Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1718 | 1719 | (Page 1720) | 1721 | 1722 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde inaeleza kuwa Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo wa Jimbo la Moshi Mjini na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Kilimanjaro, Mzee Philemone Ndesamburo amefariki Dunia asubuhi ya leo katika Hospitali ya KCMC, Mkoani humo. 

  Katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema amethibitisha muda huu juu ya kifo hicho na kwamba bado haijafahamika chanzo cha kifo chake.

  Kwa sasa mwili wa marehmu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti hospitali ya rufaa ya KCMC .

  Ndugu wakiwemo watoto wa marehemu wamefika Hospitalini hapo na kuomba mwili wa marehemu kufanyiwa uchunguzi kutokana na kifo kuwa ni cha ghafla.

  Lema alisema, Mzee Ndesamburo alifika ofisini kwake majira ya asubuhi na alionekana mwenye afya njema, ilipofika majira ya saa nne hali ilibadilika na kushindwa kuendelea na majukumu yake.

  Ndipo walipomkimbiza KCMC kwa ajili ya matibabu na alifariki dunia akiwa kitengo cha emergency, Taarifa zaidi tutajulishana kadri zitakapokuwa zikitufikia.

  0 0

  Katika kuhakikisha Mkoa wa Rukwa Upo salama kutokana na maambukizi ya ugonjwa wa Ebola yatakayoweza kujitokeza, Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amefanya ziara ya siku tatu katika mwambao wa ziwa Tanyangika kwenye Kata ya Kirando, Kabwe na Kasanga vijiji ambavyo vipo jirani na nchi  ya DRC ili kujionea namna Halmashauri ya Nkasi na Kalambo zilivyojipanga kuhakikisha kuwa ugonjwa huo hautii mguu katika Mkoa na nchi kwa ujumla.

  Ziara hiyo aliianza siku ya Ijumaa tarehe 26 hadi 28. 05. 2017 mara baada ya kumaliza kumalizika kwa mafunzo ya siku tatu yaliyohusu utumaji wa taarifa za magonjwa kwa kieletroniki (e-idsr) yenye kusisitiza tahadhari ya ugonjwa wa ebola uliopo katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) yaliyotolewa kwa wahudumu wa afya wa Serikali na Sekta binafsi kwa Halmashauri mbili za Manispaa ya Sumbawanga na Sumbawanga vijijini.

  Mafunzo ya awamu ya pili yanatarajiwa kumalizika tarehe 31. 05. 2017 kwa Halmashauri za Kalambo na Nkasi ikiwa ni muendelezo wa awamu ya kwanza kwa Halmashauri ya Sumbawanga Vijijini na Manispaa ya Sumbawanga yaliyoisha tarehe 26. Mwezi wa tano.

  Ili kujiridhisha na maandalizi ya Halmashauri zinazopakana na nchi za jirani yaani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) pamoja na Zambia Mkuu wa Mkoa alipita katika bandari maarufu za pwani ya ziwa Tanganyika na kuongea na vyombo vya usalama ikiwemo uhamiaji, Sumatra, TRA, jeshi la polisi, jeshi la wananchi, maafisa forodha pamoja na maafisa afya kutoka Wilayani.

  Pia Mh. Zelote aliongea na viongozi wa serikali za vijiji na kata wakiwemo madiwani, watendaji wa kata na vijiji, wenyeviti wa vijiji na vitongoji, maafisa ugani wa kata na vijiji, maafisa afya wa kata na vijiji na kufanya mikutano ya hadhara ili kuwapa wananchi ujumbe aliokwenda nao katika kuhakikisha ugonjwa huo haunusi katika mkoa wa Rukwa na nchi ya Tanzania.
  Pamoja nae Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa aliambatana na Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Boniface Kasululu, Mratibu wa Chanjo Mkoa Gwakisa Pamoja na Afisa kutoka Wizara ya Afya wa usimamizi na ufuatiliaji Solomon Mushi, Mkuu wa Wilaya, makatibu tawala wa wilaya pamoja na kamati za ulinzi na usalama za Wilaya.

  Katika kila Wilaya aliyopita Mh. Zelote alihakikisha anapewa taarifa za maandalizi ya Wilaya na kisha kwenda kwenye mipaka ili kujionea kwa macho yake maandalizi hayo na pia kuongea na wananchi wanoishi karibu na mipaka hiyo.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  Profesa Honest Prosper Ngowi akiwaelekeza baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe kuhusu utafiti unaoangazia masuala ya kodi. Kulia ni Profesa Arne Wiig akitoa maelekezo kwa mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho. Utafiti huo unafanywa kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Christian Michelsen Institute (CMI) ya Norway na Chuo Kikuu Mzumbe cha nchini Tanzania.

