Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110090 articles
Browse latest View live

Wasanii wanogesha uzinduzi wa tamasha la Gulio la Mtaa la kituo cha redio cha 102.5 Lake FM

$
0
0

Zaidi ya wasanii 20 wa muziki wa hip hop, bongo fleva, zouk, taarabu na ngoma za asili wa Kanda ya Ziwa walinogesha uzinduzi wa kampeni ya Gulio la Mtaa iliyoanzishwa na kituo cha redio cha 102.5 Lake FM katika mnada wa wafanya biashara wa National, Nyakato wilaya ya Ilemela mjini Mwanza.

Wasanii hao ni Dogo D, Ngeta, H Mkali, G Stanza, Goliath, D Chance ambao ni wa hip hop wakati wa bongo fleva ni Abuu Mkali, King Suva, l Mavoko, Sania, na Lakezonia wakati wa zouk ni Sanja, Man Je Paul na Pradetha.

Mbali ya wasanii hao, pia kulikuwa na msanii wa taarabu, Fatina huku kwa upande wa ngoma za asili kulikuwa na Kanyau, Shimba na KG wakati kwa upande wa muziki wa Raga alikuwa myota wa miondoka hiyo Volcano.

Tamasha hilo pia hakikuwa sahau wasanii wa vichekesho kama Mama Manungwa, Malale na Mayala huku kikundi cha Tanzania Youths Talent (THT) kikionyesha staili mbalimbali za muziki na msanii wa wa wafanyabiashara wa Mnadani, Kembo akionyesha ujuzi wake katika miondoko ya hip hop.

Mbali ya kupata uelewa wa masuala ya biashara, wafanyabiashara hao walipata burudani kutoka wasanii hao nyota kutoka kanda ya ziwa chini ya udhamini wa kampuni ya Tigo, Pepsi, Genic Studios, Lake Zone tents, Busybees Enterprises, Mama Sarakikya decoration na Mamba Entertainment.
 Wasanii wa kikundi cha ngoma za asili wa kikundi cha Thimba wakifanya onyesho lake kwenye tamasha la Gulio lililoandaliwa na kituo cha redio cha 102.5 Lake FM kwenye mnada wa National, Nyakato mkoani Mwanza.  
 Umati wa watu uliofika katika uzinduzi wa tamasha la Gulio la Mtaa lililoandaliwa na kituo cha redio cha 102.5 Lake FM ambalo lilifana sana.
 Mkurugenzi Mkuu wa 102.5 Lake FM, Doreen Noni akiwapongeza wafanyabiashara waliojitokeza katika kampeni hiyo na kuwaomba kuitumia kituo chao kupaza sauti.
 Wafanyakazi wa kituo cha 102.5 Lake FM wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mama Ntilie waliopewa mafunzo ya upishi wenye usafi wa hali ya juu na kuzawadiwa zawadi mbalimbali wakati wa tamasha la Gulio la Mtaa.
Mwakilishi wa kampuni ya Tigo, Baraka Siwa akizungumza katika tamasha hilo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

IGP MPYA SIMON SIRRO AAPISHWA IKULU DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
  Kamshina wa Polisi nchini Simon Sirro akiandaliwa kwenda kula kiapo  mbele ya  Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  kuwa Kamshina Jenerali wa Polisi nchini  leo Mei 29,2017 Ikulu jijini Dar es salaam
 Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimvua cheo cha Kamishna wa Polisi Simon Sirro na kumvalisha cheo cha Kamishna Generali wa Jeshi la polisi nchini leo Mei 29,2017 Ikulu jijini Dar es salaam
 Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mkuu wa Jeshi la Polisi Mteule, Kamishna wa Polisi Simon Sirro kuwa Kamishna Generali wa Jeshi la Polisi Nchini Mei 29,2017 Ikulu jijini Dar es salaam
 Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kufanyia kazi Kamshina Jenerali wa Polisi nchini Simon Sirro mara baada ya kumuapisha Mei 29,2017 Ikulu jijini Dar es salaam
  Kamshina Jenerali wa Polisi nchini Simon Sirro akila kiapo cha maadili ya utumishi wa Umma mara baada ya kumuapisha  na Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  kuwa Kamshina Jenerali wa Polisi nchini Mei 29,2017 Ikulu jijini Dar es salaam
 Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, makamu wa Rais Mhe. Samia suluhu Hassan, Waziri wa mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba, Kaimu Jaji Mkuu Profesa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakiwa katika picha ya pamoja na Kamshina Jenerali wa Polisi nchini Simon Sirro pamoja na aliyekuwa IGP Ernest Mangu
 Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, makamu wa Rais Mhe. Samia suluhu Hassan, Waziri wa mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba,  Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakiwa katika picha ya pamoja na Kamshina Jenerali wa Polisi nchini Simon Sirro pamoja na aliyekuwa IGP Ernest Mangu pamoja na Makamishna wa Polisi
  Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, makamu wa Rais Mhe. Samia suluhu Hassan, Waziri wa mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba,  Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakiwa katika picha ya pamoja na Kamshina Jenerali wa Polisi nchini Simon Sirro pamoja na aliyekuwa IGP Ernest Mangu pamoja na Makamishna wa Polisi na maafisa waandamizi
Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Kamshina Jenerali wa Polisi nchini Simon Sirro pamoja na aliyekuwa IGP Ernest Mangu. Picha na IKULU

