Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live

Bunge lapitisha Bajeti ya Wizara

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Philip Mahiga (Mb) akiwasilisha hotuba ya bajeti ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2017/2018 Bungeni mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba (Mb) akijibu hoja mbalimbali za Wabunge wakati wa Kikao cha Bunge baada ya kuwasilishwa kwa bajeti ya Wizara Mjini Dodoma. 
Baadhi ya Waheshimiwa Mabalozi wanaoziwakilisha nchi mbalimbali nchini wakifuatilia uwasilishwaji wa Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bungeni mjini Dodoma. 

Waziri Mhe.Balozi Dkt. Mahiga akifurahia jambo na Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Peter Msigwa mara baada ya kuwasilisha hotuba ya bajeti Bungeni mjini Dodoma. 


MWENGE WA UHURU KUWASILI WILAYA YA UBUNGO KESHO 31 MEI 2017

0
0
Mwenge wa Uhuru Mwaka 2017 utawasili kesho Tarehe 31 Mei 2017 katika Wilaya ya Ubungo kuanzia saa moja kamili asubuhi na kuzuru katika Miradi mitano ya Maendeleo.   
     
Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori amesema kuwa katika mbio hizo za Mwenge wa Uhuru Mradi mmoja wa kituo cha Polisi Gogoni utawekwa jiwe la msingi.

Alisema kuwa Miradi mingine itakayozinduliwa ni Mradi wa Ujenzi wa Jengo la kutolea huduma za VVU katika Kituo cha afya Mbezi, Uzinduzi wa madarasa nane katika shule ya Msingi Malambamawili iliyopo Kata ya Msigani, Uzinduzi wa Kituo cha mabasi SIMU 2000 Kata ya Sinza na Uzinduzi wa Zahaanti ya Mburahati.

Mhe Makori alisema kuwa Miradi yote hiyo itakayotembelewa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 itagharibu Bilioni 2,854,647,991.89

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori amewasihi wakazi wa Manispaa ya Ubungo kujitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge wa Uhuru ambao utawasili katika eneo la SAISAI Kata ya Gobaukitokea Manispaa ya Kinondoni.

Pia amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi katika Viwanja vya Barafu, Shule ya Msingi Mburahati kwenye mkesha wa Mwenge wa Uhuru.

Imetolewa Na:
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake Kibamba Chama-Dar es salaam
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akizungumza na Waandishi wa habari

TPSF: MAZINGIRA YA VIWANDA YANAHITAJI USHIRIKIANO KATI YA SEKTA YA UMMA NA BINAFSI

0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

Mfuko wa Sekta Binafsi Nchini (TPSF) umesema kuwa katika kujenga mazingira ya biashara kunahitaji kuwepo kwa sekta ya umma pamoja na sekta binafsi katika kuandaa maeneo tengefu ya biashara.

Hayo ameyasema leo Makamu Mwenyekiti wa TPSF, Salum Shamte kwa niaba ya Mwenyekiti wa TPSF wakati akifungua mkutano wa 17 wa mwaka wa Mfuko wa Sekta ya Binafsi (TPSF) uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Shamte amesema kuwa katika kuendana na mipango ya kufikia uchumi wa kati sekta binafsi na sekta ya umma zinatakiwa kushirikiana katika kuangalia mazingira ya kufanya uwekezaji wa viwanda. 

Amesema katika maagizo ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa wakuu wa mikoa , kutenga maeneo ya viwanda ambapo kuna uwezekano huo upo lakini changamoto ni miundombinu ya maeneo hayo.

Aidha ameiomba serikali kuanizisha Benki ya kuendeleza viwanda ili sekta hiyo iweze kukua na kufikia uchumi wa kati kwa kuajili watanzania wengi.
Shamte ameimba serikali kuongeza bajeti kwa mamlaka ya EPZA ili kuweza kutenga maeneo tengefu ya viwanda.

Hata hivyo amesema kuwa sekta binafsi ndio inaajiri kwa sehemu kubwa kuliko sekta ya umma, kutokana na takwimu zinaonesha kwa mwaka vijana wanahitimu 800,000 kwa sekta ya umma inaajiri vijana 40,000. 

Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye amesema mkutano 17 kwa majadiliano yatayofanyika yataongeza uhai wa TPSF .Amesema ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi unazidi kuimarika hivyo kunaleta tija juu mahusiano.
Makamu Mwenyekiti wa TPSF, Salum Shamte akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa 17 wa Mfuko wa Sekta Binafsi nchini uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye akikaribisha wajumbe wa mkutano mkuu wa mfuko huo leo katika uliofanyika katika ukumbi wa Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa EPZA ,Joseph Simbakalia akiwasilisha mada katika mkutano mkuu wa 17 wa TSPF, uliofanyika katika ukumbi wa Serena jijini Dar es Salaam.
Sehemu wajumbe wa Mkutano 17 wa TPSF uliofanyika katika ukumbi wa Serena jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka Globu ya Jamii.

