Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109605 articles
Browse latest View live

WATATU WALIOSHITAKIWA KWA KESI YA MADAWA YA KULEVYA WAACHIWA HURU

0
0

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewafutia kesi washtakiwa watatu waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya milioni 25 na kuamuru wasikamatwe.

Amesema washtakiwa hao wasikamatwe na kushtakiwa kwa kufunguliwa shtaka linalofanana na hilo labda kwa maelekezo ya Mahakama Kuu.

Hatua hiyo ua kufuta kesi hiyo imekuja baada ya washtakiwa kuwa rumande kwa zaidi ya miaka mitatu bila ya upelelezi kukamilika na jalada ya polisi kutokuwepo mahakamani mara kadhaa. Washtakiwa walioachiwa huru ni, Salma Juma , Amos Sosoma na Rashid Mtitu.

Kesi hiyo iliyokuwa na namba 21 ya mwaka jana imefutwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage baada ya kukaa mahakamani hapo kwa miaka mine bila ya upelelezi kukamilika.

Amesema Machi 6, mwaka huu, mahakama iliamuru upande wa mashtaka ifikapo Machi 23, itoe taarifa juu ya hatua ya upelelezi lakini ilipofika siku hiyo upande wa mashtaka ulidai upelelezi bado haujakamilika na jalada la polisi halipo.


NEEC NA TSN WASAINI MAKUBALIANO UHAMASISHAJI WA WANANCHI JUU YA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI

0
0
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),Bi. Beng’I Issa kushoto na Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Magazeti ya TSN (Tanzania Standard Newspapers) Dk. Jim Yonazi kulia wakisaini makubaliano ya kufanya kazi pamoja ya uhamasishaji na uelimishaji wananchi juu ya uwezeshaji wananchi kiuchumi. Kazi hiyo itaanza na kongamano  la uwezeshaji wananchi linalotarajia kufanyika mjini Dodoma Juni 10, 2017 ambapo mgeni rasmi ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.(Picha na Mwanadishiwetu, Dar es Salaam).
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uuwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),Bi. Beng’I Issa kushoto na Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Magazeti ya TSN (Tanzania Standard News PaperS), Dk. Jim Yonazi kulia wakibadilishana nyaraka baada ya kusaini  makubaliano ya kufanya kazi pamoja ya uhamasishaji na uelimishaji wananchi  juu ya uwezeshaji wananchi kiuchumi. Kazi hiyo itaanza na kongamano  la uwezeshaji wananchi linalotarajia kufanyika mjini Dodoma Juni 10, 2017 ambapo mgeni rasmi ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),Bi. Beng’I Issa kushoto na Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Magazeti ya TSN (Tanzania Standard Newspapers), Dk. Jim Yonazi kulia (wote waliokaa) wakisaini makubaliano ya kufanya kazi pamoja ya uhamasishaji na uelimishaji wananchi juu ya uwezeshaji wananchi kiuchumi. Kazi hiyo itaanza na kongamano  la uwezeshaji wananchi linalotarajia kufanyika mjini Dodoma Juni 10, 2017 ambapo mgeni rasmi ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na waliosimama kulia ni Meneja Mauzo na Masoko, Bw. Januarius Maganga na k

wananchi wamekuwa na uelewa wa utekelezaji wa bajeti katika kipaumbele- Tacosode

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

BARAZA la Vyama vya Hiari na Maendeleo ya Jamii (Tacosode) limesema wananchi wamekuwa na uelewa kuhamasisha bajeti kuwa na kipaumbele kwa changamoto zinazowakabili.

Hayo ameyasema leo Meneja wa Miradi wa Tacosode, Koga Mihama wakati akizungumza waandishi wa habari juu wananchi kuwa na uelewa kuweka umuhimu bajeti katika halmashauri kutatua changamoto zinazowakabili.

Koga amesema kuwa uelewa huo umetokana na elimu waliopata katika mradi wa uhamasishaji wananchi kushiriki katika masuala ya afya katika kuangalia vipaumbele vya bajeti uliokuwa ukitekelezwa katika Mikoa ya Iringa pamoja na Dodoma.

Amesema kuwa wananchi mradi huo katika utekezwaji wake katika Halmashauri ya Iringa pamoja na Kongwa mkoani Dodoma wananchi wamekuwa na mwamko katika masuala ya afya ushiriki kwa kuchangia katika huduma za afya.

