Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110119 articles
Browse latest View live

MAGAZETI YA LEO JUMATANO JUNE 14, 2017


VETA na Airtel watangaza kozi 5 mpya za ufundi stadi kupitia simu ya mkononi

$
0
0
Mamlaka ya elimu ya ufundi Tanzania (VETA) kwa kushirikiana Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia application ya VSOMO leo wametangaza na kuzindua kozi mpya za ufundi stadi za VETA zitakazotolewa  kupitia simu za mkononi ili kuwawezesha watanzania kujiunga na kupata utaalamu na vyeti vya VETA kwa gharama nafuu

Kozi hizo mpya zinazoongezwa katika mfumo wa vsomo ni  Huduma ya chakula na mbinu za kuhudumia wateja, Matengenezo ya kompyuta,umeme wa viwandani, ufundi Bomba wa Majumbani na Umeme wa magari.

Tangu kuzinduliawa kwa mfumo huu wa mafunzo kwa njia ya mtandao kupitia application ya VSOMO mwezi wa Juni 2016 ulianza kutoa kozi mbalimbali za ufundi za VETA ikiwemo Ufundi umeme wa manyumbani, Ufundi pikipiki, Ufundi wa simu za mkononi, Ufundi Alluminium,  Utaalamu wa maswala ya urembo pamoja ma Ufundi wa kuchomea vyuma.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel, Beatrice Singano, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kozi tano mpya kwenye awamu ya pili ya mpango wa kutoa mafunzo ya ufundi stadi kupitia programu ya VSOMO inayoratibiwa na kampuni ya Airtel. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dk. Bwire Ndazi.

Lengo la mfumo huu likiwa ni kutimiza dhamira ya VETA ya kutanua wigo wa mafunzo ya ufundi stadi nchini na kuongeza idadi ya vijana kujipatia fani mbalimbali za ufundi ili waweze  kuajirika  au kujiajiri.  Mafunzo haya yanawawezesha wanafunzi kujisomea wakati wowote kwa gharama nafuu kupitia simu zao za mkononi za Airtel.

Mfumo huu wa masomo kwa njia ya Mtandao VSOMO,  sasani maarufu kwa vijana ambapo takwimu zinaonyesha zaidi ya vijana 30,000 tayari wamepakua application ya VSOMO, 8000 wamejiandikisha na kati yao 50 wanasoma kozi mbalimbali zilizopo pia wapo waliomaliza na kupata vyeti vya VETA.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dk. Bwire Ndazi akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kozi tano mpya kwenye awamu ya pili ya mpango wa kutoa mafunzo ya ufundi stadi kupitia programu ya VSOMO inayoratibiwa na kampuni ya Airtel, Dar es Salaam jana.Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel, Beatrice Singano.

Akiongea wakati wa kuzindua na kutangaza kozi hizo, Mkuu wa chuo cha Veta Kipawa, Eng. Lucius Luteganya alisema “mafunzo ya ufundi kwa njia ya mtandao ya VSOMO yametuwezesha kuongeza wigo na kuwafikia watanzania wengi nchini. Tunaamini bado tunayofursa ya kuongeza wigo  zaidi na kuongeza idadi ya vijana wenye ueledi ili kwenda sambamba na agenda ya serikali ya awamu tao ya uchumi wa viwanda kwa kupata nguvu kazi yenye taaluma muhimu katika kuendesha uchumu wa nchi”

“Tunaamini kozi hizi mpya zitatawavutia vijana wengi kujiandikisha, kusoma na kupata ujuzi zaidi.”  Alisisitiza Eng Luteganya

Eng, Luteganya alisema kuwa  “Ili kupata mafunzo ya VSOMO kupitia Airtel, ukiwa na Airtel pakua application katika google play store, na kujisajiri na kisha chagua kozi inayokidhi mahitaji yao.

ili kuhakikisha tunasimamia viwango vya elimu vilivyowekwa na VETA, wale watakaomaliza masomo yao nadharia kupitia VSOMO watafanya mtihani ili kufaulu na kujiunga na mafunzo ya vitendo katika vituo vya VETA vilivyopo nchi nzima. Vyeti vya kuhitimu mafunzo vitatolewa kwa wale watakaofaulu mafunzo katika hatua zote mbili ya nadharia na vitendo”.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dk. Bwire Ndazi akionyesha jinsi ya kutumia simu ya mkononi kupata progaramu ya masomo ya mafunzo ya ufundi Stadi VSOMO wakati wa uzinduzi wa programu ya pili ya mfunzo hayo jana.Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel, Beatrice Singano na Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam,Habib Burko.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya alisema “Tunajisikia furaha kuongeza kozi nyingi zaidi katika mfumo huu  wa masomo kwa njia ya mtandao wa VSOMO  kwani itatuwezesha kufikia idadi kubwa ya vijana wanaosoma kwa kupitia simu zao za mkononi. Lengo letu ni kuhakikisha tunakuwa na kozi nyingi ili kwenda sambamba na matarajio na mahitaji ya wanafunzi na watanzania kwa ujumla”.