  Wanafunzi wa Mzumbe Dar Es Salaam wakifanya shughuli za utafiti kwa vitendo katika mradi wa utafiti wa mambo ya kodi. Mradi huu ni ushirikiano kati ya taasisi ya Christian Michelsen Institute (CMI) ya Norway na Chuo Kikuu Mzumbe. 

  Unafadhiliwa na Baraza la Utafiti la serikali ya Norway na upo katika mwaka wa mwisho katika miaka yake mitatu. Professor Ngowi wa Mzumbe ni mtafiti mkuu katika mradi huu Tanzania. Watafiti kutoka Norway waliokuwepo Mzumbe ni Prof. Odd Fjeldstad na Prof. Arne Wiig. 

  Katika utafiti huu wanafunzi walijibu maswali mbalimbali yahusuyo kodi. Matokeo yake yatatumika kushauri mamlaka kuhusu mambo kadhaa ya kodi Tanzania. Utafiti wa aina hii unafanyika pia Angola na Zambia.
  Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe wakiendelea na utafiti huo jijini Dar es Salaam jana.
  Wanafunzi wengine wakijadiliana jambo katika Chuo Kikuu cha Mzumbe ambako utafiti huo unaendelea leo.

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri  ya wilaya ya Mbogwe ndg Elias Kayandabila akionge na timu ya UMISETA ya  Wilaya wakati akifunga mashindano hayo kwa ngazi ya wilaya.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri  ya Mbogwe Ndg Elias kayandabila akiwakabidhi wanamichezo bendera ya michezo  ya Wilaya 

  Timu ya Wilaya ya UMISETA imekabidhiwa bendera ya michezo ya Wilaya na kutakiwa kwenda kuiwakilisha wilaya kwenye mashindano ya UMISETA 

     


  0 0

  TUMBAKU ni zao ambalo husababisha uharibifu wa Misitu katika uzalishaji wa tumbaku ya Mvuke, kwa kukabiliana na Changamoto hiyo Kampuni ya kuuza na Kununua tumbaku ya Alliance one Wilayani Kasulu imeandaa utaratibu wa kupanda Miti kwa kuwashirikisha Wakulima kutoa Ardhi yao na halmashauri kwa kupanda hekta 288 kwa kila msimu wa kilimo lengo ikiwa ni kuhakikisha kuni zinazotumika katika uchomaji wa tumbaku zinatoka katika chanzo endelevu cha miti wanayoipanda. 

  Akizungumza mara baada ya makabidhiano ya Mashamba ya Miti hekta 144 jana yalitooteshwa kwa kipindi cha mwaka 2014 - 2015 katika Kijiji cha Mganza na Chogo kata ya Heru juu baina ya halmashauri na kampuni hiyo Meneja uzalishaji jani katika Kampuni hiyo, David Mayunga, alisema kampuni hiyo inajihusisha na uendelezaji wa nishati mbadara ya kuchomea tumbaku, kuborsha mabani ya kuchomea iliyaweze kutumia kuni chache.

  Mayunga alisema uzalishaji wa tumbaku ya Mvuke unategemea kiasi kikubwa cha kuni hapa Tanzania na Nchi nyingine pia na husababisha uteketezaji wa misitu, kampuni hiyo wamedhamilia kuwa ifikapo mwaka 2020 uzalishaji wa tumbaku utatumia kuni kutoka katika vyanzo endelevu ambapo Wakulima na serikali watatoa maeneo yao waweze kupandiwa miti lengo ikiwa ni kuinua uzalishaji wa tumbaku pamoja na Wakulima.

  Alisema tumbaku ni zao la pili kwa Tanzania linalo ingiza fedha za kigeni, kampuni hiyo inafanya zoezi hilo katika maeneo ambayo yanalima tumbaku ilikuweza kiwasaidia Wakulima kutunza mazingira na kufanya biashara ya tumbaku bila kiathiri mazingira, kwa kipindi kilicho pita zao la tumbaku limeshuka sana kutokana na Wakulima wengi kushindwa kulima kutokana na gharama ya zao hilo.

