Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1748 | 1749 | (Page 1750) | 1751 | 1752 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Na Fredy Mgunda, Iringa.

  Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alilazimika kufanya kazi ya uokoaji wa maiti ya mchimbaji madini katika mgodi wa Nyakavangala bwana Vaspa nyenza mkazi wa Itengulinyi Kata ya Ifunda wilaya ya Iringa kwa takribani masaa kumi na nane

  Kasesela alisema kuwa alianza kazi hiyo majira ya saa mbili asubuhi alipowasili katika mgodi huyo wa Nyakavangala lakini yeye,waandishi wa habari na viongozi wengine wa wilaya ya Iringa walijitahidi kuokoa mwili wa marehemu hadi majira ya saa sita usiku lakini zoezi hilo lilikuwa likiendelea

  "Hadi saizi tumepiga dua zote lakini hali ngumu sijui nini kinaendelea katika hili shimo maana waokoaji kila wakiukaribia mwili wa marehemu miamba laini inavungika na kujaza udongo ndani ya shimo ndio maana mmeniona naangaika na ndugu wa marehemu kujaribu kusali huku na kule lakini hali ni ngumu hadi muda huu wa saa tano usiku"alisema Kasesela

  Aidha Kasesela aliwataka ndugu wa marehemu na viongozi mbalimbali kuwa na subila wakati wanalishugulikia swala la kuokoa mwili wa mpendwa wao kwa kuwa wameshaukaria mahali ulipo.

  "Ungalia tayari kichwa na kiwiliwili vimeshaonekana kwa hiyo tumebakiza sehemu ndogo tu naombeni tuwe wavumilivu kwa kuwa tuvumilia toka siku ya jumapili hadi usiku huu basi tuungane kumuombea mwenzetu ili tutoe mwili wake ukiwa salama" alisema Kasesela
  Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa katika mgodi wa nyakavangala uliopo katika Kata ya malengamakali Mkoani Iringa wakati wa Juhudi za kuuokoa mwili wa marehemu viskadi nyenza katika shimo alilosimama Mkuu huyo wa Wilaya.
  Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akisaiadiana na wachimbaji madini katika mgodi wa nyakavangala ili kuokoa mwili wa marehemu Nyenza
  Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alipokuwa akiwasili katika mgodi wa nyakavangala uliopo Kata ya malengamakali Mkoani Iringa.  0 0
 • 06/14/17--22:50: Article 15


 • 0 0

  Mwanasayansi Samweli Mduma akipima kiasi cha damu ambacho ni mililita 450 iliyotolewa leo na Frank Mapunda katika kituo cha kuchangia damu cha Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kuchangia damu Dunia ambayo kaulimbiu yake ni Changia damu, Changia sasa, Changia mara kwa mara.
  Afisa Mtoa Damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama Peter Chami akiangalia wingi wa damu ya Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Pedro Pallangyo ambayo aliitoa katika kituo cha kuchangia damu cha Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kuchangia damu Dunia ambayo kaulimbiu yake ni Changia damu, Changia sasa, Changia mara kwa mara.
  Mwanasayansi Samweli Mduma akitafuta mshipa wa damu kwa ajili ya kumtoa damu George Marcus katika kituo cha kuchangia damu cha Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kuchangia damu Dunia ambayo kaulimbiu yake ni Changia damu, Changia sasa, Changia mara kwa mara.
  Mtoa huduma Jema Mwampashi akipima wingi wa damu ya mmoja wa wachangia damu aliyefika katika kituo cha kuchangia damu cha Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwa ajili ya kuchangia damu ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kuchangia damu Dunia ambayo kaulimbiu yake ni Changia damu, Changia sasa, Changia mara kwa mara. Picha na JKCI.