Tunapenda kuwapongeza wote waliojiunga na kumaliza kozi zao na kuhimiza wote ambao hawajapakua application ya VSOMO kufanya hivyo kwa kujiandikisha katika mojawapo ya kozi 12 zinazopatikana katika application ya VSOMO kwa gharama nafuu ya shilingi 120,000 tu na  kulipia kwa njia ya Airtel Money kwa kupiga *150*60#.

Tunapenda kuwahimiza vijana kutumia fursa hii na kujiunga na kozi na kujisomea wakati wowote na mahali popote. kozi hizi zinazochukua hadi mienzi mitatu kumalizika lakini pia zinaweza kuisha mapema kulingana na muda utakaotengwa na mwanafunzi kuweka bidii ili kumaliza mapema.

Wafanyakazi wa Hospitali ya Sanitas wajitolea damu

$
0
0
Kuelekea siku ya kuchangia damu duniani, Hospitali ya Sanitas iliyopo Mikocheni imeandaa kambi ya kuchangia damu ambayo ilifanyika siku ya jumanne, Juni 13 2017.

Katika kambi hiyo jumla ya chupa za damu 50 zilikusanywa ambapo wachangiaji walikuwa ni wafanyakazi wa hospitali hiyo na baadhi ya watu kutoka nje ambao walijumuika na wafanyakazi hao hao kwa ajili a uchangia damu kwa ajili ya wahitaji.

Akizungumzia kambi hiyo ya kutoa damu, Meneja Msaidizi wa Hospitali ya Sanitas, Dr. Sajjad Fazel alisema utoaji wa damu huo ni muhimu kwa kusaidia maisha ya watu wengine kwani hata chupa moja ya damu ina muhimu mkubwa na inaweza kusaidia kuoa maisha ya watu watatu.

"Kuna uhaba wa damu, kwa kila Mtanzania ahakikishe kuwa anaonyesha uzalendo na upendo wako kwa Watanzania wenzake kwa kuchangia damu na kuokoa maisha yao," alisema Dk. Fazel.

Dk. Fazel alisema makundi ambayo yana uhitaji mkubwa wa damu ni wajawazito waliokuwa na tatizo wakati wa kujifungua, watoto waliokuwa na upungufu wa damu, watu waliokuwa na ugonjwa wa sikla na watu waliokuwa wamepata ajali na wanaofanyiwa upasuaji.

MAFANIKIO YA TANZANIA KATIKA NAFASI YA UENYEKITI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO 

Februari 2015,  Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta alimkabidhi Rais mstaafu wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete nafasi ya Uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika mkutano wa 16 wa Wakuu wa Jumuiya hiyo Jijini Nairobi Kenya. 

Kutokana na hali ya mgogoro wa kisiasa katika nchi ya Burundi, ambayo ilipaswa kukabidhiwa nafasi ya Uenyekiti wa Jumuiya mwaka 2016, Wakuu wa  Jumuiya hiyo waliamua kwa kauli moja kuwa Tanzania kupitia Rais Dkt. Rais John Pombe Magufuli kuendelea na nafasi hiyo. 

Katika Mkutano wa 18 wa kawaida wa Wakuu wa Jumuiya hiyo uliofanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Mei,2017,  Rais Magufuli alisema katika kipindi cha  Uongozi wa Tanzania katika Jumuiya hiyo  mafanikio mbalimbali yalipatikana ikiwemo utekelezaji wa ajenda ya utengamano katika eneo la ushuru wa forodha linaloshuguhulikia vikwazo vya biashara visivyo na kodi. 

Anasema katika ushirikiano wa kifedha Tanzania imewezesha kuandwa miswada ya uanzishwaji wa taasisi ya fedha ya Jumuiya itakayokuwa Taasisi ya mpito kabla ya kuanzishwa kwa Benki kuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Aidha, Rais Magufuli alisema mafanikio mengine ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ikiwemo mradi wa ujenzi wa barabara ya Arusha - Holili - Taveta hadi Voi, na kukamilika kwa upembuzi wa mradi wa barabara ya Malindi- Lungalunga- Tanga – Bagamoyo. 
Aidha Rais Magufuli alisema pia barabara za Lusahunga- Lusumo- Kigali na Nyakanazi- Kasulu- Rumonge –Bujumbura ziko kwenye hatua mbalimbali za usanifu, ikiwa ni sambamba na ujenzi wa vituo vya ukaguzi mipakani, ambapo vituo 9 kati ya 15 tayari vimeanza kufanya kazi.   

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Magreth Sinyangwa wa Kilosa Morogoro azoa Milioni 20 za Biko

$
0
0
MOTO wa bahati nasibu ya Biko ama ‘Ijue Nguvu ya Buku’, umezidi kuchanja mbuga baada ya droo yake ya 14 kufanyika leo jijini Dar es Salaam, huku mkazi wa Kilosa Morogoro, Magreth Sinyangwa, akiwa mwanamke wa kwanza kuzoa jumla ya Sh Milioni 20 zinazotolewa na waendeshaji wa bahati nasibu hiyo inayotikisa hapa nchini.

