Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1722 | 1723 | (Page 1724) | 1725 | 1726 | .... | 3284 | newer

    0 0


    0 0


    0 0

    Na Nte Hosseah 

    Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo amekutana na wadau wa sekta ya utalii mkoani humo na kujadili nao namna mbalimbali wanazoweza kuboresha sekta ya utalii mkoani humo. 
    "Mkoa wa Arusha unachangia mapato ya utalii nchini kwa zaidi ya asilimia 80 hivyo sisi kama mkoa tukiwa na mikakati madhubuti ya kuiboresha hii sekta tutakua tumeikuza sekta hii kiasi cha kuleta matokeo chanya kwa taifa kiujumla." Alisema Gambo. 
    Nao chama cha wafanyabiashara wa utalii (TATO) walisema changamoto katika biashara hiyo ni nyingi lakini kwa sehemu kubwa wanaishukuru serikali ya awamu ya tano kwani katika awamu hii changamoto nyingi zimeonekana kutatuliwa, kwa kuongezea walisema kinachowapa hofu kwa kipindi hii kuelekea mwaka mpya wa fedha ni kuanza kwa tozo mpya ya ada ya mahoteli yanayolaza wageni porini (concession fee) ambapo wao kama walaji wa mwisho wanaona itawaathiri sana kwakua tangazo la serikali limetoka ndani ya muda mfupi, 
    "Tangazo limetoka mwezi Mei na wageni walishafanya booking toka mwezi Machi na tuliwapa bei zisizokua na tozo hizi, hivyo tunaomba serikali ilifikirie hili mara mbili na kutuongezea muda tuanze kulipa januari ili isituathiri kibiashara." Alisema bwana Willy Chambulo mwenyekiti wa TATO. Akiwatoa hofu hiyo Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA bwana Allan Kijazi amekiri kua hiyo tozo kwa wakati ni changamoto ila akawatia moyo kuwa bado kuna muda wa kulizungumza hilo kwani serikali hii ya awamu ya tano ni sikivu, na aliwataka wakutane wadau wote wajadiline waone namna ya kuishauri wizara kuongeza muda ili isiathiri biashara hii kwa ujumla. 
    Naye Mhe Gambo amewachagiza wadau hao kushirikiana na viongozi wa mkoa kuandaa tamasha kubwa la utalii la kimataifa litakalotumika kama jukwaa la kuutangaza mkoa na taifa kwa ujumla hasa kwa kualika mabalozi wa nchi ambazo huleta watalii wengi hapa nchini.
    Vilevile akatoa rai kwa wageni wawe na amani wawapo mkoani hapa kwani kwa sasa mkoa ni shwari na kamati yake ya ulinzi na usalama imejikita katika kuzima viashiria vyote vya uvunjifu wa amani. Vile vile Mhe Gambo amepokea jumla ya mablanketi 200 kati ya 400 kutoka Leopard tours na kuyabidhi kwa jeshi la magereza kwa ajili ya wafungwa katika gereza kuu Kisongo,
    Pia amekabidhi kompyuta moja na printer kwa wafungwa wa gereza hilo la Kisongo ikiwa ni katika utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa kwa wafungwa hao kipindi alipowatembelea mapema mwezi wa tano.
     Mkuu wa mkoa Mhe Gambo akiwa katika kikao na wadau wa utalii mkoani humo.
     Mkuu wa mkoa Mhe Gambo akiwa katika kikao na wadau wa utalii mkoani humo.
     Mkurugenzi wa TANAPA bwana Allan Kijazi akisikiliza kwa makini michango ya wadau katika kikao hicho,akifuatiwa na mkurugenzi wa Leopard Tours bwana Fazal,mwenyekiti wa TATO na bwana Willy Chambulo
     Mkurugenzi wa mamlaka ya Ngorongoro bwana Fredy Manongi akitoa mchango wake katika kikao hicho
    Mhe Gambo akipokea msaada wa mablanketi kwenda katika gereza la Kisongo Arusha

