Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1728 | 1729 | (Page 1730) | 1731 | 1732 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


  Shindano la Sprite Bball Kings 2017  limeingia katika hatua ya 16 baada ya timu 52 kukipiga wikiendi hii ikiwa ni ufunguzi wa michuano hiyo.

  Michezo hiyo 26 iliyochezwa katika viunga vya viwanja vya Jakaya M Kikwete Park (JKM Park) na kuzikutanisha timu hizo 52 katika mechi 26 za mtoano na 16 kufanikiwa kuingia hatua inayofuata.

  Akitoa tathmini ya michuano hiyo Mratibu wa Sprite Bball Kings Basilisa Biseko amesema kuwa hatua ya mtoano imefanyika wikiendi hii na timu 16 kufanikiwa kuingua hatua inayofuata ila katika mechi hizo kuna baadhi walipewa ushindi wa mezani.

  Basilisa amesema kuwa kuna baadhi ya timu hazikufanikiwa kufika siku hiyo na  ratiba ilikuwa tayari imeshapangwa katika droo iliyokuwa imepangwa na kupelekea timu iliyokuwa imefika uwanjani kupatiwa ushindi wa mezani.


  "Katika michezo 26 iliyochezwa siku ya Jumamosi katika viwanja vya JMK Park timu 16 zimefanikiwa kuingia hatua ya 16 bora, ila kuna timu zingine zimeingia kwenye hatua hiyo bila kucheza na timu pinzani kutokana na mpinzani wake kutokufika na kupelekea kupewa alama zitakazomruhusu kuingia hatua inayofuata,"amesema Basilisa.

  Amesema kuwa, kwa timu zilizopata alama nyingi ndizo zilizofanikiwa kuingia katika hatua ya 16 bora na mashindano hayo yataendelea tena ili kumpata mshindi wa Sprite Bball Kitaa kwa mwaka 2017.

   Timu zilizofuzu kuingia hatua ya 16 bora katika shindano la Sprite Baball Kings 2017 ni DMI, Dream Chaser, UDSM, Oysterbay, Ukonga Warriors, The Fighter, Ardhi na Bongo Hits.Timu zingine ni Chanika Legends, Montfort, Heroes S/B, Kigamboni Heroes, TMT, Mchenga, Kurasini na Landforce.

  Mashindano ya Bball Kings mwaka huu yanadhaminiwa na Sprite wakishirikiana na kituo cha East Africa Redio na TV  na yalizinduliwa mapema mwezi wa tano na kuanza usaili kwa wilaya za Teemek, Kindondoni na Ilala na kupata timu 4.52 zilizojitokeza kushiriki shindano hilo.
  Timu ya mpira wa kikapu ya UDSM wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mtanange wao.
   Timu ya mpira wa kikapu ya UDSM (jezi ya njano) wakipambana katika hatua ya mtoano ya shindano la Sprite Bball Kings iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii katika viwanja vya  Jakaya M Kikwete Park (JKM Park).
   Mashabiki na timu zingine zilizoshiriki katika  hatua ya mtoano ya shindano la Sprite Bball Kings iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii katika viwanja vya  Jakaya M Kikwete Park (JKM Park) wakiwa jukwaani wakifuatilia baadhi ya michezo mingine.
  Timu za mpira wa kikapu wakiwa wanachuana katika shindano la Sprite Bball Kings iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii katika viwanja vya  Jakaya M Kikwete Park (JKM Park).
  Kamishna wa Ufundi na Uendeshaji Mashindano wa chama Shirikisho la Mpira wa Kikapu (TBF) na Mratibu  wa Sprite BBall Kings Manase Zablon  (kushoto) akiwa pamoja na mtangazaji wa East African Drive David Rweganyira wakichambua baadhi mechi zilizokuwa zikiendelea.

  0 0

  Na Dickson Mulashani

  Mkuu wa wilaya Ilala Mh. Sophia Mjema amekipongeza Chuo cha St Mark (Chuo Kikuu Kishiriki Cha St Joseph) kwa jitihada za kutoa elimu bora kwa manufaa ya wilaya na Taifa kwa ujumla alipofanya ziara ya kikazi chuoni hapo mwishoni mwa juma.

  Akiwasili chuoni hapo Mh. Sophia Mjema alikuwa ameambatana na ujumbe wa timu ya wataalamu katika ngazi mbalimbali a wilaya ya Ilala akiwemo Mratibu Mwadamizi wa Polisi, Mshauri wa Majeshi ya akiba, Mratibu wa Magereza, Mhandisi , Afisa uhamiaji, Afisa Elimu Taaluma, Afisa mipango miji, Afisa ustawi wa jamii, Afisa wa Benki ya NMB, Afisa Tarafa, Diwani pamoja na Mwenyekiti wa mtaa.