Koga amesema kuwa mradi huo ni wa miaka minne lakini umekuwa na matokeo katika wilaya ambazo umetekelezwa kwa wananchi kuwa na mwamko katika masuala ya huduma za afya kwa kuchangia hata nguvu zao pale panapobidi.

Aidha amesema kuwa mradi huo ukiisha wanaweza kufanya katika sekta zingine ili kuwa maendeleo ya katika masuala mbalimbali kutatuliwa.

Meneja wa Miradi wa Tacosode, Koga Mihama akizungumza na waandishi wa habari juu ya baraza hilo linavyofanya kazi katika mradi wa afya, leo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Afisa Habari,Said Juma na Kushoto ni Afisa mradi wa Tacosode, Nobelrich Ekonea

MAJALIWA ATEMBELEA MAONYESHO YA UJENZI WA NYUMBA

0
0
*Ataka VIGUTA iende kwenye halmashauri, ihamasishe watumishi
*Asema Watanzania wanataka nyumba bora, hawana muda wa kusimamia ujenzi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezitaka Halmashauri za wilaya nchini ziangalie uwezekano wa kuwapatia watumishi wake nyumba za bei nafuu kwa malipo kidogo kidogo.

Amesema Halmashauri za wilaya kupitia mapato ya ndani, japo si makubwa zinaweza kuandaa mazingira yatakayowawezesha watumishi wake kupata nyumba kupitia mpango wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu unaofanywa na Muungano wa Vikundi vya Vicoba Tanzania (VIGUTA). 

Ametoa wito huo leo (Jumatano, Mei 31, 2017) mara baada ya kutembelea maonyesho ya Mpango wa Ujenzi wa Nyumba za Waheshimiwa Wabunge (Low Cost Housing) yanayoendelea kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma. 

Waziri Mkuu aliwashauri viongozi wa VIGUTA wafanye mawasiliano na Halmashauri zote na akawataka watenge muda wa kuzitembelea Halmashauri hizo ili kuonyesha nia na uwezo wao wa kujenga nyumba za gharama nafuu ambazo malipo yake hulipwa kidogo kidogo kwa lengo la kuboresha maisha ya Watanzania.

“Watanzania wengi hivi sasa wanapendelea nyumba ndogo, nzuri na ambazo zimekamilika. “Wengi wao, na hasa wafanyakazi, siku hizi wana shughuli nyingi na hawana muda wa kujenga nyumba na kuzisimamia wenyewe kama zamani. Hivyo, wanahitaji makampuni yanayoweza kuwanjengea nyumba na wao wakalipa kidogo kidogo,” amesisitiza.

Aliwaaasa viongozi wa VIGUTA wahakikishe kuwa wanajenga nyumba zenye ubora unaokubalika ili waweze kuaminika hali ambayo itawawezesha kupata wateja wengi zaidi.

“Katika kipindi hiki ambacho Serikali inahamia Dodoma, Muungano wa Vikundi vya VICOBA au VIGUTA unayo nafasi kubwa ya kuwapatia watumishi wanaohamia nyumba za kuishi kupitia mpango wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu,” Waziri Mkuu alisema.

Alisema watumishi wengi wanaoingia gharama kubwa kwa kuishi katika nyumba za kupanga huku wakilipa kodi, sasa wamepata kimbilio kwani wanaweza kujengewa nyumba kwa muda mfupi na kwa bei nafuu na wakalipa kidogokidogo kwa kipindi cha hadi miaka 15.

Naye, Mwenyekiti wa VIGUTA Taifa, Dkt. Salmin Ibrahim Dauda alimweleza Waziri Mkuu kwamba wana uwezo wa kujenga nyumba kwa gharama ya shilingi milioni 12, milioni 15, milioni 25 na milioni 60 kutegemeana na ukubwa wa nyumba.

Alisema wameweka viwango tofauti ili kuwawezesha Watanzania wenye kipato cha chini kumiliki nyumba zao wenyewe.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

S. L. P. 980,

40480 - DODOMA. 
JUMATANO, MEI 31, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama picha za nyumba wakati alipotembelea Maonyesho ya Mpango wa ujenzi wa Nyumba za Gharama Nafuu kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 30, 2017. Maonyesho hayo yameandaliwa na Muungano wa Vikundi Vya Vicoba Tanzania (VIGUTA) .Kushoto ni Mwenyekiti wa Taifa wa VIGUTA, Dkt. Salmin Ibrahim Dauda.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kifo cha Philemon Ndesamburo

GAZETI LA TANZANIA DAIMA LATAKIWA KUOMBA RADHI

BALOZI SEIF ALI IDD AONGOZA MAZISHI YA MAMA MZAZI WA VUAI ALI VUAI.

