Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1706 | 1707 | (Page 1708) | 1709 | 1710 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Vyombo vya habari nchini hususani redio za kijamii zimetakiwa kuandika habari ambazo zinaelezea changamoto ambazo zinawakabili wananchi katika maisha yao ya kila siku na jinsi ambavyo wanaweza kuzitatua.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kuhusu wajibu wa redio za kijamii kwa maendeleo vijinini ambayo yamehusisha wasimamizi wa redio za kijamii na wawakilishi wa Halmashauri wa wilaya hizo ambao wanawakilisha halmashauri zao katika shughuli za uendeshaji wa redio hizo za jamii.

  Alisema wanahabari na vyombo vya habari ni muhimu nchini kwa maendeleo ya Taifa lakini kama wasipokuwa makini katika utendaji wao wa kazi kunaweza kuwa na madhara makubwa hivyo ni wajibu wao kuhakikisha wanazingatia maadili ya uandishi wa habari.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (wa kwanza kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura (wa pili kulia) kabla ya kufungua mafunzo ya siku mbili kuhusu wajibu wa redio za kijamii kwa maendeleo vijinini ambayo yamehusisha wasimamizi wa redio za kijamii na wawakilishi wa Halmashauri wa wilaya hizo ambao wanawakilisha halmashauri zao katika shughuli za uendeshaji wa redio hizo za jamii.

  Alisema sehemu kubwa ya wananchi ambao wanaishi vijijini hawapati taarifa muhimu zinazohusu maendeleo yao zikiwepo taarifa za kilimo, afya, mazingira na haki za kibadamu hivyo ni wajibu wao kuhakikisha wanaandika habari ambazo wananchi wamekuwa hawazipati kwa muda mrefu.

  “Ni jukumu lenu sasa kuhakikisha redio hizo zinatimiza malengo yake hususani katika kumuelimisha wanajamii, kuwajengea uwezo wa kutambua na kupambana na mazingira ili kuinua hali zao za kimaisha,” Mhe. alisema Wambura.

  Alisema mafunzo hiyo ni muhimu kwao kama wawakilishi wa redio za kijamii sababu itawapa mbinu ambazo wanaweza kuzitumia ili waweze kujisimamia wao wenyewe bila kuwa tegemezi kwa kuomba fedha kutoka sehemu zingine.
  Picha juu na chini ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura akisoma hotuba ya kufungua mafunzo ya siku mbili kuhusu wajibu wa redio za kijamii kwa maendeleo vijinini ambayo yamehusisha wasimamizi wa redio za kijamii na wawakilishi wa Halmashauri wa wilaya hizo ambao wanawakilisha halmashauri zao katika shughuli za uendeshaji wa redio hizo za jamii.

  “Natambua changamoto zilizopo katika uendeshaji wa redio za kijamii ambazo ni kama upatikanji wa habari endelevu na zinazolingana na mahitaji ya jamii husika, uhaba wa rasilimali fedha za kuendeshea redio husika, na udhaifu katika usimamizi stahiki wa taasisi hizo lakini kwa hakika mafunzo haya ni muhimu kwa vile yanalenga kutatua changamoto hizo,” alisema Wambura.

  Aidha Naibu Waziri Wambura amewashukuru Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa kutoa mafunzo hayo ambayo yatasaidia kujenga Taifa lenye waandishi na wasimamizi wa habari wenye weledi na kazi zao pia mafunzo hayo yanakwenda sambamba na dira ya wizara ya kuwa na Taifa lililohabarishwa vizuri ifikapo 2025.
  Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida amesema mafunzo hayo yamekuja baada ya kufanyika utafiti mwaka 2014 kwa ufadhili wa UNDP, utafiti ambao ulifanyika kwenye wilaya tano nchini na kugundua kuwa njia bora ya upashaji habari katika maeneo hayo ni kwa kutumia redio.

  Amesema baada ya matokeo hayo ya utafiti walipendekeza kuanzishwa kwa redio jamii katika maeneo ambayo utafiti ulifanyika ili kurahisisha taarifa mbalimbali za kuelimisha wananchi ambazo zitakuwa chachu kubwa ya maendeleo kuwafikia wananchi kwa urahisi.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho katika mafunzo ya siku mbili kuhusu wajibu wa redio za kijamii kwa maendeleo vijinini ambayo yamehusisha wasimamizi wa redio za kijamii na wawakilishi wa Halmashauri wa wilaya hizo ambao wanawakilisha halmashauri zao katika shughuli za uendeshaji wa redio hizo za jamii.


