Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110021 articles
Browse latest View live

‘STACA’ MRADI WA WENYE MAFANIKIO LUKUKI MAHAKAMA MKOANI MTWARA

$
0
0
Na Nurdin Ndimbe

Kwa miaka ya hivi karibuni Mkoa wa Mtawara umekuwa na maendeleo makubwa ya Kichumi na ya Kisiasa. Kutokana na mabadiliko hayo maendeleo ya Mkoa wa Mtwara yameongeza ari na matumaini mapya ya maisha bora kwa wananchi wa Mkoa huo. 

Mtwara ya sasa ni yenye fursa lukuki kutokana na miradi mbalimbali ya maendeleo yaliyotokana na uchimbaji wa gesi asilia, maendeleo ya uboreshaji wa miundombinu na ongezeko na mapato katika zao la korosho.

Maendeleo haya yameikumba Sekta mbalimbali Mkoani humo ikiwemo ya Sekta ya Sheria hususani Mahakama. Mahakama ya Tanzania kanda ya Mtawara yenye watumishi 218 ilianza kutekeleza Mradi wa Mapambano dhidi Rushwa (Strengthening Tanzania Anti-Corruption Action ) kwa kifupi STACA Mwaka 2011/2012 chini ya ufadhili wa Uingereza kupitia Shirika lake la misaada la Kimataifa la DFID. 

Lengo kuu la mradi huu ilikuwa ni kuzuia na kupambana na rushwa mahala pa kazi, Katika Mkoa wa Mtwara mradi huu ulihusisha Wilaya zote tano za Tandahimba, Masasi, Newala, Mtwara na Nanyumbu. Mradi huu ulijikita katika ugawaji wa vitendea kazi kama kompyuta na ‘printer’ zake, mafaili ya kufungulia mashauri (case files), makabati ya kutunzia mafaili na kumbukumbu, pikipiki kwa watumishi wa Mahakama pamoja na baiskeli kwa ajili ya kusambazia ‘Summons.’
Baadhi ya pikipiki zilizotolewa chini ya Mradi wa STACA, pikipiki hizi na baadhi ya vifaa vingine tajwa ni miongoni mwa vitendea kazi vilivyotolewa kurahisisha utoaji huduma ya haki.
Muonekano wa picha ya bango lenye ujumbe wa kuzuia na kupambana na Vitendo vya Rushwa ikiwa imebandikwa katika jengo la Mahakama Kuu-Kanda ya Mtwara. Bango hili ni kati ya Mabango mengi ambayo yamebandikwa katika majengo ya Mahakama nchini lengo likiwa ni kuzuia rushwa na vitendo vitendo vyenye ukosefu wa maadili.




BENKI YA NMB YAIKABIDHI SERIKALI GAWIWO LA SHILINGI BILIONI 16.5

$
0
0

Na Benny Mwaipaja-WFM

Benki ya NMB imepata faida ya ya shilingi bilioni 153.8 kwa mwaka 2016 hivyo kuiwezesha kutoa gawiwo la shilingi bilioni 16.5 kwa Serikali ambayo inamiliki asilimia 32 ya hisa za Benki hiyo.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) alikabidhiwa hundi kifani ya gawiwo hilo katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa wanahisa wa Benki hiyo uliofanyika Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Mpango amezipongeza juhudi za watendaji wa Benki hiyo waliofanikisha kupatikana kwa faida iliyowezesha Serikali kupata gawiwo. Aidha, Serikali inajivunia mafanikio makubwa ya kiutendaji ya NMB na uwekezaji wake ambao unatija na unaifanya serikali isijutie uamuzi wake wa kuibinafsisha Benki hiyo.

Amesema fedha hizo zilizopatikana kutokana na gawiwo zitaelekezwa kwenye maendeleo ili kutatua baadhi ya kero zinazowakabili wananchi.

Ameahidi kuwa, Serikali kama mwanahisa itaendelea kuitumia Benki hiyo kikamilifu katika huduma za kibenki ili kuiwezesha kuongeza mapato.

“Shughuli ambazo Serikali itazifanya kupitia NMB Bank Plc ni pamoja na malipo ya mishahara ya wafanyakazi wa Umma na pia kukusanya mapato ya Serikali yanayotokana na kodi na yasiyo ya kodi.

Waziri Mpango ametumia nafasi hiyo kuagiza kampuni ambazo zenye ubia na Serikali kuiga mfano wa NMB Benki Plc na kupeleka gawiwo katika faida wanayopata.

