Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1713 | 1714 | (Page 1715) | 1716 | 1717 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Baada ya kufanya mkutano mkubwa sana Sheikh Shariff Majini ameongeza siku tatu za kusikiliza shida za wakaazi wa Arusha ili afanye dua kwa ajili yao.
  Maamuzi ya kukaa siku tatu zaidi Jijini Arusha yametokana na  maombi ya wakazi wa Arusha waliojitokeza kwa wingi katika mkutano wake uliofanyika katika ukumbi wa C.C.M Mkoa wa Arusha.
  Kwa wakaazi wa Arusha wamtafute Sheikh kwa namba 0715-581552 watapewa utaratibu wa wapi Sheikh anapopatikana. 
  Baada ya kumaliza mkoa wa  Arusha, Sheikh Shariff anatarajia kuendelea kufanya mkutano mwingine Mkoa wa Tanga katika ukumbi wa C.C.M Mkoa Jumamosi tarehe 10 Juni na Jumapili tarehe11 Juni.
  Wabillahi Tawfiq.
   Baadhi ya wakazi waliojitokeza kwenye mkutano wa sheikh Shariff katika ukumbi wa C.C.M Mkoa wa Arusha
  Sheikh shariff Majini akiongoza mkutano huo jijini Arusha
   Baadhi ya wakazi waliojitokeza kwenye mkutano wa sheikh jijini Arusha
  Sheikh shariff Majini akiongoza mkutano huo jijini Arusha

  0 0

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harisson Mwakyembe akikagua timu za Sekondary zilizoshiriki michuano ya Copa/UMISSETA Dar es Salam mwishoni mwa wiki. Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harisson Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa timu za Sekondari zilizoshiriki michuano ya Copa/UMISSETA Dar es Salam mwishoni mwa wiki.
  Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa kampuni ya Coca-Cola Bw. Eric Ongara akiongea machache wakati wa ufunguzi wa michezo ya Copa/UMISSETA ambayo inashirikisha shule za Sekondari za Serikali na Binafsi mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harisson Mwakyembe akifungua michezo ya Copa/UMISSETA ambayo inashirikisha shule za Sekondari za Serikali na Binafsi mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0

  Na Lydia Churi, Songea
  Katika ziara hiyo Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mheshimiwa Ferdinand Wambali amesema Mahakama itashirikiana na wadau wake ili kuhakikisha kesi zinamalizika kwa haraka kwenye mahakama mbalimbali nchini. 
  Amesema kupitia nguzo ya tatu ya Mpango Mkakati wa miaka mitano wa mahakama ya Tanzania ambayo inasisitiza kujenga imani ya wananchi kwa Mahakama na ushirikishwaji wa wadau katika shughuli za mahakama, Mahakama itatoa elimu kwa wananchi pamoja na viongozi wakiwemo wakuu wa wilaya juu ya masuala mbalimbali yanayohusu utoaji wa haki kwa wananchi. 
   Jaji Kiongozi amesema Mahakama imejiwekea mikakati ya kuhakikisha kesi zinamalizika kwa wakati na kwa haraka ukiwemo mkakati wa kesi kutokukaa kwa zaidi ya miaka 2 kwenye Mahakama Kuu, miezi 12 Mahakama za mikoa na Wilaya pamoja na miezi sita kwenye Mahakam za Mwanzo. Mikakati mingine ni ile ya kesi kusikilizwa kwa mfululizo na kuwekwa kwa maahirisho mafupi mafupi ya kesi kwenye Mahakama mbalimbali nchini na Majaji na Mahakimu kupangiwa idadi ya kesi watazosikiliza katika kipindi cha mwaka moja. 
  Aidha, kila Jaji amepangiwa kusikiliza na kumaliza kesi 220 kwa mwaka ambapo Mahakimu wamepangiwa kumaliza kesi 250 kwa mwaka. 
  Akizungumzia Maadili kwa watumishi wa Mahakama, Jaji Wambali amewataka watumishi hao kuwahudumia wananchi wanaofika mahakamani kwa bidii, uaminifu, na uadilifu ili kujenga imani ya wananchi kwa Mahakama. 

  Amesema watumishi wa Mahakama hawana budi kufanya kazi kwa upendo na ushirikiano kwa kuwa kazi za mahakama zinategemeana ambapo kila kada ina umuhimu wake katika wananchi kufikia haki zao za msingi.
   Jaji Kiongozi yuko kwenye ziara katika kanda za Songea na Mtwara kwa ajili ya kukagua shughuli za kimahakama pamoja na kusisistiza utekelezaji wa Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania. Tayari ametembelea mahakama zilizoko Songea mjini na zile za wilaya za Mbinga, Nyasa, Namtumbo, na Tunduru.

   Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Ruvuma (Hawapo Pichani) wakati alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Binilith Mahenge ofisini kwake akiwa katika ziara ya kukagua shughuli za Mahakama na Kusisitiza Utekelezaji wa Mpango Mkakatiwa Miaka Mitano wa Mahakama ya Tanzania katika Kanda ya Songea. 
   Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Binilith Mahenge akizungumza
   Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali akizungumza na Watumishi wa Mahakama Kuu kanda ya Songea (Hawapo Pichani) akiwa katika ziara ya kukagua shughuli za Mahakama na Kusisitiza Utekelezaji wa Mpango Mkakatiwa Miaka Mitano wa Mahakama ya Tanzania katika Kanda ya Songea. 
  Mtendaji wa Mahakama, Samson Mashalla akifafanua masuala mbalimbali yanayohusu Utumishi kwa Watumishi wa Mahakama Kuu kanda ya Songea (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Jaji Kiongozi kwenye kanda hiyo. 

  0 0

  Serikali inafikiria kuunganisha taasisi zote zinazohusika na sekta ya uhifadhi wa wanyamapori nchini kuwa chombo kimoja chenye nguvu  kwa lengo la kupunguza gharama za uendeshaji wa taasisi hizo pamoja na kuongeza ufanisi wa kiutendaji katika sekta hiyo muhimu hapa nchini.
  Akizungumza mwishoni mwa wiki bungeni mjini Dodoma wakati akihitimisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe alisema anaunga mkono ushauri uliotolewa na wabunge mbalimbali ukiwemo wa Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Atashasta Nditiye juu ya umuhimu wa kuunganisha taasisi hizo za uhifadhi.
  "Wakati umefika sasa, tusiwe na makampuni (taasisi) zaidi ya manne ndani ya sekta hii ya wanyamapori, tuwe na kampuni (taasisi) moja tu ambayo itapunguza gharama katika uendeshaji, tutaunganisha jeshi la wahifadhi na jeshi hilo tutakalolitengeneza ni jeshi moja tu ambalo litakua na malezi chini ya jeshi la wananchi wa Tanzania, ili kujenga nidhamu, kuheshimu haki za binadamu na kufanya kazi kwa mujibu wa maslahi ya taifa,". alisema Maghembe. 
  Aliongeza kusema "Jeshi hilo ambalo tunaliandaa kisasa, jeshi usu litakua na "chain ya comand" moja na litawajibika kijeshi kwa makosa ya haki za kibinadamu na usaliti wa taifa au usaliti wa uchumi wa nchi yetu".

   Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akijibu hoja mbalimbali wakati akihitimisha mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka 2017/2018 bungeni mjini Dodoma.
   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo makani akijibu hoja mbalimbali wakati wa kuhitimisha mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka 2017/2018 bungeni mjini Dodoma.
  Picha ya pamoja ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe, Viongozi wakuu na baadhi ya watumishi wa Wizara hiyo wakiwa nje ya lango la Bunge mara baada ya kikao cha Bunge kupitisha bajeti ya Wizara hiyo.
  Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0  Familia ya Marehemu Mh. Samuel Sitta inawatangazia ndugu, jamaa, majirani na marafiki kuwa imepata pigo la kuondokewa na Mdogo wa Marehemu Mhe. Samuel Sitta, ambaye alikuwa Meya wa mji mdogo wa Urambo Ndg. Peter Sitta.
  Marehemu Peter Sitta amefariki dunia usiku wa kuamkia Jumamos  katika hospital ya Hindu Mandal jijini Dar es salaam. Msiba upo Masaki nyumbani kwa Hayati Samuel Sitta Mtaa wa Twiga Karibu na Makao makuu ya UNHCR jijini Dar es salaam.

  Bwana ametoa, 
  Bwana ametwaa.
   Jina lake na lihimidiwe.
  AMEN

  0 0

  Semina ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kuhusu VVU na Ukwimu iliyoandaliwa na Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania TACAIDS,mjini Dodoma.

  Miongoni mwa masuala yaliyozungumzwa katika semina hiyo ni changamoto mbalimbali zinazoikabili Tanzania katika mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi.

  Changamoto hizo ni pamoja na Sheria ya Magereza, adhabu ndogo kwa wanaoambukiza watu wengine VVU kwa makusudi zilizoanishwa katika Sheria ya Ukimwi, mila na desturi zilizopitwa na wakati (ukiwamo ukeketaji) na unyanyasaji wa kijinsia.

