Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110021 articles
Browse latest View live

Rais Kikwete ampongeza Askofu Mkude kutimiza miaka 25 ya Uaskofu

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza askofu Telesphori Mkude wa jimbo katoliki Morogoro wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 25 ya Uaskofu wake (Silver Jubilee)zilizofanyika katika viwanja vya St.Peters junior Seminary mjini Morogoro leo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu Katoliki wakati wa maadhimisho ya Sherehe za Miaka 25(Silver jubilee) ya Uaskofu wa Askofu Telesphori Mkude wa jimbo Katoliki Morogoro zilizofanyika katika Viwanja vya Seminary ya St.Peters mjini Morogoro leo.(picha na Freddy Maro)

balozi sef ali iddi akutana na kamati ya mapinduzi cup leo

$
0
0
Na Othman Khamis Ame
Timu zipatazo 13 za Mchezo wa Soka za Kitaifa na Kimataifa zinatarajiwa kushiriki katika mashirndano ya Kombe la Mapinduzi yanayotarajiwa kufanyika ndani ya kipindi cha Maadhimisho ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 2014. Hayo yamejiri wakati Uongozi wa Kamati ya Mapinduzi Cup ulipokutana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kumpatia taarifa kufuatia hatua za awali za maandilizi ya mashindano hayo yanayotarajiwa kuwa ya Kimataifa. 
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Sharifa Khamis alimueleza Balozi Seif kwamba Kamati hiyo imezingatia agizo la Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohd Sheni la kuzialika pia kwenye mashindano hayo Timu za Soka za China, Vietnam na Oman kutokana na uhusiano mzuri uliopo baina ya Zanzibar na Nchi hizo. Sharifa alizitaja baadhi ya timu nyengine zitakazoalikwa katika mashindano hayo kuwa ni pamoja na Yanga, Simba na Azam za Tanzania Bara, Tasker ya Kenya, URA ya Uganda, APR ya Rwanda na wenyeji wa mashindano hayo timu za KMKM,Jamuhuri na Chuoni. 
 “ Kamati yetu imeamua kuanza mapema maandalizi hayo kutokana na umuhimu wa sherehe zenyewe na kikao chetu cha kwanza tumefikia hatua za kufikiria njia za kupata fedha za maandalizi pamoja na timu tutakazozialika kushiriki mashindano hayo “. Alifafanua Sharifa Khamis. 
 Alieleza kwamba mashindano hayo yanatarajiwa kupangwa katika mfumo wa makundi mawili Unguja na Pemba ili kuwapa fursa wapenzi wa michezo kisiwani pemba kuona mashindano hayo. Naye mjumbe wa Kamati hiyo ambae pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Dr. Ali Mwinyikai alisema Kamati hiyo pia imefikiria kushirikisha michezo ya Pete pamoja na Riadha ili kuongeza vugu vugu la mashindano hayo.
 Dr. Mwinyikai alieleza kwamba Kamati hiyo imeanza hatua za kuwasiliana na baadhi ya wadau wa michezo ndani na nje ya Nchi katika hatua ya kuona mashindano hayo yanafanyika kwa mafanikio makubwa kulingana na maadhimisho yenyewe. 