0
0
NA IS-HAKA OMAR,  ZANZIBAR.

MAMIA ya Wananchi wameudhuria mazishi ya Mama mzazi wa Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM Zanzibar.Vuai Ali Vuai, Marehemu Bi.Mwanaisha Hassan Vuai huko Kijijini kwao Bwejuu, Mkoa wa Kusini Unguja.

Mazishi hayo yameongozwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, aliyeambatana na viongozi mbali mbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  pamoja na  jamhuri ya muungano Tanzania.

Bi. Mwanaisha amefariki jana wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Tasakhtaa  iliyopo  Vuga  Mjini  Zanzibar.

Akizungumza mara baada ya mazishi hayo, Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM Zanzibar, Nd. Vuai Ali Vuai alisema kifo cha Mama yake mzazi kimeacha pengo kubwa katika  familia hiyo  kwani marehemu huyo alikuwa akitegemewa na jamii kutokana na busara zake.

Aidha  Vuai amewashukru wananchi mbali mbali waliojitokeza kumuunga mkono katika mazishi hayo na kuwasihi waendelee kuwa na umoja wa kushirikiana katika mambo mbali mbali ya kijamii.

“  Mama yetu tulimpenda sana lakini ndio hivcyo amefariki sasa kilichobaki kwetu sisi tuliobaki ni kumuombea dua yeye pamoja na wazee wetu wengine waliofariki kabla yake.”, alisema  Naibu Katibu Mkuu huyo. 

Mbali na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Balozi Seif Ali Idd pia  Mazishi hayo yameudhuriwa na Viongozi  mbali mbali  wakiwemo Katibu Mkuu wa CCM   Abdulrahman Omar Kinana, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar   Dkt. Abdalla Juma Saadala “ Mabodi”,Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Tanzania Shaka Hamdu Shaka,  Mkuu wa Mkoa kusini Unguja    Dk.Idrissa  Muslim Hija, Katibu  wa Kamati Maalum  ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi Zanzibar, Waride Bakari  Jabu.

Viongozi wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja, Idrissa  Kitwana  Mustafa, Mnadhimu wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi  wa CCM, Ali Salum Haji pamoja na baadhi ya Mawaziri, Manaibu Mawaziri  na Makatibu wakuu wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 Bi.Mwanaisha Hassan Vuai amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 85 ameacha watoto tisa (9) pamoja na wajukuu kadhaa.

Mungu ailaze roho ya marehemu pahali pema peponi-Amin.
 Viongozi  mbali mbali wa Chama na serikali pamoja na wananchi wakiiombea Dua  Maiti ya Bi. Mwanaisha Hassan Vuai ambaye ni Mama mzazi wa Naibu Katibu Mkuu Msitaafu wa CCM Zanzibar  Vuai Ali Vuai katika msikiti wa kijiji cha Bwejuu.
 Viongozi  mbali mbali wa Chama na serikali pamoja na wananchi wakiiombea wakiwa msikitini kabla ya kuanza kuiswalia Maiti ya Bi. Mwanaisha Hassan.
 Baadhi ya Viongozi na wananchi kwa upande wa wanawake wakiomba dua katika mazishi ya Marehemu Bi. Mwanaisha Hassan Vuai ambaye ni Mama mzazi wa Naibu Katibu Mkuu Msitaafu wa CCM Zanzibar  Vuai Ali Vuai katika msikiti wa kijiji cha Bwejuu.
Viongozi mbali mbali wa Chama na serikali wakiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Nd. Abdulrahman Omar Kinana wakimfariji Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM  Zanzibar  katika mazishi ya Mama yake mzazi yaliyofanyika huko kijijini kwao Bwejuu, Mkoa wa Kusini Unguja.( PICHA NA AFISI KUU CCM ZANZIBAR).