KAMPUNI YA TECNO MOBILE YAWAPA ZAWADI WATEJA WAKE KUANGALIA SINEMA BURE JIJINI DAR

MICHUZI TV: IGP SIRRO ATUMA SALAMU KWA WAHALIFU

JIWE LA MSINGI LA UENDELEZAJI WA BARABARA YA KUUNGANISHA DARAJA LA NYERERE LAWEKWA WAKATI WA MBIO ZA MWENGE

$
0
0
 Jiwe la Msingi la mradi wa ujenzi wa Barabara ya Kiungo kati ya Daraja la Nyerere na Barabara ya Kigamboni-Kibada  lililowekwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Amour Hamad Amour. (Picha na Francis Dande)
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni. 
  Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara, akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa Barabara ya Kiungo kati ya Daraja la Nyerere na Barabara ya Kigamboni-Kibada yenye urefu wa kilometa 1.2 wakati kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Amour Hamad Amour alipoweka jiwe la Msingi.
 Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Amour Hamad Amour, akizindua wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa mradi wa Barabara ya Kiungo kati ya Daraja la Nyerere na Barabara ya Kigamboni-Kibada.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Amour Hamad Amour (wa pili kulia) akiwa ameongozana na Meneja Mradi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi Jamal Mruma (kulia), wakati wa uzindua wa Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Kiungo kati ya Daraja la Nyerere na Barabara ya Kigamboni-Kibada. Habari kamili BOFYA HAPA



MD KAYOMBO ASHAURI WATANZANIA KUFUATA FURSA ZILIPO

$
0
0
Watanzania wametakiwa kuwa na utamaduni wa kuzifuata fursa zilizopo katika maeneo mbalimbali nchini ili kuiunga mkono Serikali katika jitihada zake za kukuza uchumi wa viwanda.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya ubungo Ndg John Lipesi Kayombo wakati akizungumza wakati akitoa taarifa ya mbio za Mwenge unaotaraji kuzuru katika Manispaa ya Ubungo Tarehe 31, Mei 2017.

Alisema kuwa katika mikoa mbalimbali Mwenge wa Uhuru ulipopita umekutana na fursa ambazo Watanzania wakizitafuta na kuzifanyia kazi wataondokana na uvivu, kukaa bila kufanya kazi na umasikini kwa kuwa sasa Serikali iliyopo madarakani ni ya kazi.

Aliongeza kuwa, nchi nyingi zimekuwa kiuchumi kupitia viwanda na kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kukuza uchumi wa viwanda, wananchi wanapaswa kuzichangamkia fursa mbalimbali ili kufanikisha dhamira ya Serikali kufikia uchumi wa viwanda.

MD amesema kuwa Mwenge wa Uhuru katika Manispaa ya Ubungo utapita katika Miradi mitano ya Maendeleo ambapo Miradi minne kati ya hiyo itazinduliwa na Mradi mmoja wa Ujenzo wa Kituo cha Polisi Gogoni utawekwa jiwe la Msingi.

Alisema kuwa Miradi yote hiyo itakayotembelewa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 itagharibu jumla ya shilingi Bilioni 2,854,647,991.89

Imetolewa Na;
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
Mkurugenzi wa Manispaa ya ubungo Ndg John Lipesi Kayombo.

REHEMA FOUNDATION YAGAWA FUTARI KIJIJI CHA KILOMO BAGAMOYO

$
0
0

Mwakilishi wa taasisi ya Rehema foundation ,Zuber akigawa chakula kwa ajili ya futari kwa wakazi wa Bagamoyo ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa na taasisi yao kutoka kwa wanancha mbali mbali wa nchi ya Uturuki kwa kipindi hiki cha Ramadhani
Mwenyekiti wa Taasisi ya Rehema ,Mustafa Diriel akigawa mifuko ya futari kwa wasiojiweza na wazee wa kijiji cha Kilomo Bagamoyo Pwani.Chakula hicho kimechangishwa na watu mbali mbali katika inchi ya Uturuki
Mohamedd akimpatia mzee Miraji fuko lake la futari katika kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani
Wafanyakazi wa taasisi ya Rehema Foundationi wakigawa mifuko ya chakula
Mbunge wa Bagamoyo akiwa na timu mzima ya Taasisi ya Rehema na wakazi wa kilomo baada ya kupewa msaada huo.

INTERNATIONAL COMMUNITY APPLAUDS TANZANIA’s LEADERSHIP OF SADC ORGAN AND EFFORTS TO STABILIZE POLITICAL SITUATION IN LESOTHO

$
0
0

Tanzania’s President Dr. John Pombe Magufuli has been applauded by the international community for his impeccable leadership of the SADC organ on politics, defense and security cooperation at this juncture when the community is ushering Lesotho into yet another National Parliamentary Election, the third within five years. 

Representatives from international organizations operating within SADC region and Lesotho in particular including the United Nations and European Union have commended SADC urgent call to the incoming government for serious structural and constitutional reforms. 

During the recent launch of SADC Electoral Observation Mission (SEOM) in Lesotho held in Maseru, Hon. Dr. Augustine Mahiga, Tanzania’s foreign Minister, Chairperson of the Ministerial Committee of the Organ and mission head reiterated SADC ‘s earlier mandate to the current government to undertake reforms in order to stabilize its political system and avoid a repeat of previous political crises. 

