Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

BUNGE LAPITISHA BAJETI YA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO SHILINGI TRILIONI 11.752

$
0
0
 Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.  Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) ndani ya Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, baada ya wabunge kupitisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
 Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akimpongeza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.  Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ndani ya Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, baada ya Wabunge kupitisha Bajeti ya Wizara hiyo ya jumla ya shilingi trilioni 11.752 kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
 Gavana wa Benki Kuu (BOT), Prof. Beno Ndullu (kushoto), akimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), baada ya Bunge kupitisha makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo ya shilingi trilioni 11.752 kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 Mjini Dodoma
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akipeana mkono na Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Bw. Mohamed Mtonga, nje ya ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma baada ya Bunge kupitisha bajeti ya Wizara hiyo ya shilingi trilioni 11.752 kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoro) akimshukuru na kumpongeza Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kusimamia na kuhakikisha kuwa Bajeti ya Wizara hiyo inaandaliwa kwa viwango vya juu na hatimaye kupitishwa na Bunge Mjini Dodoma ambapo Wizara hiyo imeidhinishiwa kukusanya nakutumia shilingi trilioni 11.752 kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.



Dkt. Yamungu Kayandabila na Dkt. Bernard Kibese wateuliwa kuwa Naibu magavana benki kuu ya Tanzania

BULEMBO AMALIZA ZIARA MKOA WA TABORA KWA ZIARA YA WILAYA YA KALIUA

$
0
0
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhajj Abdallah Bulembo akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Wilaya ya Kaliua, Mabalozi, watendaji wa CCM na wa Serikali, mwanzoni mwa ziara yake katika Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, leo.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Wilaya ya Kaliua, Mabalozi, watendaji wa CCM na wa Serikali wakiwa kwenye kikao hicho,

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhajj Abdallah Bulembo akihitimisha  mazungumzo yake  na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Wilaya ya Kaliua, Mabalozi, watendaji wa CCM na wa Serikali, mwanzoni mwa ziara yake katika Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, leo, Wilaya hiyo ya Kaliua ndiyo imehitimisha ziara yake katika mkoa wa Tabora. PICHA; BASHIR NKOROMO.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhajj Abdallah Bulembo akizungumza na Walimu wa Msingi Ushokora inayomilikiwa na Jumuia hiyo, mwanzoni mwa ziara yake katika Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, leo. Pamoja na mambo mengine, Bulembo alitaka kujua kwa nini walimu kwenye shule hiyo kongwe wanafanyia kazi yao chini ya miti kama alivyowakuta. Wapili kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyoAsher Msemwa na Kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo Abeid Busalama ambaye Bulembo alimpa jukumu la kufuatilia tatizo hilo la walimu kufanyika azi chini ya miti.

MBUGA ZA WANYAMA UNAZOWEZA KUTEMBELEA BURE WIKENDI HII

$
0
0
Na Jumia Travel Tanzania
Siku ya Jumatatu ya Juni 5 itakuwa ni maadhimisho ya ‘Siku ya Mazingira Duniani’ ambayo huadhimishwa na mataifa tofauti duniani ikiwa imebeba kauli mbiu ya ‘Kuwaunganisha Watu na Mazingira Asilia.’ 

Mapema wiki hii Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba  alitoa taarifa kwa umma kuwa kwa hapa nchini maadhimisho ya siku hiyo kitaifa yatafanyika kijijini Butiama mkoani Mara, mahali alipozaliwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl. Julius Nyerere, ikiwa ni kuenzi jitihada zake za kulinda na kuhifadhi mazingira.

Katika kunogesha sherehe hizo Waziri huyo amesema kuwa serikali imetoa ofa kwa wananchi kutembelea hifadhi yoyote ya mbuga ya wanyama bila ya kiingilio chochote kwa siku tatu, kuanzia Ijumaa ya Juni 2 mpaka Jumapili ya Juni 4. Alisema kuwa lengo kubwa ni kuona uwepo wa wanyama na kujifunza kuwa mazingira yanahitaji kulindwa zaidi na zaidi.
Kauli hiyo ya Waziri imekuja siku chache baada ya kampuni inayojihusisha na masuala ya huduma za hoteli mtandaoni barani Afrika, Jumia Travel kuzindua kampeni ya ‘DemocratizeTravel’ inayolenga kuwakomboa waafrika na watanzania kiujumla katika kusafiri na kutalii vivutio mbalimbali nchini huku wao wakirahisisha huduma za malazi na hoteli.
Kusoma zaidi BOFYA HAPA

PROFESA MWANDOSYA AMLILIA NDESAMBURO

$
0
0

Mheshimiwa Freeman Mbowe(MB), 

Mwenyekiti wa Taifa, CHADEMA: 

NIMEPOKEA KWA MASIKITIKO NA HUZUNI KUBWA TAARIFA ZA KIFO CHA MZEE WETU MHESHIMIWA PHILEMON NDESAMBURO. 