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, PROF. JUMANNE MAGHEMBE AFANYA MAZUNGUMZO LEO NA BALOZI WA CHINA NCHINI, DKT. LU YOUGING, MJINI DODOMA

0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza na balozi wa China nchini, Dkt. LU Youqing ofisini kwake leo mjini Dodoma ambapo wamejadili na kukubaliana mambo mbali mbali ya kuimarisha uhusiano wa China na Tanzania katika sekta ya maliasili na utalii. Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na kuwakaribisha wawekezaji katika sekta ya viwanda vya uchakataji wa mazao ya misitu na ujenzi wa hoteli katika fukwe za Tanzania na Hifadhi za Taifa.
 Balozi wa China nchini, Dkt. LU Youqing akimueleza jambo Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe alipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma leo. Balozi huyo amekubali ombi la Waziri Maghembe kuwaleta wadau wa mashirika ya utalii kutoka nchini China kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii vya Tanzania na kuvitangaza nchi kwao.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akimfafanulia jambo balozi wa China nchini, Dkt. LU Youqing alipomtembelea ofisi kwake leo mjini Dodoma. Waziri Maghembe kupitia balozi huyo ameipongeza Serikali ya China na Wananchi wake kwa uamuzi wake wa hivi karibuni wa kufungia biashara haramu ya meno ya tembo nchini humo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akiagana na Balozi wa China nchini, Dkt. LU Youqing baada ya mazungumzo marefu ofisini kwake leo mjini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kulia), Balozi wa China nchini, Dkt. LU Youqing (kushoto), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili, Dkt. Aloyce Nzuki (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Justa Nyange wakijadili jambo muda mfupi baada ya mazungumzo hayo. (PICHA ZOTE NA HAMZA TEMBA - WMU)

VIONGOZI WA DINI WAMPONGEZA KAMANDA SIRRO KUWA IGP

0
0
Na Jonas Kamaleki- MAELEZO
Viongozi wa Dini hapa nchini wamempongeza Kamanda Saimon Sirro kwa kuteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP).Pongezi hizo zimetolewa leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa jamii ya dini zote, Askofu William Mwamalanga kwa niaba ya viongozi wa dini.
Katika mahojiano maalum, Kiongozi huyo wa dini amemuelezea IGP Sirro kuwa ni mchapakazi na mtu makini katika utendaji wake wa kazi.
“IGP Sirro ni mtulivu wa na ni mtu anayetafakari maamuzi yake kwa kutafakari bila kujali presha au maagizo ya kisiasa,” Askofu Mwamalanga alisema.
Alimuelezea IGP Sirro kuwa ni kiongozi ambaye anawashirikisha wafanyakazi wenzake na wananchi kwa ujumla ili kuleta amani kazi ambayo huifanya kwa weledi.
Ameongeza kuwa kiongozi huyo wa juu katika Jeshi la Polisi ni mtu mwenye kuthubutu hasa katika vita dhidi ya matumizi ya madawa ya kulevya na ujambazi.
“Nakumbuka Kamanda Sirro ni polisi wa kwanza kupata tuzo katika kufanikiwa kudhibiti majambazi,”alisema Askofu Mwamalanga.
Kiongozi huyo wa dini ametoa ushauri kwa IGP Mpya kushughulika maslahi ya askari, vitenda kazi katika jeshi la polisi na kurudisha uhusiano mwema kati ya Jeshi la Polisi na raia wema ambao amesema wanafikia takribani asilimia 99.
Aidha, Askofu Mwamalanga ameshauri kuwa IGP aelekeze zaidi nguvu katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani, Dar es Salaam, Morogoro, Tanga na Kagera. Ameitaja mikoa mingine kuwa ni Mwanza, Arusha, Kigoma, Dodoma, Pemba na Mara, mikoa ambayo ameitaja kuwa iko kwenye hatari ya vitendo vya uhalifu.
Kamanda Sirro ameapishwa Siku ya Jumatatu Ikulu jijini Dar es Salaam na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli. Baada ya kuapishwa, IGP Saimon Sirro alikula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma.
Kabla ya Uteuzi huo, Kamanda Sirro ambaye sasa in IGP akichukuwa nafasi aliyokuwa nayo Kamanda Ernest Mangu, alikuwa Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

IGP Simon Sirro.

DKT. NCHIMBI AAGIZA HALMASHAURI KUANZISHA BENKI ZA WANA MICHEZO NA KUTENGA VIWANJA VVYA MICHEZO MKOANI SINGIDA.