  "Pamoja na malengo tuliyonayo ya kuinua zoezi la upandaji miti tunakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa Ardhi hili linatokana na baadhi ya Wananchi kuzuia mashamba yao yasipandwe miti kwa kuhofia kwamba watazulumiwa, kukosekana kwa ushirikiano baina ya Viongonzi na kampuni hili linasababisha kampuni kushindwa kupanda miti kwa malengo yaliyo pangwa", alisema Mayunga.
   Meneja wa uzalishaji jani wa kampuni ya Alliance one David Mayunga  akisain hati ya makabidhiano ya mashamba ya  miti kwa Halmashauri ya Wilaya ya kasulu.
  Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa kasulu Twallib Mangu, akisaini baadhi ya mikataba ya makabidhiano baina ya kampuni ya Alliance one na halmashauri.  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimfariji Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai aliyefiwa na Mama yake Mzazi Bibi Mwanaisha Hassan Vuai aliyezikwa kijijini kwao Bwejuu Mkoa wa Kusini Unguja.
  Waumini wa Dini ya Kiislamu wakimsalia Bibi Mwanaisha Hassan Vuai katika Msikiti wa Ijumaa Bwejuu aliyefariki Dunia jana katika Hospitali ya Global alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.
  Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu na Viongozi wa Serikali na Kisiasa wakimuombea Dua Marehemu Bibi Mwanaisha Hassan Vuai baada ya kumsalia kwenye Msikiti wa Ijumaa wa Bwejuu Mkoa Kusini Unguja.
  Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu na Viongozi wa Serikali na Kisiasa wakimuombea Dua Marehemu Bibi Mwanaisha Hassan Vuai baada ya kumsalia kwenye Msikiti wa Ijumaa wa Bwejuu Mkoa Kusini Unguja.
  Balozi Seif Ali Iddi kushoto akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa Kusini Unguja Nd. Ramadhan Abdullah Ali wakati wa msiba wa Mama Mzazi wa Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Zanzibar hapo Bwejuu Mkoa Kusini Unguja.

                                                       Picha na – OMPR – ZNZ.

  0 0

   Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)  Jaji Mstaafu Thomas Mihayo,akisisitiza jambo wakati akiongea katika hafla ya kuwaaga wasanii maarufu wa filamu kutoka China waliokuja nchini kwa shughuli za kisanii na kuangalia vivutio vya utalii kuwa Tanzania ni tajiri kwa vivutio vyingi vya utalii. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam.
   Wasanii wa kikundi cha Sanaa cha Wanne Star wakitumbuiza katika hafla ya kuwaaga wasanii maarufu wa filamu kutoka China waliokuja nchini kwa shughuli za kisanii na kuangalia vivutio vya utalii kuwa Tanzania ni tajiri kwa vivutio vyingi vya utalii. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam.juzi usiku.
   Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)  Jaji Mstaafu Thomas Mihayo (kushoto)akiteta jambo na Mwambata wa Ubalozi wa China nchini, Bw. Gou Haodong katika hafla ya kuwaaga wasanii maarufu wa filamu kutoka China waliokuja nchini kwa shughuli za kisanii na kuangalia vivutio vya utalii kuwa Tanzania ni tajiri kwa vivutio vyingi vya utalii. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam.

   Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania(TTB), Bi. Devota Mdachi akiandaa zawadi ya shuka ya kimasai kabla ya kumkabidhi Mwenyekiti wa Bodi hiyo  Jaji Mstaafu Thomas Mihayo (katikati)iliamkabidhi mmoja wa wasanii maarufu wa filamu katika hafla ya kuwaaga wasanii maarufu wa filamu kutoka China waliokuja nchini kwa shughuli za kisanii na kuangalia vivutio vya utalii kuwa Tanzania ni tajiri kwa vivutio vyingi vya utalii. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es salaam.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)  Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akimfunika shuka mmoja wa wasanii kutoka China katika hafla ya kuwaaga wasanii maarufu wa filamu kutoka China waliokuja nchini kwa shughuli za kisanii na kuangalia vivutio vya utalii kuwa Tanzania ni tajiri kwa vivutio vyingi vya utalii. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam.

  0 0  0 0

  Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha (kushoto) akitambulishwa wafanyakazi wa kampuni ya Monsanto Tanzania baada ya ofisi yao kufunguliwa hapa nchini eneo la Njiro mkoani Arusha, kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Monsanto Afrika, Dk Shukla Gyanendra. Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha (kushoto) akikagua ghala la mbegu bora zenye uwezo wa kumpa mkulima mazao bora.Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha akizungumza jambo baada ya kukagua ghala la mbegu bora za kampuni ya Monsanto zenye uwezo wa kumpa mkulima mazao boraMeneja Kiongozi wa kampuni ya mbegu ya Monsato Tanzania, Frank Wenga akieleza mipango kamambe ya kuwafikishia mbegu bora wakulima kote nchini.
  Wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa ofisi ya Monsanto Tanzania.
  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Chelestino Mofuga amewataka wananchi wamuunge mkono Rais John Mafuguli, katika kuhakikisha anasimamia rasilimali za watanzania na kufanikisha maendeleo ya sekta mbalimbali.

