Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

PEREIRA: TUTAPAMBANA NA WALIOPANDIKIZWA KUPANGA SAFU KATIKA UCHAGUZI WA CCM.

0
0


NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka viongozi na watendaji wa zamani wa ngazi za matawi waliowania tena nafasi za uongozi katika uchaguzi unaoendelea hivi sasa ndani ya chama hicho kutoshiriki kwenye vikao vya kuchuja na kujadili fomu za wagombea wa nafasi za uongozi.

Tahadhari hiyo imetolewa na Katibu wa NEC, Idara ya Organazesheni CCM Taifa, Nd. Pereira Ame Silima katika mwendelezo wa ziara yake huko Mkoa wa Kusini kichama Unguja, alisema mtu aliyewania nafasi ya uongozi ndani ya chama hicho hana haki ya kujadili na kuchuja fomu za wagombea wenzake kwani kufanya hivyo ni kinyume na Katiba ya Chama hicho.

Alisisitiza kwamba katika zoezi hilo ni lazima kila kiongozi asimamie taratibu za uchaguzi ili kuepuka malalamiko yasiyokuwa ya lazima.

“ Kuna baadhi ya matawi kumetokea changamoto za baadhi ya wagombea kujadili na kupitisha fomu za wagombea wenzao jambo ambalo ni kinyume na taratibu za Kikatiba hivyo hatuwezi kuvumilia vitendo hivyo ni bora uchaguzi urejewe katika maeneo yaliyoripotiwa ukiukaji wa miongozo yetu”, alisema Nd. Pereira.

Nd. Silima alisema dhamira ya chama hicho ni kuhakikisha chaguzi zote zitakazofanyika ndani ya chama na jumuiya kuhakikisha wanapatikana viongozi bora waliopatikana kwa mujibu wa matakwa ya Kikatiba na sio watu binafsi.Katibu huyo aliweka wazi msimamo wake kwamba atapambana vikali na baadhi ya watu waliopandikizwa katika uchaguzi huo ili wapange safu na makundi ya viongozi wanaowataka wao kwa baadhi ya ngazi za uongozi .

Katibu wa NEC, Idara ya Organazesheni CCM Taifa, Nd. Pereira Ame Silima akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja, kichama, Ramadhan Abdallah Ali “ Kichupa” mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Mkoa huo zilizopo Dunga Wilaya ya Kati Unguja.

Katibu wa NEC, Idara ya Organazesheni CCM Taifa, Nd. Pereira Ame Silima akitoa nasaha kwa viongozi wa CCM Mkoa na Wilaya za Kusini na Kati Kichama katika ziara ya kiongozi huyo visiwani Zanzibar.
Baadhi ya viongozi na Watendaji wa ngazi mbali mbali za Chama na jumuiya zake Mkoa wa kusini na Wilaya zake kichama. ( PICHA NA AFISI KUU CCM ZANZIBAR). 


Mkazi wa Arusha Oscar Haule aibuka na Milioni 20 za Biko

0
0
DROO ya 12 ya Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’ imechezeshwa leo asubuhi, huku ikimpata mshindi wake wa nonge nono la Sh Milioni 20 ikiwa ni maalum kwa Jumatano hiyo kutoa mshindi wa Sh Milioni 20 ambapo mkazi wa Arusha, Oscar Haule kuibuka kidedea kwa kuzoa mamilioni hayo.

Donge nono hilo limekwenda kwa mshindi huyo wa Arusha, ikiwa ni mwendelezo wa kutoa mamilioni katika zawadi mbalimbali za bahati nasibu huyo inayoanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja kwa zawadi za hapo hapo huku droo kubwa ya Jumatano na Jumapili hii pia itatoa Sh Milioni 20 kama Jumatano mbili zilizopita.

Akizungumza leo asubuhi katika uchezeshaji wa droo hiyo, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba ni wakati wa kushinda mamilioni ya Biko kwa kuchezesha bahati nasibu yao rahisi na yenye nafasi kubwa ya ushindi wa zawadi za papo kwa hapo na zile za wiki zinazotoa mamilioni kwa droo ya Jumatano na Jumapili.

Alisema hadi sasa zaidi ya washindi 55,000 wameshinda zawadi kutoka Biko, huku wakiamini kuwa Biko ni chanzo cha mapato na kinachoweza kubadilisha maisha ya washindi wao wanaoamua kujitokeza kwa wingi kuwania mamilioni kwa kupitia mchezo huo.

Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akichezesha droo ya 12 ya Bahati Nasibu ya Biko, ambapo mkazi wa Arusha, Oscar Haule alitangazwa mshindi wa donge nono la Sh Milioni 20. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid.

“Kucheza Biko ni rahisi kwa sababu kila mtu anaweza kucheza kwa kupitia simu yake ya mkononi hususan kwa Tigo, Vodacom na Airtel ambapo wataingia kwenye vipengele cha kufanya miamala kwenye simu hizo kwa kuingiza naamba ya kampuni ambayo ni 505050, huku namba yetu ya kambukumbu ikiwa ni 2456.


Balozi wa Biko Tanzania Kajala Masanja akionyesha namba ya ushindi wa Sh Milioni 20 aliyopata mkazi wa Arusha, Oscar Haule, katika droo iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akichezesha droo ya 12 ya Bahati Nasibu ya Biko, ambapo mkazi wa Arusha, Oscar Haule alitangazwa mshindi wa donge nono la Sh Milioni 20. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid.
 

Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Bakari Maggid kushoto akiandika namba ya ushindi ya mkazi wa Arusha, Oscar Haule katika droo ya Sh Milioni 20 iliyochezeshwa leo.

HASS PETROLEUM GROUP SELLS 40% OF ITS OWNERSHIP TO OMAN TRADING INTERNATIONAL

0
0
  Hass Petroleum Group has sold 40% of its shares to Oman Trading International (OTI) in a move that will see the Kenyan oil marketing company embark on its strategic growth and expansion plans across the Eastern, Central and Horn of Africa. The Group will invest the additional funding from the transaction to enhance its market visibility through new distribution assets specifically Service Stations across its key markets in the region.

 It will also boost the marketer’s working capital and increase competitiveness in the Open Tender System. In turn, OTI will provide its supply and trading capabilities to strengthen the Hass service offering, enhance services to consumers and contribute to economic growth across the region. 

The Hass founder and management team will continue to operate the business and work closely with OTI to grow and continue long-standing relationships with customers, suppliers and regulators. This acquisition is in line with the respective companies’ long-term strategies. 

OTI’s strategic priority of accelerating its growth by entering new emerging markets with high potential will fit well with Hass’s aspiration of being Africa’s leading oil marketing company. As a regular supplier of refined products to the Southern and East African region, this transaction will enable OTI and its new partner Hass to strengthen their businesses across a substantial African footprint. 

The completion of the transaction remains subject to approval by the relevant regulatory authorities in the various countries in which Hass operates in. Abdinasir Ali Hassan Chairman and founder of Hass, commented, "I am delighted to conclude this transaction with OTI.

 I am convinced that this partnership is a major step in ensuring Hass’ continued competitiveness across the region and I am confident that with OTI we can achieve our mutual long term growth aspirations.” Talal Hamid Al-Awfi, CEO of OTI, has expressed his satisfaction at the conclusion of the deal “We are delighted to move onto the next phase of growth for OTI, agreeing our first major investment into Africa with Hass. 

Hass is a unique business with substantial scale and growth potential where we have enjoyed a long standing relationship; most importantly we share a common understanding and vision of the African energy market.” Standard Advisory London Limited, a member of the Standard Bank Group (“Standard Bank”)acted as exclusive financial advisors to OTI and KPMG Advisory Services Ltd Kenya acted as exclusive financial advisors to Hass.

The Chairman of Hass Petroleum- Mr. Abdinasir Ali Hassan (left) and Mr. Talal Hamid Al-Awfi sign agreements following the sale of Hass Shares to Oman based OTI in Muscat. 
Hass Petroleums’ Chairman Mr. Abdinasir Ali Hassan (left) and the Chief Executive of the Oman Trading International (OTI), Mt. Talal Hamid Al-Awfi exchange documents during an event to mark OTI’s acquisition of 40% shareholding in Hass Petroleum.

MAKALA : ASANTE OMOG,TUMEREJEA ALIKOTUTOA RC LIBOLO

0
0
Mchezo wa soka ni mchezo ambao ili ufanikiwe hauhitaji jitihada za mtu mmoja ila jitihada za timu nzima kuanzia wachezaji,viongozi na benchi la ufundi. Klabu ya Simba imeweza kutembea katika tafsiri hiyo ya mafanikio ya soka yanahitaji ushirikiano wa timu nzima ili kufikia malengo waliyojiwekea.

Ni kitu ambacho wapenzi na wadau wengi wa soka hawajafahamu dhana ya viraka vilivyopo katika mpira na mwisho vinaunda mpira mwenyewe. Viraka vya mpira ni sehemu ya kuelezea muunganiko unaohitajika katika watu ili kuleta mafanikio ya kitu kizima na pia utofauti wa rangi katika viraka huelezea timu mbili tofauti katika uwanja zinazocheza mchezo wenyewe.

Msimu wa 2016/2017 umekua bora sana kwa klabu ya simba na kufanya klabu imalize ligi nikiwa nafasi ya pili na kufanikiwa kubeba kombe la Azam Sport Federation Cup ( ASFC) msimu huu katika fainali Kali dhidi ya Mbao fc ya Mwanza.

Maandalizi ya klabu ya Simba waliyoyafanya ndiyo matunda ya walichokipata na kitawaletea mafanikio zaidi kama wakiendekea nacho kwa misimu mingine inayokuja.

Moja ya eneo ambalo klabu ya simba ilikua na changamoto na kujikuta wanashindwa kujishika vizuri ilikua katika eneo la benchi la ufundi,naweza kusema Benchi la simba limetibiwa ipasavyo.

Joseph Omog huyu mkameruni ni moja ya makocha wazuri na wenye kuamini katika nidhamu ya mchezaji mmoja na baadae nidhamu ya klabu kwa ujumla. Hakuna asiyefahamu mafanikio aliyoyapaya Omog akiwa na klabu Fc Leopard ya Congo Brazzaville alipoifikisha katika fainali ya kombe la shirikisho katika fainali waliyocheza dhidi ya Sc vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Omog alijitangaza katika mashindano ya afrika kama ilivyo kwa George Lwandamina wa yanga alivyojitangaza kupitia Mashindano ya ligi ya mabingwa. Kabla ya ujio wa Omog klabu ya simba ilikua klabu iliyokua ikicheza soka safi lisilo na faida kwao kutokana na upungufu wa nidhamu ya mchezo kupitia utimamu wa mwili na kuhimili mikiki mikiki ya ligi kwa dakika tisini za mchezo.