0
0
Halmashauri zote saba za Mkoa wa Singida zimeagizwa kutenga maeneo yenye hadhi ya kuwa viwanja vya michezo pamoja na kuhakikisha zinakuwa na benki ya wanamichezo katika halmashauri zao.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi ametoa maagizo hayo leo asubuhi kabla ya kuzindua mashindano ya michezo kwa shule za Sekondari (UMISSETA) kwa ngazi ya mkoa ambapo wanamichezo hao wataunda timu za Mkoa kwa ajili ya mashindano ya kitaifa yatakayofanyika jijini Mwanza mwezi ujao.

Dkt. Nchimbi amesema halmashauri zimekuwa zikiwatelekeza wanamichezo mahiri hivyo wakianzisha benki ya wanamichezo kwa maana ya kuhifadhi kumbukumbu za wana michezo mahiri pamoja na kuwaendeleza hawatapata shida kipindi cha mashindano yoyote. 

Ameongeza kuwa halmashauri zimekuwa zikijisahau katika kuandaa maeneno ya michezo hadi inapofika kipindi cha UMISETA hali inayopelekea kukosekana kwa viwanja vya kufanyia mazoezi ili kuwa na timu bora.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akihutubia kabla ya kuzindua mashindano ya UMISSETA ngazi ya Mkoa wa Singida.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (aliyenyanua ubao) akipiga ubao wa kuashiria uzinduzi wa michezo ya UMISSETA mkoa wa Singida, mbele yake ni wanariadha wakianza mashindano.
 Wanamichezo kutoka Shule za Sekondari za Halmashauri ya wilaya ya Itigi wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza mashindano ya UMISSETA ngazi ya Mkoa.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

GAZETI LA TANZANIA DAIMA LAKIRI KUKOSA UMAKINI, LAOMBA RADHI

RAIS DKT. MAGUFULI AOMBOLEZA KIFO CHA MZEE NDESAMBURO, ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI

MAMA BISHANGA AMLILIA IVAN X HUSBAND WA ZARI

0
0
Nimesikitishwa sana na kifo cha Ivan, ni mapema sana kwa yeye kuondoka duniani kuacha watoto wadogo sana, wanahitaji sana uwepo wa baba na mama, lakini Mungu ni Mwema amependezwa nae kuwa karibu yake mbinguni.
Zari binti yetu pole sana kwa pigo hili kubwa lisilozibika kwa wepesi, Mungu akutie nguvu. Wewe ni mmoja kati ya mabinti wachache walio na msimamo imara kimaisha, wasioyumba, wanaojitegemea zaidi kimaisha kwa kufanya biashara na shughuli mbalimbali kujipatia kipato, usieyumbishwa na mapito ya maisha ya dunia kirahisi. 
Naweza kusema nimekufahamu baada ya kuwa na mpenzi wako Diamond, umeonyesha msimamo na uimara wako ambao ni ushahidi mzuri kuwa utawatunza wanao watatu ambao sasa wako mikononi mwako forever. Usikate tamaa wengi tumepitia uliyopitia, kuvunjika kwa ndoa na kufiwa na wenzetu na kubakia na watoto, yalinikuta mimi binafsi hayo sikujua ada, nauli, kusomesha watoto  hadi mwenzangu alipofariki mwaka 1994 nikiwa Idara ya elimu ya juu na mshahara wa ualimu, na watoto kurudi kwangu, hapo ndio niliona jinsi Mungu huongeza baraka zake, na jinsi ukoo wa Kamota ulivyosimama nami kulea watoto. 
Na wewe daima muweke Mungu mbele mambo yatakuwa mazuri, hasa ukizingatia ulishajiimarisha na baba watoto wako amewaacha vizuri. Mungu atakuongezea na kukutia furaha ya maisha ya familia yako, na bila kusahau kuwa Diamond yuko pemebeni yako, tabasamu lake linatosha kukuongezea amani na nguvu ya maisha na kilo za uzito wa mwili confidence! 
Diamond amelelewa vizuri sana na mama yake na yuko wazi katika penzi lenu, sasa ni wakati wa kushikamana kikamilfu kupeana raha na amani na kuijenga familia yenu .
Kila la heri Zari, huenda tukaonana JHB maana sehemu ya maisha yangu ni JHB kwa mume wangu Orange Grove na Alexander township!
GOD BLESS YOU AND YOUR FAMILY ZARI
MAMA BISHANGA / MRS MAROLEN
CLEVELAND. OHIO

