Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

Mwakilishi wa Jimbo la Donge, Dkt. Khalid Salum Mohamed asisitiza umuhimu wa elimu dini

$
0
0
Na Juma Farid, Zanzibar.
WAZAZI na walezi nchini wameshauriwa kuwahimiza watoto wao kusoma kwa bidii elimu ya dini ya kiislamu ili kuandaa  viongozi bora wa baadae watakaosimamia  kwa uadilifu misingi imara ya dini hiyo.
Rai hiyo imetolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Donge, Dkt. Khalid Salum Mohamed wakati akizungumza katika mashindano ya kuhifadhi Quran yaliyoandaliwa na Jumuiya  ya kuhifadhisha Kanda ya Donge  yaliyofanyika Donge Kitaruni katika Madrasa ya Twalibina Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja.
Alisema elimu ndio urithi wa kudumu na wenye manufaa kwa watoto wa jinsia zote kwani wanakuwa na misingi ya  maadili mema  na kuepuka mambo maovu.
Pia Dkt. Salum ambaye pia ni Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, aliwasihi wazazi, walimu na viongozi wa madrasa za Wilaya hiyo kukaa pamoja na kupanga mikakati ya kudumu ya kuthibiti tatizo la wanafunzi wa kiume wanaoacha mapema masomo ya kidini hiyo bila sababu za msingi.
Akizungumza kwa niaba ya Mwakilishi huyo, Ostadh Idd Shekha Makame alieleza kwamba waumini wa dini hiyo wanatakiwa kuwa wamoja na wenye kuamrishana mema na kukatazana mabaya wakati wote na sio katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani pekee.
“Elimu ndio nyenzo pekee ya kuleta maendeleo ya kudumu kwa mwanadamu yeyote na jamii yetu itapiga hatua za kimaendeleo kwa haraka kama vijana wetu tutakuwa tumewarithisha rasilimali hiyo.”, alisema Ostadh Shekha kwa niaba ya Dkt. Salum.
Hata hivyo  Ostadh Shekha alitoa wito kwa madrasa zilizoshiriki katika masindano hayo kwamba licha ya kutoa elimu ya dini wanatakiwa kuanzisha miradi ya maendeleo itakayozalisha kipato kitakachosaidia kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili.
Pamoja na hayo Dkt. Salum alitoa zawadi ya misahafu 140 na magunia manne ya Tende kwa vyuo vilivyoshiriki mashindano hayo.
 Oustadh Idd Shekha Makame kwa  niaba ya Mwakilishi wa jimbo la Donge  Dkt. Khalid Salum Mohamed akitoa nasaha kwa washiriki wa mashindano ya kuhifadhi Quran huko Donge Kitaruni Unguja.
 Mwanafunzi Juma Kassim Choum akikabidhiwa zawadi ya msahafu baada ya kuhifadhi juzuu tano na kushinda kwa Alama 85.
Oustadh Idd Shekha Makame kwa  niaba ya Mwakilishi wa jimbo la Donge  Dkt. Khalid Salum Mohamed akikabidhi misahafu 140 kwa Amir wa jumuiya ya kuhifadhisha Quran Kanda ya Donge, Wakanda Haji Kombo.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LEO TAREHE 04.06.2017

WAONGOZA UTALII WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KATIKA KUWAPENDEKEZA WATAKOINGIA KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA KUMPATA MUONGOZAJI BORA WA MWAKA 2017

$
0
0
Na.Vero Ignatus Kilimanjaro.

 Wito umetolewa kwa waongoza watalii nchini kutoa ushirikiano ,kuwapendekeza watakaoingia katika kinyang'anyiro cha kumtafuta mshindi wa Tuzo ambayo imeandaliwa kwaajili ya kumpata Balozi atakaewawakilisha waongoza utalii nchini Tanzania,Afrika ya Mashariki na Kati .

Akizungumza na blog hii Muasisi na mwenyekiti wa Tuzo hiyo Sadock Mugetta amesema kuwa tuzo  inafahamika kama  TANZANIA TOUR GUIDE AWARDS   ambapo mwaka jana ilikuwa imegawanyika   katika vipengele vya kumtafuta muongoza watalii bora wa Mlima,Safari pamoja na Wapagazi,ila mwaka huu wameongeza vipengele viwili ambavyo ni Muongoza utalii wa Utamaduni pamoja na Mpishi bora.