While commending political parties for signing pledges to accept election results and Independent Electoral Commission of Lesotho (IEC) for its preparedness for the upcoming national elections, Ambassador Mahiga sends a strong message to Lesotho,

“After three elections within less than five years the fatigued voters deserve a different and durable outcome. SADC will definitely take these pledges and commitments seriously in supporting the reform process in the Kingdom of Lesotho by the next government” said Ambassador Mahiga
Ambassador Mahiga flagged with SADC Secretariat together with members of SADC Organ with all SADC Elections Observation Mission in a group photo. SADC has deployed about 40 observers from 9 member states in this year's election. 
Ambassador Mahiga in conversation with the United States Ambassador to the Kingdom of Lesotho H.E. Matthew T. Harrington after launching SEOM at AVANI Hotel in Maseru Lesotho. 
Head of SADC Elections Observation Mission in Lesotho and Chairperson of the Ministerial Committee of the Organ Amb. Dr. Augustine Mahiga, delivering his statement during the launch of the mission recently in Maseru Lesotho. 



UVCCM SIMANJIRO YAMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI

$
0
0
Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilayani
Simanjiro Mkoani Manyara, imeungana na wapenda maendeleo nchini
kumpongeza Rais John Magufuli kwa hatua ya kuzuia usafirishaji mchanga
wa madini (makinikia) nje ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa UVCCM wilayani
Simanjiro, Bakary Mwacha alisema hatua aliyochukua Rais Magufuli ni ya
kupongezwa na kuungwa mkono na wapenda maendeleo nchini.

Mwacha alisema kitendo hicho kinapaswa kupongezwa kwani kimeonyesha
uzalendo na kulinda rasilimali za nchi na kuchukua hatua kwa viongozi
wazembe waliosababisha hali hiyo.

Alisema Rais Magufuli alipokuwa anatoa ahadi kwa wananchi kipindi
anachoomba kura mwaka 2015, kuwa atakuwa mstari wa mbele kulinda
maslahi ya Taifa ndivyo anavyofanya hivi sasa.“Ni muda mrefu nchi yetu imeibiwa kupitia madini hayo yaliyokuwa yanatoroshwa ila mara baada ya Rais Magufuli kuunda tume na kubaini madudu yaliyopo alikomesha jambo hilo,” alisema.

Hata hivyo, Mwacha alimpongeza Kaimu Katibu wa UVCCM Taifa, Shaka
Hamdu Shaka kwa kutoa tamko la kumtetea na kumlinda kwa gharama yoyote
Rais Magufuli kwa hatua ya kutekeleza mambo ya mabadilikoya kiuchumi
kisiasa na kijamii. “Sisi jumuiya ya UVCCM wilayani Simanjiro tupo bega kwa bega katika kuhakikisha tunatekeleza na kuunga mkono yale yote yanayotamkwa na
viongozi wetu wa UVCCM ngazi ya Taifa,” alisema Mwacha.

Alisema anapongeza jitihada zinazofanywa na Shaka kufanya ziara zake
za kuzunguka nchi nzima na kuzungumza kwenye vikao vya ndani kwani
anaimarisha jumuiya hiyo na kuongeza mshikamano wa vijana.

SERIKALI YAWEKA MIKAKATI YA KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA MAZIWA NCHINI

$
0
0
Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.

Serikali kupitia Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi imeweka mikakati mbalimbali ili kukabiliana na upungufu wa maziwa nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe.Dk Charles Tizeba wakati akijibu swali la Mbunge wa Wete Mhe.Mbarouk Salum Ali leo Bungeni MJini Dodoma katika Kikao cha thelathini na sita cha bunge la 11.

“Nakubaliana na Mhe.Mbunge kuwa Tanzania ina idadi kubwa ya mifugo lakini bado kuna upungufu wa maziwa,ambapo takwimu za makadirio za mwaka 2016 zinaonyesha lita bilioni 2.09 za maziwa zilizalishwa na unywaji wa maziwa kwa mtu kwa mwaka ulifikia lita 47 ukilinganisha na lita 200 zinazopendekezwa na Shirika la chakula Duniani(FAO)”,Alisema Mhe.Tizeba

Aidha kati ya Ngombe milioni 28.4, Ngombe rasmi wa maziwa ni 782,995 tu sawa na asilimia 3 ya Ng’ombe wote.Aidha kati ya mbuzi milioni 16.7 ni mbuzi rasmi takribani 50,000 ndio wa maziwa ambao ni asilimia 0.3 ya mbuzi wote.

Amezitaja jitihada ambazo Serikali imechukua ili kukabiliana na upungufu wa maziwa nchini ni pamoja na kumarisha mashamba ya kuzalisha mifugo ya Serikali (LMU’s) ili kuongeza idadi ya Ng’ombe wenye uwezo wa kuzalisha maziwa kwa wingi.