  Mzungumzaji mkuu katika semina alikuwa ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania TACAIDS,  Elizabeth Kaganda. 
   Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania TACAIDS,  Elizabeth Kaganda akitoa elimu ya sheria ya maambukizi ya ukimwi wakati wa semina ya wahariri wa vyombo  vya habari na waandishi wa habari kuhusu VVU na Ukwimu iliyoandaliwa na Tacaids mjini Dodoma.
    Mkutumbi (LIBRARIAN) Bwana Elisha Mngale kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania TACAIDS, akifafanua tafiti za maambukizi ya Ukimwi zinazofanywa na Tume hiyo.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  · Wateja wa mtandao wa simu Zantel sasa kufurahia mawasiliano na ndugu jamaa na marafiki waliopo mashariki ya kati kwa bei nafuu kwa kutumia kifurushi cha kimataifa cha uarabuni.

  Kampuni ya simu ya Zantel inaendelea kutimiza ahadi yake ya kuongeza thamani katika maisha ya wateja wao na sasa kutangaza ofa maalum inayowalenga waumini wa dini ya Kiislamu nchini ili kuadhimisha mwezi mtukufu wa mfungo wa Ramadhani duniani kote.

  Akitangaza habari hii makao makuu ya kampuni ya Zantel yaliyopo Msasani jijini Dar es salaam Mkurugenzi mkuu wa Zantel Bw. Benoit Janin amesema “Ramadhani ni muda muafaka wa kujenga mahusiano mazuri na ndugu, jamaa na marafiki na ofa hii ni ishara ya Zantel kuwasaidia wateja wake kuweza kuungana na kuwasiliana kwa urahisi zaidi na wapendwa wao”.

  Aliongeza kwa kusema mtandao wa Zantel utaendelea kutoa huduma kwa mamilioni ya Watanzania kuwasaidia kutimiza malengo na ndoto zao kupitia vipengele mbali mbali vya huduma za kampuni hiyo ikiwa ni pamoja bidhaa na huduma za upigaji simu, vifurushi vya internet na mtandao.

  Alisema kampuni itahakikisha vyote hivi kwa kutoa huduma na bidhaa bora za upigaji simu na vifurushi vya intaneti huku tukihakikisha tunawekeza faida endelevu. Kwa mwaka 2016 kulikua na matatizo mbali mbali ila kwa sasa mkakati wetu ni kuhakikisha tunatoa vipao mbele kwa vitu vyenye umuhimu mkubwa kwa wateja ikiwemo kuwa mtandao bora unaotoa intaneti ya kasi zaidi wa 4G, kupenya na kuwafikia watumiaji wengi zaidi,na kujiandaa kwa siku zijazo kuwa kampuni ya bidhaa inayopendwa zaidi.

  “Tunahitaji kuwa tayari kwa siku zijazo kwa njia mbali mbali za kuongeza mapato pamoja na huduma zinazoongeza thamani ya mtandao wa zantel ikiwemo uboreshaji wa vifurushi vya intaneti, tayari tunaona mabadiliko makubwa katika mtandao wetu” aliongezea kwa kusema “Kutakua na bidhaa mbali mbali tutakazozitoa kipindi hiki zitakazofurahiwa na wateja wetu kukiwa na mpangilio wa ofa zilizoanza tarehe 24/05/2017” Aliongezea.

  Akielezea zaidi kuhusu ofa hii, Mkurugenzi wa masoko wa Zantel Bw. Gasper Mbowa amesema”Ofa hii ya Ramadhani imelenga kuwazawadia wateja wetu wa malipo ya kabla watakaojiunga na vifurushi vyetu kwa kiasi chochote au kwa kuongeza muda wa maongezi kwenye kipindi cha mfungo wa Ramadhani. Mteja yoyote atakayeongeza mda wa maongezi atapata asilimia 50 ya muda wa maongezi moja kwa moja utakaomuwezesha kupiga simu Zantel kwenda Zantel, ofa hii itakua inatumika kuanzia saa 5 usiku hadi saa 12 asubuhi.

  Vivyo hivyo wateja wataweza kutumia huduma zetu zilizozinduliwa hivi karibuni kama ‘Zantel madrassa itakayowawezesha kujifunza dini ya kiislamu kwa kupokea mafunzo ya Quran, hadith, dua, habari za BAKWATA na huduma nyingine nyingi kwa kupitia simu zao za mkononi kupitia ujumbe mfupi wa maneno au kwa kupiga simu.

  Mbowa aliongezea kuwa wateja wa Zantel wanaweza kuwapigia simu ndugu, jamaa na marafiki waliopo mashariki ya kati kwa bei nafuu zaidi kupitia kifurushi cha kimataifa cha uarabuni. “Kwa shilingi za kitanzania 2,000 wateja watapata dakika 4 za kupiga simu Qatar, Oman, UAE, Lebanon, Pakistan, Yemen & Saudi Arabia, na kwa shilingi 5,000 watapata dakika 7 kupiga simu kwenda kwenye nchi tajwa, na fedha hizo zitakatwa moja kwa moja kwenye akaunti zao”

  Vifurushi vyote hivi vitapatikana kwa kujiunga kwa kupiga *149*15# na kwa vifurushi vya ‘Bonga Mpakabasi’, ‘Zantel Madrassa’ wateja wataweza kujiunga kwa kutuma ujumbe wa maneno kwa kutumia neno SUB na kutuma kwenda namba 15586 au kwa kupiga namba 15586

  0 0

  Mgeni Rasmi Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Ndg Rodrick Mpogolo akizungumza na Wahitimu Makada wa CCM Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM katika Sherehe za Mahafali ya kuwaaga Makada wa CCM idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu uvccm Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa King Solomon Kinondoni jana.