Sadock amesema kuwa wameamua kuwepo kwa Tuzo hiyo kutokana hali halisi iliyopo ya ugumu wa kazi wanayoifanya waongoza watalii (Mabalozi) ili mshindi atakayepatikana atawawakilisha katika mambo yao ambayo wanataka Serikali iyafahamu,pamoja na wageni mbalimbali waitambue Tanzania pamoja na vivutio vya Utalii vilivyopo.

 Ameongeza kuwa tangia kuanzishwa kwa huduma ya  utalii hapa nchini waongoza Watalii  hawajawahi kupewa kipaumbele, hivyo ni vyema Serikali ikatambua kuwa muongozaji watalii huwa  anatumumia 99% ya muda wao  kukaa na mgeni awapo nchini na anapewa taarifa zote sahihi na muhimu  hadi anaondoka nchini. 
Wa kwanza kushoto ni Muasisi wa Tanzania Tour Guide Awards Sadock Mugetta, aliyepo kushot kwake ni Katibu wa Freelance Guides Society of Tanzania(FGST )anayefuata ni mjumbe wa  wakiwa katika maonyesho ya (3)Utalii ya Kilifair  katika uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Mganga Mkuu Wilaya ya Gairo kukaguliwa-Waziri Mkuu

$
0
0
Na. Benjamin Sawe 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza mkaguzi kutoka ofisi yake kuchunguza hali ya upatikanaji wa dawa kwenye zahanati na kituo cha afya cha mjini Gairo mkoani Morogoro.

Akiwahutubia wananchi wa Gairo na vitongoji vyake Mh. Majaliwa alisema amechukua uamuzi huo baada Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Dk. Albert Lyaruu kukiri kuwa baadhi ya watumishi wa Idara yake wanamiliki maduka ya dawa.

“Sasa ni lazima nilete mkaguzi kutoka ofisi yangu ili tupate picha halisi kama dawa zinazoletwa zinafika, na kama zinafika zinatumikaje.” alisema Waziri Mkuu.

Mh. Majaliwa alisema kumekuwa na baadhi ya watumishi wa afya wasiokuwa waaminifu kuchukua dawa katika vituo vya afya vya Serikali na kuzipeleka kwenye maduka yao hivyo kupelekea wananchi kukosa huduma za madawa katika hospitali za Serikali.

Alifafanua kuwa, Serikali haizuii watumishi wa afya kuwa na maduka ya dawa,bali inachokataa ni tabia ya baadhi ya watumishi wasiowaaminifu kuchukua dawa za Serikali na kuzipeleka kwenye maduka yao.

Katika Mkutano huo Dtk. Albert Lyaruu alisema amekuwa akipokea sh. milioni 109 kila robo mwaka na katika kipindi cha miezi mitatu ya mwisho amepokea kiasi cha fedha hizo na kati ya hizo asilimia 33 sawa na sh. milioni 36 zimetumika kununua dawa na vifaa tiba.

Aidha Mh. Majaliwa amewaagiza wahudumu wa afya kutokaa ofisini badala yake waende kwenye vituo vya afya na zahanati kuangalia na kusimamia matumizi ya dawa zinazotolewa na serikali akitolea mfano wa kesi ya mganga wa kituo cha afya cha Shinyanga kukutwa na dawa za Serikali nyumbani kwake.

Kuhusu sekta ya elimu Wilayani humo, Waziri Mkuu alisema Serikali imepeleka sh. milioni 419 ili kuongeza vyumba vya madarasa ikiwa ni pamoja na kupelekea sh. milioni 500 kwa kila Halmashauri kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu na sh. bilioni 1.2 ili kukamilisha ujenzi wa ofisi za halmashauri hiyo” alisema.

