Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110109 articles
Browse latest View live

WATUMISHI 10,931 WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA WAPEWA MAFUNZO YA UHASIBU

$
0
0
Na Mathew Kwembe, Lindi 

Jumla ya watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa 10,931 kutoka Halmashauri 93 za Mikoa 13 inayotekeleza Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) wamepewa mafunzo ya uhasibu na utoaji wa taarifa za fedha katika awamu ya kwanza na ya pili ya mafunzo hayo yaliyofanyika katika mikoa hiyo.

Mkuu wa Mifumo ya Mawasiliano PS3 bwana Desderi Wengaa ameyasema hayo jana mjini Lindi kabla ya kumalizika kwa awamu ya pili ya mafunzo hayo ambayo yaliwahusisha waratibu wa elimu kata na waganga wafawidhi wa vituo vya afya kutoka mikoa 13 iliyo chini ya Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3).

Bwana Wengaa amefafanua kuwa katika awamu ya kwanza ya mafunzo ambayo yalitolewa kwa wakufunzi waliowafundisha watumishi kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa, jumla ya wakufunzi 2883 walipewa mafunzo hayo kwenye mikoa hiyo.

Akizungumza kabla ya kuhitimishwa kwa awamu ya pili ya mafunzo hayo yanayoendelea katika mkoa wa Lindi bwana Wengaa amesema kuwa katika awamu ya pili ya mafunzo jumla ya watumishi Mamlaka za Serikali za Mitaa 10,048 kutoka Mikoa 13 inayotekeleza Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) walifaidika na mafunzo ya uhasibu na utoaji wa taarifa za fedha.
  Mkuu wa Mifumo ya Mawasiliano PS3 bwana Desderi Wengaa akizungumza  mafanikio yaliyopatikana kwa watumishi 10931 wa Halmashauri 93 ambazo zinatekeleza Mradi wa PS3 nchini 
Baadhi ya waratibu elimu kata na waganga wafawidhi wa vituo vya afya kutoka Manispaa ya Lindi na halmashauri ya wilaya ya Lindi wakimsikiliza Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi bwana Jomaary Satura wakati alipoyafungua mafunzo hayo katika mkoa wa Lindi. 
Baadhi ya waratibu elimu kata na waganga wafawidhi wa vituo vya afya kutoka Manispaa ya Lindi na halmashauri ya wilaya ya Lindi wakimsikiliza Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi bwana Jomaary Satura wakati alipoyafungua mafunzo hayo katika mkoa wa Lindi 
Baadhi ya watoa mada ambao ni wahasibu kutoka Manispaa ya Lindi na halmashauri ya wilaya ya Lindi wakimsikiliza Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi bwana Jomaary Satura wakati alipoyafungua mafunzo hayo katika mkoa wa Lindi. 


Wilaya za Mufindi na Kilolo Mkoani Iringa zatumia Tehama kuboresha utoaji wa Huduma kwa umma

$
0
0
Je unajua jinsi TEHAMA inavyoboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa umma katika Mkoa wa Iringa hasa Wilaya ya Kilolo na Mufindi. Usikose kuangalia kipindi hiki.

JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAWAANDALIA HAFLA FUPI WAFANYAKAZI WAPYA JIJINI ARUSHA

$
0
0

Mkurugenzi mpya wa Miundombinu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Dkt Kamugisha Kazaura akitoa neno la shukrani kwenye hafla hiyo ya kuwakaribisha wafanyakazi wapya makao makuu ya jumuiya hiyo jijini Arusha.

Baadhi ya wafanyakazi wapya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) wakiwa na furaha  katika hafla ya kuwakaribisha iliofanyika makao makuu jijini Arusha.

Wafanyakazi wapya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) wakijitambulisha  katika hafla ya kuwakaribisha iliofanyika makao makuu jijini Arusha.

Mratibu wa Habari katika Sekretariat ya EAC,Florian Mutabazi(kushoto),Afisa Habari Mwandamizi wa bunge la Eala,Bob Odiko na wadau wengie wakiwa katika hafla ya kuwakaribisha wafanyakazi wapya wa jumuiya hiyo.


