Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110019 articles
Browse latest View live

ofa ya tanapa


WAANDISHI WA HABARI ZA KILIMO TANZANIA (TAJF) WAKUTANA MALAIKA BEACH RESORT JIJINI MWANZA KUPANGA MIKAKATI

$
0
0
Na Dotto Mwaibale, Mwanza
WAANDISHI wa Habari wanaounda Chama cha Waandishi wa Habari za Kilimo wamekutana Malaika Beach Resort jijini Mwanza kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali ya chama hicho.
Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika jana Mwenyekiti wa chama hicho, Gerald Kitabu pamoja na mambo mengine alihimiza wanachama ambao bado hawajatoa michango yao ya mwaka waitoe ili kutunisha mfuko wa chama hicho.
"Ni muhimu wanachama ambao bado hawajaotoa michango yao kuhakikisha wanaitoa kwa wakati" alisema Kitabu.
Katibu wa Chama hicho, Elias Msuya alisema chama hicho kipo katika mchakato wa kutengeneza vitambulisho kwa ajili ya wanachama na wakati wowote vitakapo kuwa tayari vitatolewa kwa wahusika.
 Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Kilimo Tanzania (TAJF), Gerald Kitabu (kulia), akizungumza na waandishi wa habari wanachama wa TAJF wakati wa kikao kilichofanyika Ufukwe wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza jana kujadili masuala mbalimbali ya chama hicho.
 Katibu wa Chama hicho, Elias Msuya akizungumza katika kikao hicho. Kulia ni Mtunza Fedha wa chama hicho, Ellen Manyangu.
 Wanachama wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.


GREEN WASTE PRO YAJITOLEA KUREKEBISHA SANAMU LA ASKARI JIJINI DAR ES SALAAM

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 30.05.2017

MAGAZETI YA LEO JUMATANO MAY 31,2017

BRITAM INSURANCE TANZANIA YAZINDUA BIMA YA AFYA KWA MAKAMPUNI

$
0
0
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Britam Insurance Tanzania, Stephen Lokonyo akizungumza na waandishi wa habari habari (hawapo pichani) juu ya uzinduzi wa bima ya Afya kwa wagonjwa wanaolazwa ambayo ni maalum kwa Wafanyakazi wa makampuni Makubwa, ya Kati na Madogo, katika Mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es salaam.
Meneja wa Bima ya Afya wa Britam Insurance Tanzania, Christine Mwangi (wa pili kulia) akielezea namna Bima hiyo itakavyokuwa inafanya kazi kwa wateja wawatakaojinga na faida zake, wakati wa Mkutano na waandishi wa habari habari (hawapo pichani) uliofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es salaam. wengine pichani toka kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Utawala, Irene Godson, Afisa Mtendaji Mkuu Britam Insurance Tanzania, Stephen Lokonyo, Meneja wa Mauzo, Godfrey Mzee pamoja na Afisa Oparesheni, Farai Dogo. Picha na Othman Michuzi.
 Meneja wa Mauzo wa Britam Insurance Tanzania, Godfrey Mzee akizungumza.

BULEMBO AONGOZA MAZISHI YA MDOGO WA SPIKA WA ZAMANI MAREHEMU SAMWELI SITTA

$
0
0
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhajj Abdallah Bulembo akimkabidhi rambirambi ya CCM, mjane wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania Samwel Sitta, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa mdogo wa Spika huyo wa zamani wa Bunge la Tanzania marehemu Samweli Sitta, Peter John Sitta, nyumbani kwa marehemu, Urambo mkoani Tabora leo 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhajj Abdallah Bulembo akimpa pole, Ben Sitta, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa mdogo wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania marehemu Samweli Sitta, Peter John Sitta, nyumbani kwa marehemu, Urambo mkoani Tabora leo .
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhaji Abdallah Bulembo na Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri, wakiwa na nyuso za majonzi wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa mdogo wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania marehemu Samweli Sitta, Peter John Sitta, nyumbani kwa marehemu, Urambo mkoani Tabora leo 
Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa salam za rambirambi wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa mdogo wa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania marehemu Samweli Sitta, Peter John Sitta, nyumbani kwa  marehemu, Urambo mkoani Tabora leo 

WATUMISHI KATIKA HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO IPASAVYO

$
0
0
Na,Vero Ignatus Arusha.