Aidha Serikali imeanzisha vituo vya uhimilishaji katika kanda 6 hapa nchini ambazo ni kanda ya Ziwa(Mwanza),kanda ya Magharibi(katavi),Kanda ya kati(Dodoma),Kanda ya Mashariki(Kibaha),Kanda ya Kusini(Lindi) na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini(Mbeya) kwa lengo la kutoa huduma ya uhilimishaji wa Ng’ombe wa Maziwa walioko kwenye maeneo hayo pamoja na Ng’ombe wa Asili ili kuzalisha idadi kubwa ya Ng’ombe wa Maziwa.

Amehimiza kuwa Jitihada hizi zitawezesha idadi ya Ng’ombe wa Maziwa kufikia milioni 2.9 ifikapo mwaka 2021/22 ambao pamoja na ng’ombe wa asili wataweza kuzalisha lita bilioni 3.8 za maziwa.

“Serikali inaendelea kuhamasisha sekta binafsi na wadau wengine wa maendeleo kuwekeza katika uzalishaji wa mitamba ya maziwa na mashamba ya ng’ombe wa maziwa kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa maziwa hapa nchini”,Aliongeza Mhe.Tizeba

MASHINDANO YA EUROPEAN YOUTH FILM COMPETITION (EYFC) 2017 YAZINDULIWA RASMI.

$
0
0

Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

Mashindano yanayoitwa European Youth Film Competition yamezinduliwa rasmi leo, May 29, 2017 ambapo yatafanyika nchini Tanzania kwa mara ya kwanza.

Mashindano hayo yameandaliwa na Umoja wa Ulaya (EU) na washirika nchi za Netherlands, United Kingdom, Ubalozi wa Ufaransa, Alliance Française, British Councils pamoja na Bodi ya Filamu nchini Tanzania.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Afisa Habari wa Umoja wa Ulaya (EU), Susanne Mbise amesema katika shindano hilo vijana watapata fursa ya kuzungumzia mijadala ya maendeleo wakati watakapokuwa wakizungumzia Suala la Ongezeko la idadi ya watu nchini Tanzania, Afrika na Duniani. Swali likiwa Je suala hilo ni changamoto au fursa ya maendeleo?

"Ndani ya Filamu za dakika 5 au 10 Washiriki wanatakiwa kuandaa Filamu ya aina yoyote, iwe 'Documentary', Maigizo lakini iwe dakika 5 au 10 katika Maudhui hayo", amesema Mbise.

Mbise amesema kuwa Kati ya vijana hao wenye umri kati ya miaka 18-35 watashindana na Washindi wa tano bora watakwenda kwenye Mashindano makubwa.

Kwa upande wa Bodi ya Filamu nchini, Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa Bodi hiyo, Abuu Kimario amewapongeza Umoja wa Ulaya kwa kuandaa Mashindano hayo, kwani yamekuja siku muafaka, kutokana na Soko la Filamu linapanda na kushuka.

Naye Mratibu wa Mashindano hayo, Moses Saka amesema kuwa mshindi wa kwanza katika Shindano hilo atazawadiwa kiasi cha Shilingi Milioni 7, mshindi wa pili Sh. Milioni 5, na mshindi wa tatu Sh. Milioni 3 za Kitanzania.
 Afisa Habari wa Umoja wa Ulaya (EU), Sussane Mbise (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mashindano ya European Youth Film Competition (EYFM) yanayozinduliwa May 29. Kulia ni Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa Bodi ya Filamu nchini, Abuu Kimario, Kushoto ni Mratibu wa Shindano hilo, Moses Sakar. 

BOHARI KUU YA DAWA ZANZIBAR KWA KUKSHIRIKIANA NA OFISI YA MFAMASIA MKUU WAMUAGA RASMI ALIEKUWA MKUU WA KITENGO CHA KUSAMBAZA DAWA ABDALLA SULEIMAN AMBAE AMESTAAFU.

$
0
0
Mkurugenzi Utumishi na Uendeshaji Wizara ya Afya Ramadhan Khamis Juma akimkabidhi cheti cha utumishi bora aliekuwa Mkuu wa Kitengo cha kusambaza dawa Zanzibar Abdalla Suleiman ambae amestaafu kazi kwa mujibu wa sheria.
Aliekuwa Mkuu wa Kitengo cha kusambaza dawa Zanzibar Abdalla Suleiman akiwapa mkono wa kwaheri wafanyakazi wenzake katika sherehe za kumuaga, wa kwanza (kushoto) Mkurugenzi wa Bohari Kuu ya dawa Zahran Ali Hamad na (kati) Mkurugenzi Utumishi na Uendeshaji Wizara ya Afya Ramadhan Khamis Juma. 
Picha ya pamoja ya mstaafu wa Bohari Kuu Abdalla Suleiman akiwa na mke wake Dkt. Aza Said (kulia) waliokaa na baadhi ya wafanyakazi wa Bohari kuu ya dawa na Ofisi ya Mfamasia Mkuu katika sherehe za kumuaga zilizofanyika Bohari Kuu ya dawa Maruhubi.

Picha na Makame Mshenga.

KINANA AKUTANA NA BALOZI WA JAMHURI YA KOREA KUSINI HAPA NCHINI.

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Ndg Abdulrahman Kinana akutana na Balozi wa Jamhuri ya Korea kusini hapa nchini Mhe Song Geum-Young alipomtembelea kwa ajili ya mazungumzo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es salaam, leo Mei 29, 2017.