Droo hiyo iliyompelekea utajiri mshindi huyo wa Morogoro, imechezeshwa na Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja na kushuhudiwa pia na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humud Abdulhussein.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa droo hiyo, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema moto wa Biko umezidi kuchanja mbuga baada ya kumpata mshindi wao wa Sh Milioni 20, huku kwa mara ya kwanza wakimpata mshindi ambaye ni mwanamke tangu kuanzishwa kwa bahati nasibu yao.

Alisema washindi hao ni wale wanaocheza bahati nasibu yao kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu zao za M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money, ambapo watatakiwa kuingia kwenye lipa bili au lipa kwa M-Pesa na kuingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 na namba ya kumbukumbu 2456 tayari kwa kucheza.

“Baada ya kuingiza namba ya kumbukumbu pia atatakiwa kuweka kiasi cha kucheza ambacho kinaanzia Sh 1000 na kuendelea ambapo kiasi cha Sh 1000 kitampatia nafasi mbili ambazo ni ushindi wa papo kwa hapo pamoja na donge nono la Sh Milioni 20 kwa Jumapili ijayo kama tulivyompata mwingine kwa droo tuliyochezesha jana.

“Kwa zawadi za papo kwa hapo zinaanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja ambapo mshindi hutumiwa fedha zake dakika chache baada ya kupokea ujumbe wa Biko ukimtaarifu juu ya ushindi wake kutokana na kucheza Bahati Nasibu yetu,” Alisema Heaven na kuwataka Watanzania wacheze mara nyingi zaidi ili waweze kujiwekea mazingira mazuri ya kuibuka na zawadi mbalimbali za Biko.
Balozi wa Biko Kajala Masanja na mwakilishi wa Bodi Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humud Abdulhussein, wakihakiki namba ya mshindi wa Sh Milioni 20 kutoka Kilosa, mkoani Morogoro, Magreth Sinyangwa na kumpigia ili kumjulisha juu ya ushindi wake.
Balozi wa Biko Kajala Masanja akiagana na mwakilishi wa Bodi Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humud Abdulhussein, mara baada ya kumaliza kuchezesha droo ya 14 ya Sh Milioni 20 iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam, huku Magreth Sinyangwa akiwa mwanamke wa kwanza kuibuka na mamilioni hayo ya Biko tangu kuanzishwa kwa bahati nasibu hiyo hususan kwa droo kubwa za Sh Milioni 10 hadi 20.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DC BYAKANWA ASIMAMIA ZOEZI LA UONDOSHAJI WA MIUNDO MBINU YA UMWAGILIAJI KATIKA SHAMBA LA KILIMO CHA KISASA LA MBOWE

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Hai,akiwaongoza wajumbe wa kamati ya ulinzi na Usalama ya wilaya Hai ,pamoja na askari Mgambo wakiingia katika shamba la Kilimo cha Kisasa cha Mboga mboga la Kilimanjaro Vegees Ltd linalomilikiwa na Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe.
Shamba la Kilimo cha Kisasa,(Green House) lililopo Nshara Machame wilaya ya Hai la Kilimanjaro Vegees Ltd.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akiwa na kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Hai,wakiwa katika moja ya shamba hilo pamoja na asakari polisi wenye silaha wakiondoa miundo mbinu ya umwagiliaji pamoja na unyunyiziaji wa dawa.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akizungumza katika eneo hilo wakati zoezi la kuondoa miundo mbinu katika eneo hilo ikiendelea.Zoezi hilo limefanyika kwa kile kinachodaiwa shughuli za kilimo kufanyika kando ya mto kinyume cha sharia.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

TAARIFA KUTOKA JESHI LA KUJENGA TAIFA (JKT)

MATUKIO KATIKA PICHA: YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 47 CHA MKUTANO WA SABA WA BUNGE LA 11 LEO JUNE 14, 2017.

$
0
0
 Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu akiongoza Kikao cha 47 cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo June 14, 2017 Mjini Dodoma.
 Mbunge Kyerwa (CCM) Mhe. Innocent Bilakwate akiuliza swali katika Kikao cha 47 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo June 14, 2017 Mjini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Ashatu Kijaji akijibu swali katika Kikao cha 47 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo June 14, 2017 Mjini Dodoma.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akijadiliana jambo na Mbunge wa Buyungu Mhe.Kasuku Bilago katika Kikao cha 47 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo June 14, 2017 Mjini Dodoma.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akiwasili Bungeni kuhudhulia Kikao cha 47 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo June 14, 2017 Mjini Dodoma.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akijadiliana jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Prof Jumanne Maghembe katika  Kikao cha 47 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo June 14, 2017 Mjini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS MAGUFULI NI MZALENDO NAMBA MOJA –DK BANA

$
0
0
Jovina Bujulu-MAELEZO.

Baadhi ya wasomi wameonyesha kuridhishwa na kuunga mkono hatua ya Rais John Magufuli kuagiza wahusika wote wachukuliwe hatua za kisheria baada ya kupokea ripoti ya pili ya Kamati ya Wachumi na Wanasheria aliyoiunda kwa ajili ya kuchunguza Mchanga wa Madini unaosafirishwa kwenda nje ya nchi.

