Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109588 articles
Browse latest View live

TAIFA STARS YAANZA KUJIFUA NCHINI MISRI KUIKABILI LESOTHO JUNI 10 UWANJA WA TAIFA

0
0

Wachezaji wa Taifa Stars wakipasha joto miili yao kabla ya kuanza mazoezi ya nguvu kwenye Uwanja wa Tolip Sports City jijini Alexandria leo asubuhi Juni 01, 2017. Taifa Stars  inajiandaa kushindana na Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.
 Makipa wa Taifa Stars kutoka kushoto, Said Mohammed, Aishi Manula na Benno Kakolanya wakivuta pumzi baada ya mazoezi ya timu ya Tanzania ya Mpira wa Miguu ‘Taifa Stars’ yaliyofanyika jana usiku kwenye Uwanja wa Tolip Sports City jijini Alexandria jana usiku Mei 31, 2017. Taifa Stars  inajiandaa kushindana na Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.
Daktari wa Viungo wa Taifa Stars, Dk. Gilbert Kigadye akimfanyisha mazoezi ya kifundo cha mguu beki wa timu hiyo, Mohammed Hussein Zimbwe maarufu kama Tshabalala katika mazoezi ya timu ya Tanzania ya Mpira wa Miguu ‘Taifa Stars’ yaliyofanyika Uwanja wa Tolip Sports City jijini Alexandria jana usiku Mei 31, 2017. 


 Wachezaji wa Stars wakiwania mpira katika mazoezi ya nguvu yaliyofanyika leo. Taifa Stars inajiandaa kushindana na Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.
 Wachezaji wa Stars kutoka kushoto, Mohammed Hussein, Simon Msuva, Said Mohammed, Ibrahim Ajib na Hassan Kessy wakionesha faraja yao mara baada mazoezi ya nguvu yaliyofanyika leo. Taifa Stars  inajiandaa kushindana na Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


DAWASCO YATOA NOTISI KWA WADAIWA SUGU WA BILI ZA MAJI

0
0
Dawasco inawatangazia wateja wake wote wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, pamoja na Mji wa Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani wenye madeni ya bili za Maji kwa kipindi cha zaidi ya Mwezi mmoja kuwa, wanatakiwa kulipa madeni yao kabla ya tarehe 11.06.2017, kinyume na hapo Dawasco inakusudia kuwafikisha Mahakamani wateja wote wanaodaiwa kipindi hicho cha zaidi ya mwezi mmoja.

Taarifa hii inawahusu wateja wote wenye madeni pamoja na wale watakaoshindwa kulipa madeni yao ndani ya muda uliotajwa.

Mteja atakayeshindwa kulipa deni lake ndani ya muda tajwa atalazimika kulipia bili yake, pamoja na gharama zote za kuendesha kesi kwa wale watakaofikia hatua ya kufunguliwa mashtaka na faini.

Kumbuka Dawasco haipokei Malipo taslimu (Mkononi), malipo yote yafanyike kupitia huduma za Kibenki, mawakala wa Selcom na Maxcom, pamoja na mitandao yote ya simu ambayo imeidhinishwa.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia kituo chetu cha huduma kwa wateja kwa namba 0800110064 (BURE)

IMETOLEWA NA MKURUGENZI MKUU
DAWASCO

Tatizo la ugonjwa wa macho ni kubwa kwa kukosa rasilimali watu yenye utaalam-Dk. Bernadetha

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Tatizo la ugonjwa   wa macho katika nchi ni kubwa ambalo linachangiwa kwa kukosa rasilimali watu pamoja na vifaa vya kisasa katika kutatua changamoto hiyo.

Akizungumza katika kikao cha wadau wanaoshughulika na masuala ya macho kilichoandaliwa na Sightsavers , Kaimu Meneja wa Mpango wa Taifa wa Huduma za Macho wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto, Dk. Bernadetha Shilio amesema tatizo la macho ni dogo katika nchi lakini kutokana na kukosa kwa rasilimali watu pamoja na vifaa vya kufanyia oparesheni linafanya tatizo kuwa kubwa.