  Kaimu Mwenyekiti wa Idara ya Vyuo na Vyuo vikuu UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam Asha Ferouz akikabidhiwa Cheti cha pongezi na Mgeni Rasmi ndg:Rodrick Mpogolo katika Sherehe za Mahafali ya kuwaaga Makada wa CCM idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu uvccm Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa King Solomon Kinondoni jana.

  Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akizungumza katika Sherehe za Mahafali ya kuwaaga Makada wa CCM idara ya Vyuo na
  Vyuo Vikuu uvccm Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa King Solomon Kinondoni jana


  Meza Kuu wakiburudika na nyimbo ya CCM uku wa kionesha Ishara Mshikamano na Umoja.

  Wahitimu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu Wakicheza uku wa kishikana Mikono ishara ya Umoja.


  0 0


  Na Sixmund J. Begashe 

  Serikali ya Uswisi imeamua kuinga mkoni Serikali ya Jamhuuri ya Muungano wa Tanzania katika mapambano dhidi ya Rushwa kwa kuziwezesha program tano kiasi cha Dola za kimarekani 100,000 ambazo ni takribani Shilingi milioni 220/= ili ziweze kutoa elimu kwa njia za burudani ya mapambano dhidi rushwa nchini.

  Akizungumza kabla ya kusaini mikataba ya program hizo, Balozi wa Uswisi hapa nchini Mh ARTHUR MATTLI amesema kuwa Tanzania kwa sasa inafanya vizuri zaidi katika mapambano dhidi ya rushwa ukilinganisha na nchi nyingi barani Afrika hivyo wameona ni vyema ikaungwa mkono katika mapambano haya.

  Balozi Mattli ameongeza kuwa hadi sasa takwimu zinaonesha kuwa katika nchi za Afrika mashariki Tanzania inaongoza katika mafanikio yanayotokana na mapambano dhiri ya rushwa hivyo serikali yake imeona nivyema ikaunga mkono jitihada hizi kwa kuziwezeshwa program zitakazo toa elimu juu ya madhara ya rushwa kwa kupitia sanaa ili watanzania waweze kuipokea nakuielewa elimu hiyo kwa urahisi zaidi.

  Akizungumza baada ya kusaini makubaliano ya kupokea fedha za kuendesha programa ya Museum Art Explosion, kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Bw Saimon Maliti pamoja na kuishukuru Serikali ya Uswizi kwa kutambua jitihada za Makumbusho ya Taifa katika kuelimisha jamii juu ya mambo yanayo wahusu, amemwakikishia Balozi huyo kuwa fedha walizo pata zitatumika kama zilivyo kusudiwa na si vinginevyo.

  Nae Mkurugenzi wa Elimu kwa Jamii wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) Bw EKWABI MUJUNGU ameishukuru Serikali ya Uswizi kwa kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ya Rushwa na kuahidi kufanya kazi kwa karibu na Taasisi zilizo wezeshwa na Ubalozi huo ili kuhakikisha malengo yaliyokusudia ya kupambana na rushwa yanafanikiwa.

  Taasisi zilizo wezeshwa ni pamoja Makumbusho ya Taifa kupitia Program ya MUSEUM ART EXPLOSION AGAINST CORRUPTION, Tanzania House of Talent (THT), Kijiji Studii Tanzania, Goba Africa LTD na Art in Tanzania.
   Katikati ni Balozi wa Uswisi nchini mh ARTHUR MATTLI akizungumza na viongozi wa program zilizowezeshwa na Ubalozi huo katika mapambano dhidi ya rushwa nchini.


   Balozi wa Uswisi nchini mh ARTHUR MATTLI akizungumza na viongozi wa program zilizowezeshwa na Ubalozi huo katika mapambano dhidi ya rushwa nchini.

   Katikati ni Balozi wa Uswisi nchini Mh ARTHUR MATTLI  na kulia ni Mkurugenzi wa Mkumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Achiles Bufure wakishuhudia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Bw Saimon Maliti akitia sahii makubaliano ya fedha za kuendeshea program ya Museum Art Explosion kwa mapambano dhidi ya rushwa  Kulia ni Mkurugenzi wa Elimuli kwa Jamii wa TAKUKURU Bw Ekwabi Mujungu na Muanzilishi wa THT Bw Ruge Mutahaba wakimsikiliza kwa Makini Balozi wa Uswisi nchini Mh  ARTHUR MATTLI(ayupo pichani)  . 

