Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1730 | 1731 | (Page 1732) | 1733 | 1734 | .... | 3272 | newer

  0 0


  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akipokea kadia kutoka kwa Niniani Bakhari, aliyekuwa Kada machachari wa Chadema, ambaye alitangaza kuhamia CCM wakati wa mkutano wa ndani uliofayika leo katika mji mdogo wa Ngara mkoani Kagera
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akimpongeza Ninian kwa uamuzi wake wa kurejea CCM
  Baadhi washiriki wa kikao wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Ngara, Mabalozi na viongozi kutoka Jumuia zote za CCM wakimpongeza Ninian kwa furaha baada ya kukabidhi kadi yake ya Chadema kwa Bulembo wakati wa kikao hicho.
  Wengine waliamua kumkabidhi Ahaj Bulembo hadi bendera ya Chadema baada ya kulifunga tawi lao
  Baadhi ya kadi za Chadema zilizorejeshwa kwa Alhaj Bulembo
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo (kushoto) akishiriki wakati wachama wapya 71waliohamia CCM wakitokea Chadema, walipokuwa wakila kiapocha Mwana CCM, baada ya kukabidhiwa kadi za Chama kwenye kikao hicho,leo.


  0 0

  Na Tiganya Vincent-RS-Tabora

  Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amewataka Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi na wakuu wa Idara za halmashauri zote za mkoa huo kutoa elimu ya usafi wa mazingira pamoja na matumizi sahihi ya vyandarua vyenye viuatilifu vya muda mrefu ili kukabiliana na ugonjwa wa malaria.

  Bw. Mwanri alitoa wito huo jana mjini Tabora wakati akifungua mkutano wa siku moja kwa viongozi mbalimbali mkoani humo kuhusu mpango endelevu wa ugawaji wa vyandarua vyenye viuatilifu vya muda mrefu kupitia vituo vya kutolewa huduma za afya na shule za msingi. Alisema kuwa elimu sahihi itasaidia wananchi kuacha kutumia vyandarua kwa matumizi mengine badala ya kujikinga na mbu ili kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa na malaria . 


  Mkuu huyo Mkoa aliongeza wananchi wakifahamu juu ya usafi wa mazingira utasaidia kuondoa mazalia mbu katika makazi yao. Kwa upande wa Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt. Thea Ntara alitoa wito kwa watalaam kusaidia mkakati wa kuangamiza kabisa mazalia ya mbu kama sehemu ya kuondoa ugonjwa wa malaria hapa nchini.
  Aidha , Katibu Tawala huyo wa Mkoa wa Tabora aliiomba jamii kubadirika na kuanza kutumia vyandarua vyenye viutilifu ili kuokoa maisha ya Mama na mtoto.

  Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Gunini Kamba alisema mpango wa kugawa vya ndarua katika vituo vya kutoa huduma za afya ,shule za msingi na katika ngazi ya familia unakusudia kupunguza maambuzi ya maralia hapa nchini.

  Aliongeza kuwa vyandarua hivyo vitasaidia kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa malaria mkoani hapa kutoka asilimia 19.5 ya sasa na kushuka zaidi.

  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri akifungua Mkutano jana mjini Tabora wa viongozi mbalimbali kuhusu mpango endelevu wa ugawaji wa vyandarua vyenye viuatilifu vya muda mrefu kupitia vituo vya kutolea huduma za afya na shule msingi mkoani humo.

  Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt. Thea Ntara akisisitiza umuhimu wa wataalam kutafuta mbinu ya kuangamiza mazalia ya mbu kama njia ya kukabiliana na malaria nchini wakati wa mkutano uliofanyika jana mjini Tabora kuhusu mpango endelevu wa ugawaji wa vyandarua vyenye viuatilifu vya muda mrefu kupitia vituo vya kutolea huduma za afya na shule msingi mkoani humo. Picha na Tiganya Vincent-RS-Tabora.
   