  Akimkaribisha mgeni huyo, kaimu Mkuu wa Chuo Dr.Peter Kopweh alianza kwa kuelezea historia fupi ya chuo hicho kilichopo eneo la Buguruni Malapa jirani na shule ya msingi viziwi, kuwa ni sehemu ya Chuo Kikuu cha St. John’s chenye makao yake makuu mjini Dodoma ambacho kinatoa kozi katika ngazi astashada na shahada za sanaa katika elimu, utawala wa biashara, rasilimali watu, elimu na biashara pamoja na theolojia mathalani shahada ya uzamili katika elimu hili kwa ushirikiano na kampasi mama ya Dodoma.

  Sambamba na ukaribisho huo Dr. Kopweh hakusita kuelezea Changamoto zinazokikabili chuo hicho zikiwemo za miundombinu ya barabara, usalama wa mali pamoja na wadau wake kadhalika suala la mipaka ambayo inaonekana kuingiliwa na wakazi wanaozunguka chuo hicho.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akizungumza na wanajumuiya ya Chuo cha St. Mark kilichopo Buguruni Malapa alipofanya ziara ya kikazi chuoni hapo.Kulia kwake ni Makamu Mkuu wa Chuo Dr. Peter Kopweh na kushoto ni Mshauri wa majeshi ya akiba Chripin Makota.
  Wanajumuiya ya Chuo cha St. Mark kilichopo Buguruni Malapa wakimsikilia Mh.Sophia Mjema alipofanya ziara ya kikazi chuoni hapo.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akianza ziara kuzuru maeneo mbalimbali yaliyopo katika mazingira ya chuo cha St.Mark akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama pamoja na timu ya wataalamu wa wilaya ya Ilala.


  0 0

  Na Jonas Kamaleki- MAELEZO.

  Viongozi wa Dini wanajiandaa kumpa tuzo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi kwa utendaji mzuri uliojaa ubunifu na uwajibikaji.

  Hayo yameelezwa katika mahojiano maalum jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maadili na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Dini zote Tanzania, Askofu William Mwamalanga.

  Askofu Mwamalanga amesema kuwa Waziri Lukuvi amekuwa kiongozi imara katika kufuatilia masuala yanayohusu ardhi ikiwemo utatuzi wa migogoro ambayo imedumu kwa muda mrefu.

  “Lukuvi ameing’arisha Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuendana na kasi ya Rais John Pombe Magufuli, hakika amevaa viatu vya Magufuli, hivyo tumeamua kumpa tuzo maalum kwa ajili utendaji wake”, alisema Askofu Mwamalanga.

  Ameeleza kuwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imefanya jambo zuri kwa kutoa elimu ya ardhi kiasi kwamba karibu kila mtu amefahamu matumizi ya ardhi na umuhimu wake.

  Askofu Mwamalanga amesema kuwa ardhi imefanywa kuwa lulu na kufanya sura mpya ya ardhi kuonekana ambapo takriban asilimia 85 ya Watanzania wameiona kuwa ni mali.

  Mhe. Lukuvi amewapa nafasi ya kwanza wananchi kuliko Sheria jambo ambalo limewafanya Watanzania kujisikia kuwa wanathaminiwa na Serikali yao, aliongeza Askofu Mwamalanga.  0 0

  Mwenge wa Uhuru umekabidhiwa rasmi wilaya ya Mkuranga ukitokea wilaya ya Rufiji huko mkoani Pwani na umetembelea miradi 11 ya Maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi billion 24.7.

  Akizungumza wakati wa kubadhiwa mwenge wa Uhuru mkuu wa wilaya ya Mkuranga, Filibeto Sanga amesema miradi hiyo 11 iliyotembelewa ni pamoja na afya, elimu, kilimo na mradi wa ujasilia Mali kwa vijana.

  Aidha katika miradi hiyo kumi na moja mwenge wa Uhuru umezindua miradi mitatu ambayo ni huduma ya upasuaji katika kituo cha afya Kilimahewa, kufungua nyumba za walimu katika shule ya sekondari Mkugilo pamoja na kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Mwanambaya wilayani humo.

  Kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2017 Amour Hamadi Amour ametoa wito kwa watanzania kuwa na uzalendo wa kuthamini vya kwao ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi na kuifanya Tanzania ya viwanda.

  Kiongozi huyo ameongeza kuwa katika kuelekea nchi ya viwanda ni vyema Watanzania wakawa na utamaduni wa kutumia bidhaa za ndani ili kukuza uchumi wa nchi na taifa kwa ujimla.