Amesema kutokana na tatizo la ugonjwa wa macho kuwa kubwa wameandaa mikakati ya kutatua,ikiwemo kuongeza rasilimali watu pamoja na vitendea kazi kwa ajili ya kufanyia operesheni.

Dkt.Bernadetha amesema kuwa kuna ushirikiano na mashirika mbalimbali katika yanayosaidia kutoa huduma ya ugonjwa wa macho katika sehemu mbalimbali nchini.Mkurugenzi Mkazi wa Sightsavers, Gosbart Katuzi amesema kuwa tatizo la ugonjwa wa macho unatokana na kitoto cha jicho na kufanya wengine kupofoka.

Amesema kuwa katika mradi mwaka 2009 walipeleka vifaa katika mkoa morogoro ambapo katika kliniki hiyo zaidi watu 12000 walibainika kuwa na ugonjwa wa macho.Katuzi amesema kuwa kwa sasa ya watu milioni moja wana matatizo ya macho hali hiyo jitihada zinatakiwa kufanyika katika kuifikia idadi hiyo ambayo itakuwa ikiongezeka kwa kila mwaka.

Mkurugenzi wa Help Age International, Smart Daniel amesema ugonjwa wa macho umekuwa ukiwakumba wazee ambapo hushindwa kufanya kazi zao kutokana na ugonjwa wa macho.

Amesema kuwa kuna jitihada ambazo zimekuwa zikifanyika katika  kuwafikia wenye ugonjwa macho na watu wengine kwa kufanyiwa oparesheni.
Kaimu Meneja wa Mapngo wa Taifa wa Huduma za Macho wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto, Dk. Bernadetha Shilio akizungumza katika kikao juu wadau wanashughulika na ugonjwa wa macho leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Sightsavers, Caroline Harper akizungumza juu ya taasisi hiyo ilivyoweza kusaidia maeneo mbalimbali nchini kwa watu wenye ugonjwa macho leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Help Age International, Smart Daniel akizungumza katika mkutano wa wadau wanaoshughulika na ugonjwa macho juu ya wazee walivyokuwa wahanga wa ugonjwa huo leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Mahusiano na Masoko wa Standard Chartered ,Juanita Mramba akizungumza juu ya utoaji wa msaada wa benki hiyo kwa watu wenye ugonjwa wa macho leo jijini Dar es Salaam
Wadau wa wanaoshulika na ugonjwa wa macho wakiwa katika picha pamoja leo jijini Dar es Salaam.

KAMPUNI YA MAZIWA YA ASAS DAIRIES LTD YANYWESHA MAZIWA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI MANISPAA YA IRINGA

0
0

WAKATI leo ni siku ya unywaji maziwa duniani kampuni ya maziwa ya Asas Dairies Limited imenywesha maziwa wanafunzi zaidi ya 4000 wa shule mbali mbali za Manispaa ya Iringa .

Shule hizo za msingi zilizopo kanda ya Ruaha ambazo zimeanza kunufaika na unywaji maziwa ,huku walimu wao wakidai baadhi ya wanafunzi wa shule hizo wamekuwa na matokeo mabaya katika mitihani kutokana na unywaji wa pombe ya kienyeji aina ya ulanzi .

Meneja wa miradi wa kampuni ya Asas Dairies Ltd Hassan Swedi alisema kuwa maadhimisha ya mwaka huu yamelenga zaidi vijana hasa wanafunzi wa shule za msingi mjini Iringa na ndio sababu kampuni yake imelazimika kutoa msaada wa maziwa na majaketi kwa wanafunzi wanaotoka katika familia duni .