Na Honorius Mpangala.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Mwanasheria wa TBS apandishwa Mahakama ya Kisutu kujibu tuhuma zinazomkabili.

0
0

Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii

Mwanasheria Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Baptister Marco Bitaho (54) amepandishwa katika kizimba cha mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma tatu zikiwemo za kuishi na kufanya kazi nchini bila kibali.

Mshtakiwa Bitaho amesomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa.

Akisoma hati ya mashtaka leo, wakili wa Serikali kutoka Uhamiaji, Novatus Mlay amesema, Mei 19, mwaka huu huko Kinondoni katika ofisi ya uhamiaji Bitaho akiwa raia wa Burundi alikutwa nchini Tanzania bila ya kuwa na kibali cha kumuwezesha kuishi nchini.
 
Aidha imedaiwa kuwa, siku na mahali hapo Mshtakiwa Bitaho alikutwa akifanya kazi kama mwanasheria Mkuu wa TBS bila ya kuwa na kibali kinachomruhusu kufanya kazi hapa nchini.
 
Katika shtaka la tatu Mlay amedai kuwa, Julai 6 mwaka 2011 katika ofisi ya Uhamiaji ya Dar es Salaam iliyopo wilaya ya Ilala, mshtakiwa akiwa raia wa Burundi alitoa taarifa za uongo kuhusu maelezo yake binafsi wakati akijaza fomu ya kuomba pasi ya kusafiria namba CT (5)(Ai).
 
Wakili Mlay aliongeza kuwa, kitendo hicho cha kutoa taarifa za uongo kilimuwezesha Bitaho kupata pasi ya kusafiria ya Tanzania yenye namba AB 474856 huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria za nchi.
Hata hivyo mshtakiwa amekana mashtaka hayo na yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana.
 
Mahakama imeamuru mshtakiwa Bitaho kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika watakaosaini dhamana ya milioni 20,na Kesi hiyo itatajwa tena Juni 21.

MKUU WA WILAYA YA ILALA, SOPHIA MJEMA AMEPOKEA MSAADA WA VYAKULA KWA AJILI YA WATU WASIOJIWEZA NA MAYATIMA

0
0
Ubalozi wa Kuwait nchini kwa kushirikiana na Taasisi  ya Human Relief wamekabidhi msaada wa vyakula mbalimbali kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema kwa ajili ya watu wasiojiweza na mayatima ili kupata futari katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo mapema leo, Mjema amesema, chakula hicho kitapelekwa katika vituo vya watoto yatima na wasiojiweza ili waweze kuufurahia mwezi wa Ramadhani.

"Chakula hiki tunaenda kuwapa wananchi ambao hawana uwezo na familia ambazo kwa kweli tunaona hwana uwezo," alisema Mh. Mjema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kampuni ya Bigbon, Mohammed Bahashwan amesema, taasisi hiyo imekuwa ikitoa misaada mbalimbali na hasa kwa mayatima bila kujadili dini zao,amesema na kuongeza kuwa kuwa mbali na kutoa misaada hiyo lakini pia taasisi hiyo imekuwa ikijenga visima na misikiti katika maeneo mbalimbali nchini.

Kwa upande wake, balozi wa Kuwait nchini, Mhe Jaseem Al Najem amesema kuwa, nchi hiyo itaendelea kushirikiana na serikali katika mambo mbalimbali ya kusaidia jamii.

Amesema msaada huo wameanza na wilaya ya Ilala lakini watakuwa wakitoa misaada na maeneo mengine kulinga na uhitaji wa mambo mbalimbali katika jamii nzima kwa kushirikiana na serikali.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala ,Sophia Mjema (kulia) akipokea Msaada wa vyakula mbalimbali kutoka kwa Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jaseem Al Najem.Pichani kushoto ni Katibu Tawala wilaya ya Ilala,Edward Mpogolo.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala ,Sophia Mjema Akizungumza wa Globu ya jamii baada ya kupokea msaada huo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala ,Sophia Mjema na Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jaseem Al Najem wakiwa katika picha ya pamoja. leo Jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem akiwasili katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala ,Sophia Mjema.

NATAMANI KUCHEZA LIGI YA TANZANIA - MUKHWANA

0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Beki wa kati wa timu ya Nakuru All Stars James Sadicky Mukhwana amesema kuwa anaamini ipo siku atacheza katika mojawapo ya timu za ligi kuu nchini Tanzania.

Beki huyo mwenye mwili uliojazia n a urefu wa futi sita amesema kuwa anaitamani sana ligi ya Tanzania na kama ikitokea timu itakayomuhitaji yupo tayari kuitumikia ili mradi wakubaliane.

Mukhwana ambaye jana katika mchezo wa Nakuru All Stars dhidi ya Simba alionekana mwiba kwa safu ya ushambuliaji wa timu ya Simba na kuweza kuhakikisha hakuna mshambuliaji anayetikisa nyavu za timu yao.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 26, amepitia katika timu mbalimbali za nchini ikiwemo kituo cha kukuzia vipaji cha Nakuru Youth Olympic mwaka 2002 akiwa na umri wa miaka 12 na baadae kupandishwa mpaka timu kubwa ya Nakuru All Stars na kuitumikia kwa miaka miwili.

