Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1734 | 1735 | (Page 1736) | 1737 | 1738 | .... | 3283 | newer

  0 0

  WANANCHI wa Tumbe, Kamati za mazingira na jumuiya ya Vijana Wa Tumbe na Viongozi wa Serikali wakipanda miti ya Mikoko katika bonde la Pondeani  katika maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani.
  WANANCHI wa Tumbe, Kamati za mazingira na jumuiya ya Vijana Wa Tumbe na Viongozi wa Serikali wakipanda miti ya Mikoko katika bonde la Pondeani Tumbe, katika maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani.
  MITI mbali mbali ya Mikoko ikiwa imepandwa katika bonde la Pondeani Tumbe, katika maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani ambayo huadhimishwa kila Juni 5 ya Kila mwaka.
  AFISA habari kutoka Idara ya Mazingira Pemba, Nassor Ali Salum akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kumaliza kazi ya upandaji wa Mikoko huko Tumbe, katika maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP  Simon Sirro  jana alifanya mazungumzo na wazee pamoja na viongozi wa dini wilayani Kibiti mkoani Pwani ili kubaini wahalifu wanaotekeleza mauaji ya watu wilayani humo na kusema vyovyote itakavyokuwa lazima watawarudisha kwenye msitari.
  Alisema kupitia mazungumzo hayo tayari amepata taarifa za wahalifu hao ingawa ni mapema kuziweka wazi ila amewakikishia wananchi kuwa waalifu wao ni lazima watapatikana.
  “Kubwa ni kwamba wazee wetu wa Kibiti wametueleza taarifa nyingi sana na mnavyojua hawa waalifu wanaishi ndani ya Kibiti, ndani ya Ikwiriri, kwa hiyo wazee wetu wamejaribu kutueleza ni wapi tunaweza kuwapata na chanzo cha mambo yote haya,” alisema IGP Sirro na kuongeza;
  “Kwa hiyo kimsingi mambo mengine mengi ni ya kipelelezi ambayo siwezi kuyasema kwa sasa, lakini kikubwa wametupa dira, muelekeo kwa maana kwamba wale ndugu zetu au maadui zetu kwa lugha nyepesi tumepata njia nzuri ya kudeal nao. Kwa hiyo nitume salamu kwao kwamba waendelee kukimbia lakini njia ya muongo ni fupi na mwisho wa siku tutawarudisha kwenye mstari"
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro akiongea na wanahabari wilayani Kibiti mkoani Pwani.

  0 0  0 0


  0 0


  0 0  0 0  0 0
  0 0


  Na Fredy Mgunda,Mufindi

  Halmashauri ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa inakabiliwa kuwa na watendaji wa vijiji na kata ambao sio waanilifu kutokana na matumizi mabaya ya fedha za wananchi katika vijiji kitu kinachosababisha migogoro mingi huko vijijini.

  Akizungumza na blog hii mwenyekitii wa halmashauri ya wilaya ya mufindi Festo Mgina alisema kuwa halmashuri inakabiliwa na watendaji wa vijiji ambao wanatumia vibaya pesa za wananchi na ndio sababu inayosababisha kutoitisha mikutano ya hadhara.

  “Mimi kama mwenyekiti wahalmashauri hii ni muumini mkubwa wa utawa bora hasa kwa kuzingatia dhana ya uwazi na uwajibikaji kwasasababu nikizangatia dhana hii basi kila kitu kitaenda vizuri tatizo watendaji wangu hawataki kabisa dhana ya uwazi na uwajibikaji yaani watendaji wangu wa vijiji wengi wao ni mizigo tu kwangu” alisema Mgina

  Mgina alisema kuwa wamekuwa wakiwawajibisha pamoja na kuwafukuza kazi baadhi ya watendaji hao wa vijiji ili kuepuka migogoro kwa wananchi.

  “Wananchi wanachanga pesa za maendeleo lakini unakuta mtendaji ametoka alikotoka na kuanza kuzitafuna pesa za wananchi hiyo sio haki jamani niseme ukweli maafisa watendaji wangu wa vijiji si waadilifu na nitatizo kubwa linalosababisha migogoro mingi huko vijijini”alisema Mgina

  Aidha Mgina amekiri kuwa na ubungufu wa maafisa watendaji wa kata na vijiji na ndio sababu inayosababisha kukaimisha viongozi wengine wa serikali kushika nafasi za kuwa maafisa za watendaji.

