Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

$
0
0
SIMU.TV: Wachimbaji wadogo 4 wamefariki dunia baada ya kufukiwa na kifusi kwenye machimbo moja huko mkoani Geita; https://youtu.be/Et61swLXm6U

SIMU.TV: Wananchi wamekumbushwa kuwa wazalendo katika shughuli zao ili kuhakikisha mali na rasilimali za nchi yao hazipotei; https://youtu.be/pbYmzm7Ot4E

SIMU.TV: Askari mmoja amefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya kutokea kwa tetemeko dogo la ardhi mkoani Mwanza; https://youtu.be/8PLnuUdNXjQ

SIMU.TV: Waziri wa ardhi William Lukuvi amesema serikali itaendelea kuongeza hazina ya ardhi kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo uwekezaji; https://youtu.be/s3i-Bj3HaYc

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka amemuagiza mkuu wa shule ya sekondari Mpitimbi kuwarudisha bwenini wanafunzi wake; https://youtu.be/IRXyNI0o6r0

SIMU.TV: Kampuni ya kutengeneza mkaa kwa kutumia Pumba ya RT imeendesha mafunzo kwa wanawake wajasiriamali ili watumie mkaa huo; https://youtu.be/sh42dZyQSXw

SIMU.TV: Wanawake wajasiriamali wa kata ya Mabwepande jijini Dar Es salaam wametakiwa kuchangamkia fursa za mikopo kuboresha maisha yao; https://youtu.be/xmMC3c9vQrY

SIMU.TV: Waziri wa fedha na mipango Dkt Philip Mpango amevitaka vikundi vya ujasiriamali vinavyopata mikopo kuhakikisha wanarudisha ili waweze kukopeshwa tena; https://youtu.be/xhz7ctaX7Pk  

SIMU.TV: Shirikisho la mpira wa miguu TFF limetoa pongezi kwa watanzania wote kwa namna walivyoiunga mkono timu ya taifa ya vijana Serengeti Boys; https://youtu.be/kQoOQqxLxiQ

SIMU.TV: Timu ya Mbao FC ya mkoani Mwanza imesema kuwa inataka kuandika historia mpya kwenye soka kwa kuifunga Simba kwenye Fainali ya kombe la shirikisho; https://youtu.be/SJS1nNB9mLE

SIMU.TV: Klabu ya Manchester United imekata tiketi ya kucheza klabu bingwa barani Ulaya baada ya kuitandika Ajax kwa mabao mawili kwa bila; https://youtu.be/_df1s20Hxw8


MGODI WA BUZWAGI WAPIGWA STOP KUZALISHA DHAHABU

TAARIFA YA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI GEITA

Mfuko wa LSF watoa semina kwa wahariri wa vyombo vya habari

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF), Kees Groenendijk (kulia) akiwasilisha mada kwa baadhi ya wahariri na wanahabari waandamizi katika semina kwa wanahabari iliyoandaliwa na LSF. Mfuko huo leo umekutana na baadhi ya wahariri na waandishi waandamizi na kutoa semina juu ya mchango wa vyombo vya habari katika kusaidia taasisi zinazotoa msaada wa sheria kwa jamii.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF), Kees Groenendijk (kushoto) akiwasilisha mada kwa baadhi ya wahariri na wanahabari waandamizi katika semina kwa wanahabari iliyoandaliwa na LSF. Mfuko huo leo umekutana na baadhi ya wahariri na waandishi waandamizi na kutoa semina juu ya mchango wa vyombo vya habari katika kusaidia taasisi zinazotoa msaada wa sheria kwa jamii.
Mwanasheria kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Wakili Harold Sungusia (kulia) akiwasilisha mada kwa baadhi ya wahariri na wanahabari waandamizi katika semina kwa wanahabari iliyoandaliwa na LSF. Wanatasnia hao wa habari wamepata fursa ya kujadiliana kwa pamoja na LSF namna vyombo vya habari vinavyoweza kusaidia upatikanaji wa haki kwa ujumla kwa jamii.
Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) kwa na kuzungumzia mchango wa vyombo vya habari katika kusaidia taasisi zinazotoa msaada wa sheria kwa jamii. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

Wizara ya ardhi yawasilisha hotuba ya Makadirio ya mapato na matumizi ya wizara kwa mwaka wa fedha 2017/18.