Baada ya kuachana na Nakuru Mukhwana alijiunga na Complay Fc ya ligi daraja la kwanza mwaka 2013 na kuitumikia timu hiyo kwa mwaka mmoja na baadae kuhamia Osiria Fc mwaka 2014.

Mukhwana hakuweza kudumu sana katika timu ya Osiria na kujiunga na Bitiko United mwaka 2015 na kucheza kwa miezi sita na kuamua kwenda St joseph na kumalizia miezi sita iliyobaki ambapo zote zinashiriki ligi daraja la kwanza. Mwaka 2016, Mukhwana alijiunga na Nakumat na 2017 kuhamia Nakuru All stars ambapo anacheza mpaka sasa. 

Mukhwana amesema bado anaamini anauwezo wa kucheza mpira na anatamani sana kucheza ligi kuu ya Uingereza huku akisfia uwezo wa mchezaji raia wa Kenya Victor Wanyama anayekipiga katika timu ya Totenham, David Kalaba wa Zesco na mchezaji wa nje Thiago Silva. 

Nakuru wapo nchini kwa ajili ya michuano ya Sportpesa Super Cup inayoendelea ikizikutanisha timu nane ambapo kwa sasa umeingia katika hatua ya nusu fainali mechi zitakazopigwa kesho kati ya Yanga na AFC Leopard huku mchezo wa pili ukiwa kati ya Nakuru All Stars na Gor mahia.
Beki wa kati wa timu ya Nakuru All Stars James Sadicky Mukhwana akipambana na kiungo wa Simba Mohamed Ibrahim wakati wa mpambano wao uliofanyika jana katika michuano ya Sportpesa Super Cup.


JOKETI MWEGELO AKABIDHI MIFUKO 100 YA SARUJI KWA SHULE YA SEKONDARI YA MAPOSENI- RUVUMA

0
0

WATOTO WENYE MATATIZO YA USIKIVU SASA KUTIBIWA NCHINI.

0
0

NA WAMJW-DAR ES SALAAM.

WATOTO wenye matatizo ya usikivu watapata matibabu ya kupandikizwa vifaa vya usikivu hapa nchini katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili badala ya kwenda nje ya nchi kwa matibabu kama ilivyokuwa awali.

Hayo yamesemwa na Waziri wa afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipozindua huduma hiyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo jijini Dar es salaam.

“Serikali haitapeleka mgonjwa mwenye matatizo ya kusikia nje ya nchi kwa ajili ya kupandikizwa vifaa vya kusikia na badala yake atatibiwa nchini ili kupunguza rufaa za wagonjwa wan je ya nchi” alisema Mh. Ummy.

Aidha Waziri Ummy amesisitiza juu ya umuhimu wakujiunga na mfuko wa Afya wa Jamii wa NHIF ili kupata fursa ya kutibiwa kwa gharama ndogo zaidi, huku akisisitiza kuwa wananchi wote watakaokuwa na kadi ya NHIF wataweza kupata matibabu ya upandikizaji wa kifaa cha kusikia bure kupata huduma hii.

Mbali na hayo Mh. Ummy ameahidi kuwa Serikali kupitia Wizara yake ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuunga mkono kwa kuisaidia hospitali ya Muhimbili ili kuendelea kufanikisha upasuaji wa Watoto hivyo kupunguza gharama inayopata Serikali kusafirisha Watoto hao nje ya nchi pindi wapatapo matatizo hayo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili Lawlence Mseru amsisitiza kuwa moja kati ya mipango ya Hospitali ya Muhimbili ni kuhakikisha kuwa wanapunguza idadi ya wagonjwa wanaokwenda kutibiwa nje ya nchi kila mara jambo linaloigharimu Serikali pesa nyingi. 

Aidha Dkt. Mseru aliongeza kuwa licha ya kufanikisha tukio hilo la Kihistoria wanaomba Serikali kupitia Wizara ya Afya kusaidia kuboresha Wodi za Wagonjwa mahututi, ununuzi wa Vifaa tiba, kuongeza vyumba vya upasuaji jambo litalopunguza msongamano wa shughuli za hospitali pia kuongeza Wataalamu waendao nje ya nchi kwaajili ya mafunzo ili kuendeleza huduma katika nchi yetu jambo litakalosaidia kuwa na Wataalamu wengi hivyo kuweza kufanikisha huduma kwa wagonjwa wengi zaidi.

Nae Prof. Sunil Narayan Dutt kutoka Hospitali ya Apollo nchini India ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa jitihada inayoonesha hasa katika kutetea haki za watoto.