  Kwa mujibu wa Mofuga, wakati inakaribia miaka miwili ya utawala wa Rais Magufuli amefanikisha maendeleo mengi ambayo yangeweza kufanyika kwa kipindi cha utawala wamuda wa miaka 40.

  Akizungumza na wananchi wa wilaya ya Mbulu, alisema miongoni mwa maendeleo hayo ni kuzindua na kuanza kwa ujenzi wa reli ya umeme, kuhamisha makao makuu ya nchi Dodoma mpango uliodumu tangu mwaka 1973 na kuanza maandalizi ya ujenzi wa barabara za ghorofa kwenye jiji la Dar es salaam.

  Alisema amefanikisha kuongezeka kwa pato la Taifa kupitia ukusanyaji wa kodi kutoka sh850 bilioni kwa mwezi alipokuwa anaingia madarakani hadi kufikia sh1.2 trilioni kwa mwezi hivi sasa.

  Alisema pia Rais Magufuli amefanikisha ununuzi wa ndege na kufufua shirika la ndege la ATCL, kutoa elimu bure kwa shule za msingi na sekondari jambo linaloongeza usajili wa wanafunzi mara mbili.

  "Amegundua watumishi wenye vyeti feki 9,932 na watumishi hewa 19,706 ambao mishahara yao ilikuwa inatumiwa na watu wachache badala ya kupelekwa kwenye shughuli za maendeleo za wananchi ikiwemo elimu, afya na maji," alisema Mofuga.

  Alisema Taifa lilishuhudia historia nyingine baada kupokea ripoti ya tume aliyounda ya kuchunguza mchanga wenye dhahabu (makinikia) yenye wajumbe nane wenye taaluma mbalimbali za uhandisi na kuchukua hatua stahiki mara baada ya kupokea.

  "Kwenye taarifa hiyo ilibainika kuwa thamani ya madini yote kwenye makinikia ni makontena 277 yenye thamani ya sh829.4 bilioni kwa viwango vya wastani na viwango vya juu ni sh1.4 bilioni yaani dhahabu iliyokuwa kwenye makontena 277 ni sawa na lori mbili za tani saba ba pick up tani 1.5," alisema Mofuga.

  Alisema Taifa lilikuwa linahitaji kiongozi aina ya Rais Magufuli kwa muda mrefu na kutokana na utekelezaji huo unaofanyika wananchi wanatakiwa kumuunga mkono ili aongeze jitihada za kuhakikisha Tanzania inafika kwenye nchi ya maziwa na asali.

  Mmoja kati ya wakazi wa eneo hilo Yohana Amnaay alisema pamoja na jitihada hizo za Rais Magufuli pia mkuu huyo wa wilaya ya Mbulu Mofuga, amekuwa na utaratibu mzuri wa kutatua kero za jamii hasa migogoro ya ardhi kwa kukutana na wananchi.

  "Kila alhamisi DC wetu amekuwa na utaratibu wa kukutana na wananchi hivyo kupitia nafasi hiyo jamii imekuwa inatatuliwa kero zake kuliko kukaa na kusubiri viongozi wakubwa wafike Mbulu ndiyo wananchi wafikishe malalamiko yao kwao," alisema Amnaay.'

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mheshimiwa Kisare Makori amekabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Ally Happi tayari kwa kuzuru katika Miradi mitano ya Maendeleo katika Manispaa ya Ubungo.

  Akizungumza wakati wa Makabidhiano hayo Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori amesema kuwa Mwenge wa Uhuru umezuru kwa Mara ya Kwanza katika Wilaya mpya ya Ubungo hivyo historia mpya imeandikwa.

  Alisema kuwa Mwenge wa Uhuru Kwa Mwaka 2017 katika Wilaya ya Ubungo utakimbizwa umbali wa Kilomita 46 na gharama ya Miradi yote Mwenge utakapopita ni Zaidi ya Bilioni 2.8

  Mwenge wa Uhuru Mwenye kauli mbiu ya kutilia msisitizo kushiriki Kukuza Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo ya Nchi yetu umebeba jumbe mbalimbali ikiwemo ile ya Mapambano dhidi ya dawa za kulevya, tuwajali na tuwasikilize watoto na vijana utakapomaliza kutembelea Miradi ya Maendeleo katika Wilaya ya Ubungo utaelekea Mkoani Pwani.

  Katika mbio za Mwenge Umebaba ujumbe mwingine wa kuhamasisha kupungua kwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, Unyanyapaa na vifo vitokanavyo na UKIMWI.