MAGAZETI YA LEO JUMANNE JUNE 13,2017

Article 0

Kesi ya dawa za kulevya inayomkabili Masogange, kuanza kuunguruma mwezi ujao.

$
0
0
Na Karama Kenyunko,blogu ya jamii.

Julai 13, mwaka huu Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu imepanga kuanza kusikiliza kesi ya dawa za kulevya inayomkabili video Queen Agnes Gerald (28) maarufu kama Masogange.

hatua hiyo imekija baada upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi na leo kumsomea mshtakwa maelezo ya awali (PH).

Katika Ph Hiyo Masogange amekiri kupelekwa kwa Mkemia Mkuu kuchukuliwa sampuli ya mkojo wake ili kuthibitisha kama anatumia dawa za kulevya.

Masogange amekubali hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri wakati Wakili wa Serikali, Costantine Kakula alipokuwa akimsomea maelezo ya awali ya mashitaka yake.

Pia Masogange amekiri kuwa Februari 14, mwaka huu alikamatwa nyumbani kwake Makongo juu Kinondoni Dar es Salaam na kupelekwa Kituo cha Polisi Central

Ikadaiwa kuwa, Februari 15, mwaka huu Masogange alipelekwa kwa mkemia kuchukuliwa sampuli zake.Aidha, alikiri kuwa na hati ya kusafiria yenye namba AB 783597.

Hata hivyo, Mshitakiwa huyo amekana kuwa Februari 20, mwaka huu Mkemia Mkuu alitoa taarifa iliyothibitisha kwamba mkojo wake ulikuwa na dawa aina ya heroin na Oxazepam.

Kufuatia hayo, kesi hiyo itaendelea Julai 13 mwaka huu ambapo upande wa mashtaka utaleta mashahidi wake.

Masogange anakabiliwa na mashitaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya heroin diacety na Oxazepam.

Inadaiwa kuwa, kati ya Februari 7 na 14 mwaka huu, maeneo yasiyofahamika jijini Dar es Salaam Masogange alitumia dawa za kulevya aina ya heroin (diacety/morpline) kinyume na sheria.

Aidha anadaiwa kutumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam. 

Masogange yupo nje kwa dhamana.

MBUNGE PANGANI AWATAKA WANANCHI KUWEKEZA KWENYE KILIMO ILI KUPATA MAFANIKIO

$
0
0
MBUNGE wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso amewataka wananchi kuwekeza kwenye kilimo chenye tija kwa kuongeza uzalishaji ili waweze kupata mafanikio na kijikwamua kichumi. 

Aweso aliyasema hayo wakati akizungumza na Mtandao huu ambapo alisema wilaya ya Pangani imejaliwa kuwepo na ardhi yenye rutuba ambayo inaweza kustawisha mazao ya aina yoyote. Alisema kutoka na fursa hivyo wananchi wanapaswa kuitumia kama mtaji wa kuweza kulima kilimo chenye manufaa ambacho kinaweza kuwa mkombozi wao. 

Aidha pia alisema lazima wabadilike waona namna ya kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo ikiwemo mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kwa kuongeza wigo mpana wa kujikita kwenye kilimo. 

“Mradi mkubwa wa bomba la mafuta hii ni fursa kubwa hivyo lazima wananchi wa Jimbo langu la Pangani waone ni vipi wanaweza kuitumia kwa kuongeza uzalishaji wenye tija na manufaa kwao “Alisema. 

Hata hivyo aliwataka wakazi wa wilaya hiyo kushikamana kwa pamoja ili kuweza kupata maendeleo ikiwemo kuongeza bidii katika kuzalisha mazao mbalimbali yanayolimwa na kustawi vizuri. 

Hata hivyo aliwataka kulinda maeneo yao na kuacha kuyauza jambo ambalo linaweza kuwarudisha nyuma kimaendeleo na kujikita wakishindwa kuendana na ujio wa fursa mbalimbali ikiwemo mradi wa bomba la mafuta. 