  0 0

  Wanafunzi wa kike kutoka shule mbalimbali Jijini Mwanza wameiomba serikali kusaidia ujenzi wa viwanda vya pedi za kisasa vitakavyosaidia pedi hizo kuuzwa kwa beo nafuu.

  Hayo yamesemwa kwenye risala yao iliyosomwa na mwanafunzi Edna Ignas kutoka shule ya msingi Malulu, kwenye maadhimisho ya Siku ya hedhi duniani yaliyofanyika jana katika uwanja wa mpira Nyamagana.

  Aidha wameomba ujenzi wa viwanda hivyo vya pedi uendani na kupunguza ama kuondoa kabisa kodi kwenye mauzo ya kodi hizo, hatua ambayo itasaidia kuuzwa kwa bei nafuu na hivyo kuwafikia wasichana wote hususani wanaotoka kwenye kaya zenye uwezo mdogo wa kiuchumi.

  Mkurugenzi wa Shirika la Tanzania Youth With New Hope in Life Organization (TAYONEHO) la Jijini Mwanza, Dkt.Iman Tinda, amesema suala la hedhi limekuwa na changamoto kubwa ikiwemo baadhi ya mabinti wanafunzi kukosa masomo wakati wa hedhi.

  Amesema mabinti hupoteza vipindi darasani kati ya siku mbili hadi saba kwa mwezi, siku 86 kwa mwaka na hivyo kuwa kikwazo kwao kimasomo ambapo ni vyema wadau wa elimu wakaungana pamoja ili kuvunja ukimya juu ya suala la hedhi na hivyo kuwasaidia mabinti kuondokana na changamoto wanazokumbana nazo katika kipindi hicho.
  Muuguzi Mkuu mkoani Mwanza Agness Hassan, akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Hedhi Duniani 2017, kimkoa Mwanza yakifanyika uwanja wa Nyamagana hii leo Mei 28,2017.
  Mkurugenzi wa Shirika la TAYONEHO, Dkt.Iman Tinda, akizungumza kwenye maadhimisho hayo
  Mwanafunzi Edna Ignas kutoka shule ya Msingi Malulu Jijini Mwanza, akisoma Risala kwa niaba ya wnafunzi wenzake kwenye maadhimisho hayo
  Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho hayo
  Tazama Video hapo chini

  0 0

  Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki (kulia) akibadilishana mkataba wa ushirikiano wa kuboresha sekta ya utumishi wa umma jimboni Puntland na Waziri wa Kazi,Vijana na Michezo wa Puntland Abdurahman Ahmed Abdulle, serikali kupitia Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Puntland itaendesha mafunzo hayo. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Puntland Mahmood Hamad.Hafla ilifanyika mwishoni mwa wiki (Picha zote na Ino Communications) 
  Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki (Kulia) na Waziri wa Kazi,Vijana na Michezo wa Puntland Abdurahman Ahmed Abdulle wakisaini mkataba wa Makubaliano ya ushirikiano wa kuboresha sekta ya utumishi wa umma jimboni Puntland ambapo serikali kupitia Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) itaendesha mafunzo hayo kwa kushiriakana na Chuo Kikuu cha Puntland. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Puntland Mahmood Hamad.
  Mashauri wa kisheria kutoka Puntland Burhan Adam Omar akijadili jambo kabla ya kutia saini makubaliano baina ya Tanzania na Jimbo la Puntland makubaliano ya ushirikiano wa kuboresha sekta ya utumishi wa umma jimboni Puntland ambapo serikali kupitia Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) itaendesha mafunzo hayo kwa kushiriakana na Chuo Kikuu cha Puntland. 
  Sehemu ya ujumbe wa Tanzania katika hafla hiyo.
  Picha ya pamoja , katikati ni Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki, wa Kwanza kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Puntland Mahmood Hamad, wa Pili Kushoto ni Waziri wa Kazi,Vijana na Michezo wa Puntland Abdurahman Ahmed Abdulle,Wanne kushoto ni Mkuu wa TPSC Dk. Henry Mambo na wa kwanza kulia ni Mustapha Said Shaba Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma ya Puntland.  0 0