  0 0

  Kundi la Uigizaji wa Filamu ‘Bongo Movie Shinyanga’ limempongeza rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa hatua anazozichukua katika kulinda rasilimali za nchi hususani madini ya Tanzania.
  Mwenyekiti wa Bongo Movie Shinyanga, Juma Songoro amesema rais Magufuli anapaswa kuungwa mkono na wananchi wote wa Tanzania na wazalendo wote."Wasanii wa filamu mkoa wa Shinyanga tunampongeza sana rais Magufuli kwa hatua anazozichukua kulinda nidhamu na rasilimali za nchi,tunamuombea kila la heri atufikishe tunapopatarajia,tumeandaa filamu hii kama zawadi yetu kwake na na watanzania wote",amesema Songoro.
  Katika kufikisha pongezi hizo,Bongo Movie Shinyanga wameandaa Filamu fupi inaitwa'Tanganyika Karne ya 18' inayoonesha  jinsi nchi za nje zinavyoiba madini ya Tanzania.
  TUMIKA DAKIKA ZAKO 3 TU KUTAZAMA FILAMU HII HAPA CHINI

  0 0

  .Washirika wa maendeleo nchini wamekutana jijini Dar es Salaam leo kujadili, pamoja na mambo mengine, umuhimu wa usafi wa mazingira katika lishe bora kwa watoto na kuunga mkono kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira yenye kauli mbiu ya “Nipo Tayari”. 

  Kampeni hiyo inayoratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Njisia, Wazee na Watoto imejikita katika kuhamasisha watu, mijini na vijijini, kujenga utamaduni wa kuwa na vyoo na kuvitumia kikamilifu na kunawa mikono na sabuni mara baada ya kutoka chooni. 

  “Bila kuzingatia usafi wa mazingira, lishe bora kwa mtoto inaweza kuathiriwa na magonjwa ya kuhara kama vile kipindupindu, hivyo kuondoa virutubisho vyote mwilini. Ndio maana usafi wa mazingira na lishe bora kwa watoto ni vitu vinavyotakiwa kwenda pamoja”, anasema Dkt Generose Mulokozi kutoka shirika la IMA World Health. 

  Akizungumza katika mkutano huo, Mratibu wa kampeni hiyo ya kitaifa Bw. Anyitike Mwakitalima alisema: “Mazingira machafu na ukosefu wa vyoo umethibitika kuwa chanzo kikubwa kinachosababisha kudumaa kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano. Takwimu zinaonyesha kwamba asilimia 34 ya watoto wa umri huo nchini wamedumaa kutokana na kuishi katika mazingira yasiyokuwa na vyoo na kutozingatia kanuni za afya. 

  Alisema kuwa ukosefu wa lise bora pia hupunguza kinga ya mwili kwa watoto hivyo kuugua mara kwa mara na kuwafanya kushindwa kukua vizuri kimwili na kiakili. 
  Mratibu wa kampeni ya kitaifa Bw. Anyitike Mwakitalima akizungumza wakati wa mkutano kujadili uhusiano kati ya usafi wa mazingira na lishe bora kwa watoto jijini Dar es Salaam juzi.
  Dkt Generose Mulokozi (kulia) kutoka shirika la IMA World Health akisema ‘Nipo Tayari’ kuunga mkono kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira kwa lengo la kuzuia magonjwa ya kuhara kama vile kipindupindu yanayogharimu maisha ya Watanzania. 
  Mtaalamu wa lishe wa Unicef Mauro Brero akitoa ishara ya kuunga mkono kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira yenye kauli mbiu ya Nipo Tayari ikiwa na lengo la kuzuia magonjwa ya kuhara kama vile kipindupindu yanayogharimu maisha ya Watanzania.
  0 0


  0 0

  Rais anakubalika zaidi miongoni mwa makundi ya wazee na wenye kiwango kidogo cha elimu