  0 0

  Mkuu mpya wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Anna Mghwira akikwea gari kuelekea kituo chake cha kazi baada ya kauapishwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli asubuhi hii Ikulu jijini Dar es salaam. Habari kamili, picha zaidi na video kuja baada ya muda si mrefu

  0 0

  Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama (alieshika panga) akikata muwa kuashiria uzinduzi uzinduzi wa mpango maalumu wa uwezeshaji wa wakulima wa miwa wa nje (Outgrowers scheme) katika mradi wa sukari wa Mkulazi wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika mkoni Morogoro mwishoni mwa wiki.Anaeshuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mkulazi ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof Godius Kahyarara (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw.William Erio (kushoto).

  Na Mwandishi wetu,

  SERIKALI imesema uamuzi uliofanywa na Mifuko ya Hifadhi ya jamii wa kuwekeza kwenye sekta viwanda hapa nchini ni uamuzi sahihi huku ikitoa wito kwa wanachama na wadau wa mifuko kushiriki kikamilifu katika kutumia fursa zitokanazo na miradi hiyo.

  Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama  wakati akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu wa uwezeshaji wa wakulima wa miwa wa nje (Outgrowers scheme) katika mradi wa Mkulazi iliyofanyika mkoni Morogoro mwishoni mwa wiki chini ya uratibu wa Kampuni  Hodhi ya Mkulazi Holding Ltd ambayo imetokana na na ubia kati ya mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF na PPF.
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw Charles Mwijage (alieshika panga)akikata muwa kwenye uzinduzi huo.Anaeshuhudia ni Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama (kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mkulazi ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof Godius Kahyarara (kulia).

  Mpango huo mpya sehemu ni utekelezaji wa mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha sukari kitakachojengwa na kwa ubia wa mifuko hiyo miwili katika eneo la Mkulazi, mkoani Morogoro na unalenga kuwashirikisha wakulima wa (outgrowers scheme)katika kilimo cha miwa kwa kiasi kikubwa ukuanzia na wananchi wa mkoa wa morogoro na Pwani.

   “Mbali na kuipongeza mifuko yetu ya Hifadhi ya Jamii kwa uwekezaji huu wenye tija kwa taifa naomba niwasihii sana msikatishwe tamaa na maneno ya watu yanayolenga kupotosha dhana nzima ya uamuzi huu makini lakini nataka niwathibitishie kuwa hadi sasa tupo kwenye mstari sahihi na dalili njema zimeanza kuonekana,’’ alisema.

   “Mpango huu licha ya kutengeneza ajira kwa watu zaidi ya 10,000 pia utapunguza na kuondoa kabisa tatizo la upungufu wa sukari nchini, kuzuia na kupunguza makali ya mfumuko wa bei kwa kuhakikisha bei ya sukari inaendana na gharama za uzalishaji,’’ aliongeza.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk Steven Kebwe (alieshika panga) akikata muwa kwenye hafla ya uzinduzi huo.Anaeshuhudia ni Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama pamoja na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw Charles Mwijage.

  Kwa upande wake Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw Charles Mwijage mbali na kuipongeza mifuko hiyo kwa utekelezaji wa  mradi huo mkubwa pia aliongeza kuwa licha ya uwekezaji huo kuhusisha pia kilimo cha mazao mengine ikiwemo mpunga, alizeti, mahindi na mtama pia kuna haja ya kuhakikisha unahusisha uwekezaji katika sekta ya maziwa hoja iliyongwa mkono pia na Waziri Mhagama.

  “Pamoja na pongezi zangu ninaomba mradi huu pia uhusishe uzalishaji wa maziwa kwa kuwa tunatarajia kupata mabaki mengi yatokanayo na mazao ambayo yanaweza kugeuka kuwa chakula cha mifugo,’’ alishauri.

  Awali wakizungumzia mradi huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mkulazi ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof Godius Kahyarara pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw.William Erio, walihakikishia serikali, wananchama na wadau wote wa mifuko hiyo kuwa utekelezaji wa mpango huo unahusisha  uadilifu na uwazi ili kuleta matokeo chanya.
  ZAWADI! Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mkulazi ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof Godius Kahyarara (kushoto) akimkabidhi zawadi Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama (kwa kutambua mchango wake kwenye mradi huo. Wanaoshuhudia ni pamoja na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw Charles Mwijage pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk Steven Kebwe, baadhi ya wabunge wa mkoa wa Morogoro pamoja na muwakilishi kutoka Gereza la Mbigili lililopo mkoani humo.

