Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

NAHODHA WA SIMBA JONAS MKUDE ANUSURIKA KIFO KATIKA AJALI YA GARI MKOANI MOROGORO LEO

0
0
NAHODHA wa Mabingwa wa kombe la Shirikisho na Kiungo wa timu hiyo, Jonas Mkude ni miongoni mwa watu waliojeruhiwa katika ajali ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo ilipotokea ajali hiyo, Dumila katika shamba la Mitiki, zinaarifu kuwa kuna watu wawili ambao bado majina yao hajapatikana wameumia na Mkude kupata majeraha madogo na kupelekwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu zaidi.

 Watu hao walikuwa katika gari aina ya Toyota VX lenye namba za Usajili T 834BLZ na walikuwa wakitokea Dodoma kushuhudia fainali za kombe la Shirikisho la Soka Tanzania uliopigwa jana katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma uliozikutanisha Simba na Mbao.

Simba ilishinda mchezo huo kwa bao 2-1 na kutwaa ubingwa huo na kujipatoia tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Barani Afrika. Chanzo: Daily News Blog


TADB YAASWA KUWAFIKIA WAKULIMA WADOGO NCHI NZIMA

0
0

Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa William Tate Ole Nasha (MB) (mwenye tai) akikaribishwa katika Banda la Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) mara baada ya kufungua Maadhimisho ya Kampeni ya Wiki ya Maziwa inayofanyika Kitaifa mjini Bukoba, mkoani Kagera kuanzia tarehe 28 Mei had Juni 01.

Wito umetolewa kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) kuwafikia wakulima, wafugaji na wavuvi wadogo nchi nzima ili kuweza kuwakwamua katika changamoto zinazorudisha nyuma juhudi zao za kujiongezea kipato kwa kukosa mitaji ya uhakika katika kuongeza tija ya kilimo nchini.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa William Tate Ole Nasha (MB) wakati akifungua rasmi Maadhimisho ya Kampeni ya Wiki ya Maziwa inayofanyika Kitaifa mjini Bukoba, mkoani Kagera.

Mhe. Ole Nasha amesema kuwa dhima ya kuanzishwa kwa TADB ni kutoa suluhisho la ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha na mikopo kwa wakulima wadogo nchini ili kuchagiza maendeleo ya kilimo nchini hivyo Benki ina wajibu wa kuwafikia wakulima wote wadogo wenye uhitaji wa mikopo.

“Nawaomba mujielekeze kutoka mikopo yenu ya gharama nafuu kwa wakulima wadogo ambao hawawezi kupata mikopo kwenye benki za biashara ili kutekeleza lengo la Serikali la kuwainua wakulima kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini,” Mhe. Ole Nasha alisema.

Aliongeza kuwa anafahamu kuwa Serikali ikishirikiana na TADB ilifanya mazungumzo na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na kupelekea Bodi ya Benki ya Maendeleo Afrika kutoa kibali cha kuipatia TADB fedha za kukopesha kwenye sekta ya kilimo, na kuitaka Benki hiyo kutumia fedha hizo kwa kuwapatia wakulima wadogo ambao ni wahitaji zaidi wa miko hiyo.

“Naomba muwakopeshe wakulima hizo fedha ya zaidi  Bilioni 200 ili kuwaongezea tija katika shughuli zao,” aliongeza.

Kwa mujibu wa mpango kazi wa TADB hadi kufikia miaka mitano ijayo itakuwa imefungua ofisi sita za kikanda zenye lengo la kuwahudumia wakulima wote nchini. Ambapo katika hatua za awali Benki hiyo inaendelea kuwajengea uwezo wakulima wa nchi nzima ili kuwaandaa kupata mikopo kutoka Benki hiyo.

Mpango kazi huo unaweka bayana malengo mengine yanayojumuisha utafutaji wa fedha toka vyanzo mbalimbali zenye gharama nafuu kwa minajili ya kuwakopesha Wakulima katika hatua zote za mnyororo wa ongezeko la thamani kwenye mazao ya Kilimo na kupanua wigo wa utaoji mikopo toka Minyororo Kumi na Minne (14) ya mwanzo na kuhusisha pia mazao mengine ya Kilimo na pia kuwaunganisha wakulima na masoko ya ndani na nje ya nchi.