 Katika kukifanyia maandalizi ya mapema kiwanja cha michezo cha Amani Mwinyikai alisema Kamati hiyo kwa kushirikiana na Wizara inayosimamia michezo Zanzibar wamefikiria kukiwekea nyasi bandia kiwanja hicho ili kiwahi kutumika katika mashindano hayo ya Mapinduzi Cup. 
 Alisema Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo imeweka kifungu maalum kitakachounga mkono kazi hiyo ndani ya makadirio ya Mapato na Matumizi yake kwa mwaka wa fedha endapo kitapita katika kikao cha baraza kinaoendelea. 
 Akitoa shukrani zake kwa hatua iliyofikiwa na Kamati hiyo kwa kuanza vizuri maandalizi hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na yeye binafsi itajitahidi kuunga mkono Kamati hiyo ili ifikie lengo iliyojipangia. Balozi Seif aliihakikishia Kamati hiyo kwamba atachukuwa jitihada za ziada katika kuona wale wadau, Mashirika na hata Taasisi zinazofikiriwa kuunga mkono harakati hizo kimawazo na hata uwezeshaji wanasaidia.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuhimiza Uongozi wa Kamati hiyo ya Mapinduzi Cup kuendelea na maandalizi katika hatua kubwa na makini ili kuona lile kusudio la kufanikisha mashindano hayo muhimu linafikiwa.
 “ Katika kulipa nguvu za himizo la ziada suala hili nitakuombeni kwa hatua zinavyosonga mbele ni vyema tukakutana tena mwishoni mwa mwezi wa Julai ili kuangalia tumefikia hatua ipi na tumekwama wapi katika Maandalizi hayo “. Aliagiza Balozi Seif.
 Mashindano ya Kombe la Mapinduzi yanayofanyika mnamo Mwezi wa Januari kila mwaka mara hii fainali yake imepangwa kufanyika siku ya Pili ya Maashimisho ya Sherehe za Mapinduzi Januari 12 ambayo itakuwa Tarehe 13 Januari 2014. 
 Uamuzi huo umechukuliwa na Kamati hiyo ili kuwapa nafasi nzuri Wananchi na wapenzi wa Michezo na sanaa kushiriki katika matukio yote yanayoambatana na sherehe hizo ikiwemo burdani na muziki wa Taarabu uliozoeleka kufanyika usiku wa kilele cha sherehe hizo.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiipongeza Kamati ya Mapinduzi Cup aliyokutana nayo kuangalia hatua wanazochukuwa katika maandalizi ya Mashindano ya kombe hilo ambapo maadhimisho ya Sherehe za Mapinduzi zinafikia nusu Karne (miaka 50)
  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mapinduzi Cup Sharifa Khamis akielezea hatua inazoendelea kuchukuwa Kamati yake katika maandalizi ya mashindao hayo ambayo mara hii yanatarajiwa kuwa ya Kimataifa.
Mjumbe wa Kamati ya Mapinduzi Cup ambae pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Dr. Ali Mwinyikai akifafanua Mikakati iliyojipangia Kamati hiyo katika kutafuta fedha za kufanikisha mashindano ya Mapinduzi Cup.
Moja kati ya mikakati hiyo ni kuhakikisha uwanja wa michezo wa Amani unawekewa nyasi bandia ili kuuwezesha uwanja huo kuhimili mashindano hayo.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Vote for Richard Kazimoto in the Under-30 Youth innovation award

