Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1731 | 1732 | (Page 1733) | 1734 | 1735 | .... | 3286 | newer

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa  Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania { Tanzania Media Foundation – TMF } Bwana Ernest Sungura  amesema hadhi ya Sekta ya Habari Nchini itaheshimika na kuaminika zaidi endapo wanahabari wenyewe watajiwekea malengo ya kufanya kazi kwa agenda katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

  Alisema mfumo wa agenda kwa Wanahabari ndio njia pekee itakayosaidia  kuamsha ari sambamba na kuibua changamoto zinazokwaza Jamii na kuzipa nguvu za uwajibikaji Taasisi za Umma na hata zile binafsi katika kuwahudumia kwa umakini Wananchi.

  Nd. Ernest Sungura  Alisema hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye Jengo la Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar akiuongoza Ujumbe wa Viongozi Wanne wa TMF uliokuwepo Zanzibar  kwa ziara maalum ya kukagua  Maandalizi na Mikakati  ya mradi wa kuwapatia Mafunzo Wanahabari wa Zanzibar.

  Alisema kupitia Mfuko wa Vyombo vya Habari zipo agenda zilizowahi kuibuliwa na Wanahabari wa Vyombo tofauti Nchini akizitolea mfano  vita dhidi ya Dawa  za Kulevya, Udhalilishaji wa Kijinsia na ubalozi wa Usalama barabarani ambazo zimesaidia kuleta faraja kwa Jamii na kuzipunguzia matumizi mabovu yasiyo na msingi Serikali zote mbili.

  Alieleza kwamba yapo mambo mengi na mazuri ya kujivunia  kutokana na kuanzishwa kwa mfumo huo wa agenda  jambo ambalo limeziletea sifa Taasisi za Habari kwa Taifa na Wananchi jambo ambalo lilisaidia kuibua changamoto zinazokwaza Serikali na Jamii kwa ujumla.

  Bwana Sungura alimueleza Balozi Seif  kwamba katika kuwajengea uwezo uliobobea Waandishi wa Habari katika utekelezaji wa kazi zao.

  Alisema kuwa tangu kuanzishwa kwake, TMF tayari imeshatoa ruzuku kwa   Wanahabari  binafsi zaidi ya 600 na taasisi za  kutoka kihabari 120 nchini.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd  akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa  Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania { Tanzania Media Foundation – TMF } Bwana Ernest Sungura alipokuwa akizungumza nae jambo ofisini kwake.  0 0


  0 0

  Frank Mvungi- Maelezo

  Serikali imetumia shilingi bilioni 16.9 kununua vifaa vya maabara na vile vya wanafunzi wenye mahitaji maalum vitakavyonufaisha shule za sekondari 1696 ambapo shule 1625 ni za Kata na 71 ni kongwe ambazo kwa sasa zipo katika ukarabati.

  Akihutubia wakati wa hafla ya kuzindua  mpango wa  kusambaza vifaa vya maabara na vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalum leo Jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ambaye alikuwa mgeni rasmi, amesema dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kuwa inaboresha sekta ya elimu  ili azma ya ujenzi wa Tanzania ya Viwanda itimie kwa kuwa Taifa litaweza kuzalisha wanasayansi kulingana na mahitaji.

  “Tunatoa vifaa hivi kwa awamu ya kwanza kwa shule zilizokamilisha ujenzi wa maabara, hivyo ni matumaini yangu kuwa wale ambao hawajakamilisha watafanya hivyo ili awamu ijayo nao wapate vifaa hivi.” Alisisistiza Majaliwa.

  Aliongeza kuwa dhamira ya serikali ni kuhakikisha zaidi ya shule 4,000 nchini zinakuwa na vifaa vya maabara, walimu, vifaa vya kujifunzia na kufundishia na mazingira rafiki ili kuwawezesha wanafunzi kupata elimu bora itakayowasaidia kushiriki katika ujenzi wa Taifa.

  Pia Waziri Mkuu ameonya kuwa Serikali itachukua hatua kali dhidi ya mtu yoyote atakaye sababisha mwanafunzi wa kike kupata ujauzito na kushindwa kuendelea na masomo ambapo atakabiliwa na adhabu ya kwenda jela miaka thelathini.