TADB ni taasisi ya serikali ambayo ilianzishwa kwa ajili ya kutatua ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini ambao ulikuwa unachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa; riba kubwa kwenye mikopo ya kilimo; mikopo ya muda mfupi; masharti magumu ya kukopa bila kuzingatia hali halisi ya sekta ya kilimo  na mazao ambayo inaathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa.
Afisa Mahusiano na Masoko Mkuu wa TADB, Bw. Saidi Mkabakuli (kushoto) akizungumza wakati Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa William Tate Ole Nasha (MB) (mwenye tai) alipotembelea Banda la TADB.
Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa William Tate Ole Nasha (MB) (mwenye tai) akizungumza na maafisa wa TADB (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa Benki hiyo kuwafikia wakulima wote nchini.

TAMKO LA WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA)

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba, akiwa katika mkutano na waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli Jijini Dar Es Salaam leo, akizungumza kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo hufanyika kila mwaka Tarehe 5 Juni, ambapo Kitaifa mwaka huu yatafanyika Mkoani Mara kijijini Butiama kumuenzi Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambapo Pamoja na Mambo Mengine pia alikuwa Mwanahakati wa Mazingira. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Mkamu wa Rais Mwandisi Ngosi Mwihava.

EFM REDIO KUGAWA PESA KWA WASIKILIZAJI WAKE

0
0
Efm redio imezindua rasmi msimu wa tatu wa mchezo wa sakasaka. Mchezo huu huchezeshwa kila mwaka na mwaka huu utachezeshwa katika wilaya ya Temeke, Kigamboni, Ubungo, Ilala na Bagamoyo. Siku ya leo tarehe 28/05/2017 umezinduliwa rasmi katika kiwanja cha Sinza Tippi wilaya ya Ubungo.

Mchezo huu wa sakasaka huchezeshwa kwa kuficha vitu vyenye thamani ya pesa katika uwanja husika ambapo inampasa msikilizaji afatilie dondoo za kitu hicho pamoja na mahali ili ajue sehemu na aina ya kitu kilichofichwa na atakae kipata atakua mshindi wa pesa taslimu.

Mwaka huu washindi nane katika kila wilaya watajishindia pesa taslimu, ambapo mshindi wa kwanza ataondoka na kitita cha shillingi milioni moja akifuatiwa na washindi wa shilingi laki moja na elfu hamsini.
Sehemu ya washiriki wakitafuta vitu vilivyofichwa katika uwanja huo.
Washiriki wa mchezo wa Sakasaka wakisubiri kuhakikiwa vitu walivyoviokota kama ni sahihi.
Meneja matukio Efm redio Neema Mukurasi (wakwanza kulia) akiwa ameshikilia vitu vitatu vilivyo okotwa na mshiriki Mr. Denis Charles (wakwanza kushoto ) vyenye thamani ya shilingi Laki mbili wakiwa na Mtangazaji Denis Rupia (Chogo)
Meneja matukio, uhusiano na mawasiliano Neema Mukurasi akimkabidhi mmoja wa washiriki wa mchezo huo shilingi elfu 50 baada ya kuokota kitu chenye thamani hiyo.

Biko kutoa Milioni 20 jumatano hii, mwingine aibuka na 10M Arusha

0
0
BAHATI Nasibu ya Biko Ijue Nguvu ya Buku, sasa imezidi kuchanja mbuga baada ya kuongeza donge nono la washindi wa droo zao kubwa, ambapo sasa mshindi wa droo ya Jumatano hii anatarajiwa kunyakua jumla ya Sh Milioni 20.

Mbali na kutoa kiasi hicho cha pesa, tayari imempata mshindi wake wa droo ya tisa ya Jumapili ambaye ni Leopard Mpande wa jijini Arusha, aliyenyakua Sh Milioni 10 huku pia Biko ikiwa imeshapata washindi zaidi ya 35,000 wa papo kwa hapo. 