“Ndugu zangu wananchi wanaweza kutokea watu wakawarubuni muwauzie maeneo yenu niwaambie tu achane kuuza maeneo yenu ovyo kutokana na ujio wa fursa hiyo muhimu “Alisema.
MBUNGE wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso akizungumza na Wananchi.Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

SIFA ZA MGOMBEA NAFASI YA RAIS WA TFF

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


Kuelekea katika uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF), Kamati ya Uchaguzi ya TFF, imetangaza Uchaguzi Mkuu wa shirikisho hilo utakafanyika Agosti 12, mwaka huu mjini Dodoma.

Zifuatazo ni sifa za wagombea
1. Awe raia wa Tanzania.
2. Awe na kiwango cha elimu kisichopungua kidato cha nne (Cheti cha Elimu ya Sekondari).

3. Awe na uzoefu wa uendeshaji Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano.

4. Asiwe na hatia yoyote ya kosa la jinai na asiwe amewahi kuhukumiwa kifungo kisicho na mbadala wa faini.

5. Awe na umri angalau miaka 25.

6. Awe amewahi kuwa ama Mchezaji Mpira wa Miguu, Kocha, Mwamuzi. Au kushiriki katika uendeshaji wa Mpira wa Miguu angalau katika ngazi ya Mkoa au ngazi ya daraja la kwanza.

7. Awe muadilifu na muaminifu mwenye uwezo wa utendaji katika utekelezaji na utimizaji wa majukumu na malengo ya TFF.

8. anayegombea nafasi ya Rais au makamu wa Rais awe na kiwango cha elimu kisichopungua shahada moja, mwenye utu na uwezo wa kuiwakilisha TFF ndani na nje ya nchi.

Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni tarehe 16-20/06/2017 saa kumi (10:00) jioni.

MBUNGE MLATA AHAMASISHA MICHEZO MASHULENI

$
0
0
MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Singida,Marther Mlata amesema ili kukabiliana na utoro mashuleni pamoja na kusuasua kwa elimu,walimu hawana budi kutafuta namna ya kuwavutia watoto kupenda shule kupitia njia ya michezo.

Mbunge Mlata alitoa ushawishi huo alipokuwa akiongea na wanafunzi,wazazi na walezi wa watoto wa shule ya sekondari ya Mtakatifu Vincent iliyopo katika Mji mdogo wa Mitundu,wilayani Manyoni,Mkoani Singida.

 “Ni lazima walimu mtafute namna ya kuwavutia watoto kupenda shule,kwa mfano michezo mtu mwingine anaweza akaenda shule kwa ajili ya michezo tu anasema shuleni huwa kuna mpira,huwa wanacheza ngoja niende”alifafanua Mlata ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida.

Kwa mujibu wa Mlata mwanafunzi pindi anapokwenda shuleni kwa lengo la kushiriki katika michezo,inakuwa ni rahisi pia kumpata kwenye masomo darasani.

Aidha Mbunge huyo aliweka bayana kwamba ili kuhakikisha michezo mashuleni inawezekana kuwepo kwa kipindi chote,alitumia hafla hiyo kukabidhi mipira kumi na jezi pea kumi kwa ajili ya kugawa katika shule zilizopo katika kata ya Mitundu.

“Mimi sikuwa najua kwamba mmeongoza mmewafunga wanyiramba sisi wakimbu tumewafunga wale wanyiramba goli 3- 0 kwa hiyo nakuja kuhimiza michezo mashuleni”alibainisha Mbunge huyo mpenda michezo.

Hata hivyo aliweka bayana kwamba ndiyo maana utoro mashuleni na kusuasua kwa elimu kunakochangiwa na wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata masomo alilazimika kumuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Itigi kuhakikisha anazisajili shule ambazo bado hazijasajiliwa ili kuwapunguzia watoto adha ya kutembea umbali huo mrefu.