   “Tunajitahidi sana kuzuia kashfa yoyote katika utekelezaji wa mradi huu ili tusiitie doa nia njema ya Mheshimiwa  Rais lakini pia kuhakikisha kwamba fedha za wanachama wa NSSF na PPF zinabaki kuwa sehemu salama,’’ alisema Prof Kahyarara.


  0 0

  DAR ES SALAAM – Vodacom Tanzania’s initial Public Offering (IPO) is on track to be the largest in the 19-year history of the Dar es Salaam Stock Exchange. More than 40 000 Tanzanians, many of them first time participants in the capital market, have subscribed for shares in the IPO, a milestone that executes on Government’s vision to empower more Tanzanians to own stakes in local companies. Vodacom Tanzania is due to list on the DSE during June 2017, pending final verification by the CMSA.

  Ian Ferrao, Managing Director of Vodacom Tanzania commented:

  “I would like to thank all of the individuals and institutional investors for their participation in the listing process. We look forward to a fruitful relationship with our new shareholders as we take Vodacom Tanzania PLC forward into a new era as a public listed Company. Vodacom has a proven track record as the leading telco in Tanzania and it is fitting that we were the first to heed the call by the Parliament of Tanzania requiring licensed telco operators to list on the Dar es Salaam Stock Exchange.”

  Due to the sheer volume of applications and the size of the Vodacom Tanzania IPO, it has taken slightly longer than initially anticipated to ensure all applications could be processed and to ensure the creation of new central securities depository (CSD) account numbers for the many first-time investors in the DSE.  NBC, the receiving bank for the IPO, has now concluded with reconciliation of funds and applications with each of the brokers that participated across the Country.

  Vodacom Tanzania PLC, through its lead advisor Orbit Securities, submitted the full register of IPO participants to the CMSA, who are now undertaking the task of verifying each of the applications.  This exercise, given the volumes of applications, may take some additional time and Vodacom Tanzania will only be in a position to announce the final results once the CMSA concludes its verification process. Further information on the results and the next steps towards the listing will be announced in due course.

  Ferrao concludes: “We now look forward to listing our shares on the DSE and begin trading soon. This is going to be a great milestone for Vodacom Tanzania, the CMSA and the DSE.”

  0 0  0 0

   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi (kulia), akimkaribisha Rais Mstaafu, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, katika futari waliyowaandalia wateja wao jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Katikati ni Meneja Mahusiano wa benki hiyo, William Kallaghe.
   Rais Mstaafu, Alhaji Ali Hasaan Mwinyi (wa pili kushoto), akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na benki  ya NBC kwa wateja wake jijini Dar es Salaami. Kutoka kushoto ni  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi, Mkurugenzi wa Wateja Binafsi, Filbert Mponzi na Waziri Mkuu wa zamani, Salim Ahmed Salim .  
   Rais Mstaafu, Alhaji Ali Hasaan Mwinyi (katikati), akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi (kushoto), katika hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Wateja Binafsi, Filbert Mponzi.  
   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kushoto), akimpa zawadi Waziri Mkuu wa zamani, Salim Ahmed Salim katika hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake jijini Dar es Salaam.
  Rais Mstaafu, Alhaji Ali Hasaan Mwinyi (kushoto), akizungumza na Meneja wa Tawi la Corporate, Mariam Kombo (kulia), baada ya kuhudhuria hafla ya futari  iliyoandaliwa na NBC jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi na Meneja Mahusiano wa benki hiyo, William Kallaghe.

  0 0

  Mshambulaji wa kitanzania Jerome Nturukundo (kushoto) anayekipiga katika timu ya Nakuru Stars ya nchini Kenya.