NSSF YASHIRIKI MAONYESHO YA BIASHARA TANGA TRADE FAIR

0
0

Ofisa Matekelezo wa NSSF Mkoa wa Tanga, Athuman Rajabu (kushoto), akimwandikisha mwanachama mpya wa Hiari wa mfuko huo, Moses Francis, baada ya kupata elimu juu ya mafao yatolewayo na NSSF wakati wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Tanga Trade Fair) yaliyofanyika katika viwanja vya Mwahako jijini Tanga, mwishoni mwa wiki.
Ofisa Matekelezo Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Tanga, Abuu Mshangama (kulia), akimkabidhi fulana ya NSSF, Hamis Chika, mmoja wa watu waliotembelea banda la NSSF kwenye Maonyesho ya Biashara-Tanga Trade Fair yaliyofanyika katika viwanja vya Mwahako jijini Tanga, mwishoni mwa wiki.
Ofisa Matekelezo Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Tanga, Abuu Mshangama (kulia), akimkabidhi fulana ya NSSF, Hamis Chika, mmoja wa watu waliotembelea banda la NSSF kwenye Maonyesho ya Biashara-Tanga Trade Fair yaliyofanyika katika viwanja vya Mwahako jijini Tanga.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akipata maelezo alipotembelea banda la NSSF.
Ofisa Masoko na Uhusiano wa NSSF, Anna Nguzo akitoa elimu juu ya mafao yanayotolewa na NSSF kwa wananchi waliofika katika maonyesho ya Biashara ya Tanga Trade Fair.

SPIKA WA BUNGE ATEMBELEWA NA MCHUNGAJI ANTHONY LUSEKELO LEO MJINI DODOMA.

0
0

Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mchungaji Anthony Lusekelo (kulia) alipomtembelea leo katika ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akipiga picha ya pamoja na ugeni kutoka Kanisa la Maombezi (GRC) ukiongozwa na Mchungaji Anthony Lusekelo (wa tatu kulia) baada ya kikao kilichofanyika leo katika ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akizungumza jambo wakati alipotembelewa na ugeni kutoka Kanisa la Maombezi (GRC) ulioongozwa na Mchungaji Anthony Lusekelo (wa pili kulia) katika kikao kilichofanyika leo katika ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kulia) akimsikiliza Mchungaji Anthony Lusekelo (kulia) kutoka Kanisa la Maombezi (GRC) pale alipomtembelea leo katika ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.

MKUU WA WILAYA YA MBOGWE AKAMATA MBAO 1889 NA MABANZI 570

0
0
Wananchi wa wilaya ya Mbogwe wametakiwa kutoa ushirikiano wa kutosha kuwafichua wavunaji haramu wa mazao ya misitu. 
 
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Mhe Martha Mkupasi alipofanya doria maalumu iliyoandaliwa na ofisi ya TFS kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W) - Mbogwe kwa lengo la kukamata mazao ya misitu yaliyovunwa kinyume cha Sheria ya Misitu. Katika doria hii jumla ya mbao 1889 za vipimo tofauti tofauti na mabanzi 570 vilikamatwa kwenye kijiji cha Masumbwe, vitongoji vya Kibondo A na B.

Akiongea wakati wa zoezi hilo meneja wa TFS wilaya ya Mbogwe Yohana France aliwasisitiza wananchi wahakikishe wanazingatia taratibu za biashara ya mazao ya misitu ikiwa ni pamoja na kuwa na usajili, kulipa ushuru wa serikali na kuzingatia taratibu za uvunaji wa mazao ya misitu kama unavyoelekeza mwongozo wa uvunaji wa mazao ya misitu wa mwaka 2015, “Mazao yote yanayomilikiwa kinyume cha utaratibu ni haramu na yakikamatwa yatataifishwa na wamiliki kupewa adhabu kwa mujibu vifungu 88,89, 95 vya Sheria ya Misitu Na. 14 ya mwaka 2002 na marekebisho yake”.

Pamoja na hayo Bwana Yohana aliwatahadharisha wananchi kujiepusha na matapeli wanaojiita watumishi wa Idara ya Maliasili na wanaopita mitaani kuwatapeli wananchi mali zao na kuwaomba rushwa kwa madai kuwa wametumwa na ofisi, tayari watu wawili ambao ni walinzi wa kampuni ya ulinzi ya Summit iliyopo Masumbwe wameshakamatwa na kufikishwa mahakamani.

Akitoa taarifa fupi wakati wa zoezi la kusaka wavunaji haramu wa misitu, Meneja wa TFS (W) amemueleza Mkuu wa Wilaya kuwa wameshatoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu taratibu za kuzingatia mtu anapotaka kufanya biashara ya mazao ya misitu na umuhimu wa kulinda rasilimali za misitu.

 baadhi ya mazao ya misitu  yaliyokamatwa
Meneja Tfs akikagua mazao ya misitu  yaliyofichwa ndani

WAWILI WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA KUDAIWA KUHARIBU MALI YA MILIONI 47

0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Watu wawili, Ally Sadick na Anna Kimaro, wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kuharibu mali ya milioni 47.

Hata hivyo, washtakiwa watatu wanaodaiwa kutenda kosa pamoja na hao hawakuweza kufika mahakamani na bado wanatafutwa.