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kushoto) pamoja na Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya NMB, James Meitaron (wa pili kulia) wakifunua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa NMB FANIKIWA ACCOUNT leo jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Meneja Mwandamizi Kitengo cha Biashara, Donatus Richard akishuhudia. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa NMB FANIKIWA ACCOUNT uliofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya NMB, James Meitaron kushoto ni Meneja Mwandamizi Kitengo cha Biashara, Donatus Richard akiwa katika mkutano huo. Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya NMB, James Meitaron akifafanua jambo katika uzinduzi wa 'NMB FANIKIWA ACCOUNT'. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker na Meneja Mwandamizi Kitengo cha Biashara, Donatus Richard (kushoto)

  BENKI ya NMB imezindua akaunti mpya kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati ijulikanayo kama 'NMB FANIKIWA ACCOUNT' ili waweze kukua kibiashara pamoja na kupata maendeleo ya biashara wanazozifanya. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa akaunti hiyo ya wafanyabiashara wadogo na wakati, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Ineke Bussemaker, alisema kuwa akaunti hiyo haina masharti magumu wakati wa kuifungua pamoja na uendeshaji wake hivyo kuwataka wafanyabiashara wote kuitumia. 


  0 0

  NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

  NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma Saadala  “ Mabodi”  amewataka viongozi wa kisiasa wa chama hicho waliopewa dhamana ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015/2020 kwa wananchi waanze kujitathimini mapema kabla ya uchaguzi mkuu ujao.

  Rai hiyo ameitoa katika hafla ya utekelezaji wa Ilani hiyo iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Donge, Nd. Sadifa Juma  katika jimbo hilo huko Kaskazini “B” Unguja.

  Dkt. Mabodi aliwambia viongozi wa kisiasa waliochaguliwa na wananchi kuanzia ngazi za Madiwani, Wawakilishi, Wabunge na Rais wa Zanzibar  kuwa utaratibu wa kubuni na kutekeleza miradi ya maendeleo sambamba na kuimarisha miradi ya huduma za kijamii sio suala la hiari bali ni lazima kwa kila aliyetumia tiketi ya chama hicho kuomba  ridhaa ya kuwatumikia wananchi.

  Naibu Katibu Mkuu huyo amesifu juhudi za baadhi ya viongozi wanaoendelea kutekeleza ahadi walizoahidi kwa wananchi awamu kwa awamu kuanzia ngazi za chini hadi taifa, na kuwataka waliojisahau kurudi Majimboni mwao kutatua kero zinazowakabili wananchi.

  “ Njia pekee ya CCM kubaki madarakani ni kutatua kero za wananchi mijini na vijijini bila kujali itikadi za kisiasa na kidini ili jamii endelee kujenga imani na upendo wa kudumu kwa Chama kilichoiweka serikali madarakani”, alisema Dkt. Mabodi.

  Hata hivyo Naibu Katibu Mkuu huyo Dkt. Mabodi alitoa ahadi ya shilingi 300,000 kwa skuli ya maandalizi Mkataleni pamoja na kusaidia ujenzi wa vyoo vya skuli hiyo ili watoto waweze kusoma katika mazingira bora.

  Akizungumza  Mbunge wa Jimbo hilo, Nd. Sadifa Juma mara baada ya kutoa mabati 400 yenye thamani ya shilingi milioni saba ili kuezekea Hospitali ya Vijibweni, Maskani ya Kitaruni, Maskani ya Karange, vijibweni “B” Maskani, Donge bridge, pamoja na Skuli ya maandalizi ya Mkataleni.

  Aidha  Nd.Sadifa mbali na kugawa mabati hayo pia alitoa fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 1.5 kwa hospitali ya Vijibweni inayotegemewa na wananchi wa Jimbo hilo na maeneo jirani kwa huduma mbali mbali za afya ili kiweze kufanyiwa matengenezo na kuwa cha kisasa.

  Akitoa shukrani zake Daktari dhamana wa Kituo hicho, Bi.Miza Ali Ussi alipongeza juhudi za mbunge huyo na alisema msaada huo umepatikana kwa wakati mwafaka kwani kwa muda mrefu walikuwa wakikabiliwa na changamoto za upungufu wa vifaa tiba na mabati ya kuezekea baadhi ya nyumba za hospitali hiyo.

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo leo Mei 25, 2017 amekutana na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye na kufanya nae mazungumzo ofisini kwake.

  Katika mazungumzo yao wamekubaliana kuendelea kushirikiana katika kufanya kazi na pia jeshi la zimamoto na uokoaji wameomba ushirikiano toka kwa mkuu wa mkoa ili kuweza kuliunganisha jeshi hilo na mamlaka za serikali za mitaa ili liweze kufanya shughuli zake kwa ufanisi kwani mnufaika mkubwa wa huduma zao ni mamlaka hizo husika.

