Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110150 articles
Browse latest View live

Ngoma azipendazo ankal

$
0
0

Matinda (Franco) - Franco & L'O.K. Jazz 1968

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JUNE 16,2017

DKT HAMISI KIGWANGALLA AZINDUA KONGAMANO LA WATOTO KUELEKEA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA

HABARI NJEMA KWA WANAOSUBIRI AJIRA

$
0
0
Akizungumza na Wanahabari Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Thecla Makundi ameeleza kuwa semina hiyo itamuwezesha mdau kujiamini, kujitambua, kujiandaa na kuwa na uwezo mkubwa wa kuthubutu.

Huduma ya Semina hiyo itakayofanyika Juni 30, mwaka huu katika ukumbi wa Msasani Tower mkabala na Hospitali ya CCBRT Kuanzia Saa 8 mchana hadi 12 Jioni
Mkurungenzi wa Melva International Ltd, ,Amedeus Deogratius akifafanua jambo katika mkutano huo.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni Melva International Ltd,Thecla Makundi (kulia) akizungumza na waandishi wa habari juu ya semina maalumu ya huduma ya kazi kwa wadau wa kazi ili kuwajengea Uwezo leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni,Amedeus Deogratius

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KUWA MGENI RASMI MASHINDANO YA QU-RAN KIDUNIA YATAKAYOFANYIKA JUNI 18, MWAKA HUU JIJINI DAR

$
0
0
Jumla ya Washiriki 18 kutoka mataifa mbalimbali Duniani wanatarajia kushiriki fainali ya mashindano hayo yatakayo fanyika siku ya Ijumapili Juni 18, 2017 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es salaam.

Kwamujibu wa Mjumbe wa kamati inayo Ratibu Mashindano hayo Thabit Badi amesema mpaka sasa wameshawasili washiriki 15 na mpaka kufikia saa nane usiku kuamkia kesho watakuwa wamewasili wote.

Katika Fainali hiyo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi.
Washiriki wa mashindano hayo wakiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Mjumbe wa kamati inayo ratibu Mashindano ya Qu-ran, Thabit Badi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya Mashindano ya Qu-ran yatakayofanyika siku ya Ijumapili Juni 18, mwaka huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es salaam.

Benki ya NMB yafuturu pamoja na wateja wake Mjini Zanzibar

$
0
0
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud (kulia) akimshukuru Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB – Abdulmajid Nsekela baada ya kupokea zawadi maalumu kwa ajili ya Ramadhani mara baada ya kumalizika kwa tafrija ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa ajili ya Wateja wake walio kwenye mfungo Mtukufu wa Ramadhani. Hafla hii ya Futari ilifanyika Mjini Zanzibar- Unguja juzi. Baadhi ya wateja wa Benki ya NMB walio kwenye mfungo Mtukufu wa Ramadhani mjini Zanzibar wakiwa kwenye hafla ya futari Mjini Zanzibar. Hafla hiyo ya futari ilifanyika Mjini Zanzibar- Unguja juzi. Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB – Abdulmajid Nsekela (wa kwanza kulia) akijiandaa kumkabidhi zawadi ya ramadhani Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud ikiwa ni zawadi maalumu kwa ajili ya Ramadhani mara baada ya kumalizika kwa tafrija ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa ajili ya Wateja wake walio kwenye mfungo Mtukufu wa Ramadhani. Hafla hii ya Futari ilifanyika Mjini Zanzibar- Unguja juzi. Baadhi ya wateja wa Benki ya NMB walio kwenye mfungo Mtukufu wa Ramadhani mjini Zanzibar wakiwa kwenye hafla ya futari Mjini Zanzibar. Hafla hiyo ya futari ilifanyika Mjini Zanzibar- Unguja juzi. Baadhi ya viongozi mbalimbali na wa Benki ya NMB wakiwa kwenye hafla ya futari Mjini Zanzibar. Hafla hiyo ya futari ilifanyika Mjini Zanzibar- Unguja juzi.