    0 0    0 0

     Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Msaada wa Kisheria {LSF} Tanzania Bwana Kees hapo Zanzibar Beach Resort Mazizini.
     Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akibonyeza kitufe cha Kompyuta kuashiria kuzindua rasmi Ofisi ya Taasisi ya Msaada wa Kisheria  Zanzibar { LSF} hapo Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini. Kulia ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa LSF Jaji Jouquine De Mello na kushoto ya Balozi Seif ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh. Omar Othman Makungu.
    Balozi Seif akiagana Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Msaada wa Kisheria Tanzania {LSF} Jaji  Jouquine De Mello baada ya kuizindua rasmi Ofisi ya Taasisi hiyo itakayokuwa mastakimu yake kwenye Jengo la ZSTC Kinazini Mjini Zanzibar. Picha na – OPMR – ZNZ. 

    0 0

    Timu ya Vijana ( Juvenile) ya Caltex Zanzibar na vikombe vyao mwaka 1964. Kutoka kushoto waliosimama ni Muhammed Ali, Muhamed Popat, Ahmed Ali, Hamad Suleiman,Khalid Sheikhan na Muhamed Peter na Team Manager Hija Saleh Hija.Walioketi: Hemed Haji, Muhammed Seif Khatib, Hassan Chita, Abass Fadhili na Seif Muhammed.

    0 0


    0 0

    Kufuatia kifo cha mmoja wa Waasisi wa CHADEMA, Mzee Philemon Ndesamburo Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA), Dkt. Vincent Mashinji, ametoa maelekezo kwa watendaji nchi nzima kupeperusha bendera nusu mlingoti.
    Mashinji ametoa maelekezo hayo leo wakati akiongea na Waandishi wa Habari Makao Makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam na kusema bendera zinapaswa kupeperushwa nusu mlingoti hadi mwili wa kiongozi huyo utakapopumzishwa katika nyumba yake ya milele.
    "Chama kitashiriki katika msiba huu kwa heshima zote kumuenzi mmoja wa waasisi wa siasa za mabadiliko ya kweli na Uhuru wa kweli nchini, msiba huu ni msiba wa CHADEMA, ni msiba wa Watanzania, ni msiba wa Taifa letu kutokana na mchango mkubwa wa Mzee wetu kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa nchi yetu, Mhe. Ndesamburo ndiye aliyekifadhili Chama kwa mara ya kwanza kwa kukipatia ofisi eneo la Kisutu jijini Dar es salaam" amesema Dkt. Mashinji

    0 0    Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa, John Mongela akisoma hotuba ya ufunguzi wa mafunzo kwa watumishi wa Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Maofisa Mipango wa Halmashauri za Wilaya wa Mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu kuhusu uandaaji wa mipango mikakati     Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwenye mafunzo kwa watumishi wa Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Maofisa Mipango wa Halmashauri za Wilaya wa Mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu kuhusu uandaaji wa mipango mikakati. 

    Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa, John Mongela (katikati) akizindua mwongozo wa kuandaa mipango mkakati ya wilaya. 
    Bwana Apolinary Tamayamali kutoka Ofisi ya Rais Ikulu akitoa neno kwa washiriki kuhusu mipango na mchakato wa uandaaji bajeti. 
    Mkurugenzi Mtendaji wa Self Microfinance Fund, Mudith Cheyo akitoa mada kwa washiriki kuhusu uandaaji wa mipango mikakati.
    Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA    0 0

    Rais wa Special Olympics Kanda ya Afrika ambaye pia ni mtendaji mkuu Bw. Charles Nyambe  (pichani) anatarajia kufanya ziara nchini Tanzania kuanzia tarehe 5/6/2017 hadi 9/5/2017. 

    Kwa mujibu wa Charles Rays, Mkurugenzi Special Olympics Tanzania, akiwa Tanzania Bw. Nyambe atapata fursa ya kuendesha mafunzo ya uongozi wa michezo ya Special Olympics  kwa makocha  50, ambao ni waratibu wa mikoa yote 30, pamoja na wengine 20 kutoka Dar es Salaam. 