Akizungumza leo katika droo iliyompata Mpande, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage, alisema kwamba wameamua kuongeza zawadi ya droo kubwa ya jumatano hii kutoka Sh Milioni 10 hadi 20 ili kuwawesha washiriki nafasi ya kujikwamua kimaisha kwa zawadi za BIKO, "Changamkieni fursa hii" alisema.

Alisema droo ya kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 20 itafanyika Jumatano, huku akiwataka watu wacheze mara nyingi zaidi kwa kufanya miamala kwenye simu zao za MPESA, TIGOPESA na AIRTEL Money kwa kuingia kwenye kipengele cha lipa bili au lipa kwa MPESA ambapo watatakiwa waingize namba ya kampuni ambayo ni 505050 na kuweka pia namba ya kumbukumbu ambayo ni 2456.

Balozi wa Biko Tanzania Kajala Masanja kulia akizungumza jambo wakati wa kuchezesha droo ya tisa ambapo mkazi wa Arusha, Leopard Mpande aliibuka kidedea kwa kutangazwa mshindi hivyo atajinyakulia Sh Milioni 10 kutoka Biko. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo.

Kajala Masanja akizungumza na Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo.
Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo kushoto akiandika dondoo za mshindi wa Sh Milioni 10 wa Biko aliyetangazwa leo jijini Dar es Salaam, ambapo mkazi wa Arusha, Leopard Mpande aliibuka kidedea katika droo hiyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MGOGORO WA BWAWA LA UMWAGILIAJI LA ULUWA WAKARIBIA MWISHO

0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii
Prof. Jumanne Maghembe
Na Tiganya Vincent, Sikonge

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ameteua timu ya Maafisa watano  wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kwa ajili ya kuandaa taarifa (ripoti) itakayowasilishwa kwake Jumatano (wiki inayoanza kesho) ili imwezeshe kutoa maamuzi yatakaondoa kuondoa mgogoro uliosababisha ujenzi Mradi wa Bwawa la Umwagiliaji la Uluwa ushindwe kuendelea kwa sababu ya maji yake kuelekezwa katika Msitu wa Hifadhi  wa Ipembampazi.

Hatua hiyo itasaidia kuokoa zaidi ya shilingi milioni 313 ambazo hadi hivi sasa zimeshatumika katika ujenzi wa mradi huo ambao ni kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji wa mpunga katika vijiji viwili vya Mtakuja na Kiloleni kama mradi utaendelea.

Profesa Maghembe alichukua uamuzi huo jana wilayani Sikonge baada ya kutembelea Mradi huo huku akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri ili kujionea hatua ulipokuwa umefikia na hiyo mifereji ilijengwa kuelekea katika Msitu wa Hifadhi.

Alistaja wataalam hao kuwa ni Ofisa wa Maliasili, Misitu, Kilimo na Mhandisi wa Maji, Mhandishi wa Ujenzi kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Mteandaji wa Halmashauri ya Sikonge ambao aliwapa jukumu la kuandaa  taarifa itakayoonyesha mambo mbalimbali ikiwemo kupima na kuonyesha kiasi cha eneo ambalo wananchi wanalohitaji kwa ajili ya kilimo hicho na eneo lilobaki katika Msitu huo wa Hifadhi.

Profesa Maghembe aliwaambia  kuwa  uharaka na ubora wa  ripoti ya Halmashauri ndio utakaoisaidi Wizara ya Maliasili na Utalii kufikia maamuzi haraka ambayo baada ya wataalam wake kuipitia atawalisha mapendekezo na hatua waliofikia kwa Mkuu wa Mkoa  kwa ajili ya hatua zaidi.

Aliongeza kuwa wakati hatua za kupata eneo hilo zikiendelea ni vema uongozi wa  Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge ukaanza kujipanga kwa kuandika andiko la mradi wa kuomba fedha kutoka Wizara ya Maji ili kazi ya ujenzi huo ikamilike na ianze kuwanufaisha wananchi.