$
0
0
Vote for Richard Kazimoto in the Under-30 Youth awards via http://www.youthawards.or.tz/polls.html
Richard Kazimoto has been nominated in the innovation category and among his innovation is www.mnada.co.tz - a perfect solution for selling new, used, excess / unsold and perishable inventory.

He has successfully executed a complete re-design & development of a professional news website for the Tanzania government News media (TSN) DailyNews (http://www.dailynews.co.tz/) and HabariLeo (http://www.habarileo.co.tz/) online Editions

Played part as a developer for www.mrushwa.com an anti-corruption platform with the objective of providing an avenue for the public to report bribery incidents, an initiative by the Deputy Minister for the Ministry of Science & Technology, Mr January Makamba

Conducted research on the “Effectiveness of an Intranet in Enhancing Performance and Communication within an Organization” and successfully developed and implemented an intranet portal for the Tanzania Meteorological Agency which is currently in use for unifying access to the entire organization’s information and applications.
Richard Kazimoto

Maadhimisho ya Magereza Day leo

$
0
0
Wasanii wa Bendi ya Magereza Jazz(Maarufu kwa jina na Mkote Ngoma) wakituumbuiza leo katika Maadhimisho ya Magereza Day yaliyofanyika katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam.

Picha ya chini Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akimvisha Cheo cha Kamishna Msaidizi wa Magereza, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Erasmus Kundy wa Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga. Hafla ya uvikaji Vyeo kwa Maafisa hao wa Mkoa wa Dar es Salaam umefanyikia Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Dar es Salaam.
Tume ya Polisi na Magereza katika Kikao chake Namba 2/2012/2013 kilichofanyika leo tarehe 22/6/2013 chini ya Mwenyekiti wake Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Dkt. Emmanuel John Nchimbi imewapandisha Vyeo Maafisa 36 wa Ngazi mbalimbali kuanzia tarehe 22/6/2013.
Kwa Mamlaka aliyopewa Kisheria na Tume ya Polisi na Magereza ya Mwaka 1990, Kamishna Jenerali wa Magereza amewavisha Vyeo Maafisa wa Mkoa wa Dar es Salaam leo katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga.
Akizunzungumza na Maafisa hao waliopandishwa Vyeo hivyo amewapongeza kwa  kutunukiwa Vyeo hivyo na kuwataka kutenda kazi zao kwa kuzingatia Maadili ya kazi pamoja kuzingatia Weledi na kasi ya utekelezaji wa Majukumu ya kazi.
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Magereza wa Mkoa wa Dar es Salaam ambao wametunukiwa vyeo leo na Tume ya Polisi na Magereza katika Maadhimisho ya Magereza Day. Zoezi hilo la uvishaji Vyeo kwa  Maafisa hao umefanyikia  katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam
Kikundi cha Askari wa Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani kikiingia Uwanjani kutoa Onesho la Maalum la Kutuliza Ghasia zinapotokea Magerezani leo katika Maadhimisho ya Magereza Day
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa maelezo kwa Mgeni Rasmi pamoja na Wageni Waalikwa kuhusu Magereza Day leo katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akihutubia hadhara (Hawapo pichani)leo wakati wa Maadhimisho ya Magereza Day yaliyofanyika katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam, anayefuatia kutoka kulia kwa Mgeni Rasmi ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja




Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akikagua Gwaride Maalum lililoandaliwa na Askari wa Jeshi la Magereza kwa ajili ya Maadhimisho ya Magereza Day Tangu kuundwa kwa Jeshi la Magereza Nchini mwaka 1931. Maadhimisho hayo yamefanyika leo Jijini Dar es Salaam katika Chuo cha Maafisa Magereza. Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza

PPF yatoa msaada wa madawati kwa shule za msingi Mtwara

$
0
0
Kaimu Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya Mtwara,Bi. Kauthar Nassoro (kushoto) akipeana mkono na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Mtwara,Bw. Ally Mpenye wakati wa zoezi la kukabidhi sehemu ya msaada wa madawati 30 yenye thamani ya Tshs milioni mbili na laki saba yaliyotolewa na Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.
Kaimu Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya Mtwara,Bi. Kauthar Nassoro akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanyika kwa makabidhiano hayo,ambapo alieleza umuhimu wa fao la elimu ambalo linatolewa na Mfuko wa Pensheni wa PPF pekee.
Baadhi ya Maofisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya Mtwara wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kukabidhi msaada wa madawati.kutoka kulia ni Kauthar Nassoro,Tumpe Mwaitenda,Lilian Mhina pamoja na Shida Michael.
Viongozi wa halmashauri ya Mtwara,Kaimu Mkurugenzi Bw.Ally Mpenye na Kaimu afisa elimu wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF.

amsha amsha za Tamasha la Kili Music Tour 2013 ndani ya Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma leo

$
0
0
 Jukwaa liko tayari kwa Show Babkubwa itakayoangushwa na Wasanii mbali mbali waliopo kwenye Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013 ndani ya Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma hivi sasa.ambapo leo hii ni sherehe ya wakazi wa Dodoma Kiburudani.
 Dj akiwa tayari tayari kwa kuangusha Bonge moja la Burudani.
 Mabaunsa wakiwa tayari washajipanga kwa kazi moja.

kijana aliyevujisha taarifa nyeti za mawasiliani ya watu marekani afunguliwa mshtaka ya ujasusi

$
0
0
Na Ripota wetu Washington

Kijana Edward J. Snowden (pichani), mfanyakazi wa zamani wa wakala wa Usalama wa Taifa  wa Marekani (NSA) aliyevujisha nyaraka nyeti zinazohusu mawasiliano ya watu yanayonaswa na wakala hiyo kwa vyombo vya habari amefunguliwa mashitaka ya kuvunja sheria ya Ujasusi na kuiba mali ya serikali ili kuvujisha taarifa nyeti kwa gazeti la Guardian na Washington Post, Idara ya Sheria ya nchi hiyo imesema.