Alitumia fursa hiyo kuwahimiza wajiunge na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili waweze kupata huduma za matibabu bila kulazimika kuwa na fedha taslimu pindi wanapougua wao wenyewe na familia zao.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwahutubia mamia ya wakazi wa mji wa Gairo kwenye uwanja wa shule ya msingi Gairo ‘A’ uliofanyika Juni 3, 2017. Waziri Mkuu alikuwa wilayani humo kwa ziara ya siku moja. (Picha na OWM).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisikiliza maelezo yanayotolewa na Mbunge wa Gairo, Bw. Ahmed Shabiby kuhusu mradi wa maji wa mjini Gairo unaosimamiwa na MORUWASA ambao haujakamilika wakati alipofanya ziara ya siku moja wilayani humo, Juni 3, 2017. Kulia ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Eng. Gerson Lwenge. (Picha na OWM).

BULEMBO ACHANJA MBUGA NA KUMALIZA ZIARA YA MKOA WA KIGOMA KWA KUPIGA KAZI KATIKA WILAYA YA KAKONKO, LEO

$
0
0
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Alhaj Abdallah Bulembo akipandisha bendera, kuzindua Shina namba sita la CCM la Kiyobela, Katika Kijiji cha Kabiko wilayani Kakonko mkoani Kigoma, leo.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulelmbo akimwambia jambo Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala, baada ya kuzindua Shina namba Sita la CCM la Kiyobela, Katika Kijiji cha Kabiko wilayani Kakonko mkoani Kigoma, leo. Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Kigoma Naomi Kapambala
 Mjube wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akipata maelezo kutoka kwa baadhi ya viongozi, alipokagua ujenzi wa Ofisi ya CCM Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma, leo
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Alhaj Abdallah Bulembo akimsalimia Mwenyekiti wa Sina la CCM Namba Sita, Tawi la Kakonko Msufini, Wilayani Kakonko mkoani Kigoma, Ramadhan Adam mwenye ulemavu wa miguu, baada ya kuzindua shina hilo.
 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Kakonko, Mabalozi, Viongozi na watendaji wa CCM, Watendaji wa Serikali na Viongozi mbalimbali wa CCM na Jumuia zake. Walisimama kwa nderemo na vifijo Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Alhaj Abdallah Bulembo alipokuwa akiingia ukumbini kuzungumza nao katika kikao cha ndani.

MAZOEZI YA AFC LEOPARDS YA KENYA UWANJAWA KARUME JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Wachezaji wa timu ya AFC Leopards ya Kenya wakiwa katika mazoezi ya pamoja katika Uwanja wa karume jijini Dar es Salaam, leo Juni 4, 2017 kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya 'SportPesa Super Cup' inayoanza kutimua vumbi kesho Juni 5 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini, ambapo fungua dimba itakuwa ni kati ya Singida Utd na AFC Leopards, mechi ya pili itakuwa ni kati ya wenyeji Yanga na Tusker Fc na Juni 6 mchezo wa kwanza utakuwa ni kati ya Simba vs Nakuru Nakuru All Stars na mchezo wa pili utakuwa ni kati ya Gor Mahia ya Kenya Vs Jang'ombe Boys Fc. ya Zanzibar
 Wachezaji wa timu ya AFC Leopards ya Kenya wakiwa katika mazoezi ya pamoja katika Uwanja wa karume jijini Dar es Salaam, leo Juni 4, 2017 kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya 'SportPesa Super Cup' inayoanza kutimua vumbi kesho Juni 5 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini
 Wachezaji wa timu ya AFC Leopards ya Kenya wakiwa katika mazoezi ya pamoja katika Uwanja wa karume jijini Dar es Salaam, leo Juni 4, 2017 kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya 'SportPesa Super Cup' inayoanza kutimua vumbi kesho Juni 5 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini
 Wachezaji wa timu ya AFC Leopards ya Kenya wakiwa katika mazoezi ya pamoja katika Uwanja wa karume jijini Dar es Salaam, leo Juni 4, 2017 kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya 'SportPesa Super Cup' inayoanza kutimua vumbi kesho Juni 5 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini.
 Picha na Montage Onpoint

WAZIRI MKUU MAJALIWA AHUTUBIA WANANNCHI MJINI GAIRO

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwahutubia mamia ya wakazi wa mji wa Gairo kwenye uwanja wa shule ya msingi Gairo ‘A’  Jumamosi
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwahutubia mamia ya wakazi wa mji wa Gairo kwenye uwanja wa shule ya msingi Gairo ‘A’ Jumamosi
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisikiliza maelezo yanayotolewa na Mbunge wa Gairo, Bw. Ahmed Shabiby kuhusu mradi wa maji wa mjini Gairo unaosimamiwa na MORUWASA ambao haujakamilika wakati alipofanya ziara ya siku moja wilayani humo, Juni 3, 2017. Kulia ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Eng. Gerson Lwenge. 