Katika mazungumzo yao, wamehimiza suala la kuboresha mahusiano baina ya Jamhuri ya Korea Kusini na Tanzania pamoja na kuzungumzia ushirikiano wa muda mrefu katika kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini.
 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Ndg Abdulrahman Kinana akimsikiliza Balozi wa Jamhuri ya Korea kusini hapa nchini Mhe Song Geum-Young alipomtembelea kwa ajili ya mazungumzo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es salaam, leo Mei 29, 2017.
  Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Ndg Abdulrahman Kinana akizungumza jambo na Balozi wa Jamhuri ya Korea kusini hapa nchini Mhe Song Geum-Young alipomtembelea kwa ajili ya mazungumzo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es salaam, leo Mei 29, 2017.

  Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Ndg Abdulrahman Kinana akimkaribisha Balozi wa Jamhuri ya Korea kusini hapa nchini Mhe Song Geum-Young alipomtembelea kwa ajili ya mazungumzo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es salaam, leo Mei 29, 2017.

CUF NGOMA BADO MBICHI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Bodi ya Wadhamini ya CUF kupitia wakili wao, Hashimu Mziray leo imewasilisha kusudio la kukata rufaa kupinga uamuazi uliotolewa na mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu uliotupilia mbali kesi yao sababu CUF haina Bodi ya wadhamini.

Bodi hiyo inapinga uamuzi wa uliotolewa mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ambapo maombi yao dhidi ya Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya (CUF), Mbunge wa Mtwara Mjini, Maftah Nachuma(CUF) na wenzao sita yakuomba mahakama iwazuie kwa muda kujihusisha katika masuala ya uongozi na kufanya mikutano ya chama.

Wakili wa bodi ya Wadhamini ya CUF, Hashimu Mziray amesema wamewasilisha kusudio hilo la kukata rufaa kupinga uamuzi uliotolewa na hakimu Mashauri kwa kuwa si kweli kuwa CUF haina bodi ya wadhamini.Amedai kuwa CUF IPO hai, inawabunge, madiwani, majengo, wanachama na kwamba msajili wa vyama vya siasa hajakifuta.

ameongeza Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri hakulielewa tangazo la Wakala wa Vizazi na Vifo (Rita) na kuiomba Mahakama Kuu itengue maamuzi ya Hakimu Mashauri kwa kuwa ni batili.Mei 21 mwaka huu, Hakimu Mashauri alitoa uamuzi wa kuitupilia mbali kesi hiyo baada ya kusikiliza pande zote mbili.

Akitoa uamuzi huo, Hakimu Mashauri alisema Joram Bashange ambaye aliapa katika kiapo kuwa ni Katibu wa Bodi ya Wadhamini ya CUF aliapa uongo kwa sababu bodi hiyo ilisha isha muda wake na kwamba pande zote mbili wana maombi RITA ya kuomba usajili.ameongeza kuwa Bashange ni Katibu wa Bodi ya Wadhamini ya CUF na kwamba yeye binafsi ndiye atabeba gharama za kesi. 

Katika kesi hiyo Sakaya na wenzake walikuwa wakiwakilishwa na Wakili, Mashaka Ngole huku bodi ya Wadhamini ya CUF ikiwakilishwa na Wakili Hashimu Mziray.

Katika pingamizi wajibu maombi wanadai maombi hayawezi kusikilizwa katika mahakama hiyo kwa sababu yanashughulikiwa katika maombi namba 23/2016 yaliyopo Mahakama Kuu.Wanadai mwombaji hana miguu ya kusimamia kufungua kesi dhidi ya wajibu maombi, maombi hayo hayana msingi kwa kushindwa kubainisha jina la mwandishi wa masuala ya fedha hivyo wanaiomba mahakama kuyatupilia mbali maombi hayo kwa gharama.

Maombi hayo yaliyowasilishwa chini ya hati ya dharura ni dhidi ya wajibu maombi Sakaya, Nachuma, Thomas Malima, Omar Masoud, Abdul Kambaya, Salama Masoud, Zainabu Mndolwa na Jaffari Mneke.

Bodi ya wadhamini ilikuwa inaomba mahakama itoe zuio la muda kuwazuia wajibu maombi, mawakala wao au watu wao wowote kujihusisha katika masuala yoyote ya uongozi au kufanya mikutano ya chama hicho, hadi maombi yao hayo yatakaposikilizwa kwa pande zote husika.Wakili Mziray aliomba maombi hayo yasikilizwe kwa haraka kwa madai kwamba wajibu maombi wanataka kujiingiza katika kufanya mikutano ya chama hicho, wakati hawana uwezo wa kufanya hivyo.

Bodi hiyo ya wadhamini ya CUF iliamua kufungua kesi hiyo mahakamani hapo siku moja baada ya Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahimu Lipumba, kutangaza kutengua nafasi tano za wakurugenzi wa chama hicho na kutangaza majina mapya.

WABUNGE WATAKIWA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA KUWASAIDIA WASICHANA WANAOPATA MIMBA SHULENI

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii 

Mtandao wa Mashirika yanayopinga ndoa za utotoni wameitaka serikali kuweka mfumo madhubuti utakaowawezesha wanafuzni wa kike kuendelea kufurahia haki yao ya kupata elimu bora mara baada ya kujifungua.