  Hata hivyo mbio hizo za mwenge wa Uhuru wilayani mkuranga mkoani Pwani zimeudhuriwa na watendaji mbalimbali wa Halmashauri hiyo akiwemo Mkurugenzi injinia Mshamu Munde na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Juma Abeid.
   Mkuu wa Wilaya ya mkuranga, Filibeto Sanga (kulia) akipokea mwenge wa uhuru kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Rufiji Juma Abdalah tayari kwaajili ya kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya hiyo.mkoani Pwani.
   Mganga mkuu Wilaya ya Mkuranga Dkt.Steven Mwandambo wa (kwanza kulia) akitoa maelekezo mbele  ya viongozi wengine ya namna chumba upasuaji kitakavyo saidia kinamama wajawazito kijiji cha kilomahewa.mkoani Pwani. 
   Kiongozi Mkuu wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa,Amour Hamad Amour akizindua nyumba za walimu katika shule ya Sekondari Mkugilo mkoani Pwani.
   Kiongozi Mkuu wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa,Amour Hamad Amour akipanda mti katika shule ya Sekondari Mkugilo mkoani Pwani ikiwa  ni ishara ya kuhimiza wananchi kutunza na kuhifadhi mazingira.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Baadhi ya wananchi wakiteremka katika Kivuko cha MV. KAZI mara baada ya kukabidhiwa rasmi kwa Serikali mapema hii leo Magogoni jijini Dar es Salaam toka Kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd. Iliyokuwa ikikijenga Kivuko hicho.


  Picha na MAELEZO

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd. Bw. Major Songoro (kulia)  wakati wa makabidhiano ya Kivuko cha MV. KAZI mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Mtendaji Mkuu toka Wakala wa Ufundi na Umeme  (TEMESA) Dkt. Mussa  Mgwatu.

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kulia) akizungumza na baadhi ya wananchi waliopanda Kivuko cha MV. KAZI mara baada ya kukabidhiwa kwa Serikali toka kwa  Kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd. Iliyokuwa ikikijenga Kivuko hicho.

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliana Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akizungumza na mmoja  ya mkazi wa Kigamboni wakati wa kukabidhiwa kivuko cha MV. KAZI kwa Serikali toka kwa Kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd. Iliyokuwa ikikijenga Kivuko hicho.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliana Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akizungumza na mmoja  ya mkazi wa Kigamboni wakati wa kukabidhiwa kivuko cha MV. KAZI kwa Serikali toka kwa Kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd. Iliyokuwa ikikijenga Kivuko hicho.

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea ujumbe kutoka kwa Mjumbe Maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Leonard  She Okitunda alipofika Ikulu jijini Dar es salaam kuwasilisha ujumbe huo leo Juni 5, 2017.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na  Mjumbe Maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Leonard  She Okitunda na ujumbe wake na wa Tanzania alipofika Ikulu jijini Dar es salaam kuwasilisha ujumbe huo leo Juni 5, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Ibrahim Al Najem alipofika kumtembelea Ikulu jijini Dar es salaam  leo Juni 5, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia malori mawili ya kuzolea taka baada ya kumaliza mazungumzo na Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Ibrahim Al Najem alipofika kumtembelea na kukabidjhi msaada wa magari hayo Ikulu jijini Dar es salaam  leo Juni 5, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimlaki Mjumbe Maalumu wa Rais wa Msumbiji na Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Jenerali  Atanasio Salvador Ntumuke alipofika Ikulu jijini Dar es salaam kuwasilisha ujumbe huo leo Juni 5, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wajumbe walioongozana na Mjumbe Maalumu wa Rais wa Msumbiji na Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Jenerali  Atanasio Salvador Ntumuke alipofika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi ujumbe maalumu leo Juni 5, 2017.PICHA NA IKULU.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Ramadhani Ali – Maelezao Zanzibar.

  Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wameshtushwa na idadi kubwa ya vifo vinavyotokana na homa ya Ini wakati wananchi wengi hawana uelewa juu ya maradhi hayo na Serikali haijaandaa mikakati imara ya kupambana nayo.

  Wajumbe hao walieleza hisia zao wakati wakichangia mada ya hali halisi ya homa ya Ini katika mkutano wa kushajihisha wajumbe hao kuhusu maradhi ya Kifua kikuu, Ukimwi na Homa ya Ini ulioandaliwa na Kitengo Shirikishi cha maradhi hayo katika Hoteli ya Ocean View Kilimani.

  Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Rashid Makame Shamsi alisema wakati homa ya Ini inaongoza kwa kusababisha vifo vingi zaidi ikilinganisha na maradhi mengine haikuzungmzwa katika Bajeti ya mwaka huu ya Wizara ya Afya.

  Amesema kukosekana taarifa ya homa Ini ndani ya Bajeti ya Wizara huku wananchi hawana uelewa juu ya homa hiyo itapelekea kuenea kwa kasi na kupoteza maisha ya wananchi.