  “Saizi tunawatumia waajiliwa wa serikali hasa maafisa kilimo kuwa watendaji wa vijiji kutokana na kuwa uhabari wa wanayakazi wa kada hiyo na labda niseme ukweli nimepiga marufuku waalimu kukaimishwa nafasi hiyo kwa kuwa hata walimu wengi wamekuwa wakisababisha migogoro kutokana n wao kutokujua nini cha kufanya” alisema Mgina


  Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi mhe Festo Mgina akizungumza na Mwandishi wa habari juu ya maafisa watendaji wa vijiji vyote vya halmashauri ambao si waadilifu katika kufanya kazi walizopewa.


  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na wajumbe wakati wa kikao hicho
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akitulia kumsikiliza kwa makini mshairi Mansur Athan wakati akighani shairi mwishoni mwa kikao hicho
   Wajumbe wakiwa ukumbini tayari kumsikiliza Alhaj Bulembo
   Mwenyekiti wa CCM wa CCM Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera, Haji Seruhu akifungua kikao hicho.
   Wajumbe wakihamasika kwenye kikao hicho.


  0 0

  Mhandisi wa mitambo ya kusoma Taarifa za hali ya hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Bw. Michael Minja akieleza matumizi ya kifaa cha kupima mvua kwa Maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu walipotembelea vituo hivyo vinavyotekelezwa na Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari uliopo Lushoto Mkoani Tanga Juni 6, 2017.
  Mhasibu Mwandamizi Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Consolata Mazigo akiuliza swali kwa Mhandisi wa mitambo ya hali ya hewa Bw. Michael Minja wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari wa Ofisi ya Waziri Mkuu Juni 6, 2017 Lushoto Tanga.
  Mhandisi wa mitambo ya kusoma Taarifa za hali ya hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Bw. Michael Minja akieleza matumizi ya mtambo wa kisasa wa usomaji wa taarifa za hali ya hewa kwa Maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (hawapo pichani) wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari ulio chini ya Ofisi hiyo.
  Baadhi ya Watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu wakinukuu maelezo ya Fundi Sanifu Mkuu Bonde la Pangani Bw. Vendelin Basso (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa kutathimini Utekelezaji wa Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari katika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo Kilimanjaro, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango Ofisi ya Waziri Mkuu (bajeti) Bi. Grace Moshi Juni 7, 2017.
  Fundi Sanifu Mkuu Bonde la Mto Pangani Bw. Vendelin Basso akiwasilisha utekelezaji wa Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari kwa upande wa Bonde la Mto Pangani mkoani Kilimanjaro wakati wa ukaguzi wa Utekelezaji wa mradi huo uliofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu Juni 7, 2017.


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel, Le Van Dai, Akizungumza na waandishi wa habari wakati kampuni hiyo ilipokuwa ikitoa pongezi kwa serikali kwa kuanzisha mfumo wa wawazi wa ulipaji kodi kwa njia ya kielektroniki, Kampuni hiyo ni miongoni mwa makampuni matatu ya simu ya kwanza kujiunga na mfumo huo ambao amefafanua kuwa unaweka uwazi katika biashara. Pamoja nae katika picha ni Meneja Uhusiano wa Kampuniu hiyo Stela Pius na Meneja Mawasiliano Hindu Kanyamala (Kushoto).
  Meneja Mawasiliano wa Halotel, Hindu Kanyamala akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Wakati kampuni hiyo ilipofanya mkutano wa kuipongeza serikali kwa kuanzisha mfumo wa ulipaji kodi kwa njia ya kielectroniki. Katikati ni Mkurugenzi Mtenzaji wa Kampuni hiyo Le Van Dai na Meneja Uhusiano Stella Pius.


  Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Halotel, imeipongeza serikali kwa kuweka mfumo wa kukusanya kodi kwa njia rahisi na yenye uwazi na kufafanua kuwa wao wamekuwa kampuni ya kwanza kujiunga na kufurahia utaratibu huo kama ilivyobainishwa na kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere, kwani unawezesha kampuni kuwa wazi katika malipo yote ya kodi na tozo wanazozifanya kwa wateja.