Akiongea na Idara ya Habari (Maelezo) Dk Benson Bana ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alisema kitendo kilichofanywa na Rais Magufuli kimewafungua macho viongozi wengi wa Afrika na dunia na kitakuwa ni mfano wa kuigwa kwa Serikali nyingi za Afrika na dunia kwa ujumla

“Ningefurahi kama tungetenga siku maalumu kuandamana kwa nia ya kuunga mkono nia njema ya Rais ya kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi hii hazitumiwi hovyo hovyo” amesema Dk Bana.

Aliongeza kusema kuwa kitendo cha kutafuta ukweli katika makinikia na biashara ya madini na kuweka wazi taarifa hiyo kwa umma  na kusema wahusika wa sakata hilo wachukuliwe hatua za kisheria kimeonyesha uzalendo wa dhati kwa nchi yake.

Aidha aliunga mkono kitendo cha Rais kukubali kufanyia kazi mapendekezo yote 21 yaliyotolewa na Tume ya Uchunguzi, kwani yataweka wazi mwenendo mzima wa biashara ya madini na kuziba mianya ya wizi wa madini.

Dk. Bana alimpongeza pia Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Mwigulu Nchemba kwa kuchukua uamuzi wa haraka wa kuwazuia kusafiri nje ya nchi watuhumiwa wa sakata hilo.

Alisema wale wote waliotajwa kuhusika na suala hilo kukaa nje ya utumishi wa umma kwa muda wakati uchunguzi dhidi yao ukiendelea na  endapo watabainika kuwa hawana hatia warudishwe kazini na ikibainika kuwa walihusika wachukuliwe hatua stahiki.

Alitoa wito kwa Watanzania kuuunga mkono  nia njema ya Rais Magufuli kwa sababu hatua hiyo ni harakati za kuweka sawa uchumi wa nchi ili kuboresha maisha ya Watanzania.


Dkt. Benson Bana-Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 

WADAU WA KILIMO WAKUTANA KUJADILI MIKAKATI YA KUBORESHA UWEZESHAJI KWENYE KILIMO NA VIWANDA

$
0
0
Katika kuhakikisha dhamira ya Serikali ya dhamira ya Serikali ya kujenga Uchumi wa Viwanda wadau wa kilimo na viwanda wamekutana ili kuzungumzia nafasi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) katika  kuhakikisha Benki hiyo inasaidia sekta ya Kilimo nchini.

Wakizungumza katika Kikao hicho kilichoandaliwa na TADB ili kujadili mikakati ya kuboresha uwezeshaji kwenye kilimo na viwanda nchini.
Akizungumza katika kikao hicho Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga amesema kuwa Benki imejipanga kuleta matokeo makubwa kwenye mapinduzi ya kilimo na viwanda hasa vya uchakakataji na usindikaji wa mazao ya kilimo.

Bw. Assenga amesema kuwa mipango hii itasaidia upatikanaji wa mali ghafi kwa viwanda vya ndani hivyo kusukuma ndoto ya Serikali kufikia lengo lake la Kujenga Uchumi wa Viwanda na kuhuisha uwekezaji kwenye Viwanda vidogo vidogo na vya kati vya usindikaji na uchakataji wa mazao ya Kilimo na mifugo.

“Benki imejikita kwenye kusaidia Sekta ya Kilimo iweze kusukuma dhamira ya Serikali ya Uchumi wa Viwanda uweze kutoa matunda yaliyokusudiwa ili kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini,” alisema.

Bw. Assenga amesema katika kuhakikisha azma hiyo inatimia TADB imejipanga kutoa elimu ili kuwajengea uwezowakulima na taasisi mbali mbali za fedha pamoja na vyama vya ushirika kuweza kukopa toka TADB pamoja na kushirikiana na wadau mbali mbali kusaidia uwekezaji mkubwa kwenye Sekta ya Kilimo ili iweze kuinua pato la Taifa na kumkomboa Mwananchi.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji huyo ameongeza kuwa TADB imeanza kujiimarisha  na kuchochea mabenki na taasisisi za fedha kuongeza utoaji wa mikopo na fedha zingine kwenye Sekta ya Kilimo ili kuongoza utoaji mikopo ya uongezaji wa thamani katika shughuli za kilimo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB), Bibi Rosebud Kurwijila (kushoto) akizungumza na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mzee Peniel Lyimo (kulia) wakati wa Kikao cha Wadau wa Kilimo Kujadili Mikakati Ya Kuboresha Uwezeshaji Kwenye Kilimo Na Viwanda kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Biashara ya TADB, Bibi Rehema Twalib (kulia) akizungumza wakati wa Kikao cha Wadau wa Kilimo Kujadili Mikakati Ya Kuboresha Uwezeshaji Kwenye Kilimo Na Viwanda kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam.
 Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mzee Peniel Lyimo (kulia) akiongoza Kikao hicho.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kushoto) akisisitiza nafasi ya Benki yake katika kuleta matokeo makubwa kwenye mapinduzi ya kilimo na viwanda hasa vya uchakakataji na usindikaji wa mazao ya kilimo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WIZARA MALIASILI KUPITIA BODI YA UTALII TTB YATOA SEMINA KWA WABUNGE WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA PIC MJINI DODOMA

$
0
0
NA HAMZA TEMBA - WMU

Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii Tanzania TTB, imefanya semina ya mafunzo ya siku moja kwa wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kwa lengo la kuwajengea uelewa wajumbe hao kuhusu majukumu ya taasisi hiyo ambayo imefanyika jana mjini Dodoma na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Ramo Makani na Katibu Mkuu, Meja Jenerali Gaudence Milanzi.