Katibu wa CCM mkoa wa Arusha Ernest Mpanda amekutana na watumishi katika Halmashauri ya Jiji  la Arusha ambapo amesema kuwa serikali ya awamu ya tano inatambua na kuthamini kazi kubwa wanayoifanya ,huku chama hicho kikiwa na imani ya kwamba binadamu wote nisawa,heshima ,kutambuliwa pamoja na Ujamaa na kujitegemea.

Ameyasema haya leo katika kikao cha kuimarisha utendaji kazi na  kuwataka watumishi hao kuutanguliza Uzalendo mbele,wafanye kazi kwa manufaa ya Taifa na kwa Watanzania kwa ujumla , kwa maadili na kwa usahihi.

"wakati wa kupiga umekwisha,hatutakubali tumekupa uongozi  hukuwa na mali nyingi, ndani ya miaka miwili  unakutwa unazo mali nyingi ulizojilimbikizia bila kufahamika vyanzo vyake lazima tutakuhoji,kila mtu atimize wajibu wake kwa kumuogopa Mungu" alisema katibu huyo.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro amesema kuwa ni vyema kila mtumishi akasimamia eneo lake la kazi ipasavyo bila kuingiza undugu kwenye kazi,kwani kila mmoja akisimamia eneo lake kikamilifu hakuna mtu yeyote yule atakayekuwa na shida na wao.

"Umepewa eneo lako la uitumishi lisimamie ipasavyo usilete undugu kwenye kazi,ukifanya kazi yako vizuri hakuna mwenye shida na wewe,unalipwa mshahara ni vyema ukajiuliza je unafanya kazi kama ipasavyo?"alihoji mkuu wa wilaya .

Aidha Daqqaro amewataka watumishi hao kuwahudumia wananchi kwa moyo safi,lugha nzuri ,kila mmoja afanye kazi yake kwa usahihi japokuwa wananchi wengine wanakera ,amewataka kutambua kuwa mwisho wa siku wao ndiyo wameajiriwa na siyo wale ambao wanawahudumia. 

"Wahudumieni kwa moyo safi na lugha nzuri,tendeni kazi kwa kuzingatia maadili na kwa usahihi,usije ukapigiwa simu na kiongozi wako ukaanza kuingiwa na hofu na kujiuliza kuna jambo gani tena" alisisitiza Daqqaro.
Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha Ernest Mpanda akiwa anazungumza katika kikao cha kuimarisha Utendaji  katika Halmashari ya Jiji ,aliyepo kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro ,aliyepo kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Juma Kihamia 
 
 Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro akizungumza na Watumishi wa Halamashauri ya Jiji la Arusha katika kikao hicho kilichofanyika leo 
 
 Baadhi ya watumishbi waliobhudhuria katika kikao hicho kilichofanyika leo.Picha na Vero Ignatus Blog.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

KAMISHNA WA USTAWI WA JAMII ATEMBELEA KITUO CHA KULEA WAZEE CHA KIBIRIZI KILICHOPO MKOANI KIGOMA.

$
0
0

Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi akitia saini katika kitabu cha wageni mara bada ya kuwasili katika kituo cha kulea Wazee cha Kibirizi mkoani Kigoma mapema wiki hii.
Afisa Mfawidhi wa kituo cha kulea Wazee cha Kibirizi Bw. Heradius Mushi (kulia) akifafanua mambo mbalimbali yahusuo kituo hicho kwa Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi(katikati) wakati Kamishna huyo alipotembelea kituo hapo mapema wiki hii Mkoani Kigoma.
Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi(katikati) akitoa maelekezo kwa Afisa Mfawidhi wa kituo cha kulea Wazee cha Kibirizi Bw. Heradius Mushi (kulia) wakati wa ziara yake kituo hapo mapema wiki hii Mkoani Kigoma kushoto ni Mkurugenzi wa Manunuzi kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ( Idara ya Ustawi wa Jamii) Bibi Martha Chuma.