$
0
0
 Waziri wa Wizara ya Ardhi; Mhe. William Lukuvi na Naibu wake; Mhe. Angeline Mabula katika picha ya pamoja na Balozi wa Denmark, nchini Tanzania; Einar H. Jensen na Mshauri wa Programu ya kuwezesha umilikishaji Ardhi (LTSP); Suleiman Dabbas na watendaji wakuu wa Wizara – bungeni, Dodoma baada tu ya kuwasilisha hotuba ya Makadirio ya mapato na matumizi ya wizara kwa mwaka wa fedha 2017/18.

Kaimu Kamishna wa Ardhi; Mary Makondo na watendaji wakuu wengine wa Wizara wakiteta nje ya bunge, baada tu ya kuwasilishwa kwa hotuba ya Wizara ya Ardhi. 

 Watendaji wakuu wengine wa Wizara wakiteta nje ya bunge baada tu ya kuwasilishwa kwa hotuba ya Wizara ya Ardhi.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Ardhi, Ezekiel Mpanda akiwa nje ya bunge na timu yake, baada tu ya kuwasilishwa kwa hotuba ya Wizara ya Ardhi. 
Watendaji wa Wizara ya Ardhi, wakiendelea na kazi ya kujibu hoja zilizowasilishwa bungeni



Kwa Simu Toka London Na Freddy Macha: Mwanamitindo wa "Nyorido Fashion" London

MAADHIMISHO YA SIKU YA AFRIKA, WAUZAJI WA BIDHAA ASILI JIJINI MWANZA WANENA

$
0
0
Mei 25 kila mwaka Mataifa mbalimbali Barani Afrika huadhimisha Siku ya Afrika kama sehemu ya mataifa hayo kukumbuka ukombozi wake barani Afrika. Jijini Mwanza, watengenezaji na wauzaji wa vitu vya kitamaduni wamewataka watanzania kuongeza kasi ya matumizi ya vitu hivyo badala ya kutegemea vitu kutoka mataifa ya Maghabiri.

Kulia ni Mzee Francis Gabriel pamoja na Bi.Salome Babae ambao ni watengenezaji na wauzaji wa bidhaa za asili wakiwa kwenye eneo lao la biashara. Wanapatikana eneo la darajani Jijini Mwanza. 
Mawasiliano yao ni 0783 83 83 73

Na George Binagi-GB Pazzo
Watanzania wameshauriwa kupenda kutumia bidhaa za asili ikiwemo mavazi na urembo ili kuondoakana na utumwa wa kutovipa thamani vitu hivyo.
Wauzaji wa vitu vya asili katika eneo la darajani jijini mwanza, wayasema hayo wakati wakizungumza na lake fm kuhusiana na maadhimisho ya siku ya afrika hii leo.
Maadhimisho ya siku ya afrika yalianza kuadhimishwa tangu mei 25 mwaka 1963 yakilenga kuyahamasisha mataifa ya bara la afrika kujikomboa kutoka utumwani hususani kiakiri na kifira ili kuthamini zaidi tamaduni za kiafrika.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA MAY 26,2017


Mfuko wa LSF watoa semina kwa wahariri wa vyombo vya habari

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF), Kees Groenendijk (kulia) akiwasilisha mada kwa baadhi ya wahariri na wanahabari waandamizi katika semina kwa wanahabari iliyoandaliwa na LSF. Mfuko huo leo umekutana na baadhi ya wahariri na waandishi waandamizi na kutoa semina juu ya mchango wa vyombo vya habari katika kusaidia taasisi zinazotoa msaada wa sheria kwa jamii Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF), Kees Groenendijk (kushoto) akiwasilisha mada kwa baadhi ya wahariri na wanahabari waandamizi katika semina kwa wanahabari iliyoandaliwa na LSF. Mfuko huo leo umekutana na baadhi ya wahariri na waandishi waandamizi na kutoa semina juu ya mchango wa vyombo vya habari katika kusaidia taasisi zinazotoa msaada wa sheria kwa jamii Mwanasheria kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Wakili Harold Sungusia (kulia) akiwasilisha mada kwa baadhi ya wahariri na wanahabari waandamizi katika semina kwa wanahabari iliyoandaliwa na LSF. Wanatasnia hao wa habari wamepata fursa ya kujadiliana kwa pamoja na LSF namna vyombo vya habari vinavyoweza kusaidia upatikanaji wa haki kwa ujumla kwa jamii. Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) kwa na kuzungumzia mchango wa vyombo vya habari katika kusaidia taasisi zinazotoa msaada wa sheria kwa jamii.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA MAY 26,2017