  Mwakilishi wa kuteuliwa Ahmada Yahya ameishauri Wizara ya Afya kupitia Kitengo Shirikishi kutoa taaluma zaidi kwa wananchi ili kuwa na uelewa mpana wa homa ya Ini na njia za kujikinga nayo.

  Spika wa Baraza la Wawakilishi ambae alikuwa Mwenyekiti wa mkutano huo ameishauri Kamati ya Bajeti ya Baraza hilo kuangalia uwezekano wa kukipatia fedha Kitengo Shirikishi cha Ukimwi, Kifua Kikuu na homa ya Ini ili kiweze  kukabiliana nayo.
   Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akitoa maelezo kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika mkutano wa kushajihisha wajumbe hao kuhusu kifua kikuu, Ukimwi na homa ya Ini katika Hoteli ya Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar.
   Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid ambae alikuwa Mwenyekiti wa mkutano huo akiufungua rasmi katika Hoteli ya Ocean View (kulia) Mnadhimu wa Baraza  Ali Salim Haji na (kushoto) Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo.
   Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia ufunguzi wa mkutano wa kuwashahishaji kuhusu Kifua kikuu, Ukimwi na homa ya Ini uliofanyika Hoteli ya Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

    Kaimu Mkurugenzi  Idara ya  ya Uongozaji ndege na Huduma(ANS), John Chambo akizungumza kwenye mkutano wa mwaka wa Idara ya Uongozaji ndege uliofanyika Mkoani Morogoro.

   Wajumbe wakiwa kwenye mkutano wa mwaka wa Idara ya Uongozaji ndege na Huduma(ANS) wakifuatilia mkutano.

  0 0  0 0

  Mafunzo hayo ya siku mbili Juni 5 na 6, 2017, yanafanyika katika ukumbi wa Vigirmark Hotel mjini Shinyanga, na yamekutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi kutoka PS3, TAMISEMI, Wizara ya Afya, Wizara ya Elimu, na wakufunzi kutoka mikoa mbalimbali ambako mradi unatekelezwa. 

  Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo, Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela, alisema mfumo wa FFARS utasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuhakikisha kuwa vituo vya kutolea huduma vinakusanya na kuhifadhi taarifa za mapato na matumizi zilizotengwa na Serikali kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya vituo hivyo ili wananchi waweze kupata huduma bora. 

  “Ikumbukwe kuwa Mheshimiwa Rais katika kutekeleza mpango wa elimu bila malipo aliamuru kuwa fedha za ruzuku za gharama za uendeshaji wa shule lakini pia vituo vya kutolea huduma zitapelekwa moja kwa moja katika vituo hivyo, hivyo basi usimamizi wa ruzuku hizo utafanywa na vituo husika,” alieleza Msovela. 

  “Lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo ili kuhakikisha kuwa vituo vyetu vya kutolea huduma kupitia fedha za ruzuku vinakuwa na mfumo maalum wa kuandaa taarifa za mapato na matumizi, hali ambayo itachangia uwajibikaji na utoaji wa huduma bora kwa wananchi,” aliongeza Msovela. 

  Aidha, alisema Serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa na PS3 katika kuunganisha wadau, na kuongeza kuwa ni wakati mzuri watanzania wakaiga mfano wa nchi kama Marekani ambao wapo mbele zaidi katika masuala ya uwazi na utawala bora katika kuwapa taarifa wananchi zinazohusu maeneo yao. 
  Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela, amefungua mafunzo ya mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and Reporting System – FFARS) kupitia mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ‘ Public Sector Systems Strengthening – PS3’.
  Mgeni rasmi, Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela, akifungua mafunzo kuhusu mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and Reporting System – FFARS) katika ukumbi wa Vigirmark Hotel mjini Shinyanga 
  Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela, akifungua mafunzo mafunzo kuhusu mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa kwa wakufunzi zaidi ya 130 kutoka mikoa ya kanda ya ziwa na kati waliohudhuria mafunzo hayo.
  Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela, akizungumza ukumbini. Kulia ni Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi TAMISEMI, Elisa Rwamiago, na kushoto ni Mkuu wa Idara ya Ufuatiliaji, Tathmini na Tafiti Tendaji kutoka PS3, Dkt. Suma Kaare .


  0 0

    Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema  akimkabidhi  kombe Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Osterbay Zefrin Lubuva kuwa  mshindi wa Mazingira.
   Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema  akizungumza katika  maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani,yaliyofanyika viwanja vya Mnazi mmoja,jijini Dar es Salaam leo.
    Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema  akikabidhi cheti kwa Mwandishi wa ITV , Benjamini Mzinga kuwa mmoja wa wadau makini katika utunzaji wa Mazingira
   Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akizungumza katika mkutano wa kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja wa Dar es Salaam.