ASILIMIA 24.9 HUVUTISHWA MOSHI WA TUMBAKU KWENYE SEHEMU ZA KAZI.

$
0
0

NA ALLY DAUD-WAMJW DODOMA

ASILIMIA 24.9 ya watanzania huvutishwa moshi wa tumbaku katika sehemu za kazi hivyo kuchangia kuongezeka kwa wagonjwa wa saratani nyingi hapa nchini.

Hayo yamebainishwa kwenye taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu inayohusu Maadhimisho ya siku ya kutotumia tumbaku duniani.

“Hali hii isipodhibitiwa vifo vitaongezeka kufikia asilimia 80 kwenye nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania na milioni 8 kwa mwaka duniani kote ifikapo 2030” iliongeza taarifa hiyo.

Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa katika uchunguzi uliofanywa mwaka 2013 na Wizaya ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia Taasisi ya Utafiti wa Maradhi ya Binadamu(NIMR) wakishirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) ulionyesha asilimia 24.9 huvutishwa moshi wa tumbaku sehemu za kazi, asilimia 14 ya watanzania hutumia tumbaku na asilimia 17 ya watanzania hawavuti lakini wanavutishwa moshi wa tumbaku.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa tumbaku inaua watu takribani milioni 6 kila mwaka na moshi wake huua zaidi ya watu laki 6 ambao sio wavutaji wa tumbaku duniani .

Mbali na hayo Wizara ya afya imedhamiria kupiga vita matumizi ya tumbaku kwa kuhakikisha hakuna matangazo ya tumbaku kyupitia kwenye mabango barabarani,luninga,redio,sinema,au kubandikwa ukutani na kwenye magari ya matangazo.

Madhimisho ya Siku ya kutovuta Tumbaku huadhimishwa Mei 31 kila mwaka duniani kote na kwa mwaka huu imebeba kauli mbiu isemayo”TUMBAKU-TISHIO KWA MAENDELEO” .

Serikali Yatoa Bilioni 13 Kumalizia Ujenzi wa Jengo la Moi

$
0
0

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

Serikali imetoa jumla ya shilingi bilioni 13.5 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa awamu ya tatu wa jengo jipya la Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) linalotegemewa kukamilika na kuanza kutumika kwa asilimia mia moja mwaka huu.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Respicious Boniface alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku nne ya madaktari kutoka nchi mbali mbali za Afrika.

Dkt. Boniface amesema kuwa changamoto kubwa inayoikabili taasisi hiyo ni ongezeko la wagonjwa sababu iliyopelekea kuanzishwa kwa mradi wa ujenzi wa jengo jipya litakalokuwa na vifaa vya kutosha hivyo kupanua huduma za afya pamoja na kupunguza gharama za rufaa za wagonjwa kutibiwa nje.

“Awamu ya tatu ya mradi wa ujenzi wa jengo jipya la MOI ulianza na jumla ya shilingi bilioni 17.9 ambazo ni fedha za mkopo kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) lakini fedha hizo hazikuweza kukamilisha ujenzi hivyo tumeongezewa na Serikali jumla ya bilioni 13.5 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo,”alisema Dkt. Boniface.

Mkurugenzi huyo amemshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwezesha kupatikana kwa fedha hizo ambazo zitasaidia kumalizika haraka kwa ujenzi wa jengo hilo ambalo litaondoa changamoto ya kujaa kwa wagonjwa.

Akizungumzia mafunzo hayo ya madaktari, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Msiru amesema kuwa huu ni mwaka wa tano tangu mafunzo hayo yaanze kufanyika nchini ambapo yanashirikisha wakufunzi kutoka MOI pamoja na Marekani.

“Lengo la mafunzo hayo ni kutoa elimu ya tiba za majeruhi wa ajali kwa madaktari kutoka nchi mbalimbali za Afrika zikiwemo za Zimbabwe, Liberia, Sudan,Ethiopia, Namibia na Malawi yakiwa na nia ya kubadilishana ujuzi wa jinsi ya kutibu wagonjwa wenye ulemavu na kuzuia vifo,”alisema Prof. Msiru.