Wakili wa Serikali, Patrick Mwita amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa washtakiwa hao ni Omary Sadick, Tumsifu Kimaro na Steven Kimaro ambao wanaendelea kutafutwa ili waweze kukabiliana na kesi hiyo.

Katika kesi hiyo imedaiwa kuwa, huko katika eneo la Kunduchi Mtongani wilaya ya Kinondoni washtakiwa waliharibu nyumba mbili, choo na miti ya minazi mitatu vyote vikiwa na thamani milioni 47 mali ya Mohamed Mshindo.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, walikana na upelelezi bado haujakamilika.

Mahakama imewaamuru washtakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao kila mmoja asaini dhamana milioni 10.

Kesi imeahirishwa hadi Juni 13, mwaka huu.

TWIGA CEMENT KUENDELEA KUWA VINARA WA UZALISHAJI SARUJI LICHA YA KUIBUKA KWA MAKAMPUNI MENGINE NCHINI

0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Kampuni ya Saruji nchini ya Tanzania Portland Cement inayozalisha Twiga Cement, imesema kuwa itaendelea kuwa kinara kwa mauzo ya Saruji hapa nchini, licha ya kuwepo wa viwanda vingi katika miaka ya hivi karibuni.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa kampuni hiyo Alfonso Velez, alipokuwa akitoa ripoti ya mauzo ya kampuni hiyo na changamoto inazokabiliana nazo katika mkutano wa wanahisa wa kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.

“licha ya makampuni mengine kuja na mpango wa ujanja wa kushusha gharama za saruji bado Twiga Cement imeendelea kuwa ndio saruji bora kwenye soko licha ya changamoto ya kupambana na bei ya soko”

Amesema wao wameshuhudia wakiona washindani wao wakihangaika juu ya upataji wa mali ghafi ambazo zitaweza kuwasaidia kuendelea kufanya bishara kwa bei ya chini lakini TPCC bado haijatetereka.

Amesema kuwa mshindani wake bado ana wakati mgumu kwani yuko mbali na soko na inamchukua muda mrefu kusafirisha mzigo mpaka sokoni hivyo wakati wowote atapandisha bei ya saruji na Twiga itabaki pale pale, kwani ameweza kufanya hivyo katika nchi zingine alizowekeza ambapo amepandisha bei kuwa juu hili kufidia gharama za uzalishaji.
Mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya TPCC , Osward Urasa akizungumza katika mkutano huo juu ya wanahisa kutoa taarifa zitakazosadia kujenga kampuni  kuwa imara.
Mwenyekiti wa kampuni ya Tanzania Portland Cement, Alfonso Rodriguez akizungumza katika mkutano huo wa wanahisa wa kampuni hiyo uliofanyika leo katika hotel ya Ramada.


MAGHEMBE APONGEZA OPERESHENI YA KUONDOA MIFUGO HIFADHINI MKOANI KAGERA

0
0

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Kagera unaongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Meja Jenerali Mst. Salum Kijuu kwa kufanikisha operesheni ya kuondoa mifugo katika maeneo ya hifadhi mkoani humo huku akitoa tahadhari kwa watumishi wa hifadhi hizo kupoteza ajira zao endapo wataruhusu mifugo hiyo kurudi tena katika hifadhi hizo.


Ametoa pongezi na tahadhari hiyo jana mjini Bukoba wakati akizungumza na uongozi wa mkoa huo na kusema kuwa, kazi hiyo ni ya kupongezwa sana kwakua imeleta matumaini ya uhifadhi mkoani Kagera na taifa kwa ujumla.


“Napenda niwashukuru kipekee kabisa kwa jinsi ambavyo mlifanya ile operesheni ya kuondoa mifugo kwenye hifadhi zetu, tulifanya kwa ueledi uliotukuka, hata kama umesikia watu wanalalamika lakini hakuna aliyesema kuku wangu waliuawa, walipigwa risasi, tulinyang’anywa mifugo, kazi hii ilifanywa vizuri na kwa ueledi mkubwa sana”, alisema Prof. Maghembe.


Aliongeza, “Hatutaruhusu tena mifugo hiyo irudi huko ndani ya hifadhi, hili ni jambo kubwa ambalo ni wajibu wa wahifadhi wote kuhakikisha  kwamba hakuna mifugo itakayokuwa inaingia humo ndani, Kuanzia sasa kama tutakuta mtu ameingia kwenye hifadhi yako wakati tunamuondoa tunamuondoa yeye na wewe na familia yako yote ili mbegu yako mbaya isibaki katika uhifadhi wa wanyamapori”.


Alisema ili kuimarisha ulinzi katika hifadhi hizo, utaratibu wa kutumia ndege maalum za doria na “drones” (ndege zisizo na rubani) utawekwa ili kuwabaini wahalifu watakaokuwa wamekaidia agizo hilo ili wachukuliwe hatua za kisheria.  


“Tutakua tunarusha ndege mara moja kila baada ya wiki tatu au wiki mbili kuhakikisha kwamba hakuna mtu anaingia na mifugo humo ndani, lakini pili tutafanya doria na ndege zile ambazo hazina marobani kuhakikisha kwamba tunaangalia kinachotokea humo ndani wakati wote.