“Katika Serikali ya Awamu ya Tano ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli haiingii akilini kusikia kila mwaka mnapata hasara lakini mpo hamtoki, tumevumilia vya kutosha sasa imetosha, haiwezekani unawekeza miaka 10 lakini watanzania hawapati chochote” alionya Dkt. Mpango.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB , Ineke Bussemaker (kulia) baada ya kupokea mfano wa hundi wa gawiwo la shilingi bilioni 16.5 ambazo Serikali kama mwanahisa imepata katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa wanahisa wa Benki hiyo uliofanyika Jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mafanikio ya Benki hiyo ambayo kwa mwaka ulioishia Disemba 31,2016 ilipata faida ya shilingi bilioni 153.8 licha ya changamoto za kibenki, likiwa ni ongezeko la asilimia 2,  ukilinganisha na mwaka 2015 ambapo ilipata faida ya shilingi bilioni 150.3.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Isdor Mpango (Mb) akiishukuru Benki ya NMB kwa kutoa gawiwo la shilingi bilioni 16.5 kwa Serikali wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa wanahisa uliofanyika jijini Dar es Salaam .
Wanahisa wa Benki ya NMB wakiwa katika Mkutano wao Mkuu wa Mwaka ambapo uliofanyika Jijini Dar es Salaam ambapo Benki hiyo imetangaza jumla ya shilingi bilioni 52 kama gawiwo kwa wanahisa wote. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango) 


ALICHOKIZUNGUMZA RC MAKONDA BAADA YA KUTEMBELEA UJENZI WA FLYOVER TAZARA

Barclays Bank takes the lead in developing young minds through Education and Human Resource Programmes

$
0
0
Barclays Bank Tanzania Limited today visited the University of Dar es Salaam (UDSM) to speak to potential graduates about ‘great careers’ being offered by Barclays and introduce them to an exciting Scholarshp program that will allow students the opportunity of receiving one full year of tuition fees and other student fees paid by Barclays.

 A group of Barclays employees were also at the University to equip the students with important life and professional skills. For the graduates, Barclays is availing them with two channels to join the bank i.e.


1) As an entry level graduate or postgraduate candidate though the resourcing process being followed that will allow more than 20 candidates to join the bank every year.


2) A special ‘Graduate Development Program’ running in partnership with Delloite and Touché, providing opportunities for high calibre - high potential graduates aiming at developing future leaders of the bank.


Both channels aim at providing a consistent talent pipeline to meet current and future Human capital demands, taping from more than 300 years of experience and gathered knowledge to train and grow local talent via classroom, on-the job learning, inter-Africa mobility plan as well as global exposure.

 Barclays Tanzania Chief Finance Officer, Obedi Laiser (centre), talking to some University of Dar es Salaam (UDSM) students about the career opportunities being offered by Barclays and introduce them to an exciting scholarship program that will allow students the opportunity of receiving one full year of tuition fees and other student fees paid by BBT. It was during the banks career fair day at the University of Dar es Salaam Business School premises in Dar es Salaam at the weekend. On his left is Barclays Head of Marketing and Corporate Relations, Aron Luhanga and Dakshit  Pandya (on the right), the banks Head of IT and Change. 
 Barclays Tanzania Head of Learning and Leadership Training, Veronica Muumba (right), talking to some University of Dar es Salaam (UDSM) students about the career opportunities being offered by Barclays and introduce them to an exciting scholarship program that will allow students the opportunity of receiving one full year of tuition fees and other student fees paid by BBT. It was during the banks career fair day at the University of Dar es Salaam Business School premises in Dar es Salaam at the weekend.
 Barclays Bank Tanzania Head of Marketing and Corporate Relations, Aron Luhanga (right), talking to some University of Dar es Salaam (UDSM) students during the banks career fair day at the University of Dar es Salaam Business School premises in Dar es Salaam at the weekend. A group of Barclays employees were also at the University to equip the students with important life and professional skills. 
 Barclays Bank Tanzania Head of IT and Change, Dakshit Pandya (right),  talking to some University of Dar es Salaam (UDSM) students during the  banks career fair day at the University of Dar es Salaam Business School premises in Dar es Salaam at the weekend.

WANANCHI WA CHILONWA, DODOMA WAIOMBA SERIKALI KUJENGA DARAJA.