    "Amependekeza  pia kutumia masaa matatu kati ya siku nne atakazokuwa nasi hapa Tanzania kukutana na kuendesha  mafunzo ya uongozi kwa  wajumbe wote wa board ya Special Olympics Tanzania", amesema Bw. Rays.

    0 0

     Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya WazaziTanzania, Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka wilaya za Uvinza, Kigoma Vijijini na Kigoma Mjini, Mabalozi, Watendaji wa Chama na wa Serkali, mjini Kigoma, leo
     Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka wilaya za Uvinza, Kigoma Vijijini na Kigoma Mjini, Mabalozi, Watendaji wa Chama na wa Serkali, mjini Kigoma, wakishangilia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya WazaziTanzania, Alhaj Abdallah Bulembo alipokuwaakizungmza nao katika kikao kilichofanyika Kigoma mjini, leo.
     Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho.
     Wajumbe kutoka Uvinza wakishangilia walipotambulishwa
     Afisa Afya wa mkoa wa Kigoma, Ambakisye Mhune akitoa darasa kwa wajumbe wa kikao hicho namna ya kujihami na ugonjwa wa Ebola, ambao alisema, hivi sasa umelipika ena katika nchi jirani ya Congo DRC.
     Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya WazaziTanzania, Alhaj Abdallah Bulembo, akizungumza na wajumbe kutoka ufafanuzi wa maswala mbalimbali ikiwemo uhaguzi ndani ya Chama, Ndugu Bulembo kabla ya kuzungumza na wajube hao alitawazwa kufalishwavazi la heshima la Waha laaina ya Mpuzu, ambalo ni ishara ya kiongozi makini na mwenye kuheshimika
     Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya WazaziTanzania, Alhaj Abdallah Bulembo, akikabidhi fedha kwa uongozi wa shina hilo, fedha hizo alichangisha kwa wadau waliokuwemo kisha akajazia mwenyewe. PICHA: BASHIR NKOROMO


    0 0
    0 0


    0 0

    SHIRIKA la Nyumba la Taifa Mkoani Tanga (NHC) limewa tahadharisha watu wanaoghushi fomu za maombi ya kupangisha katika nyumba zao na kuziuza kwa wananchi kuacha mara moja tabia hiyo kwani watakabanika watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kufikishwa kwenye vyombo vya dola.

    Kauli hiyo ilitolewa juzi na Meneja wa Shirika hilo,Mussa Kamendu wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu mipango mbalimbali ya shirika hilo ikiwemo kuzifanyia ukarabati nyumba wanazozimiliki ili ziweze kuwa katika muonekana mzuri kwa zile ambazo zimeonekana kuchakaa.

    Alisema kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wananchi kughusi fomu ambazo zinatolewa na shirika hilo kwa kuzisambaza kwa wengine na kuwauzia jambo ambalo ni kinyume na utaratibu uliopo.

    “Ukiangalia sisi kama shirika tumekuwa tukitoa fomu kwa wananchi ambao wanataka kupangisha kwenye nyumba zetu lakini katika hilo kumejitokeza baadhi ya watu wanazitoa kopi na kuziuza kitendo ambacho ni uvunjifu wa taratibu tulizoziweka “Alisema.

    “Jambo hili ni hatari hasa kwa ustawi wa shirika letu kwani
    linachangia kukosesha mapato hivyo tutahakikisha tunawa shughulikia watakaobainika kufanya hivyo bila kuangalia nafasi yake kwa maslahi ya ustawi wa shirika letu “Alisema Meneja huyo. 
    Meneja wa Shirika la Taifa la Nyumba(NHC) mkoani Tanga Mussa Kamendu katikati akionyesha moja kati ya chemba ambazo zinafanyiwa ukarabati eneo la mtaa wa market Jijini Tanga na Fundi Mchundo wa Shirika hilo jana wakati alipotembelea kuona hali ya ukarabati huo unavyoendelea.
    Meneja wa Shirika la Taifa la Nyumba(NHC) mkoani Tanga Mussa Kamendu katikati akionyesha waandishi wa habari maeneo mbalimbali waliokarabati
    Mafundi wakiendelea na kazi kama wanavyoonekana
    Meneja wa Shirika wa Shirika la Taifa la Nyumba Mkoani Tanga (NHC),Mussa Kamendu akikagua mitaro iliyochimbwa kwa ajili ya kupitisha mfumo wa maji taka.
    0 0

    Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini

    MAZISHI ya Mbunge mstaafu wa jmbo la Moshi mjini na Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro Philemon Ndesamburo Kiwelu (82) yanataraji kufanyika kwa siku mbili mfululilizo huku watu zaidi ya laki 2 wakitaraji kushiriki katika mazishi hayo.

    Shughuli nzima za mazisihi zinataraji kufanyika June 5 na sita katika uwanja wa mashujaa mjini Moshi kabla ya kuhitimishwa siku ya Jumanne kwa ibada itakayoanzia kanisani na kumalizikia nyumbani kwa marehemu. 

    Hatua ya maziko ya Ndesamburo kufanyika kwa siku mbili inatokana na uwepo wa idadi kubwa ya marafiki wa familia kushiriki katika maziko hayo ya kihistoria yatakayotanguliwa na kutoa heshima za mwisho ,shughuli zilizopangwa kufanyika katika uwanja wa mashujaa mjini Moshi.

    Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichodumu kwa zaidi ya saa nne ,Msemaji wa Chadema katika maandalizi ya mazishi hayo Amani Golugwa amesema uamuzi huo unatokana na kutoa nafasi kwa watu mbalimbali kutoa heshima za mwisho kwa Ndesamburo.

    “Tumekua na kikao na wanafamilia viongozi wa chama na mashaurizano kuhusiana na msiba huu ,tumekuwa na watoto wa marehemu ,walikuwepo wachungaji na viongozi wa chama ,kimsini tumekubaliana mazishi ya mze wetu Ndesamburo yatafanyika kwa siku mbili mfululizo”alisema Golugwa.
    Kikao cha Wanafamilia,Viongozi wa siasa na Viongozi wa Dini kikifanyika nyumbani kwa marehemu Ndesamburo kwa ajili ya maandalizi ya mazishi yake.
    Ndugu na Baadhi ya watoto wa marehemu Philemoni Ndesamburo wakiwa katika kikao hicho.
    Baadhi ya Viongozi wa Chadema wakishiriki katika kikao hicho.
    Baadhi ya watoto wa marehemu Philemoni Ndesamburo.
    Baadhi ya Wabunge wakishiriki katika kikao hicho.
    Baadhi ya wanandugu wa familia ya marehemu Ndesamburo.
    0 0


    * Ni kwenye malipo ya mawakala wa mbolea, awali yalifikia sh. bilioni 65.
    *Akiri kukutana nao, asema wenye madai halali wote watalipwa

    WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imebaini madudu katika uhakiki wa madeni ya mawakala wa mbolea kwa sababu baadhi yao hawakuwa waaminifu.

    “Tulipoanzisha mfumo wa kutoa pembeje kwa njia vocha kwa kuwatumia mawakala kupeleka pembejeo vijijini, tulibaini kuwa baadhi yao walikuwa siyo waaminifu. wakiorodhesha majina ya wakulima na kuandika kuwa wamewapa madawa napembejeo wakati hawapo.”

    Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Juni mosi, 2017) wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (Morogoro), Bi. Devotha Minja kwenye kipindi cha maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu bungeni mjini Dodoma.

    Bi. Minja alitaka kujua ni kwa nini Serikali haijawalipa mawakala hao hadi sasa licha ya kuwa inatambua kwamba walifanya kazi ya kusambaza pembejeo hizo.