  Gambo ametoa rai kwa Jeshi hilo kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala ya kusubiri matukio ya ajali za moto kutokea wanapaswa kutoa elimu kwa wananchi namna ya kuyazuia matukio hayo na kwa kufanya hivyo watapunguza sana kazi yao kwani majanga ya moto yatakua historia.

  Pia wamekubaliana kuhakikisha ramani  za majengo na michoro ya mpango kabambe (master plan) kwa jiji la Arusha zinapitiwa, lengo ni kuona mapungufu ya kiusalama dhidi ya majanga ya moto na kuona namna ya kuzitatua mapema.

  Mkoa wa Arusha hasa kwa jiji la Arusha ni miongoni mwa maeneo ambayo kuna changamoto kubwa sana hasa panapotokea majanga ya moto kwani miundo mbinu na vituo vya zimamoto havitoshelezi mahitaji.
  Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kulia) akiwa katika mazungumzo na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye (wa pili kulia) alipokutana nae ofisini kwake leo. Wengine ni Kamisha Msaidizi wa Uhamiaji Mkoa wa Arusha, Ali Dady (kushoto) pamoja na Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji  mkoa wa Arusha, Bakari Mrisho
  Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akimsikiliza Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye walipokuwa katika mazungumzo ofisini kwake leo. 
  Baadhi wa Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakifatilia mazungumzo hayo.
  Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye (kushoto), Kamisha Msaidizi wa Uhamiaji Mkoa wa Arusha, Ali Dady (wa pili kulia) pamoja na Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji  mkoa wa Arusha, Bakari Mrisho baada ya mazungumzo. Picha zote na James Mhilu, Arusha.

  0 0

  Wadhamini wakuu wa Ligi ya Mpira wa miguu Tanzania Bara kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC, jana ilitoa zawadi zenye thamani ya shilingi 232,974,660 kwa washindi mbali mbali wa ligi. 

  Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji zawadi iliyofanyika jijini Dar es Salaama jana, Mkurugenzi Mkuu wa biashara na Masoko wa kampuni hiyo,Hisham Hendi  (pichani) alisema Vodacom imeongeza kiasi cha fedha zaidi mwaka huu. 
  Mwaka jana tulitoa shilingi 219,502,500. Kwa ajili ya zawadi lakini mwaka huu fedha hizi zimeongezeka na kufikia shilingi232,974,660,” alisema. 
  Hendi alisema, Vodacom Tanzania inavutiwa na jinsi ambavyo umaarufu wa ligi unavyokuwa  ukiongezeka siku hadi siku huku ukiwavutia na kuwaburudisha Watanzania  walio wengi wanaoishi mijini na vijijini bila kujali kama timu za maeneo wanayoishi zinashiriki ligi hii. 
  “Pamoja na umaarufu wa ligi hii kuongezeka na mafanikio yanayozidi kupatikana, sisi kama wadhamini tunajua kuwa bado kuna changamoto mbalimbali za kuboresha ligi yetu iwe na viwango vya hali ya juu na ili kuondokana na changamoto hizi unahitajika ushirikiano mkubwa baina ya wadau wote wa mchezo wa soka nchini japo mabadiliko hayawezi kuja kwa siku moja,” alieleza. 
   Waziri wa Michezo Utamaduni na sanaa Dkt, Harrison Mwakyembe(katikati) Mkurugenzi mkuu wa biashara wa Vodacom Tanzania,Hisham Hendi(kushoto)wakimkabidhi tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2016/2017  baba mzazi wa mchezaji wa simba,Mohamed Hussein”Tshabalala” baada ya mtoto wake kuchukua tuzo hiyo hapo jana wakati wa halfa ya utoaji tuzo mbalimbali za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini dar es Salaam.
  Waziri wa Michezo Utamaduni na sanaa Dkt, Harrison Mwakyembe,akipewa hongera na Mkurugenzi wa biashara wa Vodacom Tanzania,Hisham Hendi baada ya kuongea na wadau walioshiriki katika hafla ya utoaji tuzo mbalimbali za washindi  wa Ligi kuu bara,Iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi Vodacom Tanzania na  kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam,katikati ni Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC,Nandi Mwiyombella.
  Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC,Nandi Mwiyombella,akimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 84/- Katibu mkuu wa Yanga,Boniface Mkwasa baada ya timu yao kuibika mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2016/2017 wakati wa halfa ya utoaji tuzo mbalimbali jana katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.Taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0

   Mzee Francis Maige Ngosha (kwenye kitanda) akiwa kwenye gari la wagonjwa tayari kwa kupelekwa Hosptali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi. (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii).