Kila kosa katika hayo matatu aliyoshtakiwa nayo yanabeba adhabu ya kifungo cha miaka 10 jela, na habari zinasema huenda akaongezewa mashtaka. Zaidi ya shitaka la wizi, mashtaka mengine mawili ni kufanya mawasiliano yanayohusu taarifa za ulinzi wa taifa, na kuwasilisha kwa hiari yake taarifa nyeti za kiintelijensia kwa mtu asiye na idhini kuzipata.


Mashtaka hayo yalifunguliwa Juni 14, 2013 na waendesha mashtaka wa wilaya ya Mashariki ya Virginia, ambako ndiko kesi nyingi za usalama wa Taifa za Marekani huendeshwa. Maafisa wa Marekani wamesema tayari wamewaomba maafisa wa Hong Kong, ambako Snowden anaaminika amejichimbia, kumtia mbaroni  wakati maombi ya kumpeleka Marekani yakiandaliwa.

Jaribio la kumhamishia Snowden nchini  Marekani huenda likasababisha zogo refu la kisheria ambapo matokeo yake hayajulikani. Makubaliano ya kidiplomasia kati ya Marekani na Hong Kong yanahusisha pia kipengele cha kutomhamisha mtuhumiwa yeyote wa kisiasa toka nchi moja hadi ingine, ambapo Snowden anaweza kudai kuwa kesi yake ni ya kisiasa.

Maswala yote ya Hong Kong yanayohusu usalama wa Taifa hushughulikiwa na Serikali ya China huko Beijing. Katibu wa zamani wa Usalama wa Hong Kong Bi Ip ambaye sasa ni mbunge amesema leo kuwa hakuna jinsi bali kukubaliana na Marekani na hati ya kukamatwa Snowden ikija polisi wao watamsaka na kumtia mbaroni.


Hata hivyo, Bi Ip amesema kwamba Snowden anaweza uhamisho wake kwa kudai alichokitenda ni kosa la kisiasa, ama anaweza kuomba hifadhi ya ukimbizi, na kwamba kesi aina hiyo huchukua hata miaka 10 kukamilika.

Juma lililopita mamia ya watu waliandamana kwenye mvua nje ya ubalozi mdogo wa Marekani mjini Hong Kong wakiwataka maafisa wao wasitoe ushirikiano kwa ombi lolote la kumhamisha Snowden.


Mashtaka kama anayokabiliwa nayo Snowden ni ya saba chini ya utawala wa Rais Obama, wakati utawala wa marais wote waliopita  ni mashtaka matatu tu yaliyofunguliwa dhidi ya ofisa wa serikalikuvujisha taarifa nyeti kwa vyombo vya habari.

Snowden, ambaye Ijumaa iliyopita alitimiza umri wa miaka 30, alikimbilia Hong Kong mwezi uliopita, baada ya kuacha kazi yake ya kijasusi katika kituo cha Hawaii. Ameshavujisha taarifa kibao nyeti sana kwa gazeti la The Guardian, ambalo limekuwa likichapisha mfululizo wa makala kuhusu serikali za Marekani na Uingereza kusikiliza mawasiliano ya watu kwenye mitandao na simu.

Kwa kuvujisha taarifa hizo nyeti, Snowden amefungua dirisha lisilotarajiwa kuhusu mwenendo wa kiintelijensia wa N.S.A, ikiwa ni pamoja na kukusanya kwake kwa taarifa karibu zote za simu zinazopigwa Marekani pamoja na mkusanyiko wa email za kutoka watu wan je ya nchi hiyo kutioka katika makampuni makubwa ya mtandao, ikiwa ni pamoja na Google, Yahoo, Microsoft, Apple na Skype.

Snowden, ambaye alisema alishangazwa kwa kile alichoamini kuwa ni hatua ya NSA inayoingilia mambo binafsi ya Wamarekani na watu wan je ya nchi hiyo, aliliambia gazeti la The Guardian kwamba amevujisha nyaraka hizo nyeti kwa kuwa anaamini mipaka ya kufuatilia habari za watu iamuliwe sio na maafisa wa serikali bali rais wa Marekani.


