Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

Halotel yashusha Neema kwa wateja wake

0
0
Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Halotel, imezindua kampeni mpya ya Switch to Halotel, yenye lengo la kuwahamasisha Watanzania kujiunga na Mtandao huo sambamba na kuzindua utaratibu wa wafanyakazi wa kampuni hiyo kuwatembelea wateja wa Mtandao huo katika maeneo yote nchi nzima mjini na vijijini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo iliyofanyika katika soko la Makumbusho lililoko Kinondoni Dar es Salaam, Naibu Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Mr Nguyen Van Son, amesema tangu kuzinduliwa kwa huduma za kampuni hiyo, wamepata mapokezi mazuri kutoka kwa watanzania ambao hadi sasa zaidi ya wateja milioni tatu na laki tano, tayari wamejiunga na mtandao huo na wanafurahia huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo ya simu.

“Tunafarijika sana kwa namna ambavyo Watanzania wameendelea kutuunga mkono katika jitihada zetu za kuboresha huduma za mawasiliano kwa jamii hii, ni faraja kubwa kwetu kwamba katika kipindi hiki kifupi tumepata mafanikio makubwa na bado tunaendelea kupata wateja wanaojiunga na mtandao wetu siku hadi siku,” Jambo hili linatufanya tusilale tufikilie ni namna gani tunapaswa kuendelea kukizi mahitaji yao.

“Kuzinduliwa kwa kampeni hii itakuwa ni sehemu ya sisi kusogea karibu na wateja wetu, kuwahudumia pamoja na kuwasikiliza ni nini wanahitaji kutoka kwetu,” Tunaamini kabisa kwamba kuwa karibu na wateja wetu tutajenga mtandao bora kabisa utakao kuwa na huduma zinazolenga maisha halisi ya Watanzania.
Naibu Mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Van Son akiweka Laini ya simu ya Halotel kwa mteja mpya wa Mtandao huo, Simon Mkumbo, ambae amejiunga na Mtandao huo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya “Switch to Halotel” yenye lengo la kuwahamasisha Watanzania kujiunga na Mtandao huo, Kampeni hiyo pia itahusisha wafanyakazi wa Mtandao huo kutembelea maeneo mbalimbali na kutoa huduma kwa wateja katika maeneo yao.
Meneja Mawasiliano wa Halotel, Hindu Kanyamala, kwa pamoja na Naibu Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Nguyen Van Son, wakitoa maelezo juu ya huduma za mtandao huo kwa wafanya biashara wa Matunda wa soko la Makumbuso, Wakati wa uzinduzi wa huduma ya” Switch to Halotel” yenye lengo la kuhamasisha Watanzania kujiunga na Mtandao huo, Pamoja na wafanya kazi wa Mtandao huo kutembelea maeneo mbalimbali kutoa huduma kwa wateja. Pamoja nao katika picha ni Mkurugenzi wa Tawi la Dar es Salaam Vu Huy Thiem.
Meneja Mawasiliano wa Halotel, Hindu Kanyamala, kwa pamoja na Naibu Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Nguyen Van Son, wakitoa maelezo juu ya huduma za mtandao huo kwa wafanya biashara wa Matunda wa soko la Makumbuso, Wakati wa uzinduzi wa huduma ya” Switch to Halotel” yenye lengo la kuhamasisha Watanzania kujiunga na Mtandao huo, Pamoja na wafanya kazi wa Mtandao huo kutembelea maeneo mbalimbali kutoa huduma kwa wateja. Pamoja nao katika picha ni Mkurugenzi wa Tawi la Dar es Salaam Vu Huy Thiem.

 

MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMAKUFANYIKA JUNE 14- 23, 2017

0
0

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe.Angellah Kairuki akizungumza na Waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yatakayofanyika kuanzia tarehe 14-23 Juni ,2017 yenye kauli mbiu “Kuimarisha Ushirikishwaji wa Jamii katika Utoaji Huduma,Vijana washirikishwe kuleta mabadiliko Barani Afrika”.Kulia kwake ni Naibu katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi,Susan Mlawi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe.Angellah Kairuki akiwa katika mkutano na waandishi wa Habari leo Mjini Dodoma.
Picha na Daudi Manongi, MAELEZO, DODOMA.

FAINALI ZA MABINGWA WA KUDUNDA KIKAPU 2017 ZAENDELEA KURINDIMA MWANZA.