TASAF YANG’ARISHA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI KISIWANI UNGUJA.

$
0
0
NA ESTOM SANGA-ZANZIBAR.

Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF – unaendelea kuboresha maisha ya walengwa wake Kisiwani Unguja ambao wameanza kujiimarisha kiuchumi kwa kuanzisha miradi midogo midogo ya uzalishaji mali kwa kutumia fedha za zitolewazo na Mpango huo.

Mmoja ya walengwa wa Mpango huo kutoka shehia ya kijini ,kisiwani Zanzibar Bi. Hafsa Seleman Abdallah mama wa watoto WANANE amewaambia wadau wa maendeleo na viongozi nwa TASAF waliotembelea kijijini hapo kuonana na walengwa wa Mpango huo kuwa kwa kutumia fedha za ruzuku kutoka TASAF ameweza kuanzisha shamba la migomba ambalo limeanza kumwingizia kipato kutokana na mauzo ya ndizi kutoka shambani humo.

“Ninaishukuru sana serikali na watu wa TASAF kwa kunitoa kwenye dimbwi la umaskini hadi sasa namiliki shamba hili la migomba kupitia fedha walizonipatia” amesema mama huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40 hivi.

Amesema mikungu ya ndizi iliyoko shambani mwake imekwishanunuliwa hata kabla ya kuvunwa kutokana na mahitaji makubwa ya bidhaa hiyo hasa wakati huu wa kuelekea mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan unaotarajiwa kuanza hivi karibuni ambapo mkungu mmoja huuzwa kwa shilingi 20,000.

Katika hatua nyingine walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini katika eneo la Kijini huko Makunduchi kisiwani Unguja wameanzisha vitalu vya miche ya matunda na kupanda mboga mboga kupitia utaratibu wa Ajira ya Muda .Kwa mujibu wa maelezo ya sheha , eneo hilo hapo awali halikuwa likizalisha mboga mboga kutokana na aina ya ardhi iliyochanganyika na mawe.

Hata hivyo chini ya utaratibu wa ajira za muda walengwa wa Mpango wa Kunusuru kaya masikini wameweza kuboresha ardhi hiyo kwa kufuata ushauri wa wataalamu wa kilimo na wameweza kulima mboga za majani , pilipili hoho na hata vitunguu mazao ambayo huyauza na kujiongezea kipato.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bwana Ladislaus Mwamanga aliyeshika kitabu akiwa na mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Kijini kisiwani Unguja Bi. Hafsa Seleman Abdallah wakiwa katika shamba la migomba alilolianzisha mlengwa huyo kwa kutumia fedha za ruzuku kutoka TASAF ikiwa ni njia ya kujiongezea kipato.
Baadhi ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini wa kijiji cha Kijini ,Makunduchi kisiwani Unguja wakisikiliza nasaha kutoka kwa wadau wa maendeleo (hawapo pichani ) waliotembelea eneo hilo kuona na mna walengwa hao wanavyonufaika na fedha za Mpango huo.
Wadau wa Maendeleo na viongozi wa TASAF wakiangalia Kamba za kungia mifugo zilizosukwa na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika eneo la Kijini,Makunduchi –Unguja kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato. Uanzishwaji wa miradi midogo midogo ya kiuchumi kwa walengwa ni sehemu muhimu ya Mpango wa Kunusuru Kaya masikini.
Picha ya juu na chini ni baadhi ya wadau wa maendeleo na viongozi wa TASAF wakiwa katika bustani ya mboga iliyoanzishwa na walengwa wa Kijini ,Makunduchi kisiwani Zanzibar chini ya utaratibu wa Ajira ya Muda ambayo hutekelezwa kwa siku 15 kila mwezi kwa kipindi cha miezi minne wakati wa hari na kisha hulipwa ujira ili kuwaongezea kipato.