$
0
0
Wananchi wa kata ya Chilonwa, wilaya Chamwino mkoani Dodoma wameiomba Serikali kuchukua hatua za haraka kujenga daraja la Chilonwa lililopo katika kata hiyo ili kutatua kero ya usafiri kwa wananchi hao na maeneo jirani hususan katika kipindi cha masika. 

Wakieleza kero yao kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, wananchi hao wamesema wanaamini kuwa ujio wa Naibu Waziri huyo katika kata yao kutaleta ufumbuzi wa kero hiyo.

“Tunaamini sasa tutapata mwarobaini wa daraja hili kwani tatizo hili ni la muda mrefu, siku hadi siku daraja linakuwa fupi kutokana na kufukiwa na mchanga na hivyo hupelekea maji kujaa darajani hapa kipindi cha masika na watu kushindwa kuvuka”, amesema mmoja wa wananchi hao.

Aidha, wananchi hao wamemwomba Naibu Waziri huyo kurekebisha daraja hilo kwa kulijenga juu zaidi ili kupitisha maji na kupitika katika vipindi vyote vya mwaka kutokana na kwamba lililopo sasa lipo chini zaidi mara baada ya kufukiwa na mchanga.

Wananchi hao wameeleza masikitiko yao kwa Naibu Waziri huyo hususan katika kipindi cha masika ambapo wamesema hutumia kiasi cha shilingi elfu kumi kuvushwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine na wengine hupoteza maisha wakiwa wanavuka.
Muonekano wa Daraja la Chilonwa lililopo kata ya Chilonwa, wilayani Chamwino mkoani Dodoma. Daraja hilo ni kiungo kati ya mkoa wa Dodoma, Manyara na Arusha. 
Sehemu ya daraja la Chilonwa iliyoathirika kutokana na shughuli za kibinaadamu kama vile kilimo na hivyo kupelekea kwa daraja hilo kufukiwa na mchanga na kuwa fupi. 

Mbunge wa jimbo la Chilonwa, Mhe. Joel Makanyaga, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani (kushoto kwa Mbunge), alipofika jimboni hapo kukagua daraja la Chilonwa, wilayani Chamwino mkoani Dodoma leo. 

MSIUZE hOVYO CHAKULA KABLA YA KUWA NA AKIBA YA KUTOSHA- RC TABORA

$
0
0
Na Tiganya Vincent-RS-Tabora

Wakazi wa Mkoa wa Tabora wametakiwa kuweka akiba ya chakula cha kutosha ili kuepuka njaa inayoweza kuwakabili kutokana na mavuno ya msimu huu kutokuwa mazingira kufuatia mvua kuchelewa kuanza na kuwahi kukatika.

Wito huo umetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri wakati wa kilele cha maadhimisho siku ya mazingira duniani ambapo kimkoa yalifanyika katika Manispaa ya Tabora.

Alisema mvua za msimu huu zilikuwa kidogo na hivyo mavuno ya mazao kama vile mahindi , mpunga na maharagwe ni hayaridhishi hivyo ni vema wananchi wakahakikisha wanatenga chakula cha kutosha kwa ajili ya matumizi yao kabla ya kuanza kuuza.

Mkuu huyo Mkoa alisema kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara kutoka Mikoa mbalimbali wamekuwa wakipita katika maeneo mbalimbali ya vijiji na kuwarubuni wakulima wawauzie mahindi yao nao bila kuchukua tahadhari wanafanya wamekuwa wakiuza bila kuweka akiba ya kutosha jambo ambao sio jema.

Aliongeza kuwa watu aina hiyo ambao wanakimbilia kuuza mahindi yao bila kuweka aakiba ya kutosha kwa ajili ya familia zao ndio wamekuwa wakimbilia kwa viongozi wa Serikali wanaishiwa chakula.

Mkuu huyo wa Mkoa alisisitiza kuwa ameamua kuwatahadharisha mapema ili kila mkazi wa Tabora akatumia fursa hii ya upatikanaji wa vyakula vya kutosha katika masoko kuweka akiba kwa ajili ya familia zao badala ya kukaa ili kugonja msaada na wakati mwingine kulaumu Serikali bila sababu za msingi.