  0 0


  Serikali Mpya ya Lesotho yashauriwa kutekeleza Mageuzi - SADC

  Serikali itakayoingia madarakani baada ya Uchaguzi wa Wabunge uliofanyika nchini Lesotho Julai 3, imeshauriwa kutekeleza kikamilifu na kwa nia ya dhati maazimio yote ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC yanayohusu mageuzi kwenye sekta muhimu za katiba, sheria na mahakama, ulinzi na usalama, utumishi na sekta ya umma na vyombo vya habari kwa muda muafaka ili kuimarisha utawala bora na wa kidemokrasia nchini humo. 

  Mnamo mwezi Machi mwaka 2017, baada ya Mfalme Letsie wa III wa Lesotho kutangaza tarehe ya uchaguzi mkuu, kikao cha juu cha maamuzi cha Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC Summit), kilielekeza Serikali mpya itakayoshinda uchaguzi na kuingia madarakani, itekeleze maazimio hayo kwa kuweka muda maalum na vigezo vya utekelezaji ili kuepuka chaguzi za mara kwa mara. 

  Msimamo huo wa Jumuiya ya SADC umetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Mheshimiwa Augustine P. Mahiga, Mwenyekiti wa Kamati ya Asasi ya Ushirikiano ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC alipokuwa akitoa taarifa ya awali ya timu ya uangalizi siku mbili baada ya zoezi la upigaji kura kukamilika. 

  Mheshimiwa Mahiga alisema, japokuwa zoezi la kuhesabu kura bado linaendelea, ni dhahiri kuwa wapiga kura nchini Lesotho wanatarajia mageuzi makubwa kutoka kwenye Serikali mpya yatakayoandika historia mpya nchini Lesotho, ambayo imafanya chaguzi tatu kuu ndani ya miaka mitano. 

  Mapendekezo mengine yaliyotolewa kwenye taarifa hiyo ya awali ya SADC yanaitaka Serikali mpya kupitia na kufanyia mageuzi mfumo mzima wa uchaguzi ambao kwa sasa unatoa fursa kwa wabunge kuhama chama bila kupoteza ubunge wao (Floor Crossing). Alisema mfumo huo unayumbisha mfumo wa siasa na wa kibunge kwenye Falme ya Lesotho. 
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Mkuu wa Timu ya waangalizi ya SADC ya uchaguzi wa Lesotho akiwasilisha taarifa ya awali kuhusu uchaguzi huo .
  Waziri Mahiga akiendelea kuwasilisha taarifa ya awali ya uchaguzi wa Lesotho jijini Maseru .
  Waziri Mahiga bado anasoma taarifa ya awali ya uchaguzi wa Lesotho kwa wajumbe.   0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  WIZARA ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wameanzisha siku ya mazingira kwa kufanya usafi katika eneo la Mabibo sokoni leo jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi ,Mawasiliano na Uchukuzi-Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho amesema katika uchafuzi wa mazingira sekta ya uchukuzi inachangia kutokana na magari kwa kutoa moshi mchafu.

  Amesema katika kuadhimisha siku hiyo kwa sekta ya uchukuzi ni lazima kuchukua hatua katika ulinzi wa mazingira katika vyombo vya moto kafanyia ukaguzi.

  Dk. Chamuriho amesema kuwa katika kuendana na sera ya viwanda ni lazima kufanya mazingira kuwa bora ya kuweza kuwavutia wawekezaji mbalimbali .

  Aidha amesema kuwa katika maadhimisho ya mwaka huu iwe ni chachu kwa kila mdau wa wa uchukuzi kuwa mtu wa kwanza katika ulinzi wa mazingira.
  Nae Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji Nchini (NIT), Profesa Zakaria Mganilwa amesema kuwa katika maadhimisho hayo wamedhamiria kuwa sehemu mhimu wa kutunza mazingira.

  Katika maadhimisho hayo taasisi zilizo chini ya Uchukuzi zimeweza kufanya usafi katika soko la mabibo pamoja na kupanfa miti katika chuo hicho kwa kuungana na shule ya msingi mpakani.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi ,Mawasiliano na Uchukuzi-Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho akzingumza katika siku ya maadhimisho ya Mazingira Duniani juu sekta ya uchukuzi kuwa sehemu ya kulinda mazingira.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi ,Mawasiliano na Uchukuzi-Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho akipanda mti mti katika chuo cha NIT katika Maadhomisho ya siku ya Mazingira duniani leo jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Viwanja vya Ndege Mikoani , Valentine Kadeha akipanda mti katika chuo cha NIT katika maadhimisho ya siku ya mazingira duniani leo jijini Dar es Salaam.
  Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wakiwa katika usafi katika soko la mabibo katika mti katika maadhimisho ya siku ya mazingira duniani leo jijini Dar es Salaam.