  Na  Bashir   Yakub  
  Mikataba yote ya kimataifa huongozwa na wajibu wa aina mbili. Wajibu ulioandikwa(express obligation) na wajibu ambao haukuandikwa(implied obligation). 
  Wajibu ulioandikwa ni masharti yote ya mkataba yaliyo katika maandishi  ambayo wahusika husoma na kuridhia, wakati wajibu usioandikwa ni masharti ya mkataba ambayo hayakuandikwa katika mkataba lakini  yapo kwa asili au yapo kwa kuwa tayari yalishasemwa na sheria na hivyo si lazima kuyaandika katika mkataba. 
  Mathalan, mfanyakazi  wako wa duka hawezi kukuibia halafu akasema kwenye mkataba wangu wa ajira hakuna sharti la uaminifu. Laa hasha  uaminifu  ni sharti la asili "implied obligation" kwa hiyo liandikwe au lisiandikwe  bado lipo tu.Kwenye mikataba ya kimataifa kama ile ya kwetu na makampuni  ya madini masharti yafuatayo ni ya  asili na hayahitaji kuwa yameandikwa ili kuyatekeleza :

  1. Wajibu wa kuanika taarifa zote muhimu kuhusu  shughuli inayotekelezwa katika mkataba( Implied covenant to disclose all necessary information over the subject matter). 
  2. Wajibu wa kutekeleza na kutenda  kwa nia njema(Implied covenant to act in good faith and fair dealing). 
  3. Wajibu wa kila mhusika katika mkataba kuwa  mkweli . Hili huwa ni katazo la udanganyifu(Fraud). 
  Haya yawe yameandikwa kwenye mkataba au hayakuandikwa yakikiukwa tafsiri  yake ni kukiuka masharti ya mkataba.


  Matendo kama kulaghai kuhusu uzito wa madini yanayochukuliwa, kulaghai kuwa unachukua dhahabu huku ukijua unachukua zaidi ya dhahabu, kulaghai kuhusu bei , kutotoa taarifa sahihi za kipi unapata na kipi hupati,nk ni kukiuka wajibu  na masharti ya mkataba jambo ambalo  ni kinyume cha sheria. Na ikiwa wamekiuka mkataba kwa misingi hiyo  basi Tanzania inaweza kufanya yafuatayo. 

  0 0

  Kata ya Iponya Wilayani Mbogwe,mkoani Geita,imevuka lengo la uandikishaji watoto wenye umri chini ya miaka mitano kwa ajili ya kupatiwa vyeti vya kuzaliwa kwa zaidi ya watoto 900 sawa na 154.7%

  Kauli hiyo ilitolewa na mratibu wa zoezi la usajili wa watoto chini ya umri wa miaka mitano wa wilaya ya Mbogwe,Fredrick Chotamasege, alipokuwa akiwasilisha taarifa ya hali ya uandikishaji kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe aliyefanya ziara ya ufuatiliaji katika kata ya Iponya.

  “Kata ya Iponya imefanikiwa kuvuka lengo katika zoezi la uandikishaji watoto chini ya umri wa miaka mitano zoezi linaoendeshwa na wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA). Kata ya Iponya iliwekewa lengo la kuandikisha watoto 1,806 lakini hadi kufikia tarehe 16/05/2017 ilikuwa imeandikisha watoto 2,794” alisema Fredrick. Aliongeza kuwa usajili huo ni sawa na ongezeko la watoto 988 waliosajiliwa sawa na 54.7%.

  Pamoja na mafanikio makubwa ya zoezi hilo,zipo changamoto za mawasiliano ya mtandao wa Tigo unaotumika kutuma takwimu hizo. Aliongeza kuwa mtandao huo umekuwa ukitumia muda mrefu kutuma majina na hivyo kusababisha kuwa na takwimu tofauti kati ya zile zilizopo kwenye vitabu na zile za kwenye mtandao wa RITA.

  Haya yalielezwa wakati Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe Elias Kayandabila, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya zoezi la uandikishaji watoto wenye umri chini ya miaka mitano katika kata za Masumbwe na Iponya wilayani Mbogwe.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0
  0 0


  Usikose kutazama matangazo ya moja kwa moja ya kuapishwa kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro kutoka Ikulu Jijini Dar es Salaam. Matangazo haya yatarushwa hewani kuanzia saa 3:30 asubuhu hii kupitia TBC, AZAM TV na ITV. Pia yatapatikana kupitia tovuti rasmi ya Ikulu ambayo ni www.ikulu.go.tz(tembelea tovuti hiyo kupitia simu ya mkononi, computer, tablet ama kifaa chochote cha mtandao)