Akitoa tamko hilo Mwenyekiti wa mtandao huo, Valerian Msoka amesema Serikali ,wabunge na wadau wengine kujikita katika kupambana na changamoto zinazopelekea mimba za utotoni ikiwemo ubovu wa miundombinu ya elimu kukosekana kwa elimu bora ya afya ya uzazi.

“Mtandao wa kupinga ndoa za utotoni unaamini kuwa Tanzania ina uongozi na wawakilishi wanaojali maslahi ya wananchi ambapo watoto wa kike ni miongoni mwa hao . Na ni kwa sababu hiyo mtandao una imani kuwa sauti yao itsikilizwa kwani wasichana hawa wanaopoteza masomo kutokana na mimba ni sehemu ya nguvu kazi muhimu ya msingi na yenye tija kufikia Tanzania ya Viwanda” amesema Msoka.

Msoka amemaliza kwa kusema kuwa utafiti wa kitaifa kuhusu Vichocheo na madhara ya ndoa za utotoni nchini Tanzania uliofanywa mwaka 2016 umebaini kuwa wasichana wana uelewa mdogo juu ya afya ya uzazi.
Mwenyekiti wa Mtandao wa kutetea wadada wadogo, Valerian Msoka 
Mwenyekiti wa Tamwa , Eda Sanga akizungumza juu ya kuwaomba wabunge kutunga sheria kuwasaidia watoto wanaopata mimba mashuleni 
Mkurugenzi wa Tawla nchini ,Tike Mwambipile akizungumza wakati wa kutoa tamko hilo .
Waandishi wa habari wakifatilia mkutano huo.



HOSPITALI YA MKURANGA YAKABILIWA NA CHANGAMOTO-DK.KIGWANGALA

$
0
0
Na Chalila Kibuda ,Globu ya  Jamii.

Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga inakabiliwa na changamoto mbalimbali kutokana kuanzishwa kwake kulianzia katika zahanati.

Hayo ameyasema na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala wakati alipofanya ziara katika Hospitali ya Wilaya ya  Mkuranga,  amesema Hospitali ya Mkuranga kuanzia majengo kuwa mbalimbali tofauti na inavyotakiwa.

Amesema katika ziara hiyo amesema hata mfumo wa kuhifadhi taka katika hospitali hiyo hauko sawa pamoja  na hali ya usafi katika wodi ya wazazi.
Dk.Kigwangala amesema kutokana na mazingira yaliyopo katika hospitali itachukua hatua katika kuiweka hospitali hiyo kwenye .ubora mzuri.

Aidha amesema Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega amekuwa bega kwa bega na hospitali ya  Mkuranga  ikiwa ni pamoja na kutafuta wadau katika kusaidia hospitali katika maeneo mbalimbali.

Dk. Kigwangala amesema kuwa Mganga Mkuu wa Hospitali  kujitoa katika kufanya masuala mengine bila kusubiri serikali kuu ikiwa ni pamoja na kutenga siku ya kufanaya  usafi katika hospitali hiyo.

Nae Mbunge wa  Mkuranga , Abdallah Ulega amesema ziara ya Naibu Waziri huyo itazaa matunda kwa hospitali ya Mkuranga kuwa na sifa ya hospitali ya Wilaya.

Amesema  watakuwa na utaratibu wa kufanya usafi kwa mara moja kwa wiki hali ambayo inaweza kuleta mabadiliko katika hospitali hiyo.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangalla akizungumza na watendaji wa Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga na Halmashauri wakati ziara yake katika Hospitali hiyo. .(picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii).
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga akizungumza na watendaji wa Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga na Halmashauri katika ziara ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala.
 Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akitoa neno la shukurani kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala kufanya ziara katika hospitali hiyo.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala akikabidhi gari la wagonjwa na vifaa kwa  Uongozi wa Wilaya ya Mkuranga.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

DARUSO yampongeza JPM kwa kusimamia rasilimali za Taifa

$
0
0
Frank Mvungi-MAELEZO



RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amepongezwa na Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (DARUSO) kwa kusimamia vyema rasilimali za Taifa ili ziweze kuwanufaisha watanzania wote.



Kauli hiyo  imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na  Rais wa (DARUSO) Bw.John Jilili wakati wa mkutano wao na vyombo vya habari uliolenga kutoa tamko la kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais kwa kuunda Tume iliyochunguza na kutoa matokeo kuhusu mchanga (makinikia) unaosafirishwa nje ya nchi.



“Kuanzia  sasa uchakataji (processing) ufanyike hapa nchini na mikataba yote iwe na kipengele kinachoyalazimisha makampuni yanayopewa leseni ya kuchimba madini kuwa na mitambo ya kuchenjua makinikia ya madini yanayozalishwa na migodi hiyo.” alisema  Jilili.



Akifafanua zaidi Jilili amesema kuwa mikataba yote ya Madini ni vyema ikatazamwa upya na kuzingatia maslahi mapana ya Taifa na si ya watu wachache, kwani kwa kufanya hivyo kuonyesha dhamira ya dhati ya Serikali katika kuleta mageuzi katika sekta ya madini nchini.