0
0
Kufuatia michuano ya mpira wa kikapu iliyozinduliwa na makamu wa raisi Mhe. Samia Suluhu Hassan wiki zilizopita, ameonyesha kuunga mkono zoezi hilo la kuwasaka wawakilishi lililofanyika katika mikoa mbalimbali. Sprite inaendelea kuibua hisia zaidi ikizileta pamoja zile timu zilizofuzu katika ngazi ya kimkoa kwenye fainali. 

Michuano ya kinyang'anyiro hiko yalishaanza toka 12 na tayari baadhi ya timu zilishaanza kuchuana huku kila timu ikiwa na matumaini makubwa ya kuibuka bingwa wa kudunda kikapu kitaifa mwaka 2017.
Finali hizi zitaendelea kupigwa mkoani Mwanza ndani ya viwanja vya chuo cha Butimba hadi tarehe 14 huku timu zikicheza mfululizo kwa mtoano ambapo bingwa atapatikana. Maandalizi yakiwa yamepamba moto, timu nazo zinaendelea kujinoa huku wachezaji wakijigamba kuwa mafahali katika finali hizo. 

Mshikemshike huu umewazoa mashabiki mbalimbali wa mpira wa kikapu kutoka Mwanza na wengine kutoka mikoa ya jirani kuja kushuhudia. Finali hizi pia zinasindikizwa na burudani za kukata na shoka kutoka kwa wasanii mbalimbali wa muziki ambapo msanii Dogo Janja alitokelezea kuchangamsha mshabiki na pafomansi la kibabe.

Washiriki wengine wakiwemo wadau wakubwa wa mpira wa kikapu nchini, pia wamejitokeza kushuhudia nani ataibuka kinara.
Lengo kubwa hasa la mashindano haya ni kuibua vipaji vya vijana katika michezo hususani mpira wa kikapu hapa nchini kuanzaia ngazi za chini hadi kitaifa. Na itakuwa ni fursa nzuri kwa vijana kujumuika pamoja na kuleta hamasa kwa vijana wengine kushiriki katika mchezo huu na hatimaye kuibua wachezaji mabingwa kitaifa hata kimataifa.

Amani: Milioni 20 za bahati nasibu ya Biko zitanikomboa

0
0
MSHINDI wa Milioni 20 wa bahati nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’ wa droo ya 13, Amani Kabuku, jana amekabidhiwa fedha zake huku akisema kuwa zawadi hiyo ya donge nono itamkomboa kiuchumi, licha ya umri mdogo aliokuwa nao, akiwa na miaka 23 tu.

Makabidhiano hayo ya Biko na Kabuku ambaye pia anatokea katika familia ya mwanahabari nguri nchini Tanzania, Generali Ulimwengu, yalifanyika katika benki ya NMB jijini Dar es Salaam, sambamba na kumpatia elimu ya kifedha saa chache kabla ya kufungua akaunti kwa ajili ya kuingiza fedha zake alizoshinda katika droo hiyo ya aina yake.

Alisema amecheza mara nne tu kabla ya kutangazwa mshindi katika droo ya 13 iliyofanyika Jumapili iliyopita, ambapo hata hivyo hakuamini haraka hadi alipowaona baadhi ya wafanyakazi wa Biko walipomfuata nyumbani kwao kwa ajili ya kumhakikishia juu ya ushindi huo.

“Ni furaha kubwa niliyokuwa nayo kwa sababu naamini huu ni wakati wa kuaga umasikini maana wengi wanatafuta nafasi kama hii ambayo leo Mungu ameniletea mimi ili niweze kutimiza ndoto zangu katika umri niliokuwa nao, hivyo nawashukuru Biko, huku nikiwataka Watanzania wacheze kwa wingi ili nao washinde kama ilivyokuwa mimi,”

Mshindi wa Sh Milioni 20 wa Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku', Amani Kabuku, akiwa katika furaha baada ya kukabidhiwa fedha zake katika benki ya NMB, jijini Dar es Salaam jana.  


Mshindi wa Sh Milioni 20 wa droo ya 13 ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku', Amani Kabuku, katikati akiwa amepakatia fedha zake baada ya kukabidhiwa jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven na kushoto ni afisa wa NMB aliyekamilisha mchakato wa kufungua akaunti ya mshindi huyo na kuingiza pesa zake. 

Akizungumza kwa furaha kubwa, mshindi huyo alisema ndio kwanza amemaliza kidato cha sita na kuibukia kwenye fedha hizo za Biko, hivyo anaamini zitamkomboa kiuchumi kwa ajili ya kuhakikisha kwamba maisha yake yanakuwa mazuri.