  “Awe baba au mama au mtu yoyote ambaye itathibitika kuwa amemsababishia ujauzito mwanafunzi, adahabu yake ni kifungo cha miaka thelathini jela.” Alisisitiza Majaliwa.
   Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa (mwenye tai nyekundu) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa zoezi la usambazaji wa vifaa vya maabara na vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalum mapema hii leo katika viwanja vya hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.
    Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa (kulia) akikabidhi moja ya kifaa cha kufundishia masomo ya sayansi kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Juhudi wakati wa uzinduzi wa zoezi la usambazaji wa vifaa vya maabara na vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalum  mapema hii leo katika viwanja vya hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.
   Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya walimu na wanafunzi wa shule za sekondari za mkoa wa Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa zoezi la  usambazaji wa vifaa vya maabara na vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalum  mapema hii leo katika viwanja vya hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.

   Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa (mwenye tai nyekundu) akipata maelekezo toka kwa moja ya mwalimu wa masomo ya sayansi wakati wa uzinduzi wa zoezi la usambazaji wa vifaa vya maabara na vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalum  mapema hii leo katika viwanja vya hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakimsikiliza Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa zoezi la usambazaji wa vifaa vya maabara na vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalum  mapema hii leo katika viwanja vya hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Wafanyakazi wa Manispaa ya Ilala pamoja na wafanyakazi wa Green Waste Pro Ltd wakiendelea kufanya usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi kata ya Kivukoni eneo la Aga Khan jijini Dar ikiwa ni wiki ya Mazingira. Mwenye shati nyeupe ni  Meneja Msaidizi wa kampuni Green WastePro ltd, Erick Mark.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akisitiza jambo kwa wadau walioshiriki zoezi la usafi katika fukwe ya bahari ya Hindi eneo la Aga Khan na kuwaomba waendelee na kufanya usafi na hata kuwahamasisha watu wengine kuwa mabalozi wa mazingira ili kufikia malengo waliyojiwekea katika manispaa ya Ilala.
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Mstahiki Omary Kumbilamoto akizungumza jambo kwa wadau mbalimbali waliokuja kujumuika katika zoezi la usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi eneo la Agha Khan katika wiki ya mazingira.

  Meneja wa uendeshaji wa kampuni ya Green Waste ProLtd, Abdallah Mbena akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushiriki wa kampuni hiyo katika zoezi la kufanya usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi kata ya Kivukoni eneo la Aga Khan jijini Dar ikiwa ni wiki ya Mazingira.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Green WastePro Ltd  mara baada ya kumaliza kufanya usafi kwenye fukwe ya Bahari ya Hindi eneo la Aga Khan kata ya Kivukoni ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Mazingira.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0  TAA 2
  Na Jonas Kamaleki-MAELEZO.

  Zaidi ya vijana wapatao  1230  wametoa siri nzito kwa  Maaskofu na Mashekhe  kutoka katika Kamati ya Kitaifa ya Maadili , Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu ya Dini  Nchini  kufichua mtandao  haramu  wa watu  wanaoendesha mauaji na uhalifu mwingine kwenye   mikoa  13, nchini kama njia muhimu ya kumpongeza IGP mpya, Saimoni Sirro.

   Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Askofu William Mwamalanga, siri hiyo imetolewa  jana  na vijana hao katika   siku ya  tatu  mkutano wa kujenga maadili kwa vijana unao fanyika Mbagala, jijini Dar es Salaam na kuwashirikisha   vijana  wa madhehebu mbalimbali ya dini  kutoka katika  mikoa ya Pwani, Tanga, Lindi,  Morogoro,Dar es Salaam  ambapo wameyataja maeneo ya Mkuranga, Rufiji  Kigamboni, Kibiti, Msata, Tanga mjini, Pemba na Unguja kuwa maeneo hatari yanayowajengea vijana imani za  kigaidi.

   Aidha, Askofu Mwamalanga alisema kuwa vijana 147  wa kiislamu wanaohudhuria mkutano huo  wamewataja  baadhi ya watu  ambao ni   hatari  na wamekuwa wakieneza elimu ya mauaji  kwenye  misikiti mbali mbali nchini kwa kuiita Serikali ya Awamu ya Tano jina la katili na kwamba elimu hiyo imesambazwa kwa kasi  katika mikoa ya  Kagera, Tanga, Mwanza, Arusha, Pemba, Unguja, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Morogoro, Iringa, Singida, Dodoma, Pwani na Kigoma huku vikosi vya vijana vikiandaliwa kufanya mauaji  mara baada ya mufungo mtukufu wa Ramadhani kama yale ambayo yamekuwa yakifanywa  Mukuranga, Kibiti  na Rufiji. 