    “Tulijikuta tuna deni la shilingi bilioni 65. Nilipokutana na mawakala wiki mbili zilizopita, niliwaahidi kwamba tutawalipa lakini ni lazima watupe muda tufanye uhakiki ili kubaini kama kweli pembejeo zilifika. Kati ya shilingi bilioni 35 za madeni ya awali, imebainika kuwa sh. bilioni 6 tu ndiyo za halali. Na bado kuna sh. bilioni 30 nyingine zinafanyiwa uhakiki,” amesema Waziri Mkuu.

    “Tumewasihi waendelee kuwa wavumilivu ili tukamilishe zoezi hili na tujue Serikali inadaiwa kiasi gani. Napenda niwahakikishie kuwa kazi hiyo inaendelea na tuko kwenye hatua za mwisho, na wale wote wenye madai halali ambao ni waaminifu watalipwa na Serikali.”

    Akijibu swali la nyongeza ni kwa nini Serikali isiharakishe malipo hayo kwani kuna baadhi nyumba zao zimepigwa mnada na mabenki, na wengine wamepoteza maisha kwa sababu ya mshtuko, Waziri Mkuu alisema siku ya mwisho ya kufanya uhakiki ilikuwa jana Mei 31 kwa hiyo anasubiri taarifa kutoka Halmashauri zote kupitia kwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

    KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

    0 0

     Exim Bank Tanzania imetambuliwa kama Benki bora ya mwaka katika wateja binafsi na biashara ndogondogo na saizi ya kati, yaani ‘Retail banking’ katika tuzo za Banker za Afrika Mashariki zilizofanyika Nairobi, Kenya. 

    Tuzo za Banker za Afrika Mashariki zimedhamiria kuhamasisha ubora kwenye sekta ya fedha katika kanda ya Afrika Mashariki. Kupitia kura 77,000 zilizopigwa na jamii ya sekta ya fedha katika kanda hii benki ya Exim ilichaguliwa kama mshindi wa mwaka huu katika wateja binafsi na biashara ndogo - Retail. 

    Akiongea kwa niaba ya benki hiyo, Mkuu wa kitengo cha fedha Selemani Ponda alisema, “Tunajivunia sana na kushukuru kwa tuzo hii. Tumefanya kazi kubwa kwa muda mrefu kujenga msingi wa kuendeleza operesheni zetu za baadae. Matokeo yanajionyesha, katika miaka ya karibuni amana kutoka kwa wateja wetu imeongezeka na wateja pia wameongezeka. Vilevile faida baada ya kodi imeendelea kukua hadi kufikia kiasi cha shilingi bilioni 72 kwa mwaka 2016.” 

    Ponda ambaye alihudhuria hafla ya tuzo hizo alitoa pongezi kwa waandaaji kwa kuandaa tukio lenye mafanikio kwa miaka mine mfululizo. Hadi sasa tuzo hizo zimevutia ushiriki wa wanataaluma wengi zaidi katika sekta ya benki katika kanda hii. Zaidi ya hapo aliongeza kuwa washirika muhimu kama vile kampuni za teknolojia ambazo husaidia kubadilisha sekta hii pia zilitambuliwa kwa mchango wao. 

    KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


    0 0

    Na Jamila Omary, Arusha.
    Shirika la Maendeleo  ya Mitaji la Umoja wa Mataifa(UNCDF), limezindua  mpango wa kuziwezesha halmashauri za majiji na Manispaa kuweza kunufaika na masoko ya mitaji kwa kuwekeza katika soko la hisa kuuza vipande na kutoa hati za dhamana.

    Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, alizindua mpango huo jijini hapa kwa niaba ya Waziri wa nchi ofisi za Rais (TAMISEMI), George Simbachawene  na kuwataka watendaji na halmashauri za majiji na manispaa ,wanaohudhuria mafunzo hayo kujiandaa kutumia fursa hiyo.