Ni Baadhi ya vifaa vya michezo vilivyotolewa msaada na Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Singida,Marther Mlata kwa ajili ya kuhamasisha michezo katika shule zilizopo katika kata ya Mitundu,tarafa ya Itigi,wilayani Manyoni,Mkoani Singida wakati wa sherehe za Juma laa Taaluma lililoandaliwa na kata hiyo.(Picha Na Jumbe Ismailly)

MKURUGENZI MANISPAA YA UBUNGO KUJENGA MADARASA MATANO MAPYA SHULE YA MSINGI HONDOGO

$
0
0
Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo Leo June 13, 2016 amefanya ziara ya kikazi kwa kutembelea shule ya Msingi Hondogo iliyopo katika Kata ya Kibamba Jijini Dar es salaam kujionea hali ya Miundombinu ikiwemo majengo ya shule na ufanisi wa utoaji elimu katika Shule hiyo.


Mara baada ya kuzuru katika Shule hiyo Mkurugenzi Kayombo amebaini kuwapo na ubovu wa madarasa hivyo kuamua kujenga madarasa mengine mapya matano kwa ajili ya wanafunzi kujisomea kwa uhuru na amani shuleni hapo.



Mkurugenzi Kayombo alisema kuwa ujenzi huo utakaoanza hivi karibuni wa vyumba vitano vya madarasa utaakisi pia ujenzi wa vyumba vya madarasa nane na matundu ya vyoo katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza, vivyo hivyo katika Shule ya Msingi Kawawa na Shule ya Sekondari Mburahati ambapo kote huko ameelekeza kuanza haraka ujenzi wa Madarasa sambamba na Vyoo kwa ajili ya wanafunzi na walimu.



MD Kayombo alisema kuwa mara baada ya kukamilika kwa madarasa hayo yatapunguza kadhia ya mbanano wa wanafunzi darasani ambapo pia amesema ujenzi wa madarasa hayo utakuwa wa kisasa ili kukidhi mahitaji ya ubora wa majengo ya serikali.


Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza jambo mara baada ya kuzuru kwa ziara ya kikazi katika Shule ya Msingi Hondogo iliyopo Kata ya Kibamba
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (kushoto) na Afisa Uchumi Mkuu Ndg Yamo Wambura wakikagua majengo ya shule ya msingi Hondogo iliyopo Kata ya Kibamba wakati wa ziara ya kikazi
Madarasa manne yaliyoamuliwa kuvunjwa na kujengwa upya madarasa mengine matano katika Shule ya Msingi Hondogo Jijini Dar es salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MKUU WA MKOA WA ARUSHA MRISHO GAMBO KATIKA ZIARA YA MAFUNZO NCHINI UFARANSA

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo akikaribishwa na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe. Samwel Shelukindo katika ubalozi wetu uliopo jijini Paris. Mhe Gambo yupo katika ziara ya mafunzo nchini Ufaransa, ambapo pamoja na mafunzo hayo amekua akiutangaza mkoa wa Arusha kama kitovu cha utalii nchini Tanzania. 

Mhe Gambo, akiwa huko mefanya mazungumzo na Balozi Shelukindo, na kubadilishana mawazo ya namna ya kuvutia wananchi wa nchi hiyo kutembelea Tanzania. 

Ufaransa ni moja ya zinazoleta watalii wengi nchini Tanzania. Pamoja na mambo mengine  Mhe RC na Balozi wamejadiliana mambo ya Msingi ya kufanya ili kuongeza watalii kutoka Ufaransa kuja Arusha, kupata wawekezaji kutoka Ufaransa kuja Arusha pamoja na namna ya kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo Mkoani humo, pamoja na kuanzisha tukio la kimataifa la kutangaza utalii mkoani Arusha kila mwaka.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo akiweka saini katika kitabu cha wageni baada ya kukaribishwa na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe. Samwel Shelukindo katika ubalozi wetu uliopo jijini Paris. 

DC KASESELA- TUTAUFUNGA MGODI WA NYAKAVANGALA HALI IKIENDELEA HIVI

$
0
0

Na Fredy Mgunda, Iringa

Wachimbaji wa madini katika mgodi wa nyakavangala wamefukiwa na mchanga kutokana na wachimbaji hao kuingia kinyume cha makubaliano yaliyowekwa baina ya wachimbaji na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela.

Akizungumza na blog hii Kasesela alisema kuwa Jana mida ya saa 1 jioni Duara la mgodi mmoja ulioko Nyakavangala uliporomoka na kufukia wachimbaji 4 . 