  Na Anthony John Globu ya Jamii.
  Serikali imeahidi kumpatia matibabu Mzee Francis Ngosha  aliyebuni Nembo  ya taifa. Hatua hiyo imekuja baada ya kituo cha Runinga cha ITV  Dar es salaam kumuonesha mzee huyo akiwa katika hali mbaya katika eneo Buguruni ambapo alikutwa akiishi kwenye chumba kimoja alichopewa  na msamaria mwema.

  Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo hii katika hospitali ya Rufaa ya Amana  DKT, Hamisi Kigwangalla amesema mchango wamzee huyu ni mkubwa ambao utakumbuka na vizazi vyote nchini kwa suala hilo alilolifanya.

  Aidha  Kigwangalla amesema kuwa  serikali ilipata tarifa juu ya madhira  anayoyapata hivyo serikali ilimuagiza kuchukua hatua za haraka  za kumsaidia mzee huyu.

  ‘’Katika hatua hii tunashughulika na  suala matibabu na baada ya matibabu kukamilika tutamtafutia makazi ya kuishi kama atakubali atapelekwa katika nyumba ya wazee wasiojiweza iliyopo Nunge au tumtafutie nyumba kwaajili ya kuishi’’amesema Kigwangalla.
    Naibu Waziri,Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Hamisi Kigwangalla akimjulia hali Mzee Francis Maige Ngosha aliyelazwa kwenye wodi ya Wanaume Hospitali ya Rufaa Amana leo jijini Dar es Salaam.
    Mzee Francis Maige Ngosha (kwenye kitanda) akitolewa katika Hospitali ya Rufaa Amana tayari kwa kupelekwa Hosptali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi.
   Naibu Waziri Dk. Hamisi Kigwagalla akiongea na waandishi wa habari kuhusu hatua waliyochukua ya kumuhamishia Mzee Maige kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Kitengo cha Dharura Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Juma Mfinanga akizungumza na Mzee Francis Maige mara baada ya kupakiwa kwenye gari ya kubeba wagonjwa tayari kwa kupelekwa Muhimbili leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Mbogwe bi Martha Mkupasi amewataka wananchi wa Mbogwe watoe ushirikiano wa kutosha kwa Mradi Pendekezwa wa ujenzi wa Bomba la Kusafirishia Mafuta Ghafi (EACOP) linalotarajiwa kujengwa kutoka Ziwa Albert kupitia Kabaale (Uganda) hadi Rasi ya Chongoleani iliyo karibu na Bandari ya Tanga nchini Tanzania.

  Mkuu wa wilaya ameyasema hayo alipofungua kikao cha maoni ya wadau (scoping) kwa Wakuu wa Idara na watendaji wa kata wa Halmashauri ya wilaya ya Mbogwe kuhusu Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Jamii (TAM) ya mradi wa EACOP. Akiongea wakati wa ufunguzi bi Martha amesema mradi huo utaleta maendeleo kwa wanambogwe wote hivyo ni jukumu lao kuulinda .

  Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Kusafirishia Mafuta Ghafi kutoka Uganda (Ziwa Albert) hadi Tanzania (Tanga) lenye urefu wa kilometa 1445 linatarajiwa kupita katika wilaya ya Mbogwe. Akiongea wakati wa kikao hicho ,mwezeshaji kutoka kampuni ya JSB Envi-Dev Ltd Dr. Godfrey Kamukara ameelezea faida zitakazopatikana kutokana na mradi huo zikiwemo upatikanaji wa ajira kwa wakazi wa Mbogwe .

  Hata hivyo alitahadharisha kuwa mradi huo unatarajiwa kusababisha mwingiliano wa makabila mbali mbali hivyo kuwataka watendaji hao wawaelimishe wananchi kujikinga na maradhi ikiwemo ugonjwa wa ukimwi.

  Dr.Kamukara amewataka watendaji kuwaelimisha wananchi kuhusu mafuta ghafi ili wananchi wasitoboe bomba wakidhani ni mafuta yanayofaa kwa matumizi . Alieleza kuwa mafuta ghafi ni mafuta ambayo bado hayajasafishwa kwa matumizi ya kawaida.

  Kampuni ya RSK ya Uingereza na washirika wake kutoka Uganda ( ECO partners ) na Tanzania ( JSB Envi-Dev Ltd) wameanza kazi ya Tathimini ya Athari kwa Mazingira na Jamii kwa kushirikisha jamii yote inayopitiwa na mradi kwa kutoa maoni ya mambo muhimu ya kuzingatiwa wakati wa utekelezaji wa mradi huo. 