WARSHA YA KARIKACHA & VIBONZO YAMALIZIKA, YAFUNGWA NA BALOZI ARTHUR MATTLI

$
0
0
Balozi na Mwakilishi wa Uswisi Afrika Mashariki, Arthur Mattli, akimkabidhi cheti cha ushiriki wa “Warsha ya Uchoraji Karikacha & Vibonzo,” Saidi Michael maarufu kama “Wakudata” hivi karibuni baada ya kushiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyoendeshwa na asasi ya Nathan Mpangala Foundation (NMF) na kufadhiliwa na Ubalozi wa Uswisi nchini. Katikati ni Mwenyekiti wa NMF, Nathan Mpangala.
Mchora vibonzo Musa Ngarango aka “Masikio Mchongoko”, akilamba ganda lake.
Mchora vibonzo chipukizi, Brenda Kibakaya alidhihirisha kuwa uchoraji vibonzo si kwa wanaume tu.
Magret Liwembe akimkabidhi zawadi mgeni rasmi (karikacha cha mke wa balozi iliyonakshiwa kwa saini za washiriki) kwa niaba ya washiriki wenzake. 

MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2017 JIJI LA MBEYA

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi.Susan Mlawi akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi kwa viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya alipofanya ziara ofisini hapo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma 2017.
Mkurugenzi Idara ya Uchambuzi na Ushauri kazi Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw.Micky Kiliba,akitoa ufafanuzi kuhusu ujazaji wa fomu za OPRAS zinazopima utendaji kazi wa mtumishi.
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Bw. Musa Mapunda (wa pili kutoka kushoto) akieleza majukumu ya jiji hilo wakati wa kikao kati ya viongozi wa Jiji hilo na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi.Susan Mlawi (kulia) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.
Kaimu Katibu Tawala wa Jiji la Mbeya Bw.Nyasembwa Sivangu akisoma taarifa ya Jiji la Mbeya wakati wa kikao kati ya viongozi wa Jiji hilo na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi.Susan Mlawi (wa pili kutoka kulia) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. Kulia ni Mkurugenzi Idara ya Uchambuzi na Ushauri kazi Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw.Micky Kiliba.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

BALOZI MASIMA AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO KWA RAIS WA TAIFA LA ISRAEL

$
0
0

Kufuatia kukamilika kwa mchakato wa kufungua ubalozi wa Tanzania jijini  Tel Aviv nchini Israel, na balozi mteule kuwasili kituoni, jana Alhamis tarehe 15 June 2017  Balozi wa Tanzania nchini humo, Mhe. Job Masima amewasilisha Hati za utambulisho kwa Mhe. Reuven Rivlin, Rais wa Taifa la Israel jijini Jerusalem. 
Katika sherehe hiyo, Rais Rivlin alimshukuru Mhe. Dr John Pombe Joseph Magufuli, kwa kumteua balozi mkazi wa kwanza ubalozi nchini Israel . Ampongeza pia kwa hatua mbali mbali anazozichukua katika kukukuza uchumi na kusifia serikali yake kwa kudumisha hali ya utulivu na amani nchini Tanzania. Kwamba anaiona nchi  ya Tanzania ikiwa yenye maendeleo makubwa mbeleni chini ya uongozi wake. Kwa upande wake, pamoja na mambo mengine, balozi aliwasilisha salamu maalimu za Rais Magufuli kwa Rais Ruvlin, serikali na wananchi wa Israel na kuahidi kudumisha mahusiani yaliyopo na yenye historia kubwa. Ubalozi wa Tanzania umepewa usajili wa kibalozi namba 88.
 Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe. Masima akipokewa kwa nyimbo za taifa baada ya kuwasili kwenye Ikulu ya nchi hiyo mjini Jerusalem kabla ya kuwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais wa taifa hilo Mhe. Reuven Rivlin
Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe. Masima akiweka saini kwenye kitabu maalumu cha wawakilishi wa nchi za nje kwenye Ikulu ya nchi hiyo mjini Jerusalem kabla ya kuwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais wa taifa hilo Mhe. Reuven Rivlin aliyesimama kulia kwake
Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe. Masima akijitambulisha kwa  Rais wa taifa hilo Mhe. Reuven Rivlin kabla ya kuwasilisha hati zake za utambulisho

 Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe. Masima akiwasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Taifa la Israel Mhe. Reuven Rivlin  Ikulu ya nchi hiyo mjini Jerusalem 
  Akiwa amevaa baragashia ya kitamaduni ya Kiyahudi maarufu kama "Kippah" Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe. Job Masima akiwasilisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  pamoja na kusoma salamu maalumu za mwanzo wa urafiki mpya wa ushirikiano wa karibu kwa ki-Hebrew baada ya kuwasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Taifa la Israel Mhe. Reuven Rivlin  Ikulu ya nchi hiyo mjini Jerusalem. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Kwa taarifa zaidi za hafla hiyo BOFYA HAPA

MAMBO MAZURI YA EID EL FITR KWA WATOTO

$
0
0
Mpe tabasaamu la nguvu mtoto wako kwa kumfanyia manunuzi ya bidhaa moya ndani ya #babyshop kwa bei nafuu tembelea #gsmmallmsasani#gsmmallpugu#mlimanicity

DEATH ANNOUNCEMENT OF THE LATE DR. PATRICIA FRANCIS MLOZI

Magreth Sinyangwa wa Kilosa Morogoro apokea Milioni 20 za Biko

$
0
0
MJASIRIAMALI mwanamke mwenye umri wa miaka 26, Magreth Sinyangwa amekabidhiwa jumla ya Sh Milioni 20 za ushindi wa bahati nasibu ya Biko, aliyoupata katika droo kubwa iliyochezeshwa juzi Jumatano, jijini Dar es Salaam, huku akiwa mwanamke wa kwanza kuibuka na ushindi huo.

Sinyangwa amekabidhiwa fedha hizo Kilosa katika benki ya NMB, mkoani Morogoro na Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, ambaye pamoja na mambo mengine, alimpongeza mshindi huyo na kumtaka azitumie fedha zake kwa uangalifu pamoja na kuboresha maisha yake ya kila siku.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Heaven alisema ni wakati wa kutajirika kwa kutumia vyema bahati nasibu ya Biko, ‘Ijue Nguvu ya Buku’ iliyozidi kuchanja mbuga na kutoa mamilioni ya Sh kwa washindi wa droo kubwa zinazofanyika Jumatano na Jumapili, sanjari na zawadi za papo kwa hapo.


“Tunajivunia kumpata mshindi mwanamke ambaye leo (jana) tumemkabidhi zawadi yake ya Sh Milioni 20, tukiamini kuwa atazitumia vizuri katika kuhakikisha kwamba anakuza biashara zake, ukizingatia kuwa tayari yupo kwenye tasnia ya biashara kabla ya kupata donge nono la Biko.


“Kucheza ni rahisi kwa sababu Biko inachezwa kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money, ambapo mtu atafanya muamala kuanzia Sh 1,000 na kuendelea ambapo ataweka namba ya kampuni ambayo ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456, huku mbali na donge nono la Sh Milioni 20 linatoka kila Jumatano na Jumapili, pia zipo zawadi za papo hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni,” Alisema Heaven.
Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven kulia akiwa katika makabidhiano ya Sh Milioni 20 kwa mshindi wao wa Kilosa, mkoani Morogoro, Magreth Senyangwa aliyeibuka kidedea katika droo kubwa iliyofanyika Jumatano iliyopita. Kushoto ni mume wa Magreth, Bahati Ramadhani na mwingine ni Ofisa wa NMB Tawi la Kilosa, akiwa kwenye makabidhiano hayo.
Mshindi wa donge nono la Sh Milioni 20 kutoka Kilosa, mkoani Morogoro, Magreth Senyangwa akiwa ameshika fedha zake baada ya kukabidhiwa kutoka kwa waendeshaji wa bahati nasibu ya Biko.
Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven kushoto akiwa ameshika hundi tayari kwa kumkabidhi mshindi wao wa Sh Milioni 20 wa Kilosa Morogoro, Magreth Senyangwa, wa pili kutoka kushoto akifuatiwa na mumewe Bahati Ramadhan pamoja na familia yao.