HATUA KALI ZA KISHERIA ZICHUKULIWE KWA VIWANDA NA MIGODI INAYOFANYA SHUGHULI ZAKE ZA UZALISHAJI KWA KUHARIBU MAZINGIRA-MAKAMU WA RAIS.

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameagiza kuchukuliwa kwa hatua kali za kisheria kwa viwanda na migodi ambayo inafanya shughuli zake za uzalishaji kwa kuharibu mazingira ikiwemo utitirishaji wa kemikali kwa wananchi kwani kufanya hivyo kunahatarisha usalama wa wananchi na viumbe hai wengine.

Makamu Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo tarehe 4-Jun-2017 kijijini Butiama mkoani Mara wakati anahutubia wananchi katika kilele cha siku ya mazingira Duniani.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema uharibifu wa mazingira ukiachiwa uendee nchini ni hatari kwa usalama wa maisha na viumbe hivyo ni muhimu kwa viongozi katika ngazi zote kuchukua hatua zitakazosaidia kukabiliana na vitendo hivyo kote nchini.

Makamu wa Rais amesisitiza kuwa umefika wakati kwa viongozi kwa ushirikiano na jamii kuhakikisha wanaweka mikakati ya kuokoa mifumo ya ikolojia, uhifadhi wa bioanuai, kudhibiti uchomaji miti kiholela ili kurejesha uoto wa asili ambao umeharibiwa na shughuli mbalimbali za kibinadamu katika maeneo mengi nchini.

“Kutozingatia hifadhi ya mazingira kunaweza kusababisha kuparaganyika kwa mfumo huo na kufanya maisha yetu na ya vizazi vijavyo kuwa mashakani”. Amesisitiza Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema katika kuadhimisha siku ya mazingira Dunia viongozi wanapaswa kuchukua hatua za kuelimisha wananchi na kuwahamasisha ili kila mtu ashiriki katika juhudi za kuwa na uchumi unaozingatia hifadhi ya mazingira.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka shda la maua kwenye Mnara wa kumbukumbu ya ajali ya ndege ya kivita iliyotokea mwaka 1978 kwenye Msitu wa Muhunda ,wilayani Butiama mkoani Mara. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akutana na Mama Maria Nyerere nyumbani kwa Mama Maria Butiama leo mara baada ya kuhutubia kwenye kilele cha siku ya mazingira Duniani.#Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipanda mti kwenye Msitu wa asili ulioasisiwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwenye kilele cha siku ya mazingira duniani ambapo kitaifa imeadhimishwa Butiama. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimwagia maji mti alioupanda kwenye Msitu wa asili ulioasisiwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwenye kilele cha siku ya mazingira duniani ambapo kitaifa meadhimishwa Butiama. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akiwahutubia Wananchi kijijini Butiama mkoani Mara wakati wa kilele cha siku ya mazingira Duniani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia kiatu cha kusaidia walemavu wakati alipotembelea banda la Kituo cha Walemavu cha Ziwa Victoria (Lake Victoria Disability Centre) kinachoshughulika na kutengeneza viungo bandia kwa watu wenye ulemavu kabla ya kuhutubia kwenye kilele cha siku ya mazingira duniani ambapo kilele chake kimefanyika kwenye viwanja vya Mwenge,Butiama
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia namna samaki anaweza kufugwa vizuri bila kuharibu mazingira na kuleta manufaa kabla ya kuhutubia kwenye kilele cha siku ya mazingira duniani ambapo kilele chake kimefanyika kwenye viwanja vya Mwenge,Butiama.