  0 0


  Sanduku lenye Mwili wa Marehemu wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Marehemu Phillemon Ndesamburo,ukiandaliwa tayari kwa kuagwa katika uwanja wa Majengo,mjini Moshi mkoani Kilimanjaro mapema leo mchana.
    Gari lililobeba mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo lilielekea katika viwanja vya Majengo kwa ajili ya kuagwa mwili huo.
  Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akiwapungia mkono wananchi waliofika kwenye uwanja  huo mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Majengo kwa ajili ya kuagwa mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Marehemu Phillemon Ndesamburo.
  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akiwasili katika viwanja vya Majengo kwa ajili ya kuagwa mwili wa  aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Marehemu Phillemon Ndesamburo.
  Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiwa wamebeba jeneza lililobeba mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Marehemu Phillemon Ndesamburo. 

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Frank Mvungi-Maelezo.

  Takriban wakazi 234,398 wa  Chalinze watanufaika na  mradi wa upanuzi wa mtambo na ujenzi wa mfumo wa kusafirisha na kusambaza maji safi pamoja na matenki ya kuhifadhi unaolenga kuondoa changamoto ya upatikanaji wake katika Jimbo hilo.

  Akizungumza  kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa hafla ya kukagua maendeleo ya mradi  huo, Waziri wa Maji na Umwagiliaji,  Mhandisi Gerson Lwenge amesema kuwa Serikali inaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo na kumtaka mkandarasi kuongeza kasi katika kutekeleza mradi huo.

  “Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maji safi na salama ndio maana tumeweka wataalamu wetu hapa kumsimamia mkandarasi ili afanye kazi  kwa ubora na kwa kasi kama ambavyo Waziri Mkuu aliagiza alipotembelea mradi huu mwezi Machi mwaka huu”, alisisitiza Lwenge.

  Akifafanua, Mhandisi Lwenge amesema kuwa hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa  mradi huo awamu ya tatu ni ulazaji wa mabomba ya kusafirisha na ya kusambaza maji, ujenzi wa matanki 19, na ujenzi wa  mtambo wa kusafishia maji ambao unaendelea. 

  Kazi nyingine zinazoendelea katika kutekeleza mradi huo ni ujenzi wa vituo 351 vya kuchotea maji ambapo vituo 27 vimekamilika,vituo 226 vipo katika hatua mbalimbali na vituo 98 havijaanza kujengwa.

  Akizungumzia hatua zinazochukuliwa na mkandarasi wa mradi huo, Mhandisi Lwenge amesema kuwa ni kuongezeka kwa upatikanaji wa vifaa kwa wakati katika eneo la mradi, kuongeza wafanyakazi na maeneo ya kazi na kuteua mwakilishi wa kampuni anayeweza kutoa maamuzi kwa niaba ya kampuni inayotekeleza mradi.

  Aidha, Waziri Lwenge amesema kuwa Serikali itatoa ufumbuzi wa changamoto ya wananchi wa Jimbo hilo kulipia malipo ya huduma  (service charge) hata pale wanapokuwa hawajapata huduma hiyo ili kuwe na utaratibu mzuri unaowezesha wananchi kulipia huduma pale wanapotumia tu na si vinginevyo.
   Moja ya tenki la maji linalojengwa katika chanzo cha maji cha mto Ruvu ikiwa ni sehemu ya mradi huo.
   Mbunge wa Jimbo la ChalinzeChalinze, Mhe. Ridhiwan Kikwete akimshukuru Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Mhandisi Gerson Lwenge kwa hatua nzuri iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo.

  Mafundi wakiendelea na maandalizi ya ujenzi wa matenki yakuhifadhi maji katika chanzo cha maji Ruvu. (Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo).

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0

  Amesema anaamini kuwa kwa wananchi kushiriki watashawishika kuendelea kuishi kwenye maeneo hayo na kuyaenzi.

  Amesema kitendo hicho kidhati kitakuwa kimewaunganisha watu na asili na hivyo kuondoa dhana ya zamani ya kuweka maeneo hayo mbali na watu.

  “Inaweza kuwa vigumu kuamini sasa, lakini miaka hamsini iliyopita ilidhaniwa kuwa njia bora ya kulinda asili ni kuiweka mbali na watu ...Hii leo, tunajua vyema zaidi kwamba kwa kadri uhusiano baina ya watu na mazingira yao unavyokuwa wa karibu zaidi ndivyo watu wanavyofahamu zaidi juu ya umuhimu wa asili na viumbe hai, urithi na maji, kwa ajili ya ustawi wao binafsi na kwa ajili ya hali ya baadaye ya sayari yetu.” Alisema.