    Gambo alisema katika mpango huo, ambao unatarajiwa kuongeza mapato kwa halmashauri za majiji na manispaa nchini, kutokana na kuelimisha ni jinsi gani wataweza kuwekeza katika soko la hisa na kupata fedha za miradi ya maendeleo.
    Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akizungumza wakati wa kufungua semina ya siku mbili ya fursa mpya ya kuongeza mapato ya halmashauri nchini iliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo la UNCDF iliyofanyika katika hotel ya Mount Meru jijini Arusha jana.

    Alisema mpango huo, ambao unataribiwa na UNCDF unaziezesha halmashauri kupata fedha nyingi ambazo zitawezesha kuendesha miradi mikubwa ya miundombinu na hivyo kuchochea wanannchi.

    Awali, Mratibu wa mfuko wa mitaji wa umoja wa mataifa(UNCDF) Peter Malika alisema,mpango huo wa kuwezesha halmashauri za majiji na manispaa, umeanza kwa majiji matato na manispaa tatu.

    Malika alisema Majiji ambayo yatakuwa katika mpango huo ni Dar es Salaam,Mwanza, Arusha, Mbeya na Tanga na Manispaa ambazo zitahusika ni Kinondoni,Temeke,Ilemela na Dodoma.
    "majiji haya na manispaa wanauwezo wa kuanza kuwekeza katika masoko ya hisa kwa kuuza hati za dhamana na wataweza kupata fedha kwa miradi mikubwa ya maendeleo"alisema.

    Mkurugenzi wa jiji la Arusha, Athuman Kihamia, alisema mpango huo tayari umeonesha mafanikio katika majiji kadhaa, ikiwepo Afrika Kusini,  Marekani na Asia na wanatarajiwa utaboresha mapato ya halmashauri.

    Kihamia alisema jiji la Arusha tayari limejiandaa kunufaika na mpango huo na tayari lina kampuni ya Arusha Investment ambayo inaweza kushiriki katika masoko ya hisa.
    Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuzindua mpango wa kuziwezesha halmashauri za majiji na Manispaa kuweza kunufaika na masoko ya mitaji kwa kuwekeza katika soko la  la hisa kuuza vipande na kutoa hati za dhamana, jana.

    0 0

    Katibu Tawala mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari aliyesimama, akizungumza na wahariri na waandishi wa Habari katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na mfuko wa Bima ya Afya nchini, NHIF. Katika warsha hiyo, NHIF imepokea taarifa ya utafiti uliofanywa kwa ushirikiano na wanahabari kuangalia ubora/changamoto za utoaji wa bima ya afya nchini.
    Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bernard Konga, Agnes Chaki, wa kwanza kushoto, na kulia kwake ni Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Theophil Makunga na karibu wake, Nevil Meena. Picha na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
    ⁠⁠⁠Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya nchini, NHIF, Bernard Konga akiongea na wahariri na waandishi wa Habari wakati wa warsha ya siku moja ya kupokea taarifa ya utafiti juu ya kuangalia ubora/ changamoto za utoaji wa bima ya afya nchini
    Mkurugenzi msaidizi Habari maelezo, (Habari) Rodney Thadeus akiongea kwa niaba ya Serikali juu ya huduma zinazofanywa na NHIF nchini wakati ya warsha hiyo.
    Baadhi ya wahariri wa nyombo mbalimbali vya habari nchini wakifuatilia warsha ya siku moja ya wanahabari iliyofanyikoa mkoani Morogoro, wakati NHIF ikipokea taarifa ya utafiti uliofanywa na baadhi ya waandishi wa Habari kuangalia ubora/ changamoto za utoaji wa bima ya afya nchini.
    Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia warsha hiyo.

    0 0

    Jana, Juni 1, 2017, Wakurugenzi wa Mfuko wa Maendeleo ya Soka Tanzania (TFDF), Derek Murusuri na Taasisi ya Media Tanzania (TMF) Ernest Sungura, walimtembelea Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson, ofisini kwake mjini Dodoma. Pichani, Bw Sungura akiongea na Mh Naibu Spika, Dk Tulia Ackson.

older | 1 | .... | 1722 | 1723 | (Page 1724) | 1725 | 1726 | .... | 3284 | newer