NILIPATA BAHATI KUFANYA KAZI NA MZEE NDESAMBURO TUKIWA WABUNGE WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. BINAFSI NILIFAIDIKA SANA NA MAWAZO, HEKIMA, FIKRA, NA USHAURI WAKE KATIKA MASUALA MBALI MBALI YA KIBUNGE NA KITAIFA BILA KUJALI KWAMBA TULIKUWA VYAMA TOFAUTI. 


PANDE ZOTE ZA BUNGE ZILIMTAMBUA NA KUMHESHIMU KWA UTULIVU WAKE NA HEKIMA KUBWA KATIKA KUWASILISHA HOJA ZAKE. KWA SABABU HIZO HAKIKA AMESAIDIA KATIKA KUJENGA NA KUIMARISHA DEMOKRASIA NCHINI. 

TAFADHALI TUFIKISHIE SALAAM ZANGU NA FAMILIA YANGU KWA FAMILIA YA MZEE NDESAMBURO NA WANA CHADEMA KWA KUMPOTEZA MUASISI NA MHIMILI WA CHAMA. 


KWA MWENYEZI MUNGU TULITOKA NA HAKIKA SOTE TUTARUDI KWAKE. 
MWENYEZI MUNGU AIREHEMU ROHO YA MAREHEMU NDESAMBURO. 
AMEN.

MARK MWANDOSYA

Milioni 20 za Biko zatua kwa Huruma Mkongwa wa Arusha

$
0
0
DROO ya kwanza ya Sh Milioni 20 na ya kumi kufanywa na waendeshaji wa bahati Nasibu ya Biko hatimae imepata mwenyewe baada ya kutangazwa mshindi wake ambaye ni Huruma Mkongwa wa jijini Arusha, akiibuka kidedea katika droo iliyochezeshwa jana, jijini Dar es Salaam.

Droo hiyo ni ongezeko la Sh Milioni 10 ambapo hapo awali droo zote zilikuwa zikihusisha kiasi hicho cha pesa kabla ya kuongezwa katika droo ya Jumatano ambapo waliongeza Milioni 10 nyingine hivyo kufikia Sh Milioni 20 na hivyo kutua kwa Mkongwa.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati wa kuchezesha droo hiyo, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema Jumatano ya Sh Milioni 20 imekuwa tamu baada ya fedha hizo za zawadi ya juu kabisa kutoka kwenda kwa Mkongwa ambapo anakuwa mshindi wa kwanza kuzoa kiasi hicho cha pesa kutoka kwenye bahati nasibu yao inayotikisa nchini.

Alisema ni imani yao ni kwamba kutoka kwa fedha hizo kutazidi kuibua fursa sahihi kwa washindi wao katika kuhakikisha wanatumia vema fedha hizo ili wanufaike kiuchumi kwa kutumia rasilimali fedha wanazopata kutoka Biko.

“Jumatano ya leo imekuwa Jumatamu kwa mshindi wetu Huruma Mkongwa wa Arusha kupata mkwanja kutoka kwetu, huku Biko tukiwa na lengo kubwa la kukuza uchumi wa wananchi wote hususan wale wanaoamua kutuunga mkono kwa kucheza Biko mara nyingi zaidi kwa kufanya miamala kwenye simu zao za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo watakapoingia kwenye lipa bili au lipa kwa Mpesa wataweka namba ya kampuni ambayo ni 505050 na ile ya kumbukumbu 2456.


Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akisalimiana na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Bakari Maggid kabla ya kuanza kuchezesha droo ya 10 ya Jumatano ya Sh Milioni 20 ambapo mkazi mwingine wa Arusha, Huruma Mkongwa aliibuka kidedea.
Balozi wa Biko Kajala Masanja akimtangaza mshindi wa Sh Milioni 20 Huruma Mkongwa kutoka mkoani Arusha baada ya kumaliza kuchezeshwa droo hiyo ya 10 ya Biko. Kushoto ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Bakari Maggid.

ESRF yatoa Mafunzo ya Uandaaji Mipango Mkakati kwa Watumishi wa Serikali za Mikoa na Wilaya

$
0
0
Tafadhali pokea CODES hapa chini Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imetoa mafunzo kwa watumishi wa Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Maofisa Mipango wa Halmashauri za Wilaya wa Mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu kuhusu uandaaji wa mipango mikakati ambayo itatumika katika halmashauri za mikoa hiyo. 

Akizungumza kwenye uzinduzi wa mafunzo hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa, John Mongela alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa watumishi hao kwani yatawasaidia kupata mbinu mpya ambazo watazitumia wakati wa kutengeneza mipango mikakati katika maeneo yao. 

