Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109973 articles
Browse latest View live

WADAU WA JOTOARDHI WAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Juliana Pallangyo akifungua warsha ya siku moja ya wadau wa Jotoardhi uliofanyika katika Kituo cha mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam leo Juni 15 2017. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogspot) 
Ofisa misitu Mkuu Kitengo cha Nishati Mbadala, Paul Kiwele akiongea wakati wa Warsha ya wadau wa Jotoardhi iliyofanyika Dar es Salaam leo. 
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania, Mhandisi Kato Kabaka akiwasilisha mada wakati wa Warsha ya wadau wa Jotoardhi iliyofanyika Dar es Salaam leo. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Juliana Pallangyo (katikati) akibadilishana mawazo na Meneja Maendeleo wa Biashara pia Mwanajeolojia Mwandamizi wa Kampuni ya GeothermEx, Ann Robertson-Tait baada ya kufungua warsha ya siku moja ya wadau wa Jotoardhi uliofanyika katika Kituo cha mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania, Mhandisi Kato Kabaka. 
Meneja Maendeleo wa Biashara pia Mwanajeolojia Mwandamizi wa Kampuni ya GeothermEx, Ann Robertson-Tait akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Carbon Counts, Mshauri wa Nishati na Mabadiliko ya Tabia Nchi Paul Zakkour (kushoto) na Mshirika wa Kampuni ya Norton Rose Fulbright, Richard Metcalf walipohudhuria warsha hiyo. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Juliana Pallangyo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo. 


Mamlaka ya Mapato ya Tanzania yatumia Tehama kuboresha utoaji wa huduma zake kwa umma

$
0
0
Serikali Mtandao inarahisisha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa umma. Usikose kuangalia kipindi hiki cha Seikali Mtandao katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) uone jinsi wanavyotumia mifumo mbalimbali ya TEHAMA katika kazi zao za kila siku.

CCM YAWATAKA WALIOTAJWA KATIKA TAARIFA MBILI ZA UCHUNGUZI WA MCHANGA KUTOA USHIRIKIANO KWA VYOMBO VYA DOLA

$
0
0
Chama Cha Mapinduzi kimewataka viongozi waliotajwa katika taarifa mbili za uchunguzi wa Mchanga wa Madini kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola kwa kuwa wamelisababishia Taifa hasara kubwa ya Matrilioni ya Fedha, kutokana na Mchanga wa Madini kwenda nje ya nchi.

Mbali na hilo Chama kimesisitiza kuwa hakitasita kuchukua hatua kwa wanachama wake iwapo watabainika kuliingizia Taifa hasara kupitia Mchanga wa Madini, ila kwa sasa kinaviachia kwanza vyombo vya dola vifanye kazi yake ya kuwahoji waliotajwa kwenye ripoti hizo mbili.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Hamphrey Pole Pole, amesema CCM imetoa pongezi za dhati kwa Rais Dkt Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM kwa hatua yake ya uthubutu wa kusimamia raslimali za Taifa. 

Pole Pole amesema katika Histori ya nchi hatua zilizochukuliwa na Rais Magufuli hazijawahi kuonekana popote, hivyo inashangaza kuona baadhi ya Wanasiasa wanakejeli hatua hizo za kishujaa zilizochukuliwa na Kiongozi wa nchi. 

Pamoja na mambo mengine, Pole Pole, amesema kilichofanywa na Rais Magufuli ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ambayo imeelekeza kukomesha wizi unaofanywa na baadhi ya Wawekezaji katika Migodi ya Madini hapa nchini. 

Hata hivyo, CCM kimepongeza hatua za awali zilizooneshwa na MmIliki wa Kampuni ya Acacia kwa kukiri kukosea na kuahaidi kufanya mazungumzo na serikali ili kulipa kiasi cha pesa kinachodaiwa na Tanzania.

BENKI YA CRDB KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KWA WIKI NZIMA NCHINI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

BENKI  ya CRDB imeamua kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika mwaka huu kwa kutoa elimu kwa wazazi kuhusiana na  masuala mbalimbali yanayohusu mtoto ili kuweza kuwajenga vizuri katika malezi.

Siku ya Mtoto Afrika kila mwaka yanadhimishwa Duniani huku Benki ya CRDB  ikiadhimisha kwa mwaka wa tano mfululizo ikiwa ni muendelezo wa kuhakikisha watoto na kuwaelimisha wazazi watakaofika katika matawi ya benki huyo..