Aidha , Waziri huyo wa Maliasili na Utalii alitoa wito kwa wananchi wote watakaopata maeneo karibu na Hifadhi mbalimbali kuwa walinzi wa kwanza wa rasilimali hizo na kuwakemea wale wote watakaonekana kutaka kuzihujumu kwa faida binafsi.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri alisema kuwa sehemu kubwa ya ardhi ya Halmashauri ya Sikonge ni mistu ya hifadhi ambayo inafikia asilimia 95 na asilimia tano tu ndio inatumika kwa matumizi mengine ya binadamu ikiwemo kilimo.

Kufuatia hali hiyo aliwaasa viongozi wa Halmashauri hiyo kuwa makini wakati wanaendesha zoezi hilo la kuomba eneo hilo lenye ukubwa wa hekta 500 kwa kuangalia mahitaji yao halisi  ili isije ikatokea wameshapewa wanaanza tena kuomba nyongeza.

Aidha , Mkuu huyo wa Mkoa alimweleza Waziri Maghembe, Ofisi yake itatuma Wataalam wiwili waungane na wa Halmashauri kwa ajili ya kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa haraka na umakini ili wananchi waanze kufanikisha mradi huo.

Akisoma taarifa ya mradi huo Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Abel Busalama  alisema kuwa mradi huo uliogharimu hadi sasa milioni 313 .8  ambao ungevinufaisha vijiji vya Mtakuja na Kiloleni ulishindwa kuendelea baada mjenzi kujenga mifereji ya umwagiliaji akielekeza katika Msitu wa Hifadhi wa Ipembampazi jambo lililopelekea wananchi wa vijiji hivyo kuvamia msitu na kuanzisha mashamba ya mpunga na wengine kuingiza mifugo kwa ajili ya malisho.

Hivyo alimwomba Waziri huyo mwenye dhamana ya Maliasili na Utalii kutoa ruhusa ya eneo la hekta 500 katika Msitu wa Hifadhi ya Ipembampazi liweze kupima na kutumika kwa shughuli za kilimo cha umwagiliaji .
Ujenzi wa mradi huo ulifika hatua ya pili ambapo ilibaki hatua ya tatu ili uanze kutumika na ndipo ulisimamishwa.

NMB yatoa elimu ya kifedha kwa wanafunzi Shule ya Msingi Wailes

0
0
Ofisa wa Benki ya NMB Tawi la Temeke, Latifa Ayoub Dadah (kushoto) akimkabidhi mpira wa miguu mmoja wa viongozi wa michezo wa Shule ya Msingi Wailes kwa ajili ya shule hiyo. Mpira huo umetolewa na Benki ya NMB kama zawadi kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes mara baada ya elimu ya masuala ya fedha na akiba iliyotolewa na benki hiyo. Wa kwanza kusho to ni Mwalimu wa Taaluma wa Shule ya Msingi Wailes, Zabibu Wasia akishuhudia. Ofisa wa Benki ya NMB Tawi la Temeke, Latifa Ayoub Dadah (kushoto) akitoa elimu ya masuala ya kifedha na akiba kwa wazazi na wanafunzi walioshiriki mafunzo ya programu ya wajibu ya NMB katika Shule ya Msingi Wailes ya jijini Dar es Salaam. Mmoja wa wachezaji vijana (kulia) wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Azam kupitia kituo chao cha michezo akimkabidhi mpira wa pete mmoja wa viongozi wa michezo wa Shule ya Msingi Wailes kwa ajili ya shule hiyo. Mpira huo umetolewa na Benki ya NMB kama zawadi kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes mara baada ya elimu ya masuala ya fedha na akiba iliyotolewa na benki hiyo.
Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes akijibu swali kwenye mafunzo ya programu ya wajibu iliyotolewa na Benki ya NMB shuleni hapo.

BENKI ya NMB imetoa elimu ya masuala ya kibenki na umuhimu wa kujijengea utamaduni wa uwekaji akiba kwa wanafunzi na baadhi ya wazazi wa Shule ya Msingi Wailes iliyopo Temeke jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes walioshiriki mafunzo hayo ya kifedha, Ofisa wa Benki ya NMB Tawi la Temeke, Latifa Ayoub Dadah alisema NMB inaendelea kutoa elimu ya masuala ya kifedha ikiwa ni pamoja na kujifunza mbinu za kuweka akiba kwa ajili ya maisha ya baadae. 