Kwa upande wake Daktari bingwa wa Mifupa MOI, Edmund Ndalama amesema kuwa nchi nyingi bado hazijachukulia ajali kama ni jambo la kuwekewa msisitizo wakati ajali ni tatizo kubwa linalopoteza maisha ya watu wengi na kuwaacha wengine wakiwa na vilema vya maisha.

“Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha kuwa takribani watu milioni sita wanafariki kwa ajali kila mwaka na kati ya watu milioni 20 hadi milioni 50 wanabaki na ulemavu wa maisha, hii ni idadi kubwa ya watu ambayo hata ukilinganganisha na idadi ya vifo vinavyotokana na magonjwa mengine havifikii idadi hiyo”, alisema Dkt.Ndalama.

Amemalizia kuwa umefikia muda kwa madaktari kufahamu njia nyingi zinazohusiana na kutibu magonjwa ya mifupa yanayosababishwa na ajali ili kupunguza idadi ya vifo vya wananchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI), Dkt. Respicious Boniface akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku nne kwa madaktari kutoka nchi mbali mbali za Afrika, Kushoto ni Daktari bingwa wa MOI, Dkt. Edmund Ndalama.Ufunguzi huo umefanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Msiru akiongea na waandishi wa habari juu ya uendeshaji wa mafunzo hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku nne kwa madaktari kutoka nchi mbali mbali za Afrika.

Daktari bingwa wa Mifupa wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI), Dkt. Edmund Ndalama akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya ajali ilivyo nchini wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku nne ya madaktari kutoka nchi mbali mbali za Afrika. Ufunguzi huo umefanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya madaktari kutoka nchi mbalimbali za Afrika wakisikiliza mafunzo yenye lengo la kubadilishana ujuzi wa jinsi ya kutibu wagonjwa waliopata ajali. Mafunzo hayo ya siku nne yameanza leo Jijini Dar es Salaam.

WAZIRI WA ARDHI AFUNGUA SEMINA YA WANACHAMA WA CHAMA CHA WAPIMA ARDHI TANZANIA.

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William Lukuvi (katikati waliokaa) akipiga picha ya pamoja na wanachama wa chama cha wapima Ardhi Tanzania, baada ya kumaliza semina iliyofanyika jana katika hoteli ya Morena Mjini Dodoma.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William Lukuvi (wa pili kulia) akisisitiza jambo wakati akifungua semina ya wanachama wa chama cha wapima Ardhi Tanzania, iliyofanyika jana katika hoteli ya Morena Mjini Dodoma.
Wanachama wa chama cha wapima ardhi Tanzania wakifwatilia semina iliyoendelea leo katika hoteli ya Morena Mjini Dodoma.

Waajiri na Mamlaka za Ajira watakiwa kuzingatia Sheria na Miongozo ya Utumishi wa Umma

$
0
0
Na Fatma Salum (MAELEZO)

Serikali imewataka Waajiri na Mamlaka za Ajira na Nidhamu kote nchini kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo inayosimamia Utumishi wa Umma ili kuleta ufanisi katika usimamizi na uendeshaji wa masuala ya Rasilimali Watu kwenye Utumishi wa Umma.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi wa Umma Bw.Nyakimura Muhoji wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Muhoji alisema kuwa kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Tume hiyo imefanya ukaguzi wa Rasilimali Watu katika Taasisi 41 na kubaini kwamba kuna baadhi ya Waajiri, Mamlaka za Ajira na Nidhamu hazitekelezi ipasavyo majukumu yao hususan katika usimamizi wa masuala ya ajira na nidhamu hivyo kupunguza ufanisi katika utendaji kazi.

“Ukaguzi wa Rasilimali Watu umefanyika katika Taasisi 41 ambazo ni Sekretariet za Mikoa mitano ikiwemo Morogoro, Iringa, Mbeya, Arusha na Mwanza, Mamlaka za Serikali za Mitaa 30 zilizopo kwenye mikoa hiyo pamoja na Wakala na Taasisi 6 kwa lengo la kuangalia ni kiasi gani Waajiri na Mamlaka za Ajira na Nidhamu wanafanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya Utumishi wa Umma.” alieleza Muhoji.