Akizungumza na waandishi wa habari, MkurugenzI Mtendaji wa CRDB Charles Kimei amesema kuwa wao kama beki ya CRDB wataadhimisha siku ya mtoto wa Afrika katika kila tawi kwani ni siku muhimu kwa kila mtoto nchini kwetu.

"Tutaadhimisha siku ya mtoto Afrika nchini kwetu katika kila tawi la benki yetu pia itakuwa ni siku muhimu sana na kuienzi kwa kuelimisha wazazi masuala mbalimbali ya watoto,"alisema Kimei.

Kimei amesema kuwa,kuanzia kesho itakuwa ni wiki ya ya mtoto wa Afrika katika benki yao na watatoa elimu mbalimbali, kuelimisha wazazi masuala ya watoto pamoja na kuwahamasisha kufungua akaunti ya watoto ya Junior Jumbo.

Mbali na kuwa na elimu mbalimbali zinazohusu watoto, kila tawi la CRDB limejipanga kuhakikisha linatoa huduma nzuri kwa wateja watakaokuja siku ya kesho na wiki nzima kiujumla na hivyo ni katika kuboresha maisha ya mtoto wa kesho.

"Kuwa na wiki hii itakayokuwa inaadhimisha siku ya mtoto wa Afrika na wazazi watapewa elimu kwa watoto wao, pia CRDB wamelenga zaidi katika kusaidia mazingira ya watoto kupitia nyanja ya elimu  na kufanya hivyo ni kuboresha maisha ya mtoto wa kesho,"
amesema Kimei.

Amemalizia kwa kusema kuwa wateja watakaojitokeza ndani ya wiki ya mtoto wa Afrika katika matawi ya benki ya CRDB watahudumiwa kipekee na zaidi amewaomba kwenda kwa wingi kupata elimu mbalimbali kuhusu watoto na kuwafungulia akaunti kwa manufaa ya baadae.

MkurugenzI Mtendaji wa CRDB Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari kuelekea siku ya Mtoto wa Afrika itakayoazimishwa siku ya kesho na wao kama CRDB wataiadhimisha kwa wiki nzima ili kutoa elimu  kwa wazazi kuhusiana na  masuala mbalimbali yanayohusu mtoto ili kuweza kuwajenga vizuri katika malezi.
Waandishi wa habari wakimsikiliza MkurugenzI Mtendaji wa CRDB Charles Kimei.

WATANO WATIWA MBARONI KWA KUJIHUSISHA NA SHUGHULI ZA UHAMIAJI

$
0
0
 Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

Kamishana wa usimamizi wa mipaka idara ya Uhamiaji Tanzania, Samwel Magweiga, amepiga marufuku Mawakala wanaojihusisha na shughuli za uhamiaji na kuwataka waache mara moja kufanya hivyo.

Badala yake amewataka wananchi wanaohitaji huduma hiyo kufika ofisi husika ya Uhamiaji.

Kamishana Magweiga ametoa wito huo leo, wakati akizungumzia ukamatwaji wa watu watano wenye umri wa kati ya miaka 55 na 64 ambao walikutwa wakimiliki ofisi na mitambo wa kughushi nyaraka mbalimbali ikiwamo ya kughushi miradi ya maendeleo ya Serikali na machine za risiti za kielektroniki (EFDs).
Kufuatia ukamataji huo, Kamishna Magweiga amewaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa idara ya Uhamiaji ili kudhibiti mianya ya watu wanaojihusisha na kughushi nyaraka za aina mbalimbali kwa kuwa zinapelekea uhujumu wa uchumi.

Mapema wiki hii, makachero kutoka ofisi za uhamiaji baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasalimia wema kuhusu kuwepo kwa hujuma hiyo, walifanya msako na kuwakamata wazee watano ambao ofisi yao ipo eneo la BibiTiti Mohammed kiwanja namba 16/47 lililopo Wilaya ya Ilala mtaa wa Mtendeni.

Wazee waliokamatwa ni Hemed Ali Mchepe(56), Edga Samson Mwafongo(55), Huruma Mwakidete(57), David Tumpange (64),At human Mohammed (61) na Simon Joseph Veso (62).