Professor Patrick Loch Otieno Lumumba speaks in Dar es salaam

UWT Zanzibar yawataka wanawake kuchangamkia fursa za Uongozi

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

UMOJA wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi  Tanzania (UWT)  umewataka wanawake kuchangamkia fursa za Uongozi wa ngazi mbali mbali  kupitia uchaguzi unaondelea hivi sasa ndani ya Chama na jumuiya zake.

Wito huo umetolewa Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja huo Zanzibar  Bi.Tunu Juma Kondo    katika mwendelezo wa ziara ya  UWT  ya kuzungumza na Viongozi wapya wa ngazi za matawi wa umoja huo uko Jimbo la Kijini  Wilaya ya Kaskazini "A" kichama Unguja.

Awambia  Akina Mama hao kuwa Uchaguzi  wa ngazi mbali mbali unaoendelea  katika taasisi hiyo ndio fursa moja wapo ya wanawake  kupata nafasi za uongozi ili waweze kufikia malengo ya kupata uwakilishi wa viongozi wenye idadi sawa na wanaume ndani ya Chama hicho.

Alifafanua kuwa wanawake wanatakiwa kuondokana na dhana ya kuendelea  kuongozwa kwa kila nafasi za uongozi ndani ya CCM bali wanatakiwa kujiongeza kwa kuwania wenyewe uongozi ndani ya chama hicho ili kuleta maendeleo endelevu ndani ya chama na jumuiya zake.

Pia alisisitiza viongozi hao kuwa pamoja na majukumu ya kiuongozi waliyonayo ni lazima wawahamasishe  kwa wingi wanawake  kuwania nafasi za uongozi ili kupata viongozi makini na wenye  uwezo  wa kwenda na kasi  za kiutendaji za chama hicho.

"Wanawake wenzangu tutumieni fursa ya Uchaguzi wa Chama kuwania nafasi mbali mbali za uongozi , tusisubiri nafasi za uteuzi  bali tusimame wenyewe  kupambana kwa kuhakikisha nasi tunakuwa na nyadhifa za uongozi kama walivyo wanaume kwani tunaweza wenyewe bila ya kuwezeshwa’’,. Alisema Bi.Tunu.
 Kaimu  Naibu  Mkuu wa UWT Zanzibar, Bi. Tunu Juma Kondo akizungumza na viongozi wa Matawi ya Jimbo Kijini Wilaya ya Kaskazini “A” kichama Unguja.
  Katibu Msaidizi wa  Idara ya  Organazesheni  UWT Zanzibar, Bi. Mgeni  Ottow akitoa nasaha kwa viongozi wa Matawi ya Jimbo Kijini Wilaya ya Kaskazini “A” kichama Unguja.
Baadhi ya viongozi wa UWT  wa Matawi jimbo la kijini Wilaya ya Kaskazini “A”  kichama Unguja wakisikiliza kwa makini nasaha zinazotolewa na viongozi wa UWT Zanzibar  uko Tawi la CCM Muange.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TSA YAWATAKA WAZAZI KUWALEA WATOTO KATIKA MAZINGIRA BORA

$
0
0
Na Zainab Myamka, Globu ya Jamii.


CHAMA cha Kuogelea Nchini (TSA) kimewataka wazazi kuwalea watoto katika misingi ya michezo ili kuweza kuwa na afya njema pamoja na mazingira bora.


Hayo yamesemwa leo na Katibu  Mkuu wa Chama cha Kuogelea Nchini (TSA) Ramadhan Namkoveka  ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishwa kila Juni 16  kila mwaka .

Akizungumza na Mtandao huu, Namkoveka amesema kuwa mtoto anatakiwa kulelewa katika mazingira mazuri basi anaweza kuwa na afya njema pamoja na kujijenga kiuwezo katika kufikiria.

"Mtoto akilelewa katika mazimngira mazuri atakuwa na afya njema pamoja na kujijenga kiuwezo katika kufikiria na hilo ndiyo jambo kubwa la msingi," amesema Namkoveka.

Namkoveka amesema kuwa kwa upande wa TSA huwa wanawashauri sana wazazi kuja kuwaleta watoto wakiwa na umri mdogo kwani mchezo wa kuogelea unatakiwa mtoto aanze kujifunza akiwa mdogo kwani wanaanza kuleta ushindani katika mchezo huo.