PROF TIBAIJUKA AONYA UPOTOSHAJI WA MITANDAONI NA KUTOA UFAFANUZI KUHUSU MCHANGO WAKE BUNGENI

SAMSUNG WAJA NA STIKA MBILI KUTOKOMEZA BIDHAA FEKI NCHINI

$
0
0
Balozi wa Samsung,Latifa Ally akitoa elimu kwa mteja kuhusu stika mbili zinazohusishwa na kampeni ya Samsung inayotarajiwa kuanza hivi karibuni stika hizo inayolenga kutokomeza bidhaa feki nchini.
Mabalozi wa Samsung wakitoa burudani na kutoa elimu kwa wateja juu ya stika mbili zinazohusishwa na kampeni ya Samsung katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Mabalozi wa Samsung wakiwa katika picha ya pamoja.

PEREIRA ATOA NASAHA NZITO KWA VIONGOZI WA CCM Z'BAR

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

KATIBU wa NEC, Idara ya Organazesheni ya CCM Taifa, Nd. Pereira Ame Silima amewataka viongozi na watendaji wanaochaguliwa kwenye uchaguzi wa chama na jumuiya zake kwa sasa kuwa na fikra na mitizamo mipya itakayoongeza ufanisi wa kiutendaji ndani ya CCM.

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na Wajumbe wa Kamati za siasa za Mikoa ya CCM Mjini na Magharibi pamoja na wajumbe wa sekreterieti na kamati Tekelezaji za jumuiya za Chama hicho huko Amani Unguja, alisema chama hicho kitaendelea kuwa imara kutokana na utamaduni wa kupata viongozi kwa njia za kidemokrasia hasa Uchaguzi huru na wa haki.

Alisema lengo la ziara hiyo ni kuimarisha chama sambamba na kujitambulisha kwa viongozi hao kwani tangu alipoteuliwa kushika nafasi hiyo hivi karibuni Mjini Dodoma hiyo ndio ziara yake ya mwanzo.

Alizitaka kamati mbali mbali zilizopewa dhamana ya kusimamia na kuchuja viongozi katika uchaguzi wa chama hicho kuhakikisha wanapatikana viongozi wenye nia ya kweli ya kuleta mabadiliko ya kiutendaji ndani ya chama hicho na sio wababaishaji.
Ni Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya siasa ya Mkoa ya CCM Mjini pamoja na Wajumbe wa sekreterieti na kamati Tekelezaji za jumuiya za Chama hicho wakimsikiliza kwa Umakini Katibu wa NEC, Idara ya Organazesheni CCM Taifa, Nd. Pereira Ame Silima huko Katika Ukumbi wa CCM Amani Unguja.
Katibu wa NEC, Idara ya Organazesheni CCM Taifa,Nd. Pereira Ame Silima akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya siasa ya Mkoa ya CCM Mjini pamoja na Wajumbe wa sekreterieti na kamati Tekelezaji za jumuiya za Chama hicho huko Katika Ukumbi wa CCM Amani Unguja.

SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUPITIA UPYA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZA MISAMAHA YA KODI

$
0
0
Benny Mwaipaja, WFM

Serikali imesema inaendelea kupitia sheria, kanuni na taratibu za misamaha ya kodi mwaka hadi mwaka ili kuhakikisha kuwa misamaha yote isiyokuwa na tija inafutwa na hivyo kuiwezesha Serikali kuongeza mapato kwa ajili ya kupeleka huduma za maendeleo kwa wananchi wake.

Kauli hiyo imetolewa Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), alipokuwa akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Masasi, Mhe. Rashid Mohamed Chuachua (CCM), aliyetaka kujua namna Serikali inavyodhibiti misamaha ya kodi tangu irekodiwe kwa viwango vya juu Mwaka wa Fedha 2011/2012.

Mhe. Chuwachuwa alihoji mwenendo wa utoaji wa misamaha ya kodi kwa wawekezaji kwa maelezo kuwa Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi zilizopoteza fedha nyingi kwa ajili ya misamaha ya kodi ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika Mashariki kwa kigezo cha kuvutia Wawekezaji.

Alisema kuwa kwa mujibu taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2009-2010, Tanzania ilipoteza asilimia 15 ya Pato la Taifa lililotarajiwa kukusanywa kutokana na misamaha ya kodi, mwaka 2010-2011 asilimia 8, kwa mwaka 2011-2012 asilimia 27 ya mapato ya Serikali yalipotea.

“Je hali ya misamaha ya kodi kuanzia 2013-2014 hadi sasa ikoje’’. Alihoji Mhe. Chuachua.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb),misamaha ya kodi kama sehemu ya asilimia ya Pato la Taifa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2013/14 hadi sasa imekuwa ikipungua mwaka hadi mwaka. 