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  Mshambulaji wa timu ya Nakuru All Stars Mtanzania Jerome Nturukundo amesema kuwa mechi yao dhidi ya Simba itakuwa ni ngumu sana ila watahakikisha wanafanya vizuri ili kuingia hatua ya nusu fainali.

  Nakuru wanatakutana na mabingwa wa kombe la FA Simba katika mchezo wa mtoano utkaoafanyika leo saa 10:15 alasiri kwenye dimba la uwanja wa Uhuru.

  Nturukundo amesema kuwa wanajua Simba ni timu nzuri sana lakinina wao wamekuja kupambana na kuhakikisha wanapata ushindi na kuingia hatua inayofuata.

  "Tutajua simba ni team nzuri lakini na sisi  pia tunekuja kiushindani na wafahamu timu yetu imekamilika na leo wapo katika wakati mgumu kwa sababu  sisi pia tumekuja kushinda,"amsema Jerome

  Kwa upande wa beki wa kati  James sadicky mukhwana yeye amesema kuwa ujio wao Tanzania ni kwa ajili ya kuhakikisha wanapat ushindi katika michezo yao na malengo yao ni kuona kombe la Sportpesa Super Cup likienda nchini Kenya.

  "Simba wasifikiri itakua rahisi kuweza kuoata ushindi katika mchezo wetu wa leo kwani tunataka kombe liiende nyumbani Nchini Kenya na mimi kama mlinzi nitahakikisha hakuna makosa yatakayofanyika katika eneo langui,"amesema  mukhwana.  

  Timu ya Nakuru inanolewa na kocha mzawa George Maina imekuja nchini katika michuano ya Sportpesa Super Cup iliyoandaliwa na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Sportpesa.


  0 0  0 0  Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
  Kwa mara nyingine tena mfanyabiashara Shabani Hussein maarufu kama "Ndama mtoto wa Ng'ombe" amekiri shtaka la utakatishaji wa fedha iliyofunguliwa na Jamhuri.
  Ndama anayekabiliwa na mashtaka sita katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, amekiri shtaka hilo la kutakatisha fedha ambazo ni dola za Marekani 540,000.


  Kwa mujibu wa sheria ya kutakatisha fedha kifungu cha 12(a)na 13(1)(a) namba 12 cha 2016 mshitakiwa huyo anaweza kuhukumiwa kifungo cha miaka isiyopungua mitano ama isiyozidi kumi au kulipa faini isiyopungua milioni 100 na isiyozidi milioni 500.
  Ndama alishawahi kukiri kosa hilo lakini aliposomewa mashitaka yake maelezo ya awali, alikana shtaka na kesi yake kuamriwa iendelee kusikilizwa.
  Wakili wa Serikali, Estazia Wilson amedai mbele ya Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa kuwa kesi hiyo leo imekuja kwa ajili ya kutajwa hata hivyo, mshitakiwa Ndama aliomba mahakama kumkumbushia mashitaka yake ambapo kwa mara nyingine alikiri kosa la sita la utakatishaji fedha.
  Kutokana na hali hiyo, Hakimu Nongwa aliahirisha kesi hiyo hadi ijumaa wiki hii (Julai 9, mwaka huu) kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.

  Katika mashauri yaliyopita, upande wa utetezi katika kesi hiyo ukiongozwa na Wakili, Jeremiah Ntobesya waliomba upande wa mashitaka kurekebisha hati ya mashitaka ili kumsomea upya mteja wao kwa kuwa yaliyopo yana mapungufu.
  Baadaye upande wa mashitaka ulifanya marekebisho ya hati ya mashitaka na kumsomea upya ambapo Ndama alikiri lakini kesi hiyo ilipopangwa kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali, alikana mashitaka.
  Anadaiwa kuwa, kati ya Februari 26 na Machi 2014, Dar es Salaam, akiwa mwenyekiti na mtia saini pekee wa Kampuni ya Muru Platinum Tanzania Investment Limited na akaunti ya benki ya kampuni hiyo iliyoko kwenye Benki ya Stanbic alijihusisha moja kwa moja kwenye uhamishaji wa dola za Marekani 540,000 na kuzitoa huku akijua fedha hizo ni zao la kosa la uhalifu la kujiapatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
  Licha ya kukubali mashitaka hayo, Ndama alikana makosa mengine yakiwemo ya kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu. Mashtaka mengine yanayomkabili ndama ni, kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
  0 0