  15 Juni 2017, Dar es Salaam: Asilimia 71 ya wananchi wanaukubali utendaji wa Rais Magufuli tangu alipoingia madarakani. Kiwango hiki kimeshuka kutoka asilimia 96 mwezi Juni 2016.  Viwango vya kukubalika kwa Rais vinatofautiana katika makundi mbalimbali:
  • Asilimia 68 wenye umri chini ya miaka 30 wanamkubali Rais ikilinganishwa na asilimia 82 wenye umri zaidi ya miaka 50
  • Asilimia 75 ya wananchi wenye elimu ya msingi au chini yake wanamkubali Rais ikilinganishwa na asilimia 63 ya wale wenye elimu ya sekondari au zaidi
  • Asilimia 75 ya wananchi masikini wanamkubali Rais ikilinganishwa na asilimia 66 ya wananchi matajiri.
  Viwango vya kukubalika kwa viongozi wengine navyo pia vimeshuka katika kipindi hicho hicho.
  • Wabunge:  Kukubalika kwa utendaji wa wabunge kumeshuka kutoka asilimia 79 (Juni 2016) hadi asilimia 58 (Aprili 2017).
  • Madiwani: Kukubalika kwa utendaji wa madiwani kumeshuka kutoka asilimia 74 (Juni 2016) hadi asilimia 59 (Aprili 2017).
  • Wenyeviti wa vijiji/mitaa: Kukubalika kwa utendaji wa wenyeviti wa vijiji/mitaa kumeshuka kutoka asilimia 78 (Juni 2016) hadi asilimia 66 (Aprili 2017).
  • -----------------------------------------------------------
   15 June 2017, Dar es Salaam: 
   Seven out of citizens (71%) approve of the performance of President Magufuli since taking office. This is down from 96% in June 2016. Approval ratings for the President vary between groups.
   • 68% of those under age 30 approve of the President compared to 82% of those over 50
   • 75% of citizens with no education or some primary approve of the President compared to 63% of those with secondary education or higher
   • And approval is slightly higher among poorer citizens (75%) than among the richest (66%).
   Approval ratings for other political leaders have also fallen over the same period.
   • MPs: 58% approval rating (April 2017) compared to 68% (June 2016)
   • Councilors: 59% approval rating (April 2017) compared to 74% (June 2016)
   • Village / street chair-people: 66% approval rating (April 2017) compared to 78% (June 2016)
  • KUPATA TAARIFA KAMILI BOFYA HAPA/FOR MORE CLICK HERE

  0 0


  0 0
  0 0
 • 06/15/17--02:00: Article 7

 • 0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  WAKALA WA NISHATI VIJIJINI (REA)
  Juni 16, 2017

  Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unatambua kuwa baadhi ya wakandarasi wanaotekeleza miradi ya kusambaza umeme vijijini hawajakamilisha miradi kwa mujibu wa MIKATABA waliyosaini na Wakala (REA). Aidha, kuna baadhi ya wakandarasi wamekamilisha miradi lakini hawajakabidhi rasmi miradi hiyo na vifaa au hawajafanya marekebisho kasoro zilizobainishwa na wasimamizi wa miradi kutoka (TANESCO na REA).

  Kwa tangazo hili, Wakala unawataarifu wakandarasi wote ambao hawajakamilisha matakwa hayo ya kimikataba kufanya hivyo mara moja. Wakandarasi watakaoshindwa kutimiza masharti hayo hawataruhusiwa kushiriki katika zabuni zitakazotangazwa na Wakala (REA) baada ya TANGAZO hili na hatua nyingine zitachukuliwa juu yao kwa mujibu wa mikataba hiyo.


  Imetolewa na:
  Mkurugenzi Mkuu
  Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
  Jengo la Mawasiliano, Ghorofa ya 2
  Barabara ya Sam Nujoma, 14414
  S. L. P 7990
  Dar es Salaam, Tanzania
  Barua Pepe: info@rea.go.tz
  Simu: +255 22 2412001, +255 22 2412002, +255 22 2412003
  Nukushi: +255 22 2412007 

  0 0

  Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Dk Richard Masika(wa tatu kushoto) na Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology(DIT)Profesa Preksedia Marco Ndomba(wa pili kulia) wakisaini mkataba wa mashirikiano (MoU) kati ya taasisi hizo mbili. MoU imejikita kwenye ushirikiano wa Utafiti, Taaluma, kubadilishana wataalamu, ziara za kitaaluma kwa wanafunzi.
  Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Dk Richard Masika(kushoto) na Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology(DIT)Profesa Preksedia Marco Ndomba(kulia) wakisaini mkataba wa mashirikiano (MoU) kati ya taasisi hizo mbili uliofanyika katika chuo cha ufundi Arusha. 
  Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Dk Richard Masika(kushoto) na Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology(DIT)Profesa Preksedia Marco Ndomba(kulia) wakibadilishana mkataba wa mashirikiano (MoU) kati ya taasisi hizo mbili uliofanyika katika chuo cha ufundi Arusha. 
  Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology(DIT)Profesa Preksedia Marco Ndomba(kulia) akizungumza jambo baada ya taasisi hiyo na Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)kuweka saini mkataba wa mashirikiano (MoU) kati ya taasisi hizo mbili uliofanyika katika chuo cha ufundi Arusha,kushoto ni Dk Richard Massika. 