“Najua wanaweza kubadilisha “system” (utaratibu) ikawa ya usiku na hawa askari hawa tutawapa mafunzo maalum chini ya jeshi la wananchi wa Tanzania, kuanzia miezi sita mpaka tisa, wajifunze namna ya kuhangaika na hawa ambao wanaingia kwenye hifadhi zetu”, alisema. 
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kagera, mjini Bukoba kuhusu operesheni ya kuondoa mifugo kwenye maeneo ya hifadhi pamoja na taratibu sahihi za kuendesha minada ya mifugo iliyotaifishwa kisheria. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa huo, Meja Jenerali Mst. Salum Kijuu, Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Deodatus Kinawiro (kulia), Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Diwani Athuman (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Prof. Alexander Songorwa. 
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akizungumza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kagera, mjini Bukoba. 
Picha ya pamoja kati ya Waziri wa Maliasili (katikati waliokaa) na kamati ya ulinzi na usala ya Mkoa wa Kagera muda mfupi baada ya kikao cha kujadili operesheni ya kuondoa mifugo kwenye maeneo ya hifadhi pamoja na taratibu sahihi za kuendesha minada ya mifugo iliyotaifishwa kisheria.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BULEMBO AENDELEA NA ZAIRA YAKE SIKONGE MKOANI TABORA LEO.

0
0
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza katika kikao cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya, Mabalozi, watendaji wa Seikali na wa Chama, leo. Katikati ni Mweneyekiti wa CCM Wilaya ya Sikonge Bisa Mbogo na kulia ni Katibu wa CCM Wilaya hiyo Emmanuel Alex
 Katibu wa CCM Wilaya ya Sikonge Emmanuel Alex akikabidhi taarifa ya uchaguzi nchani ya Chama kwa Ndugu Bulembo
Katibu wa CCM Wilaya ya Sikonge Emmanuel Alex akitoa maneno ya utambulizi kabla ya Ndugu Bulembo kuzungumza na Kamati ya Siasa ya Wilaya hiyo leo.Wajumbe Ukumbini. Picha zote na Bashir Nkoromo
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi, Alhaj Abdallah Bulembo akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Ofisi ya CCM Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora leo, kuendelea na ziara yake ya mikoani kukagua na kuimarisha uhai wa chama na Jumuia zake, na pia kuzungumzia masuala ya uchaguzi unaoendelea ndani ya Chama. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Ndugu Wagasubi na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Sikonge Abisa Mbogo.

Mshindi wa Milioni za Biko Arusha apokea fedha zake

0
0
WAENDESHAJI wa Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, jana wamemkabidhi zawadi yake jumla ya Sh Milioni 10 mshindi wao wa jijini Arusha, Leopard Mpande, aliyetangazwa mshindi katika droo ya tisa iliyofanyika Jumapili, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Biko, Charles Mgeta, alisema Mpenda ni mshindi akitokea jijini Arusha, baada ya kuamua kucheza bahati nasibu ya Biko.

Alisema wanajisikia faraja kubwa kuona watu wanaingia kwa wingi kucheza mchezo wao wa kubahatisha na kuzoa mamilioni ambapo zaidi ya Watanzania 35,000 wameshinda zawadi mbalimbali.

Mgeta anasema hadi sasa wameshafanya droo kubwa tisa huku washindi wote wakiwa wameshakabidhiwa fedha zao hivyo kufanya jumla ya Sh Milioni 90 kuwafikia washindi wa droo kubwa za Sh Milioni 10.

“Huku Jumatano ya kesho tukitoa Sh Milioni 20 kwa mshindi wetu wa droo kubwa, tunajivunia kuona idadi ya wanaovuna mamilioni kutoka Biko inaongezeka kwa kucheza kwa kupitia M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money ambapo jinsi ya kucheza ni kufanya miamala kwenye simu zao kwa kuingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 na kumbukumbu namba ikiwa ni 2456.

“Mtu anaweza kucheza kuanzia Sh 1000 au zaidi huku kila tiketi moja inayopatikana kwa Sh 1000 ikiwa na nafasi mbili ya ushindi wa papo kwa hapo pamoja na nafasi ya kuingia kwenye droo kubwa ya kuwania Sh Milioni 10, huku kwa Jumatano hii dau likipanda hadi Sh Milioni 20,” alisema Mgeta.
Mkurugenzi Mtendaji wa Biko Tanzania Charles Mgeta mwenye miwani akishuhudia katika makabidhiano ya Sh Milioni 10 kwa mshindi wao wa jijini Arusha Leopard Mpande aliyepatikana katika droo ya Jumapili iliyopita. Aliyeshikana mikono na Mpande ni Balozi wa Biko Kajala Masanja.
Mshindi wa Sh Milioni 10 wa Biko jijini Arusha, Leopard Mpande wa tatu kutoka kushoto akipokea nyaraka na fedha zake baada ya kukabidhiwa kutokana na ushindi wa droo ya nane ya Biko iliyochezeshwa Jumapili. Wengine wanaoshuhudia ni Balozi wa Biko, Kajala Masanja, Msanii Mpoki na maofisa wa NMB jijini Arusha.
Mshindi wa Biko jijini Arusha akisikiliza ushauri wa kifedha kutoka kwa afisa wa NMB Jijini Arusha jana.