"Inasemekana wachimbaji hao walikuwa wameingia kuiba kwani duara hilo ni kati ya maduara ambayo Mkuu Wa wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela aliifungia ili ijengwe nguzo na ngao" alisema Kasesela

Kasesela alisema kuwa Watu 4 waliingia mgodini baada ya mafundi Wa ujenzi Wa ngao kupumzika kwa vile ni usiku ndipo wachimbaji nao wakaingia mgodini bila ruhusa

"Hadi sasa tumefanikiwa kuokoa 3 mpaka sasa huyo mmoja hajaokolewa bado yupo ndani ya mgodi kutokana na changamoto za uokoaji ili Juhudi zinaendelea za kumuokoa huyo mmoja" alisema Kasesela

Kasesela alisema kuwa changamoto ilikuwa ni namna ya kumuokoa kwani sehemu iliyokuwa imejifukia juu mwamba mwingine ulionekana kuwa na dalili za kushuka.ikawapasa kujengea kwanza eneo hilo kazi iliyochukua mda mrefu na ndipo waaze kuokoa.kwahiyo tunasubiri hatua nyingine sasa.

"Naendelea kuwaonya wachimbaji wasiendelee na uchimbaji eneo la chini maarufu kama kwenye "vein" mpaka wajenge ngao ili wasihatarishe maisha yao. Wakiendelea na kiburi tutaamua tufunge mgodi" alisema Kasesela.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza na blog hii juu ya kitu kinachiendelea kwenye mgodi wa nyakavangala.

RAIS DK.SHEIN AWAAPISHA MKUU WA JKU NA MKUU WA CHUO CHA MAFUNZO ZANZIBAR

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha Viongozi wa Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), aliowateua hivi karibuni kuwa Wakuu katika Vikosi hivyo. 

Katika hafla hiyo, Dk. Shein kabla ya kumuapisha Naibu Kamishna wa Chuo cha Mafunzo Ali Abdalla Ali, alimfisha cheo cha Ukamishna na baadae kumuapisha kuwa Kamishna wa Chuo cha Mafunzo, Zanzibar.

Wakati huo huo, Dk. Shein, amemuapisha Kanal Ali Mtumweni Hamad kuwa Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi, Zanzibar (JKU).

Hafla hiyo, ilifanyika Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar  Omar Othman Makungu, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said, 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za (SMZ), Haji Omar Kheir, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji.

Wengine ni Mkuu wa  Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud,  Wakuu wa Vikosi vya SMZ, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib, Washauri wa Rais wa Zanzibar pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimvalisha cheo cha Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Nd,Ali Abdalla Ali katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja kabla alikuwa  Naibu Kamishana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Nd,Ali Abdalla Ali kuwa  Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar  katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja kabla alikuwa  Naibu Kamishana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Kanal Ali Mtumweni Hamad  kuwa   Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi, Zanzibar (JKU )  katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zubeir Ali Maulid ni miongoni mwa Viongozi waliohudhurika katika hafla ya kuwapishwa Mkuu wa JKU na Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MATUKIO KATIKA PICHA: YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 46, MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO JUNI 13, 2017.

$
0
0
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akiongoza kikao cha 45 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 13, 2017.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe.Angeline Kairuki akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 46 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 13, 2017.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Edwin Ngonyani akifuatilia jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dk Suzan Kolimba  hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha 46 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 13, 2017.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana  Mhe.Anthony Mavunde akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 46 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 13, 2017.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera ,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akizungumza jambo na Mbunge wa Mtama Mhe.Nape Nnauye  katika kikao cha 46 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 13, 2017.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

TAARIFA YA MSIBA

$
0
0
Familia ya Bw.  Byabato wa Kinondoni, Morroco Dar es salaam inasikitika kutangaza kifo cha baba yao mpendwa Bw. Francis Byabato kilichotokea tar 12 June katika hospitali ya Muhimbili Dar es salaam. Miaka ya Awali,  Marehemu alifanya kazi na kampuni ya East African Community Nairobi na Arusha,  na katika ofisi ya Hazina ( Treasury) Dar es salaam. Baada ya kustaafu alianzisha biashara  kampuni ya Bureau de Change jijini Dar es salam.