Amesema, “kuna magenge ya wahalifu huko mitaani ambao wanafanya kazi kwa niaba ya serikali, hawa ni wahujumu uchumi, ni lazima wafichuliwe.” Amesisitiza Kamishna Magweiga.


Ameongeza kuwa, nyaraka hizo za mara nyingi zimekuwa zinatumika kuchukua hati za kusafiria, mikopo benki na kupelekea benki husika kupata hasara na serikali kukosa mapato.

Amesema, upelelezi dhidi ya watuhumiwa hao umekamilika na siku yoyote watapelekwa mahakamani ila badoa wanahitaji kujua mtandao wao ni mkubwa kiasi gani na upo hapa nchini pekee ama na nje ya nchi.

Wakielezea jinsi walivyokamatwa mbele ya Kamishana mzee David Tumpange alikubali kuwa yeye ni mmiliki wa ofisi iliyokutwa na nyaraka hizo za kughushi iliyopo eneo la barabara ya Bibi Titi Mohammed na kwamba yeye hashughuliki nayo alimkabidhi ndugu yake Huruma Mwakidete.

Aliongeza kuwa, kwa sasa yeye anajishughulisha na masuala ya ujenzi na siku ya tukio, alikwenda kwenye ofisi yake hiyo kwa ajili ya kumsalimia ndugu yake huyo aliyemkabidhi ofisi na vyote vilivyokutwa humo havitambui.

PRECISION AIR SASA KUTUA SERENGETI

$
0
0
Shirika la Ndege la Kitanzania Precision Air limetangaza kuanzisha rasmi safari za ndege katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, kupitia uwanja ndege wa Seronera. Safari hizo zitazinduliwa rasmi tarehe 1 Oktoba 2017. Tangazo hilo limetolewa huku shirika hilo pia likitarajia kuanzisha safari kati ya Tanzania na Uganda kupitia Uwanja wa kimataifa wa Entebbe mwanzoni mwa mwezi Julai.

Precision Air imekua ikafanya safari za kuelekea Seronera kupita utaratibu wa kukodishwa, na kuanza kwa safari hizi kutaifanya Precision Air kuwa shirika la kwanza ambalo ni mwanachama wa IATA kufanya safari za kwenda hifadhi ya Serengeti.

Mkurugenzi wa Biashara wa Precision Air Bw. Robert Owusu amesema Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ni moja ya maajabu saba ya Dunia na ni moja sehemu nzuri ambayo kila mtu hana budi kutembelea, na ili kufanikisha hilo Precision Air itafanya safari nne kwa wiki kati ya Dar es Salaam – Seronera na Zanzibar.

“Safari zetu kuelekea Seronera zinakwenda kufanya mapinduzi ya safari za kitalii. Sasa watalii watakuwa na uwezo wa kutua moja kwa moja ndani ya Hifadhi ya Serengeti na kupata fursa ya kutumia mda mrefu zaidi ndani ya hifadhi, tofauti na awali ambapo walitumia muda mwingi barabarani. Ratiba ya safari zetu itakua kila siku ya Jumatatu,Jumatano,Jumamosi na Jumapili.” Ameeleza Bw.Owusu.

“Tunaamini kupitia safari hizi watalii wanaoitembelea Hifadhi ya Serengeti wataongezeka. Tumejidhatiti kutoa huduma za uhakika na kuchangia katika maendeleo ya utalii nchini.” Shirika la Ndege la Precision Air lilianzishwa mwaka 1993 kama kampuni binafsi ya usafiri wa anga ikitumia Ndege aina ya Piper Aztec inayobeba abiria watano.

Mwanzoni Precision ilikua ikitoa hudma za usafiri wa anga kwa watalii waliokua wakitembelea vivutio vya mali asili katika hifadhi za Taifa za Serengeti,Ngorongoro na Visiwa vya Zanzibar na maeneo mengine nchini.

Shirika hilo limekua siku hadi suku na kuwa moja ya mashirika yanayoheshimika katika ukanda wa Afrika Mashariki na Afrika. Precision Air inafanya safari zake kutokea Dar es Salaam (makao makuu) kuelekea Arusha, Bukoba, Kigoma, Kilimanjaro, Musoma, Mtwara, Mwanza, Tabora, Zanzibar and Nairobi.