  Mkuu wa wilaya ya Mbogwe bi Martha Mkupasi

  0 0

   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai akisalimiana na Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta wakati wa ibada Maalum ya kuliombea Taifa la Kenya iliyoandaliwa na Bunge la nchi hiyo. Wengine katika  pichani kutoka kushoto ni Spika wa Bunge la Kenya  Justin Muturi, Spika wa Bunge la Seneti la Kenya Mhe  Ekwee Ethuro na Jaji Mkuu wa Kenya Jaji David Maraga. Mhe Ndugai yuko katika ziara ya kibunge nchini Kenya kwa mwaliko Bunge la Kenya ambapo amembatana na wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge, Mhe Mary Chatanda, Mhe Salim Turky na Mhe Mch.Peter Msigwa.

   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai (katikati ya waliokaa kulia) akizungumza na Rais wa Kenya Mhe Uhuru Kenyatta na Makamu wake Mhe William Rutto walipokutana wakati wa ibada Maalum ya kuliombea Taifa hilo. Wengine katika picha ni Spika wa Bunge la Kenya  Mhe Justin Muturi (kulia kwa Mhe Ndugai),Spika wa Bunge la Seneti la Kenya   Mhe. Ekwee Ethuro  (wa kwanza kulia),Mke wa Rais wa Kenya Margaret Kenyatta na Mke wa Makamu wa Rais wa Kenya Rachel Chebet.
   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (wa pili kulia) Mhe Job Ndugai akizungumza na Spika wa Bunge la Seneti la Kenya Mhe Ekwee Ethuro  (wa pili kushoto). Mhe Ndugai yuko katika ziara ya kibunge nchini Kenya kwa mwaliko Bunge la Kenya ambapo amembatana na wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge, Mhe Mary Chatanda, Mhe Salim Turky na Mhe Mch.Peter Msigwa.
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai akizungumza na Spika wa Bunge la Seneti la Kenya Mhe Ekwee Ethuro  alipomtembelea Ofisini kwake Jijini Nairobi, Kenya. Mhe Ndugai yuko katika ziara ya kibunge nchini Kenya kwa mwaliko Bunge la nchi hiyo. Picha na Ofisi ya Bunge

  0 0


    Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai akisalimiana na Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta wakati wa ibada Maalum ya kuliombea Taifa la Kenya iliyoandaliwa na Bunge la nchi hiyo. Wengine katika  pichani kutoka kushoto ni Spika wa Bunge la Kenya  Justin Muturi, Spika wa Bunge la Seneti la Kenya Mhe  Ekwee Ethuro na Jaji Mkuu wa Kenya Jaji David Maraga. Mhe Ndugai yuko katika ziara ya kibunge nchini Kenya kwa mwaliko Bunge la Kenya ambapo amembatana na wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge, Mhe Mary Chatanda, Mhe Salim Turky na Mhe Mch.Peter Msigwa.
   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai (katikati ya waliokaa kulia) akizungumza na Rais wa Kenya Mhe Uhuru Kenyatta na Makamu wake Mhe William Rutto walipokutana wakati wa ibada Maalum ya kuliombea Taifa hilo. Wengine katika picha ni Spika wa Bunge la Kenya  Mhe Justin Muturi (kulia kwa Mhe Ndugai),Spika wa Bunge la Seneti la Kenya   Mhe. Ekwee Ethuro  (wa kwanza kulia),Mke wa Rais wa Kenya Margaret Kenyatta na Mke wa Makamu wa Rais wa Kenya Rachel Chebet.
   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (wa pili kulia) Mhe Job Ndugai akizungumza na Spika wa Bunge la Seneti la Kenya Mhe Ekwee Ethuro  (wa pili kushoto). Mhe Ndugai yuko katika ziara ya kibunge nchini Kenya kwa mwaliko Bunge la Kenya ambapo amembatana na wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge, Mhe Mary Chatanda, Mhe Salim Turky na Mhe Mch.Peter Msigwa.
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai akizungumza na Spika wa Bunge la Seneti la Kenya Mhe Ekwee Ethuro  alipomtembelea Ofisini kwake Jijini Nairobi, Kenya. Mhe Ndugai yuko katika ziara ya kibunge nchini Kenya kwa mwaliko Bunge la nchi hiyo.

  (Picha na Ofisi ya Bunge)

  0 0

  Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH- imeanza kumfanyia uchunguzi mchoraji  wa Nembo ya Taifa , Mzee Francis Maige Kanyasu.

  Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali Dk. Juma Mfinanga amesema  Mzee Kanyasu amechukuliwa leo asubuhi kutoka Hospitali ya Amana ambako alipelekwa jana na majirani zake na kupatiwa matibabu ya awali.

  ‘’ Tumemchukua kutoka Hospitali ya Amana baada ya kupata habari zake kwenye vyombo vya habari kuwa hali yake kiafya sio nzuri hivyo  Mkurugenzi Mtendaji wa MNH , Profesa Lawrence Museru akatuagiza tumfuate ili apatiwe matibabu hapa Muhimbili ‘’ Amesema Dk. Juma.