Alisema kuwa kampuni hiyo inaamini kuwa iwapo shule zitaweka utaratibu wa kutoa maziwa kwa wanafunzi afya za wanafunzi hao zitakuwa bora na kiwango cha elimu kinaweza kuongezeka zaidi mashuleni.

Mbali ya unywaji wa maziwa kuhamasishwa zaidi mashuleni bado viongozi wa serikali wanapaswa kuanza kuhamasha unywaji wa maziwa katika ofisi hizo za umma badala ya kutumia maziwa kutoka nje ya nchi .
Alisema kuwa kampuni ya Asas Dairies

Ltd imeendelea kuunga mkono mpango wa lishe mashuleni kama njia ya kuboresha afya na uwezo wa wanafunzi kufanya vizuri kwenye masomo Iringa unazalisha maziwa zaidi ya lita milioni 14 kwa mwaka ila bado kiwanda cha Asas kinasindika lita 400,000 pekee kwa siku .

Meneja miradi wa kampuni ya maziwa ya Asas Dairies Ltd Hassan Swedi akimpa maziwa mlemavu 
leo siku ya unywaji maziwa duniani

wafanyakazi wa kampuni ya Asas wakigawa maziwa kwa wanafunzi leo siku ya unywaji maziwa duniani .


YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 39, MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO JUNI 01, 2017.

0
0
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk. Tulia Ackson akijibu miongozo mbalimbali ya wabunge mara baada ya kumaliza kipindi cha Maswali ya Kawaida katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 01, 2017.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akijibu maswali ya papo kwa papo mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 1, 2017.
 Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 1, 2017.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mhe.George Simbachawene katika kikao cha 39 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 1, 2017.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MKEMIA MKUU WA SERIKALI KUIMARISHA OFISI ZA KANDA

0
0
Frank Mvungi-Maelezo
Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali imedhamiria  kuimarisha Ofisi za Kanda ili kusogeza huduma kwa wananchi katika Mikoa yote, ikiwa ni katika juhudi zake za kuimarisha utendaji na kuongeza tija na uwajibikaji.

Kauli hiyo imetolewa  leo Jijini Dar es Salaam na Meneja Mawasiliano na Masoko wa Ofisi hiyo Bw. Cletus Mnzava ,alipozungumza na waandishi wa  habari juu ya   majukumu ya Ofisi hiyo na huduma zinazotolewa.

“Mwelekeo ni kuimarisha Ofisi zetu za Kanda ili kusogeza huduma karibu  kwa wananchi, kwa sasa tunaendelea kuimarisha Ofisi ya Dodoma kama Makao Makuu ya Nchi ambayo pia itahudumia Mikoa ya Iringa,Morogoro na Singida” Alisisitiza Mnzava.

Akifafanua Mnzava alisema Ofisi hiyo imejipanga kuendana na sera ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga Tanzania ya Viwanda  kwa sababu viwanda vitakuwepo kila kona ya nchi na viwanda vinatumia kemikali hivyo vinatakiwa vifuatiliwe kwa ukaribu ili matumizi yafanyike kwa mujibu wa Sheria na taratibu zilizowekwa.

Aliongeza kuwa moja ya mikakati ya Ofisi hiyo ni kuwepo kwa watumishi wanaodhibiti uingizwaji wa kemikali usiofuata taratibu ambapo wakaguzi hao kwa sasa wako katika mipaka ya Namanga,Holili na Horohoro kwa upande wa kanda ya Kaskazini.

Kwa upande wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wakaguzi hao wako katika mipaka ya Tunduma,Kasumulu na Mutukula ,Sirari kwa upande wa Kanda ya Ziwa ambapo mpango mkakati wa Ofisi hiyo ni kuhakikisha kuwa Lengo la Serikali kusogeza huduma karibu na wananchi linatimia.