Alisema kwa dhamana waliyonayo watumishi hao ni vyema kutumia mafunzo hayo ya siku mbili vizuri ili baada ya mafunzo waweze kupata njia mbadala katika uandaaji wa mipango mikakati ambayo itasaidia kuleta maendeleo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa, John Mongela akisoma hotuba ya ufunguzi wa mafunzo kwa watumishi wa Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Maofisa Mipango wa Halmashauri za Wilaya wa Mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu kuhusu uandaaji wa mipango mikakati 

“Hampo hapa kwa ajali, mpo kwasababu dhamana zenu ni kubwa, kwa kupitia mafunzo haya mtapata nyezo za kupangia mikakati ya kweli na mimi nataraji mtatoka hapa vizuri, haya ni mafunzo muhimu sana, “Tusiishie kwenye mikakati, tatizo ni jinsi gani ya kuanzisha miradi, tumekuwa na mawazo mengi sana lakini tuna changamoto ya kuyaweka kwenye miradi, tutoke kwenye kuwa na mawazo na sasa tuanze kuyafanyia kazi,” alisema Mongela. 

Pia Mongela aliwashukuru ESRF kwa kuandaa mafunzo hayo na kuwataka washiriki kufanya kazi kwa ushirikiano na ESRF kwani tayari wameonyesha nia ya kushirikiana nao ili kuhakikisha mipango ambayo wanaipanga inafanyiwa kazi. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwenye mafunzo kwa watumishi wa Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Maofisa Mipango wa Halmashauri za Wilaya wa Mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu kuhusu uandaaji wa mipango mikakati. 

“Tuone jinsi gani tunatumia fursa hii vizuri, tunatakiwa tukitoka hapa tukatekeleze mipango hii na ESRF wapo tayari kushikana mikono na sisi hadi waoane mafanikio na mimi niwahakikishie sisi tupo tayari … nategemea mambo makubwa baada ya kuanzisha ushirikiano huu,” alisema Mheshimiwa Mongela. 

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida alisema kwa kipindi kirefu wamekuwa mstali wa mbele kusukuma mbele Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa kufanya shughuli mbalimbali ambazo zinakuwa muhimu kwa maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla. “Kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, wa nje na ndani ya nchi, ESRF imekuwa ikisimamia na kuhimiza ufikiwaji wa malengo hayo sio tu katika ngazi ya Taifa bali pia katika ngazi ya wilaya na hata Kata,” alisema Dk. Kida Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa, John Mongela (katikati) akizindua mwongozo wa kuandaa mipango mkakati ya wilaya. 

Dk. Kida aliendelea kusema kuwa mafunzo hayo kutakuwa na mada zinazoelezea maelezo ya Jumla kuhusu mpango mkakati, upangaji wa bajeti, ufuatiliaji na namna ya kutoa taarifa, mikakati ya maendeleo ya kitaifa na kimataifa SDGs, FYDP II, Africa Agenda 2063, Vision 2025, mchakato wa kuandaa mpango mkakati na ufuatiliaji, upimaji, na utoaji wa taarifa (reporting, monitoring and evaluation) Aidha ESRF imezindua mwongozo wa kuandaa mipango mkakati ya wilaya, mwongozo ambao umetokana na andiko kubwa lililoandaliwa na serikali siku za nyuma kuhusu uandaaji wa mipango mkakati ya muda wa kati pamoja na bajeti (Government’s Medium Term Strategic Planning and Budgeting Manual). 

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS JUNI MOSI,2017


BARAZA LA WAZEE JIJINI ARUSHA WAMUOMBA RAIS MAGUFULI AWAKUMBUKE WAZEE AMBAO HAWAJALIPWA STAHIKI ZAO ZA ILIYOKUWA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
Na.Vero Ignatus, Arusha.

 Baraza la Wazee Jijini Arusha wamemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwaangalia wazee ambao walikuwa  Jumuiya ya Afrika Mashariki awalipe  stahiki zao kwani wameifanyia nchi hii mambo mazuri bali manufaa wameyakosa baada ya kuvunjika Jumuiya hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari  kwa niaba ya wazee hao mwenyekiti wa Baraza hilo  Mathius Kichao amesema  kuwa hadi sasa kuna wazee ambao hawajalipwa stahiki zao jambo ambalo siyo zuri hata kidogo kwani wazee hao wananung'unika

  "Kuna muda wazee hawa waliandamana wakenda Dar es salaam ,wakalala barabarani,lakini viongozi wawakati ule hawakuona umuhimu kuwa kilio cha wazee ni hatari sana wakawafukuzwa,nitamke kuwa hadi sasa kuna wazee wa jumuiya ya Afrika Mashariki hawajalipwa chochote kile, niikumbushe Serikali wale wazee wanalaani ,naomba hii laana isitokee,Mhe,Magufuli awalipe stahiki zao kwani wameifanyia nchi hii vizuri zaidi  "alisema Mwenyekiti huyo

 Aidha wazee hao  katika jiji la Arusha wameiomba serikali ya awamu ya tano ipeleke  mswada wa wazee katika Bunge la Jamhuri ya Muungano  na upitishwe  ili  Wazee nchini Tanzania  waweze kunufaika na matunda ya nchi yao kwani  wao ni chombo cha harakati hivyo Taifa likiwasahau wazee hakuna maendeleo kwasababu  wazee  huwa  wanafahamu mambo mengi ya kihistotia ya Nchi pamoja na mila nzuri na desturi.