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

0
0

SIMU.TV: Tanzania leo imeungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha siku ya kutotumia Tumbaku  huku serikali ikijipanga kudhibiti matumizi ya Tumbaku; https://youtu.be/e3IN5M8LMZM

SIMU.TV: Wananchi wilayani Musoma wameilalamikia mamlaka ya maji safi wilayani humo kwa kushindwa kukamilisha miradi kadhaa ya maji; https://youtu.be/TKAQy537ZdI

SIMU.TV: Madiwani wanawake jijini Dar Es salaam wamelalamikia tabia ya kutengwa na kutoshirikishwa katika baadhi ya maamuzi kwa kile walichokiita mfumo dume; https://youtu.be/8M6RtCBejg0

SIMU.TV: Mkuu wa wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi Joseph Mkirikiti, ametembelea hospitali ya wilaya hiyo na kubaini mrundikano mkubwa wa wagonjwa; https://youtu.be/enEUEbeX6BA

SIMU.TV: Jumla ya shilingi Bilioni 4.4 zimetengwa kwa ajili ya kuwajengea uwezo wananchi wa mikoa ya Iringa na Dodoma katika sekta ya afya; https://youtu.be/Ag7abnMjfVk  

SIMU.TV: Waigizaji wa filamu kutoka nchini China wamesema kuwa watatangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini Tanzania kwa kutumia filamu zao; https://youtu.be/nivQ1hi7b4A

SIMU.TV: Droo ya kwanza ya shilingi milioni 20 imepata mshindi baada ya Huruma Mkongwa kutoka Arusha kuibuka mshindi kwa kujinyakulia shilingi milioni 20; https://youtu.be/VWNnPweNayQ 

SIMU.TV: Kampuni ya simu ya Vodacom imezindua huduma mpya inayojulikana kama Ukarimu wa Vodacom katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani; https://youtu.be/0cc_7l2mEmM  

SIMU.TV: Mtendaji mkuu wa klabu ya soka ya Azam Fc Saad Kawemba amekanusha taarifa zinazogaa kwenye mitandao kuwa amefukuzwa kazi katika timu hiyo; https://youtu.be/3fbY4GyGBxw

SIMU.TV: Klabu ya soka ya Azam imesema kuwa wachezaji wake wanatarajia kurejea kambini hivi karibuni kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao; https://youtu.be/heIXhC70e6U

SIMU.TV: Mkoa wa Mtwara umeanza maandalizi ya kusaka wachezaji bora ambao watakwenda kuuwakilisha mkoa kwenye mashindano ya Umiseta; https://youtu.be/cY5iruvbH20

SIMU.TV: Mashindano ya Umiseta kwa mkoa wa Dar Es salaam yameendelea hii leo kwa kuzikutanisha shule za wilaya ya Ubungo na Ilala katika dimba la Uhuru; https://youtu.be/vxuhYnQnDhU

H.E. Ambassador Wilson M. Masilingi attends Global Platform for Disaster Risk Reduction, Cancun, Mexico.

0
0
H.E. Wilson M. Masilingi, Ambassador of the United Republic of Tanzania to the United States and Mexico participated in the Global Platform for Disaster Risk Reduction, held in Cancun, Mexico from May 22 - 26, 2017. With him was a delegation from Tanzania led by Brig. General Mbazi Msuya, the Director of Disaster Management Department, Prime Minister’s Office, Hon. Hamza Hazzan Juma, Member of Parliament, House Representative, Zanzibar and other officials.

H.E. Wilson M. Masilingi, Ambassador of the United Republic of Tanzania to the United States and Mexico reads Tanzania’s Official Statement to the Global Platform for Disaster Risk Reduction, 2017
H.E. Wilson M. Masilingi, Ambassador of the United Republic of Tanzania to the United States and Mexico (centre) Brig. General Mbazi Msuya, the Director of Disaster Management Department, Prime Minister’s Office and (left) and Hon. Hamza Hazzan Juma, Member of Parliament, House Representative, Zanzibar at the Global Platform for Disaster Risk Reduction, Cancun, Mexico.
Delegation of the United Republic of Tanzania to the Global Platform for Disaster Risk Reduction, 2017

Castle Lite Unlocks Navy Kenzo crew kuwa ni kundi la wasanii ndani ambao watapanda jukwaa moja na Cassper Nyovest, Diamond na Future Julai 22, 2017