MAGAZETI YA LEO JUMATATU JUNE 5,2017

Dau nono la Milioni 10 za Biko laenda kwa Junior Pesambili wa Makete

$
0
0
DAU nono la Sh Milioni 10 linalotolewa kama zawadi ya droo kubwa ya Mchezo wa Kubahatisha wa Biko limeenda kwa Junior Ashery Pesambili wa Lupela, Makete, mkoani Njombe, ikiwa ni mwendelezo wa kugawa fedha kwa washindi wake ikitokana na matokeo ya droo ya 11 iliyochezeshwa jana Jumapili.

Droo hiyo iliyochezeshwa jana iliendeshwa na Balozi wa Biko Kajala Masanja, akishirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid. Akizungumza katika droo hiyo jana, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage, alisema wamedhamiria kugawa mamilioni kwa washindi wao wanaocheza mchezo wa Biko uliozidi kushika kasi katika kona mbalimbali nchini Tanzania.
Alisema tayari wameshafanya droo 11 kubwa ambapo watu mbalimbali wameendelea kupokea fedha zao ikihusisha vijana bila kusahau mzee Stanley Kapondo naye aliyekuwa miongoni mwa Watanzania waliovuna zawadi mbalimbali kutoka Biko.

“Kucheza Biko mara nyingi zaidi ndio nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi, hivyo ni wakati wa Watanzania kucheza mara nyingi ili washinde, ukizingatia kuwa mbali na donge nono la Milioni 10 linalotolewa Jumatano na Jumapili, pia mtu anaweza kushinda zawadi mbalimbali kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000, 1,000,000, huku droo ya Jumatano hii ikitoa Sh Milioni 20 kwa mshindi wake kama ilivyokuwa Jumatano iliyopita.

“Mchezo wetu unachezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo utakapoingia kwenye kipengele cha Lipa Bili au lipa kwa Mpesa, mshiriki wetu ataingiza namba ya kampuni 505050 na baadaye kuweka namba ya kumbukumbu 2456, huku akianzia kucheza kwa Sh 1000 au zaidi,” Alisema Grace.


Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja, kulia akionyesha namba ya ushindi wa Sh Milioni ya mshindi wao wa Lupela, Makete,mkoani Njombe, Junior Ashery Pesambili aliyepatikana katika droo ya jana Jumapili. Kushoto ni mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid.

Balozi wa Biko Kajala Masanja akifurahia namba ya mshindi wa Sh Milioni 10 kutoka Makete, mkoani Njombe, droo iliyochezeshwa jana jijini Dar es Salaam.

MAONENSHO YA SWAHILI FASHION WEEK YAFANA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mbunifu wa mavazi, Maryimaqulate Kavishe (kulia) akiwahudumia wageni waliotembelea kununua bidhaa zake wakati wa maonesho hayo. 
Mbunifu wa mavazi, Jesca Matei (kushoto) akiwasikiliza wageni waliotembelea kununua bidhaa zake wakati wa maonesho hayo. 
Mshiriki wa maonesho hayo Coleta Mzena (kushoto) akitabasamu kwa kamera pamoja na wageni waliotembelea kununua bidhaa zake wakati wa maonesho hayo. 
William Gilhi akiwaonesha wageni bidhaa za Kampuni ya African Splash zinazopatikana pia online walipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonesho hayo. 
Balozi wa Italia Nchini Tanzania, Roberto Mengoni (kushoto) akibadilishana mawazo na Mbunifu wa Mavazi nguli Mustafa Hassanal pia Mwasisi na Mtendaji Mkuu wa Basila Mwanukuzi Foundation, Basila Mwanukuzi katika maonesho ya Mavazi na bidhaa za Kitamaduni nyumbani kwa Balozi huyo Kando ya Barabara ya Kenyatta Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Maonesho hayo yaliratibiwa na Swahili Fashion Week. (Picha zote na Robert Okanda Blogspot) .