TAASISI ZA KIBENKI ZATAKIWA KUBORESHA MIFUMO YAO YA KIUTENDAJI

0
0
TAASISI za kifedha nchini, zimetakiwa kuboresha mifumo ya utendaji kazi, ili kwenda sambamba na mabadiliko ya ukuaji wa uchumi.

Kauli hiyo, imetolewa leo na Msajili wa Hazina Dkt .Osward Mashindano, wakati akizindua Ofisi kuu ya Benki ya TPB iliyoko katika eneo la Mwanjelwa Jijini Mbeya.Amesema, wakati uchumi wa dunia unakua ni vema taasisi hizo zikajiimarisha kiutendaji ili kukidhi vigezo vya ushindani wa kibiashara ndani na nje ya nchi.

“Serikali imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha sekta za kifedha nchini zinatoa msukumo unaotakiwa kwenye shughuli za kiuchumi, hivyo ni wakati wenu nanyi kubadili mifumo ya utendaji kazi ili kwenda sambamba na ukuaji huo wa uchumi“,alisema.

Aidha ametoa wito kwa taasisi za kifedha nchini kuhakikisha inaweka mazingira rafiki kwa wananchi wa kipato cha chini kwa kuweka gharama nafuu za huduma zao ili waweze kuzimudu.Pia, Mashindano ameipongeza benki ya TPB kutokana na na jitihada zake za kupeleka huduma karibu na wananchi kwa kutumia teknolojia ya kisasa na mawakala.

Hata hivyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, alisema benki hiyo imetoa gawio kwa serikali kiasi cha shilingi Bilioni 1.2 ambapo hundi hiyo inatarajiwa kukabidhiwa mjini Dodoma.
Msajili wa Hazina Nchini Dkt ,Osward Mashindano (kushoto)akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Jengo la Ofisi mpya ya Benki ya TPB,kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu TPB,Sabasaba Moshingi ,ambapo ofisi hiyo mpya ipo katika eneo la Mwanjelwa Jijini Mbeya. 
Msajili wa Hazina Nchini Dkt ,Osward Mashindano akizindua jiwe la msingi katika benki ya TPB iliyopo eneo la Mwanjelwa. 
Msajili wa Hazina Nchini Dkt ,Osward Mashindanoakizungumza katika hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la ofisi ya benki ya TPB Mwanjelwa. 
Afisa Mtendaji Mkuu TPB SabaSaba Moshingi ,kushoto akimkabidhi ripoti ya Mwaka Msajili wa Hazina Dkt Osward Mashindano katika hafla ya uzinduzi wa ofisi mpya ya jengo la Tpb Mwanjelwa jijini Mbeya. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Hatua kali Kuchukuliwa kwa Madereva Wazembe: Kamanda Muslimu

0
0
  
 Na Eliphace Marwa – Maelezo.

 Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu Jijini Dar es Salaam limetahadharisha, madereva kuwa makini wakati wakiendesha vyombo vya moto ili kuepuka ajali zinazosababishwa na ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani.

Hayo yamesemwa na Kaimu Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani SACP Fortunatus  Muslimu wakati akitoa taarifa ya hali ya usalama barabarani katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari mpaka Mei mwaka huu ukilinganisha na kipindi kama hicho kwa mwaka jana.

Akisoma taarifa hiyo kwa waandishi wa habari Kamanda Muslimu amesema kuwa ajali za barabarani zimepungua ukilinganisha na mwaka jana kwani katika kipindi cha mwezi Januari mpaka Mei jumla ya ajali za magari zilikuwa 4,177, vifo 1,286 na majeruhi 3,882 ukilinganisha na ajali 2,411, vifo 1,034 na majeruhi 2,291 katika kipindi kama hicho mwaka huu.

Aidha kwa upande wa ajali za pikipiki Kamanda Muslimu amesema kuwa katika kipindi cha Januari mpaka Mei mwaka jana jumla ya ajali za pikipiki zilikuwa 1,110, vifo 347 na majeruhi 950 ukilinganisha na ajali 607, vifo 302 na majeruhi 455 katika kipindi kama hicho mwaka huu.