  ‘’ Wenzetu wa Hospitali ya Amana wamemfanyia uchunguzi wa awali na wakatueleza shida yake kubwa ni kukosa nguvu na kushindwa kutembea hivyo tumemleta hapa Idara ya magonjwa ya Dharura na Ajali kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Baada ya uchunguzi  tutamuanzishia tiba haraka  kwa kushirikiana na Idara zingine hapahapa MNH.’’ Amesema Dk. Juma.

  Kwa mujibu wa Dk. Juma  kukosa lishe , mazingira magumu pamoja na umri kunasababisha mtu kupata magonjwa  mbalimbali.
   Mchoraji  Nembo ya Taifa , Mzee Francis Maige Kanyasu akiwa katika Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake. Mzee Kanyasu amefikishwa leo MNH akitokea Hospitali ya Amana.
  Daktari Bingwa wa magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni Mkuu wa Idara  hiyo  Juma Mfinanga akimuhudumia Mzee Kanyasu mara baada ya kufikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.


  0 0


  Wadhamini wakuu wa Ligi ya Mpira wa miguu Tanzania Bara kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC, jana ilitoa zawadi zenye thamani ya shilingi 232,974,660 kwa washindi mbali mbali wa ligi.

  Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji zawadi iliyofanyika jijini Dar es Salaama jana, Mkurugenzi Mkuu wa biashara na Masoko wa kampuni hiyo,Hisham Hendi alisema Vodacom imeongeza kiasi cha fedha zaidi mwaka huu.

  Mwaka jana tulitoa shilingi 219,502,500. Kwa ajili ya zawadi lakini mwaka huu fedha hizi zimeongezeka na kufikia shilingi 232,974,660,” alisema

  Hendi alisema, Vodacom Tanzania inavutiwa na jinsi ambavyo umaarufu wa ligi unavyokuwa ukiongezeka siku hadi siku huku ukiwavutia na kuwaburudisha Watanzania walio wengi wanaoishi mijini na vijijini bila kujali kama timu za maeneo wanayoishi zinashiriki ligi hii.

  “Pamoja na umaarufu wa ligi hii kuongezeka na mafanikio yanayozidi kupatikana, sisi kama wadhamini tunajua kuwa bado kuna changamoto mbalimbali za kuboresha ligi yetu iwe na viwango vya hali ya juu na ili kuondokana na changamoto hizi unahitajika ushirikiano mkubwa baina ya wadau wote wa mchezo wa soka nchini japo mabadiliko hayawezi kuja kwa siku moja,” alieleza.

  Mkurugenzi huyo alitoa wito kwa wadau wote kushiriki kubuni mikakati ya kuboresha ligi hii na ikiwezekana wajitokeze wafadhili wengine zaidi ili wachezaji wazidi kunufaika.
  Waziri wa Michezo Utamaduni na sanaa Dkt, Harrison Mwakyembe(katikati) Mkurugenzi mkuu wa biashara wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi(kushoto) wakimkabidhi tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2016/2017 baba mzazi wa mchezaji wa simba, Mohamed Hussein ”Tshabalala” baada ya mtoto wake kuchukua tuzo hiyo hapo jana wakati wa halfa ya utoaji tuzo mbalimbali za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC,Nandi Mwiyombella, akimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 84/- Katibu mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa baada ya timu yao kuibika mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2016/2017 wakati wa halfa ya utoaji tuzo mbalimbali jana katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa masoko wa Vodacom Tanzania, Ashutosh Tiwary (kushoto) akimkabidhi tuzo ya heshima, Kitwana Manara wakati wa halfa ya utoaji tuzo mbalimbali za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Michezo Utamaduni na sanaa Dkt, Harrison Mwakyembe(katikati) akimshuhudia Mkurugenzi mkuu wa biashara wa Vodacom Tanzania,Hisham Hendi(kushoto)akimpongeza baba mzazi wa mchezaji wa simba, Mohamed Hussein ”Tshabalala” baada ya mtoto wake kuibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2016/2017 wakati wa halfa ya utoaji tuzo mbalimbali za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Timu za vijana za Ghana na Mali zimefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika chini ya umri wa miaka 17.

  Ghana wametinga fainali baada ya kupata ushindi wa penati 6-5 dhidi ya Niger baada ya kwenda sare katika dakika tisini za mchezo.

  Mabingwa watetezi Mali wao wamefanikiwa kutinga fainali yao ya pili mfululizo baada ya kuwaondosha Guinea kwa penati 2-0 huku kipa wa Mali Youssouf Koita, akiwa shujaa wa timu hiyo kwa kuokoa michomo mingi na penati.