Naye Katibu Msaidizi Idara ya Afya kutoka Tume hiyo Bw. Peleleja Masesa alisema kuwa hali ya uwasilishaji wa taarifa zinazohusu usimamizi wa Rasilimali Watu hairidhishi kwa kuwa zipo baadhi ya Taasisi za Umma hazitekelezi jukumu hilo la kisheria.

“Nasisitiza kuwa uwasilishaji wa taarifa kwa Tume ni jukumu la kisheria hivyo Waajiri na Mamlaka za Ajira na Nidhamu ambao hawajawasilisha taarifa hizo wanakumbushwa kuziwasilisha kwa mujibu wa mwongozo uliotolewa.” alisisitiza Masesa.

Aidha Masesa alieleza kuwa Tume hiyo pia ina jukumu la kupokea na kushughulikia Rufaa na malalamiko yanayohusu masuala ya kiutumishi kutoka kwa Watumishi wa Umma ambao hawakuridhika na jinsi masuala yao ya kiutumishi yalivyoshughulikiwa na mamlaka zao.

Pia alitoa wito kwa Watumishi wa Umma na Watendaji wote kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, maadili ya Utumishi wa Umma na taaluma zao ili Utumishi wa Umma ukidhi matarajio ya wananchi.
Katibu Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Nyakimura Muhoji akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu majukumu mbalimbali yaliyotekelezwa na Tume hiyo katika mwaka wa fedha 2016/17 kwa ajili ya kuboresha utendaji katika utumishi wa umma. Kushoto ni Katibu Msaidizi wa Tume hiyo Bw. Peleleja Masesa.
Katibu Msaidizi Idara ya Afya kutoka Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Peleleja Masesa akifafanua kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu Sheria ya Utumishi wa Umma Na.8 inayoelezea majukumu ya Tume hiyo. Kulia ni Katibu Msaidizi Idara ya Utumishi Serikalini kutoka Tume hiyo Bw. John Mbisso.
Katibu Msaidizi Idara ya Utumishi Serikalini kutoka Ofisi ya RaisTume ya Utumishi wa Umma Bw. John Mbisso akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taratibu za kupokea na kushughulikia rufaa za watumishi wa umma katika Tume hiyo. Kulia ni Katibu Msaidizi wa Tume hiyo Bw. Peleleja Masesa.(PICHA ZOTE NA FATMA SALUM- MAELEZO)

JAFO AWAONYA WAKANDARASI WA MIRADI YA TAMISEMI

$
0
0
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amewataka wakandarasi wanaojenga miradi ya miundombinu mbalimbali kwenye Halmashauri nchini kuhakikisha miradi hiyo inakamilika ndani ya muda na inakuwa na ubora unaotakiwa.

Jafo alitoa kauli hiyo leo katika uzinduzi wa mradi wa Maji Wilunze wilayani humo.

Mradi huo umefanikiwa kukamilika na kuzinduliwa rasmi kufuatia maagizo aliyoyatoa Machi,26 mwaka huu baada ya kutembelea na kubaini kuna uzembe Mkubwa katika utekelezaji wa mradi huo.

Baada ya kubaini hilo, Jafo alitoa kalipio kwa watendaji wa Halmashauri pamoja na Mkandarasi wa ujenzi wa mradi na kuagiza mradi huo ukamilike haraka ifikapo leo Mei 30, mwaka huu, kinyume cha hapo atawachukulia hatua kali watendaji na Mkandarasi endapo angeshindwa kukamilisha ndani ya muda huo.

Aidha, Jafo alimwambia mkandarasi wa Mradi huo kuwa endapo asipotekeleza asitegemee kupata kazi yeyote iliyo chini ya Halmashauri yeyote hapa nchini kwani Ofisi ya Rais Tamisemi haiwezi kuvumilia wakandarasi wazembe. 
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo pamoja na Mbunge wa Jimbo la Chilonwa Joel Mwaka wakipiga makofi baada ya kuzindua mradi wa maji Wilunze.
Jiwe la msingi la Mradi wa maji Wilunze
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza mara baada ya kumtwisha ndoo ya maji mmoja wa wananchi wa kijiji cha Wilunze.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MKUU WA MKOA WA ARUSHA,MRISHO GAMBO AMPONGEZA MFUGAJI ALIYEJENGA HOTELI

$
0
0


Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akizindua hoteli ya Eserian ,kulia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)mkoa wa Arusha,Michael Lekule Laizer.