ALICHOKIZUNGUMZA KAIMU KAMISHNA WA USTAWI WA JAMII BAADA YA MKUTANO ULIOANDALIWA NA UNHCR NA UNICEF

MWANAMUZIKI HALILA TONGOLANGA AFARIKI DUNIA

$
0
0

HALILA TONGOLANGA, mwanamuziki wa siku nyingi ambaye alikuwa amelazwa katika hospitali ya Muhimbili amefariki dunia usiku wa kuamkia leo. Halila alikuwa amesafirishwa kutokea Ndanda kuja Muhimbili akihisiwa kuwa na matatizo ya figo. Licha ya kuwa alifika Muhimbili juzi Ijumaa usiku, lakini alikuwa hakufanyiwa vipimo vyovyote vikubwa mpaka umauti unamkuta. 
Jana Jumapili ililazimika kuanza kufanya jitihada za kupata daktari ambaye angemshughulikia kwa karibu zaidi, na daktari alipatikana ambaye aliahidi angeanza kufwatilia swala lake leo asubuhi lakini mapenzi ya Mungu yalikuwa tofauti. Juzi nilipomuona alinambia kuwa ana mengi anataka kunambia, lakini moja aliloweza kunambia pale ni kuwa yeye anajihisi ana kansa, 'Nilimuuliza anajuaje hilo, kwa vile hajapimwa hakuwa na jibu"

Wengi tutamkumbuka Tongolanga kwa wimbo wake wa Kimakonde aliouimba kwa mara ya kwanza akiwa na Les Mwenge 'Kila Munu Ave Na Kwao"

Mwili wa marehemu unategemewa kusafirishwa leo saa tano kuelekea kwao Newala. Habari zaidi zitawafikia kupia hapa

Mungu amlaze Pema peponi Halila Tongolanga 

MKOLANI VETERANI NDIYO MABINGWA WA 'JEMBE FM SPORTS RIPOTI BONANZA 2017' MWANZA

$
0
0
Mkurugenzi wa Jembe Media Group Dr. Sebastian Ndege (kushoto) akiwa na mgeni Rasmi Katibu Mkuu wa Chama cha Soka mkoa wa Mwanza, Leonard Malongo (katikati) kwa pamoja wakikabidhi zawadi ya seti moja ya jezi kwa team captain wa Mkolani Veterani Fc mara baada ya kuibuka kuwa Mabingwa wa 'JEMBE FM SPORTS RIPOTI BONANZA 2017, katika uwanja wa Nyamagana. Chini ya udhamini wa Nebrix Limited wauzaji wa vifaa vya michezo na Lake Zone Tents Supply.
Si mchezo 'Miaka miwili ya changamoto hatimaye sasa nuru imeonekana'
Risala ya maadhimisho ilisomwa na Elikana Mathias.
Safu ya Meza kuu.
Mbele ya eneo la kivuli tulilolichagua kuwa jukwaa kuu.

DKT NCHIMBI ATOA RAI KWA VYUO KUTOA WASOMI WENYE TIJA NA SIO KUTENGENEZA MIGOMO.

$
0
0



Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ametoa rai kwa vyuo vikuu na vyuo vinavyotoa elimu ya juu kuwa sehemu ya kuwafundisha na kuwatengeneza wasomi wenye kutambua fursa na tija za maisha na sio sehemu ya kuendekeza migomo isiyo na faida katika maisha ya wanachuo hao.

Dkt. Nchimbi ametoa rai hiyo jana wakati akizindua kikundi cha Bright Focus kilichopo chuo cha Uhasibu tawi la Singida chenye wana kikundi 89 ambao ni wanachuo, walimu na walezi wenye malengo ya kutambua fursa za kuboresha maisha.

Amesema wakati akizindua kikundi hicho anatambua kuwa kikundi hicho kitasaidia kubuni mawazo yenye tija, fursa, na mwelekeo wa kuboresha uchumi huku akiwasisitiza kuelekezana namna bora ya matumizi ya rasilimali walizonazo hususani rasilimali fedha.

Dkt Nchimbi amekitaka kikundi hicho kuwa chachu ya mabadiliko ya tabia na mienendo yote mibaya iwe mizuri kutokana na baadhi ya wanachuo katika vyuo mbalimbali kuhusishwa na tabia zisizo njema.