  Mchezo wa fainali ya michuano hiyo ya vijana utapigwa jumapili ya tarehe 28 mchezo ukichezwa katika dimba la Amitié Sino-Gabonaise, mjini Libreville,

  Mchezo wa kusaka mshindi wa tatu kati ya Niger na Guinea nao utafanyika siku hiyo hiyo ya jumapili katika uwanja wa katika uwanja Amitié Sino-Gabonaise.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Kiungo mahiri wa timu ya Mbeya City Kenny  Ally amejiunga rasmi na klabu ya Singida United kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania bara kwa kandarasi ya miaka miwili.

  Kenny ni miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa wakiwindwa vikali na klabu kubwa za hapa nchini Simba na Yanga kila mmoja akitaka kupata saini yake ila walikuwa wakishindwana katika dau.
  Usajili huo wa Kenny kwenda  Singida United ni pigo kwa timu ya Mbeya City kwani inaonekana ikiendelea kuvunjwa  kwa kusajiliwa wachezaji wao na klabu mbalimbali.

  Singida United ni miongoni mwa timu ambazo zimeanza kutazamwa na wadau wa soka kwamamba huenda wakaleta mapinduzi katika soka hapa nchini hii inatokana na mipango yao ikiwemo usajili wa wachezaji wa kigeni.
   Mchezaji Kenny Ally akipokea jezi yake kutoka kwa Katibu Mkuu wa Singida United Abdulrahman Sima baada ya kukamilisha kutia saini kandarasi ya miaka miwili ya kuitumikia klabu hiyo, katikati ni  Mwenyekiti wa kamati ya Usajili wa Singida Festo Sanga.
   Mchezaji Kenny Ally akitia saini kandarasi ya miaka miwili ya kuitumikia klabu hiyo. Kulia ni  Katibu Mkuu wa Singida United Abdulrahman Sima na  Mwenyekiti wa kamati ya Usajili wa Singida Festo Sanga.

  0 0

  Na Daudi Manongi, MAELEZO DODOMA

  Serikali kupitia Baraza la Uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) lililopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu imewataka wananchi kuitumia vyema mifuko 19 ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ili kujipatia mitaji yenye riba nafuu.

  Hayo yamesemwa leo Bungeni na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira na Vijana Mhe.Anthony Mavunde wakati akijibu maswali mbalimbali ya wabunge leo Mjini Dodoma.

  “Serikali inawawezesha wananchi ili waweze kukopesheka kupitia Sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ya mwaka 2004 na Sheria ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi Na.6 ya mwaka 2004, Alisema Mhe.Mavunde.

  Amesema Sera hii imeainisha nia ya Serikali ya kuweka mazingira mazuri ya upatikanaji wa mitaji kwa kuboresha vyanzo vya akiba na kuchukuwa hatua za kuondoa vikwazo mbalimbali ili kuwezesha mabenki kukopesha kikamilifu amana zilizopo kwa gharama nafuu,kupitia vikundi vidogo,SACCOS na Vicoba.

  Aidha kutokana na Sera hii Mipango, Miradi na Mifuko kadhaa imeanzishwa na Serikali ili kuwezesha wananchi kukopa kwa urahisi ambapo katika mifuko hiyo 19 baadhi yake ni pamoja na Mfuko wa kuendeleza wajasirimali wananchi,mfuko wa uwezeshaji wa mwananchi,mfuko wa pembejeo za kilimo,mfuko wa maendeleo ya vijana, mfuko wa dhamana za mikopo kwa wajasiriamali wadogo na wa kati,mfuko wa dhamana za mikopo kwa mauzo ya nje ya nchi ambapo hadi kufikia mwaka 2016 mifuko hii ilikuwa imetoa mikopo ya trilioni 1.7 kwa wajasiriamali 400,000.

  Pamoja na hayo Serikali imeendelea kuweka mazingira mazuri kwa vyombo hivyo kuweza kutoa huduma kwa wananchi.

  “Serikali kupitia Benki kuu ya Tanzania kulingana na mazingira inaendelea kuangalia viwango vya riba kwa mabenki na Taasisi za fedha ili zimudu kupata fedha zaidi kwa ajili ya kukopesha wajasiriamali kwa riba ndogo,ambapo pia imechukua hatua ya kupunguza kiwango cha riba kwa mikopo yake kutoka asilimia 16 hadi asilimia 12 ”,Alisisitiza Mavunde.


  0 0


  0 0


  Na Mathias Canal, Dar es salaam

  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori Leo Mei 25, 2017 amefanya ziara ya kutembelea Shule ya Msingi Kawawa iliyopo Katika Kata ya Mabibo Jijini Dar es salaam.