  0 0

  Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga (Kulia)akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Sweden Nchini Mhe. Katarina Rangnitt katika ukumbi wa Wizara Juni 14,2017. Katika mkutano huo walijadiliana masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano wa Tanzania na Sweden pamoja na hali ya usalama nchini Burundi.
  Mheshimiwa Waziri Mahiga, Balozi wa Sweden nchini pamoja na Wataalam kutoka Wizarani wakiwa katika mkutano huo,

  0 0

  Na  Bashir  Yakub.           

  Jirani  yako  au  mtu  mwingine  yeyote  amejenga   na  kuziba  njia. Njia  yoyote iwe  kubwa  kama  barabara  ama  ndogo  ambayo  hata  gari  haiwezi  kupita. Iwe  tu kama  ya   pikipiki  au  baiskeli au hata  ya  miguu  tu.  Yote  haya  hayajalishi  na hizi  zote  ni  njia kwa  mujibu  wa  sheria.


  1.HAKI  YA  NJIA  KISHERIA .

  Kifungu  cha  151  cha  sheria  namba  4  sheria  ya  ardhi  ya  mwaka  1999 kinaeleza  haki  hii. Kinaitambua  haki  hii  kwa  kusema  kuwa  haki  ya  njia  ipo  kwa  njia  zile  ambazo  ni  kwa ajili  ya  matumizi  ya  umma.  Umma  hapa  humaanisha  watu  wote  lakini  pia  wakazi  wa  eneo  fulani  wanaotumia  njia  hiyo  kwa  ajili  ya  shughuli  zao  mbalimbali.

  Kifungu  kimepanua matumizi  ya  njia  ya  umma  kwa   kumaanisha  hata  njia  zilizotengwa  kwa ajili  ya  makampuni  binafsi. 

  Kwa  mfano  kuna  sehemu  ukipita  utaona njia  au  sehemu  ya  lami  ya  barabara imekatwa  maalum  kwa  ajli  ya  kuruhusu watu  au magari  ya  kampuni  fulani  kupata  sehemu  ya  kuingilia.


  Lakini  pia  zipo  njia  zimetengwa  kwa  ajili  ya  shughuli  za serikali. Haraka  utaona  kuwa haki  ya njia  haijagusa tu  kule  mitaani  wanakoishi  watu  tu  bali  hata  sehemu  za  makampuni  binafsi  nk.


  2.   KUZIBA  NJIA  YA  UMMA.


  Kuziba  njia  ya  umma  ni  kosa  kwa  mujibu  wa  kifungu  cha  177( 4 )  cha  sheria  ya  ardhi. Wako  watu  wakorofi  huko  mitaani  huziba  njia  kwa  makusudi.  Yawezekana kabisa  mtu  akiwa  anajua kabisa eneo  fulani  ni  njia  na  watu  hupita  hapo  lakini  kwa makusudi  au bila  kujali  akajenga  ukuta au akaweka uzio  wa  sinyenge  au  akapanda  mti  pale  au  akaweka  kifusi au  kwa  namna  nyingine  yoyote. 


  Na  wengine  huambiwa  na  watu  lakini  wasisikie   kwasababu  ya  pesa,  au  urafiki  na  viongozi  wa  serikali  au  cheo  au  rushwa  au  vinginevyo.  Basi  yatupasa  kujua kuwa  watu  hawa  huwa  wakitenda  makosa  na si  wakunyamazia.