TIRA YAZINDUWA MFUMO WA KUKAGUA NA KUHAKIKI UHALALI WA STIKA ZA BIMA KUPITIA SIMU ZA MIKONONI

$
0
0
Kamishina wa Bima, Dr.Baghayo Saqware akizungumza na wadau mbalimbali wa masuala ya bima mkoa wa Mbeya katika uzinduzi wa mfumo mpya wa kielectroniki kuhakiki uhalali wa Stika za Bima.

Uzinduzi wa kukaguwa na kuhakiki stika za bima uliofanyika katika ukumbi mdogo wa mkapa jijini mbeya kwa lengo la kupeleka elimu zaidi mtaani kwa watumiaji wa vyombo vya moto ikiwemo magari, pikipiki, bajaji na kadhalika, juu ya kujikinga na majanga mbalimbali ya tokanayo na ajari za barabarani pamoja na wezi, na mahalamia wa wa bima feki.

Bima hii yenyekulenga kuepusha ajari mbalimbali za barabarani kutoka katika kampuni ya bima ya (TIRA) “Tanzania Insurance Regulatory Authority” pia  imetoa huduma hii ya kwa mfumo wa kisasa wa kuhakiki bima kupitia simu ya mkononi kwa kushirikiana na kampuni mbili za mtandao wa simu, Tigo na Vodacom Tanzania kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) na Kwa Intanenti.
Waweza kuhakiki bima yako kwa kupitia mitandao ya simu (TIGO na VODACOM) kwa kwenda kwenye uwanja wa ujumbe mfupi wa simu ya mkononi  kwa kuandika neno STIKA acha nafasi kisha Andika Namba ya Stika i.e STIKA 8091390, kisha itume kwenda nambari 15200 ambapo utatozwa shilingi Mia Moja (100) Tu.
Kupitia Intanenti waweza kwenda kwenye Tovuti ya TIRA MIS https://mis.tira.go.tz, Kisha bofya Hakiki Stika za Bima/Validate Motor Insurance Sticker, kisha ingiza namba ya stika na bofya Hakiki/Validate.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari nae akichangia machache katika uzinduzi huo wa  mfumo mpya wa kielectroniki kuhakiki uhalali wa Stika za Bima.
Zoezi la uhakiki likiendelea kuanzia hii leo barabarani hivyo wamiliki wote wa vyombo vya usafiri kuimizwa kuhakiki Stika za Bima kwenye vyombo vyao.
Moja kati ya wadau wa Bima akifuatilia kwa makini semina ya Kamishna wa Bima Tanzania katika ukumbi wa mkapa Jijini Mbeya leo. 
PICHA ZOTE NA MR.PENGO MBEYA.

YANGA YATINGA NUSU FAINALI YA SPORTPESA SUPER CUP KWA KUITOA TUSKER YA KENYA KWA PENATI

$
0
0
Mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara Yanga imekuwa timu ya kwanza toka Tanzania kutinga nusu fainali ya Sports Pesa Super Cup kwa mikwaju ya penati. 
Katika mchezo wa kwanza Singida United ilicheza dhidi ya AFC Leorpads ya Kenya na vijana hao wa Hans Van Der Pluijm walitolewa  kwa  penalti 5-4 
Yanga imeing’oa Tusker ya Kenya kwa mikwaju ya penalti 4-2 baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya bila bao. 
 Kipa wa Yanga, Deo Munishi maarufu kama Dida alichangia kung’olewa kwa Tusker baada ya kupangua moja ya mikwaju ya Wakenya hao. 
Yanga sasa watakutana na AFC Leorpads siku ya Alhamis na Fainali ya Michuano hiyo itachezwa siku ya Jumapili Juni 11 na bingwa atacheza na Everton katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam July 13 mwaka huu.
 Mshambuliaji wa Yanga Chipukizi, Said Mussa, akijipinda kupiga shuti katikati ya mabeki wa Tusker, wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. 
 Mshambuliaji wa Yanga Chipukizi, Said Mussa, akimtoka beki wa Tusker, Corins SHivachi, wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. 
 Juma Mahadhi wa Yanga (kushoto) akichuana na beki wa Tusker, James Situma, wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
 Yanga Chipukizi na Tusker ya Kenya wakichuana katika mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Picha zote na Montage Ltd