Mmiliki wa hoteli ya Eserian,Issaya Yassi(kulia)akimweleza Mkuu wa mkoa,Mrisho Gamb(wa pili kushoto),Askofu Masangwa(kushoto) na Mwenyekiti CCM mkoa wa Arusha,Michael Lekule Laizer namna alivyotumia mifugo kuwekeza kwenye nyumba ya wageni.

Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akiangalia mandhari ya hoteli ya Eserian akiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)mkoa wa Arusha,Michael Lekule Laizer.

Mfanyabiashara maarufu wa jijini Arusha,Philemon Mollel maarufu kwa jina la Monaban (kushoto) akikabidhiwa tuzo maalumu na Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo iliyotolewa na shirika la kidini World Mission International kwa kutambua mchango kwa jamii. 


TAARIFA KWA UMMA

SIX YEARS IN HEAVEN

$
0
0
Time is a healer, so people say
It is now six years since God took you away
You went into a sleep that was long and deep
The vacant place you left in our home, will never be filled

Our darling mother, wife, sister, grandmother, we will always remember you

Your special smile

Your caring heart

That warm embrace, you always gave us

And most importantly, the astounding legacy you left behind

In our heart you will forever remain, Dr Helen IgobekoLugina


Helen, the bole of our family tree you are dearly missed by:

Husband – MaxmillianLugina

Son – Dr. Emmanuel Lugina

Daughter – Mary LuginaZangira

Son in law – Richard Zangira

Daughter – RoselindaLugina Reuben

Son in law – Kelvin Reuben

Granddaughter – Gabriella Zangira

Grandson – Nathan Zangira

Granddaughter – Joanna Reuben

Granddaughter – Juliana Reuben
Family and friends

KARIBU ULIPE KODI YA MAJENGO

Article 1

TBS YAWASHAURI WAZALISHAJI WADOGO WADOGO WA BIDHAA KUTUMIA FURSA YA BURE YA UKAGUZI

$
0
0

Hayo yamesemwa na Afisa Masoko Mwandamizi kutoka katika shirika hilo,Gladnes Kaseka pichani kushoto juu wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya tano ya biashara ya Mkoa wa Tanga .

Alisema kuwa licha ya TBS kutoa fursa hiyo lakini bado wazalishaji wadogo na wakati wameshindwa kuitumia fursa hiyo kwa ukamilifu wake na kusababisha kuendelea kuwepo kwa bidhaa ambazo hazina nembo ya ubora.

"Bado wazalishaji wetu wengi hawajaweza kuifikia fursa hiyo ambayo itaweza kuwasaidia kuhakikisha wanazalisha bidhaa zenye ubora lakini wataweza kuingiza bidhaa zao kwa urahisi katika masoko ya ushindani tofauti na sasa" alisema Kaseka.

Aidha alisema kuwa bado wanaendelea na jitihada za kuhakikisha wanaziondosha katika soko bidhaa ambazo ni hafifu kwa kufanya ukaguzi wa Mara kwa Mara katika masoko na maeneo yote yanayohusika na shughuli za uuzaji wa bidhaa.

Nae Mfanyabiashara Aisha Kisoki alisema kuwa changamoto kubwa ni muingiliano wa bidhaa kutoka nje ambazo kwa hapa nchini zinauzwa kwa bei rahisi tofauti na wanazozizalisha.

Alisema kuwa iwapo TBS wataweza kudhibiti uingiaji usio rasmi wa bidhaa kutoka nje utasaidia sana wafanyabiashara wa ndani ya nchi kuona umuhimu wa kuweka nembo bidhaa zao.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
Wazalishaji wadogo wadogo wa bidhaa nchini wameshauriwa kutumia fursa ya bure ya ukaguzi wa bidhaa zao inayotolewa na Shirika la Viwango Tanzania TBS.
Viewing all 110019 articles
Browse latest View live


Latest Images