 



msafiri kafiri...

$
0
0
Mambo ya Kondoa hayo...
Sent from my iPhone by Mdau

DKT FENELLA MUKANGARA afungua Semina ya UVCCM Kinondoni na Kukabidhi Vifaa vya Michezo.

$
0
0
 Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo ambaye pia ni mjumbe wa NEC Dkt Fenella Mukangara akibidhi vifaa vya michezo kwa Katibu wa UWT kata ya Ubungo Bi. Rose Ndunguru.Vifaa hivyo vimetokana na ombi maalum kwa ajili ya ligi ya mpira wa Pete inayojulikana kama Rose Wasiri Cup.Mashindano hayo yameanza leo jijini Dar es Salaam katika viwanja vilivyoko Ubungo Msewe jijini Dar es Salaam.Jumla ya mipira tisa na seti mbili za jezi  zimekabidhiwa.

Article 3

Mdau Kelvin Msuya na Gladys Munanka wameremeta usiku huu

$
0
0
Maharusi Kelvin Msuya na Gladys Munanka wakiwa katika mnuso wao wa kumeremeta unaofanyika usiku huu ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee hall Jijini Dar es Salaam baada ya kumeremeta katika kanisa la KKKT la Azania Front.

Mapicha kede kede na video ya Mnuso huu utawajia baadae kidogo.

Tamasha la Kili Music Tour 2013 lafana sana ndani ya Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma leo

$
0
0
 Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Linex akiwasalimia mashabiki na wapenzi wa Muziki waliofurika kwa wingi ndani ya Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma leo,ambapo usiku huu kulikuwa na bonge moja la Show ya Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013.
 Msanii aliejinyakulia Tuzo kadhaa za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013,Ommy Dimpoz akienda sambamba na timu yake ya Madansa wakitoa burudani ya kufa mtu ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma usiku huu.
 Msanii Ben Pol akighani moja ya nyimbo zake.
 Msanii wa Hip hop Mwenye tuzo nne za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013,Kala Jeremier akifanya vitu vyake usiku huu ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
 Mashabiki hawakutaka kabisa kupitwa na taswira za show hii.
 Ni shangwe kwa kwenda mbele ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma hivi sasa. 

mchiriku wa Jagwa music band toka mwanyamala wapagawisha watasha

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Ngoma ya Suma Lee na Linex ya 'Boda Boda' ni noma!

mkataa kwao mtumwa


miondoko ya kumeremeta kwenya mnuso

chemsha bongo toka kwa mdau

taswira mbalimbali toka accra, ghana, leo

$
0
0
 Askari polisi wa jiji la Accra wakiongoza na kuhakikisha usalama wa washiriki kutoka nchi mbalimbali za Afrika zipatazo 20 wakati wa Maandamano na mbio fupi kuadhimisha Siku ya Utumishi wa Umma Barani Afrika katika mtaa  Mkuu wa Opera, maarufu kwa jina la High Street Opera Square Ministries, jijini Accra
 Soko maarufu la Makola jijini Accra bidhaa zikiwa zimepangwa kila kona.
 Kariakoo ya Ghana!!, maarufu kama MAKOLA pilikapilika za wachuuzi na wanunuzi zikiendelea kwa mbali kulia kule ni madafu ya kukata kiu
moja ya bango la  maduka ya bidhaa za Elekroniki sokoni MAkola jijini Accra likiwa na baadhi ya maneno kama  ya Kiswahili kwa kutohoa kutoka lugha ya Kiingereza, ubunifu huo!!Picha na mdau Florence Lawrence