Pamoja na kupungua kwa ajali nchini Kamanda Muslimu amesema kuwa ajali nyingi zimekuwa zikisababishwa na makosa ya kibinadamu ikiwa ni pamoja mwendokasi wa madereva, kupita magari bila ya tahadhari, ulevi pamoja na kubeba abiria kupita kiasi kwa njia zilizo hatarishi.

Kamanda Muslimu aliongeza kuwa kwa sasa ukamataji wa makosa ya barabarani yatakuwa kipaumbele, hivyo dereva atakeyekiuka sheria atachukuliwa hatua palepale ili kujenga utii wa sheria bila ya shuruti.

“Ukamataji wa makosa utakuwa ni moja ya kipimo cha utendaji wa askari barabarani  ili waweze kukamata makosa mengi mpaka pale madereva watakapoacha kukiuka sheria”, alisema Kamanda Muslimu.

Aidha Kamanda Muslimu amesema kuwa jeshi hilo halitomuonea mtu wala kumbambikia mtu makosa kwani ukamataji huo wa makosa ya barabarani unalenga kuzuia ajali na sio kukusanya mapato na hivyo kuwataka askari kuacha kufanya kazi kwa mazoea bali wafanye kazi kwa nidhamu na maadili ya jeshi hilo.

Kamanda Muslimu amewataka watumiaji wa barabara kutii sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zisizokuwa za lazima ambazo husababisha vifo na majeruhi na kupelekea kuathiri uchumi wa jamii na nchi kwa ujumla kutokana na kupoteza nguvu kazi ya Taifa.

 Kaimu Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani SACP Fortunatus  Muslimu 

WANDISHI WAPEWA ELEMU JUU YA MATONE YA VITAMIN A

0
0
Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar.

Mkuu wa Kitengo cha Lishe kutoka Wizara ya Afya Bi. Asha Hassan amesema Zanzibar bado ipo nyuma katika kiwango cha Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) cha kuwapatia matone ya Vitamn A watoto wenye umri kuanzia miaka miwili hadi miaka mitano.

Bi. Asha alieleza hayo katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu zoezi la kuwapatia matone ya Vitamen A watoto wenye umri huo lililoanza tarehe 1 Juni ambalo linategemea kumalizika mwishoni mwa mwezi huu kwa awamu ya kwanza mwaka huu na awamu ya pili itafanyika mwezi Disemba.

Alisema Zanzibar hadi hivi sasa imefikia asilimia 82 katika  mpango huo wakati kiwango kilichowekwa na Shirika la Afya  Ulimwenguni ni asilimia 95.Alizitaja Wilaya tatu za Mkoa Mjini Magharibi ndizo zenye asilimia ndogo zaidi chini ya asilimia 70 wakati Wilaya ya Kati inaongoza kwa kuwa na zaidi ya asilimia 95.

Alisema Kitengo kimeanzisha utaratibu wa kuwafuata wazazi wanaoishi mbali na vituo vya afya ili kuwapatia watoto  matone ya Vitamin A lakini baadhi ya wazazi wamekuwa hawatoi mashirikiano.

Aliwasisitiza wazazi kufanya juhudi kuhakikisha watoto wao wanapata matone hayo kwa vile ni muhimu katika kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya maambukizo ya maradhi ikiwemo kuharisha na kutoona vizuri.Afisa Kitengo cha Lishe Wilaya ya Mjini Fatma Ali Saidi alisema kumekuwa na dhana potofu  kwa wananchi hasa wanaoishi mjini kwamba watoto wao hawahitaji matone ya Vitamin A kwa vile wanakula vizuri lakini dhana hiyo sio sahihi.

Alisema utafiti uliofanywa na Kitengo hicho unaonyesha kwamba watoto  wenye hali nzuri ya Vitamin A  Zanzibar ni asilimia 12 na asilimia 88 iliyobaki wanaupungufu.Aliwatoa wasi wasi wazazi kuwa hata wale wachache wenye Vitamin A vya kutosha mwilini wanapopewa matone hayo hayana madhara yoyote na wanaweza kutumia. 