BENKI KUU YATOA MAFUNZO YA NOTI HALALI KWA WATUMISHI WA OFISI YA MKUU WA MKOA SINGIDA.

0
0
Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imetoa mafunzo kwa watumishi wote wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida juu ya alama zinazopatikana katika noti halali za fedha ya Tanzania leo asubuhi katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa. 

Akitoa mafunzo hayo Afisa Kutoka Benki Kuu ya Tanzania Rehema Zongo amewafafanulia watumishi hao namna ya kutambua noti halali kwa vitendo huku akisisitiza alama muhimu zinazopatikana katika noti halali ili waweze kutofautisha na zile bandia.

Zongo amesema watumishi wanatakiwa kuichunguza noti halali, waipapase ili kuhisi mparuzo kwenye maneno yaliyoandikwa kwa maandishi maalumu mfano maandishi yanayoeleza fedha halali kwa malipo ya shilingi mia tano, elfu moja, elfu mbili, elfu tano na elfu kumi.

Amewasisitizia kuwa wanaweza kuitambua noti halali kwa kuangalia sura ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere inayoonekana unapoimulika noti kwenye mwanga na pia kukagua utepe maalumu kwenye noti za shilingi 500, 1000, 2000, 5000 na 10,000 unaoonekana kama madirisha yenye umbo la almasi ambapo hubadilika badilika noti inapogeuzwa geuzwa. 
Afisa Utumishi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Justo Herman akikagua noti halali wakati wa mafunzo yaliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania.
Mwangalizi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida Khadija Hamisi na Mkaguzi wa ndani Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Alfred Kalama wakisikiliza kwa umakini alama zinazopatika katika noti halali wakati wa mafunzo yaliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania.
Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida George Kulwa akitoa shukrani kwa niaba ya watumishi wote waliopata mafunzo ya Benki kuu ya Tanzania.
Maafisa kutoka Benki Kuu ya Tanzania Rehema Zongo na Rajab Ibrahimu wakisikiliza maswali na kutoa ufafanuzi kwa watumishi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa mara baada ya kutoa mafunzo ya alama za noti halali.

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAWASILISHA BAJETI YAKE BUNGENI MJINI DODOMA

0
0
  


Benny Mwaipaja, WFM-Dodoma

Wizara ya Fedha na Mipango imeliomba Bunge iidhinishie makadirio ya mapato na matumizi (Bajeti) ya zaidi ya shilingi trilioni 11.757 ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa mwaka wa fedha 2017/2018, kwa mafungu yote 9 yaliyochini ya Wizara hiyo.

Maombi hayo yametolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizaya hiyo, Bungeni Mjini Dodoma, leo.

Dkt. Mpango amesema kuwa kati ya fedha hizo, shilingi trilioni 10.328 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi trilioni 1.429 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Amefafanua kuwa Matumizi ya Kawaida yanajumuisha shilingi bilioni 87.996 kwa ajili ya mishahara, shilingi bilioni 778.612 kwa ajili ya matumizi Mengineyo (OC) na shilingi trilioni 9.461 ni kwa ajili ya kulipa Deni la Taifa na Huduma nyingine.

Aidha, katika fedha za matumizi ya maendeleo, shilingi trilioni 1.382 ni fedha za ndani na shilingi bilioni 46.108 ni fedha za nje.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi (Bajeti) ya Wizara yake ya zaidi ya shilingi trilioni 11.757, Bungeni Mjini Dodoma ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa mwaka wa fedha 2017/2018, kwa mafungu yote 9 yaliyo  chini ya Wizara hiyo. 
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi (Bajeti) ya Wizara yake ya zaidi ya shilingi trilioni 11.757, Bungeni Mjini Dodoma ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa mwaka wa fedha 2017/2018, kwa mafungu yote 9 yaliyo  chini ya Wizara hiyo. 
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi (Bajeti) ya Wizara yake ya zaidi ya shilingi trilioni 11.757, Bungeni Mjini Dodoma ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa mwaka wa fedha 2017/2018, kwa mafungu yote 9 yaliyo  chini ya Wizara hiyo. 
Viongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Taasisi zake, wakifuatilia kwa makini Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo, Bungeni Mjini Dodoma, ambapo kiasi cha shilingi trilioni 11.757 kimeombwa ili Wizara hiyo iweze kutekeleza majukumu yake ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa mwaka wa Fedha 2017/2018. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt. Albina Chuwa akimpongeza Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), kwa uwasilishaji makini wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.



POLISI TABORA YAKAMATA KIJANA MMOJA KWA KUTUMIA NGUO ZA JWTZ KUTAPELI

0
0
Mkulima mmoja Kitangili mkoani Shinyanga Francis Martin Kilalo (31)anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora kukutwa na sare na vifaa vingine vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) ambavyo anatuhumiwa kuvitumia kupateli na kuwadanganya kwa kuchukua fedha kutoka kwa vijana wanaotafuta nafasi ya kujiunga na Jeshi hilo.