Alisema elimu hiyo inatolewa kupitia Programu maalum ya Wajibu ambayo hutoa fursa kwa watoto, vijana na wazazi kujifunza masuala ya kifedha ili kumjengea mtoto utamaduni wa kujiwekea akiba, elimu ambayo watoto wengi hawapati fursa ya kujifunza. 

Tanzania yatumia Siku ya Afrika Saudi Arabia kutangaza utamaduni wake

0
0
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia akifurahia chakula cha asili ya Tanzania na mabalozi wa nchini nyingine katika maadhimisho ya Siku ya Afrika nchini hapa yaliyofanyika hivi karibuni.


Na Mwandishi Wetu, Riyadh

Balozi wa Tanzania UBALOZI wa Tanzania nchini Saudi Arabia, uliungana na ofisi nyingine za balozi za nchi mbalimbali kusherehekea Maadhimisho ya Siku ya Afrika yaliyofanyika hivi karibuni nchini Saudi Arabia.

Maadhimisho hayo yalikwenda sambamba na kutangaza utamaduni, ambapo kwa Tanzania, shamra shamra hizo zilikonga nyoyo za wahudhuriaji wengi, ambapo wanafunzi wa Tanzania wanaosoma nchini hapa waliimba nyimbo za kuisifu na kuipamba Tanzania.
Wanafunzi wa kitanzania baada ya kutumbuiza nyimbo za kuisifu Tanzania.

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, aliuambia Mtandao huu kuwa kusudio la kuungana na mabalozi wengine lilifanikiwa kwa sababu lengo halisi ni kuitangaza Afrika na nchi zao, ambapo anaamini kwa maadhimisho hayo nchi yake imepiga hatua kujitangaza kwa kuonyesha utamaduni wao kwa kupitia, ngoma, nyimbo, ngojera, maonesho ya mavazi na maonesho ya vyakula vya asili vya nchi zilizoshiriki,
Wakati wa Maakuli. Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia akiwa ameshika sahani ya chakula katika maadhimisho ya Siku ya Afrika ambapo vyakula vya asili, ngoma na utamaduni wa Tanzania ulionyeshwa katika tukio hilo.

Kwa Simu Toka London na Freddy Macha: Upupu ni Washawasha au Dawa?

WAZIRI CHARLES MWIJAGE AFUNGUA MAONYESHO YA TANO YA KIMATAIFA YA BIASHARA TANGA

0
0


Meneja Mkuu Idara ya Masoko kiwanda cha saruji cha  Rhino Tanga, William Malonza, akimuonyesha moja ya bidhaa zizalishwazo na kiwanda hicho, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage, wakati wa maonyesho ya tano ya Kimataifa ya biashara yanayofanyika  katika viwanja ya maonyesho Mwahako ambayo yamezishirikisha kampuni kutpka mataifa mbalimbali ya Barani Afrika na Asia.


Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage, akisalimiana na Afisa Masoko kiwanda cha saruji cha  Rhino Tanga, Carolina Hillary wakati alipotembelea banda la maonyesho ya tano ya Kimataifa yalifunguliwa leo jijini Tanga katika viwanja vya maonyesho Mwahako.

 Waziri wa viwanda na Biashara, Mhe. Chales Mwijage, akibadilishana mawazo na Meneja Mkuu Idara ya Masoko kiwanda cha Saruji cha Rhino Tanga, Bw. William Malonza wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika Tanga.
 Waziri wa Viwanda na Biashara, Chales Mwijaga akipata maelekezo ya namna mkonge unavyoweza kutengeneza dawa  pamoja na mafuta aina mbalimbali.
 Simba ni moja katika wanyama ambao wameletwa kwa ajili ya maonyesho hayo ya Tanga. Wapo katika banda la idara ya Wanyamapori.