Washiriki wa mkutano huo walikishauri Kitengo cha Lishe kuongeza kutoa elimu kwa wazazi kwani baadhi yao bado hawajaelewa umuhimu wa matone ya Vitamin A na wengine wanadhani kuwa matone hayo ni sawa na chanjo jambo ambalo sio sahihi.                            
 Mkuu wa Kitengo cha Lishe kutoka Wizara ya Afya Asha Hassan akizungumza na waandishi wa habari kuhusu zoezi la kuwapatia matone ya Vitamin A watoto wenye umri wa miaka miwili hadi mitano katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Malaria Mwanakwerekwe.
 Washiriki wa mkutano huo wakiwa katika kazi za vikundi kupanga mikakati ya kuihamasisha jamii kuitikia kampeni ya kuwapatia watoto matone ya Vitamin A katika ukumbi wa Malaria Mwanakwerekwe.
 Mwandishi wa habari wa Gazeti la Zanzibar Leo Nasra Manzi akiwasilisha kazi ya kukundi chake katika mkutano wa kuwaelimisha waandishi kuhusu matone ya Vitamin A katika ukumbi wa Malaria Mwanakwerekwe.
Picha na Makame Mshenga.

KAMISHNA MSAIDIZI WA ARDHI KANDA YA KATI AELEZA KUHUSU ULIPAJI WA KODI YA PANGO LA ARDHI


MANISPAA YA UBUNGO KUBORESHA SOKO LA SHEKILANGO

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

MSTAHIKI  Meya wa Manispaa ya Ubongo, Boniface Jacob  amefanya kikao na wafanyabiashara wa Soko la Shekilango ili kuweka makubaliano ya maboresho ya soko hilo. 

Maboresho hayo ambayo yamelenga kuliweka soko la Shekilango na masoko mengine ya Manispaa ya Ubongo katika hadhi nzuri na kuongeza mapato kwa serikali.   

Akizungumza na wafanyabiashara katika soko hilo, Jacob amesema, maboresho ya soko hilo yametengewa Tsh milioni 50 ambazo ni mapato ya ndani ambayo  yaliyotokana na kodi zao. Amesema maboresho hayo yataanza baada ya siku 7, yatachukua siku 14 kukamilika na wafanyabiashara waliopisha marekebisho hayo kurudi sehemu zao za biashara.

Jacob amesema mara baada ya wafanyabiashara kurejea katika maeneo yao, makubaliano ya ushuru yatakuwa  baina ya Manispaa ya Ubungo na mfanyabiashara na siyo tena mfanyabiasha na mfanyabiashara.
"Nimekuja kuwasikiliza wafanyabiashara wote  sitaki kuwaletea njaa,nataka tuangalie hali ya sasa na mzunguko wa ela tangu 2000 na tukubaliane".

 Jacob amesema mara baada ya maboresho ya mabanda ya mbogamboga ambayo ushuru wake utapanda kidogo, awamu itayofuata itawagusa wapanga na wamiliki wa fremu 12 na vyoo ambao kwasasa wanalipa sh 200 kwa siku.

 Aidha Jacob aliwataka wamiliki wa fremu hizo kwenda kwa Mkurugenzi wa Manispaa kufanya mazungumzo naye ili kupata makubaliano ya pamoja ya kisheria ili fremu hizo ziwe mali ya serikali na wao kulipia ushuru unaoendana na mahitaji ya sasa kiuchumi.
 Mstahiki Meya wa Ubungo, Boniface  Jacob akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Shekilango juu ya maboresho ya soko hilo leo jijini Dar es Salaam.
 Mstahiki Meya wa Ubungo, Boniface  Jacob akimununuza wafanyabiashara katika Soko la Shekilango alipotembelea soko hilo.
Mstahiki Meya wa Ubungo, Boniface  Jacob akitembelea Soko la Shekilango  juu ya kulifanyia maboresho leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

SPIKA NDUGAI APATA UGENI KUTOKA TAASISI YA UTSS (UNDER THE SAME SUN) LEO OFISINI KWAKE MJINI DODOMA

0
0
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu na Mwanzilishi wa Taasisi ya UTSS (Under the Same Sun) Ndg. Peter Ash (kushoto) pale ugeni kutoka Taasisi ya UTSS (Under the Same Sun) ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu na Mwanzilishi wa Taasisi ya UTSS (Under the Same Sun) Ndg. Peter Ash (kushoto) alipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu na Mwanzilishi wa Taasisi ya UTSS (Under the Same Sun) Ndg. Peter Ash (katikati) pale ugeni kutoka Taasisi ya UTSS (Under the Same Sun) ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya UTSS (Under the Same Sun) Ndg. Vicky Ntetema 
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati)akiwa katika picha ya pamoja na ugeni kutoka Taasisi ya UTSS (Under the same Sun) ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu na Mwanzilishi wa Taasisi hiyo Ndg. Peter Ash (wa tatu kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Vicky Ntetema (wa tatu kulia) baada ya kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

UMOJA WA WAZAZI CCM Z’BAR WAWAASA VIONGOZI KUONGEZA KASI YA UTEKELEZAJI WA AHADI ZAO WALIZOTOA

0
0

NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

MAKATIBU wa Wilaya za Umoja wa Wazazi CCM Zanzibar wamewashauri viongozi mbali mbali wa Chama cha Mapinduzi kuongeza kasi ya utekelezaji wa ahadi walizotoa ndani ya taasisi hiyo ili kupunguza changamoto za kiutendaji.