  Vijana hao wanamuomba  IGP  Sirro kuwachukulia hatua kali maafisa wa jeshi hilo ambao wanatumia jeshi kupandikiza Umngiki, na  kwamba wana imani na IGP Sirro amabaye kwa mujibu wa hao vijana hatamwangusha Rais  Magufuli na watanzania kwa ujumla.

  Akifunga  Mkutano huo  Askofu Mwamalanga  amemtaja IGP  Sirro kama polisi mahiri wa maadili na jemadali  mweledi wa mapambano hivyo amewataka  vijana kote nchini kumuunga mkono kwa kuwafichua polisi wote wanaoenzi uhalifu. “Tusipofanya hivyo tutakuwa  kama  pipa zuri  tunalo jaza maji wakati tukijua chini limetoboka”,alisema Askofu Mwamalanga na kuongeza kuwa raia wema ni asilimia 99.9  wahalifu ni 0.1   hii ina maana kuwa ukiondoa polisi wahalifu  ndani ya jeshi hilo wahalifu ni wachache mno  mitaani  watayeyuka wenyewe. 


  0 0

  Wahasibu zaidi ya 130 kutoka halmashauri za wilaya za mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kati wamepatiwa mafunzo ya Mfumo wa Kielekroniki kuhusu Usimamizi wa fedha ngazi za msingi zikiwemo zahanati,vituo vya afya,hospitali na shule za msingi na sekondari.

  Mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and Reporting System – FFARS) kupitia mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ‘ Public Sector Systems Strengthening – PS3’ unaotarajiwa kuanza kutumika Julai 1,2017 katika halmashauri mbalimbali nchini.

  Wahasibu hao wanashiriki katika mafunzo yanayofanyika katika ukumbi wa Vigimark Hotel Mjini Shinyanga ambayo yamekutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi kutoka PS3,TAMISEMI,Wizara ya afya,wizara ya elimu.

  Mwezeshaji wa Mafunzo hayo, Elizeus Rwezaula ambaye ni Mshauri wa Masuala ya Usimamizi wa Fedha za Umma kutoka Mradi wa HPSS Dodoma,alisema mfumo wa kutumia njia za kielektroniki (kompyuta) katika kuingiza taarifa za kifedha za vituo vya kutolea huduma unasaidia kurahisisha kazi.

  “Katika Afrika Mashariki,Tanzania ndiyo nchi pekee itakayoanza kutumia mfumo huu wa kisasa wa kielektroniki katika uingizaji taarifa za fedha katika ngazi za msingi za kutolea huduma,na umetengezwa na vijana wa hapa nchini ili kuhakikisha kuwa mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma (FFARS) unafanikiwa”,alieleza Rwezaula.

  Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi TAMISEMI, Elisa Rwamiago akizungumza wakati wa mafunzo kuhusu mfumo huo kupitia mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ‘ Public Sector Systems Strengthening – PS3’ unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID)

  Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi TAMISEMI, Elisa Rwamiago akielezea kuhusu mfumo wa kielektroniki katika ujazaji taarifa za fedha katika vituo vya kutolea huduma.

  Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi TAMISEMI, Elisa Rwamiago akizungumza ukumbini

  Mwezeshaji wa Mafunzo ya FFARS ,Elizeus Rwezaula ambaye ni Mshauri wa Masuala ya Usimamizi wa Fedha za Umma kutoka Mradi wa HPSS Dodoma,akitoa mada kuhusu njia/mfumo wa kielektroki katika ujazaji taarifa za fedha katika vituo vya kutolea huduma   0 0


  Na matukiodaimaBlog

  SERIKALI Imewataka wananchi wanaolima kilimo kwenye maeneo oevu maarufu kama vinyungu kutafuta shughuli nyingine ya kufanya nje ya kilimo hicho kulinda mto Ruaha mkuu kukauka.

  Akitoa salam za mkoa wa Iringa wakati wa sherehe ya tuzo ya TANAPA ya uhifadhi mazingira na kilele cha siku ya mazingira Duniani leo maadhimisho yaliyofanyika kwa kijiji cha Madabaga wilaya ya Mbarali mkoa wa Mbeya Jana mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema iwapo ulimaji wa vinyungu utafumbiwa macho mto Ruaha mkuu utaendelea kukauka.

  Alisema kuwa chanzo kikubwa cha uharibifu wa ikolojia ya mto Ruaha mkuu pamoja na hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

  Kwani alisema uhifadhi wa hifadhi ya Ruaha ni pamoja na uhifadhi wa mto Ruaha mkuu hivyo mikoa ya Iringa,Njombe na Mbeya wana wajibu wa kulinda mto Ruaha mkuu na kuchukua hatua kwa wote wanaolima kwenye vyanzo vya maji.

  Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza kulia na mkuu wa wilaya ya Kilolo   Asia Abdalah wakimpongeza mwakilishi wa kikundi cha familia ya Festo Mhanga wa Kilolo kwa kushinda tuzo ya Mazingira ya Tanapa na kuzawadiwa shilingi milioni jana wakati wa kilele cha siku ya Mazingira na utoaji wa Tuzo za TANAPA kwa wananchi wa mikoa ya Iringa , Njombe na Mbeya

  Mgeni rasmi katika kilele cha siku ya mazingira duniani jana Amos Makala mkuu wa mkoa wa Mbeya akiteta jambo na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza na meneja ujirani mwema wa Tanapa Ahmed Mbugi kushoto .

  Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akitoa salam siku ya Mazingira Duniani mkoani Mbeya .

  Kikundi cha skauti cha elimisha jamii wilaya ya Mufindi wakikabidhiwa hundi ya shilingi milioni 1 toka Tanapa .

  0 0

  Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe wameadhimisha Siku ya Mazingira Duniani kwa kupanda miti kwenye eneo la Gereza la Kanegere.
  Akiongea baada ya kupanda miti Kaimu Mkurugenzi  Mtendaji (W), Bi Furaha Chiwile amewataka wananchi  na watumishi  kwa ujumla kupanda miti kwa wingi na kuitunza na waepuke kukata miti ovyo  kwani kwa kufanya hivyo wanahatarisha mazingira na  vyanzo vya maji.

  Jumla ya miti 200 ilipandwa lengo likiwa ni kupanda miche 2500 kwenye eneo hilo la magereza. Miche hiyo inayofadhiliwa na TASAF awamu ya tatu inapandwa kwenye Taasisi za serikali  wilayani  Mbogwe.

  Wakati huo huo Afisa Mazingira wa Wilaya Charles  Karibu Tuyi alisema “ Kauli Mbiu ya Siku ya Mazingira    kitaifa ni Hifadhi Mazingira Mhimili kwa Tanzania ya Viwanda”. Amewashukuru watu wote waliojitokeza kupanda miti na amewaomba waonyeshe ushirikiano wa kuitunza  miti hiyo kwani itasaidia sana kutunza vyanzo vya maji.

  Pamoja na  hayo ,Afisa  Mazingira (W)  alikabidhi jumla ya miche 920 kwa mwakilishi wa mkuu wa Gereza  Sgt. Kuyi  Kalulumila ambaye ameahidi kuitunza miche hiyo na amemshukuru Mkurugenzi kwa kulikumbuka gereza hilo kwani lina eneo kubwa na linauwezo wa kutunza miti hiyo.
   Afisa Mazingira (W) Charles Karibu Tuyi akipanda mti kwenye zoezi la upandaji miti ambalo kiwilaya lilifanyikia kwnye gereza la Kanegere wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani 
   Afisa Mazingira(W) Charles Karibu Tuyi akimkabidhi Kaimu mkuu wa Gereza Kuyi Kalulumila miche ya miti inayotakiwa kupandwa kwenye Eneo la Gereza wakti wa Siku ya Mazingira Duniani.
  Baadhi ya Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya wilaya ya Mbogwe Wakiwa Wanapanda Miti na kuimwagilia.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameuagiza uongozi wa wilaya ya Serengeti na wa mkoa Mara kukamilisha haraka awamu ya kwanza ya ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo ili kuondoa adha ya wananchi kusafiri kwenda mikoa ya jirani ya Arusha na Mwanza kwenda kupata huduma afya.

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa agizo leo 6-June-2017 kwenye mkutano wa hadhara mjini Mugumu wilayani Serengeti mkoani Mara mara baada ya kutembelea ujenzi wa hospitali hiyo ya wilaya  na kuweka jiwe la msingi.

  Makamu wa Rais amesema kutokana na wilaya ya Serengeti kupata wegeni wengi kutoka nje ya nchi ambao wanaenda kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti  hivyo ni muhimu kwa viongozi wa wilaya na mkoa kwa ushirikiano na wadau wa maendeleo kukamilisha ujenzi huo haraka ili wananchi waweze kupata huduma za afya za uhakika katika wilaya yao.

  Makamu wa Rais amesema kukamilika kwa ujenzi huo wa awamu ya kwanza kutaondoa taabu kubwa wanayopata wananchi wa wilaya ya Serengeti katika kupata huduma ya afya karibu na maeneo yao.