  Njia  kuzibwa si  lazima  iwe  imezibwa yote.  Hata kuibana na kuitoa  katika  uhalisia  wake  katika  kiwango  chochote  nako  ni  kuziba  njia.  Njia  yafaa  iachwe  vilevile  ilivyo.

            
    KUSOMA  ZAIDI sheriayakub.blogspot.com
  0 0

  Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mwakilishi Mkaazi wa UNIDO nchini, Bw.Stephen Bainous Kargbo, Juni 14,2017, katika ukumbi wa Mikutano Wizarani. 
  Mhe. Waziri Balozi Augustine Mahiga (Katikati), Mwakilishi Mkaazi wa UNIDO, Bw. Stephen(Kushoto) Bainous Kargbo na kulia ni Balozi Grace Martin, Mkurugenzi Idara ya Itifaki wakiwa katika mazungumzo.
  Mhe. Waziri Balozi Mahiga, Mwakilishi Mkaazi wa UNIDO na Wataalam kutoka Wizarani na Ofisi za UNIDO wakiwa katika picha ya pamoja baada ya makabidhiano ya Hati za Utambulisho..

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akijibu Maswali Bungeni mjini Dodoma Juni 15, 2017. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenya Ulemavu, Jenista Mhagama bungeni mjini Dodoma, Juni 15, 2017. 
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Katibu wa Bunge, Dkt, Thomas Kashililah, Mbunge wa Igunga, Dkt.  Dalaly Kafumu na Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia kwenye viwanja wa Bunge mjini Dodoma Juni 15, 2017.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitea na Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 15, 2017. 
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mbunge wa Rombo, Joseph Selasini kwenye jengo la Utawala la Bunge Juni 15, 2017.

  0 0


  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akizungumza na Ujumbe wa Madaktari wa Kichina wanaotoa huduma katika Hospitali mbali mbali za Unguja na Pemba wakiongozwa na Balozi Mdogo wa China anayefanyia kazi Zanzibar Mhe.Xie Xiaowu (wa tatu kulia) katika mazungumzo yao aliwakaribisha Madakatari 21 wapya na kuwaaga 21 waliomaliza muda kutoka  Jamhuri ya Watu wa China katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akizungumza na Ujumbe wa Madaktari wa Kichina unaoongozwa na Balozi Mdogo wa China anayefanyia kazi Zanzibar Mhe.Xie Xiaowu (wa pili kushoto) katika mazungumzo yao Rais aliwakaribisha Madakatari 21 wapya na kuwaaga 21 waliomaliza muda kutoka  Jamhuri ya Watu wa China (hawapo pichani) katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo,(kushoto) Kiongozi wa Madakatari waliomaliza muda Xu Zhuoqun.
   Baadhi ya Madakatari wa Kichina waliofika Ikulu Mjini Unguja kuoanana na Rais leo ambapo jumla yao ni  Aroubaini na mbili wakiwemo wapya Ishirini na moja wanaomaliza muda wao wa kazi waliofika kumuaga Rais na Ishirini na Moja walikaribishwa na Rais katika mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Mjini Unguja.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na  Ujumbe wa Madaktari wa Kichina unaoongozwa na Balozi Mdogo wa China anayefanyia kazi Zanzibar Mhe.Xie Xiaowu (wa nne kushoto) baada ya mazungumzo na kuwaaga Madaktari hao waliomaliza muda wao wa kazi hapa Nchini, leo walipofika Ikulu Mjini Unguja.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akimkaribisha Kiongozi wa Madaktari wapya Ishirini na moja kutoka Jamhuri ya Watu wa China Wang QI baada ya mazunguzo na Madaktari hao waliofika Ikulu Mjini Unguja leo wakiongozwa na Balozi Mdogo wa China anayefanyia kazi Zanzibar Mhe.Xie Xiaowu (katikati) Kiongozi wa Madaktari waliomaliza muda Xu Zhuoqun.

  0 0


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  MASHINDANO ya Sprite Bball Kings 2017 yanaendelea tena wikiendi hii kwa michezo mitano kupigwa katika

  Viwanja vya Bandari, Mivinjeni huku washindi wa jumla wa mechi hizo wataungana na wa wiki iliyopita.