"Tunawaomba viongozi mbalimbali wa Taifa hili wanapotembelea mkoa wa Arusha watenge muda wao ili waweze kuonana na wazee tutawashauri kwa yale tunayoyafahamu kwaajili ya manufaa ya nchi yetu na watoto pamoja na wajukuu zetu.
Mwenyekiti wa Baraza la wazee mkoa wa Arusha Mathius Kichao aliyeshika karatasi mkononi,akiwa anazungumza na waandishi wa habari hivi katibuni Jijini hapo.Picha na Vero Ignatus Blog.
Katibu wa wazee wa Baraza la wazee Jijini Arusha Kassim Seremuka  akizungumza jinsi ambavyo wazee hao wamenifaika na vitambulisho vya bima ya afya .Picha na Vero Ignatus Blog.
Baadhi ya viongozi na wajumbe wa Baraza la wazee katika mkoa wa Arusha wakiwa katika picha ya pamoja .Picha na Vero Ignatus Blog.
Katibu wa Baraza la wazee Kassim Seremuka Jiji la Arusha akionyesha Kadi ya matibabu wanazotumia wazee wakienda kutibi wa Hospitalini.


TAARIFA KUHUSU UJIO WA RAIS WA SPECIAL OLYMPICS KANDA YA AFRIKA

Application for Ordinary Diploma Admissions for the Year 2017-2018

Vijana waungana kuendeleza elimu ya afya ya uzazi baina yao

$
0
0
Jumla ya taasisi kumi za vijana zimeungana ili kuzidisha nguvu ya kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana wenzao nchini Tanzania na zaidi ikilenga matumizi ya mpango wa uzazi. Vijana hao wamejizatiti kuhahakisha kuwa kuna uwekezaji wa kutosha kwenye elimu juu ya uzazi wa mpango na pia vijana kuhusisha kwenye maamuzi yanayohusu vijana na afya ya uzazi.

Taasisi hizo zimetiliana saini makubaliano na kuwa taasisi moja ikayoitwa Tanzania Adolescent and Youth Reproductive Health (TAYAHR) jana jijini Dar es Salaam ambapo taasisi hiyo itajikita zaidi kwenye kutoa elimu, kuhusisha vijana na kuhakikisha huduma inafika kwenye maeneo sahihi kwa muda sahihi.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutia saini makubaliano hayo, Mwenyekiti wa TAYAHR William Otuck alisema Tanzania ina changamoto kuona ya kwamba asilimia 27 ya vijana wenye miaka 15-19 wana mtoto au ni wajawazito huku utumiaji wa uzazi wa mpango na hasa vidonge vya uzazi kati yao ikiwa ni chini sana – yaani asilimia 13 peke yake huku pia wakiwa hawana elimu yeyote kuhusu afya ya uzazi na hivyo kukosa uamuzi sahihi kwenye masuala ya kujamiiana.

‘Robo ya wasichana wenye umri kati ya 15 na 19 Tanzania wana watoto au ni wajawazito na hali ni mbaya kwenye mkoa wa Katavi yenye asilimia 45 na Tabora asilimia 42 kwa wasichana wenye umri huo. Hii inamaanisha kuna idadi kubwa ya wasichana ambao wanakatisha masomo na kuingia kwenye hali ya kuwa mzazi wangali wana umri mdogo na hii kwa kiasi kikubwa uchangia kuongeza hali ya umasiki kwenye jamii’, alisema Otuck huku akiongeza kuwa idadi kubwa ya wasichana wadogo wakipata mimba pia kunachangia kuongezeka vifo vitokanavyo na uzazi.

Akizungumzia kuhusu elimu na hali ya kupata mimba za utotoni, Otuck alisema tafiti zinaonyesha kuwa ni asilimia 10 wa wasichana ambao wana elimu mpaka ya sekondari ambao hupata mimba wakiwa na umri mdogo kulinganisha na wale wana elimu ya msingi ambao ni asilimia 34 na wale ambao hawana elimu kabisa ni asilimia 52.