Akizungumza katika semina hiyo, Meneja wa Huduma za Utalii wa taasisi hiyo, Philip Chitaunga alisema bodi hiyo iliyoanzishwa mwaka 1993 ilipewa jukumu la jumla la kukuza sekta ya utalii nchini ikiwemo kutumia mbinu mbalimbali za utangazaji, kuhamasisha uendelezaji wa mazao ya utalii na miundombinu yake, kufanya tafiti za masoko na utalii kwa ujumla pamoja na kuhamasisha uelewa wa watanzania kufahamu umuhimu na faida za utalii.

Alisema taasisi hiyo imefanya juhudi mbalimbali za kutangaza utalii wa Tanzania nje ya nchi ikiwemo kuratibu ziara za waandishi wa habari za kitalii, kuweka matangazo katika magazeti ya utalii ya kimataifa, kushiriki katika maonesho ya utalii ya kimataifa na kutangaza kupitia Televisheni za kimataifa kama CNN ya Marekani.

“Jitihada zingine tulizofanya ni kutumia balozi zetu nje ya nchi na mabalozi wa utalii wa hiari yaani 'Goodwill Ambasadors', kutumia mitandao ya kijamii na matangazo kwenye vyombo vya usafiri vya umma ambapo mwaka 2008 hadi 2009 tulitangaza kwenye mabasi 124 jijini london Uingereza, taxi 100, treni mbalimbali na katika uwanja wa ndege wa Heathrow” alisema Chitaunga.

Alisema jitihada za hivi karibuni za kutangaza utalii zimefanyika kupitia michezo ya Ligi Kuu ya Uingereza ikiwemo timu za mpira wa miguu za Seattle Sounders na Sunderland, kupitia majarida, CD na filamu fupi kwa lugha mbalimbali kama Kiingereza, Kijerumani, Kifaransa na Kiswahili. Pia, kupitia tovuti maalum ya utalii ya taifa (www.tanzaniatourism.gotz), App kwenye ‘Smart Phones’ na kufanya ziara za utangazaji wa utalii yaani Roadshows katika nchi za China, Afrika ya Kusini, bara la Ulaya, Amerika na Australia.
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kushoto) akizungumza jana mjini Dodoma katika semina iliyoandaliwa na Wizara hiyo kupitia Bodi ya Utalii Tanzania kwa ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kuhusu majukumu ya bodi hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Albert Obama. 
Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (kushoto) akizungumza jana mjini Dodoma katika semina iliyoandaliwa na Wizara hiyo kupitia Bodi ya Utalii Tanzania kwa ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kuhusu majukumu ya bodi hiyo. Katikati ni Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Albert Obama.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Albert Obama (kulia) akizungumza jana mjini Dodoma katika semina iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili kupitia Bodi ya Utalii Tanzania kwa ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe wa kamati hiyo kuhusu majukumu ya bodi hiyo. Katikati ni Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani na Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi. 
Meneja wa Huduma za Utalii wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Philip Chitaunga (kushoto) akiwasilisha mada ya jumla kuhusu shughuli za taasisi hiyo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) katika semina iliyoandaliwa na Wizara hiyo kupitia bodi hiyo mjini Dodoma jana. 

Maadhimisho ya Siku ya Kuchangia Damu Duniani Yafana Muhimbili

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imeshiriki katika madhimisho ya Siku ya Kuchangia Damu duniani kwa kuendesha shughuli ya utoaji damu kwa watu mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya huduma hiyo kwa wagonjwa wenye uhitaji.

Shughuli hiyo inaendelea katika hospitali hiyo kwenye Jengo la Maabara kuu ambako watu wamekusanyika kwa ajili ya kuchangia damu. Mmoja wa viongozi walishriki katika maadhimisho hayo ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Mheshimiwa Sophia Mjema pamoja na Watanzania mbalimbali.

Akizungumza katika shughuli hiyo Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo wakiwamo kinamama na watoto wadogo.