Rai hiyo imetolewa na baadhi ya Makatibu wa Wilaya Sita za Umoja huo Zanzibar mara baada ya kukabidhiwa Komputa zilizotolelewa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja huo, Bi. Najma Giga ikiwa ni miongoni mwa utekelezaji wa ahadi alizowahi kutoa wakati wa ziara zake Visiwani humo.

Katibu wa Wazazi Wilaya ya Amani , Bi.Mwanaisha Ame Mohamed amesema upatikanaji wa vifaa hivyo utaongeza ufanisi wa kiutendaji ndani ya umoja huo kwani watakuwa na vitendendea kazi vya kisasa vitakavyorahisisha utendaji wa kazi zao.

Aidha Katibu huyo amewataka baadhi ya Wabunge, Wawakilishi na Madiwani ambao bado hawajahamasika kuanza kutekeleza ahadi zao kwa umoja huo na chama kwa ujumla kufuata nyayo za viongozi wenzao walioanza kutatua kero za taasisi hiyo hatua kwa hatua.

“Huu ni wakati wa viongozi mbali mbali wa Chama chetu pamoja na jumuiya zetu kujitokeza kusaidia baadhi ya Mikoa na Wilaya zenye upungufu wa vitendea kazi ili waweze kukamilisha shughuli za uchaguzi kwa ufanisi.”, alisema Katibu Mwanaisha.

Naye Katibu wa Wazazi Wilaya ya Wete Pemba, Bi. Mariam Ali Said amemshukru Naibu Katibu Mkuu wa Wazazi Zanzibar kwa kutekeleza ahadi zake kwa vitendo na kuongeza kuwa vifaa hivyo ni chachu ya kumaliza changamoto za kufuata huduma za uchapaji wa nyaraka za kiofisi masafa ya mbali.

Akizungumza Kaimu Naibu Katibu Mkuu Wazazi Zanzibar, Nd. Mustafa Rashid Kumwalu kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu wa umoja huo Bi. Najma Gina mara baada ya kukabidhi Komputa hizo ametoa wito kwa watendaji wa umoja huo kutumia komputa hizo kwa matumizi yaliyokusudiwa ili shughuli za kiutendaji zifanyike kwa wakati mwafaka.

Nd. Rashid alieleza kuwa lengo la umoja huo ni kuhakikisha watendaji wake wanapata vitendea kazi vya kisasa vitakavyosaidia kutekeleza kwa wakati shughuli za kiutendaji kwa lengo la kwenda sambamba na matakwa ya Katiba ya CCM iliyofanyiwa mabadiliko miezi kadhaa iliyopita.

Aidha alisema Komputa zilizokabidhiwa mpaka sasa ni tisa bado kumi kwa mujibu wa idadi ya komputa zilizoahidiwa kutolewa na Naibu katibu Mkuu wa Umoja huo, ambaye pia ni Mbunge wa kuteuliwa kutoka ndani ya Umoja wa Wazazi Tanzania.

Komputa hizo zina thamani zaidi ya shilingi milioni Saba zimekabidhiwa kwa Wilaya 6 za Umoja wa Wazazi CCM Wilaya ya Amani, Wilaya ya Mfenesini, Wilaya ya Kati, Wilaya ya Kaskazini “B”, Wilaya ya Wete na Wilaya ya Chake Chake Pemba.
Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Zanzibar , Mustafa Rashid Kumwalu akimkabidhi Katibu wa Wazazi Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja , Bi. Salma Shaibu, kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja huo Bi.Najma Giga.
Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Zanzibar Nd. Mustafa Rashid Kumwala akitoa nasaha kwa Makatibu wa Wilaya Sita za Umoja huo kabla ya kuwakabidhi komputa hizo.
Baadhi ya Komputa zilizotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Zanzibar, Bi.Najma Giga kwa Wilaya Sita za umoja huo Zanzibar.

