Kikao kazi hicho ilikuwa ni kukutana wa wadau hao kwa lengo la kujadiliana, kubadilishana mawazo na kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali ambazo wadau hao pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wanakumbana nazo wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku. Wadau walioshiriki kikao hicho ni kutoka Mahakama, Takukuru, Magereza, Polisi, Wakala wa Barabara, Maliasili, Halmashauri, Mawakili wa Serikali, Wanasheria na wanajamii. Kushoto kwa Naibu Mwanasheria Mkuu Wakili Mfawidhierikali Kanda ya Tabora Bw. Jackson Bulashi na kulia ni Kamanda wa Takukuru Tabora Bw. Fidelis Kalungura.
  Sehemu ya wadau ambao wamekuwa na mazungumzo na majadiliano na Ujumbe wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ulioongozwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bw. Gerson Mdemu. Majadiliano hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Takukuru Mkoani Tabora siku ya Ijumaa ( June 16) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
  Wadau kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali, Mahakama, Polisi, Takukuru, Maliasili, Magereza, Halmashauri, Wakala wa Barabara,Mawakili wa Serikali na Wanasheria wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa kikao kazi cha majadiliano baina ya wadau hao na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambapo wameazimia kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali zilizoibuliwa katika kikao hicho na kisha kupeana mrejesho.

  Na Maura Mwingira, Tabora 

  Katika kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali leo ( Juni 16) imekutana na wadau mbalimbali mkoani Tabora kwa madhumuni ya kujadiliana na kubadilishana mawazo yenye lengo la kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali za kiutendaji.

  Akitoa maelezo ya awali mbele ya wadau hao kutoka taasisi za serikali zinazofanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Mdemu pamoja na mambo mengine amesisitiza haja na umuhimu kwa wadau hao pamoja na Ofisi yake kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu ili kuiwezesha serikali kutekeleza majukumu yake kwa ukamilifu.

  “ Nyinyi ni wadau wetu muhimu sana sana, ni kwa sababu hiyo, katika wiki hii ya maadhimisho ya Utumishi wa Umma tukaamua kuja Mkoani Tabora ili tukutane nanyi.


  0 0


  Mtoto Ethan Thedore Yona akitoa maelezo kwa watoto wenzie jinsi ya kutumia App yake ya Ethan Man kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika viwanja vya JKY Park Jijini Dar Es Salaam leo. 

  JUNI 16, 2017: Dar es Salaam, Tanzania. Katika maadhimisho ya Siku yaMtoto wa Afrika mwaka huu mtoto mwenye umri wa miaka sita Ethan Theodore Yona anayesoma darasa la kwanza amezindua zana(App) yake ya android ambayo inaonesha shujaa wa hali ya juu akiwa ni muhusika anayejulikana kama EthanMan. Mhusika anaegemea upande wake ni mwenye kipaji kikubwa, ameandika vitabu vya kuvutia, kubuni michezo ya kijifunza na kuwapelekea watoto katika safari za mafunzo.

  Ethan alianza kujishughulisha na mradi huo alipokuwa na umri wa miaka mitano katika shule ya awali ikiwa ni matokeo ya mapenzi yake katika michezo na kujifunza. “Kila mara nilikuwa na nguvu , kufurahia kujifunza vitu vipya na kupenda kucheza michezo mbalimbali. Siku moja niliwaambia wazazi wangu ningependa kuanzisha mhusika mkuu jasiri kwa kuzingatia ubora wangu. 


  Baadaye waliniuliza ubora huo ni upi na nikawaambia mimi ninakipaji kikubwa na ninaweza kuwa kitu chochote ninachokipenda , naweza kuwa mchezaji soka, nyota wa muziki, mhandisi n.k. Na hivyo ndivyo wazo la mhusika shujaa mkuu lilivyoanza.”
   

  Mtoto Ethan Thedore Yona akitoa maelezo kwa watoto wenzie jinsi ya kutumia App yake ya Ethan Man kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika viwanja vya JKY Park Jijini Dar Es Salaam leo. 


  Ethan alifanya kazi hiyo na mshauri wa teknolojia ya elimu katika i-LearnEast Africa, na ambayo inatoa kozi kwa njia ya mtandao na mafunzo ya mabadiliko kuunda mhusika huyo na kuanzisha kitabu chake cha kwanza cha picha alichokiita “Nitakapokuwa Mkubwa”. Tulivutiwa sana kufanya kazi na Ethan katika mradi huu. 