“Nawapongeza wote walifika leo hapa Hospitali ya Muhimbili kuchangia damu, ni jambo la muhimu mmefanya kwa ajili ya kuokoa maisha ya wagonjwa,” amesema Mheshimiwa Mjema.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi wa hospitali hiyo, Dk Praxeda Ogweyo amewataka wananchi,mashirika  ya umma na yasiyo ya kiserikali, shule, vyuo mbalimbali na taasisi za dini  kujitokeza kuchangia damu hospitali hapo.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Mheshimiwa Sophia Njema akizungumza na Jonas Hans Atile (kushoto) ambaye amejitokeza kuchangia Damu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo.
 Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi Katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Praxeda Ogweyo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Kuchangia Damu Duniani. Pia Dk. Ogweyo amewataka Watanzania wajitokeze kwa wingi kuchangia damu.
 Mmoja wa Wananchi akishiriki katika maadhimisho ya Siku ya Uchangiaji Damu duniani Leo katika hospitali hiyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

UZINDUZI WA WIKI YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA WAFANA LEO MJINI DODOMA

$
0
0
Watoto wa Shule ya Santhome ya Mjini Dodoma wakiongoza watoto wenzao kutoka shule mbalimbali za mji wa Dodoma kuelekea viwanja vya Nyerere Square kushiriki uzinduzi wa maonesho ya Wiki ya Siku ya Mtoto wa Afrika ambayo kilele chake ni tarehe siku 16 juni mwaka huu.
Kilanja Mkuu wa Shule ya Santhome ya Mjini Dodoma Martha Linje akiongoza watoto wenzake kutoka shule mbalimbali za mjini Dodoma kuelekea viwanja vya Nyerere Square kushiriki uzinduzi wa maonesho ya Wiki ya Siku ya Mtoto wa Afrika ambayo kilele chake ni tarehe siku 16 juni mwaka huu.
Baadhi ya watoto kutoka shule za msingi mjini Dodoma wakiwa na mabango ya kupinga ukatili dhidi ya watoto kuelekea viwanja vya Nyerere Square kushiriki uzinduzi wa maonesho ya Wiki ya Siku ya Mtoto wa Afrika ambayo kilele chake ni tarehe siku 16 juni mwaka huu.
Mkurugenzi wa Watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto pamoja na Mbunge viti maalumu ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya Siku ya Mtoto wa Afrika wakipata maelekezo kutoka Maofisa wa Plan International hawapo pichani mara baada ya kutembelea mabanda ya maonesho hayo.

TATIZO LA MKAA JIJINI DAR ES SALAAM KUMALIZWA

$
0
0
Na Tulizo Kilaga, Mafinga

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo amesema tatizo la uhaba wa mkaa jijini Dar es Salaam litakwisha kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Kampuni ya Tractor inayomiliki kiwanda cha kuzalisha na kusambaza mkaa endelevu kilichopo Mafinga mkoani Iringa.

Kiwanda hicho kinatarajia kuanza uzalishaji mwishoni mwa mwezi huu kwa kuzalisha tani 40 za mkaa kwa siku na kuzisambaza katika jiji la Dar es Salaam, Mwanza na Dodoma kwa kuanzia kutokana na miji hiyo kuwa na matumizi makubwa ya mkaa hali inayohatatisha Misitu ya Asili nchini.

Akizungumza mara baada ya kujionea uwekezaji uliofanywa na kiwanda hicho, Prof. Santos alisema kuanzishwa kwa kiwanda hicho kinachozalisha na kusambaza mkaa inaouzalisha kutokana na takataka zitokanazo na uchakataji wa mbao na mabaki ya miti kwa teknolojia ya kisasa kutasaidia kupunguza matumizi makubwa ya mkaa katika miji mikubwa ambayo imekuwa kichocheo cha ukataji wa miti katika mikoa mingine.

Inakadiriwa kuwa karibu hekta 300,000 hadi 400,000 za misitu ya asili huharibiwa kila mwaka kutokana na utengenezaji mkaa.

Prof. Santos alisema kuanzishwa kwa kiwanda hicho kutasaidia kuongeza ufanisi wa matumizi ya mazao ya misitu ya kupanda, utapunguza utegemezi wa nishati ya kuni na mkaa kutoka misitu ya asili na kuongeza uhakika wa upatikanaji wa nishati ya mkaa kwa miji mikubwa nchini sambamba na kuongeza mchango wa sekta ya misitu kwenye ushiriki wa uchumi wa viwanda nchini Tanzania.

Hata hivyo alisema jitihada hizo zitafanikiwa ikiwa watumiaji wa nishati ya mkaa watabadilika na kuwa na mtizamo chanya juu ya matumizi ya mkaa mbadala pamoja na nishati nyingine mbadala.

“Tuongeze kasi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabiawatu na kila mmoja kwa nafasi yake atimize wajibu wake ipasavyo, kwa pamoja tutafanikiwa kuinusuri nchi yetu kugeuka jangwa,” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Bw. Benjamin Lane alisema kiwanda hicho kitazalisha mkaa bora na kuhifadhiwa katika hali ya usafi kwenye mifuko ya kilo 50 na 25 kwa kuanzia ikiwa lengo nikuwa na mifuko hadi ya kilo moja itakayouzwa kwa bei rahisi zaidi ukilinganisha na bei ya mkaa halisi.