Taasisi hiyo chini ya uongozi wa vijana pia imelenga kuhamasisha wenye kutoa maamuzi (policy makers) kuwekeza kwenye kupanua wingo la matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango ili kufikia walengwa ambao bado hawajafikia, ambapo kwa sasa inaonyesha asilimia 23 ya wanawake vijana wanatamani kutumia uzazi wa mpango lakini bado huduma hiyo haiwajafikia na pia kuongeza matumizi ya uzazi wa mpango kwa vijana angalau kufikia asilimia 80 ifikapo 2010 na pia kuendeleza elimu ya afya ya uzazi kwa vijana.

Taasisi hizi kabla ya kufikia makubaliano yao zilianza mazungumzo mwezi Oktoba na Novemba mwaka jana chini ya FP2020 Secretariat, mradi wa Advance Family Planning (AFP) Tanzania pamoja na taasisi ya Torchlight Collectives. TAYAHR inaundwa na taasisi za Hope Centre for Children, Girls and Women in Tanzania, YAM-UMATI, AfriYAN, TYVA, SAYI, Restless Development, Zanzibar Youth Forum (ZAFAYCO), IYAFP/Young and Alive Initiative (YAAI), SHDEPHA+ na YUNA.

UPDATES; MSIBA WA MBUNGE MSTAAFU WA JIMBO LA MOSHI MJINI PHILEMONI NDESAMBURO.

$
0
0
Baadhi ya Waombolezaji wakiwemo Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wakia nyumbani kwa Mzee Ndesamburo. 
 Nyumbani kwa Marehemu Mzee Philemoni Ndesamburo aliyefariki dunia jana katika Hosptali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi. 
 Baadhi ya waombolezaji wakiwemo ndugu wakijiandaa kwenda kutizama mwili wa Mzee Ndesamburo katika HospItali ya Rufaa ya KCMC.
Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini ,Godbless Lema pamoja na mkewe Neema Lema wakiwasili nyumbani kwa marehemu Mzee Ndesamburo.
Mbunge wa jimbo la Arusha mjini ,Godbless Lema akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Rombo ,Joseph Selasini mara baada ya kukutana nyumbani kwa marehemu Mzee Ndesamburo . 

SHUWASA YAKUTANA NA WADAU WA MAJI KUJADILI MKATABA WA HUDUMA KWA WATEJA

$
0
0
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA) imekutana na wadau wa huduma ya maji kujadili rasmu ya Mkataba wa Huduma Kwa Wateja ambapo mkataba utakaopitishwa na wadau utaanza kutumika kuanzia Julai Mosi ,2017.

Warsha ya kujadili mkataba wa huduma kwa wateja imefanyika leo Jumatani June 1,2017 katika ukumbi wa Vijana Center Mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro.

Akizungumza katika warsha hiyo,Matiro aliwataka wadau wa maji kujadili rasmu hiyo kwa umakini zaidi ili kuweka mambo ya msingi ambayo yatapunguza malalamiko kutoka wateja ikiwemo ongezeko la bei ya maji kwa watumiaji wa majumbani.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Reuben Mwandumbya alisema kutokana mamlaka hiyo kuwajali wateja wake imeona ni vyema kukutana na wadau ili kujadili mkataba mpya wa huduma kwa wateja.
 

“Mkataba uliokuwepo umemaliza muda wake hivyo tumeleta kwenu rasmu ya mkataba ili tujadili kwa pamoja tuweze kuboresha zaidi huduma ya maji kwa wateja wetu”,alieleza Marco

Miongoni mwa wadau walioshiriki katika warsha hiyo ni meya wa manispaa ya Shinyanga,madiwani,viongozi wa dini,viongozi wa taasisi mbalimbali,watendaji wa kata,wenyeviti wa serikali za mitaa,waandishi wa habari na wadau mbalimbali.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro akizungumza katika warsha hiyo.Kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya SHUWASA,Deogratius Sulla,kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Reuben Mwandumbya .

Wajumbe wakiwa ukumbini

Wadau wakiwa ukumbini .Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog .

BENKI YA KCB TANZANIA INAFANYA ZIARA KATIKA MIJI MIKUU NCHINI MAREKANI

$
0
0

 Benki ya KCB Tanzania kupitia dawati lake la Diaspora Banking inafanya ziara katika miji waishio watanzania nchini Marekani. Ziara hii imeanza tarehe 26 Mei na kutegemewa kumalizika tarehe 7 Juni. Miji inayotembelewa ni Washington Dc, Houston, Tx, Dallas, Durham Raleigh, Nc Boston, Ohio, Minnesota Na Chicago. 

Meneja Mahusiano wa huduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya Nchi, Bi. Shose Kombe akizungumza kuhusiana na ziara hii, alisema “Kuna watanzania wengi wanaoishi nje ya nchi na wanahitaji kuwekeza na kupata huduma za kibenki nyumbani wakiwa mbali na Tanzania, hivyo Benki ya KCB inatembelea miji ya Marekani yenye watanzania wengi ili kuwapatia huduma bora kwa haraka, usalama na bila usumbufu”. 