  Mkufunzi anayesimamia mafunzo ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 (2017/18 HBS) Sergiy Redyakin akimwelekeza mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) namna ya kujaza dodoso litakalotumika katika utafiti huo unaotarajia kufanyika nchini kuanzia mwezi Agosti, 2017.
  Baadhi ya Watakwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakifuatilia kwa makini mafunzo yanayotolewa na mkufunzi anayesimamia mafunzo hayo Sergiy Redyakin (hayupo pichani) wakati wa mafunzo ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 yaliyofanyika hivi karibuni katika makao makuu ya NBS Dar es Salaam.
  Baadhi ya watakwimu kutoka NBS wakijifunza namna ya kujaza madodoso kwa njia ya kieletroniki wakati wa mafunzo ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 unaotarajia kufanyika nchini kuanzia mwezi Agosti, 2017.
  Mtakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Hellen Mtove (wa kwanza kulia) akimhoji mmoja wa wanakaya wakati wa majaribio ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 unaotarajia kufanyika nchini kuanzia mwezi Agosti, 2017.


  (PICHA NA EMMANUEL GHULA) 

  0 0

  MAAFISA Afya toka kitengo cha magonjwa ya dharura mkoa wa Songwe wameweka kambi kwenye kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Songwe (SIA), ili kubaini abiria wenye dalili za ugonjwa wa Ebola ulioibuka hivi karibuni kwenye nchi ya jirani ya Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo.

  Kiwanja cha Kimataifa cha Songwe kilichojengwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) mwaka 2012 kinapokea abiria 500,000 kwa mwaka kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi, ikiwemo nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. TAA inahudumia viwanja 58 vilivyopo chini ya serikali.

  Afisa Afya Bw. Peter Alfred amesema wamefunga mashine maalum na ya kisasa kiwanjani hapo, ambayo abiria akipita umbali wa mita tano hadi 10 inampiga picha na kuonesha joto alilonalo mwilini, na endapo atakuwa na joto la nyuzijoto 37.5 mashine hiyo itatoa mlio wa kengele.

  Bw. Alfred amesema abiria atakayekuwa na joto hilo, atachukuliwa na kupelekwa eneo maalum lililotengwa umbali wa mita 300 kutoka eneo la kiwanja cha ndege na baadaye kupelekwa hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya matibabu zaidi.
  Afisa Afya Bw. Peter Alfred (katikati) akikagua hati ya kusafiria ya Bw. Paluku Ngahngondi (kushoto) Mkongo anayeishi Zambia, kabla ya kupanda ndege ya Fastjet kuja Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Afya Bi. Shukrani Nkonjeka akiwa kwenye mashine maalum inayompima kila abiria anayepita mbele yake kwa kupiga picha na kutoa mlio wa endapo anajoto kali la mwili.
  Bi. Shukrani Nkonjeka, Afisa Afya akimpa maelezo kuhusiana na ugonjwa wa Ebola, mmoja wa wafanyakazi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Songwe (SIA), Bw. Fred Martin (kushoto).
  Bi Shukrani Nkonjeka, Afisa Afya akiwapa maelezo yanayohusiana na ugonjwa hatari wa Ebola madereva wa taxi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Songwe (SIA).
  Madereva wa taxi wa kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Songwe (SIA), wakipokea vipeperushi vyenye maelezo mbalimbali yanayohusu ugonjwa hatari wa ebola kutoka kwa Afisa Afya, Bi. Shukrani Nkonjeka


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni William Makufwe awashukuru BAY PORT Taasisi ya kifedha kwa msaada wa kompyuta mbili walizozitoa Jana kwa Idara ya Utumishi na Rasilimali watu..