Kwa upande Bi. Hilda Bohela ambae ni mzazi wa Apulie Bohela aliyepata huduma hiyo nchini amewasihi wazazi wenzie kuwapeleka watoto kufanyiwa uchunguzi pindi waonapo hali isiyokuwa yakawaida kwa watoto wao na kuachana na mila potofu jambo linalopelekea watoto wengi kupata ulemavu .

waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watot, ummy Mwalimu (katikati) akizungumza leo jijini Dar es Salaam kwenye uzinduzi wa Upasuaji wa Upandikizaji Kifaa cha Usikivu (Cochlear-Implant) kulishoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH), Profesa Charles Majinge.
waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ummy Mwalimu akiwajulia hali wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili leo jijini Dar es Salaam.
waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ummy Mwalimu akiwasili katika hospitali ya Taifa Muhimbili leo jijini Dar es Salaam.
waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pomoja na watendaji wa hospitali ya Taifa Muhimbili leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

MAKAMU WA RAIS AMALIZA ZIARA MUSOMA MJINI LEO

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kamwe Serikali haitagawa chakula kwa wananchi wavivu ambao hawataki kufanya kazi na kusubiri chakula kutoka Serikalini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassana ametoa kauli hiyo wakati akihutubia mamia ya wananchi wa Manispaa ya Musoma katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mukendo mjini Musoma.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa Serikali itapeleka chakula kwa wananchi ambao mazao yao yaliharibiwa kwa mvua au yalikauka kwa ukame au kwa  maafa mengine na sio kwa wananchi wanaokaa vijiweni mchana kutwa bila kufanya kazi wakisubiri neema ya chakula kutoka kwa Serikali.

Amewahimiza wananchi kote nchini kuendelea kufanya kwa bidii ikiwemo shughuli za kilimo na pindi wanapovuka wajiwekee akiba na waache tabia ya kuuza mazao yote wanayovuka ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa chakula kwenye familia zao.

Makamu wa Rais pia amewataka viongozi wa mkoa wa Mara washirikiane na wananchi katika kuwaelemisha mbinu bora za kilimo ili waweze kupata mazao mengi ikilinganishwa na hali ilivyo kwa sasa.

Kuhusu tatizo la uvuvi haramu, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameziagiza Kamati za Ulinzi na Usalama kufanya misako ya hali na mali katika kupambana na tatizo hilo ambalo limechangia kupunguza samaki katika maeneo mbalimbali nchini.

Ametoa mfano kwa mkoa wa Mara kuwa ulikuwa na viwanda Vinne vya kuchakata samaki lakini kutokana na shughuli za uvuvi haramu na wa kutumia sumu umepelekea viwanda Vitatu kukosa malighafi hiyo na kusitisha uzalishaji.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema jambo hilo ni baya kwa sababu limeikosesha Serikali mapato na kusababisha wananchi wakose ajira kutoka kwenye viwanda hivyo jitihada za makusudi lazima zifanyike katika kukomesha uvuvi haramu katika maeneo mbalimbali nchini hasa katika Ziwa Victoria.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia wakazi wa Musoma mjini kwenye kiwanja cha Mukendo ikiwa ni siku ya mwisho ya ziara yake mkoani humo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia boksi lililohifadhiwa samaki tayari kwa kusafirisha nje ya nchi wakati alipotembelea kiwanda cha Kuchakata Samaki cha Musoma.



TUTAINGIA KWA AJILI YA USHINDI DHIDI YA GOR MAHIA- KOCHA NAKURU

0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

KOCHA Msaidizi wa timu ya Nakuru All Stars Jimmy Angila amesema kuwa mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Sportpesa Super Cup 2017 dhidi ya Gor Mahia utakuwa ni mgumu sana ila wana imani watatoka na ushindi.

Akizungumza na mtandao huu,  Angila amesema kuwa katika mchezo wao huo hawatakubali kuona wanapoteza kwani kwa wao ni muhimu sana kuingia fainali na cha zaidi hawataingia kwa kuidharau bali watahakikisha wanashinda.

Amesema kuwa, wanaifahamu vizuri timu ya Gor Mahia na zaidi wanatarajia mechi hiyo kuwa ngumu sana kwa kila upande.

"mechi yetu dhidi ya Gor Mahia ni ngumu sana ila tutaingia uwanjani kwa kuhakikisha tunashinda mchezo huo ambao ni muhimu sana kwetu kwani lengo letu ni kuingia fainali,"amesema Angila.

Angila alisisitiza kuwa kikosi chao kipo vizuri na benchi la ufundi ndiyo litapanga kikosi cha kesho na mabadiliko yanaweza kufanywa kulingana na hali za wachezaji.

Daktari wa timu ya Nakuru Vicent Angwenyi amethibitisha kutokuw ana majeruhi katika kikosi chao na zaidi wote wanaweza kucheza katika game mechi ya kesho dhidi ya Gor Mahia.

Timu hizo kutoka Kenya zinakutana katika hatua ya nusu fainali ya  Kombe la Sportpesa Super Cup 2017 na mchezo huo unatarajiwa wa ushindani mkubwa kwani timu hizo mbili zinajuana huku Gor Mahia ikiwa inashiriki ligi kuu ya Kenya na Nakuru ikiwa ligio darala la kwanza.