  0 0

  Mtaalam wa Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima Bw. David Plotner (kushoto) kutoka shirika la CDC Marekani akijadiliana na maafisa wa TEHAMA wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Munir Mdee (katikati) na Abdullah Othman (kulia) wakati wa mafunzo ya awali ya utafiti huo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima unatarajia kufanyika nchini mwezi Agosti, 2017.
  Afisa TEHAMA kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Munir Mdee akitoa mafunzo ya kutumia Dodoso kwa njia ya tablet kwa washiriki wa mafunzo ya Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima wakati wa mafunzo ya awali ya utafiti huo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima unatarajia kufanyika nchini mwezi Agosti, 2017.
  Mratibu wa Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima Bi. Hellen Hillary (kushoto) kwa upande wa Tanzania Bara akijadiliana na mratibu wa utafiti huo kwa upande wa Tanzania Zanziar Bi. Nuru Masoud (kulia) wakati wa mafunzo ya awali ya utafiti huo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima unatarajia kufanyika nchini mwezi Agosti, 2017.
  Meneja wa Takwimu za Jamii Bi. Sylvia Meku (katikati) akiwaelekeza washiriki wa mafunzo ya awali ya Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima Bw. Frank Mapendo (kushoto) na Jocelyne Rwehumbiza (kulia) wakati wa mafunzo ya awali ya utafiti huo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima unatarajia kufanyika nchini mwezi Agosti, 2017.
  Mwananchi kutoka kata ya Kijitonyama jijini Dar es Salaam akijibu maswali kutoka kwa Mtakwimu Bw. Stephen G. Cosmas wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakati wa majaribio ya Dodoso litakalotumika wakati wa Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima unaotarajia kufanyika nchini mwezi Agosti, 2017.
  Mtakwimu Bi. Hellen Mtove wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu akimhoji mwananchi kutoka kata ya Kijitonyama jijini Dar es Salaam wakati wa majaribio ya Dodoso litakalotumika wakati wa Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima unaotarajia kufanyika nchini mwezi Agosti, 2017.(PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)

  0 0

  Suala la uhaba wa vitabu vya masomo ya Sayansi, maabara pamoja na walimu wa masomo hayo limekuwa likisababisha baadhi ya wananfunzi kushindwa kumudu na hivyo kuyaepuka masomo hayo,licha ya serikali na wadau mbalimbali kuhamasisha wanafunzi kuchukua masomo hayo.

  Kutokana na hali hiyo Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel imetoa msaada wa Vitabu vya Masomo ya Sayansi vyenye thamani ya Shilingi Milioni Tatu katika Shule ya Sekondari Vianzi iliyopo  Mkuranga Mkoani Pwani ambayo ina zaidi ya wanafunzi 400 ikiwa na walimu watatu kwa masomo yote ya Sayansi (biolojia, fizikia, kemia na hesabu). Hatua hiyo ni mwendelezo wa Kampuni  hiyo kusaidia katika elimu shule mbalimbali hapa nchini ili kuinua kiwango cha elimu katika masomo ya Sayansi.

  Mkuu wa Shule ya Sekondari Vianzi Mwl. Ashura Manaki amesema kuwa shule yake imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa walimu, maabara za kutosha pamoja na vitabu hali ambayo imekuwa ikisababisha wanafunzi kukimbia masomo ya Sayansi.
  “Tunaishukuru sana Airtel kwa msaada huu wa vitabu ebu fikilia tuna upungufu wa walimu,sasa likija tatizo la ukosefu wa vitabu unadhani wanafunzi watayapenda masomo ya sayansi,lakini kwa sasa nina matumaini tutaweza kusonga mbele,”alisema Manaki.

  Kwa upande wa Meneja wa Huduma kwa Jamii kutoka Airtel Hawa Bayumi ameleeza kuwa licha ya Kampuni hiyo kujikita katika mambo mbalimbali ya Kijamii wameona umuhimu wa kuisaidia shule hiyo ambayo inachangamoto ya walimu wa sayansi lakini wakakuta hata vitabu navyo ni changamoto wakaamua kutoa msaadahuo.

  ”Licha ya Airtel kusaidia mambo mbalimbali ya kijamii tumeona kuna umuhimu mkubwa kuisaidia vitabu vya sayansi shule hii kutokana na kukabiliwa na changamoto ya uhaba wa walimu wa sayansi pamoja na vitabu vya sayansi tuna matumaini vitaweza kusaidia shule hii kujenga wataalamu wa sayansi hasa ukizingatia serikali inaweka juhudi kufikia Tanzania ya viwanda ni muhimu kuwekeza katika rasilimali watu na kujenga watanzania weny weledi. Lengo letu ni kuendelea kuwezesha vijana kufikia malengo yao kupitie elimu na ujasiriamali,”alisema Bayumi.

  Zamda Said ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo amesema kuwa shule hiyo bado ina mahitaji ya walimu wa sayansi lakini kwa kupatiwa vitabu hivyo vitasadia hata wanafunzi kuweza kujisomea huku akiwaasa wanafunzi kutumia fursa hiyo kufaulu masomo ya sayansi.

