Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

WORLD MERIT TANZANIA YAJIPANGA KUMRUDISHA RAIS TRUMP KATIKA MABADILIKO YA TABIA NCHI

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akimpongeza Kiongozi wa World Merit Tanzania , Rose Mmbaga katika siku ya kilele cha Mazingira Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Taasisi isiyo ya Kiserikali inayojihusisha na utunzaji wa Mazingira nchini ya Word Merit Tanzania,  imesema ipo katika kampeni maalum ya kuhakikisha kuwa Rais wa Marekani Donald Trump anatambua uwepo wa mabadiliko ya tabia nchi Duniani kwa kuanzisha kampeni ya GREEN TRUMP.

Hayo yamesemwa na kiongozi wa shirika hilo nchini Tanzania , Rose Mmbaga alipokuwa akizungumza na Ripota wa globu ya Jamii wakati wa kufunga siku ya Mazingira Duniani iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam jana.

“kwa sasa tumeamua kuwa na kampeni moja ambayo inakwenda kwa jina la ‘GREEN TRUMP’ Ambayo itawakutanisha vijana wanaojitolea kwa kupanda miti nchi nzima ili waweze kumuaminisha Rais wa Marekani kuwa mapinduzi ya kijani yanawezekana licha ya kiongozi huyu kujitoa katika ule mkataba wa Paris” amesema Mmbaga.

Ameongeza kuwa yeye kama kiongozi kijana ameamua kujikita katika kuhamasisha swala la mazingira ili kusaidia vijana wengine kuingia katika mapambano haya,ili nchi yetu iweze kujikinga na majanga mbalimbali.

Amesema kuwa mabadiliko ya tabia nchi yamekuwa yakileta majanga mengi sana nchini ikiwemo suala kurudisha maendeleo nyuma kwa kuharibu miundombinu, ambayo imejengwa kwa gharama kubwa kutoka katika fedha za watanzania.

Alimaliza kwa kusema kuwa ufike wakati wa Vijana sasa kutambua na kuheshimu mazingira ili yaweze kututunza kwa ajili ya kizazi chetu cha baadae.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akiwa katika picha ya pamoja na Vijana wa World Merit Tanzania ambao wamejitolea kutunza Mazingira nchini

MAALIM SEIF AJUMUIKA NA WAKAZI WA BUGURUNI KUPATA FUTARI NA SWALA

$
0
0

 Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif akiwasili katika Mtaa wa Buguruni akipokewa na Naibu Meya wa Jiji Omary Kumbilamoto
 Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na wakazi wa Buguruni aliojumuika nao pamoja katika futari na swala
  Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad  akiwa katika ibada iliyofanyika katika Baraza la Mtendeni 2 Buguruni
  Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na Wananchi wa Buguruni ambao alijumika nao katika futari ya pamoja
 Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akiwa na viongozi wa juu wa Chama mara baada ya kupata futari

MBUNGE COSATO CHUMI ATOA MSAADA WA AMBULANCE NYINGINE JIMBONI KWAKE

$
0
0
Na Fredy Mgunda,Mafinga

MBUNGE wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi kwa kushirikiana na wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wametoa msaada wa gari la kubeba wagonjwa (ambulance) kwa ajili ya matumizi ya kituo cha afya cha Igohole ya wilayani Mufindi, mkoani Iringa iliyopo katika jimbo lake hilo.

Gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser lilikabidhiwa kwa uongozi wa halmashauri ya mji wa Mafinga inayosimamia uendeshaji wa kituo hicho katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika Igohole, mjini Mafinga.

Akikabidhi msaada huo Chumi alisema; “napenda ifahamike kwamba gari hilo limenunuliwa na wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Uadilifu na uaminifu kwa serilikali ndio umetufanya tushirikiane vyema katika mambo mengi kwa faida ya wananchi wa jimbo langu la Mafinga.”

Alisema gari hilo la wagonjwa ni rafiki kwa wagonjwa na wajawazito kwa kuwa lina vifaa tiba vinavyoweza kutumika kutolea huduma wakati wakipelekwa hospitalini.
MBUNGE wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi akizungumza na wananchi wa Igohole wakati kukadhi gari la kubebea wagonjwa ambalo amepewa na wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto 
MBUNGE wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi sambamba na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa mafinga Charles Makoga wakikata utepe wa gari la kubebea wangonjwa la kituocha afya cha Igohole
hawa ni baadhi ya wananchi waliojitokeza wakati wa kupokea msaada wa gari hilo la kubebea wagonjwa lilotelewa na mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi kwa kushirikiana na wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto .

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akutana na Mbunge wa jimbo la Serengeti

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Serengeti Mhe. Marwa Ryoba Chacha wakati wa ziara yake katika wilaya ya Serengeti, Mbunge huyo alimwambia Makamu wa Rais kuwa jimboni kwake wanafanya kazi kwa kushirikiana na Serikali bila kujali itikadi za vyama.

DIWANI KATA YA PUGU KWA KUSHIRIKIANA NA MISS UBUNGO 2014 WAADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA KWA KUPANDA MITI SHULE YA MSINGI MINAZI MIREFU

$
0
0
 Diwani wa Kata ya Pugu, Boniventure Mphuru akiwa na Muanzilishi wa Mradi wa CLEAN WATER SANITATION AND HYGIENE ambaye pia ni Miss Ubungo 2014, Diana Joachimu Kato wakiongozana na Wanafunzi wa shule ya Msingi minazi mirefu, Ukonga Jijini Dar es salaam Juni 5, 2017 wakati wa zoezi la kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani, ambapo walifanya usafi katika eneo lote la shule hiyo pamoja na kupanda miti.
 Diwani wa Kata ya Pugu, Boniventure Mphuru akiwa na Muanzilishi wa Mradi wa CLEAN WATER SANITATION AND HYGIENE ambaye pia ni Miss Ubungo 2014, Diana Joachimu Kato wakijiandaa kupanda mti katika moja ya eneo la shule ya Msingi minazi mirefu Juni 5, 2017.
 Diwani wa Kata ya Pugu, Boniventure Mphuru akipanda mti katika eneo la shule ya Msingi minazi mirefu Juni 5, 2017.
 Muanzilishi wa Mradi wa CLEAN WATER SANITATION AND HYGIENE ambaye pia ni Miss Ubungo 2014, Diana Joachimu Kato akipanda mti shuleni hapo.

MAELEZO TV: HALMASHAURI NCHINI ZAAGIZWA KUWATENGENEZEA WAZEE VITAMBULISHO KWA AJILI YA MATIBABU

UCHAMBUZI KIVUKO CHA MV KAZI: JPM aliahidi, anatekeleza

$
0
0
Na Benjamin Sawe.

Upo usemi wa wahenga usemao “mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni.” Hivi ndivyo ninavyoweza kusema kuhusiana na harakati za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kuhakikisha kuwa Sekta ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi inaimarika.

Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya kuteuliwa kuwa Rais, amekuwa Waziri katika Awamu mbili zilizopita. Anao uzoefu mkubwa wa utendaji kazi lakini pia katika kuongoza Wizara ambapo amewahi kuwa  Waziri wa Ujenzi na Miundombinu na Kilimo na Ufugaji. 
Kutokana na umuhimu wa Sekta ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi katika maendeleo ya Taifa, mara tu baada ya kuchaguliwa kuwa Rais, aliagiza ujenzi wa barabara ya kutoka Mwenge hadi Moroco ambayo ilikuwa ina msongamano mkubwa wa magari kuelekea katikati ya jiji.

Msongamano huo umekuwa ukiathiri malengo ya Wafanyakazi ambao walikuwa wakitumia muda mwingi wakiwa kwenye foleni na hivyo kupunguza muda wa kufanya kazi lakini pia uzalishaji na utoaji huduma za msingi kwa Taifa.

Aidha, Mheshimiwa Rais ameshiriki uwekaji wa jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa barabara za juu (fly over) katika makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela eneo la Tazara unaogharimu kiasi cha shilingi bilioni 100 za Kitanzania na pia ujenzi wa barabara za juu kwenye makutano ya barabara za Morogoro, Mandela na Sam Nujoma eneo la Ubungo Jijini Dar es Salaam
Hivi karibuni Serikali kupitia Waziri Mwenye dhamana ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amepokea Kivuko cha MV Kazi ambacho kimejengwa na Kampuni ya Kizalendo ya M/S Songoro Marine Transport Boatyard ya Mwanza.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia akutana na Mkemia Mkuu wa Serikali

$
0
0
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST),  Profesa Abdukarim Mruma (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Mkemia Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania Profesa Samwel Manyele wa pili kushoto aliyeambatana na timu yake kutoka ofisi ya Mkemia Mkuu, alipotembelewa ofisini kwake kwa lengo la kubadilishana mawazo ya utendaji kazi. Picha na Samwel Mtuwa - Dodoma.