Huduma za kibenki wanazopatiwa watanzania wanaoishi nje ya nchi ni; akaunti za akiba (savings), akaunti za uwekezaji (Investment), akaunti za wanafunzi, akaunti za watoto na fursa ya kununua nyumba (Mortgage) kwa lengo la kuwawezesha watanzania hao kuendesha shughuli zao za kibenki Tanzania huku wakiwa nje ya nchi na kupata akiba zao pindi watakapo rudi nchini Tanzania. 

“Huduma hizi za kibenki kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi ni za papo kwa hapo (real time transactions), hivyo kuwawezesha wateja wake kufanya mambo kwa wakati na bila kadhia popote pale walipo duniani” alisema Bi. Kombe. 

Akizungumza na Meneja Mahusiano wa huduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya Nchi, Bi. Kombe na watanzania wanaofanya kazi ubalozini, Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Balozi Dismas Assenga alifuraia ujio wa benki ya KCB nchini Marekani. 

“Watanzania wanaoishi Marekani wanahitaji sana kuwekeza nyumbani hivyo tutafurahi mkifikia watanzania wote kutoka miji tofauti ya Marekani” alisema Kaimu Balozi. Bi. Kombe alimaliza kwa kuwataka watanzania wanaoishi nje ya nchi na bado hawajajiunga na benki ya KCB kujiunga leo, mteja anahitaji kua na nakala ya Pasi ya kusafiria, Leseni ya udereva au risiti ya huduma za umeme au maji (utility bills). 

Meneja Mahusiano wa huduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi Bi Shose Kombe kwenye picha ya pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani Balozi, Dismas Assenga. 
Meneja Mahusiano wa huduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi Bi Shose Kombe (aliyesimama, wapilikushoto) akitoa maelekezo ya jinsi ya kujaza fomu za kujiunga na benki ya KCB kwa baadhi ya watanzania (pichani) wanaoishi katika mji wa Houston. 
Meneja Mahusiano wa huduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi Bi. Shose Kombe kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watanzania wanaoishi katika mji wa Dallas. 


Kesi ya meno ya Tembo ya Milioni 13 dhidi ya Raia wa China na Watanzania sasa kusikilizwa kwa usiri

$
0
0
Na Karama Kinyuko

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeridhia ombi la upande wa mashtaka la kutaka ushahidi utakaotolewa na askari polisi kutoka Makao Makuu ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kitengo cha kupambana na Ujangili,D 7847 Sajenti Beatus usikilizwe kwa usiri.

Ushahidi huo ni katika kesi ya  uhujumu uchumi kwa kujihusisha na Meno ya Tembo ya bilioni 13 inayomkabili  raia wa China anayedaiwa kuwa Malkia wa Pembe za Ndovu, Yang Feng Glan (66)na watanzania wawili.

Mapema wakili wa Serikali Paul Kadushi, aliiomba Mahakama hiyo  ushahidi wa askari huyo ambaye awali alikwishaanza kutoa ushahidi wake kwa uwazi, usikilizwe kwa usiri kwa sababu unahusisha masuala ya amani ndani ya nchi.

Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi alikubaliana na ombi hilo la upande wa mashtaka kusikilizwa kwa usiri.

Hata hivyo, mmoja wa mawakili wa utetezi, wa Masumbuko Lamwai alilipinga hilo na kudai kuwa hakuna mahusiano juu ya Pembe za Ndovu na amani ya nchi.

Alidai kuwa, upande wa mashtaka hawakueleza ni kwa namna gani ushahidi wa Pembe za Ndovu utaingiliana na amani na utulivu katika nchi hii.

Aliongeza kuwa, mtu yoyote anayetuhumiwa kutenda kosa ni haki yake kikatiba,kesi isikilizwe hadharani ili kuhakikisha Haki ionekane imetendeka na umma ujue.

 Aliongeza kuwa kufanya hivyo kunaleta uwezekano wa mtu kuleta ushahidi wa kubambika.

Alibainisha kuwa upande wa mashtaka haujaweza kutoa sababu kwa nini ushahidi wa shahidi huyo uendelee kusikilizwa kwa usiri wakati ndugu wana Haki ya kujua hii kesi inaendeleaje.

" Kesi imekuwa kijamii mno, halafu isikilizwe kwa usiri kama mahakama ya kijeshi siyo Haki, mteja wangu amepewa Umalkia wa Pembe za Ndovu huo umalkia uthibitishwe hadharani siyo kisiri siri tunaomba hilo ombi likataliwe." Aliomba Lamwai.