  Akizungumza na waandishi wa Habari, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo bwana Le Van Dai, amefafanua kuwa wao kama kampuni siku zote wamejiweka mbele katika kuhakikisha wanatimiza matakwa ya serikali kwa kufuata taratibu zote zinazowekwa na mamlaka husika.

  “Tulipofahamishwa kuhusu utaratibu huu wa ukusanyaji kodi tulifurahia sana kwa sababu unaweka wazi maendeleo ya biashara na ukusanyaji wa mapato ya serikali, sisi kama wawekezaji tunafurahia kuwa na njia bora za usimamizi wa mapato ya serikali na kampuni husika kwani unatuwezesha sisi pia kujipima kujua biashara kama ni nzuri au sivyo na kuangalia namna bora ya kushauriana na mamlaka husika katika kufanikisha mazingira bora ya kibiashara” Alisema Dai.

  Aidha, Mkurugenzi huyo pia aliwaeleza waandishi wa habari kuwa wanaendelea kufurahia mafanikio ambayo kampuni hiyo imekuwa ikiyapata tangu kuanzishwa kwake.

  “Katika taarifa ya robo ya kwanza ya mwaka huu 2017 iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeonesha namna ambavyo kampuni yetu imeendelea kufanya vyema katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita,”

  "Kimsingi, idadi ya wateja wa kampuni za simu ilipungua kutoka 40,173,783 kwa Desemba mwaka jana na kufika39,856,212 kwa Machi mwaka huu. Hii ina maana kuwa kuna baadhi ya mitandao ya simu ilipoteza wateja ila Halotel tumeweza kuongeza wateja wapya wapatao 73,872. Hii ni ishara kuwa Watanzania wanaridhika na huduma zetu. Tunawaahidi kuwa hatutawaangusha," alisema,”

  Alisema Dai na kuongeza kuwa “hii ni dalili nzuri kwetu kibiashara. Tunawashukuru Watanzania kwa kuendelea kutuamini na kuendelea kujiunga na sisi, tunawaahidi kuendelea kuboresha huduma zetu na kuufanya Halotel uendelee kuwa Mtandao chaguo namba moja kwao.” Alihitimisha Mkurugenzi huyo.

  Pamoja na mambo mengine Mkurugenzi huyo amesema kampuni hiyo bado inatoa kipaumbele kwa kutoa huduma bora kwa jamii ya Watanzania ikiwepo pamoja na kuwezesha miundombinu ya mawasiliano kwa taasisi mbalimbali za serikali pamoja na taasisi za kijamii, zikiwemo shule, hospitali, ofisi za posta na halmashauri mbalimbali. Hivi karibuni kampuni hiyo ilitangaza uwekezaji wa Zaidi ya bilioni 200 katika kuboresha ubora wa mtandao huo, ikilenga kuongeza kasi ya intaneti na ubora wa huduma za sauti. 

  0 0

  Na Dotto Mwaibale

  WAKINA Baba nchini wametakiwa kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa watoto wao badala ya kuwaachia kazi hiyo ifanywe na wakina mama pekee.

  Mwito huo umetolewa na Selemani Bishagazi wakati akichangia mada katika kongamano la siku moja lililohusu elimu ya afya ya uzazi kwa watoto hasa wa kike lililoandaliwa na TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam jana.

  "Suala la utoaji wa elimu ya afya ya uzazi kwa watoto wetu hasa wa kike ni letu sote kati ya baba na mama kwani baba ndie chanzo kikubwa cha mapato katika familia" alisema Bishagazi.