Marehemu ameacha Mke wake Mpendwa. Demetria Byabato wa Kinondoni, Dar es salaam, pamoja na wanae --Digna Byabato- Makobore (Daudi) wa Mikocheni, Dar es salaam, Alvera Byabato- Ijumba (Edmund) wa Memphis, Tennessee, Hilda Byabato Curry (Reginald) wa Frisco, Texas, William Byabato wa Mikocheni Dar es salaam na Robert Byabato (Delilah) wa Frisco, Texas: Pamoja na Wajukuu Dorothy, Daniel, Kendra, Ingrid, Ethan, Adoree, Jayden, Robert Jr., Isabella na Braxton.
Dada zake Tereza, Leonida  na Maria.

Mazishi yatafanyika Bwanjai, Bukoba, ijumaa, June 16. Kutakuwa na misa ya kumuaga marehemu jumatano tarehe 14, saa sita mchana katika kanisa la St Peters, Oysterbay, Dar es salaam.

Bwana ametoa, Bwana ametwaa. Jina la bwana libarikiwe.

JESHI LA POLISI LAWATOA HOFU WADAU USALAMA WA MASHINDANO YA NDONDO CUP

$
0
0
Jeshi la polisi limethibitisha kuungana na wadau wa soka mkoa wa Dar es Salaam katika kuhakikisha ulinzi na usalama wa wachezaji, viongozi, waamuzi, mashabiki na mali zao wakati wote wa mashindano ya Ndondo Cup 2017.

Kamisha msaidizi wa polisi (ACP) Philip Kalangi amesema, jeshi la polisi litatumia mbinu ya ulinzi shirikishi pamoja na wadau wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha amani inakuwepo wakati wote wa mashindano.
Kamisha msaidizi wa polisi (ACP) Philip Kalangi  akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya kiusalama kwenye michuano ya Ndondo Cup inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 17 mwaka huu ikiwa ni hatua ya mtoano.


“Tumejipanga lakini tutakuwa na ullinzi shirikishi ambao utahusisha wadau wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama na vikundi mbalimbali vya ulinzi navyo vitakuwepo. Tunawasihi wananchi wajitokeze kwa wingi kuja kuona vijana wao, wapate burudani na mwisho wa siku tupate kitu tunachokitarajia.”

“Suala la ulinzi na usalama ni muhimu sana katika jambo lolote kwenye maisha ya kila siku, ulinzi na usalama ni suala mtambu na linahitaji ushirikishwaji wa pamoja, makuindi yote katika jamii yetu tunatakiwa tushiriki katika nafasi yake linahitaji kushiriki moja kwa moja katika ulinzi na usalama.”

“Hata kwenye jeshi la polisi tunafanya michezo, tuna program moja inaitwa michezo na vijana ambapo tumekuwa tunahamasisha vijana kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya na uhalifu wa aina mbalimbali.

Mratibu wa michuano ya Ndondo Cup Shafii Dauda akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya kiusalama kwenye michuano ya Ndondo Cup inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 17 mwaka huu ikiwa ni hatua ya mtoano, kulia ni Kamisha msaidizi wa polisi (ACP) Philip Kalangi.

“Kama mnavyofahamu, michezo inajenga ushirikiano, upendo na mambo mengi lakini kubwa ni ajira. Vijana wengi hawana ajira kwa hiyo kwenye mashindano haya tunategemea vipaji mbalimbali vitaibuliwa na kuwasaidia hapo badae kwenye maisha yao.”

“Sisi kama jeshi la polisi tutakuwepo na tumekuwa na mahusiano na raia enzi na enzi tangu kuanzishwa kwa jeshi la poilisi, hauwezi kututenga na raia wala huwezi kuwatenga raia na askari. Kwa hiyo ushirikiano ni lazima uwepo na uendelee kwenye masuala ya ulinzi na usalama.” 