Watanzania watakiwa kumuunga mkono Rais Magufuli kwenye vita ya kulinda rasilimali za Taifa

$
0
0
Watanzania wametakiwa kumuunga mkono Rais John Magufuli kwenye vita ya kulinda rasilimali za nchi aliyoianzisha kwani kwa muda mrefu watu wachache walishiriki kufuja mali za nchi ambazo zingetumika kwa manufaa ya watu wengi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Hudson Starnley Kamoga aliyasema hayo kwenye maadhimisho ya siku ya albino duniani, ambayo kimkoa ilifanyika kituo cha 4 Angle mji mdogo wa Haydom, alipokuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa mkoa huo Dr Joel Nkaya Bendera.

Alisema vita ya kulinda rasilimali ya nchi inapaswa kuungwa mkono kwani utajiri wa nchi ya Tanzania haulingani na hali halisi iliyopo kutokana na watu wachache kupora utajiri kupitia madini mbalimbali.

Alisema ana imani Rais Magufuli na watanzania kwa ujumla watashinda vita ya kulinda rasilimali kwani kupitia ripoti ya pili ya makania imeonyesha namna wananchi wanyonge wanavyoibiwa.

“Pamoja na kuathimisha siku ya albino duniani tunapaswa kumuunga mkono Rais Magufuli katika vita hii ya kusimamia na kulinda rasilimali za nchi kupitia madini yetu kwani nia ya dhati ameionyesha,” alisema Kamoga.

Alisema aliwaagiza watumishi wa halmashauri hiyo waangalie kwenye runinga na yeye mwenyewe aliiangalia ripoti hiyo kwa lengo la kumuunga mkono Rais Magufuli katika kusimamia rasilimali zilizopo kwenye eneo hilo.

"Ukiisikiliza kwa makini hiyo taarifa ya pili ya makinikia na sisi ambao tunafanya kazi ya kumsaidia Rais kutimiza ndoto yake ya kuhakikisha kuwa wananchi wanyonge wanafaidika na rasilimali waliyonayo unaweza ukalia kwa sababu hali iliyopo ni tofauti na uhalisia," alisema Kamoga.

Alisema wananchi na viongozi wanapaswa kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli na endapo dhamira ya dhati itakuwepo kwa wote rasilimali za nchi zitawanufaisha wananchi wote.

Naye, Mwenyekiti wa chama cha maalbino mkoani Manyara, Joseph Masasi alisema wanakabiliwa na changamoto ya kutobaini idadi kamili ya watu wenye ualbino mkoani humo hivyo kukosa takwimu sahihi.

Masasi alisema tatizo hilo linasababisha hata kukitokea tatizo lolote linalohitaji msaada kwao inakuwa vigumu kwani wengine wanakosa kutokana na kutobainishwa kwa idadi yao katika wilaya za mkoa huo.

Alisema pia wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa mafuta maalum ya kujipaka kwa watu wenye ualbino yanayowasaidia kila siku ili wasiathiriwe na mionzi ya jua na kusababisha baadhi yao kuathirika.

“Pamoja na hayo tunashukuru kwenye mkoa wa Manyara hakuna matukio ya watu wenye ualbino kuuawa au kukatwa viungo na watu makatili ila kuna badhi ya matishio madogo madogo,” alisema Masasi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Joseph Mandoo alisema halmashauri yao itaendelea kushirikiana na uongozi wa ualbino kwa ajili ya kuhakikisha wanatoa msaada unaohitajika kwa watu hao.

Mandoo alitoa wito kwa wazazi na walezi wenye watoto wenye ualbino kutowafisha ndani na badala yake wawafikishe kwenye sehemu husika ili pindi misaada itakapotolewa waweze kupatiwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Hudson Starnley Kamoga, akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) katika maadhimisho ya siku ya albino duniani ambayo kimkoa ilifanyika Mji mdogo wa Haydom wilayani Mbulu.

Mamlaka ya Mapato ya Tanzania yatumia Tehama kuboresha utoaji wa huduma zake kwa umma

$
0
0
Serikali Mtandao inarahisisha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa umma. Usikose kuangalia kipindi hiki cha Seikali Mtandao katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) uone jinsi wanavyotumia mifumo mbalimbali ya TEHAMA katika kazi zao za kila siku.