  Ziara hiyo ilikuwa na dhamira ya kubaini na kutatua changamoto zinazoikabili shule hiyo hususani changamoto ya Upungufu wa Madarasa na Vyoo kwa ajili ya Walimu na Wanafunzi wa shule hiyo.

  Katika ziara hiyo ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo imehudhuriwa pia na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo, Afisa Tarafa ya Kibamba, Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Ubungo, Diwani wa Kata ya Mabibo, Mtendaji Kata ya Mabibo, Wenyeviti na Watendaji wa Mitaa, Uongozi wa vyama vya siasa, Kamati ya Shule, Walimu sambamba na Wazazi.

  Katika ziara hiyo Mhe Makori amefikia uamuzi wa kuchangia Shilingi Milioni moja kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya shule kutokana na ubovu wa vyoo vilivyopo huku akiwasihi wananchi kwa ujumla kujitokeza kuchangia ujenzi wa vyoo hivyo.

  Aidha ameahidi kuanzisha Harambee mahususi kwa ajili ya kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa kwani yaliyopo ni Madarasa 22 Kati ya Madarasa 68 hivyo kuna upungufu wa madarasa 46.

  Kwa upande wa Matundu ya vyoo alisema kuwa upungufu ni mkubwa kwani yanahitajika matundu 136 na matundu ya vyoo yaliyopo ni 26 pekee hivyo kuna upungufu wa matundu 110.
  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akizungumza na walimu pamoja na wazazi katika Shule ya Msingi Kawawa iliyopo Katika Kata ya Mabibo Jijini Dar es salaam. Leo Mei 25, 2017
  Wazazi na Walimu wa Shule ya Msingi Kawawa wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori
  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akisalimiana na Ally Khamisi Mvugalo mara baada ya kuwasili katika Shule ya Msingi Kawawa iliyopo Katika Kata ya Mabibo Jijini Dar es salaam kwa ziara ya kikazi. Leo Mei 25, 2017
  Moja ya Majengo yaliyochakaa Shule ya Msingi Kawawa Iliyopo katika Kata ya Mabibo Manispaa ya Ubungo

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

   Naibu waziri wa Fedha na Mipango Mh Dr.Ashatu Kijaji akizindua mpango wa gharama nafuu utakao wahudumia watu wote waliojiunga na mfuko huo.

  Naibu waziri wa Fedha na Mipango Mh Dr.Ashatu Kijaji akifungua mkutano mkuu wa nane wa wadau wa mfuko wa mafao ya kustaafu wa GEPF uliofanyika leo jijini Arusha na kuhudhuriwa na wadau wa mfuko(Picha na Pamela Mollel).

   Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Richard Kwitega akiongea katika mkutano huo akimuakilisha mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,katika risala yake alisema kuwa anaipongeza mfuko huo kwa makubaliano waliofikia na UTT-MFI wa kutoa mikopo nafuu kwa wanachama wake wajasiriamali
  Naibu waziri wa Fedha na Mipango Mh Dr.Ashatu Kijaji akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa mfuko huo wa GEPF jijini Arusha.  0 0

  Mbunge wa jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula hii leo ameikaribisha bungeni timu ya mpira wa miguu ya Ilemela Jijini Mwanza Mbao Fc 

  Ikumbukwe kuwa huu ni mwendelezo wa jitihada za mbunge huyo za kuhakikisha anainua michezo katika jimbo la Ilemela na kutoa fursa kwa vijana kuonyesha na kuvitumia vipaji walivyonavyo katika kujiongezea kipato, Mhe Dkt Angeline Mabula amesema 

  ‘… Huu ni mwendelezo wa jitihada za kila siku ninazozifanya za kuhakikisha tunaboresha michezo yetu lakini pia kuifanya kuwa chanzo cha kipato katika kuendesha maisha ya kila siku ya vijana wetu wa Ilemela na Tanzania kwa ujumla wake …’

  Nao wachezaji wa Timu hiyo wamemshukuru Mbunge wao Dkt Angeline Mabula  kwa jitihada zake za kuboresha na kukuza michezo jimboni humo huku wakimuahidi ushindi katika mechi yao ya hatua ya fainali ya Kombe la FA dhidi ya Timu ya Simba ya Jijini Dar es Salaam wanayotarajia kuicheza siku ya jumamosi mjini Dodoma 

  “ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga ”

  Imetolewa na
  Ofisi ya Mbunge 
  Jimbo la Ilemela
  25.05.2017

  0 0


older | 1 | .... | 1706 | 1707 | (Page 1708) | 1709 | 1710 | .... | 3272 | newer