Michuano ya Ndondo Cup 2017 hatua ya makundi inataraji kuanza rasmi Jumamosi Juni 17, 2017 ambapo mechi ya ufunguzi wa hatua ya makundi itazikutanisha Stimtosha dhidi ya Makuburi kwenye uwanja wa Kinesi.

RUVU SHOOTING YAWATEMA WACHEZAJI 10, YAPANGA KUSAJILI TISA WAPYA

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Uongozi wa timu ya soka ya Ruvu Shooting, jana Jumatatu, Juni 12, 2017 umekutana chini ya mwenyekiti wake Kanali wa Jeshi, Mkuu wa Kikosi cha Jeshi (CO) 832, Ruvu JKT Charles Mbuge, pamoja na mambo mengine kujadili taarifa ya mwalimu Malale Hamsini Keya aliyoiwasilisha baada ya kumalizika kwa msimu wa ligi 2016/17.

Kwa ushauri na mapendekezo ya mwalimu, uongozi umeamua kuachana na wachezaji 10 kwasababu mbalimbali, lakini pia kuanza mchakato wa kusajili wachezaji wengine wasiopungua tisa kutokana na ushauri na mapendekezo ya benchi la ufundi.

Afisa Habari wa timu ya Ruvu Shooting  Masau Bwire amesema wachezaji sita kati ya 10 walioachwa ni kipa Elias Emanuel ambaye alicheza mechi moja msimu mzima dhidi ya Mbao fc na kufungwa goli nne, Ismail Mgunda ambaye alicheza mechi nane, baadaye alitoroka kambini na mpaka sasa haijulikani alipo na Richard Peter ambaye hakucheza mechi hata moja kutokana na kiwango chake cha uchezaji kuwa cha chini sana kulinganisha na wechezaji wengine.

Wengine walioachwa ni Claide Luita ambaye alicheza michezo mitatu mzunguko wa kwanza, mzunguko wa pili hakucheza mchezo hata mmoja baadaye aliamua kuondoka mwenyewe ingawa kocha Malale kamsifia kwa kipaji na ubora wa kucheza mpira, Amour Bakari aliyecheza mchezo mmoja tu kutokana na uwezo na maumivu ya mara kwa mara na Alex Sety ambaye alicheza michezo sita.

Wachezaji wengine wanne walioachwa watatajwa baadaye baada ya taratibu na maelezo kuhusu ushiriki wao katika timu kukamilika.

Wachezaji tisa wanaotakiwa kusajiliwa ni beki wa kati mmoja, viungo wa pembeni wawili, viungo wakabaji wawili, full back wa kulia mmoja na washambuliaji watatu.

Kikosi kazi cha viongozi wanne kwa ushirikiano na walimu wa timu tayari kimeanza kazi ya usajili kazi inayofanywa kimyakimya, kwa usahihi sana mithili ya sumu ya nyoka Kifutu.

KLABU YA GYMKHANA DAR ES SALAAM KUADHIMISHA MIAKA 100 TANGU KUANZISHWA KWAKE.

$
0
0

Klabu ya Gymkhana Dar es salaam inayojihusisha na michezo ya aina mbalimbali imejipanga kusherehekea kutimiza miaka 100 kwa staili ya tofauti tangu kuanzishwa kwake mwaka 1916.

Katika kuadhimisha tukio hilo la kihistoria, Klabu hiyo imeandaa idadi ya michezo mbalimbali itakayosindikiza maadhimisho hayo ambapo michezo hiyo inatarajiwa kuanza tarehe 03 Julai, 2017 na kuhitimishwa tarehe 08 Julai kwa mujibu wa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Bw. Walter Chipeta.

Miongoni michezo iliyopangwa kufanyika katika kuadhimisha miaka 100 ya klabu hayo ni pamoja na Gofu, Tenisi, Skwashi, Soka, Kriketi, mchezo wa kuogelea na mingine mingi ambayo kwa ujumla itawahusisha wanachama na wasio wanachama wa klabu hiyo.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Klabu ya Gymkhana, Walter Chipeta alisema, “Maadhimisho ya miaka 100 ni tukio la kihistoria kwa ajili ya klabu yetu na tumejipanga kusheherekea shughuli hii kupitia michezo mbalimbali ambayo itaanza rasmi tarehe 03 Julai na kilele chake kuwa tarehe 8 Julai.”