WAZIRI MWAKYEMBE AFURAHISHWA NA UJIO WA TIMU YA LIGI KUU UINGEREZA EVERTON

$
0
0


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


KLABU ya Everton inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza itashuka dimbani Julai 13 kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya bingwa wa michuano mpya ya SportPesa Super Cup.

Everton ambayo ni mshirika mkubwa wa kampuni ya SportPesa itakuja chini ikiwa na kikosi kizima kinacho nolewa na kocha raia wa Uholanzi Ronald Koeman katika mchezo huo ambao pia wataumia kama maandalizi ya msimu mpya wa ligi.

Mkurugenzi Mtendaji wa klabu hiyo Robert Elston alisema mchezo huo utatumiwa na kocha wao kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi huku akijivunia kuwa timu ya kwanza inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza kucheza na timu kutoka Afrika Mashariki.

"Kocha Ronald Koeman na wachezaji wake watautumia mchezo huo kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi na pia wanategemea mchezo mzuri," alisema Elston.

Kwa upande wake Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Dk Harrison Mwakyembe alisema ujio wa klabu hiyo utakuwa msaada mkubwa kwa klabu za Tanzania kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwa Everon.

"Ujio wa Everton nchini utakuwa na faida kubwa kwa timu zetu hapa nchini kwakua zitajifunza moja kwa moja kuhusu masuala mbalimbali ya kiutawala na kiufundi," alisema Dk Mwakyembe.

Michuano ya SportPesa Super Cup itaanza Juni 5 katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam ikishirikisha timu nane kutoka Tanzania na Kenya ambazo ni Simba, Yanga, Singida United, Jang'ombe Boys, Nakuru All Stars, Tusker, Gor Mahia na AFC Leopards.

Waziei wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harisson Mwakeyembe akizungumza na waandishi wa habati wakati wa utambulisho wa Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu ya Everton Robert Eliston (Kulia) pia pamoja na mchezo wa kirafiki dhidi ya bingwa wa michuano mpya ya SportPesa Super Cup utakaofanyika Julai 13 mwaka huu
Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu ya Everton Robert Eliston akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ujio wao wa nchini Tanzania pamoja na  mchezo wa kirafiki dhidi ya bingwa wa michuano mpya ya SportPesa Super Cup utakaofanyika Julai 13 mwaka huu.

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YAWAPIGA MSASA MAAFISA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI KUHUSU SHERIA YA TAKWIMU YA MWAKA 2015

$
0
0
Na: Emmanuel Ghula.

OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imetoa mafunzo kwa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini leo mkoani Morogoro kuhusu Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 ili kuwajengea uwezo wa kufahamu namna sheria hiyo inavyofanya kazi.

Akifafanua sheria hiyo, Mwanasheria wa NBS, Oscar Mangula amesema sheria ya Takwimu No. 9 ya mwaka 2015 imeipa Ofisi ya Taifa ya Takwimu jukumu la kuratibu na kusimamia ukusanyaji wa takwimu rasmi nchini.

“Sheria ya Takwimu No. 9 ya mwaka 2015 ni sheria inayoipa NBS jukumu la kuratibu na kusimamia shughuli zote za upatikanaji wa takwimu rasmi nchini. Hivyo, kama taasisi yoyote inataka kufanya utafiti kwa minajili ya kutoa takwimu rasmi ni lazima iwasiliane na NBS ili kupata miongozo ya ukusanyaji wa takwimu rasmi,” amesema Mangula.

Mangula amesema kuwa, ni kosa kisheria kwa mtu yeyote ama taasisi kuendesha utafiti na kuchapisha au kutoa takwimu rasmi bila kuwasiliana na NBS kwani inaweza kukusanya takwimu ambazo hazina ubora na zinazoweza kupotosha umma.

Aidha, Meneja wa Takwimu za Kodi kutoka NBS Fred Matola amesema NBS hutoa takwimu rasmi kwa kuzingatia miongozo ya kitaifa na kimataifa inayotolewa na Umoja wa Mataifa ili kukidhi mahitaji ya nchi pamoja na kutumika kimataifa.

“Takwimu rasmi zinakusanywa kwa kuzingatia miongozo inayotolewa na umoja wa kimataifa ili kukidhi mahitaji ya nchi, hivyo NBS ina wajibu kisheria kusimamia upatikanaji wa takwimu rasmi nchini”, amesisitiza Matola.  