Kikosi cha Nakuru All Stars

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO JUNI 7, 2017

SAFARI YA MWISHO YA BALOZI ABDULCISCO OMAR MTIRO

0
0
 Omar, Mtoto wa Marehemu Abdulcisco Mtiro akiweka mchanga  kwenye kaburi la Baba yake
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ally Hassan Mwinyi, akiweka mchanga kwenye kaburi la Marehemu Balozi Abdulcisco Mtiro katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam
  Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete akiweka mchanga kwenye kaburi la Marehemu Balozi Abdulcisco Mtiro katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam
 Wazirio Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim akiweka mchanga kwenye kaburi la Marehemu Balozi Abdulcisco Mtiro katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam
 Jaji Mkuu Mstaafu  Mhe. Othman Chande,akiweka mchanga kwenye kaburi la Marehemu Balozi Abdulcisco Mtiro katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam
 CDF Mstaafu  Jenerali Davis Mwamunyange akiweka mchanga kwenye kaburi la Marehemu Balozi Abdulcisco Mtiro katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda, akiweka mchanga kwenye kaburi la Marehemu Balozi Abdulcisco Mtiro katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam
 Balozi Ben Mashiba akiweka mchanga kwenye kaburi la Marehemu Balozi Abdulcisco Mtiro katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam
Balozi ,Abdulhaman Shimbo, akiweka mchanga kwenye kaburi la Marehemu Balozi Abdul Cisco Mtiro katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam.Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

KATIBU MKUU WIZARA YA ARDHI DKT. KAYANDABILA AAGWA RASMI NA WATUMISHI WA WIZARA HIYO

0
0
Aliyekuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dkt. Yamungu Kayandabila amesisitiza utumishi bora unaozingatia Miongozo na Sheria.

Dkt. Kayandabila aliyeteuliwa hivi karibuni na Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), akiwaaga Watumishi wa Wizara alihimiza utendaji bora kazini katika kutoa huduma kwa Wananchi na kusihi Watumishi kuendelea na kasi hiyo.

Aidha, aliwashukuru Watumishi wa Wizara ya Ardhi kwa ushirikiano wao walioonyesha kwake ambao umesababisha kudhihirisha matukio chanya kwa Wizara. Alisema; “ Tukumbuke kuwa sisi ni Watumishi wa Umma, tuendelee kufanya kazi kwa bidii kwa kuwahudumia Wananchi kwa bidii”.

Awali akizungumza kwa niaba ya Watumishi wa Wizara; Afisa Mipango Miji, Baltazar Sumari alisema; “ Tunakushukuru Katibu Mkuu kwa jinsi ulivyotuwezesha kufanya kazi kwa umoja na nidhamu, Mungu akuwezeshe uweze kuendelea kudumisha utendaji wako wa kazi Benki Kuu kama jinsi ulivyofanya Wizarani hapa na tutaendelea kuhitaji ushauri wako”.

Naye muwakilishi wa Taasisi za Wizara; Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipangomiji (TPRB);  Helena Mtutwa alisema kuwa Dkt. Kayandabila ana karama ya kipekee ambayo imemuwezesha kuongoza vyema kwa kuweza kuonyesha njia bora katika utendaji kazi na kuonya kwa hekima.  

Dkt. Kayandabila anakwenda kutumika katika Benki Kuu ya Tanzania kama Naibu Gavana anayeshughulikia Uchumi na Fedha (Economic and Financial Policies – EFP), akiwa na Naibu Gavana mwenza aliyeteuliwa naye kwa kipindi kimoja; Dkt. Bernard Yohana Kibese atakayehusika katika eneo la Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha (Financil Stability and Deepening – FSD).

Na kitengo cha Mawasiliano Serikalini – 
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

 Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila akizungumza na watumishi alipokua akiwaaga. Dkt. Kayandabila ameteuliwa na Mhe. Rais kuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania. (BoT).
 Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila akipokea zawadi, ikiwa ni ishara ya pongezi kwa uteuzi wake mpya alioupata. Anayemkabidhi zawadi hiyo kwa niaba ya watumishi wa wizara ni Naibu Katibu Mkuu, Dkt Mosses Kusiluka.
Watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika picha ya pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo; Dkt. Yamungu Kayandabila mara baada ya kuwaaga.

SERIKALI KUENDELEA KUDHIBITI MATUMIZI YA FEDHA ZA UMMA YASIYO YA LAZIMA

0
0
Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

Serikali  kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina imeahidi kuendelea kusimamia na kufuatilia sheria na  miongozo yote iliyotolewa  ili kuhakikisha lengo la kudhibiti matumizi  yasiyo ya lazima kwenye Mashirika na Taasisi za Umma ikiwemo safari za nje na posho za wajumbe wa Bodi za mashirika na Taasisi zote za Umma linafanikiwa.

Hayo yameelezwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Vwawa (CCM), Mhe. Japhet Hasunga ambaye alitaka kujua hatua ambazo Serikali inatarajia kuchukua  kudhibiti matumizi ya fedha za Umma katika Taasisi zake.

Dkt. Kijaji alisema kuwa Serikali imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa matumizi ya fedha za Umma yasiyo ya lazima yanadhibitiwa kikamilifu kupitia   Sheria mbalimbali zilizotungwa na Bunge ikiwemo Sheria ya Bajeti Na. 11 ya mwaka 2015 ambayo imebainishwa hatua mbalimbali za kibajeti zenye lengo la kuongeza usimamizi na udhibiti wa matumizi ya fedha za Umma katika Mashirika na Taasisi za Umma.

“Sheria hiyo imebainisha utolewaji wa Mwongozo wa Mipango na Bajeti wa Serikali unaojumuisha  Mashirika na Taasisi zote za Serikali ambao unatoa miongozo mbalimbali ya kuzingatiwa katika matumizi ya Umma kwa mwaka husika”, alifafanua Dkt. Kijaji

Alisema kuwa kupitia Sheria hiyo, Ofisi ya Msajili wa Hazina imepewa mamlaka ya kupitia bajeti za Mashirika na Taasisi zilizo chini yake kwa kuzingatia miongozo na mipango ya Serikali inayotarajiwa kutekelezwa.