  Mkuu huyo alisema hayo akizungumzia umuhimu na uhifadhi kwa maeneio zaidi ya 2000 duniani ya bayongahewa, maeneo ya hifadhi ya jiolojia ya na maeneo ya Urithi wa Dunia yanayodhaminiwa na UNESCO.

  Alisema maeneo hayo pamoja na kuhifadhi urithi wa dunia pia hutoa ajira kwa watu wanaoyazunguka na milango yake iko wazi kwa umma wote.

  “Maeneo ya hifadhi ya jiolojia ni vitabu vilivyo wazi vya kihistoria ambavyo huturudisha nyuma mamilioni ya miaka. Hifadhi za Bayongahewa ni mahali ambapo jamii hukabiliana na changamoto za maendeleo kwa kuunda njia mpya za kijamii na uchumi endelevu. Maeneo ya hifadhi ya jiolojia na hifadhi za Bayongahewa huunganisha uhifadhi na elimu kwa mbinu mpya ya maendeleo endelevu, kama vile utalii wa mazingira na kilimo hai.” alisema katika ujumbe wake kwa dunia.
  Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Bi. Irina Bokova, katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, leo ametaka wananchi mbalimbali kutenga muda binafsi na kutembelea moja ya maeneo ambayo ni urithi wa dunia yakifadhiliwa na UNESCO.  0 0

   Katibu  mkuu wa Chama cha Wananchi CUF ,Maalim Seif Sharif Hamad  akiwasili katika eneo la Vingunguti
    Katibu  mkuu wa Chama cha Wananchi CUF ,Maalim Seif Sharif Hamad akiwa ameketi kwenye kiti wakati alipojumuika kwenye futari na wakazi wa Vingunguti
   katibu mkuu maalim Seif Sharif Hamad akiwa amejumuika na  wakazi wa vingunguti katika futari katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani .
  katibu mkuu maalim Seif Sharif Hamad alijumuika na wakazi wa vingunguti katik futari  na wakazi wa vingunguti

  0 0


  NA KVIS BLOG/Khalfan Said

  MANISPAA ya Ilala jijini Dar es Salaam imesema iko kwenye mkakati mkubwa wa kutengeneza bustani za kupumzika wananchi na tayari wameanza kuboresha maeneo hayo kwa kuanzia na eneo bustani ya Samora (Kaburi la Sharif), barabara ya Samora.

  Akizungumza kwenye mdahalo wa mazingira uliotayarishwa na Taasisi ya Kilimanjaro Dialogue Institute ya jijini Dar es Salaam leo Juni 5, 2017, Afisa Mazingira wa Manispaa hiyo, Bi.Esther Masomhe, alisema, pamoja na vipaumbele vingi ambavyo Manispaa hiyo inakabiliwa navyo, lakini moja ya hatua inazochukua ni kupendezesha jiji, (City beatification).

  “Kuna maeneo tayari tumeanza nayo kama vile bustani ya Samora pale kaburi la Shariff, barabara ya Samora, bustani ya Mnazi Mmoja namba mbili eneo laMcahfukoge, tunakusudia kuiboresha bustani hiyo ili wananchi wapate mahala pazuri pa kupumzika.” Alisema Bi.Masomhe.

  Akifafanua zaidi alisema, Wilaya ya Ilala ndiyo kitovu cha jiji la Dar es Salaam hivyo Manispaa inachukuajuhudi mbalimbali kuhakikisha wilaya hiyo inakuwa katika muonekano mzuri kwa kuboresha mazingira na bustani zake.
  Afisa Mazingira wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, Bi.Esther Masomhe, (kulia), akizungumza jambo wakati wa mazungumzo ya meza ya duara kuhusu mazingira kwenye Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam Juni 5, 2017, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya mazingira duniani. Kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Kilimanjaro Dialogue Institute iliyoandaa majadiliano hayo, Bw. Habib Miradji. 
  Mwenyekiti wa mdahalo huo, ambaye pia ni mdhamini wa taasisi hiyo ya Kilimanjaro Dialogue Institute, (KDI), Bw. Habib Miradji
  Mshauri wa masuala ya vyombo vya habari, Bw. Felix Kaiza akisikiliza kwa makini mjadala huo.
  Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kilimanjaro Dialogue Institute (KDI), Bw.Hassan Mzighani, (kulia), akizungumza kwenye mdahalo huo ambapo alisema anasikitishwa na jinsi Manispaa inavyoshindwa kudhibiti maji taka, yakiwemo yale yanayosababishwa na mvua na kutolea mfano nchi kama Norway, ambayo hupata mvua muda mwingi lakini sio rahisi kukuta barabara au makazi ya watu yakiwa yamezingirwa na maji.  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi waache tabia ya kuhujumu miradi ya maendeleo ikiwemo ya wawekezaji kwani kufanya hivyo ni kurudisha nyuma jitihada za Serikali za kuharakisha shughuli za maendeleo za wananchi. 