Amesema, kwa mfano kuna mtoto Isam Sepetu aliweza kupata nafasi ya kwanza na kuondoka na  medali ya dhahabu akiwa na umri wa miaka 12 katika mashindano ya CANA kanda ya tatu yaliyofanyika Rwanda. Aliwashinda watoto wenzie kutoka Afrika ya Kusini na Zambia.

TSA wameshauri wazazi kuweza kuwaacha watoto wao wafanye kila wanachokitaka hususani katika michezo kwani inawapa fursa ya kimichezo na kuepukana na vitendo viovu katika jamii.

Mtoto Isam Sepetu (KATIKATI) aliposhika nafasi ya kwanza na kupata medali ya dhahabu akiwa na umri wa miaka 12 katika mashindano ya CANA kanda ya tatu yaliyofanyika Rwanda. Aliwashinda watoto wenzie kutoka Afrika ya Kusini na Zambia.


CRDB YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KWA KUWAPATIA ZAWADI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

BENKI ya CRDB imeadhimisha siku ya  Mtoto wa Afrika kwa kuwapatia zawadi watoto mbalimbali ambao wazazi wao waliwafungulia akaunti za Junior Jumbo huku wakiwa wamewekewa fedha mara kwa mara.

Akitoa zawadi hizo, Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya CRDB Azikiwe  Nomina Msoka amesema kuwa watoto hao waliopatiwa zawadi ni kutokana na wazazi wao kuwawekea fedha mara kwa mara na hata akiba za akaunti zao zina kiasi kikubwa cha fedha.

Nomina amesema kuwa, wazazi wanatakiwa kuwafungulia na kuwawekea watoto wao fedha mara kwa mara iili kuwandaa na maisha ya baadae ikiwemo katika kulipia ada za masomo yao na pia upo taratibu wa wazazi kuwaekea hela kupitia akaunti zao..

Amesema mbali na hilo, CRDB wameweza kuandaa michezo mbalimbali ya watoto kwa ajili ya kujumuika pamoja na wenzao na kufahamiana zaidi.
Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya CRDB Azikiwe  Nomina Msoka akiwa amembeba mtoto Kinora Brown na kumkabidhi zawadi yake ya begi la Junoir Jumbo Akaunti  kwa mama yake wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishwa Juni 16 kila mwaka. 
 Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya CRDB Azikiwe Nomina Msoka akimkabidhi zawadi ya begi la Junoir Jumbo Akaunti  mtoto Orley Mwanyika wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishwa Juni 16 kila mwaka.
 Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya CRDB Azikiwe Nomina Msoka akimkabidhi zawadi ya begi la Junoir Jumbo Akaunti  mtoto Tonia Naivasha  wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishwa Juni 16 kila mwaka.
  Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya CRDB Azikiwe Nomina Msoka akimkabidhi zawadi ya begi la Junoir Jumbo Akaunti  mtoto Rashidi Jumbe wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishwa Juni 16 kila mwaka.
  Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya CRDB Azikiwe Nomina Msoka  akiwa katika picha ya pamoja na watoto aliowakabidhi zawadi za mebegi ya Junior Jumbo Akaunti  wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishwa Juni 16 kila mwaka.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

UCHAGUZI TFF: IMANI MADEGA ACHUKUA FOMU YA URAIS WA TFF

$
0
0



Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya soka ya Yanga Seneta Imani  Maugila Madega


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.



Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya soka ya Yanga Seneta Imani  Maugila Madega amejitokeza kuchukua fomu ya kuwania Urais wa Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF.

Madega anakua ni mtu wa pili kuchukua fomu ya Urais baada ya Rais anaemaliza muda wake Jamal Malinzi kuchukua mapema asubuhi ya leo.