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

$
0
0


SIMU.TV: Makamu wa rais Samia Suluhu amewataka watanzania kutowasikiliza baadhi ya wanasiasa wanaowataka kususia au kupinga miradi ya maendeleo; https://youtu.be/57_-FEoGU_g

SIMU.TV: Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli ameishukuru serikali ya Kuwait kwa kutoa mkopo wa dolla za Marekani milioni 51 zitakazosaidia ujenzi wa barabara; https://youtu.be/3yteEUAkNDE

SIMU.TV: Serikali ya Tanzania imeendelea na jitihada zake za kuboresha huduma za usafiri baada ya leo kuzindua kivuko kipya katika eneo la Kigamboni jijini Dar Es salaam; https://youtu.be/BzGTMe6MnpM

SIMU.TV: Mkandarasi anayetekeleza mradi wa maji Chalinze ameshindwa kukamilisha kwa wakati mradi huo na kulazimika kuongezewa muda mpaka mwezi Oktoba; https://youtu.be/jLmT9Ju-olg

SIMU.TV: Wakulima wanaojihusisha na shughuli za kilimo, ufugaji na uvuvi wanatarajia kunufaika na mikopo kutoka katika benki ya TADB; https://youtu.be/9XLQtfKn6uQ

SIMU.TV: Serikali ya Tanzania imeleza dhamira yake ya kufikia nchi ya viwanda kwa kuendelea kuwekeza kwenye kilimo cha biashara; https://youtu.be/iNWGeCeY6ao

SIMU.TV: Serikali ya Tanzania imetakiwa kuangalia njia bora za kutunza mazingira ikiwemo kuendelea kutoa elimu kwa watanzania juu ya utunzaji wa mazingira; https://youtu.be/rcezpMr5NLQ  

SIMU.TV: Golikipa wa Yanga Deogratius Munishi ameibuka shujaa baada ya kupangua mkwaju wa penati na kuisadia timu yake kuingia nusu fainali ya kombe la SportPesa; https://youtu.be/BNrGFPyYjNg

SIMU.TV: Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa Khalfan Haule amezindua mashindano ya ligi daraja la nne ngazi ya wilaya hiyo; https://youtu.be/kstldNKYFVk

SIMU.TV: Wasimamizi wa umoja wa michezo shule za msingi Umitashumta wametakiwa kusimamia sheria za mashindano hayo ili kuwapata washindi wa haki; https://youtu.be/1KmNF5uWVPM

MAALIM SEIF AJUMUIKA KATIKA FUTARI NA WAKAZI WA MAGOMENI MZIMUNI, DAR ES SALAAM

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi Cuf , Maalim Seif Shariff Hamad  akizungumza na wakazi wa Kata ya Mgomeni Mzimuni jijini Dar es salam ambao alijumuika nao katika futari ya pamoja iliyoandaliwa katika ofisi za umoja wa wabunge wa CUF iliyopo katika kata hiyo.
  Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi Cuf , Maalim Seif Sharif Hamad  akiomba dua pmoja na viongozi wengine waandamizi wa Chama Cha Wananchi CUF ambao walikusanyika kwa ajili ya futari katika kata ya Magomeni Mzimuni.
  Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi Cuf , Maalim Seif Sharif Hamad  akiwa ameketi katika kiti pamoja na Wanachama wengine wa CUF katika ofIsi za umoja wa wabunge wa Chama cha Wanachi CUF
 Baadhi ya wabunge wa Chama cha Wananchi CUF wakiwa wameketi wakifuturu futari iliyoandaliwa na kata ya Magomeni Mzimuni
  Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi Cuf , Maalim Seif Sharif Hamad  akiteta na Mwenyekiti wa Matawi ya CUF Rashid Abdullah mara baada ya kupata futari ya pamoja na wakazi wa Magomeni Mzimuni. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 05.06.2017