Lane alisema kuwa kiwanda hicho kimeamua kuwekeza kwenye uzalishaji mkubwa wa mkaa endelevu kwa lenga la kuiunga mkono serikali kutimiza adhima yake ya kuwa na matumizi endelevu ya misitu kwa faida ya vizasi vya sasa na vijavyo kwa kuhakikisha inatumia takataka zote zitokanazo na uchakataji wa mbao na mabaki ya miti kwa teknolojia ya kisasa kuzalisha mkaa.

Kwa upande wake, Meneja wa Shamba la Miti la Sao Hill, Bw. Saleh Baleko alisem shamba lake lina malighafi ya kutosha kukiwezesha kiwanda hicho kuwa na uzalishaji wa uhakika kutokana na wavunaji wengi nchini kutumia asilimia 70 tu ya eneo lote la uvunaji na kuacha asilimia 30 ikipotea ambayo sasa itatumika kuzalisha mkaa endelevu.

Akizungumza kuhusu mradi huo mmoja wa wananchi, Joyce Jonas alisema mradi huu ni mzuri na kuwaasa wawekezaji wengine kufanya uwekeza mkubwa kwenye mradi wa kuzalisha mkaa endelevu kutokana na kuwepo na mahitaji na matumizi makubwa ya mkaa ukilinganisha na viwanda vilivyopo

TAMKO LA SERIKALI KUHUSU MATUMIZI YA PICHA ZA MARAIS WASTAAFU KATIKA MAGAZETI NA MITANDAO YA KIJAMII KUHUSU SAKATA LA USAFIRISHAJI WA MCHANGA WA MADINI NJE YA NCHI


BREAKING NYUZZZZ....: Rais Dkt. Magufuli akutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick ya Canada Profesa John L. Thorton

$
0
0
Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick ya Canada Profesa John L. Thorton Ikulu jijini Dar es salaam. Katika mkutano huo, uliohudhuriwa pia na Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Paramagamba Kabudi na Balozi wa Canada hapa nchini, Ian Myles umemalizika kwa mafanikio makubwa ambapo pande zote zimekubaliana kukaa meza moja kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali katika sekta ya madini. Habari kamili yaja punde

Wakulima wa Tumbaku waomba serikali kupambana na changamoto zinazoikumba sekta hiyo

$
0
0
Rais wa Chama cha Wakulima wa Tumbaku Duniani(ITGA), Daniel Green(wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu mkutano unaoendelea wa kujadili changamoto zinazoikumba secta ya Tumbaku.Mazungumzo hayo yalifanyika katika Hoteli ya Lamada Dar es Salaam jana.Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Chama hicho(CEO), Antonio Abrunhosa na kutoka ktoka kulia ni Mtendaji Mkuu wa Chama cha Tumbaku Tanzania(FDTU), Miraji Mgalula na Mkurugenzi msaidizi wa Wizara ya Kilimo,Ufugaji na Uvuvi, Dk.Jackson Nkuba.
Mtendaji Mkuu wa Chama cha Wakulima Duniani(CEO), Antonio Abrunhosa (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu mkutano unaoendelea wa kujadili changamoto zinazoikumba secta ya Tumbaku unaofanyika katika Hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam.Kulia ni Rais wa Chama hicho, Daniel Green.
Mkurugenzi msaidizi wa Wizara ya Kilimo,Ufugaji na Uvuvi, Dk.Jackson Nkuba(kulia), akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu mkutano unaoendelea wa kujadili changamoto zinazoikumba secta ya Tumbaku unaofanyika katika Hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Rais wa Chama cha Wakulima wa Tumbaku Duniani, Daniel Green na Mtendaji Mkuu wa Chama hicho(CEO), Antonio Abrunhosa.
Mtendaji Mkuu wa Chama cha Wakulima wa Tumbaku Tanzania (Flue & Dark Tobacco Unio), Miraji Mgalula (kulia), akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu mkutano unaoendelea wa kujadili changamoto zinazoikumba secta ya Tumbaku unaofanyika katika Hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam.Wapili kushoto ni Mkurugenzi msaidizi wa Wizara ya Kilimo,Ufugaji na Uvuvi, Dk.Jackson Nkuba na Rais wa Chama cha Wakulima wa Tumbaku Duniani, Daniel Green.

KESI YA WEMA SEPETU YAPIGWA KALENDA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Usikilizwaji kesi ya dawa ya kulevya inayomkabili Miss Tanzania Wema Sepetu wapigwa kalenda.

Usikilizwaji wa kesi ya dawa za kulevya inayomkabili aliyekuwa Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu uliokuwa uanze leo, umesogezwa hadi Julai 10 mwaka huu sababu Hakimu anayesikiliza kesi hiyo yuko likizo.

Wema ambaye pia ni msanii wa filamu nchini, anashtakiwa na wafanyakazi wake wawili, Angelina Msigwa (21) pamoja na mkulima Matrida Abas (16) ambao wote kwa pamoja wanawakilishwa na Wakili Peter Kibatala.

Wakili wa Serikali, Elizabeth Mkunde amedai mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa kuwa kesi hiyo leo ilikuja kwa ajili ya kuanza kusikilizwa lakini Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba anayesikiliza kesi hiyo yupo likizo.