  Bishagazi alisema suala la kutoa fedha za kunulia pedi wakati mtoto wa kike anapokuwa kwenye hedhi si la mama bali hata baba anawajibu wa kutoa fedha hizo na akaomba dhana hiyo potofu kuwa mama ndiye anawajibika katika suala hilo iachwe.
  Ofisa Programu wa TGNP Mtandao, Anna Sangai (kushoto), akitoa mada katika kongamano la siku moja lililohusu elimu ya afya ya uzazi lililofanyika Makao Makuu ya TGNP Mabibo Dar es Salaam jana. Kongamano hilo liliandaliwa na TGNP.
  Mwanafunzi Leila Kisinga kutoka Sekondari ya Mabibo akitoa mada kuhusu via vya uzazi vya mwanamke vinavyofanya kazi.
  Kongamano likiendelea.
  Mwanafunzi Juma Nasoro kutoka Sekondari ya Mabibo akitoa mada kuhusu via vya uzazi vya mwanaume vinavyofanya kazi.


  0 0

  MACHO na masikio ya watanzania leo yanahamishiwa kwa muda mjini Dodoma wakati Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango atakapowasilisha bajeti ya pili ya Serikali ya Awamu ya Tano bungeni mjini hapa.

  Awali Wizara ya Fedha na Mipango iliwasilisha Bajeti ya kwanza ya Sh 29.5 trilioni iliyoonekana kubana sehemu tofauti tofauti na kusababisha wananchi kulalamika, wengi wakisema mzunguko wa fedha umedhoofika huku biashara zikifungwa.

  Bajeti hiyo ndiyo iliyowafanya wachambuzi wa masuala ya uchumi, makundi ya biashara na wabunge kumtaka waziri huyo atangaze hatua mahususi za kuiokoa sekta binafsi na zitakazoharakisha ukuaji uchumi.

  Wadau wanatarajia kuwa Dk Mpango, ambaye aliwahi kuwa mchumi mwandamizi katika Benki ya Dunia na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ataangalia kwa kina hali ya sasa ya uchumi na kutangaza hatua za kikodi zitakazozuia kupanda kwa gharama za maisha na wakati huo huo kuipa mkono sekta binafsi ili Serikali ifikie lengo lake kuifanya Tanzania  kuwa nchi ya viwanda.

   Mfumuko wa bei, ambao unahusishwa na kupanda kwa bei za vyakula, tayari umefika asilimia 6.4 kwa mwezi Aprili kutoka asilimia 5.1 mwezi kama huo mwaka jana.

  0 0

  Mkurungenzi wa Mkuu wa Tanzania Media Foundation (TMF), Bw. Ernest Sungura aliyekaa mbele katikati akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kuchora vibonzo vijana muda mfupi baada ya kuzindua rasmi warsha ya kuwajengea uwezo vijana katika Uchoraji wa Vibonzo, yanayoendelea katika kiota cha wasanii cha NAFASI, Mikocheni jijini Dar es salaam. Mafunzo hayo yanatolewa na asasi ya Nathan Mpangala Foundation (NMF) na kufadhiliwa na Ubalozi wa Uswis nchini. Kushoto kwa mgeni rasmi ni Mwenyekiti wa NMF, B. Nathan Mpangala wakati kulia kwake ni afisa utawala wa Nafasi Art Space. Mafunzo yatamalizika kesho ambapo Balozi wa Uswis nchini tanzania, bi. Florence Tinguely Mattli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
  Mwezeshaji Nathan Mpangala, akimwelekeza jambo mmoja wa washiriki wa warsha ya karikacha na uchoraji vibonzo yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
  Penye vibonzo hapakosi tabasamu.
  Baadhi ya washiriki wakifanya yao.
  Mchoraji, Said Michael maarufu kama ‘Wakudata’ akifanya yake.

  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (Mb), akiwasilisha Bungeni Hali ya Uchumi wa Taifa katika mwaka 2016, Mjini Dodoma, ambapo katika mwaka huo, pato la Taifa lilikua kwa asilimia 7.0, likichangiwa na kukua kwa sekta ya ufuaji umeme, kuimarika kwa huduma za usafirishaji na uhifadhi wa mizigo, sekta ya habari na mawasiliano, ujenzi na uchimbaji wa madini na mawe.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (Mb), akiwasilisha Bungeni Hali ya Uchumi wa Taifa katika mwaka 2016, Mjini Dodoma, ambapo katika mwaka huo, pato la Taifa lilikua kwa asilimia 7.0, likichangiwa na kukua kwa sekta ya ufuaji umeme, kuimarika kwa huduma za usafirishaji na uhifadhi wa mizigo, sekta ya habari na mawasiliano, ujenzi na uchimbaji wa madini na mawe.