  Mkurugenzi Mtendaji alisema kuwa anashukuru kwa msaada wa kumpyuta hizo ambazo zitakwenda kwenye Idara ya Utumishi na Rasilimali watu ili kuimarisha Idara na ufanisi wa Idara hiyo kwa kuzingatia unyeti wa eneo hilo na huduma wanayoitoa kwa watumishi.

  Miongoni mwa Halmashauri 80 ambazo zimelenga kufikiwa na BAYPORT tunashukuru Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imekuwa moja wapo na tunaahidi kutumia vifaa hivi vya TEHAMA kwa kuongeza ufanisi na utendaji kazi ulioboreka zaidi.

  Mratibu wa masoko na mawasiliano wa huduma za kifedha za BAYPORT Mercy Ndunguru alisema kuwa BAYPORT imeamua kurudisha faida ambayo wameipata ambapo kwa sasa wameona waguse sekta ya utumishi ambayo imekuwa na msaada mkubwa katika kufikia malengo.

  Mercy alisema kuwa, Tunaamini kwa kutoa vifaa hivi vya TEHAMA itasaidia kuongeza ufanisi kwenye sekta ya utumishi na watumishi watapata huduma kwa wakati, BAYPORT inamuunga mkono Raisi kwenye utendaji kazi kwa watumishi.

  Meneja wa BAYPORT Handeni Kanji Masanji alisema kuwa, anashukuru kwa ushirikiano anaoupata kutoka kwa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni na kwamba taasisi yao inajipanga kufanya mambo mengine makubwa zaidi ya haya ikiwa ni pamoja na kujipanga kufadhili timu mbalimbali za mipira na kuinua vipaji vya vijana waliopo Wilayani Handeni.

  BAYPORT wametoa msaada huo wa kompyuta mbili ikiwa ni miongoni mwa kompyuta zenye thamani ya zaidi ya milioni 500 zinazoendelea kutolewa kwenye taasisi nyingine za Kiserikali.

  Alda Sadango

  Afisa Habari
  Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni William Makufwe kushoto akipokea Msaada wa kompyuta kutoka Kwa Mratibu wa masoko na mahusiano kutoka BAYPORT Mercy Ndunguru.
  Afisa utumishi Wilaya Noel Abel akipokea Msaada wa kompyuta kutoka Kwa Mratibu wa masoko na mahusiano kutoka BAYPORT Mercy Ndunguru.
  Picha ya pamoja baada ya makabidhiano ambapo kushoto ni Afisa utumishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni na kulia ni Mratibu wa masoko na mahusiano na meneja wa tawi LA BAYPORT Handeni

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Aliyekuwa mshambuliaji wa timu ya Toto Afrika Waziri Junior ametambulishwa leo mbele ya waandishi wa habari baana ya kusaini kandarasi na timu ya Azam.

  Azam jana walifanikiwa kupata saini ya mshambuliaji huyo kinda kutoka Toto ikiwa ni katika muendelezo wa kuboresha kikosi chao ili kuweza kufanya vizuri katika msimu ujao unaokuja.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa habari wa Azam Jafar Iddy amesema kuwa wamefanikiwa kunasa saini ya mshambuliaji juyo kinda kutoka Toto kwani hilo limekuja ikiwa ni moja ya mapendekezo ya kocha mkuu wa timu hiyo.

  "huu ni muendelezo wa kusajili na kufa nya marekebisho katika kikosi chetu kuelekea msimu ujhao, na usajili huu unakuja baada ya kuona mapendekezo ya kocha mkuu Aristoc Cioaba na akwa sasa ni kuwapa fursa vijana,"amesema Iddy

  Awali Waziri alikuwa anawaniwa na timu Yanga lakini Azam wameonekana kuwapiga bao na kumsainisha kwa dau nono .