Taarifa hiyo imetolewa jana na Kamanda wa Mkoa wa Tabaora Wilbroad Mtafungwa alipokuwa anaongea na waandishi wa habari Ofisi kwake juu ya hatua mbalimbali walizochukua katika kupambana na uhalifu mkoani humo.

Alisema kuwa Polisi walifanikiwa kumukamata mtuhumiwa huyo katika Hoteli ya JM iliyopo Wilayani Igunga akiwa na sare mbalimbali za Jeshi la waananchi Tanzania (JWTZ) zikiwa na cheo cha Koplo ambavyo ni pamoja na kofia tatu, begi, sweta, buti jozi moja, magwanda na mikanda mitatu.

Mali nyingine zilikamatwa kwa mtuhumiwa huyo ni pamoja na fomu za likizo cha likizo , fomu za kujaza vijana wanaotaka kujiunga na Jeshi hilo na Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) kwa mujibu wa Sheria na hiari na mihuli zenye nembo inayofanana na Jeshi hilo.

Kamanda Mtafungwa alisema kuwa mtuhumiwa alikuwa akitumia nyaraka na sare za Jeshi hilo kuchukua fedha kwa kuwadanganya na kuwatapeli wananchi mbalimbali kwa kudai atawatafutia ajira katika majeshi ya Kujenga Taifa na la Wananchi.

MFUKO WA PPF WAENDELEA KUKABIDHI VIFAA TIBA

0
0
Mfuko wa Pensheni wa PPF umeendelea kukabidhi vifaa tiba katika hospitali na vituo vya afya nchini kulingana na sera yake ya uchangiaji na udhamini. 
 
Katika wilaya ya Kisarawe, Mfuko wa PPF umekabidhi vifaa tiba hivyo kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI,Utumishi na Utawala bora Mhe. Selemani Jaffo kwa ajili ya hospitali ya Wilaya ya Kisarawe ambavyo ni vitanda 2 vya kujifungulia wakinamama, vitanda 4 vya wagonjwa wa kawaida, mashuka 56 na vifaa vinavyotumika kujifungulia wakinamama. Akipokea vifaa hivyo, Mhe. Jaffo alisema Mfuko wa PPF walichofanya ni jambo kubwa kwa vile hospitali za wilaya ya Kisarawe zilikuwa zikikabiliwa na changamoto katika sekta ya afya. 
 
Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele, alisema Mfuko umetoa vifaa tiba hivyo ikiwa ni muendelezo wa zoezi la kurudisha kwenye jamii kulingana na sera ya uchangiaji na udhamini ya PPF. Alisema Kisarawe ni wilaya ya nne kupata vifaa hivyo na kwamba wataendelea kutoa kwenye hospitali nyingine 12 nchini. 
 
Lulu alisema Mfuko wa PPF, umetoa vifaa tiba vyenye jumla thamani ya Sh. 99,983,700/-. Shughuli hiyo ya kukabidhi vifaa tiba kutoka Mfuko wa PPF ilienda sambasamba na taarifa ya kukabidhi vifaa tiba kutoka kwa Mfamasia Mfawadhi wa Ofisi ya Rais (TAMISEMI),Regina Joseph kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Utumishi na Utawala bora Mhe. Selemani Jafo, alisema kuwa Rais Dkt. Magufuli ametoa vitanda 20 vya kulalia, vitanda sita vya kujifunguli. Vifaa kama hivyo vinasambazwa katika hospitali nyingine nchi nzima. Naibu wa Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Utumishi na Utawala Bora, Seleman Jaffo akipokea msaada wa vifaa tiba kutoka Meneja Uhusiano wa Mfuko wa PPF, Lulu Mengele wakati wa halfa ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika jana katika hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Pwani.
Naibu wa Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoaa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Utumishi na Utawala Bora, Seleman Jaffo akimkabidhi vifaa tiba kwa Mganga mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Elizabeth Oming'o kwa ajili ya hospitali ya wilaya ya Kisarawe.

Vifaa tiba vilivyotolewa na Mfuko wa PPF.
Naibu wa Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoaa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Utumishi na Utawala Bora, Seleman Jaffo (wa tano toka kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Nedesa wakiwa katika picha ya pamoja baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa PPF na wafanyakazi wa wilaya ya Kisarawe. 


WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKIJADILI JAMBO NA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na  Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma, Mei 30, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

SHIRIKA LA AFYA NA ELIMU YA TIBA TANZANIA (TAHMEF) LAZIDUA TAWI JIPYA MKOANI MBEYA

0
0
Shirika la afya na elimu tiba Tanzania (TAHMEF) ni shirika lisilo la kiserikali (NGO), lililosajiliwa tarehe 13/09/2015 chini ya mwanzilishi Bi. Juliana Busasi na kuzinduliwa rasmi tarehe 8/7/2016 na Naibu Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, watoto na wazee Mhe Dr. Hamisi Kigwangalla.