Katika mapendekezo yao DARUSO imebainisha kuwa Watanzania wangependa kuona Mikataba na Sheria zilizopo zinaruhusu ukaguzi wa mara kwa mara migodini ili Serikali ijiridhishe kuhusu kiwango cha madini kinachozalishwa katika migodi hiyo pamoja na Serikali kuwa na ubia wa asilimia 50 au 49 na wawekezaji katika sekta ya madini.



Aidha Jilili alisema vyema pia kwa vyema kwa Viongozi wote waliopewa dhamana ya kuwaletea wananchi maendeleo wakatekeleza wajibu huo kwa uzalendo na kuepuka kuingia mikataba inayowezesha kuiletea hasara Serikali.



“Tunapenda kuwaomba watanzania wote wasomi na wasio wasomi kumsaidia Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kufikia lengo lake la kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi na hayo yanawezekana tu kwa kuweka uzalendo mbele na maslahi ya Taifa kwanza.” Alisisitiza Jilili

Aliongeza kuwa nidhamu na uwajibikaji katika sehemu za kazi ni jambo la muhimu kwa Watendaji waliokabidhiwa majukumu ya kusimamia sekta mbalimbali kwani kwa kufanya hivyo  kutawezesha kuzaliwa kwa Tanzania mpya chini ya Uongozi wa Serikali ya awamu ya Tano.



“DARUSO inamthibitishia Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Watanzania wote kuwa iko sambamba nae katika harakati zake za kuikomboa nchi yetu katika Nyanja zote ikemo kiuchumi” Alisisitiza Jilili

Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) akitoa tamko lao mbele ya waandishi wa Habari kuhusu kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya Tano katika kuhakikisha kuwa watanzania wananufaika na rasilimali za madini.kushoto ni Waziri Mkuu wa Serikali hiyo Bw. Sintau Fredrick.

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU FUTARI YA PAMOJA NA VYAKULA VYA KUPIKA MWEZI HUU WA RAMADHANI KUFUATIA KUREJEA MARADHI YA KIPINDUPINDU

$
0
0
​Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepiga marufuku utaratibu wa kufutarishana na kupeana chakula kilichotayarishwa nyumba moja kwenda nyengine katika mwezi huu wa Ramadhani baada ya kubainika kuwepo kwa mripuko wa maradhi ya Kipindupindu katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Wizara ya Afya Mnazimmoja, Kaimu Waziri wa Wizara hiyo Riziki Pembe Juma alisema lengo la Serikali kuweka marufuku hiyo ni kujaribu kudhibiti maradhi hayo yasisambae zaidi.

Alizitaja hatua nyengine ambazo Serikali imechukua ni kuzuia uuzwaji holela wa vyakula vya kupika na vya majimaji katika maeneo yasiyorasmi na kuwashauri wananchi kuchemsha maji ya kunywa ama kuyatia dawa ya klorini, kukosha vizuri matunda na mboga za majani kwa maji yaliyochemshwa.

Alisema uchunguzi uliofanywa kwa wagonjwa waliolazwa kwa sababu  ya  kuharisha na kutapika katika vituo vya afya na hospitali mbali mbali umebainisha kuwepo ugonjwa wa kipindupindu aina ya Ogawa 01.

Waziri Riziki ameweka wazi kupokewa wagonjwa 23 waliopatikana na vimelea vya ugonjwa wa kipindupindu na tayari Wizara ya afya imefungua kambi maalum ya matibabu katika eneo la Chumbuni.

Aliyataja maeneo yaliyoathirika zaidi na ugonjwa huo ni Wilaya za Mjini na Magharibi hasa katika Shehia ya Kinuni, Darajabovu, Mtoni Kidatu, Chumbuni, Mwanakwerekwe, Fuoni na Kwarara.

Hata hivyo Kaimu Waziri wa Afya amethibitisha kuwa hadi sasa hajapatikana mgonjwa kutoka kwenye maeneo ya ukanda wa pwani na zile kanda za utalii au kwenye hoteli za kitalii na Kisiwa cha Pemba.

Amewaomba wananchi kuimarisha usafi katika maeneo wanayoishi na watakaona dalili za ugonjwa huo wakimbilie vituo vya afya huku Serikali imejipanga kwa dawa na wafanyakazi na kutoa elimu ya afya katika kukabiliana na maradhi hayo .

Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dkt. Fadhil Abdalla amewasisitiza wafanyabiashara wadogo wadogo kufuata taratibu zilizowekwa na Wizara ikiwemo kupima afya kabla ya kuanza biashara na kuandaa mazingira mazuri ya sehemu watakazofanyia biashara zao.
Kaimu Waziri wa Afya Riziki Pembe Juma akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mripuko wa maradhi ya kipindupindu Zanzibar huko Makao Makuu ya Wizara ya afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Fadhil Mohd Abdalla akijibu masuala  yaliyoulizwa na waandishi wa habari katika mkutano huo.
Picha na Makame Mshenga.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali vya Serikali na binafsi wakimsikiliza Kaimu Waziri wa Afya Zanzibar katika mkutano uliofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.

WCF yatoa elimu kwa waajiri nchi

$
0
0
Na Benjamin Sawe.
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), umeendesha semina ya siku moja kwa waajiri nchini ili kutoa elimu juu ya shughuli za Mfuko na wajibu wa waajiri kwa wafanyakazi wao katika kujisajili na kuwalipa michango kwa niaba ya waajiriwa wao.