  Inafurahisha kwamba mtoto mdogo namna hii kutaka kufanya jambo hili kubwa tulitaka kuwa sehemu ya huu mradi tangu mwanzo. Ikiwa ni kampuni ya ushauri katika masuala ya elimu tuliona umuhimu wa kujifunza ambao mradi huu utawapatia watoto. Mchango wa Ethan katika kuandaa kitabu hiki ni wa kushangaza,” alisema Ofisa Mtendaji wa Learn Tech, Deus Ntukamanzina. 


  Zana hiyo na michezo ilianzishwa kwa ushirikiana na kampuni ya Tujenge Technology ambayo imejikita katika kuanzisha masuluhisho ya kidijitali ambayo yatawezesha kukabiliana na changamoto zinazoikabili jamii.
   
  Mtoto Ethan Thedore Yona akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kitabu chake kwa njia ya mtandao(App) kijulikanacho kama Ethan Man, hafla hiyo imefanyika leo kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika viwanja vya JKY Park Jijini Dar Es Salaam. 


  “Tulipoombwa kuanzisha michezo ya EthanMan tulifurahi. Kuwa sehemu ya mradi huu wa kipekee ndicho kilichotufanya kuingia katika teknolojia na kuianzisha. Mchango wetu ilikuwa ni kuunganisha mhusika EthanMan na vipaji vyake vingi katika jukwaa ambalo itakuwa ni rahisi kufikiwa na kuanzisha uzoefu mkubwa wa kutumia miongoni mwa watoto. Mchango wa ethan katika kuanzisha michezo ni wa hali ya juu, kwa sababu kila kitu kimejielekeza katika maisha yake kama mhusika. Tulikuwa na muda mzuri wa wa kuunda kile ambacho tunaamini kuwa ni bidhaa ya kwanza ya mchezo katika anga ya teknolojia nchini Tanzania.

  Zana (App) ya EthnMan inapatikana kwa kupakua katika hifadhi ya michezo ya android , watoto wataweza kusoma vitabu, kucheza michezo. Na kuwa pamoja na muundaji wa EthanMan, Ethan Theodore Yona.

  0 0
 • 06/16/17--20:00: Ngoma azipendazo ankal

 • Dunia tunapita - Samba Mapangala

  0 0
  0 0

  Mmoja kati ya Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe akiuliza swali wakati wa kikao kazi na Naibu Katibu Mkuu-Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. #wikiyautumishi 2017
  Mkurugenzi Idara ya Uchambuzi na Ushauri Kazi Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw.Micky Kiliba,akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kiutumishi yaliyojitokeza katika kikao kazi na Watumishi wa Umma. #wikiyautumishi 2017
  Mkurugenzi Idara ya Uchambuzi na Ushauri Kazi Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw.Micky Kiliba,akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kiutumishi yaliyojitokeza katika kikao hicho. #wikiyautumishi2017
  Mkurugenzi Idara ya Ukuzaji Maadili Ofisi ya Rais,UTUMISHI Bw. Mathew Kirama akitoa mada kuhusu maadili katika Utumishi wa Umma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. #wikiyautumishi 2017
  Mmoja wa Watumishi wa Umma kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Songwe akiuliza swali wakati wa kikao kazi cha Wiki ya Utumishi wa Umma na viongozi wa Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. #wikiyautumishi 2017
  Viongozi na Watumishi wa Umma wa Halmshauri ya Wiaya ya Songwe waliohudhuria kikao hicho.#wikiyautumishi 2017

  0 0

  Meneja Miradi kutoka Social Action Trust Fund (SATF) Rogasian Massue akimkabidhi leo mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kulipia gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto watano.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimshukuru Meneja Miradi kutoka Social Action Trust Fund (SATF) Rogasian Massue mara baada ya kumkabidhi leo mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kulipia gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto watano.
  Meneja Miradi kutoka Social Action Trust Fund (SATF) Rogasian Massue akimsalimia mtoto Goodluck Msele ambaye amefanyiwa upasuaji wa moyo hivi karibuni katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na hali yake inaendelea vizuri. SATF imechangia shilingi milioni 10 fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kulipia gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto watano.
  Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kwa Watoto na Mkuu wa Idara ya Upasuaji wa Moyo kwa Watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Godwin Sharau (katikati) akimwelezea Meneja Miradi kutoka Social Action Trust Fund (SATF) Rogasian Massue (kushoto) kuhusu aina mbalimbali za magonjwa ya moyo yanayowasumbua watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Kulia ni Msimamizi wa Wodi ya watoto Afisa Muuguzi Rogers Kibula.
  Meneja Miradi kutoka Social Action Trust Fund (SATF) Rogasian Massue akimsikiliza Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kwa Watoto na Mkuu wa Idara ya Upasuaji wa Moyo kwa Watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Godwin Sharau wakati akimuelezea jinsi upasuaji wa moyo unavyofanyika katika Taasisi hiyo.Picha na JKCI

  0 0


  0 0

  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amemkutana na Mwakilishi mkazi WA Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto duniani-UNICEF bibi Maniza Zaman ofisini kwake mjini Dodoma. 