Kwa upande wake Meneja wa Ukaguzi wa Kemikali Bw. Fidelis Segumba amesema Maabara hiyo imejipanga kuwahudumia wananchi vizuri nyakati zote.
Meneja Mawasiliano na Masoko wa kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bw. Cletus Mnzava akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu uimarishaji wa Ofisi za Kanda ili kusogeza huduma karibu na wananchi. Kushoto ni Afisa Habari wa Ofisi hiyo Bw. Sylivesta Omari.
Meneja ukaguzi wa Kemikali Bw. Fidelis Segumba akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.kulia ni Meneja Mawasiliano na Masoko wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bw. Cletus Mnzava (Picha na Frank Mvungi-Maelezo)

MKUU WA MKOA NJOMBE ATEMBELEA MIRADI YA ELIMU NA AFYA

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh. Christopher Ole Sendeka akiweka jiwe la msingi kwenye  nyumba za waalimu shule ya sekondari ya wasichana Anne Makinda.Nyumba zenye uwezo wa kuishi waalimu 6 katika nyumba moja "6 in 1".
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka akikagua uimara wa milango kwenye moja ya madarasa katika shule ya sekondari ya wasichana Anne Makinda.Nyuma yake ni Mh. Mkuu wa Wilaya ya Njombe Ruth Msafiri.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka akisisitiza jambo kwa Wananchi (hawapo pichani)  kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Luponde mara baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye jengo la OPD  kituo cha afya Luponde wa kwanza kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Edwin Mwanzinga
Wananchi wa Kijiji cha Luponde wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa katika mkutano wa hadhara
Mkuu wa Mkoa wa Njombe akiwa katika Picha ya pamoja na uongozi wa wanafunzi shule ya sekondari ya wasichana Anne Makinda,Shule hiyo ya Kata ilifanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne mwaka jana na kushika nafasi ya Tano Kimkoa na Nafasi ya Kwanza Kiwilaya.

SPIKA MSTAAFU ANNE MAKINDA AWAASA MADIWANI WANAWAKE WA JIJI LA DAR KUJITAMBUA KATIKA JAMII

0
0
Madiwani wanawake wa vyama mbalimbali vya siasa katika Mkoa wa Dar es Salaam wamesema suala la kubadili mtazamo katika ushirikishwaji wa wanawake kwenye maendeleo ni la msingi na linapaswa kutekelezwa kuanzia ngazi za chini. 


Wakizungumza katika warsha ya siku tatu ya Uongozi wa Kijinsia iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP Mtandao), madiwani hao wamesema haki za wanawake bado zinakandamizwa katika jamii huku vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia vikishika kasi. 


Akizungumza katika mafunzo ya siku tatu Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Anne Makinda amesema wanawake wanapaswa kuungana kwa pamoja wanapokuwa wanapigania haki zao za msingi. Amewasisitiza kuachana na masuala ya vyama kwenye jambo linalowahusu wanawake wote. Wakifanya hivyo wataweza kupunguza tabaka kubwa kwenye utawala na hata kwenye uzalishaji mali.
Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Anne Makinda akiwahamasisha Madiwani wanawake wa Jiji la Dar es Salaam walioudhuria mafunzo  ya uongozi, jinsia na bajeti yenye mlengo wa kijinsia pamoja na kutoa uzoefu wake kwenye maswala ya uongozi  kwa wanawake hasa ngazi za juu leo kwenye ukumbi wa TGNP Mtandano jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi Lilian Liundi akizungumza na Madiwani Wanawake kuhusu nguvu ya mwanamke kwenye  jamii  pamoja na kuwapa miongozo kuhusu nafasi zao kwenye uongozi ili kufikia lengo la hamsini kwa hamsini.

Mwanachama wa TGNP Mtandao na mkufunzi wa Mafunzo ya Madiwani wanawake wa Jiji la Dar Es Salaam Profesa Ruth Meena akiwasilisha  mada kuhusu kujitambua kwa mwanamke kwenye jamii, kujua thamani yake pamoja na mchango wake kwenye jamii katika mafunzo yaliyofanyika kwenye ukumbiwa TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

KUELEKEA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI.