  Aidha watanzania wameombwa kushiriki kutokomeza Malaria kwa Manufaa ya Watanzia na jamii kwa ujumla.

  Imetolewa Na;
  Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo

  0 0

  Huduma mpya yenye lengo la ukarimu, ushirika na utoaji,Imezinduliwa rasmi na Vodacom Tanzania PLC jana,Huduma hiyo  inayojulikana kama“Ukarimu wa Vodacom” ni huduma ambayo ni muhimu kwa wateja wa kampuni hiyo katika kipindi hichi cha mwezi mutukufu wa Ramadhan na katika maisha ya kila siku. Vodacom imepata uzito wa kipekee kwa kuileta huduma hii haswa ususani kwa jamii za Pwani ambako kuna Waislamu wengi na kuwakumbusha kuendeleza mshikamano.
  Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao anasema “Tumekusanya maoni mbalimbali ya kutosha kutoka sokoni ili kuweza kuelewa ni nini hasua jamii inahitaji. Tulifikiri sana ni nini tunaweza kufanya ambacho kingeweza kuwa mahsusi katika kipindi hiki, timu yangu iliona kampeni ni muhimu ikalenga kutoa kwa jamii
  Walengwa wa kampeni hii ni jamii yetu pamoja na sifa zake za kuvutia, kampeni hii itaongeza thamani katika sifa hizo kupitia ukarimu, ushirika na utoaji chini ya kauli mbiu ya “Ukarimu wa Vodacom”
  Kwa upande wake, Hendi Hisham ambaye ni mkurugenzi mkuu wa biashara wa kampuni hiyo anasema Tumefanya jitihada zote kuhakikisha kampeni hii inakuwa na mafanikio. Kampeni inahusu kurudisha kwa jamii za wateja wetu wa ukanda wa Pwani kwa Tanzania nzima,”
  Alisema huduma hiyo itawezesha;
  ·        Kuziweka karibu zaidi familia na marafiki kutokana na dakika zaidi zitakazowawesha kupiga simu kipindi hikim cha mwezi mtukufu wa Ramadhan kupitia Ukarimu wa Vodacom
  ·        Kwa kutambua umuhimu wa Ramadhan huduma hiyo itawapatia wateja huduma za bure kama vile mawaidha na kuwa kumbusha muda wa swala
  ·        Uwezo wa kupiga simu bure wakati wakisubiri kula “Daku”
  ·        Kugawa tende kwenye foleni bara barani ili kushiriki Ramadhan pamoja na jamii.

  “Ili mteja aweza kunufaika na bando hili la Ukarimu anatakiwa kupiga *149*01# kisha kuchagua aina ya bando kulingana na uwezo wake wa kifedha. Lipo bando linalodumu kwa muda saa 24 na linalodumu kwa siku saba ,” anasema.
  Mkurugenzi huyo alieleza kuwa, bando hilo linampa mteja ujumbe mfupi wa maandishi wenye ujumbe wa dini ikiwamo hadithi, Qaswida, Dua, pamoja na Mwaidha kila siku bure.
  “Faida nyingine ni pamoja na kupiga simu bure usiku kabla ya muda wa daku, Facebook na picha bure ” alieleza.
  Alisema kwa shilingi 1000, mteja atapata dakika 150 Vodacom kwenda Vodacom, dakika 10 kwenda mitandao yote, ujumbe mfupi wa maandishi wa maandhishi  bila kikomo, simu kupitia mtandao pamoja na ujumbe wa didi bure
  Kwa mteja atakayenunua bando la shilingi 3000 atapata dakika 150 Vodacom kwenda Vodacom, dakika 30 kwenda mitandao mingine, ujumbe mfupi wa maandishi bila kikomo, simu za bure usiku Vodacom kwenda  pamoja na ujumbe mfupi wa maandishi wa dini bure kwa siku saba

   Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi (wa pili kushoto) akikaribishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao (kulia) kwenye uzinduzi wa kampeni ya Ukarimu wa Vodacom, wakati wa futali iliyoandaliwa na kampuni hiyo katika Mwezi Mtukufu wa Ramadjhan jijini Dar es Salaam jana.Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mufti wa Tanzania, Abubakary Zubery. Huduma mpya yenye lengo la ukarimu, ushirika na utoaji, itamwezesha mteja wa Vodacom Tanzania  kunufaika na bando hili la Ukarimu kwa kupiga *149*01# kisha kuchagua aina ya bando kulingana na uwezo wake wa kifedha. Lipo bando linalodumu kwa muda saa 24 na linalodumu kwa siku saba .

   Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi (kushoto) akizindua kampeni ya Ukarimu wa Vodacom  wakati wa futali iliyoandaliwa ya Vodacom Tanzania PLC  jijni Dar es Salaam jana Wanaoangalia ni Mkurugenzi Mtendaji wa  kampuni hiyo, Ian Ferrao (katikati) na Mufti wa Tanzania, Abubakary Zubery. Huduma mpya yenye lengo la ukarimu, ushirika na utoaji, itamwezesha mteja wa Vodacom Tanzania kunufaika na bando hili la Ukarimu kwa kupiga *149*01# kisha kuchagua aina ya bando kulingana na uwezo wake wa kifedha. Lipo bando linalodumu kwa muda saa 24 na linalodumu kwa siku saba

  Mkurugenzi Mkuu wa Biashara wa Vodacom Tanzania PLC, Hendi Hisham (kulia) akifafanua jambo kwa Mufti wa Tanzania Abubakary Zubery kwenye uzinduzi wa kampeni ya Ukarimu wa Vodacom, wakati wa futali iliyoandaliwa na kampuni hiyo katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan jijini Dar es Salaam jana.Kampeni hiyo ilizinduliwa na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi (katikati). Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao. Huduma mpya yenye lengo la ukarimu, ushirika na utoaji, itamwezesha mteja wa Vodacom Tanzania kunufaika na bando hili la Ukarimu kwa kupiga *149*01# kisha kuchagua aina ya bando kulingana na uwezo wake wa kifedha. Lipo bando linalodumu kwa muda saa 24 na linalodumu kwa siku saba.

  0 0

  Na Anil Ricco , Globu ya Jamii

  Mkuu wa Jeshi la polisi Nchini (IGP),Simon sirro ameahidi kutoa sh.milion 10 kwa yeyote atakayetoa taarifa za kufanikisha kuwakamata watu wanaofanya mauaji ya viongozi huko Kibiti wilayani Rufiji Utete mkoani Pwani.

  Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Sirro amesema kumekuwa na mauaji ya wananchi na Askari katika Wilaya ya Rufiji Utete pamoja na Wilaya ya Mkuranga ambayo yamekuwa yakifanywa na wahalifu wachache kwa malengo wanayoyajua wao,

  Amesema Jeshi la Polisi bado linaendelea na Operesheni mbalimbali kuhakikisha kwamba vitendo hivyo haviendelei kuweza kubaini mzizi.

  Aidha Mkuu wa Jeshi la Polisi Mpya amezungumzia juu ya waendesha boda boda kuwa na tabia ya kukaidi kufata sheria za usalama barabarani ikiwemo kubeba abiria zaidi ya mmoja ‘mishikaki.

  Sirro amesema waendesha bodaboda wanashindwa kufuata sheria za usalama barabarani kwa kupita taa nyekundu pamoja na kutovaa kofia ngumu ‘Helment’ ambapo kumesababisha wengine vifo na majeruhi ya kuwafanya kuwa na ulemavu wa kudumu .

  Hata hivyo amesema kumekuwa na malalalamiko dhidi ya baadhi ya Askari polisi kujihusisha na vitendo vya rushwa lakini pia baadhi ya wananchi kuwashawishi Askari kupokea rushwa ikiwa ni sehemu ya ngao ya kukwepa kuwajibishwa pindi wanapokuwa wamefanya makosa.
  Sehemu ya waandishi wa habari pamoja na Makamanda wa Jeshi la Polisi wakimsikiliza IGP Mpya, Simon Sirro alipokuwa akizungumza na Wanahabari mapema leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
  Mkuu wa jeshi la polisi Nchini (IGP),Simon sirro akizungumza na waandishi habari (hawapo pichani) juu ya hatua mbalimbali za kuweza kudhibiti masuala ya uhalifu likiwemo la mauaji yanayoendelea Kibiti leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Bitdefender Antivirus, the innovative security solutions provider, has released a free tool that will scan your entire Office/home network to pinpoint weaknesses that could let thieves take your private info and photos and allow hackers and snoops to take control of your Internet-connected devices.