TAHMEF hufanya kazi zake za kuboresha afya na kutoa elimu ya afya kwa kujali maadili na sheria zilizowekwa ili kuweza kuleta matokeo chanya kwa jamii nzima ya Tanzania. Kwa sasa TAHMEF Imefika zaidi ya watanzania 3,500 katika mikoa mitatu ya Tanzania Bara (Mwanza, Dar es salaam na Pwani) na Mkoa wa Mbeya ndiyo umekuwa mkoa wa nne kufikiwa na shirika hili.
Huduma mbalimbali za afya zinazotolewa ni pamoja na uwiano wa uzito na kimo (BMI),Malaria, shinikizo la damu, sukari, uchunguzi wa awali wa virusi vya ukimwi, saratani ya shingo ya kizazi na matiti kwa wanawake, tezi dume kwa wanaume na huendesha kampeni za uchangiaji damu kwa wagonjwa wa selimundu. Pia hutoa ushauri na elimu kwa watu mbalimbali wanaoudhuria kambi, midahalo na matembezi ya hisani juu ya magonjwa mbalimbali jinsi ya kuyaepuka na njia sahihi za matibabu.

Hivi sasa TAHMEF inaendesha mradi uitwao NURU YA AFYA unaolenga kuwezesha wanawake wasio na ajira rasmi na wenye kipato cha chini kuweza kukidhi huduma za afya kupitia bima za afya zitakazotolewa bure kwa muda wa mwaka mmoja pamoja na kuwapa elimu ya kuwekeza pesa kidogo kidogo ili waweze kujilipia wenyewe kwa miaka inayofuata.
Uzinduzi wa Tawi jipya mkoani Mbeya ni moja kati ya mafanikio ya mipango yao ya TAHMEF ni kumfikia kila mtanzania kupitia utoaji wa huduma za afya bure kwa wale wenye kipato cha chini pia kuchangia vifaa na mahitaji mengineyo ya hospitali katika vijiji mbalimbali, kuongeza uelewa na ufahamu wa watu juu ya magonjwa mbalimbali jinsi ya kuyaepuka na kuyakabili kuanzia katika shule za elimu ya msingi na sekondari kwa kufanya midahalo mbalimbali.

Uzinduzi huu ulifanyika tarehe 29 mwezi Mei 2017, Katika halmashauri ya wilaya ya Mbozi kwa kushirikiana na Zahanati ya Senjele na Uongozi wa Kijiji cha Senjele.Uzinduzi huu ulihusisha huduma bure za upimaji wa Afya pamoja na matibabu. Sanjari na hayo uzinduzi huu ulihusisha Elimu ya uhamasishaji wa Kuchangia Damu ambao kilele chake kitaadhimishwa kwa kampeni ya Kuchangia Damu tarehe 10 Juni 2017 mkoani Mbeya.
Shirika hili linatoa Shukrani kwa uongozi wa mkoa huu na kuendelea kuomba ushirikiano ili kufikia watanzania wengi Zaidi kwa huduma hizi.

WCF yawataka Waajiri Kutii Sheria Bila Shuruti

0
0

Na Benjamin Sawe.

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), umeendesha semina ya siku moja kwa waajiri nchini ili kutoa elimu juu ya shughuli za Mfuko na wajibu wa waajiri kwa wafanyakazi wao katika kujisajili na kuwalipa michango kwa niaba ya waajiriwa wao.

Akizungumza katika semina hiyo Mjumbe wa Bodi ya Mfuko huo Richard Wambali amesema kuanzishwa kwa mfuko huo kumekuja wakati muafaka ambapo Tanzania inaelekea katika uchumi wa viwanda hivyo kupelekea ongezeko la wafanyakazi ambapo chombo hicho ndio mkombozi wa majanga yatokanayo na kazi. 

“Ni muda muafaka kwa waajiri kutambua wajibu wenu katika Mfuko huu na pia kutambua madhara ya kutotekeleza wajibu wenu” Alisema Bw. Wambali.

Alisema Mfuko huo ulioanzishwa kwa sheria ya bunge namba 20 kifungu cha 5 ya mwaka 2008, una madhumuni ya kutoa fidia kwa Wafanyakazi kutokana na ulemavu au vifo viinavyosababishwa na ajali au magonjwa yatokanayo na kazi sambamba na kukuza mbinu za kuzuia matukio ya ajali.

Katika hotuba yake, Bw Wambali alieleza umuhimu wa waajiri kuwalipia michango wafanyakazi wake kama sheria inavyotaka, ili kuwawekea akiba pindi wapatapo na majanga wakiwa kazini.

Mfuko huo ambao umeanza kazi rasmi Julai 1, 2015, lengo kuu ni kutekeleza nia ya Serikali kukabiliana na changamoto za ulipaji wa fidia kwa Wafanyakazi katika mfumo wa utoaji fidia uliokuwepo awali

Bw.Wambali alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na kiwango kidogo cha malipo ya fidia(kiwango kisichozidi shilingi 180,000) kwa ulemavu wa kudumu na shilingi 83,000 kwa wategemezi endapo kifo kitatokea kwa Mfanyakazi husika.

Akinukuu sheria iliyoanzisha Mfuko huo, Bw. Wambali alisema, kifungu cha pili (2), cha sheria ya fidia kwa wafanyakazi namba 20/2008 cha mfuko huo unawahusu Waajiri na Wafanyakazi wote katika sekta ya Umma na Binafsi, Tanzania Bara pekee.