0
0
Usafi wa kila mwisho wa mwezi waimarisha mazingira nchini

KILA ifikapo Juni 5 kila mwaka, zaidi ya nchi 100 zinaadhimisha Siku ya Mazingira Duniani. Jovina Bujulu wa Idara ya Habari (MAELEZO) anaelezea umuhimu wa siku hii ambayo hapa nchini itaadhimishwa tarehe 3 na 4 mkoani Mara katika kijiji cha Butiama. 

Madhumuni makubwa ya maadhimisho haya ni kuhamasisha jamii duniani kote kuelewa masuala yanayohusu mazingira na pia kuhamasisha watu kulinda na kuhifadhi mazingira. Aidha, ni siku ambayo jamii inatakiwa kutambua umuhimu wa kulinda na kuhifaddhi mazingira kwa ustawi na maendeleo ya nchi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais, Muungano na Mazingira, maadhimisho hayo mwaka huu yatafanyika kijijini Butiama ili kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na kukumbuka mchango wake mkubwa katika masuala ya mazingira.

Wakati wa maadhimsho hayo shughuli mbalimbali zitafanyika zikiwemo kupanda miti, kuendesha mijadala mbalimbali na kongamano la viongozi kuhusu mazingira na pia kufanya maonyesho ya shughuli za mazingira.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ambayo Kauli Mbiu ya mwaka huu niHifadhi ya Mazingira: Muhimili kwa Tanzania ya Viwanda atakuwa Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan. Kaulimbiu hii inahamasisha Utunzaji wa mazingira wakati tukielekea uchumi wa viwanda.

Tarehe 9 Desemba mwaka jana, Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli aliamuru kusitisha maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Uhuru wa Tanganyika na badala yake siku hiyo iadhimishwe kwa kufanya usafi wa mazingira nchini kote. 

BALOZI WA CHINA NCHINI AMTEMBELEA SPIKA NDUGAI LEO WILAYANI KONGWA MKOANI DODOMA.

0
0
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Balozi Lou Youqing (kulia) kabla ya kuanza ziara ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo iliyopo wilaya ya kongwa Mkoa wa Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Banyibanyi wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo iliyopo wilaya ya kongwa Mkoa wa Dodoma.​
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kushoto) akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo iliyopo wilaya ya kongwa Mkoa wa Dodoma. kulia ni Balozi wa China nchini Tanzania, Mheshimiwa Balozi Lou Youqing na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya kongwa, Mheshimiwa Deogratius Ndejembi
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kulia) akiongozana na Balozi wa China nchini Tanzania, Mheshimiwa Balozi Lou Youqing wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo iliyopo wilaya ya kongwa Mkoa wa Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati)akitembelea shule ya msingi ya Ibwaga, shule aliyosoma wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo iliyopo wilaya ya kongwa Mkoa wa Dodoma. wa pili kushoto, ni Balozi wa China nchini Tanzania, Mheshimiwa  Balozi Lou Youqing.