  Katika kuunga mkono jitihada hizo za ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Serengeti, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ameahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni Tano na amewaahidi wananchi wa wilaya ya Serengeti kuwa atakikisha fedha kutoka Serikalini ambazo zinatakiwa kupelekwa wilayani humo zinapelekwa haraka ili kukamilisha ujenzi huo.

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan pia amewataka wananchi kote nchini kuunga mkono jitihada za Serikali za kupambana na rushwa na ufisadi ili kuhakikisha miradi inayotekelezwa inakuwa na manufaa kwa wananchi wote.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mbuzi Mugumu Serengeti ikiwa sehemu ya kukamilisha ziara yake ambapo alitumia fursa hiyo kuwashukuru wakazi wa Serengeti na kuwapongeza kwa kutunza mazingira. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa  hospitali ya wilaya ya Serengeti inayojengwa makao makuu ya wilaya Mugumu.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia mfano wa majengo ya hospitali ya wilaya ya Serengeti inayojengwa makao makuu ya wilaya Mugumu kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt. Kisaka.


  0 0


  0 0


  Mdau Emmanuela Mtatifikolo Kaganda akifurahia baada ya kulamba nondozzz ya Afya ya Umma (Masters of Public Health)  toka  City University of New York - Graduate school of Public Health kwenye sherehe zilizofanyika katika ukumbi maarufu duniani wa  Apollo  Theater kitongoji cha  Harlem 125th West, jijini New York mapema mwezi huu.

  Mdau Emmanuela  Kaganda akifurahia  pamoja na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Mhe. Balozi Modest J. Mero  na mkewe 
  Emmanuela Kaganda akiwa na marafiki zake kwenye sherehe hiyo.
  Tabasamu mubashara la ushindi baada ya kula nondozzzzz    kwa taswira zaidi jitiririshe hapa chini kiroho saf
  Emmanuela Kaganda akiwa kwenye viti vyekundu ndani ya ukumbi maarufu sana New York City na Marekani Apollo Theater, hapa ndipo sherehe zilifanyika. 

  Emmanuela Kaganda akiwa  kwenye kisiki cha 'Ngekewa' ndani ya ukumbi wa Apollo.  Kisiki hiki kina sifa ya kukupatia bahati kwenye maisha yako pale unapokigusa ukiwa na maombi ya kutaka kufanikiwa kwa imani ya unachokifanya au kukitarajia katika ndoto zako.

  0 0

  CHAMA CHA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA TANZANIA (TUMA) TANZANIA URBAN MUSIC ASSOCIATION Inakuletea Kongamano la Wasanii katika Jiji la Mbeya Watoa mada ni TUMA, BASATA, COSOTA, TRA, PCCB & NHIF.. Kuhusu : Usajili, Haki miliki, Ulipaji kodi, Maadili, Rushwa na Bima. JUMAMOSI hii, Tarehe 10/06/2017 Mahali: TUMANYENE SOCIAL HALL- Nzovwe Kuanzia saa nne asubuhi hadi saa nane na nusu mchana. HAKUNA KIINGILIO….wote mnakaribishwa #msaniijisajiliTUMA @bratonmtz


  0 0

  Na Mary Gwera, Mahakama, Iringa

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa imefanikiwa kuondosha Mashauri/kesi kwa zaidi ya asilimia tisini (90) na kuifanya Mahakama hiyo kuendana na azma ya Mahakama ya Tanzania ya kutoa haki kwa wakati ili kuondokana na mlundikano wa mashauri katika Mahakama zake nchini.

  Akizungumza ofisini kwake katika mahojiano maalum na Mwandishi wa taarifa hii aliyepo Kanda ya Iringa, mapema Juni 6, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Hakimu Mkazi-Iringa, Mhe. David Ngunyale alisema hali ya uondoshaji wa Mashauri katika Mkoa wa Iringa inaridhisha na kufafanua kuwa kwa upande wa Mahakama za Mwanzo ambazo jumla yake zipo 21, hakuna kesi inayozidi miezi sita (6) katika Mahakama hizo.

  Akiongelea katika ngazi ya Mahakama za Wilaya, Mhe. Ngunyale alisema kuwa Mahakama hizo zina jumla ya kesi 12 za mlundikano (ambazo zimezidi umri ya miezi 12 Mahakamani), huku kesi 8 zikiwa ni za Jinai na nne (4) zikiwa ni kesi za Madai.

   Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Hakimu Mkazi-Iringa, Mhe. David Ngunyale

   Mtendaji wa Mahakama-Kanda ya Iringa, Bw. Elvin Mwakajinga

   Afisa Tawala, Mahakama ya Hakimu Mkazi/Mkoa-Iringa, Bi. Dorice Kisanga akionesha maboksi ambapo mafaili ya kesi zilizomalizika yalipohifadhiwa, kwa urahisi wa rejea ya kumbukumbu za kesi za nyuma.
  Muonekano wa jengo la Mahakama Kuu-Kanda ya Iringa, katika uwanja huu, yapo pia majengo ya Mahakama ya Wilaya na Mahakama ya Hakimu Mkazi-Iringa. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

  0 0
 • 06/06/17--19:05: Article 8


 • 0 0
  0 0

  Mheshimiwa Freeman Mbowe(MB), Mwenyekiti wa Taifa, CHADEMA: 

  NIMEPOKEA KWA MASIKITIKO NA HUZUNI KUBWA TAARIFA ZA KIFO CHA MZEE WETU MHESHIMIWA PHILEMON NDESAMBURO. NILIPATA BAHATI KUFANYA KAZI NA MZEE NDESAMBURO TUKIWA WABUNGE WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. 
  BINAFSI NILIFAIDIKA SANA NA MAWAZO, HEKIMA, FIKRA, NA USHAURI WAKE KATIKA MASUALA MBALI MBALI YA KIBUNGE NA KITAIFA BILA KUJALI KWAMBA TULIKUWA VYAMA TOFAUTI.
  PANDE ZOTE ZA BUNGE ZILIMTAMBUA NA KUMHESHIMU KWA UTULIVU WAKE NA HEKIMA KUBWA KATIKA KUWASILISHA HOJA ZAKE. 


  KWA SABABU HIZO HAKIKA AMESAIDIA KATIKA KUJENGA NA KUIMARISHA DEMOKRASIA NCHINI. TAFADHALI TUFIKISHIE SALAAM ZANGU NA FAMILIA YANGU KWA FAMILIA YA MZEE NDESAMBURO NA WANA CHADEMA KWA KUMPOTEZA MUASISI NA MHIMILI WA CHAMA.
   KWA MWENYEZI MUNGU TULITOKA NA HAKIKA SOTE TUTARUDI KWAKE. MWENYEZI MUNGU AIREHEMU ROHO YA MAREHEMU NDESAMBURO. AMEEN.

  Mark Mwandosya

  0 0

   Mkuu wa kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi wa LAPF Bw. Emmanuel Mayage akichangia hoja katika moja ya mijadala inayoendelea kwenye  Kongamano la Manunuzi la Mwaka, 2017 linaloendeshwa na PPRA mjini Arusha kuanzia Jumatatu hadi Jumamosi wiki hii.
   Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Dkt. Laurent Shirima akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo.
   Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya PPRA Balozi Dkt. Matern Lumbanga akitoa hotuba ya ufunguzi wa Kongamano hilo.

  Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada zilizokuwa zinawasilishwa kwenye Kongamano hilo.
  Picha ya pamoja ya  washiriki wa Kongamano hilo.

  0 0


  0 0
  0 0

  Leo tarehe 07.06.2017, Mke wangu mpendwa Mwashabani A. LIGANJA umetimiza miaka kumi (10) tangu utwaliwe na Mola wetu. Mimi mumeo George MAPANGO pamoja na watoto wetu Mariam (Chuma), Eva (Hawa), Jackson (Kibabu), Patrick Mapango (Saidi), Rose na Richard. Kaka zako, Dada zako, wadogo zako na Wakwe zako D. Sakawa, Mama Janeth (Patrick) pamoja na Wajukuu zako Precious (Mwashaban), Pricilla(Gloria), Jasmine(Mwashaban), Prosper-John, Maria (IA), Winnie Stella, ndugu, jamaa na marafiki daima tunakukumbuka kwa ucheshi, upole, uvumilivu, utu wako, busara na hekima zako.
              Tutazidi kukuombea Roho yako ipumzike kwa Amani. AMINA

  KISOMO KITAFANYIKA LEO NYUMBANI OCEAN ROAD FLATS BLOCK A (CHIMARA ROAD) SAA KUMI JIONI (10.00) IKIFUATIWA NA FUTARI. 
  KARIBUNI TUJUMUIKE PAMOJA KATIKA DUA HILI MUHIMU.


older | 1 | .... | 1731 | 1732 | (Page 1733) | 1734 | 1735 | .... | 3286 | newer