Article 18

kikao cha kawaida cha kujadili kero za muungano chafanyika dodoma leo

$
0
0
Kikao cha kawaida cha kamati ya pamoja kati ya Viongozi na wataalamu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kimekutana kujadili changamoto mbali mbali zinazoleta kero katika masuala ya Muungano.
 Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Mohd Gharib Bilal alikiongoza kikao hicho akiambatana na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo katika Ukumbi wa Dodoma Hoteli Mjini Dodoma. 
 Akiwasilisha masuala yaliyofanyiwa kazi kufuatia agizo la kikao kilichopita Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamuhuri anayeshughulikia masuala ya Mauungano Mh. Samia Suluhu Hassan alisema ipo hatua kiasi iliyofikiwa katika kushughulikia masuala hayo zikiwemo zile kero zinazoleta changamoto ndani ya Muungano. Waziri Samia aliyataja masuala hayo kuwa ni pamoja na Ushirikia wa MIRADI YA Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, suala la mafuta na Gesi kutolewa katika mamabo ya Muungano, Ushirikiano wa Zanzibar na Taasisi za nje katika mfumo wa uhusiano wa Kimataifa, Uvuvi wa Bahari kuu pamoja na Ajira za utumishi wa wafanyakazi wa Zanzibar katika Taasisi za Muungano. 
 Alisema majadiliano ya wataalamu na viongozi teule wa pande zote mbili katika masuala ya Mafuta na Gesi pamoja na lile la Uvuvi wa Bahari kuu yemechelewa kutokana na ufinyu wa bajeti za vikao hivyo. Hata hivyo alifahamisha kwamba hatua za majadiliano hayo zitaendelea ndani ya kipindi cha miezi miwili inayofuata kwa vile mfuko wa kuratibu vikao hivyo tayari umeshapatikana. 
 Naye Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Abdulla Juma Abdulla akizungumzia suala la ushiriki wa Miradi ya Zanzibar ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki alisema Jumuiya ya Afrika Mashariki inasubiri uchambuzi yakinifu katika miradi ya Bandari ya mpiga Duri Unguja, Uwanja wa ndege wa Pemba pamoja na Chelezo cha Malindi Unguja. 
 Mh. Abdulla alisema Benki ya Maendeleo ya Afrika { ADB } kwa kushirikiana na Jumuiya ya Afrika Mashariki imekusudia kusaidia mradi wa Bandari ambao tayari makampuni matatu ya kimataifa yalijitokeza kufanya uchambuzi huo.
Kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewapongeza Viongozi na watendaji wa pande zote kwa juhudi wanazoendelea kuchukuwa za kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya Kamati hiyo. 
Balozi Seif alisema akiwa kama mtendaji mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar amekuwa na mawasiliano ya kirafiki zaidi kati yake na Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Peter Pinda wakati inapotokea hitilafu ya utendaji baina ya pande hizo mbili.
 “ Tumekuwa tukiwasiliana na kushirikiana kwa karibu zaidi kama ndugu mimi na Waziri Mkuu Mh. Pinda wakati yanapojitokeza matatizo ya utekelezaji wa majukumu katika pande zetu mbili. Na hili wakati mwengine tunalazimika kuwasiliana kwa simu wakati wowote hata kama usiku “. Alisisitiza Balozi Seif. Akikiahirisha kimao hicho cha Kamati ya pamoja ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Ile ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanziabr Makamu wa Rais wa Muungano Dr. Mohamed Gharib Bilal amewaasa Watendaji wa pande zote mbili kuhakikisha kwamba wanakuwa makini wakati wote katika kukabiliana na changamoto zinazojichomoza katika masuala ya Muungano. 

Na Othman Khamis Ame 
 Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar 23/6/2013.
 Mwenyekiti wa Mkutano wa Kamati ya pamoja ya SMT na SMZ Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Moha Gharib Bilal akiendesha Kikao hicho kilichokutana katika Ukumbi wa New Dodoma Hoteli Mjini Dodoma.Kushoto ya Dr. Bilal ni Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda na  upande wake wa kulia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
 Wajumbe wa Mkutano wa Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ waliokutana katika ukumbi wa New Dodoma Hoteli Mjini Dodoma katikakikao cha kawaida cha kuzungumzia masuala ya Muungano na change moto zinazokabili Muungano.
Waziri wa Nchi Omfisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo Zanzibar Mh. Omar Yussuf Mzee akifafanua masuala yua fedha katika mkutano wa Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ Mjini Dodoma.
Viewing all 110021 articles
Browse latest View live




Latest Images