Mhe. Kijaji alibainisha kuwa katika Sheria hiyo Ofisi ya Msajili wa Hazina imepewa jukumu la kupitia na kuridhia kanuni za fedha za Mashirika na Taasisi zote za Umma ili kuimarisha usimamizi na udhibiti wa matumizi ya fedha za Umma.

“Sheria nyingine iliyopitishwa na Bunge ni marekebisho ya Sheria ya Fedha ya Mwaka 2015 ambayo iliweka ukomo kwa Taasisi na Mashirika ya Umma kutumia asilimia 60 tu ya mapato yake kwa matumizi ya kawaida yasiyojumuisha mishahara”, aliongeza Dkt. Kijaji.

 Aidha, Dkt. Kijaji alisema kuwa katika kuhakikisha Ofisi ya Msajili wa Hazina inatekeleza majukumu yake kisheria, imetoa miongozo mbalimbali yenye lengo la kudhibiti matumizi ya Mashirika na Taasisi za Umma ili kupunguza matumizi ya Serikali yasiyo ya lazima.

“Miongoni mwa miongozo hiyo ni barua iliyotolewa na Msajili wa Hazina tarehe 10 Novemba, 2015 ya kudhibiti safari za nje ya nchi zisizo za lazima kwa watumishi wa Mashirika na Taasisi za Umma ambazo awali zilionekana kutumia sehemu kubwa ya fedha za Umma”, alisema Dkt. Kijaji.

Aliongeza kuwa waraka wa Msajili wa Hazina Na. 12 wa mwaka 2015 kuhusu Posho za Vikao vya Bodi ya Wakurugenzi wa Mashirika na Taasisi za Umma pia ni miongoni mwa miongozo ya kuzuia matumizi yasiyo ya lazima kwani waraka huo umefuta posho za vikao vya Bodi na kuondoa utaratibu wa Bodi kuwa na vikao zaidi ya vinne kwa mwaka.

Dkt. Kijaji alisema kuwa Waraka wa Msajili wa Hazina Na. 1 wa mwaka 2016 kuhusu posho za kujikimu kwa Wajumbe wa Bodi za Wakurugenzi wa Mashirika na Taasisi za Umma ulikuwa na lengo la kuendeleza jitihada za Serikali kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ya fedha za Umma.

Alisema kuwa Waraka huo uliweka ukomo wa posho hizo kwa Wajumbe wa Bodi kwa safari za ndani na nje ya nchi, huku akisisitiza kuwa bado Serikali itaendelea kuhakikisha matumizi ya fedha za Umma yasiyo ya lazima yanadhibitiwa kikamilifu.


SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda ya Dar es salaam chaendelea na msako mkali kudhibiti madereva bodaboda na abiria wanaovunja sheria

0
0

 Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda ya Dar es salaam  Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Awadhi Haji  (gwanda la kijani) amendelea kutoa  elimu kwa madereva wa bodaboda pamoja na abiria ambao wamevunja sheria za makosa ya usalama barabarani ikiwemo kutokuvaa kofia ngumu,bkupita taa nyekundu,bkupakia abiria zaidi ya mmoja na kadhalika. Watuhumiwa wamekamatwa sehemu mbalimbali wilayani Temeke katika msako mkali unaoendelea katika mkoa wa Dar es salaam.
 Watuhumiwa waliokamatwa sehemu mbalimbali wilayani Temeke katika msako mkali unaoendelea katika mkoa wa Dar es salaam wakimsikiliza Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda ya Dar es salaam  Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Awadhi Haji 

Waziri Ummy Mwalimu Azindua Huduma Mpya ya Kupandikiza Vifaa vya Usikivu Muhimbili, apiga Marufuku Wagonjwa Kutibiwa Nje ya Nchi