BREAKING NYUZZZZ...: RAIS DKT. MAGUFULI AMTEUA KAMISHNA SIMON SIRRO KUWA MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI (IGP)

0
0
Inspekta Jenerali wa Polisi (Mteule) Simon Sirro

MAZISHI YA MAREHEMU MZEE HAMISI CHIFUPA MAKABURI YA KISUTU JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Kwa hisani ya Global TV

NHIF YASHIRIKI MAONYESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA KWA KUTOA ELIMU NA KUPIMA AFYA

0
0

 Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage kulia akiteta jambo na  Msimamizi wa Ofisi ya Mfuko wa Bima ya Taifa Mkoani Tanga (NHIF) Dinna Mlwilo kulia wakati alpolitembelea banda lao  wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya kimataifa ya tano yanayofanyika kwenye  viwanja vya Mwahako Jijini Tanga
 Msimamizi wa Ofisi ya Mfuko wa Bima ya Taifa Mkoani Tanga (NHIF) Dinna Mlwilo kushoto akitoa elimu ya umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ili kuweza kunufaika na huduma zinazo tolewa nao kwa wananchi walilitembelea banda lao  wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya kimataifa ya tano yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga
 Msimamizi wa Ofisi ya Mfuko wa Bima ya Taifa Mkoani Tanga (NHIF) Dinna Mlwilo kushoto akitoa elimu ya umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ili kuweza kunufaika na huduma zinazo tolewa nao kwa wananchi walilitembelea banda lao  wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya kimataifa ya tano yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga
 Wananchi wakipima presha kwenye banda hilo wakati wa ufunguzi wa maonyesho hayo
Afisa kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Sophia kushoto akisubiri kujeza fomu za wananchi ambao wanakwenda kupima uzito na afya kwenye Banda lao ambapo wanatoa elimu namna ya kujiunga na mfuko huo,kupima afya.habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha 

Zuriel Oduwole Presents The 2017 DUSUSU Award to An African First Lady on Education Development

0
0
Following the announcement earlier this week in Los Angeles of the 2017 recipient for the DUSUSU Award in the First Lady category, 14 year old Film Maker & Girl Education Advocate Zuriel Oduwole has traveled to Dakar - Senegal to present the Award to Her Excellency Mrs. Marieme Faye Sall. The Award recognizes the work and documented successes of African First ladies in their overall gender development initiatives, with an emphasis on Girls Education. According to the UN, Africa has one of the highest rates of out-of-school children in the word, with most of them being Girls.
These young Girls end up in early forced marriages, as young as 13 or 12 years old, because of the acceptance practices in their cultures. It is against this backdrop that the UN Secretary General established the International Day of the Girl in 2011, when Zuriel was just 9 years old. She started her Dream Up, Speak Up, Stand Up project in early 2013 at age 10 to encourage out of school Girls to Dream, and launched the DUSUSU Awards in 2014 to honor First Ladies making a difference..
So far, the First Ladies of Tanzania [2014], Kenya [2015], Namibia [2016] and now Senegal [2017] have proudly received these Awards. The Award is highly regarded and anticipated by the First Ladies, because it had no political affiliation, no multilateral agency affiliation, no government backing, but rather, the simple initiative by a Girl who recognizes the importance and influences First Ladies have, in tackling this 'stubborn' and 'burgeoning' global malady.
Because of this and many other initiatives she leads across the globe including meeting one-on-one with 24 world leaders, the US Secretary of State on January 6th 2017 - The Rt Hon John Kerry, honored Zuriel in Washington DC, calling her the Worlds Most Powerful Girl. She became the youngest person since the State Department was formed in 1789, to meet with a US Secretary of State in his office.
The search for the 2018 recipient has now begun.
 Film Maker & Girl Education Advocate Zuriel Oduwole has traveled to Dakar, Senegal,  to present the Award to Her Excellency Mrs. Marieme Faye Sall.
Film Maker & Girl Education Advocate Zuriel Oduwole presents the Award to Her Excellency Mrs. Marieme Faye Sall.
Her Excellency Mrs. Marieme Faye Sall with the DUSUSU Award in the First Lady category