  Once installed on your PC, Bitdefender Home Scannerscans your Office/home Wi-Fi network to identify the devices you have connected to your local network. Then it identifies risks on any connected device, like weak usernames and passwords, unsafe communication and different vulnerabilities in the device’s firmware and delivers a thorough report. This includes tips on how to address and secure the network, based on the vulnerability identified. Click below link to get freeBitdefender Office/home scanner tool:     


  0 0


  0 0

   Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Andrew Chenge akisoma dua ya kuliombea Bunge katika  kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
   Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe.Dk.Medard Kalemani akiwasilisha Randama za Makadirio na Matumizi ya Wizara yake  kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
   Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Harrison Mwakyembe katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
   Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Mhe.George Masaju akifuatilia jambo kutoka kwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dk.Suzan Kolimba  katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Ajira,Kazi,Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  Na Tiganya Vincent, RS- Tabora

  31 Mei, 2017

  Jumla ya shilingi milioni 180 zimekusanywa na Jeshi la Polisi mkoani Tabora katika kipindi cha Mwezi huo kutokana na makosa mbalimbali yaliyofanywa na waindeshaji wa vyombo vya moto.

  Takwimu hizo zilitolewa jana mjini Tabora na Kamanda wa Mkoa wa Tabora Wilbroad Mtafungwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari ofisi kwake wakati akitoa ufafanuzi juu ya jitihada mbalimbali wanazozifanya katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu mkoani humo.

  Alisema makusanyo hayo yametokana tozo kwa madreva wa magari, pikipiki na bajaji na waendesha baiskeli walivunjia Sheria za Usalama barabarani katika kipindi hicho.

  Kamanda alitaja baadhi ya makosa ni madereva wa Bodaboda kutovaa kofia ngumu wao na abiria wao , madereva wa magari kuendesha bila kuwa na leseni, mwendokasi, kutozingatia alama za barabara na kupakia abiria zaidi ya uwezo wa chombo cha usafiri.

  Kamanda Mtafungwa alitoa wito kwa watu wote wanaoendesha vyombo vya moto Mkoani Tabora kuepuka kuvunja Sheria za Usalama Barabarani ili waokoe fedha wanazozipata zitumike kusaidia familia zao katika  matumizi mengine ya maendeleo badala kulipa faini.

  “Naomba waendeshaji wa vyombo vya moto kuzingatia Sheria za Usalama barabarani ili wasipigwe faini ambazo zinawafanya watoe fedha ambazo zingewesaidia wao na familia katika shughuli mbalimbali” alisema Kamanda huyo wa Mkoa wa Tabora.


  0 0

  Alfred Lucas, Misri.
  TIMU ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' inatarajia kuanza mazoezi jioni ya leo  kujiandaa na mchezo wa kuwania nafasi muhimu ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika NCHINI Cameroon.

  Stars walioingia majira ya saa 7 usiku na kufikia katika mji wa Alexandria, Misri uliweza kuwasili salama na kwa niaba ya timu nzima, Kocha Mkuu, Salum Shabani Mayanga pamoja na viongozi wengine akiwamo Mkuu wa Msafara, Wilfred Kidao walishukuru Mungu kwa kusafiri salama hadi kufika hapa Alexandria kwa ajili ya kambi ya wiki moja kujindaa kucheza na Lesotho.

  Akizungumza mara baada ya kukagua viwanja vya mazoezi leo asubuhi, Kocha Mayanga amesema  “Programu ya mazoezi kwa timu hii itaanza leo saa 2.00 usiku ingawa siku nyingine nitafanya asubuhi na jioni.”

  Taifa Stars inayopiga kambi nchini Misri, inajiandaa na mchezo dhidi ya Lesotho utakaofanyika Juni 10 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam mchezo uliopangwa  kuanza saa 2.00 usiku.

  Mchezo dhidi ya Lesotho ni muhimu kwa Tanzania ikiwa ni mechi ya kwanza kwa Taifa Stars katika Kundi ‘L’ wakiwa na timu za Uganda na Cape Verde kuwania nafasi muhimu ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika NCHINI Cameroon.

  Wachezaji wanaounda kikosi hicho cha Kocha Salum Mayanga akisaidiwa na Novatus Fulgence ambaye ni kocha msaidizi Patrick Mwangata - kocha wa makipa pia yumo Meneja wa timu, Danny Msangi; Mtunza Vifaa, Ally Ruvu, Daktari wa timu ni Richard Yomba na Daktari wa viungo ni Gilbert Kigadye ni makipa Aishi Manula (Azam FC), Benno Kakolanya (Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar). Walinzi wa pembeni wako Shomari Kapombe (Azam FC), Hassan Kessy (Yanga SC), Mohammed Hussein (Simba) na Gadiel Michael.

  Walinzi wa kati ni Erasto Nyoni (Azam FC), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Nurdin Chona (Tanzania Prisons) ilihali viungo wa kuzuia ni Himid Mao (Azam FC) na Jonas Mkude kutoka Simba SC ambaye kwa sasa anapatiwa matibabu baada ya kupata ajali.