Kampuni ya Wazawa, yakamilisha hatua za Msingi kuuza hisa zake kwa watanzania - Maxmalipo

0
0
Mjumbe wa Bodi ya kampuni ya Maxcom Africa Dr,Donalth Ulomi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza hati iliyopewa kampuni hiyo na Soko la hisa la Dar es salaam (Dar Es Salaam stock Exchange ) na kuanzia sasa itauza hisa zake kwa umma na kubadili jina lake kuwa Maxcom Africa PLC Maxmalipo ni Moja ya Kampuni zilizoanzishwa na kuendeshwa na wazawa watanzania ambayo imeifikia hatua za Mwisho katika kuuza hisa zake kwenye soko la hisa. 

Leo hii wametambulisha hati yao inayowafanya kuwa tayari kwa kuuza hisa kwa watanzania . Kampuni hii ilianzishwa mwaka 2008 na mpaka leo imefika nchi zaidi ya 5 barani Africa.Hafla hiyo ya uzinduzi wa uuzaji wa hisa ulifanyika mapema leo katika makao makuu ya Maxcom Africa Kijitonyama Jijini Dar Es Salaam. 
Mjumbe wa Bodi ya kampuni ya Maxcom Africa Dr,Donalth Ulomi (kulia ) akikata utepe wa kuzindua rasmi uuzaji wa hisa za Maxcom Africa PLC anayeshuhudia ni Mkurungezi wa Uendeshaji wa Maxcom Africa Bw.Ahmed Lusasi mapema leo katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika makao makuu ya Maxcom Africa Kijitonyama Jijini Dar Es Salaam. 
Mjumbe wa Bodi ya kampuni ya Maxcom Africa Dr,Donalth Ulomi (kulia ) akionesha nembo ya jina jipya Maxcom Africa PLC kuzindua rasmi uuzaji wa hisa za kampuni hiyo kushoto kwake ni Mkurungezi wa Uendeshaji wa Maxcom Africa Bw.Ahmed Lusasi mapema leo katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika makao makuu ya Maxcom Africa Kijitonyama Jijini Dar Es Salaam 
waandishi wa habari wakichukua matukio wakati wa hafla ya uzinduzi wa uuzaji wa hisa za Maxcom Africa mapema leo.
Mjumbe wa Bodi ya kampuni ya Maxcom Africa Dr,Donalth Ulomi akifanya mahojiano na mwandishi wa habari mara baada ya uzinduzi rasmi wa uuzaji wa hisa za Maxcom Africa PLC.Maxmalipo ni Moja ya Kampuni zilizoanzishwa na kuendeshwa na wazawa watanzania ambayo imeifikia hatua za Mwisho katika kuuza hisa zake kwenye soko la hisa. Leo hii wametambulisha hati yao inayowafanya kuwa tayari kwa kuuza hisa kwa watanzania . Kampuni hii ilianzishwa mwaka 2008 na mpaka leo imefika nchi zaidi ya 5 barani Africa mapema leo katika hafla ya uzinduzi ilizofanyika makao makuu ya Maxcom Africa Kijitonyama Jijini Dar Es Salaam. 

Ngoma azipendazo ankal

0
0

Maseke Ya Meme (Bavon Marie-Marie) - Franco & L'O.K. Jazz 1971

TAMBUA JINSI YA KUJIUNGA NA KUWA MWANACHAMA WA COPYRIGHT SOCIETY TANZANIA (COSOTA)

TASAF YAIBUKA KIDEDEA KATIKA SHUGHULI ZA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI.

0
0

Na Estom Sanga-TASAF

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF- umeibuka mshindi wa kwanza kati ya Mifuko 19 inayojihusisha na shughuli za kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa mwaka 2017 nchini.

Ushindi huo umetangazwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi –NEEC- baada ya tathimini ya kutambua mchango wa Mifuko hiyo iliyoanzishwa na serikali kwa lengo la kupunguza changamoto ya upatikanaji wa mitaji kwa wananchi hususani wale wa kipato cha chini ili waweze kuboresha maisha yao.

Taarifa iliyotolewa na NEEC imeonyesha kuwa TASAF imepata alama 81 ikifuatiwa na Mfuko wa SELF Microfinance uliopata alama 71 huku Mfuko wa Kuwaendeleza Wajasiliamali Wananchi NEDF ukipata alama 70 na kushika alama ya tatu.