DC MTATURU AKABIDHI NYUMBA 12 ZA WALIMU WA SEKONDARI

$
0
0


MKUU wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu amekabidhi nyumba 12 za walimu wa shule ya Sekondari ya Minyughe na Wembere huku akiwaasa walimu kumpa nguvu rais dokta John Pombe Magufuli kwa kuzitunza ili zidumu na kama sehemu ya kuunga mkono jitihada zake za kuwatumikia wananchi.

Nyumba hizo zimejengwa kupitia mpango wa serikali wa kuendeleza shule za sekondari(SEDEP II) uliogharimu shilingi milioni 300 hadi kukamilika kwake.

Akikabidhi nyumba hizo Mtaruru alimshukuru rais dokta Magufuli kwa dhamira yake njema ya kuwahudumia watanzania ili wawe na maisha mazuri ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)ya mwaka 2015 iliyoeleza uboreshaji wa elimu ikiwemo mazingira ya kufundishia.

“Tukio hili ni ushahidi tosha wa namna ilani ya CCM inavyotekelezwa kwa vitendo,nyumba hizi zitasaidia kuwasogeza walimu karibu na mazingira ya shule na hivyo kuwapa utulivu wa kuandaa masomo yao hali itakayosaidia kuongezeka kwa ufaulu kama moja ya maazimio ya mkutano wa wadau wa elimu uliofanyika mwezi disemba mwaka jana lakini pia itaondoa kero ya walimu kuhangaika mitaani,”alisema Mtaturu.

Aliwataka walimu kuendelea kuiamini serikali wakati inaendelea kushughulikia kero,stahili na madai yao na kuwapongeza kwa ushirikiano walioutoa kwa wakandarasi uliorahisisha mradi huo kukamilika kwa wakati.

Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akizindua rasmi nyumba zilizojengwa kwa ajili ya walimu wa shule za sekondari za Minyughe na Wembere baadhi ya aliofuatana nao ni mwenyekiti wa CCM wilaya Hassan Tati mwenye shati la kijani na Diwani wa kata ya Minyughe Saddack.  Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akikagua nyumba 12 za walimu baada ya kuzizindua.

Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akiwa kwenye picha ya pamoja na   viongozi wa wilaya,kata na walimu waliokabidhiwa nyumba kwenye shule ya sekondari ya Minyughe. 

SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LASHEREHEKEA KUWASILI KWA NDEGE YAKE YA 10 AINA YA A380

$
0
0
 Wafanyakazi wa shirika la ndege la Etihad wakifurahia kuwasili kwa ndege yao ya 10 na ya Mwisho aina ya A380
 Ndege ya Etihad A380s inatoa huduma kutokea nchi za uarabuni kwenda mji mkuu wa London, Sydney, New York na kuanzia tarehe 01/07/2017 watakua Paris.        

 Wafanyakazi wa shirika la Ndege la Etihad wakijumuika pamoja katika uwanja wa ndege wa Hamburg Finkenwerder nchini ujerumani barani Ulaya ambapo ndege hiyo ilizinduliwa rasmi na kukabidhiwa kwa shirika la ndege la uarabuni kabla ya kuanza safari zake za uwasilishaji nchini  Abu Dhabi.
   
Ndege za aina ya A380s zilizojishindia tuzo kadhaa, ni ndege za kibiashara zenye utofauti wa kipekee kwenye huduma zao kama malazi –vyumba vitatu vyenye ukubwa wa kuweza kuishi watu mpaka wawili vikiwa na sebule, bafu binafsi na chumba cha kulalia. Ndege hizi pia zinajivunia kuwa na “appartments” 9, studio za biashara 70, mahala pa kupumzikia na siti nzuri 415 kwenye daraja la uchumi.