“Naomba ieleweke, anayepaswa kuchangia kwa mujibu wa sheria hii ni Mwajiri na sio mfanyakazi kukatwa mshahara wake.” Alifafanua Bw. Wambali.

Akizungumza wakati akitoa mada Afisa Matekelezo Bw. Musa Mwambujule amesema, Mfuko umeamua kuandaa semina hiyo ili kutoa elimu zaidi kwa waajiri kwa kutambua kuwa waajiri ndio wadau wakuu wa Mfuko huo na semina hiyo itawasaidia kujua kazi za Mfuko lakini pia wajibu wa waajiri kwa wafanyakazi katika kutoa michango ya kila mwezi.Nae, Mwanasheria wa Mfuko huo Bw. Deogratius Ngowi, alisema, Mfuko huo upo kisheria ili kutoa fidia kwa wafanyakazi watakaoumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi.

Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi ni Taasisi ya Serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na umeundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi Sura ya 263 iliyorejewa Desemba, Mwaka 2015.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Richard Wambali akifungua Semina ya uelimishaji kwa Waajiri kuhusu haki na wajibu wa mwajiri na mfanyakazi jijini Dar es Salaam leo (jana).
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Laura Kunenge akichangia mada katika semina ya uelimishaji kwa Waajiri kuhusu haki na wajibu wa mwajiri na mfanyakazi jijini Dar es Salaam leo (jana).
Mwanasheria Mwandamizi Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Deogratius Ngowi akitoa mada katika Semina ya uelimishaji kwa Waajiri kuhusu haki na wajibu wa mwajiri na mfanyakazi jijini Dar es Salaam leo (jana).
Baadhi ya washiriki wa semina ya uelimishaji kwa waajiri wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi wa semina hiyo ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Richard Wambali (Picha Zote na Benjamin Sawe)

WATANZANIA WAMETAKIWA KUISAIDIA SERIKALI KATIKA KUTATUA CHANGAMOTO KATIKA SEKTA MBALIMBALI-BONIFACE

0
0

Watanzania wameaswa kuisaidia serikali katika kutatua changamoto katika sekta mbalimbali ili kujiletea maendeleo kwa haraka, badala ya kusubiri kila jambo lifanywe na serikali.

Kauli hiyo imetolewa na Mdau wa maendeleo Boniface Myalla wakati alipotembelea shule ya Msingi Kunguru iliyopo Goba na kugawa Daftari kwa wanafunzi 300 wa darasa la kwanza.

Mayala amesema, Watanzania hawana budi kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali inayoongozwa na Rais Dk.John Pombe Magufuli za kuhakikisha inaleta maendeleo na huduma bora kwa wananchi.

"Serikali imetekeleza jukumu lake la kutoa elimu bure, imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya wanafunzi kusoma bure, sasa imebaki upande wetu wazazi na walezi kuwawezesha wanafunzi kupata vifaasaidizi," amesema.

Amesema lengo la kutoa madaftari hayo ni kuunga mkono serikali ya Rais Dk. John Pombe Magufuli katika dhamira yake ya kuhakikisha Tanzania mpya inajengeka, Tanzania ambayo kila Mtanzania atanufaika na nchi yake lakini pia kupata elimu bora.

Akizungumza baada ya kupokea zawadi hizo, Mwalimu wa wanafunzi hao, Sikujua Ramadhani amemshukuru Myala na kuiomba serikali na wadau wengine kujitokeza na kutoa msaada ili kukamilisha malebgo na ndoto za wanafunzi. Amesema wapo wanafunzi walikjuwa wakishindwa kuandika kwa kukosa madaftari na vifaa vingine vya kujifunzia hivyo ujio wa madaftari hayo utapunguza kero changamoto hiyo.


Mdau wa maendeleo Boniface Myala akizungumza na wanafunzi alipotembelea shule ya Msingi Kunguru Goba na kugawa madaftari kwa wanafunzi 300 wa darasa la kwanza leo jijini Dar es Salaam.
Mdau wa maendeleo Boniface Myala akikabidhi daftari kwa Mwalimu wa wanafunzi hao, Sikujua Ramadhani leo jijini Dar es Salaam.(picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)
Mdau wa maendeleo Boniface Myala akigawa daftari kwa wanafunzi wa darasa la kwanza wa shule ya Msingi Kunguru Goba . Leo jijini Dar es Salaam.

DC GONDWE APOKEA MSAADA WA TAIRI 14 ZA MAGARI KUTOKA BINSLUM

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe (kushoto) akipokea sehemu ya msaada wa matairi 14, kutoka kwa Muwakilishi wa Kampuni ya Binslum, Iddi Moshi "Mnyamwezi" yaliyotolewa kwa ajili ya magari ya Halmashauri ili kufanikisha shughuli mbalimbali za maendeleo katika Wilaya hiyo ya Handeni. Makabidhiano hayo yalifanyika hivi karibuni kwenye Duka la Matairi la Kampuni ya Binslum, Sikota, Temeke jijini Dar es salaam.

Viewing all 109591 articles
Browse latest View live




Latest Images