0
0
Meneja Masoko wa Bia laini Afrika Mashariki, Amou Majok (wa pili kushoto) akiwa pamoja na wasanii wa kundi la Navy Kenzo juzi jijini Dar, wakati Meneja huyo akitangaza kuhusu wasanii wa kundi hilo kushiriki katika tamasha la Castle Lite Unlocks litakalofanyika mwezi Julai. Wa kwanza kulia ni Meneja Msaidizi wa Chapa ya Bia laini, Isaria Kilewo.
Wadau mbalimbali waliojitokeza wakiwa katika picha ya pamoja 


HIFADHI YA TAIFA MIKUMI MKOANI MOROGORO YAJIVUNIA IDADI KUBWA YA WAGENI

0
0
ikumi mkoani Morogoro ni moja ya mbuga za wanyama ambazo kwa sasa hujivunia idadi kubwa ya wageni na wanyama makundi tofauti wakiwemo simba pia ni hifadhi ambayo hufikika kwa urahisi na kuwafanya wageni kuona wanyama kwa haraka. 
Hifadhi imeshirikiana na vijiji katika kuunda ujirani mwema kupitia miradi mbalimbali ambayo imekuwa ikiibuliwa na wananchi ili kuhakikisha maafisa wa wanyamapori wanashirikiana na wanavijiji kulinda mipaka ya hifadhi ya taifa mikumi dhidi ya ujangili. 
Mbuga ya wanyama Mikumi hupokea wageni wa aina mabalimbali wakimiwemo wenyeji wakazi kwa vingilio tofauti ukilinganisha na watalii wandani ambapo vingilio vyao ni shilling 5700 kwa mtu mzima.
 Muongozaji wa hifadhi ya taifa milima ya Udzungwa mkoani Morogoro Yuston Bonike akimuonyesha muandishi wa habari wa gazeti la Nipashe Ashton Baraigwa mbegu ya mimea ambayo inaweza kuliwa na nyani kipindi cha ukosefu wa chakula na kumletea madhara na nyani huyo kugeuka kuwa kichaa.
Moja wa maporomoko ya maji kivutio ambacho kina patikana katika hifadhi ya taifa ya milima ya Udzungwa mkoani Morogoro ambacho hufikiwa kirahisi kwa njia ya miguu na hupatikana ndani ya msitu huo.
Tembo nao ni miongoni mwa wanyama wanaopatikana kwa wingi katika hifadhi ya taifa Mikumi mkoani Morogoro ambao mara nyigi hupenda kutembea kwa makundi wakati wa kujitafutia malisho.
Kikundi cha utunzaji wa mazingira kinachotokana na mradi wa utalii wa kitamaduni wakiwa wameshikilia vikapu ambavyo vimetengenezwa na mifuniko ya chupa za maji ambayo wamekuwa wakiyaokota. Wa pili kutoka kulia ni katibu wa kikundi hicho Bw. Christandus Mdoe. Picha zaidi BOFYA HAPA


UNICEF NA UNHCR WATOA ELIMU KUHUSU HAKI ZA WATOTO WAKIMBIZI MKOANI KIGOMA.

0
0
 Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto Duniani (UNICEF) Bibi. Stephenie Shanler akizungumza na washiriki wa mkutano maalum (hawapo pichani) wa  utoaji elimu juu ya Haki za watoto wakimbizi unaoendelea kwa siku mbili mkoani Kigoma.
 Washiriki kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ,Wizara ya Mamboya Ndani, Ofisi ya Waziri Mkuu, na Taasisi na Mashirika yanayotetea Haki za Watoto nchini wakifuatilia mkutano maalum wa utoaji elimu juu ya  Haki za watoto wakimbizi  unaofanyika  mkoani Kigoma.
 Washiriki kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ,Wizara ya Mamboya Ndani, Ofisi ya Waziri Mkuu, na Taasisi na Mashirika yanayotetea Haki za Watoto nchini wakifuatilia mkutano maalum wa utoaji elimu juu ya  Haki za watoto wakimbizi  unaofanyika  mkoani Kigoma.
 Washiriki kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ,Wizara ya Mamboya Ndani, Ofisi ya Waziri Mkuu, na Taasisi na Mashirika yanayotetea Haki za Watoto nchini wakifuatilia mkutano maalum wa utoaji elimu juu ya  Haki za watoto wakimbizi  unaofanyika  mkoani Kigoma.
Afisa Ustawi wa Jamii Mwandamizi kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bw.Darius Damas  akifafanua jambo kwa washiriki wa mkutano maalum(hawapo pichani)  wa utoaji elimu juu ya Haki za watoto wakimbizi unaoendelea kwa siku mbili mkoani Kigoma. Picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO Dodoma.