  Katika kikao hicho viongozi hao mbali na kufahamiana pia wamejadili namna ya kuboresha mahusiano baina ya Wizara na UNICEF .

  Katika maongezi hayo Bi. Zaman aliishukuru Wizara na taasisi zake kwa ushirikiano inayowapa UNICEF katika programu mbalimbali inazoshirikiana na Wizara.

  UNICEF inatekeleza kwa kushirikiana na Wizara katika maeneo ya usajili wa watoto chini ya miaka mitano na kuwapa vyeti vya kuzaliwa, huduma ya msaada wa kisheria na mkakati wa haki mtoto.
  Prof. Kabudi akiwa na bibi Zaman balsa ya kumaliza mazungumzo ya yaliyofanyika ofisini kwake mjini Dodoma 

  0 0

  Wakuu wa Idara wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) wakijadili masuala mbalimbali walipotembelewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Bw. Ramadhan Maleta, katika mwanzo wa Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza Juni 16-23 kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Ramadhani Maleta akimsikiliza na Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw.Joseph Nyahende (kushoto), wakati wa kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza Juni 16 hadi 23. Wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu, Bw. Mohamed Ally na kushoto ni Mkurugenzi Viwanja vya Mikoa, Bw. Valentine Kadeha.
  Mkuu wa Kitengo cha Usalama katika jengo la kuwasili na kuondokea abiria mashuhuri la VIP kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Leonard Mbogoma (wapili kushoto)akimuelezea jambo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Ramadhan Maleta alipotembelea jengo hilo ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza Juni 16-23.
  Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Joseph Nyahende akimfafanulia jambo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Ramadhan Maleta ikiwa ni siku ya kwanza ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza Juni 16-23.
  Ofisa Biashara wa JNIA, Bi. Herrieth Nyarusi (kushoto) akizungumza wakati Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Ramadhan Maleta alipotembelea Idara ya Biashara kusikiliza kero na maoni kutoka kwa watumishi, ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma. Kulia ni Meneja wa Fedha (JNIA), Bw.Shadrack Chilongani na katikati ni Bw. Godfrey Kanyama.

  0 0

  Imeelezwa kuwa sababu kubwa inayochangia watoto kuendelea kunyanyaswa na kufanyiwa vitendo vya kikatili katika maeneo ya kanda ya ziwa ni jamii kukosa elimu kuhusu haki za watoto pamoja na kukosekana kwa ushirikiano pale kesi zinazopelekwa katika vyombo vya sheria.

  Hayo yamesemwa leo June 16,2017 na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro wakati wa maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika Viwanja vya Shycom Mjini Shinyanga.

  Matiro alisema tatizo kubwa linalotokea wakati wa kutetea haki za watoto wanapofanyiwa ukatili ni kukosekana kwa ushirikiano wa jamii na wazazi pale kesi inapofika katika vyombo vya sheria ikiwemo mahakamani hivyo kusababisha kesi nyingi kufutika matokeo yake watoto wanaendelea kunyanyasika.

  “Naomba tuweke mkazo zaidi katika elimu kwa jamii kuhusu haki za watoto,jamii ikibadilika tunaweza kumaliza tatizo la unyanyasaji wa watoto,wazazi wakielimika watajitokeza katika vyombo vya sheria kutoa ushahidi kwa vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa watoto wao”,alieleza Matiro.

  “Haki za watoto zinadidimizwaa sana kanda ya ziwa hasa mkoani Shinyanga kutokana na jamii kukosa elimu na kung’ang’ania mila na desturi zinazomgandamiza mtoto hususani mtoto wa kike hivyo mashirika na serikali tushirikiane kubadilisha fikra za jamii,wananchi wajue haki za watoto na wazilinde”,aliongeza Matiro.
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa maadhimisho hayo ambapo aliwataka watoto kusoma kwa bidii kwani elimu ni mkombozi wa maisha yao
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa na watoto waliopo katika kituo cha huduma ya watoto Shirika la Compassion katika kanisa la KKKT Shinyanga
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia masweta na nguo mbalimbali zilizotengenezwa na watoto hao.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 1751 | 1752 | (Page 1753) | 1754 | 1755 | .... | 3286 | newer