YANGA ILIVYOLETA SHANGWE BUNGENI LEO MAY 25,2017

$
0
0

Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2016/17 Yanga wametembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania  Mkoani Dodoma ikiwa ni katika ziara yao ya kuelekea Mkoani Arusha kwa ajili ya kulitembeza kombe.

Yanga waliofanikiwa kulichukua kombe hilo kwa mara ya tatu mfululizo ikiwa ni mara ya 27 toka kuanz akwa Ligi Kuu Nchini, mabinhwa hao waliambatana namsafara wa viongozi ukiongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Salum Mkemi pampja na benchi la Ufundi.
 Baadhi ya wabunge wakiwa wamelibeba kombe wakionekana kufurahi leo Mkoani  Dodoma.
Baadhi ya wabunge, wachezaji na viongozi wa Yanga wakiwa katika picha ya pamoja leo Mkoani  Dodoma.

WALICHOONGEA WASANII BAADA YA RAIS DKT. MAGUFULI KUPOKEA RIPOTI WA MCHANGA WA MADINI


RAIS MSTAAFU ALHAJ ALI HASSAN MWINYI AONGOZA MAZISHI YA MZEE KITWANA KONDO

$
0
0
Na. Eliphace Marwa - Maelezo.
RAIS Mstaafu Ali Hassan Mwinyi ameongoza mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam katika maziko ya mwanasiasa mkongwe na aliyekuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Kitwana Kondo.
Mbali na Mwinyi wengine waliohudhuria maziko hayo yaliyofanyika katika makaburi ya Tambaza ni Makamu wa Rais Mstaafu, Mohammed Gharib Bilal, Mawaziri Wakuu Wastaafu, Salim Ahmed Salim na Edward Lowassa, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba pamoja na wengine.
Akizungumza nyumbani kwa marehemu, Mzee Mwinyi alisema, marehemu Kondo alikuwa  ni mtu ambaye alijitoa katika kulitumikia taifa kwa moyo wake, hivyo mchango wake ni mkubwa katika kulitumikia taifa na hasa wakazi wa jiji la Dar Es Salaam.
"Alikuwa ni rafiki yangu ambaye tumefahamiana kwa muda mrefu sana, tumepoteza mtu muhimu sana, lakini kazi ya Mungu haina makosa, tumuombee kwa Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi," alisema Mzee Mwinyi
 Mwili wa aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Mbunge wa Kigamboni Kitwana Kondo ukiwa ukiwa umeingizwa kwenye kaburi tayari kwa ajili ya maziko katika makaburi ya Tambaza yaliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili Dkt. Ali Hassan Mwinyi akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Mbunge wa Kigamboni Kitwana Kondo katika makaburi ya Tambaza yaliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Ghalib Bilal akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Mbunge wa Kigamboni Kitwana Kondo katika makaburi ya Tambaza yaliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.
 Mwanasiasa mkongwe nchini Kingunge Ngombare Mwilu akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Mbunge wa Kigamboni Kitwana Kondo katika makaburi ya Tambaza yaliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.
Jaji Mstaafu Mark Bomani akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Mbunge wa Kigamboni Kitwana Kondo katika makaburi ya Tambaza yaliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya wananchi walioshiriki mazishi ya aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Mbunge wa Kigamboni Mzee Kitwana Kondo wakiweka udongo wakati wa mazishi mapema leo jioni jijini Dar es Salaam.Picha Emmauel Massaka,Globu ya jamii.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

ORODHA YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA JKT 2017 KWA MUJIBU WA SHERIA

TAAZIA (OBITUARY) BURIANI MZEE KITWANA KONDO

$
0
0
Na Ramadhan K. Dau
Siku ya Jumatano tarehe 24 Mei 2017 ni siku ambayo itakumbukwa na Watanzania wengi na haswa Waislamu kwa kuondokewa na mzee wetu Alhaj Kitwana Selemani Kondo maarufu “KK” au mzee wa mjini. 