NHIF YASHIRIKI MAONYESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA TANGA KWA KUTOA ELIMU NA KUPIMA AFYA

0
0
 Msimamizi wa Ofisi ya Mfuko wa Bima ya Taifa Mkoani Tanga (NHIF) Dinna Mlwilo kushoto akitoa elimu ya umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ili kuweza kunufaika na huduma zinazo tolewa nao kwa wananchi walilitembelea banda lao  wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya kimataifa ya tano yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga.
 Wananchi wakipima presha kwenye banda hilo wakati wa ufunguzi wa maonyesho hayo jijini Tanga.
Afisa kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Sophia kushoto akisubiri kujeza fomu za wananchi ambao wanakwenda kupima uzito na afya kwenye Banda lao ambapo wanatoa elimu namna ya kujiunga na mfuko huo,kupima afya. 



SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Ajali Yaua Shabiki Wa Simba, yajeruhi watu kadhaa akiwemo nahodha Jonas Mkude morogoro

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANOWA AFRIKA MASHARIKI YAWAZAWADIA WAFANYAKAZI WAKE

0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz Mlima (wa kwanza kulia), akimkabidhi zawadi Afisa Mambo ya Nje, Bi. Eva Ng'itu kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa. Bi. Ng'itu amekuwa Mfakazi Hodari wa wa Wizara ya Mambo ya Nje kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017. Dkt. Mlima aliwapongeza na kuwasihi wafanyakazi waliofanya vizuri kuwa zawadi walizokabidhiwa iwe chachu ya kuongeza juhudi na ufanisi katika utumishi wao. 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora na Mratibu wa Mafunzo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Tagie Daisy Mwakawago naye akipokea zawadi ya ufanyakazi bora wa Idara ya Diaspora'
Bi. Nelusigwe kutoka Kitengo cha Ununuzi na Ugavi akipokea zawadi baada ya kuibuka mfanyajkazi bora wa Kitengo hicho. 
Bw. Erick Ngilangwa kutoka Idara ya Afrika akipokea zawadi ya mfanyakazi bora wa Idara hiyo 
Afisa Habari wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Rose Mbilinyi akipokea zawadi yake kutoka kwa Dkt. Mlima. 




MKUTANO WA BARAZA KUU LA CHADEMA WAFANYIKA MJINI DODOMA

0
0

 MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA), Mhe. Freeman Mbowe akifungua mkutano wa Baraza Kuu la Chama hicho mjini Dodoma siku ya Jumamosi.
 Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk Vincent Mashinji akizungumza.
 Wajumbe wakiimba Wimbo wa Taifa 
 Dua ilifanyika kabla ya kuanza mkutano huo.
 Wajumbe wakiwa mkutanoni. 




MBUNGE AWESO AMSHUKURU RAIS DKT.MAGUFULI KWA KUIPATIA VIFAA TIBA WILAYA YA PANGANI

0
0

Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)  Mhe. Jumaa Aweso kulia akimkabidhi vitanda kimoja kati ya 25 Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani, Bw. Sabas Chambasi ambavyo ni miongoni mwa mgao wa vifaa tiba walivyopewa na Rais John Magufuli kwa ajili ya wilaya ya Pangani kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani, Mhe. Zainabu Issa 
Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Mhe. Jumaa Aweso kulia akimkabidhi mgao wa mashuka 50 kutoka kwa Rais John Magufuli Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani, Bw. Sabas Chambasi kwa ajili ya kusaidia huduma za afya kwenye wilaya ya Pangani katika halfa iliyofanyika kwenye hospitali ya wilaya ya Pangani juzi wa pili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani, Mhe. Zainabu Issa 
Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)  Mhe. Jumaa Aweso akizungumza katika halfa hiyo ambapo alimshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kuona umuhimu wa kusaidia vifaa tiba wilaya ya Pangani
Mkuu wa wilaya ya Pangani Mhe. Zainabu Issa akizungumza katika halfa hiyo kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) akizungumza katika makabidhiano hayo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images