MAKALA YA SHERIA: UNAYO HAKI YA KUMUONA MTOTO HATA KAMA UMEACHANA NA MZAZI MWENZAKO.

0
0
Na  Bashir  Yakub

Wapo  wazazi  wanaowakatalia  wazazi  wenzao  kuwaona  watoto/mtoto   baada  ya  kuwa  wameachana.  Wengine  hawakuachana  bali  hawakuwahi  hata kuishi pamoja  isipokuwa  walizaa  tu  lakini  yule  mzazi  anayeishi  na  mtoto  anamzuia  mzazi  mwenzake  kumuona  mtoto  husika. Basi  makala  haya  yatatizama  jambo  hili  kwa  sura  ya  sheria  zetu.  Uhalali  wake  na  uharamu  wake, hatua  unazoweza  kuchukua  na  mtazamo  wa  jumla  ikiwa jambo  hili  ni  haki  kisheria  ama  laah.

Sheria  namba  21  ya  mwaka  2009  Sheria  ya  Mtoto  ndiyo  itakayotupatia  majibu  ya  suala  hili  kwa  ujumla  wake.


1.KUMUONA  MTOTO  HUMAANISHA  NINI.

Unapotizama  kwa ujumla  sheria  ya  mtoto  hasa  vile  vifungu  vinavyozungumzia   habari  ya  kumuona  mtoto   utaona   kuwa   vinazungumzia  kumuona  mtoto  kwa  maana  ya  hatua  ya  baba  mzazi,  mama  mzazi,  au  mlezi  mwenye   mamlaka  kutembelea  eneo  alilohifadhiwa  mtoto  kwa  ajili  ya  kuonana  na  mtoto  huyo.

Haijalishi  anaumwa  au  yu  mzima,  yuko  kituo  cha kulelea  watoto  au  nyumbani  kwa  mtu, na  hali  nyingine  au  mazingira  yoyote  atayokuwemo. Pia kumuona  mtoto  si  tu  kumuonesha  mtu  kuwa  mtoto  ni  yule  halafu  basi.  Bali  kumuona mtoto  kunajumuisha   kumuona  na  kumgusa  kimwili.


2.  JE  NI  MTOTO   WA  UMRI  GANI  ANAYEONGELEWA  HAPA.

Kifungu  cha  4 cha Sheria ya mtoto  kinajibu  swali  hili.  Kifungu  kinasema  kuwa  mtu  mwenye  umri   wa  chini  ya  miaka  18  ataitwa  mtoto .  Kwa  hiyo  tunapoongelea   kumuona  mtoto    tunamaanisha  mtu  ambaye  umri  wake  uko  chini  ya  miaka  18  yaani  kuanzia  miaka  17   kushuka  chini.  Mwenye  miaka  18  kamili  si  mtoto  kwa  maana  ya  kifungu  hiki.


BODI YA KWANZA YA CHUO CHA TAALUMA YA UREKEBISHAJI TANZANIA YAZINDULIWA

0
0
 Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa akitoa hotuba ya ufunguzi wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Urekebishaji Tanzania katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga, Dar es salaam  Mei 31, 2017.
 Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Urekebishaji Tanzania katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga, Dar es salaam  Mei 31, 2017.
 Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Urekebishaji Tanzania ambaye pia ni Katibu wa Bodi hiyo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza – SACP. Gideon Nkana akitoa historia fupi ya Chuo.
 Baadhi ya Wajumbe wa Bodi hiyo wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi..
 Mgeni rasmi Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Urekebishaji Tanzania. Walioketi kutoka kulia ni SACP. Gideon Nkana, Godfrey Semango na Dkt. Zena Mabeho. Kutoka kushoto ni DCP. Ally Lugendo, Bi. Catherine Jorome na Dkt. James Jesse. Waliosimama(kushoto) ni SACP. Dkt. Kato Rugainunura(katikati) ACP. Charles Novart na wa kwanza kulia ni SACP. Uwesu Ngarama(Picha zote na Kitengo cha Habari na Mawasiliano – Jeshi la Magereza)


Viewing all 109605 articles
Browse latest View live




Latest Images