Siku 4 kabla ya kifo chake, mwanawe wa kiume Bwana Adnan Kitwana Kondo maarufu “Saku” alinitumia ujumbe kwenye WhatsApp akiniarifu kuwa mzee KK amelazwa Hindu Mandal na hali ya afya yake inazidi kuzorota. Siku ya pili yake nilimtumia ujumbe “Saku” kutaka kujua hali ya mzee inaendeleaje. Majibu ya “Saku” yaliniashiria kuwa mzee wetu amekaribia kufika mwisho wa safari yake. Aliniambia kuwa kwa sababu ya ukaribu wangu na mzee KK hana budi aniarifu ukweli ulivyo. Aliniarifu kuwa hali ya mzee ni mbaya sana na kwamba kinachosubiriwa na Rehma Zake Mwenyezi Mungu. Kwa kweli ujumbe ule ulihuzunisha sana na sikuweza kuhimili uchungu ule peke yangu. Nikamwarifu Profesa Hamza Mustafa Njozi, Makamu Mkuu wa Chuo cha Waislamu Morogoro na Bwana Faraji Abdallah Tamim, mwalimu wa chuoni hapo.
Ilipofika siku ya Jumatano tarehe 24 Mei nikapata taarifa kupitia moja ya kundi sogozi (chat group) kuwa mzee KK amefariki dunia. Pamoja ya kuwa hali hiyo ilikuwa tayari inatawala fikra zangu lakini kifo hakizoeleki.  

Moja kati ya sifa zake nyingi ni ujasiri. Mzee KK hakuwa mwoga na alikuwa na ujasiri wa kusimamia jambo ambalo anaamini ni sahihi na lina manufaa kwa nchi yetu. Mifano iko mingi. Kwa leo itoshe tu kuwa alisimamia suala la upatikanaji wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro kwa kujenga hoja kwa Rais wa wakati huo Mhe Benjamin William Mkapa mpaka Mhe Rais akashawishika kuwa ni jambo jema kuanzishwa kwa chuo hicho kwenye majengo ya kilichokuwa Chuo cha Mafunzo cha TANESCO.
(Pichani ni Mhe Mkapa akiwa na KK kushoto kwake na viongozi wengine waliohudhuria sherehe ya kuzindua uanzishwaji wa Chuo cha Kiislamu Morogoro).  
Kama kuna mtu mmoja ambaye ametoa mchango wa kipekee uliopelekea upatikanaji wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM) mtu huyo ni mzee Kitwana Kondo. 

Kwa kuenzi jitihada zake hizo, na kwa kuzingatia mzee Kondo ni Mwenyekiti mwanzilishi wa Taasisi ya Maendeleo ya Waislamu (MDF), taasisi ambayo ndiyo Mmiliki wa MUM, nashauri uongozi wa Chuo utafute jengo lenye hadhi pale Chuoni lipewe jina lake. Kwa siku za usoni, Chuo kitakapoanza kutoa shahada za Uzamivu (PhD), nashauri mzee Kitwana Kondo atunukiwe PhD (Honoris Causa) posthumously.

TAARIFA YA PROF ABDULKARIM MRUMA,MWENYEKITI WA KAMATI MAALUM YA KWANZA YA UCHUNGUZI

CCM YAMPONGEZA JPM SAKATA LA MCHANGA WA MADINI, YALAANI VIKALI MAUAJI MKOANI PWANI

$
0
0

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa kutekeleza sera na kuisimamia ilani ya ushindi ya CCM ya mwaka 2015/2020 na kuwaomba watanzania wote kwa kauli moja pasina itikadi za vyama kumuunga mkono kwani atakuwa imara na madhubuti zaidi katika utendaji wake iwapo ataungwa mkono na watanzania wote.

Chama cha Mapinduzi (CCM) Kimetoa pongezi hizo kutokana na maamuzi yaliyofanywa na Rais Magufuli mara baada ya kupokea Ripoti ya kamati iliyokuwa inachunguza Hatma ya mchanga wa madini iliyoundwa na Rais Magufuli Machi 29 mwaka huu ikiwajumuisha Profesa Abdulkarim Hamisi Mruma (Mwenyekiti), Profesa Justiania Rwezaura Ikingula, Profesa Joseph Bushweshaiga, Dokta Yusuph Ngenya, Dokta Joseph Yoweza Phili, Dokta Ambrose Itika, Mohamed Zengo Makongoro na Hery Issa Gombela.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, Itikadi na Uenezi Ndg Humprey Polepole wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Mikutano Ofisi ndogo ya CCM Lumumba Jijini Dar es salaam.