  Afisa habari wa Azam Jafar Iddy(wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kumtambulisha mshambuliaji yao mpya Waziri Junior (wa pili kushoto) aliyesaini kandarasi ya kuitumikia klabu hiyo.  0 0
 • 06/06/17--13:30: ADIOS AMIGO, BRAZA CISCO!
 • Na Ankal
  Hebu jaribu kulielezea jiji la Dar, au la Arusha, ama la Mwanza,  Mbeya  ama jiji lolote lile, tena  kwa kutumia ukurasa mmoja tu na uwe umefanikiwa kulieleza kinagaubaga kiasi hata mtu ambaye hajawahi kufika hapo ajione kama keshafika na anapafahamu vizuri.

  Basi huo ndio mtihani nilikumbana nao wakati najitahidi kuandika haya, tena kwa moyo mzito, nikijaribu kumwelezea rafiki yetu, kaka yetu, ndugu yetu, jamaa yetu au vyovyote vile upendavyo kumwita mtu kama Balozi Abdul Omar Cisco Mtiro.
  Labda uamue uzungumzie kamtaa kamoja tu katika kitongoji kimoja, ndio kidooooogo unaweza kufanikiwa kueleza vitu vikaeleweka - Nami ndivyo naitajaribu kufanya hapa,  kwa kudonyoa kasehemu kamoja tu ka Braza Cisco.

  Ni kweli kwamba mtu akitangulia mbele ya haki huwa kuna hulka ya kumsifia na kumuenzi mtu huyo. Lakini si uwongo kwamba haya niandikayo hapa, japo yalikuwa nyuma ya ubongo wa wengi wetu siku zote, ni halisi na wala sio kwa sababu Cisco hatunaye tena.
  Naam, kwa wengi alikuwa mkarimu na mwingi wa bashasha saa zote. Kwa tuliobahatika kuwa karibu naye, Cisco alikuwa hivyo na zaidi. Pamoja na kuwa na wadhifa mkubwa serikalini (Balozi wetu nchini Nigeria na Malaysia katika nyakati mbalimbali na baadaye Mkuu wa Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje), Cisco alikuwa mtu wa kujichanganya na kila mtu bila kujali hali ama mali zake. Hakuwa na makuu wala makidai. Alikuwa mtu mmoja 'freshi' ile mbaya, wanasema vijana wa mjini.
  Kusoma zaidi BOFYA HAPA

  0 0   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira Ikulu jijini Dar es Salaam.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi ,Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na viongozi wengine Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo akimkabidhi Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira huku Rais Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Salum Hapi pamoja na wakuuu wa Wilaya za Ubungo na Ilala wakipiga makofi. Picha na IKULU

  0 0

  Wananchi wilayani Handeni wapigwa marufuku kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya mita 60 kutoka katika vyanzo vya maji na kutakiwa kutunza mazingira ili kuwezesha uendelevu wa maisha.

  Marufuku hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe aliyekuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yaliyofanyika ngazi ya wilaya katika Kata ya Mkata katika bwawa la Tulafimbo. 

  Gondwe alisema kuwa wananchi lazima wazingatie sheria ya Mazingira inayozuia kufanya shughuli za kibinadamu pamoja na kujenga kwenye maeneo yote ya vyanzo vya maji ndani ya mita 60. “Kwa kuzingatia sheria hiyo, kupiga marufuku kwa wananchi kufanya shughuli zozote za kibinadamu zenye kuhatarisha usalama wa maji na uchafuzi wa mazingira kwenye maeneo yanayozunguka vyanzo vya maji wilayani Handeni” alisema Gondwe. 

  Aidha, aliwataka maafisa Tarafa, maafisa watendaji wa Kata na wenyeviti wa Vijiji kuhakikisha wanatengeneza mipaka kwenye maeneo ya vyanzo vya maji vyote vilivyopo Wilayani Handeni msimu huu ambao mvua imenyesha ya kutosha na vyanzo vingi vimejaa maji. “Hii itasaidia kuzuia uvamizi wa maeneo hayo na kurahisisha kuchukua hatua kwa watu watakaokwenda kinyume na amri hiyo” alisema Gondwe.