  Hii ni wiki ya tatu toka kuanza kwa mashindano hayo ikizikutanisha timu 52 kutoka sehemu mbaalimbali za Mkoa wa Dar es Salaam.Katika michezo ya wiki hii.

  Katika wiki hii, kutakuwa na michezo mitano itakayowakutanisha Ukonga Warrior dhidi ya Mchenga Team, Heroes B dhidi ya Ardhi University na mechi ya tatu ni kati ya Flying Dribblers na UDSM.
  Mechi ya nne ni kati ya Kigamboni Heroes na St Lous Montfort huku DMI wakivaana na nOsterbay michezo itakayoanza mida ya saa 2 asubuhi mpaka sa 12 jioni.


  Mratibu wa mashindano hayo ya Sprite Bball Kings 2017 Basilisa Basike amesema hii ni muendelezo wa hatua ya pili baada ya wiki iliyopita kuchezwa kwa mechi nne na zingine tano zinamalizika wikiendi hii.


  "Baada ya michezo hiyo, washindi wa jumla wataungana na wale wa wiki iliyopita na tutachezesha droo ya timu zitakazokutana ili kuingia hatua ya tatu ya Sprite Bball Kings 2017," amesema Basilisa.

  Michuano hiyo inayodhaminiwa na Sprite kwa kushirikiana na East Africa Tv na Redio inaendelea tena wikiendi hii katika viwanja vya Bandari, Mivinjeni  na mshindi kamili ataondoka na kitita cha shiling milion 15.


  0 0

  Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

  Upelelezi dhidi ya kesi ya kumshambulia askari polisi inayomkabili aliyekuwa Naibu Waziri wa fedha na mbunge wa Mkuranga, Adam Kigoma Malima umekamilika.

  Mwendesha Mashtaka, Wakili wa Serikali Esta Martin amemueleza Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa kesi hiyo leo ilikuja kwa kutajwa."Mheshimiwa, kesi hii Leo imekuja kwa kutajwa lakini upelelezi umekamilika, tu naomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuja kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali (PH), amedai Martin.

  Hakimu Mwambapa ameiahirisha kesi hiyo kwa niaba ya Hakimu Mkazi Respecious Mwijage ambaye ndio amepangwa kusikiliza kesi hiyo kwa kuwa anaudhuru.

  " Hakimu aliyepangwa kusikiliza kesi hii anaudhuru, naiahirisha hadi Julai 10 itakapokuja kwa ajili ya kusomewa PH mbele ya Hakimu husika", amesema Hakimu Mwambapa

  Malima anashtakiwa pamoja na dereva wake Ramadhani Mohamed Kigwande anayekabiliwa na tuhuma za kujeruhi.Katika hati ya mashtaka ilidaiwa kuwa, Mei 15 mwaka huu huko Masaki katika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam mshtakiwa Malima alimzuia afisa wa polisi mwenye namba H.7818 PC Abdul kufanya kazi yake ya kumkamata dereva wake Kigwande aliyekuwa amefanya kosa la kumjeruhi Joseph Mwita ambaye ni afisa operation wa Priscane Business Enterprises.

  Ilidaiwa kuwa, siku na mahali hapo, mshtakiwa Kigwande kwa nia ya kukataa kukamatwa, alimjeruhi afisa operation hiyo(Joseph Mwita) ambaye alikuwa anakamatwa kwa kosa la kupaki gari vibaya na kumsababishia Mwita Majeraha Mwilini.

  Watuhumiwa wote wako nje kwa dhamana na upelelezi bado haujakamilika.

  Aidha, Wakili wa utetezi Peter Kibatala ameshindwa kuwasilisha pingamizi la awali juu ya mapungufu ya kisheria yaliyopo kwenye shtaka la shambulio linalomkabili Malima Peke yake kwa kuwa Hakimu husika anaudhuru.

  Mapema mwzi huu, Kibatala aliitaarifu Mahakama kuwa leo angewasilisha pingamizi kuwa shtaka linalomkabili Malima, maelezo ya kosa na tuhuma hazifanani.

older | 1 | .... | 1748 | 1749 | (Page 1750) | 1751 | 1752 | .... | 3286 | newer