UKATILI WA KINGONO BADO CHANGAMOTO KWA WASICHANA HAPA NCHINI

$
0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Hamis Kigwangalla pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Taifa Joheli Festo wakiangalia ripoti iliyozinduliwa leo na shirika Save the Children kuhusu hali ya ndoa za ututoni duniani wakati wa Kongamano la Siku ya Mtoto wa Afrika liliofanyika leo katika mji wa Dodoma.
1.Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Hamis Kigwangalla akihutubia wajumbe wa Kongamano la Siku ya Mtoto wa Afrika liliofanyika leo katika mji wa Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akihutubia wajumbe wa Kongamano la Siku ya Mtoto wa Afrika liliofanyika leo katika mji wa Dodoma.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Hamis Kigwangalla akipata Maelekezo kutoka kwa Afisa Mwandamizi masuala ya Watoto wa Wizara yake kuhusu kazi za Wiazara wakati wa Kongamano la Siku ya Mtoto wa Afrika liliofanyika leo katika mji wa Dodoma.

DC SHINYANGA AFANYA ZIARA KATA YA DIDIA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

$
0
0

Mbali na kutembelea miradi hiyo ambayo mradi wa maji wa visima virefu,zahanati ya Didia na Kituo cha Polisi Didia pia amezungumza na wananchi wa kijiji cha Chembeli kilichopo katika kata ya Didia. 

Matiro alikuwa ameambatana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Shinyanga lakini pia watalaam mbalimbali kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo,Bakari Kasinyo. 

Tazama picha za matukio yaliyojiri wakati wa ziara ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa ziara yake leo Alhamis June 15,2017 katika kata ya Didia halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini ambapo alisisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa ndani ya jengo la Kituo cha Polisi Didia ambacho kipo mbioni kukamilika ujenzi wake 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisilikiza maelezo kutoka kwa diwani wa kata ya Didia Luhende Masele ambaye alisema ujenzi wa kituo hicho unalenga kuwasogezea karibu wananchi huduma za kipolisi ili kukabiliana na vitendo vya kihalifu katika mji wa Didia ambao una wafanya biashara wengi 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama akiondoka na msafara wake katika kituo cha polisi Didia kuangalia jinsi ujenzi unavyoendelea .
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro leo Alhamis June 15,2017 amefanya ziara katika kata ya Didia halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini na kukagua miradi ya maendeleo. 

UJENZI WA MAEGESHO YA KIVUKO CHA LINDI NA KITUNDA WAANZA

$
0
0
Na Alfred Mgweno - TEMESA Lindi

Mkandarasi aliyepewa kazi ya ujenzi wa maegesho ya kivuko katika maeneo ya Lindi na Kitunda tayari ameanza kazi hiyo na anatarajia kuikamilisha ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu. Akikagua maendeleo ya ujenzi huo, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu amemtaka Mkandarasi huyo kuhakikisha anamaliza kazi hiyo mapema iwezekanavyo hata kabla ya muda uliopangwa ili wananchi wa maeneo ya Lindi na Kitunda waanze kupata huduma ya kivuko.

Amesisitiza kuwa Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuondoa kero ya usafiri kwa wakazi wa maeneo hayo hivyo ujenzi wa maegesho hayo uende kwa kasi huku ukizingatia matakwa ya kiufundi na ubora wa hali ya juu.

Aidha Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Lindi ambao ni msimamizi wa mradi huo, Mhandisi Margwe Boay alionyesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi huo na kumtaka Mkandarasi kumaliza kazi hiyo mapema iwezekanavyo.