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti wilayani Tarime mkoani Mara wakati akikagua miradi ya maendeleo, kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kiwanda cha chaki,kutembea eneo litakalojengwa kiwanda cha sukari na kwenye mkutano wa hadhara kijijini Biswari wilayani humo katika ziara yake ya kikazi ya siku Tatu mkoani Mara.

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema tabia ya wananchi kupinga kila kitu hata uwekezaji haifai hata kidogo kwani inachangia kuzorotesha shughuli za maendeleo hivyo ni lazima ikomeshwe.

  Amewataka wananchi kote nchini washirikiane na Serikali pamoja na wawekezaji wanaokuja nchini kuja kuwekeza kwani kufanya hivyo taifa litapata mapato na wananchi watapata ajira kwenye viwanda vitakavyojengwa nchini. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuzindua kiwanda cha kutengenezea Chaki cha Arwa kilichopo Tarime.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna chaki zinavyotengenezwa kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Arwa Bw. Tobias Raya mara baada ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda hicho kilichopo Tarime mkoani Mara. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna chaki zinavyotengenezwa kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Arwa Bw. Tobias Raya mara baada ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda hicho kilichopo Tarime mkoani Mara. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa kijiji cha Bisarwi kata ya Manga, Tarime  mkoani Mara.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais). 

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0  Benny Mwaipaja, WFM- Dar es Salaam.

  SERIKALI imeipatia Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), shilingi 209.5 bilioni kwa ajili ya kuendeleza Sekta ya Kilimo na Mifugo hapa nchini, leo, Jijini Dar es salaam.

  Akiongea kwa niaba ya Serikali wakati wa tukio la utiaji saini mkataba wa makabidhiano ya fedha hizo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu, alisema kuwa kiasi hicho cha fedha ambacho ni mkopo wenye masharti nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), ni sehemu ya shilingi 800 bilioni ambazo Serikali inatarajia kuipatia Benki hiyo ili iweze kukuza mtaji wake.

  “Ninaishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB kwa kuipatia Serikali mkopo wa Dola za Marekani 93.5 milioni ambazo ni sawa na kiasi hicho cha fedha cha Sh. 209.5 bilioni kwa ajili ya kuiongezea mtaji TADB ili iweze kuwafikia wakulima wengi zaidi kwa kuwapatia mikopo yenye riba nafuu” alisema Dkt. Kazungu.

  Alisema kuwa fedha hizo zitasaidia kutatua changamoto ya upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya sekta ya kilimo na mifugo ili kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo ili sekta hiyo iweze kuchangia zaidi katika ukuaji wa pato la Taifa kuliko ilivyo sasa.

  “Mwaka jana kilimo ambacho kinategemewa na idadi kubwa ya Watanzania kilichangia wastani wa asilimia 29.1 ya Pato la Taifa lakini tunataka kupitia Benki hiyo Sekta ya kilimo iiwezeshe nchi kukua kiuchumi kwa zaidi ya asilimia 7 hadi 10 katika kipindi kifupi kijacho” aliongeza Dkt. Kazungu.
  td1
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu akisaini mkataba wa kuipatia Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) fedha za kuiongezea mtaji kiasi cha shilingi bilioni 209.5. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw. Francis Assenga, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam
  td2
  Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sheria kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Eligius Mwankenja (kushoto), na Mchumi kutoka Wizara hiyo  Bw. Said Nyenge (kulia) wakiwaelekeza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB Bw. Francis Assenga, maeneo maalumu ya kutiwa saini kwenye Mkataba wenye thamani ya Sh. 209.5 bilioni utakaoiwezesha Benki hiyo kutoa mikopo ya muda wa kati na mrefu kwa riba nafuu kwa wakulima wadogo wadogo, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam
  td3
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto) akibadilishana mkataba na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania-TADB, Bw. Francis Assenga mara baana ya kusainiwa mkataba wa kuiongezea mtaji Benki hiyo wenye thamani ya Sh. Bilioni 209.5 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016/2021, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
  td4
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu wakionesha mkataba waliokwisha usaini kwa waandishi wa habari (hawamo pichani) na kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam
  td5
  Wajumbe waliohudhuria hafla ya utiaji saini mkataba wa kuiongezea mtaji Benki ya Kilimo wenye lengo la kuunganisha maboresho ya sekta ya kilimo na mpango wa mageuzi ya viwanda wenye thamani ya Sh. 209.5 bilioni, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.


older | 1 | .... | 1728 | 1729 | (Page 1730) | 1731 | 1732 | .... | 3285 | newer