  “Ni kweli tatizo la uhaba wa walimu pamoja na ukosefu wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia ni changamoto kwa shule hii lakini nawaombeni wanafunzi kutumia fursa hii kuweza kujisomea maana vitabu gharama yake ni kubwa,”alisema Said.
  Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel, Bi Hawa Bayumi akimkabidhi vitabu vya sayansi, Maria Edward, mwanafunzi wa Shule ya sekondari ya Vianzi iliyopo Mkuranga wakati Airtel ilipotembelea shule hiyo kutoa msaada wa vitabu vya taaluma .
  Mkuu wa shule ya Shule ya sekondari ya Vianzi Ashura Manaki ( wa pili kulia ) kaifatiwa na pamoja na Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel, Bi Hawa Bayumi (wapili kushoto) na Meneja Mauzo wa Airtel Pwani, Philipi Nkupuma kwa pamoja wakionyesha vitabu vya sayansi mara baada ya Airtel kukabidhi vitabu hivyo kwa shule ya sekondari ya Vianzi pindi walipotembelea shuleni hapo.
  Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel, Bi Hawa Bayumi akimkabidhi vitabu vya sayansi mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Vianzi Bi Ashura Manaki wakati Airtel ilipotembelea shule hiyo kutoa msaada wa vitabu vya taaluma . akishuhusia ni Zamda Said ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule.

  0 0

  NA HAMZA TEMBA - WMU

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry kutumia fursa ya uwepo wa Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki, Tabora, BTI mkoani humo kwa kuandaa utaratibu maalum utakaowawezesha wananchi hususan wafugaji wa nyuki kuhudhuria mafunzo ya muda mfupi ya ufugaji wa nyuki chuoni hapo kwa ajili ya kuboresha uzalishaji wa bidhaa hiyo na kuwaongezea kipato.


  Waziri Maghembe ametoa kauli hiyo leo alipotembelea chuoni hapo wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tabora kwa ajili kujionea changamoto mbalimbali za uhifadhi na kuona namna kukabiliana nazo ikiwa ni ahadi aliyoitoa bungeni wakati akihitimisha mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya Wizara yake kwa mwaka huu wa fedha 2017/2018.


  “Mkuu wa Mkoa, tafadhali andaa utaratibu maalum kwa wananchi wako, wale wafugaji wa nyuki wanaweza kuja kwenye chuo chetu hapa hata siku tatu, hata siku mbili, wafundishwe namna bora ya kufuga nyuki, yani watoke kabisa huko Skonge, waletwe hapa, walale hapa sku moja au mbili wafundishwe baadae warudi makwao wajue namna bora ya kufuga na kuvuna asali,” alisema Maghembe.


  Kwa upande wake Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora alisema maelekezo hayo kwao ni faraja kwakuwa tayari kuna maelekezo ya kiserikali kusaidia makundi ya kinamama na vijana ikiwemo utoaji wa mikopo kwa vikundi vyao vya ujasiriamali.


   “Katika Mkoa wangu tuna makundi haya ya kinamama na vijana ambao tumetakiwa kuwasaidia kwa maana ya kutenga “percent” (asilimia) fulani katika “own source” (vyanzo vya ndani vya mapato), kwahiyo kwa maelekezo hayo hayo nitakachofanya mimi ni kuhakikisha kwamba tunaenda kuwaeleza katika hali ya kawaida kwamba tungeweza kuwapa mikopo lakini tungependa tuwape mikopo baada ya kupata taaluma na waweze kujua vizuri namna bora ya kufuga nyuki na kurina asali”, alisema Mwanri.


  Mkuu wa Chuo hicho, Semu Daudi alisema chuo hicho kina jumla ya wanafunzi 155 na kinatoa mafunzo ya Cheti na Diploma ya Ufugaji wa Nyuki.


  Naye Mkuu wa Kituo kidogo cha Utafiti wa Ufugaji Nyuki chuoni hapo, Humphrey Natali alisema kituo hicho kinakabiliwa na changamoto ya vitendea kazi ikiwemo usafiria ambapo gari lililokuwepo limepelekwa matengenezo na kompyuta zilizopo nazo ni za muda mrefu.  Waziri Maghembe ameahidi kukipatia kituo hicho gari moja huku akimuagiza, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo kuona uwezekano wa kumaliza changamoto mbalimbali chuoni hapo.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akizungumza na uongozi wa chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki, Tabora BTI alipotembelea chuoni hapo leo. Kulia ni Mkuu wa chuo hicho Semu Daudi na Mratibu Mkuu wa Mafunzo, Igunda John.
  Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry (kulia) na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe wakati akitoa maelekezo mbalimbali chuoni hapo.

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry baada ya kutembelea Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki, Tabora, BTI leo.

  0 0


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. John Pombe Magufuli, mapema leo asubuhi amemuapisha Mkuu mpya wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro aliyeteuliwa jana kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Ernest Mangu ambaye atapangiwa kazi nyingine.

older | 1 | .... | 1713 | 1714 | (Page 1715) | 1716 | 1717 | .... | 3283 | newer