Ofisi ya Taifa ya Takwimu ina jukumu la kuratibu na kusimamia ukusanyaji, uchambuzi na upatikanaji wa takwimu rasmi nchini.
 Mwanasheria wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Oscar Mangula akiwasilisha mada inayohusu Sheria mpya ya Takwimu ya mwaka 2015 wakati wa mafunzo kwa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini yaliyofanyika leo mkoani Morogoro kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kuifahamu Sheria mpya ya Takwimu ya mwaka 2015.
 Meneja wa Idara ya Mbinu za kitakwimu, Viwango na Uratibu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Emilian Karugendo akitoa ufafanuzi wa namna Ofisi ya Taifa ya Takwimu inavyokusanya takwimu rasmi nchini kwa kuzingatia kanuni za kitaifa na kimataifa wakati wa mafunzo kwa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini yaliyofanyika leo mkoani Morogoro kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kuifahamu Sheria mpya ya Takwimu ya mwaka 2015.
 Baadhi ya Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini wakifuatilia uwasilishwaji wa mada wakati wa mafunzo kwa Maafisa hao yaliyofanyika leo mkoani Morogoro kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kuifahamu Sheria mpya ya Takwimu ya mwaka 2015.

Baadhi ya Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini wakifuatilia uwasilishwaji wa mada wakati wa mafunzo kwa Maafisa hao yaliyofanyika leo mkoani Morogoro kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kuifahamu Sheria mpya ya Takwimu ya mwaka 2015.

Dkt. Kyaruzi aikabidhi majukumu Bodi mpya ya TGDC

$
0
0

Na Johary Kachwamba -TGDC.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO), Dkt. Alexander Kyaruzi amezindua rasmi Bodi mpya ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi nchini (TGDC) na kuipa vipaumbele vya utekelezaji wa majukumu. TGDC ni kampuni tanzu ya TANESCO

Uzinduzi wa Bodi hiyo ulifanyika jijini Dar es Salaam katika Makao Makuu ya Ofisi za TGDC na kuhudhuriwa na wajumbe wa menejimenti ya kampuni hiyo. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo Dkt. Kyaruzi alisema kulingana na majukumu ya TGDC waliona ni vyema wachague Wakurugenzi wenye taaluma tofauti ili kuisaidia kampuni katika nyanja mbalimbali.

“Tuliona kwa shughuli za uendelezaji geothermal basi tutafute mtaalam wa jioloiia, tukamteua Dkt. Mshiu, Uhandisi Dkt. Mwinuka na mtaalam wa mambo ya fedha Ndugu. Segeja” alisema Dkt. Kyaruzi.

Akizungumza Kaimu Meneja Mkuu wa TGDC, Mhandisi. Kato Kabaka alimshukuru Mwenyekiti na wajumbe wa Bodi ya TANESCO kwa uteuzi huo, na kuahidi kuipatia Bodi ushirikiano kwa kipindi chote cha utekelezaji wa majukumu.

Naye Mwenyekiti mteule wa Bodi ya TGDC, Ndugu. Beatus Segeja alieleza watashirikiana vyema kwa kutumia taaluma zao kutimiza majukumu waliyokabidhiwa ya kuisimamia TGDC.

Mwenyekiti huyo wa Bodi ya Wakurugenzi wa TGDC, Ndugu, Beatus Segeja anaongoza wajumbe wengine wawili ambao ni Dkt. Tito Mwinuka na Dkt. Elisante Mshiu.
Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco Dkt. Dkt. Alexander Kyaruzi akitoa maelekezo wakati wa kuikabidhi rasmi majukumu bodi mpya ya TGDC. 

NGULI WA EVERTON LEON OSMAN AZINDUA PROGRAMU YA SOKA LA VIJANA LEO JIJINI DAR.

$
0
0
Na Zainab Nyamka,Globu ya jamii.


Mchezaji wa Zamani wa timu ya Everton ya Nchini Uingereza Leon Osman azindua programu ya timu za vijana nchini itakayosimamiwa na timu hiyo uzinduzi uliofanyika leo Jijini Dar es salaam.

Osman aliyekuwa ameambatana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe walizindua programu hiyo kwa vijana wadogo ambapo itakuwa endelevu hapa nchini.

Akizungumza na watoto kutoka katika vituo mbalimbali vya kukuzia vipaji vya soka Osman amewataka kujituma zaidi ili waweze kufikia malengo yao.


Osman amewapatia zawadi ya mipira  vijana hao waliokuja na kuonyeshwa kufurahia namna wanavyojituma na kuonyesha vipaji vyao.

Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe akiwa ameongozana na mchezaji wa zaman wa Everton Leon Osman (wa pili kulia) sambamba na Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara Yusuph Singo (kulia) na Mkurugenzi wa Timu ya Everton Robert Elstone leo Jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe akiwa ameongozana na mchezaji wa zamani wa Everton Leon Osman (anayewasalimia vijana ) sambamba na Mkurugenzi wa Timu ya Everton Robert Elstone leo Jijini Dar es salaam.
Mchezaji wa zamani wa Everton Leon Osman akiwa uwanjani na baadhi ya vijana akiwapa maelekezo mbalimbali.
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live


Latest Images