MICHUZI TV - PENALTI: YANGA SC 4 - 2 TUSKER FC, MICHUANO YA SPORTPESA SUPER CUP

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd aipongeza TFF

$
0
0
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, amempongeza Rais wa TFF Jamal Malinzi kwa kuhakikisha Zanzibar inapata uanachama wa FIFA.
"Mfikishie pongezi na shukurani zangu Bwana Malinzi kwa juhudi zake za kuhakikisha kuwa Zanzibar inapata uanachama wa FIFA", alisema Balozi Seif Idd mjini Zanzibar.
Akiongea na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Soka wa TFF, Derek Murusuri, katika ofisi za Baraza la Wawakilishi leo, Balozi Idd alisema Zanzibar inatambua juhudi zinazofanywa na Jamal Malinzi katika kuendeleza soka la Tanzania.
Alisema mafanikio ya Serengeti Boys kucheza AFCON ni mwelekeo mzuri wa ukuaji wa soka la Tanzania na uandaaji wa timu shindani ya Taifa.
"Tulikuwa na Mbunge mmoja wa Zanzibar aliyekuwa analipigia kelele sana suala hili. TFF imehakikisha Zanzibar inapata uanachama wa CAF na sasa tunatafuta FIFA," alisema.
Bw Murusuri alimwambia Makamu huyo wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa tayari TFF imeshapeleka maombi ya Zanzibar kufikiriwa kupatiwa uanachama wa FIFA.
Alisema TFF tayari imeanza mkakati wa kuiandaa timu ya Taifa itakayatafuta kufuzu kucheza Kombe la Dunia mwaka 2026. Mtendaji Mkuu huyo ameishukuru Zanzibar pamoja na watanzania wote kwa kujitokeza kuichangia Serengeti Boys kucheza AFCON 2017 huko GABON.
Amewasihi waendelee kuuchangia mfuko wa maendeleo ya Soka ili usaidie kufanikisha maandalizi ya timu mpya ya Serengeti Boys, Ngorongoro Heroes (U20) na Kilimanjaro Warrious (U23).
Katika ziara hiyo, Bw Murusuri aliambatana na Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation (TMF), Bw Ernest Sungura ambapo makamu wa Rais ametoa pongezi kwa taasisi hiyo kuvisaidia vyombo vya habari vya Zanzibar na Tanzania kujenga uwezo wa utendaji wa kazi zao.

 Makamu  wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd katika mazungumzo na Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation (TMF), Bw Ernest Sungura katika ofisi za Baraza la Wawakilishi, Zanzibar
  Makamu  wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd katika mazungumzo na Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation (TMF), Bw Ernest Sungura  na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Soka wa TFF, Derek Murusuri, katika ofisi za Baraza la Wawakilishi, Zanzibar
Makamu  wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akiongea na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Soka wa TFF, Derek Murusuri, katika ofisi za Baraza la Wawakilishi mjini Zanzibar.

MAKALA YA SHERIA: JE, ULIPEWA NOTISI YA SIKU 60 KABLA BENKI HAIJAUZA NYUMBA/KIWANJA CHAKO ?.

$
0
0

Na  Bashir  Yakub.

Wanaokopa  hela  kwenye  taasisi  za  fedha  wanatakiwa  kujua  haki  walizonazo. Haki  kabla  ya  kuchukua mkopo,  haki  wakati  wa  kuchukua  mkopo,  haki  wakati  wa  kurejesha,  na  haki  baada  ya  kurejesha au  kushindwa  kurejesha. Hautakiwi  kusubiri  taasisi  iliyokukopa  iwe ndiyo ya  kukueleze  haki  ulizonazo  bali  watakiwa ujue   haki    hizo  kwa  jitihada  zako.

Taasisi  ya  fedha  inaweza  kukueleza  baadhi  ya  haki  lakini  ni  muhali  kukueleza  haki  ambazo  wao  zinawabana. Watakueleza haki  ambazo  hazina  madhara  kwao.  Basi  yakupasa  ulijue  hili.

Masuala  ya  kuweka  rehani  ili  upate  mkopo  yanaongozwa  na  sheria  mbili.  Sheria  namba  4  ya  mwaka  1999    Sheria  ya  ardhi,  pamoja  nayo  Sheria  namba  17  Sheria  ya  rehani  ya  mwaka  2008. Humo  zimo haki  nyingi  za  mtoa  mkopo   wakadhalika  mchukua  mkopo.  Hata  hivyo  tutatizama  haki  moja  tu ya   notisi  kabla  ya  kuuzwa kwa   nyumba/kiwanja  cha  mkopaji.      


1.KUSHINDWA  KUREJESHA  MKOPO.