BAM INTERNATIONAL WAKARABATI SHULE YA SEKONDARI BARABARA YA MWINYI DAR ES SALAAM

$
0
0

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Temeke, Eric Kilangwa (wa pili kulia) na Mkurungezi wa Miradi wa Kampuni ya Bam International, Wolfgang Marschick wakifurahia baada ya uzinduzi wa madarasa matano, ofisi ya walimu na eneo la makusanyiko baada ya kufanya ukarabati katika shule ya sekondari Barabara ya Mwinyi iliyopo Buza jijini Dar es Salaam Juni 6 2017. Pamoja nao ni Mwenyekiti wa shule hiyo, Sostenes Nyenyembe (kulia), Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Bam International Africa Noreen Mazalla (kushoto) na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Emmentrudice Chilewa.(Picha na Robert Okanda Blogspot).
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Emmentrudice Chilewa akiwatembeza wageni kujionea ukamilishwaji wa mradi wa ukarabati wa madarasa na ujenzi wa eneo la makusanyiko kabla ya kufanya uzinduzi.
Mkurungezi wa Miradi wa Kampuni ya Bam International, Wolfgang Marschick akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Barabara ya Mwinyi alipotembelea mojawapo ya madarasa matano, kampuni hiyo iliyoyakarabati eneo la Buza jijini Dar es Salaam Juni 6 2017. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Emmentrudice Chilewa.
Waalimu na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bam International wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari Barabara ya Mwinyi iliyopo Buza jijini Dar es Salaam wakati wa hafla hiyo.

Tanzania yashiriki Mkutano wa kujadili matumizi ya Bahari na rasilimali zake

$
0
0
Ujumbe wa Tanzania unaoongozwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Charles Tizeba ukiwa kwenye mkutano wa utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu Na. 14 (Sustainable Development Goals-SDGs14) maarufu kama Oceans Conference unaojadili matumizi endelevu ya bahari na rasilimali zilizomo baharini, unaoendelea Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekan. 
Waziri wa Kilimo, Nifugo na Uvuvi, Mhe. Charles Tizeba akiwasilisha hotuba kwa niaba ya Serikali ya Tanzania kwenye Mkutano wa Kimataifa wa kuweka mikakati ya utekelezaji wa SDG14 unaoendelea Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekan. Mkutano huo ni maalum kwa ajili ya kujadili kuhusu matumizi endelevu ya bahari na rasilimali zilizomo baharini kama sehemu ya utekelezaji wa lengo la 14 la malengo ya maendeleo endelevu.

SIKU YA MTOTO WA AFRIKA 2017: WAZAZI WALEZI NA WADAU MBALIMBALI WAHAMASISHWA KUSHIRIKI KATIKA SIKU HIYO KATIKA MIKOA YAO

IGP Sirro atangaza msako mkali Kibiti na Rufiji

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro juni 6 alifanya mazungumzo na wazee pamoja na viongozi wa dini wilayani Kibiti mkoani Pwani ili kubaini wahalifu wanaotekeleza mauaji ya watu wilayani humo na kusema vyovyote itakavyokuwa lazima watawarudisha kwenye msitari.

IGP Sirro alisema kupitia mazungumzo hayo tayari amepata taarifa za wahalifu hao ingawa ni mapema kuziweka wazi ila amewahakikishia wananchi kuwa wahalifu wao ni lazima watapatikana.

“Kubwa ni kwamba wazee wetu wa Kibiti wametueleza taarifa nyingi sana na mnavyojua hawa wahalifu wanaishi ndani ya Kibiti, ndani ya Ikwiriri, kwa hiyo wazee wetu wamejaribu kutueleza ni wapi tunaweza kuwapata na chanzo cha mambo yote haya,” alisema IGP Sirro na kuongeza kuwa

“Kwa hiyo kimsingi mambo mengine mengi ni ya kipelelezi ambayo siwezi kuyasema kwa sasa, lakini kikubwa wametupa dira, muelekeo kwa maana kwamba wale ndugu zetu au maadui zetu kwa lugha nyepesi tumepata njia nzuri ya kudeal nao. Kwa hiyo nitume salamu kwao kwamba waendelee kukimbia lakini njia ya muongo ni fupi na mwisho wa siku tutawarudisha kwenye mstari"

SPIKA NDUGAI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA UONGOZI NA KAMATI YA BAJETI LEO OFISINI KWAKE MJINI DODOMA.