Kutokana na hali hiyo, Hakimu Mwambapa ameaihirisha kesi hiyo hadi Julai 10 mwaka huu kwa ajili ya kuanza kuja kusikilizwa.

Inadaiwa kuwa, Februari 4, mwaka huu huko nyumbani kwao Kunduchi Ununio jijini Dar es Salaam Watuhumiwa hao wote walikutwa wakiwa na msokoto mmoja pamoja na vipisi viwili vya bangi vyenye gramu 1.80 ambavyo ni dawa za kulevya.

Washitakiwa wote wako nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kila mshitakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao walisaini bondi ya milioni tano.

LIGI KUU MSIMU WA 2016/2017,MIZENGWE ILIZIDI.

$
0
0
Na Honorius Mpangala.

Wakati kipenga cha ufunguzi wa kigi kikipigwa agosti 20 mwaka 2016 kwa mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Azam na Yanga ilikua ni kitu kilichokua kikisubiliwa na wapenzi wengi kutokana na wadau kushuhudia usajili kabambe wa vilabu vyao.

Kuanza kwa ligi kuliweza kutoa harufu ya msisimko na ushindani katika msimu huo,mfano mechi ya kwanza kati ya Azam Fc dhidi ya African Lyon ilikua mechi ambayo iliwaduwaza sana mashabiki na benchi la ufundi la azam kutokana na shughuli waliyokutana nayo toka kwa vijana wa African lyon.

Azam katika mchezo huo ilisawazisha dakika za mwisho baada ya Lyon kutangulia kwa mpira wa kona ulioingia moja kwa moja na kumshinda kipa Aishi manula.

Kwa upande wa ratiba wadau wengi ambao wengi wao ni wanazi wa simba na yanga walilalamikia kwa kuona timu moja wapo ina pendelewa.

Changamoto ya ratiba imekua ni mfupa ulioshindikana kabisa kutokana ligi kusimama Mara kwa Mara au kutoa viporo kwa baadhi ya timu kutokana na kuwajibika kimataifa .

Mapendekezo yanayoweza kuwa bora ni uandaaji wa ratiba wa ligi kuu utazame kalenda ya FIFA  pamoja na ile ya CAF  ili wanapopanga wasiweze kuleta mkanganganyiko na kusababisha viporo.

Kwa upande wa usajili uliozua zengwe na kuleta mkanganyiko ni ule wa mchezaji Said mkopi aliyekuja kufungiwa baada ya Tanzania Prisons kupeleka pingamizi na kuonekana mkopi ana mkataba na klabu yake ya zamani huku akisajiliwa tena Mbeya City.

MAKINDA AWATAKA WANAWAKE LA BARA LA AFRIKA KUWA IMARA

$
0
0

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mtanzania ,Anna Makinda amewataka wanawake wa bara la Afrika kusimama imara ili waweze kuwa viongozi makini katika kupambana siasa kandamizi kwa Wanawake katika bara la Afrika.

Makinda amesema kuwa zaidi ya miongo kumi imetajwa kuwa huenda mwanamke wa kiafrika akapata ukombozi katika siasa za bara hili,ambazo zinatazamwa kuwa na mlengo wa mfumo dume tangu kuondoka kwa wakoloni .

Aidha hayo yamebainishwa katika mjadala wa kigoda cha Mwalimu unaofanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali,na kuongeza kuwa siasa za Africa bado zinawagawa wanawake katika mlengo wa kisiasa na kijamii.

"harakati na mambo mengi yamefanyika ili kumkomboa mwananmke wa Afrika na mfumo dume,lakini yote haya yanaonekana kutofanikiwa kwa asilimia miamoja na changamoto ikionekana kuwapo kwa wanawake wenyewe kwa kutothaminiana"amesema Makinda.

Anna makinda amekuwa kiongozi katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa serikali ya awamu iliopita,  anatazama changamoto hii kwa wasichana wa sasa kuwa ni kubwa sana kutokana na mazingira yanayowazunguka .
Spika wa Bunge Mstaafu, Anna Makinda akizungumza katika mkutano wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere chuo kikuu cha Dar es Salaam, ambapo mada ya Nafasi ya Wanawake na Siasa za vyama vingi katika bara la afrika iliwasilishwa na wanawake mbalimbali viongozi.
Mbunge wa Jimbo la Hanang,Mary Nagu akizungumza wakati wa kongamano la Kigoda cha Mwalimu Nyerere Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam ambapo mada ya nafasi ya Wanawake katika uongozi bara la afrika iliwasilishwa.
Mbunge wa Bunge la Uganda Miria Matembe, akizungumza wakati wa Kigoda cha Mwalimu juu ya nafasi ya Wanawake katika Siasa za Afrika 
Sehemu ya Washiriki waliofika kusikiliza kigoda Cha Mwalimu juu ya nafsi ya Mwanamke katika Siasa za bara la Afrika.

Viewing all 110119 articles
Browse latest View live




Latest Images