Amesema kila mwanakikundi anapaswa anatakiwa mawazo yake yaendane na malengo ya kikundi cha Bright Focus kuanzia mwenendo wa maisha yake, ufaulu wake na hata matumizi ya rasilimali yawe yenye muono wa kutengeneza faida na hasa kujifunza namna ya kuhifadhi akiba.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (katikati) akipiga ngoma kwa furaha kama ishara ya kuzindua kikundi cha Bright Focus kilichopo chuo cha Uhasibu Singida, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo.
1
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akihutubia wanakikundi cha Bright Focus (hawapo pichani) kikundi hicho kipo chuo cha Uhasibu Singida.
2
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (katikati) akipiga ngoma kama ishara ya kuzindua kikundi cha Bright Focus kilichopo chuo cha Uhasibu Singida, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo.
3
Wanachuo ambao ni wanakikundi cha Bright Focus kilichopo Chuo cha Uhasibu Singida wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Singida wakati wa uzinduzi wa kikundi hicho.
4
Makamu wa rais wa Bright Focus John Gama akiwasilisha malengo ya kikundi hicho kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida wakati wa uzinduzi katika chuo cha Uhasibu Singida.


TANZIA: BALOZI CISCO MTIRO AFARIKI DUNIA

$
0
0

Mkuu wa Itifaki mstaafu Balozi Cisco Mtiro amefariki dunia katika hospitali ya Aga Khan alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Kwa mujibu wa familia yake, msiba upo nyumbani kwa marehemu mikocheni B jijini Dar es salaam.

Taratibu za mazishi zinaendelea na mtatangaziwa mara tu itapokamilika.

Mola aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi - AMINA

KATIBU MKUU MAENDELEO YA JAMII ATEMBELEA NA KUKAGUA MAKAZI YA WAZEE NJIRO

$
0
0

Afisa Mfawidhi wa Kituo cha Makazi ya kulea wazee ya Njiro Bibi Ndeta Tenga (kushoto) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto(Maendeleo yaJamii) Bi. Sihaba Nkinga(kulia) wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea katika makazi hayo hivi karibuni.
Afisa Mfawidhi wa Kituo cha Makazi ya kulea wazee ya Njiro Bibi Ndeta Tenga (katikati) akimuonesha mazingira ya kituo hicho Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto(Maendeleo yaJamii) Bi. Sihaba Nkinga(kushoto) wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea katika makazi hayo hivi karibuni.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto(Maendeleo yaJamii) Bi. Sihaba Nkinga akisalimiana na wazee mbalimbali waishio katika Kituo cha Makazi ya kulea wazee ya Njiro wakati alipotembelea katika makazi hayo hivi karibuni.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto (Maendeleo yaJamii) Bi. Sihaba Nkinga(kushoto) akisalimiana na na Mwenyekiti wa wazee waishio katika Makazi ya kulea wazee ya Njiro yaliyopo Moshi Mkoani kilimanjaro Bw.Nyasi Athanas wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea katika makazi hayo hivi karibuni. 

KAULI YA MAKAMU WA RAIS MHE SAMIA SULUHU HASSAN KTK KILELE CHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI BUTIAMA

Taasisi kumi za vijana kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana wenzao nchini

$
0
0
Jumla ya taasisi kumi za vijana zimeungana ili kuzidisha nguvu ya kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana wenzao nchini Tanzania na zaidi ikilenga matumizi ya mpango wa uzazi. Vijana hao wamejizatiti kuhahakisha kuwa kuna uwekezaji wa kutosha kwenye elimu juu ya uzazi wa mpango na pia vijana kuhusisha kwenye maamuzi yanayohusu vijana na afya ya uzazi.