  Viungo wa kushambulia Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla (Simba SC) na Mzamiru Yassin (Simba) wakati viungo wa pembeni ni Simon Msuva (Yanga SC), Shizza Kichuya (Simba SC) na Farid Mussa (Teneriffe, Hispania). Washambuliaji wapo Mbwana Samatta (KRC Genk- Ubelgiji), Ulimwengu (AFC Eskilstuna – Sweden), Ibrahim Ajib (Simba SC), Mbaraka Yusufu (Kagera Sugar) na Abdurahman Mussa (Ruvu Shooting).
  Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga (kulia) akikagua Uwanja ambao timu itautumia kwa ajili ya mazoezi kwenye kambi ya Tolip Sports City, Alexandia, Misri. Wengine ni kutoka kushoto Mkuu wa Msafara (HOD), Wilfred Kidao ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya TFF, Meneja wa timu, Danny Msangi na Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Novatus Fulgence.

  Madakatari na lishe :Madaktari wa Taifa Stars, Dk. Gilbert Kigadye (aliyesimama kushoto) na Dk. Richard Yomba (aliyesimama kulia) wakitoa maelekezo ya chakula hitajika kwa baadhi ya wachezaji wa Taifa Stars.

  Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga (kulia) na viongozi wengine wakikagua ukumbi wa mazoezi ya viungo ‘Gym’.

  0 0
  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeteua makocha 26 kwa ajili ya kufanya skauti za vijana wenye vipaji vya soka kwenye mashindano ya shule za msingi (Umitashumta) na Sekondari (Umisseta) ngazi za mikoa watakaojumuishwa kwa maandalizi ya michuano ya Afrika.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Salum Madadi alisema TFF kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imedhamiria kuboresha mashindano hayo ili kupata vijana wengi wenye vipaji kuanzia ngazi ya mkoa na Taifa.

  Mashindano ya Umisseta ngazi ya taifa yanatarajiwa kufanyika Juni 6 hadi 17 na Umitashumta Juni 27 hadi 28 jijini Mwanza ambapo mikoa itapeleka timu zao kuwakilisha kitaifa.

  “Tumejipanga kwenda kuchagua vijana ngazi ya mkoa na baadaye kitaifa. Tunategemea makocha tuliowateua watatufanyia kazi hiyo kutoka kila mkoa na baadaye kutakuwa na jopo la makocha sita watakaokuwa Mwanza kwenye fainali Umitashumta na Umisseta,”alisema.

  Alisema wanataka kuibua vipaji kwa vijana wenye umri chini ya miaka 13 ambao watashiriki fainali za mataifa ya Afrika chini ya umri wa miaka 17, mwaka 2021. Hivyo maandalizi yaanza kuanzia sasa.

  Pia, alisema wataboresha kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 15 watakaoshiriki fainali za vijana chini ya umri wa miaka 17, mwaka 2019. Lakini pia, watachaguliwa vijana chini ya umri wa miaka 20 kuboresha kikosi hicho cha Ngorongoro Heroes.
  \
  Makocha walioteuliwa mikoa mbalimbali ni Oscar Mirambo (DSM), Kessy Mziray (Mwanza), Shaweji Nawanda (Mtwara), Charles Mayaya (Shinyanga), Mohamed Muya (Dodoma), Mohamed Laizer (Arusha), Madenge Omari (Mara),Samwel Moja (Lindi), Issa Mgaza (Kilimanjaro), Khamis Mambo (Kigoma), John Nzongwe (Geita), Zakaria Mwamba (Rukwa), Godfrey Mvula (Ruvuma) na Aloyce Mayombo (Pwani),

  Wengine ni Osuri Kosori (Simiyu), Gabriel Gunda (Singida) Zahoro Ramadhan (Tanga), Athuman Kairo (Morogoro), Fidelis Kalinga (Iringa), Ally Kagire (Kagera), Mohamed Bachoro (Katavi), Albeti Gama (Njombe), Andrew Nzoma (Tabora), Anthony Mwamlima (Songwe), Gaul Msalia (Mbeya) na Victor Kijazi (Manyara).

  0 0

   Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa akitoa hotuba ya ufunguzi wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Urekebishaji Tanzania katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga, Dar es salaam leo Mei 31, 2017.
   Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Urekebishaji Tanzania katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga, Dar es salaam leo Mei 31, 2017.
   Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Urekebishaji Tanzania ambaye pia ni Katibu wa Bodi hiyo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza – SACP. Gideon Nkana akitoa historia fupi ya Chuo.
   Baadhi ya Wajumbe wa Bodi hiyo wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 1718 | 1719 | (Page 1720) | 1721 | 1722 | .... | 3270 | newer