Mhandisi Boay, alimhakikishia Dk. Mgwatu kuwa wataisimamia kazi hiyo kwa kadri ya uwezo wao ili Mkandarasi akabidhi kazi ndani ya muda uliopangwa.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Hematec Investment Limited inayojenga maegesho hayo Mhandisi Emmanuel Lyimo, amesema mradi huo utakamilika kwa wakati na kuahidi kuwa kufikia mwisho wa mwezi Juni ujenzi wa maegesho upande wa Lindi utakuwa umefikia hatua nzuri na hatimae kuendelea na ujenzi upande wa Kitunda.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Lindi Mhandisi Margwe Boay (wa kwanza kulia) akielekeza jambo wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa maegesho ya kivuko kati ya Lindi na Kitunda unaoendelea mkoani hapo, wa pili kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu. Serikali inatarajia kupeleka kivuko eneo hilo mara baada ya ujenzi wa maegesho hayo kukamilika.
Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle (wa nne kulia) akisisitiza jambo wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa maegesho ya kivuko kati ya Lindi na Kitunda unaoendelea mkoani Lindi, kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu.
Mkandarasi wa kampuni inayojenga maegesho ya kivuko kati ya Lindi na Kitunda Mhandisi Emmanuel Lyimo (wa kwanza kulia) akimuelekeza jambo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa maegesho unaoendelea mkoani Lindi. Serikali inatarajia kupeleka kivuko mara baada ya ujenzi wa maegesho hayo kukamilika.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Lindi Mhandisi Margwe Boay (wa pili kulia) akielekeza jambo wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa maegesho ya kivuko kati ya Lindi na Kitunda unaoendelea mkoani hapo, wa pili kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu. PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA)

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA MAAFISA MIFUGO WA WILAYA NA MIKOA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa Maafisa Mifugo wa Mikoa na Wilaya kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma Juni 15, 2017. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aki kukizindua kitabu  cha "Mwongozi wa kitaifa wa Usimamizi wa Huduma za Mifugo" kwenye Mkutano wa Maafisa Mifugo wa Wilaya na Mikoa kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma, Juni15, 2017.(picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Grace Matemu ambaye ni Meneja wa tawi la Benki ya NMB la Bunge wakati alipokwenda katika tawi hilo mjini Dodoma  kupata huduma za kibenki Juni 15, 2017.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA SPORTPESA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amekubali ombi la kuwa mgeni rasmi katika mchezo kirafiki kati ya Timu ya Everton ya nchini Uingereza na timu ya Gor Mahia ya Kenya ambayo ilitwaa kombe la michuano ya Sportpesa iliyofayika hapa nchini hivi karibuni.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amekubali ombi hilo baada ya Kukutana na kufanya mazungumzo na Watendaji wa Kampuni inayojishughulisha na ubashiri wa michezo ya Sports Betting nchini ambao waliongozwa na Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji Tarimba Abbas Ikulu- Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amepongeza mipango na mikakati mizuri ya kampuni hiyo ya kutaka kukuza vipaji vya wanamichezo hasa kwa mpira wa miguu kwa Tanzania Bara na Zanzibar na kusema kama malengo hayo yatafikiwa Tanzania itakuwa bora katika mchezo wa mpira wa katika bara la Afrika na Dunia kwa ujumla.

Makamu wa Rais pia amewahakikishia watendaji wa kampuni hiyo kuwa milango ya ofisi yake ipo wazi na pindi wakiwama katika jambo lolote wawasiliane na ofisi yake ili tatizo linalowakabili liweze kutafutiwa ufumbuzi ili lisikwamishe shughuli za kampuni hiyo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya ubashiri wa michezo ya SportPesa Bw. Pavel Slavkov (kushoto), katikati ni Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji Bw. Abbas Tarimba.Viongozi hao wa SportPesa walimtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wa SportPesa waliofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa lengo la kujitambulisha.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa SportPesa Tanzania. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

NAIBU WAZIRI WA AFYA MHE.KIGWANGALLA AZINDUA RIPOTI YA WATOTO LEO MJINI DODOMA

$
0
0
Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Dk Khamis Kigwangalla akionyesha Ripoti ya Watoto baada ya kuizindua leo Mjini Dodoma.Kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi Sihaba Nkinga na Kushoto kwake ni Mwenyekiti Baraza la Watoto Joel Kiyungu.
Naibu Waziri Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Dk Khamis Kigwangalla, Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto(Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi Sihaba Nkinga na Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Joel Kiyunga wakionyesha Ripoti ya Watoto baada ya kuzinduliwa leo Mjini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto(Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi Sihaba Nkinga akisoma kipeperushi katika banda la UNICEF  katika kongamano la Watoto,Wazazi/Walezi na Wadau katika kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika Mkoani Dodoma.