Taasisi hizo zimetiliana saini makubaliano na kuwa taasisi moja ikayoitwa Tanzania Adolescent and Youth Reproductive Health (TAYAHR) jana jijini Dar es Salaam ambapo taasisi hiyo itajikita zaidi kwenye kutoa elimu, kuhusisha vijana na kuhakikisha huduma inafika kwenye maeneo sahihi kwa muda sahihi.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutia saini makubaliano hayo, Mwenyekiti wa TAYAHR William Otuck alisema Tanzania ina changamoto kuona ya kwamba asilimia 27 ya vijana wenye miaka 15-19 wana mtoto au ni wajawazito huku utumiaji wa uzazi wa mpango na hasa vidonge vya uzazi kati yao ikiwa ni chini sana – yaani asilimia 13 peke yake huku pia wakiwa hawana elimu yeyote kuhusu afya ya uzazi na hivyo kukosa uamuzi sahihi kwenye masuala ya kujamiiana.
‘Robo ya wasichana wenye umri kati ya 15 na 19 Tanzania wana watoto au ni wajawazito na hali ni mbaya kwenye mkoa wa Katavi yenye asilimia 45 na Tabora asilimia 42 kwa wasichana wenye umri huo. Hii inamaanisha kuna idadi kubwa ya wasichana ambao wanakatisha masomo na kuingia kwenye hali ya kuwa mzazi wangali wana umri mdogo na hii kwa kiasi kikubwa uchangia kuongeza hali ya umasiki kwenye jamii’, alisema Otuck huku akiongeza kuwa idadi kubwa ya wasichana wadogo wakipata mimba pia kunachangia kuongezeka vifo vitokanavyo na uzazi.
Akizungumzia kuhusu elimu na hali ya kupata mimba za utotoni, Otuck alisema tafiti zinaonyesha kuwa ni asilimia 10 wa wasichana ambao wana elimu mpaka ya sekondari ambao hupata mimba wakiwa na umri mdogo kulinganisha na wale wana elimu ya msingi ambao ni asilimia 34 na wale ambao hawana elimu kabisa ni asilimia 52.

Wanachama wa Taasisi za YAM – UMATI Johnbest Mwahaja (kushoto) na ZAFAYCO Amnah Ibuni (kulia) wakisaini makubaliano ya kuwa taasisi moja ya Tanzania Youth and Adolescent Reproductive Health Coalition (TAYAHR) ambao itakuwa na jukumu kutoa elimu ya uzazi wa mpango na afya ya uzazi kwa vijana wa Tanzania.

Wanachama wa Taasisi za AFRIYAN Fatma Said Ahmed (kushoto) na Hope Centre for Children, Girls and Women in Tanzania Penina Mgonela (kulia) wakisaini makubaliano ya kuwa taasisi moja ya Tanzania Youth and Adolescent Reproductive Health Coalition (TAYAHR) ambao itakuwa na jukumu kutoa elimu ya uzazi wa mpango na afya ya uzazi kwa vijana wa Tanzania.

Mwanachama wa Taasisi za AFRIYAN Fatma Said Ahmed (kushoto) akibadilishana mkataba na Mwenyikiti wa Taasisi ya Tanzania Youth and Adolescent Reproductive Health Coalition (TAYAHR) chairperson William Otuck baada ya kutia saini ya makubaliano ya kufanya kazi chini ya taasisi hiyo yenye lengo ya kutoa elimu ya uzazi wa mpango na afya ya uzazi kwa vijana wa Tanzania.

KAMPUNI YA ACACIA YACHANGIA MAPAMBANO YA VITA DHIDI YA UKIMWI.

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Tulia Ackson akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika lango la kupandia mlima Kilimanjaro,lango la Machame kwa ajili ya kutoa Baraka kwa washiriki wa changamoto ya kupanda mlima kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi zoezi linaloratibiwa na Kampuni ya Geita Gold Mining (GGM).
Mgeni rasmi katika shughuli ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za mapambano Vita ya Ukiwmwi ,Dkt Tulia Ackson akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mshikizi ,Mrisho Gambo (kushoto) na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ukimwi na Dawa za kulevya ,Dkt Faustine Ndugulile wakiimba wakipiga makofi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Geita Gold Mining (GGM) Terry Melpeter akizungumza katika shughuli hiyo iliyofanyika katika lango la Machame.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro mshikizi Mrisho Gambo akizungumza wakati wa shuguli hiyo ambayo hufanyika kila mwaka.
Zoezi la kuapnda Mlima likianza rasi huku likiongozwa na Naibu Spika ,Dkt Tulia Ackson ,Mrisho Mpoto akiongoza kwa nyimbo za kuhamasisha.
Zoezi la kupanda lilianza huku mvua ikinyesha

Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images