DKT SHEIN AZUNGUMZA WAKATI WA UZINDUZI WA MFUMO WA ULIPAJI MAPATO KIELEKTRONIKI

VOA SWAHILI: Ramadhani katika nchi za vita na migogoro

WANAFUNZI 40 WA SHULE YA SEKONDARI WASICHANA SONGEA MKOANI RUVUMA WAUNDA KLABU USALAMA BARABARANI

MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA MKOANI MBEYA

0
0
Afisa Maliasili Mkoa wa Mbeya Ndugu, Joseph Butuyuyu akizungumza na Globu ya Jamii alipokuwa  juu ya Maadhimisho ya kilele cha mazingira duniani yanayo tarajia kufanyika Juni 5, mwaka huu ambapo kimataifa yatafanyika Nchini Canada, na Kitaifa yatafanyika Mkoani Mara na Kwa Mkoa wa Mbeya yanatarajiwa kufanyika wilayani Mbarali katika eneo la Mabadaga siku hiyo ya Jumatatu na mgeni Rasmi kwa mkoa wa Mbeya Atakuwa ni mkuu wa mkoa wa mbeya Mh.Amos G. Makalla na watu wote mnakaribishwa.
Ndugu, Joseph Butuyuyu Pia aliongeza kwa kuwataka wananchi wa mkoa wa mbeya kutunza na kuthamini mazingira yanayo wazunguka ili kupendezesha na kuyatunza vizuri mazingira ya mkoa wa mbeya na kuwataka wananchi kuchungamkia fursa ya kutembelea vivutio mbalimbali ikiwemo mbuga za wanyama bira kulipa kiingilio chochote kwa siku tatu mfululizo kuanzia siku ya Tarehe 2, mpaka Tarehe 4, ya mwezi huu.

Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Mazingira Duniani kwa mwaka huu ni   (Mausiano endelevu kati ya Binadamu na Mazingi) hiyo ikiwa ni kimataifa na kitaifa ni.. Hifadhi ya Mazingira ni Muhimili kwa Tanzania ya Viwanda.
NA MR.PENGO MBEYA.

Baada ya Arusha, Sheikh Shariff Majini kuendelea na mikutano yake mkoani morogoro

0
0
Sheikh Shariff  Majini baada ya kumaliza ziara ya mkoa wa Arusha wikiendi hii.  Tarehe 10 na 11 Juni anataraji kufanya mikutano kwa siku hizo mbili Mkoani Tanga. Maandalizi yote yamekwisha kukamilika na mikutano itafanyikia katika ukumbi wa Makorora Community Centre.
Baada ya kumaliza mkutano Sheikh Shariff Majini atakuwa Tanga kwa siku mbili zaidi ili kusikiliza shida za watu mbalimbali ambao watakaokosa kuhudhuria mkutano. Baada ya Tanga Sheikh Shariff anataraji kwenda Morogoro.

INTRODUCING NEW SINGLE BY P ONE BLACK - TUPA SHUKA

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA KITUO KUTUNZA TAARIFA NA MFUMO WA KUKUSANYIA MAPATO KIELEKTRONIKI

0
0



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akionesha Ipad maalumu aliyopewa ili kumuwezesha  kufuatilia ukusanyaji wa mapato ya kila siku. Kulia kwake ni  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na kushoto kwake ni  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wakati wa  kutembelea kituo cha kutunzia taarifa (Data Centre) kabla ya kuzindua  Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki   kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017. Picha na Ikulu
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein  akionesha Ipad maalumu aliyopewa kumuwezesha  kufuatilia ukusanyaji wa mapato ya kila siku. kushoto kwake ni  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wakati wa  kutembelea kituo cha kutunzia taarifa (Data Centre) kabla ya kuzindua  Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki   kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017. Picha na Ikulu
 Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akionesha Ipad maalumu itayomuwezesha kufuatilia ukusanyaji wa mapato ya kila siku. Kulia kwake ni  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein na viongozi wengine wakati wa  kutembelea kituo cha kutunzia taarifa (Data Centre) kabla ya kuzindua  Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki   kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017. Picha na Ikulu

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akishuhudiwa  na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine akizindua  Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki   kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017. Picha na Ikulu

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi katika picha ya pamoja na wakuu wa makampuni ya mawasiliano mbalimbali nchini kwenye sherehe ya uzinduzi wa Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki   kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017. Picha na Ikulu

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 10.06.2017

HOTUBA YA RAIS MAGUFULI KTK UZINDUZI WA MFUMO WA UKUSANYAJI KODI KIELEKTRONIKI (e-RCS) JUNI 1, 2017

CENTRE FOR FOREIGN RELATIONS DAR ES SALAAM: Admissions Announcement-2017-18 Academic Year

Viewing all 109588 articles
Browse latest View live




Latest Images