$
0
0
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akiongoza kikao cha kamati ya Uongozi na kamati ya Bajeti leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. kulia kwake ni Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa na Kushoto kwake ni Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah na anaefuata ni Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson

(PICHA NA OFISI YA BUNGE) 

RAIS DK.SHEIN AJUMUIKA NA WAISLAMU KUMZIKA PROF.ISHAU

$
0
0


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alijumuika na Waislamu,Viongozi mbali mbali na Wananchi katika kumswalia Marehemu Mzee Prof.Ishau Abdalla Khamis katika Msikiti wa Ijumaa Donge leo,Marehemu aliwahi kushika nyazifa mbali mbali katika Serikalia ya Mapinduzi Zanzibar na Chama cha Mapinduzi.
1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja,(wa pili mkushoto) pamoja na Viongozi wengine wakielekea katika kaburi wakati wa mazishi ya  Marehemu Mzee Prof.Ishau Abdalla Khamis yaliyofanyika leo kijiji cha Donge,Wilaya ya Kaskazini BUnguja.
2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto waliosimama) alijumuika na Waislamu,Viongozi mbali mbali na Wananchi katika mazishi ya Marehemu Mzee Prof.Ishau Abdalla Khamis katika kijiji cha Donge leo
3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein  akitia udongo katika kaburi la Marehemu Mzee Prof.Ishau Abdalla Khamis aliyezikwa leo katika kijiji cha  Donge,Willaya ya Kaskazini B Unguja,[Picha na Ikulu.]07/06/2017

MASAUNI, IGP SIRRO WAWATAKA WANANCHI WILAYA YA KIBITI,RUFIJI KUFUNGUKA DHIDI YA VITENDO VYA UHALIFU NAWAHALIFU

$
0
0


unnamed
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Bungu, wilayani Kibiti Mkoa wa Pwani, kuhusiana na masuala mbalimbali ya kupambana na wahalifu wilayani humo. Masauni ambaye aliambatana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro aliwataka wananchi hao kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kuwasambaratisha wahalifu hao
1
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akipokea maoni ya wananchi wa Kijiji cha Jaribu Mpakani wilayani Kibiti, Mkoa wa Pwani wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi wilayani humo. IGP ambaye aliambatana na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) walizungumza na wazee, viongozi wa dini na watu maarufu kutoka Wilaya Rufiji na Kibiti kuweka mikakati ya kuimarisha zaidi ulinzi na usalama wa raia na mali zao.
2
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na wazee, viongozi wa dini na watu maarufu (hawapo pichani) kutoka Wilaya Rufiji na Kibiti kuhusu masuala mbalimbali na  kuweka mikakati ya kuimarisha zaidi ulinzi na usalama wa raia na mali zao. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, na kushoto ni Mkuu wa Wilaya Kibiti, Gulam Hussein. 
3
Wazee, viongozi wa dini na wa vyama vya siasa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati alipokuwa akizungumza na wananchi hao katika Ukumbi wa Mikutano wa Shule ya Sekondari ya Kibiti, mkoani Pwani. Masauni na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro pamoja na wananchi hao waliweka mikakati ya kuimarisha zaidi ulinzi na usalama wa raia na mali zao kupitia maoni ya wajumbe waliohudhuria kikao hicho. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MATUKIO KATIKA PICHA: YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 43, MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO JUNI 07, 2017.

$
0
0
 Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Najma Giga akiongoza kikao cha 43 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 07, 2017.
 Naibu Waziri Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angeline Mabula akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 41 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 5, 2017.
 Naibu Waziri Wizara ya Fedha na Mipango Mhe.Dk Ashatu Kijaji akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 43 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 7, 2017.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini Dk Medard Kalemani akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 43 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 7, 2017.
  Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Prof Makame Mbarawa akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 43 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 7, 2017.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Article 5