Akizungumza katika semina hiyo Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko huo Radhimana Mbilinyi amesema kuanzishwa kwa mfuko huo kumekuja wakati muafaka ambapo Tanzania inaelekea katika uchumi wa viwanda hivyo kupelekea ongezeko la wafanyakazi ambapo chombo hicho ndio mkombozi wa majanga yatokanayo na kazi.                


“Ni muda muafaka kwa waajiri kutambua wajibu wenu katika Mfuko huu na pia kutambua madhara ya kutotekeleza wajibu wenu” Alisema Radhimina Mbilinyi.


Katika hotuba yake, Bi Mbilinyi alieleza umuhimu wa waajiri kuwalipia michango wafanyakazi wake kama sheria inavyotaka, ili kuwawekea akiba pindi wapatapo na majanga wakiwa kazini.


Akizungumza wakati akitoa mada Afisa Matekelezo Bi. Amina Likungwala amesema, Mfuko umeamua kuandaa semina hiyo ili kutoa elimu zaidi kwa waajiri  kwa kutambua kuwa waajiri ndio wadau wakuu wa Mfuko huo na semina hiyo itawasaidia kujua kazi za Mfuko lakini pia wajibu wa waajiri kwa wafanyakazi katika kutoa michango ya kila mwezi.


Nae,  Afisa Madai wa Mfuko huo, Bi Grace Tarimo alisema Mfuko huo upo kisheria ili kutoa fidia kwa wafanyakazi watakaoumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi.


Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi ni Taasisi ya Serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na umeundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi Sura ya 263 iliyorejewa Desemba, Mwaka 2015.
 Makamu Mwenyekiti  kutoka Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi  (WCF)  Radhimina Mbilinyi akifungua Semina ya uelimishaji kwa Waajiri kuhusu haki na wajibu wa mwajiri na mfanyakazi jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya washiriki wa semina ya uelimishaji kwa waajiri wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi wa semina hiyo ambaye ni Makamu Mwenyekiti  wa Bodi ya  Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)  Bi. Radhimina Mbilinyi jijini Dar es Salaam leo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MEJA JENERALI (MSTAAFU) KIJUU: CHANGAMKIENI MIKOPO YA BENKI YA KILIMO

$
0
0
Na Mwandishi wetu, Bukoba
Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (Mstaafu) Salum Kijuu amewaasa wakulima na wafugaji wa mkoa wa Kagera kuchangamkia fursa za mikopo inayotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kujikwamua katika shughuli zao za kilimo mkoani humo.
Meja Jenerali (Mstaafu) Kijuu alitoa wito huo alipotembelea Banda la TADB wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Maziwa inayofanyika kitaifa mkoani Kagera.
Mkuu wa mkoa huyo alisema kwa kuzingatia malengo ya uanzishwaji wa Benki ya Kilimo unalenga kutimiza dhamira ya Serikali ya kuwasaidia wakulima nchini kote kukabiliana na mapungufu kwenye kuongeza tija katika shughuli zao za kilimo.
“Nawaomba wakulima na wafugaji wa Kagera kuchangamkia mikopo nafuu ya Benki yetu ya Kilimo ili muongeze tija katika kilimo chenu maana Benki ipo kwa ajili ya kuhuisha upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo na kuchagiza mapinduzi katika  kilimo nchini,” Meja Jenerali (Mstaafu) Kijuu alisihi.
Kwa mujibu wa TADB, sekta za kilimo na mifugo ni sekta za kipaumbele ambazo zinazopatiwa mikopo kwa ajili ya uongezaji wa thamani mazao na mifugo hasa katika uongezaji wa thamani wa sekta hizo nchini.
Benki hiyo inatoa mikopo ya aina tatu ambayo ni Mikopo ya Muda Mfupi (Hadi Miaka Miwili (2)), Mikopo ya Muda wa Kati (Zaidi ya Miaka 2 hadi Miaka Mitano (5)) na Mikopo ya Muda Mrefu (Zaidi ya Miaka 5 hadi Miaka Kumi na Mitano (15)).
TADB ni taasisi ya serikali ambayo ilianzishwa kwa ajili ya kutatua ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini ambao ulikuwa unachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa; riba kubwa kwenye mikopo ya kilimo; mikopo ya muda mfupi; masharti magumu ya kukopa bila kuzingatia hali halisi ya sekta ya kilimo  na mazao ambayo inaathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa.
 Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (Mstaafu) Salum Kijuu (aliyevaa Kaunda suti) akiwasili katika Viwanja vya Kyaikarabwa kutembelea na kukagua shughuli zinazoendelea wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Maziwa inayofanyika kitaifa mkoani Kagera.
 Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (Mstaafu) Salum Kijuu (aliyeshika kipaza sauti kulia) akizungumza wakati alipotembelea Banda la TADB. Anayemsikiliza kushoto ni Afisa Mahusiano na Masoko Mkuu wa TABD, Bw. Saidi Mkabakuli.
Afisa Mahusiano na Masoko Mkuu wa TABD, Bw. Saidi Mkabakuli akisisitiza jambo wakati Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (Mstaafu) Salum Kijuu (hayupo pichani) alipotembelea Banda la TADB.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110090 articles
Browse latest View live




Latest Images