  Gondwe, aliwataka wananchi wote walionunua mashamba kwa lengo la kilimo kusafisha mashamba yao kwa kuacha asilimia 30 ya uoto wa asili badala ya kusafisha maeneo yote ambayo wamenunua. “Tusipotunza mazingira, itakuwa ni ubinafsi kwa kizazi chetu na kizazi kijacho. Tukitendee haki kizazi hiki na kijacho kwa kuondoa ubinafsi wa kuharibu mazingira” alisema Gondwe.

  Wakati huohuo, aliwataka viongozi ngazi ya Wilaya, Tarafa, Kata na Vijiji kutunza kutunza mazingira kwa kusimamia uwiano wa ardhi uliyopo na idadi ya mifugo ili kutunza mazingira kwa kuwa na mifugo inayoendana na rasilimali ardhi iliyopo. Aliwataka kuweka mikakati ya kupiga chapa mifugo ili kurahisisha utambuzi wa mifugo hiyo wilayani Handeni.
   Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe akipanda mti kwenye maadhimisho.
   Mkurugenzi Mtendaji Bw William Makufwe iyeshika chepeo na mwenyekiti wa Halmashauri ya Handeni Mh Ramadhani Diliwa wakipanda mti.
   Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe akizungumza na wananchi.
   Mkurugenzi Mtendaji Bw William Makufwe akizungumza na wananchi wakati wa maadhimisho.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  KAMPUNI ya Mitindo ya BlackFox Models inazidi kujitanua huku ikiwatengenezea fursa vijana kukuza vipaji vyao mbalimbali.

  Hivi karibuni Kampuni hiyo ilifanya usahili wa wanamitindo mkoani Mwanza ambapo mamia ya vijana walijitokeza na kunolewa huku wakijipatia mikataba ya kufanya kazi na kampuni hiyo.

  Lakini pia imewachukua washiriki wa Miss Ardhi University ambao walishika nafasi tatu bora katika shindano hilo.

  Washiriki hao ni Glady John, Stella Ernest na Evodia Patrick.
  Akizungumzia maendeleo ya kampuni hiyo Mkurugenzi Mtendaji wake, Atu Mynah, Aj alisema kuwa lengo kubwa ni kuwajengea uwezo vijana wakitanzania.

  Alisema, amehakikisha kuwa anawasaka vijana wenye nia ya kuwa wanamitindo na kuwaendeleza hadi kufikia malengo yao huku akisisitiza kuwa anawanoa katika misingi yote ya uanamitindo.
  Alisema, anawaendeleza katika vipaji vyao ikiwa ni sambamba na kuwapatia elimu ya fani hiyo kuanzia kibiashara, kisheria na kila kinachotakiwa kwa mtu kuwa Mwanamitindo.
  AJ, kushoto akipitia profile za baadhi ya wanamitindo walioomba kushiriki kwenye usahili huo.
  Meza ya majaji ikiendelea na mchakato wa kuwapata wanamitindo.
  Aj, akizungumza na wanamitindo kadhaa waliofanikiwa kuchaguliwa ambapo alisikika akisisitiza suala zima la nidhamu.


  0 0

  Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo ukiingizwa kanisani.
  Waziri mkuu wa Zamani ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa akibadilishana mawazo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi katika ibada ya kumuaga aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo.
  Viongozo wa Chadema wakiwa katika ibada ya kumuombea aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo.
  Mke wa Marehemu aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo (wa pili toka kushoto) akiwa kanisani.
  Gari lililobeba mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo likielekea kwenye kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kiboriloni kwa ajili ya kuombewa. Maziko ya Marehemu Ndesamburo yanafanyika leo nyumbani kwake mtaa wa  KDC- Moshi,mkoani Kilimanjaro.


  0 0

   Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk.Tulia Ackson akiongoza kikao cha 42 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 06, 2017.
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 42 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 6, 2017.
  Waziri wa Nchi Ofisi Ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye ulemavu Mhe.Jenista Mhagama  akitolea ufafanuzi hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha 42 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 6, 2017.
  Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha 42 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 6, 2017.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Khamis Kigwangalla akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 42 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 6, 2017.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 1730 | 1731 | (Page 1732) | 1733 | 1734 | .... | 3272 | newer