GEPF yaipatia mkopo wa mil. 500 Sukari Savings & Credit Cooperative Society Ltd

$
0
0
Mwenyekiti wa bodi ya Mfuko wa GEPF, Joce Shaidi akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 500, kwa Meneja wa Chama cha sukari cha WAFANYAKAZI cha kukopa na kuweka cha mkoani kagera (Sukari Savings & Credit Cooperative Society Ltd), Robert Mshoki, kwa ajili ya Sacoss mbalimbali za Mkoani Kagera, katika hafla fupi ya kutiliana saini, iliyofanyika leo Jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa bodi ya Mfuko wa GEPF, Joce Shaidi akisaini mkataba wa Mkopo wa kiasi cha Shilingi Milioni 500 na Chama cha sukari cha WAFANYAKAZI cha kukopa na kuweka cha mkoani kagera (Sukari Savings & Credit Cooperative Society Ltd), kwa ajili ya Sacoss mbalimbali za Mkoani Kagera, katika hafla fupi ya kutiliana saini, iliyofanyika leo Jijini Dar es salaam. Katikati ni Meneja wa Chama hicho, Robert Mshoki  na kulia ni Mrajisi Msaidizi kutoka Kagera Sugar, R. Kitambo

VACANCY ANNOUNCEMENT

SIKU YA MTOTO AFRIKA : MAKAMU WA RAIS AFUNGA TAMASHA LA UELIMISHAJI NA UPIMAJI KWA WATOTO NA VIJANA KINYEREZI DAR ES SALAAM

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi kote nchi kuwafichua watu wanaonyanyasa na kudhalilisha watoto kijinsia ili waweze kukamatwa na kuchukua hatua za kisheria kama hatua ya kukomesha vitendo hivyo ambayo vimeanza kushamiri katika baadhi ya jamii nchini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo katika hotuba yake ya kuhitimisha kampeni ya kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo ilitoa huduma bure za vipimo na matibabu kwa watoto na vijana zaidi ya 1500 kampeni ambayo iliambatana na maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika katika viwanja vya Shule ya msingi Kinyerezi mkoani Dar es Salaam.

Makamu wa Rais amesema kuwa watenda maovu hao lazima vifichuliwe na wananchi, walezi pamoja na wazazi kwa kuwa watu wanaofanya vitendo hivyo vya udhalilishaji wa watoto wapo miongoni mwa jamii.

Katika kukabiliana na hali hiyo, Makamu wa Rais ameviagiza vyombo vya dola kutofumbua macho vitendo hivyo bali pindi wanapopata taarifa za matukio ya udhalilishaji wa watoto wachukue hatua za haraka za kuwakamata na kuwachukulia hatua stahiki watu wanaofanya vitendo hivyo vibaya.

Makamu wa Rais pia ametoa wito maalum kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kote nchini waache kuwaficha watu wanaotendea vitendo hivyo vibaya bali wawapatie taarifa walimu wao na polisi ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Amesema kwa kufanya hivyo watoto watakuwa salama katika mazingira ya nyumbani na wakiwa mashuleni kwani watu wabaya wanaofanya vitendo hivyo watawajibishwa kulingana na matendo maovu waliyokuwa wanawafanyia watoto hao.

“Mtoto anaweza kufaidika na fursa sawa iwapo tu atalindwa kwa kuwezeshwa kuwa afya bora”, Amesisitiza Makamu wa Rais.

Kuhusu kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema magonjwa yasiyo ya kuambukiza yameendelea kuua watu kwa kasi katika nchi zinazoendelea Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia kwenye Tamasha la Uelimishaji na Upimaji Afya na Kinga dhidi ya Magonjwa yasiyoambukiza kwa watoto na vijana kwenye uwanja wa michezo wa shule ya msingi Kinyerezi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiteta jambo na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla wakati Tamasha la Uelimishaji na Upimaji Afya na Kinga dhidi ya Magonjwa yasiyoambukiza kwa watoto na vijana kwenye uwanja wa michezo wa shule ya msingi Kinyerezi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Meza Kuu Ifurahia Jambo.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwaaga wageni mbalimbali waliofika kwenye Tamasha la Uelimishaji na Upimaji Afya na Kinga dhidi ya Magonjwa yasiyoambukiza kwa watoto na vijana kwenye uwanja wa michezo wa shule ya msingi Kinyerezi. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Mhe.Sophia Mjema
Burudani mbalimbali zilitolewa kwenye tamasha hilo 



Viewing all 110150 articles
Browse latest View live




Latest Images