  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (Mb), akiwasili katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma kwa ajili ya kuwasilisha Bungeni Hali ya Uchumi wa Taifa katika mwaka 2016.

  (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango)

  0 0

  Wadau kutoka sekta za kilimo na uchumi wamekutana kujadiliana namna bora ya uanzishwaji wa Mfuko wa Ubunifu Vijijini (rural innovation fund) wenye lengo la kuchochea, kuhamasisha na kusaidia uvumbuvi katika maeneo ya maendeleo vijijini, ukopeshaji wa shughuli za kilimo na huduma za taasisi ndogo za kifedha.

  Mkutano huo wa siku moja umeandaliwa kwa ushirikiano wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na Programu ya Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani Mazao na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF).

  Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Adam Kamanda amesema wadau wana mchango mkubwa wa kutoa maoni yatakayosaidia kuboresha usimamizi wa Mfuko huo ambao utakuwa chini ya TADB.

  “Nawaomba tujadili namna bora itakayosaidia ndoto ya Serikali ya kuchagiza upatikanaji wa fedha za gharama nafuu kwa ajili ya kuwasaidia wakulima hasa katika maeneo ya maendeleo vijijini, ukopeshaji wa shughuli za kilimo na huduma za taasisi ndogo za kifedha,” alisema.

  Bw. Kamanda ameongeza kuwa uanzishwaji wa mfuko huu unalenga kutekeleza kwa vitendo dhamira ya Serikali ya kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya kilimo ambayo ni shughuli kuu kwa Watanzania wengi wanaoishi maeneo ya vijijini.
  Mratibu wa Uanzishwaji wa Mfuko wa Ubunifu Vijijini, Bw. Albert Ngusaru akizungumza kabla ya ufunguzi wa mkutano wa siku moja wa kujadili namna bora ya kuendeleza Mfuko huo.
  Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Adam Kamanda (kushoto) akifungua mkutano wa siku moja wa kujadili namna bora ya kuendeleza Mfuko wa Ubunifu Vijijini huo.
  Washiriki wa Mkutano wa Majadiliano ya Uanzishwaji wa Mfuko wa Ubunifu Vijijini wakifuatilia kwa umakini mkutano huo.  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amemtembelea na kumjulia hali Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali David Msuguri nyumbani kwake Butiama.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi wa wilaya ya Bunda waliojitokeza barabarani kumsalimu akitokea Butiama kuelekea jijini Mwanza
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwaaga baadhi ya Wananchi wa wilaya ya Bunda waliojitokeza barabarani kumsalimu akitokea Butiama kuelekea jijini Mwanza

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  ILE michuano ya Ndondo Cup inatarajiwa kuanza kwa hatua ya makundi huku kituo cha kurushia matangazo ya Luninga cha Azam Tv wakidhamini kwa mara nyingine tena.

  Utiaji wa saini wa mkataba wa kuonesha michuano hiyo umefanyika leo baina ya Mratibu na Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media wakishuhudiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es salaam Almas Kasongo.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media, Tido Mhando amesema kuwa wanaipongeza Clouds Media kama waandaaji na waratibu wa michuano hiyo ya Ndondo Cup kwani imeweza kuwa na hamasa kubwa kwa vijana ambao wanapenda mpira na pia wanatumia kama fursa ya ajira.

  Mhando amesema, wanaonyesha michuano hiyo kwa mara ya nne ikiwa mara ya kwanza walianza kwa kuonyesha hatua ya nusu fainali ila kuanzia msimu wa 2016 wameanzia hatua ya makundi.

  Akizungumza kabla ya uwekaji wa saini wa mkataba huo, Mratibu wa michuano ya Ndondo Cup Shafii Dauda amesema kuwa huu ni mwaka wa nne toka kuanza kwa michuano hiyo na kampuni ya Azam Media wameweza kuionyesha na mwaka huu wameingia tena mkataba.

  Dauda amesema, anawashukuru sana Azam Media kwa hatua hii kubwa ya kuonyesha tena michuano hiyo na wanaamini kuwa itazidi kuhamasisha kujiajiri kwa kucheza mpira wa miguu kwani kwa sasa inaonekana Afrika Mashariki na Kati.

  Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguh Mkos wa Dar es salaam, Almas Kasongo amewapongeza Clouds Media na Azam media kwa hatu kubwa wanayoifanya ya kuhakikisha wadau na wapenzi wa Mpira wanaendelea kupata burudani.


  Droo ya hatua ya Makundi itafanyika kesho katika fukwe za Escape One majira ya saa 8 mchana na kuweza kuzifahamu timu 32 zitakazoumana Kumpata bingwa wa Ndondo Cup msimu wa 2017.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Tido Mhando wakiweka saini mkataba wa makubaliano ya urushwaji wa matangazo wa michuano ya Ndondo Cup na Mratibu Shafii Dauda ukishuhudiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es salaam Almas Kisongo. (hayupo pichani).
  Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Tido Mhando akikabidhiana mkataba wa makubaliano ya urushwaji wa matangazo wa michuano ya Ndondo Cup na Mratibu Shafii Dauda ukishuhudiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es salaam Almas Kisongo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Tido Mhando akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mkataba wa makubaliano ya urushwaji wa matangazo wa michuano ya Ndondo Cup kushoto ni Mratibu Shafii Dauda na kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es salaam Almas Kisongo

  0 0


  Kwa mara ya kwanza kampuni ya Candy and Candy imeanzisha Application mpya inayojulikana kama NIKO HUB ambayo ni mkombozi wa wafanyabiashara wengi na watumiaji wa mtandao huo.NIKO HUB inajihusisha na mambo yote yanayohusu vyakula,vinywaji na filamu (movies).

  Lengo kubwa la NIKO HUB ni kunyanyua wafanyabiashara wakubwa na wadogo kwa kupanua soko lao na kujiongezea kipato zaidi zaidi na kumuondolea usumbufu mteja wakati anapohitaji huduma ambapo Aplication hii inamfanya mteja kuagiza bidhaa na kuletewa mahali alipo kikubwa anachotakiwa kufanya ni kupakua Aplication hii kwenye Google Play bure na kisha anaanza kuitumia kwenye simu yake.

  NIKO HUB inafanya kazi mahali popote ulipo katika bara la Afrika na popote unapoenda huhitaji kupakua Aplication nyingine bali unaendelea kutumia ileile, Aplication hii pia inabadili lugha kulingana na lugha inayotumika katika nchi husika kwa mfano Tanzania inapatikana kwa kiswahili lakini ukienda kwenye nchi za kiarabu zilizoko Afrika itakuletea lugha ya kiarabu na ukienda nchi inayotumia lugha ya kifaransa itafanya hivyo pia N.K.

  Jambo kubwa ni kwamba NIKO HUB pia imeandaa tamasha litakalojulikana kama NIKO HUB EAT OUT FESTIVAL ambalo litafanyika siku ya sikukuu ya Eid na hakutakuwa na kiingilio kwa washiriki ambapo litashirikisha wajasiriamali mbalimbali wanaojihusisha na uuzaji wa vyakula mbalimbali na vinywaji.

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Candy And Candy Bw. Joe Kariuki akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelelzo leo wakati akitambulisha Aplication yake mpya kwa ajili ya kuuza Vyakula, Vinywaji na Filamu Movie leo, kushoto ni Meneja wa kampuni hiyo Bi Hasna Mwishehe.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Candy And Candy Bw. Joe Kariuki akionyesha Aplication hiyo jinsi inavyofanya kazi wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelelzo leo wakati akitambulisha Aplication yake mpya kwa ajili ya kuuza Vyakula, Vinywaji na Filamu Movie leo, kushoto ni Meneja wa kampuni hiyo Bi Hasna Mwishehe.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Candy And Candy Bw. Joe Kariuki akizmpigia simu mmoja wa wamiliki wa mgahawa ulioko Sinza na kuagiza chakula ili aletewe alipo wakati akitambulisha Aplication yake mpya kwa ajili ya kuuza Vyakula, Vinywaji na Filamu Movie leo, kushoto ni Meneja wa kampuni hiyo Bi Hasna Mwishehe.older | 1 | .... | 1734 | 1735 | (Page 1736) | 1737 | 1738 | .... | 3283 | newer