Kifungu  cha  127 ( 1 ) cha  sheria  ya  ardhi  kinaeleza   habari  ya  kushindwa  kurejesha  mkopo. Kifungu  kimeieleza  habari  hii  ikiwa  miongoni  mwa  mambo  ambayo  yanachukuliwa  kama ukiukwaji wa  masharti  ya  mkataba  wa  mkopo.  Mengine  ambayo  yanachukuliwa  kama  ukiukwaji  wa  masharti   ya  mkopo  ni  kuweka  rehani  mara  zaidi  ya  mmoja  kwa  taasisi  tofauti, kuuza, kupangisha  wakati  kuna  rehani  bila  taarifa   au  ridhaa kutoka  kwa  mtoa  mkopo n.k.  Hata  hivyo   haya  na  mengine  yatachukuliwa  kama  kukiuka  masharti  ya  mkopo  ikiwa  yamekatazwa  katika  mkataba  wako  na  taasisi  ya  fedha.

Pia  kwa  mujibu  wa  kifungu  hicho  kushindwa  kurejesha  mkopo  kunajumuisha  pesa  kamili  uliyoikopa,  riba, pamoja  na  makato  mengine  ambayo  yanajenga  sehemu  ya  mkopo.


MAGAZETI YA LEO JUMANNE JUNE 6,2017

MWILI WA HALILA TONGOLANGA WAAGWA

$
0
0
Halila Tongolanga amefariki jana usiku katika hospitali ya Muhimbili. Alikuwa mwanamuziki wa siku nyingi na alifahamika kwanza kwa wengi baada ya kuanza kusikika kibao chake cha lugha ya Kimakonde cha Kila munu ave na kwao, chenye tafsiri ya ‘Kila mtu ana kwao’ ambacho alikirekodi akiwa bendi ya jeshi ya CTU Monduli, iliyojulikana kama Les Mwenge.
 Kwa kifupi ni kuwa baada ya hapo aliitwa kujiunga na bendi iliyokuwa mali ya Dr Alex Khalid, iliyokuwa ikiitwa Makondeko Six. Wakati huo Dr Khalid alikuwa na sehemu kubwa ya burudani iliyokuwa pia na ukumbi na ilikuwa inaitwa Makondeko ikawa na bendi ya watu sita hivyo bendi hiyo ikaitwa Makondeko Six. 
Bendi hii awali ilikuwa ikipiga muziki kwa kufuata nyayo za bendi ya Tatu Nane, lakini Dr Khalid baada ya kuona bendi haina umaarufu kutokana na aina ya muziki iliyokuwa ikipiga, ndipo alipomuita Halila Tongolanga nae akaja na baadhi ya wanamuziki wakajiunga na kuanzisha kundi lililoendelea kutumia jina la Makondeko Six japo wanamuziki walikuwa wengi zaidi ya sita. 
Na ndipo katika kundi hili lilikuwa na wanamuziki wengine kama Innocent Nganyagwa, Anna mwaole wakaweza kurekodi tena wimbo wa Kila Munu Ave na kwao na kundi kupata umaarufu mkubwa mpaka baada ya kusambaratika kwa Makondeko baada ya kifo cha Dr Alex Khalid, lakini Tongolanga aliendelea kutumia jina la Makondeko. 

Tongolanga amefanya kazi nyingi za muziki ikiwemo kuwa mmoja wa kundi lililoundwa na wanamuziki wengine mahiri kama Moshi William, Muhidin Mwalim, Huluka Uvuruge, Kandaya na wengine lililojulikana kama Bana mwambe, ambapo waliweza kutoka nyimbo nyingi nzuri sana wakati biashara ya kuuza album ilipokuwa ina faida. 
 
Balozi wa Msumbiji Bi Monica Patricio Clemente akiaga sanduku lililokuwa na mwili wa Halila Tongolanga
Baadhi ya wanamuziki waliowahi kufanya kazi na Tongolanga katika kundi la makondeko Six, wakiwa wanasubiri kusafirisha mwili wa mpendwa wao.Toka kushoto, Innocent Nganyagwa, Meneja wa bendi, mpiga solo, Waninga 


John Kitime, wanamuziki wa Makondeko Six, Mngereza, Kumburu


Toka kushoto Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Nyangamale, Balozi wa Msumbiji nchini, Katibu Mtendaji wa BASATA, Mbunge wa Tandahimba Mhe Katani Katani, afisa wa Ubalozi wa Msumbiji ,Tongolanga anategemewa kuzikwa kijijini kwao Mchichila kesho Junanne 6 Juni 2017.
Mungu Amlaze Pema Halila Tongolanga .


Viewing all 110021 articles
Browse latest View live




Latest Images