Mfumo mpya wa uhasibu kupunguza hati zenye mashaka katika halmashauri

$
0
0

Na Mathew Kwembe,Mtwara

Serikali imesema kuanza kutumika kwa mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ifikapo julai mosi, 2017, kutapunguza changamoto za halmashauri kupata hati zenye mashaka pindi zinapokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Mfumo huo utaiwezesha Serikali kupeleka rasilimali fedha moja kwa moja kwenye vituo vya afya kwa ngazi za halmashauri. Vituo vya kutolea huduma ambavyo vitapokea fedha hizo vinajumuisha Zahanati, Vituo vya Afya, na Hospitali za Wilaya. Zoezi hilo litaenda sambamba na inavyotekelezwa kwenye sekta ya elimu, Serikali za Vijiji na Ofisi za Kata.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Bwana Alfred Luanda ameyasema hayo jana mjini Mtwara wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wakufunzi wa mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma kwa wahasibu kutoka halmashauri za mikoa sita ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Tanga, Pwani na Dar es salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Tehama na mawasiliano kutoka Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) bwana Desderi Wengaa akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wakufunzi wa mfumo wa Uhasibu na utoaji taarifa za fedha.Baadhi ya washiriki wa Mafunzo ya wakufunzi wa mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kutoka mikoa ya Ruvuma, Lindi, Mtwara, Pwani, Tanga na Dar es salaam wakishiriki mafunzo hayo yaliyofunguliwa jana 
Mtoa mada wa mafunzo ya wakufunzi wa mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa njia ya kielektroniki kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI bwana Hamis Zikatimu akitoa mada wakati wa mafunzo hayo yanayofanyika mkoani Mtwara.
Mgeni rasmi Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara bwana Elias Nyamusami.(aliyeketi katikati akiwa katika picha ya pamoja na washiriki kutoka mkoa wa Tanga. Aliyeketi kushoto kwa Mgeni rasmi ni Mkuu wa Kitengo cha Tehama na mawasiliano kutoka Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) bwana Desderi Wengaa na kulia kwa Mgeni rasmi ni bwana Lucas Mrema ambaye ni mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI

Mgeni rasmi Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara bwana Elias Nyamusami.(aliyeketi katikati akiwa katika picha ya pamoja na washiriki kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI na Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3). 


WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZINDUA SHUGHULI YA USAMBAZAJI VIFAA KUFUNDISHIA SAYANSI

$
0
0
Waziri  Mkuu  Kassim  Majaliwa  akiangalia Mtoto wa Darasa la saba anayesoma shule ya Uhuru  Mchanganyiko Mariana  Alex  Mwenye  ulemavu  wa macho, anavyoweza kuandika  kwa kutumia  mashine  maalumu  ya kuandika, June 6 2017 Waziri  Mkuu  alikabidhi  vifaa  vya Kujifunzia   katika shule mbalimbali hapa Nchini Shughuli hiyo imefanyika Jijini  Dar es salaam
Waziri  Mkuu  Kassim  Majaliwa  akijaribu  kuandika  kwa kutumia  kifaa maalumu  cha kujifunzia  kuandika  watoto wenye ulemavu  wa Macho 6 June2017, Kulia kwa Waziri Mkuu ni Waziri wa Elimu na Sayansi  Profesa  Joyce Ndalichako, Waziri  Mkuu  alikabidhi  vifaa  vya Kujifunzia   katika shule mbalimbali hapa Nchini Shughuli hiyo imefanyika  Jijini  Dar es salaam
 Waziri Mkuu  Kassim  Majaliwa  akisalimiana na Ofisa wa Banki ya Dunia anayeshughulikia  Elimu  nchini  Tanzania  Bibi  Cornelia  Jesse, katikati ni Ofisa  wa  Ubalozi  Swiden  Nchini Tanzania  anayeshughulikia Elimu Bibi Helena  Reutersward , maofisa hao walishiriki katika Uzinduzi  wa Usambaziji  vifaa  vya  kufundishia  Masomo ya  Sayansi  Shughuli hiyo ilifanyika 6 June 2017   katika  Viwanja  vya  Jeshi  Lugalo  Dar es salaam. Picha na Ofisi  ya  Waziri  Mkuu

SAFARI YA MWISHO YA BALOZI ABDULCISCO OMAR MTIRO

$
0
0
Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Balozi Abdulcisco Omar Mtiro almarufu kama CISCO likiwa nyumbani kwake Mikocheki B, Jijini Dar es salaam tayari kwa ibada ya kuuaga mwili kabla ya kwenda kuuhifadhi kwenye Nyumba yake ya Milele, katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar mchana huu.

Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir akizungumza machache kabla ya kuuswalia Mwili wa Marehemu Balozi Abdulcisco Omar Mtiro almarufu kama CISCO nyumbani kwake Mikocheki B, Jijini Dar es salaam.

Rais Mstaafu, Alhaj Ally Hassan Mwinyi akijumuika na viongizi wastaafu wa Serikali katika Msiba wa Marehemu Balozi Abdulcisco Omar Mtiro almarufu kama CISCO nyumbani kwake Mikocheki B, Jijini Dar es salaam.


Kisomo cha kumuombea Marehemu Balozi Abdulcisco Omar Mtiro almarufu kama CISCO kikiendelea nyumbani kwake Mikocheki B, Jijini Dar es salaam.


Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images