Polepole alisema kuwa uamuzi wa kuundwa kwa kamati hiyo ulitokana na kukamatwa kwa makontena 277 ya mchanga huo katika bandari ya Dar es salaam Machi 23 Mwaka huu baada ya Rais kufanya ziara ya kushitukiza katika bandari hiyo na kukuta makontena 20 yakiwa mbioni kusafirishwa kinyume cha maelekezo yake ya Machi 2 ya kuzuia kusafirisha mchanga huo nje ya nchi.

Alisema kuwa huu sio wakati wa kulumbana na kutofautiana kisa itikadi za vyama bali ni wakati wa kusimama pamoja na kuikabili vita ya kiuchumi kwani kwa kuzingatia taarifa iliyosomwa na Profesa Mruma mbele ya Rais Magufuli imebainisha jinsi Taifa lilivyopata hasara ya mabilioni ya fedha kwa kuwa makontena yaliyozuiliwa bandarini yana thamani ya madini yaliyomo kwa kiwango cha wastani wa shilingi Bilioni 829.4 na kiwango cha juu ni Shilingi Trioni 1.4

"Tumeibiwa na kudhulumiwa sana mali zetu ambazo tumezirithi kutoka kwa babu zetu lakini awamu ya Tano ikiongozwa na Rais Magufuli imeamua kwa dhati kabisa kutilia mkazo Vita dhidi ya Rushwa, Uhujumu uchumi, Udhalimu wa kila namna, sambamba na wizi na ufisadi kwa maslahi mapana ya Taifa la Tanzania na Watanzania wote" Alisema Polepole

Akizungumzia Mauaji yanayotokea katika maeneo mbalimbali nchini hususani Mkoani Pwani katika Wilaya ya Kibiti, Rufiji na Mkuranga alisema kuwa kipindi hiki kigumu kwa kuwapoteza ndugu zetu vyama vya siasa vilipaswa kushikamana kwa pamoja pasina kujali itikadi zao badala yake vimeanza kutumia misiba hiyo kwa maslahi ya kiuongozi kuliko maslahi ya Taifa.

Polepole alisema kuwa vyombo vyote vya serikali vinavyoshughulikia ulinzi vinapaswa kutumia Rasilimali zao, Weledi na Utendaji wao, na kuweka umaalumu katika kuyakabili matukio ya mauaji na kuyakomesha kabisa.

"Hakuna dini yoyote Duniani inayoamini katika kutoa uhai wa mtu ambapo pia kuua mtu ni kinyume na Katiba ya  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo Tunataka amani ya wananchi wetu inarudi" 

"Tunatambua kuwa wananchi wetu wanapita katika wakati mgumu kutokana na kukatishwa kinyama maisha ya Wananchi wenzao, Viongozi, Askari, Watendaji wa serikali, Wanachama wa CCM si kwa sababu ya mapenzi ya Mungu Bali kwa sababu yamekatishwa katika namna inayokiuka ubinadamu kwa kuuawa kikatili na watu wasio na Utu, Hisia na Imani ya Dini" Alisema Polepole

Polepole ametilia msisitizo wananchi kutoa taarifa kwa jeshi la Polisi kuhusu watu wanaofanya mauaji hayo kwani ushirikiano huo utasaidia kufichua uovu wa wadhalimu wanaokatisha maisha ya watanzania.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, Itikadi na Uenezi Ndg Humprey Polepole akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Mikutano Ofisi ndogo ya CCM Lumumba Jijini Dar es salaam. Picha Zote na Mathias Canal

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, Itikadi na Uenezi Ndg Humprey Polepole akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Mikutano Ofisi ndogo ya CCM Lumumba Jijini Dar es salaam.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, Itikadi na Uenezi Ndg Humprey Polepole wakati wa Mkutano wake na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Mikutano Ofisi ndogo ya CCM Lumumba Jijini Dar es salaam.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, Itikadi na Uenezi Ndg Humprey Polepole akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Mikutano Ofisi ndogo ya CCM Lumumba Jijini Dar es salaam.
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images