Naibu Waziri Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Dk Khamis Kigwangalla akipata maelezo baada ya kutembelea banda la Plan Internaltional katika kongamano la Watoto,Wazazi/Walezi na Wadau katika kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika Mkoani Dodoma.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

EMPLOYMENT OPPORTUNITIES


TASUBA WAPAMBA KONGAMANO LA KIGODA CHA MWALIMU NYERERE CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

$
0
0
 Wasanii wa kutoka Tasisi Sanaa Bagamoyo ,TASUBA, Wakipiga ngoma wakati wa onesho lao katika kigoda cha Mwalimu Nyerere lililofanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam
 Mmoja wasanii kutoka TASUBA akitamba na igizo  wakati wa onesho lao katika kigoda cha Mwalimu Nyerere lililofanyika katika ukumbi wa nkurumah Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam
 Wasanii wa kutoka Taasisi Sanaa Bagamoyo ,TASUBA, Wakicheza mchezo wa jukwaani wakati wa onesho lao katika kigoda cha Mwalimu Nyerere lililofanyika katika ukumbi wa nkurumah Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam
  Mmoja wasanii kutoka TASUBA akitamba na igizo  wakati wa onesho lao katika kigoda cha Mwalimu Nyerere lililofanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam
  Mmoja wasanii kutoka TASUBA akitamba na igizo  wakati wa onesho lao katika kigoda cha Mwalimu Nyerere lililofanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

KUFUNGIWA KWA GAZETI LA MAWIO

DMF, CBA BANK WASHIKIANA NA MPANGO WA TAIFA WA DAMU SALAMA KATIKA ZOEZI LA UCHANGIAJI DAMU, MBAGALA JIJINI DAR

$
0
0
Afisa Muuguzi kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Cesilia Meela akiwatoa damu baadhi ya Wakazi wa eneo la Mbagala, Jijini Dar es salaam wakati wa zoezi la kuchangia damu lililofanywa na Taasisi ya Doris Mollel kwa kushirikiana na Benki ya CBA, iliyofanyika kwenye Kituo kikuu cha Mabasi, Mbagala Rangi Tatu, jijini Dar es Salaam jana. Jumla ya Units 106 zilipatikana.
Sehemu ya Wakazi wa eneo la Mbagala Rangi Tatu wakishiriki zoezi la uchangiji damu, llililofanywa na Taasisi ya Doris Mollel kwa kushirikiana na Benki ya CBA, iliyofanyika kwenye Kituo kikuu cha Mabasi, Mbagala Rangi Tatu, jijini Dar es Salaam jana.
Mdau Pina Mshana alikuwa ni mmoja wa waliochangia damu katika zoezi hilo, ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya siku ya Damu Duniani.
Wachangia damu wakiwa kwenye foleni.

DIRA YA DUNIA YA BBC SWAHILI JUNI 15, 2017

MANISPAA YA KINONDONI YATAKA BILIONI 4 ZILIZOPO KWENYE AKUNTI ZA KATA ZITUMIKE KWENYE MIRADI ILIYOKUSUDIWA

$
0
0
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni ,Benjamini Sitta akizungumza wakatiwa kikao cha baraza la Madiwani katika ukumbi wa Manispa ahiyo Magomeni jijini Dar es Salaam, juni 15, 2017.

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Baraza la Madiwani la Manispaa ya Kinondoni limeagiza kuhakikisha fedha zote zilizopo katika akaunti za kata zaidi ya Bilioni 4.9 zifanyiwe utaratibu wa manunuzi ili ziweze kutekeleza miradi iliyokusudiwa katika kata hizo.

Maazimio hayo yamefikiwa katika baraza la Madiwani wa Manispaa hiyo lililongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo, Benjamini Sitta .

Aidha baraza hilo pia limeridhia maombi ya kamati ya Fedha kwa kutaka kubuni vyanzo vipya vya fedha vitakavyosaidia Halmashauri hiyo kupata fedha zaidi licha ya baadhi ya vyanzo kuhamia serikali kuu. 

pia kikao hicho kilipitisha azimio la kumpongeza Rais John Pombe Magufuli kwa kitendo chake cha kizalendo cha kuhakikisha kuwa fedha za watanzania zilikuwa zinapotea kutokana na mchanga wa Madini uliokuwa ukisafirishwa nje kiholela unapangiwa utaratibu wa kunufaisha Serikali.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ,Aron Kangurumjuli aakizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani.
Diwani wa Kata ya Magomeni, Julian Bujugo akichangaia katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Kinondoni.

Viewing all 109973 articles
Browse latest View live




Latest Images