Miongoni mwa vigezo vilivyoupa ushindi Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF ni pamoja na Idadi kubwa ya wanufaika wa huduma zake kutoka Kaya zipatazo MILIONI MOJA NA LAKI MOJA ,uwezo wake wa kuwafikia walengwa nchini kote,thamani ya fedha zilizowanufaisha walengwa na uwasilishaji wa taarifa za utekelezaji wa shughuli zake kwa wakati.

Akizungumza na Wafanyakazi kufuatia ushindi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga amewahimiza waendelee kujituma zaidi katika utendaji kazi,ili mchango wao katika vita dhidi ya umasikini uwe endelevu na wenye kutoa tija kwa taifa.

Bwana Mwamanga amesema ni vema wakati wote wa utekelezaji wa shughuli , watumishi wa TASAF waendelee kuzingatia maadili bora ya utumishi wa umma, na kuwapa huduma stahiki wananchi na kutekelezaji maagizo ya serikali ya uboreshaji wa huduma kwa wananchi ili kuwapunguzia kero ya umasikini.

  Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge ,Kazi, Vijana na Walemavu Mhe. Jennista Mhagama akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bwana Ladislaus Mwamanga Cheti cha Ushindi wa Kwanza katika ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi nchini.


 Baadhi ya wafanyakazi wa TASAF wakifurahia ushindi wa kwanza ambao Mfuko huo umepata kwa mwaka 2017 kati ya mifuko 19 inayoshughulikia uwezeshaji wananchi kiuchumi.



KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

NEWS ALERT: JENGO LA GHOROFA 27 LASHIKA MOTO JIJINI LONDON, JUHUDI ZA KUUZIMA ZINAENEDELEA MUDA HUU

0
0
Zaidi ya askari 200 wa jeshi la zimamoto asubuhi hii wako katika vita ya kuzima moto mkubwa uliorindima usiku kucha katika jengo la ghorofa 27 Magharibi ya jiji la London, Uingereza, huku mashuhuda wakidai kwamba kuna watu wamenasa kwenye jengo hilo liendalo kwa jina la Grenfell Tower.
Watu wa huduma ya kwanza wanasema watu 30 wamekimbizwa hospitali kupata matibabu, na habari zainadai kwamba huenda jengo hilo likaporomoka wakati wowote.

BALOZI PINDI CHANA AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO

0
0
Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Dkt. Pindi Hazara Chana akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta kabla ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwenye Ikulu ya Eldoret Juni 13,2017. 
Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Dkt. Pindi Hazara Chana wa pili kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Kenya (katikati) mara baada ya zoezi la kuwasilisha Hati za Utambulisho kukamilika. 

Introducing "RUBA" by Mkubwa na Wanawe featuring Dulla Makabila

MD KAYOMBO: MIL 85,000,000 ZAPATIKANA ZITAJENGA MADARASA MATANO SHULE YA MSINGI HONDOGO

0
0
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo Leo June 14, 2017 Ameeleza dhamira yake kuhusu ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa katika shule ya Msingi Hondogo iliyopo katika Kata ya Kibamba.
MD Kayombo ametoa ufafanuzi huo ofisini kwake alipokuwa akitoa tathmini ya ziara yake aliyoifanya katika Shule ya Msingi Hondogo Jana tarehe 13 June 2017.

Katika ziara hiyo ambayo Mkurugenzi aliambatana na Mchumi Mkuu wa Manispaa, na Ofisa Elimu Msingi walikagua maeneo yote ya shule hiyo ikiwemo majengo na kubaini kuwa Kuna baadhi ya majengo ambayo yapo katika hali ya uchakavu hivyo kuamua kujenga madarasa mapya matano ili kuwaimarishia wanafunzi kuwa na mazingira rafiki ya kusomea.

Mkurugenzi Kayombo alisema kuwa ujenzi huo utakaoanza hivi karibuni wa vyumba vitano vya madarasa unaakisi pia ujenzi wa vyumba vya madarasa nane na matundu ya vyoo katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza, vivyo hivyo katika Shule ya Msingi Kawawa na Shule ya Sekondari Mburahati ambapo kote huko ameelekeza kuanza haraka ujenzi wa Madarasa sambamba na Vyoo kwa ajili ya wanafunzi na walimu.

Mkurugenzi Kayombo ameishukuru Bank ya CRDB kwa kuchangia shilingi Milioni 68,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa hayo ambapo ameeleza kuwa Ofisi yake imetoa jumla ya shilingi milioni 17,000,000.

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images