0
0
Serikali imesema kwamba kuanzia sasa haitapeleka wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya kupandikiza vifaa vya usikivu kwa kuwa huduma hiyo imeanza kutolewa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Kauli hiyo imetolewa Leo na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu katika hospitali hiyo wakati akizindua huduma ya upasuaji wa kupandikiza vivaa vya usikivu (Cochlea Implant).
Ummy alisema kuwa huduma hizo zitakuwa zikitolewa Muhimbili kwa sababu ina madaktari bingwa wenye uwezo wa kufanya upasuaji huo na vifaa vya kisasa na kuokoa gharama kubwa ambazo zilikuwa zikitumika awali kupeleka wagonjwa nje ya nchi.
Waziri huyo amesema katika hospitali za umma, Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kutoa huduma ya upandikizaji wa vifaa vya usikivu na ya pili kutoa huduma hiyo katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki ikitanguliwa na Kenya.
“Nafarijika Tanzania kuwa nchi ya kwanza kutoa huduma hii kupitia hospitali ya umma ambayo ni Muhimbili yenye hadhi ya ubingwa wa hali ya juu. Wenzetu Kenya huduma hii inatolewa kwenye hospitali binafsi na inakadiriwa kugharimu dola 31,000 za Marekani ambazi ni sawa na Sh69 milioni za Kitanzania. Hivyo basi tuna kila sababu ya kujipongeza kwa hatua tuliyofikia,”
 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu Leo amezindua huduma mpya ya upandikizaji wa vifaa vya usikivu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH). Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi wa hospitali hiyo, Profesa Charles Majinge akifuatilie mkutano huo.
 Daktari Bingwa wa Masikio, Koo na Pua, Dkt. Edwin Liyombo wa Muhimbili akieleza jinsi mtu mwenye tatizo la kutosikia anavyofanyiwa upasuaji na kuwekea kifaa cha usikivu.
 Wataalamu walioshirikiana na madaktari na wauguzi wa Muhimbili kufanya upasuaji wa kupandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto wakiwa kwenye mkutano huo Leo. Kutoka kulia ni Dk Sunil Dutt kutoka India, Dk Hassan Wahba wa chuo Kikuu cha Ain Shams mjini Cairo, Misri, Mohamed El Disouky anayesimamia vifaa vya usikivu Afrika na Mona Amin kutoka Kampuni ya Med-El. Wengine ni wataalamu kutoka Tanzania, Uganda na Kenya.
 Mmoja wa wazazi ambaye mtoto wake amefanyiwa upasuaji wa upandikizaji wa kifaa cha usikivu akimweleza Waziri jinsi  mtoto wake anavyozungumza vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji na kuwekewa kifaa cha usikivu.
Mama Theodora Myalla akizungumza na mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu baada ya mtoto wake, Mekzedeck Kibona kufanyiwa upasuaji na kuwekewa kifaa cha usikivu juzi katika Hospitali ya Muhimbili. Mtoto huyo sasa anaendelea vizuri.Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

MAHAKIMU NCHINI WAKUMBUSHWA JUU YA UFANYAJI KAZI KWA WELEDI NA UADILIFU

0
0
Na Mary Gwera, Mahakama, Njombe

JAJI Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Iringa, Mhe. Mary Shangali ametoa wito kwa Mahakimu na wadau wa Mahakama nchini kushirikiana kwa pamoja katika kutoa huduma ya haki kwa wananchi.

Aliyasema hayo mapema Juni 07, 2017  alipokuwa akiongea na Mahakimu wa Mahakama mkoani Njombe baada ya kuhitimisha ziara yake ya kukagua shughuli za Mahakama katika Mahakama za Mwanzo na Wilaya za Njombe, Ludewa na Makete pamoja na Gereza la Ludewa na Makete.

“Ushirikiano wa karibu na Wadau wa Mahakama kama Polisi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mawakili na Watumishi wa Mahakama n.k  ni muhimu katika kutekeleza shughuli yetu ya utoaji haki kwa wananchi, jambo hili lina faida nyingi mojawapo ikiwa ni kusaidia kupunguza mlundikano wa kesi katika Mahakama zetu,” alifafanua Mhe. Shangali ambaye pia ni Jaji namba moja (1) wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Kwa upange mwingine, Mhe. Jaji Shangali alibainisha changamoto alizokumbana nazo katika ziara yake ya kukagua shughuli za Mahakama mkoani Njombe kuwa ni tatizo kubwa la usafiri wa kuwachukua Mahabusu kutoka Magerezani na kuwarudisha.

“Hii ni moja ya changamoto kubwa niliyokumbana nayo katika Mahakama zote nilizozitembelea mkoani Njombe, changamoto hii haiihusu Mahakama moja kwa moja ipo chini ya Jeshi la Polisi, lakini kwa kuwa tunafanya kazi kwa kutegemeana changamoto hii inatuathiri na inaweza kusababisha mlundikano wa mashauri na Mahabusu magerezani kutokana na Wahusika wa kesi kutofikishwa Mahakamani kwa ajili ya kusikiliza kesi zao kwa wakati stahiki,” alisema Jaji Shangali.
 Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Iringa, Mhe. Mary Shangali akisisitiza jambo alipokuwa akiongea na baadhi ya Mahakimu wa Mahakama mkoani Njombe baada ya kukamilisha ukaguzi katika Mahakama za Mwanzo na Wilaya zilizopo mkoani humo.
 Wahe. Mahakimu wakiandika baadhi ya masuala muhimu aliongelea Mhe. Jaji Mfawidhi katika kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Mahakama ya Wilaya-Njombe mapema Juni 8.

  Mhe. Jaji Dkt. Paul Kihwelo, ambaye pia ni Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto Mhe. Jaji Dkt. Kihwelo yupo Njombe akiendelea na zoezi la vikao maalum vya kuondosha mlundikano wa mashauri linaloendelea kwa sasa.
 Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo-Lupembe iliyopo mkoani Njombe, Mhe. Godfrey Msemwa akiuliza swali ili kupata ufafanuzi.

 Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Iringa, Mhe. Mary Shangali (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mahakimu wa Mahakama mkoani Njombe mara baada ya kika, wa tatu kushoto ni Naibu Msajili, Mahakama Kuu-Kanda ya Iringa, Mhe. Agatha Chugulu


Ajali chakechake, Pemba

0
0
 Gari aina ya Toyota DYNA lenye namba za usajili 2330GX limepata ajali leo eneo la Kiuvyu katika barabara iendayo Chake Chake, Pemba, na kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo watu watatu wamejeruhiwa  vibaya na kukimbizwa hospitali ya Mkoani kwa matibabu. Chanzo cha ajali na majina ya majeruhi havikuweza kupatikana mara moja.

Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images