Chipeta alisema klabu hiyo inawakaribisha wanachama na wasio wanachama kutoka ndani na nje ya Tanzania ili kushiriki kwenye maadhimisho hayo na kusisitiza kwamba washiriki watafurahia na kuburudika.

Mwenyekiti wa klabu ya Dar es salaam Gymkhana, Walter Chipeta (kulia) akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam. Klabu hiyo iko mbioni kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1916 ambapo imejipanga kuandaa michuano ya michezo mbalimbali kama Gofu, Kriketi, Tenisi, Skwashi, Soka, mchezo wa kuogelea na mingine mingi inayotarajiwa kuanza Julai 03 na kuhitimishwa Julai 08. Katikati ni Meneja Msaidizi wa klabu hiyo, Elizabeth Michael na kushoto ni Mratibu wa Masoko na Matukio Levina George.

Mwenyekiti wa klabu ya Dar es salaam Gymkhana, Walter Chipeta (kushoto)  akiwaeleza waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam kuhusiana na dhamira ya klabu hiyo ya kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1916. Klabu imejipanga kuandaa michuano ya michezo mbalimbali kama Gofu, Kriketi, Tenisi, Skwashi, Soka, mchezo wa kuogelea na mingine mingi inayotarajiwa kuanza Julai 03 na kuhitimishwa tarehe Julai 08 katika kuadhimisha siku hiyo ya kihistoria. Kulia ni Meneja wa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Ndugu Itandula Gambalagi.
Meneja wa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Ndugu Itandula Gambalagi akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusiana na udhamini wa mashindano yatakayosindikiza maadhimisho ya miaka 100 ya klabu ya Dar es Salaam Gymkhana tangu ilipoanzishwa mwaka 1916. Katika kuadhimisha siku hiyo ya kihistoria, klabu imejipanga kuandaa michuano ya michezo mbalimbali kama Gofu, Kriketi, Tenisi, Skwashi, Soka, mchezo wa kuogelea na mingine mingi inayotarajiwa kuanza Julai 03 na kuhitimishwa tarehe Julai 08.Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ndio mdhamini Mkuu wa mashindano hayo. Wadhamini wengine wa mashindano hayo ni pamoja na Clouds Media Group, Qatar Airways, ALAF, GSM, Serena Hotel, Eagle Africa Insurance brokers, Vodacom na Mwananchi Communications.Kushoto ni Mwenyekiti wa klabu ya Dar es salaam Gymkhana, Walter Chipeta.
Mwenyekiti wa klabu ya Dar es salaam Gymkhana, Walter Chipeta akisalimiana na Meneja wa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Ndugu Itandula Gambalagi wakati wa mkutano wa waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam. Klabu hiyo iko mbioni kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1916 ambapo imejipanga kuandaa michuano ya michezo mbalimbali kama Gofu, Kriketi, Tenisi, Skwashi, Soka, mchezo wa kuogelea na mingine mingi inayotarajiwa kuanza Julai 03 na kuhitimishwa tarehe Julai 08. 

UNICEF YASAIDIA VITANDA VYA WAGONJWA WA KIPINDUPINDU ZANZIBAR

$
0
0
 Waziri wa Afya, Mahmoud Thabit Kombo akipokea msaada wa vitanda vya wagonjwa wa kipindupindu kwa Afisa Mkaguzi Mkuu wa Shirika la kuhudumia watoto Duniani (UNICEF) Bi. Francesca Morandini katika kambi ya kipindupindu Chumbuni.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo alipotembele kambi ya kipindupindu Chumbuni.

Picha na Makame Mshenga.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA WAKUU WA MIKOA WOTE

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikutana na wakuu wa mikoa wote katika kikao kilichohudhuriwa pia na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, baadhi ya mawaziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 13, 2017


Viewing all 110109 articles
Browse latest View live




Latest Images