Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

Geita wapongeza huduma za NHIF

0
0
Hospitali Teule ya Mkoa wa Geita ambapo mpango unaoendeshwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya za huduma za Madaktari Bingwa. 

Na Grace Michael, Geita

Mamia ya wananchi mkoani Geita wamejitokeza kupata huduma za madaktari bingwa , mpango unaotekelezwa kwa ushiriiano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Mpango huo ulianza kutekelezwa siku ya Jumatatu wiki hii, katika mikoa ya Geita na Kigoma na unalenga kuwahudumia wagonjwa ambao wanahitaji huduma za kibingwa ambazo hazipo katika Hospitali hizo.

Madaktari bingwa wanaoshiriki katika mpango huo ni wa magonjwa ya watoto, mfumo wa mkojo, magonjwa ya ndani na moyo, magonjwa ya pua, masikio na koo pamoja na huduma za dawa za usingizi na huduma za wagonjwa mahututi.

Wakizungumza katika uzinduzi wa mpango huo uliofanyika katika viwanja vya hospitali ya mkoa wa Geita, wananchi waliojitokeza kupata huduma hizo wamesema ujio wa wataalamu hao umekuwa msaada mkubwa na umewaondolea usumbufu na gharama kubwa ambazo wangelazimika kuzitumia kufuata huduma hizo nje ya mkoa wao.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu na Ushauri wa Kitaalam Dk. Aifena Mramba ambaye alimwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Benrard Konga , akitoa maelezo ya awali kwenye uzinduzi wa huduma hizo. 

“ … Mfuko umetenda jambo jema sana na unapaswa kupongezwa hasa kwa kuona umuhimu wa kusogeza huduma hizi karibu na wananchi wengi wenye mahitaji kwa mfano mimi ni mjane hapa nilipo lakini mpango huu umeniwezesha kuwaona hawa wataalam ambao kwa hali ya kawaida nisingewaona hivyo napongeza Mfuko wa Serikali yetu inayoongozwa na Dk. Pombe John Magufuli,..” Alisema Bi. Leah Ezekiel.

Akitoa maelezo ya awali Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya , Dk. Aifena Mramba alisema kuwa kwa muda wa siku mbili za zoezi hilo katika mikioa ya Kigoma na Geita, jumla ya wagonjwa 1,204, wameonwa na kuhudumiwa na madaktari bingwa.

Alisema kuwa idadi hiyo imetoa taswira ya mahitaji ya wananchi katika huduma za kibingwa jambo linalotoa hamasa kwa Mfuko kuangalia namna ya kuendesha program hizo katika maeneo mengi zaidi.
Dk. Mramba akikabidhi Mashuka na Vifaa tiba kwa uongozi wa Mkoa wa Geita kwa ajili ya matumizi ya zoezi la Madaktari Bingwa.

“…Kwa madaktari tuliowaleta, wametuhakikishia kuwa wako tayari kufanya kazi kwa muda wowote ili wagonjwa wote waliofika kwa ajili ya mpango huo wahudumiwe na mfano mzuri jana kuna madaktari waliofanya kazi hadi saa sita usiku…” alisema Dk. Mramba.


WALIMU NA ASASI ZA KIRAIA WAJENGEWA UWEZO KUHAMASISHA UKUSANYAJI WA RASILIMALI ZA NDANI KUBORESHA SEKTA YA ELIMU

0
0
Katika kuzitafutia ufumbuzi changamoto za utoaji wa elimu bora hapa nchini leo Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) wakishirikiana na ActionAid Tanzania wameandaa mkutano uliowakutanisha wanachama wa chama cha walimu Tanzania (CWT/TTU) na wadau wa elimu katika mkoa wa Singida kwa siku tatu ili kupanga mpango kazi wa utetezi na ushawishi wa masuala ya elimu yatakayoleta matokeo chanya kwenye masuala ya elimu hapa nchini.

Mkutano huu  ulikuwa ulingazia changamoto zinazoikabili elimu ya msingi hapa nchini ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa, upungufu wa ofisi za walimu, upungufu wa vyoo vya wanafunzi, uwiano usiokubalika kitaratibu wa mwalimu na wanafunzi, shule nyingine kukosa kabisa mwalimu wa kike, upungufu wa nyumba za walimu, kutokutosha kwa fedha za ruzuku, utegemezi wa bajeti ya nchi unaoathiri pia bajeti ya elimu na kusababisha Serikali kushindwa kugharimia kiufanisi utoaji wa elimu.

Mgawanyo wa ruzuku usiozingatia mahitaji ya wenye uhitaji maalumu, jinsia na mahitaji ya kijiografia na pia shule changa na zile ambazo ni kongwe. Kuwa na mipango ya kibaguzi kwa shule inayofanya vizuri ndiyo inapewa fedha (payment for results- P4R) kutoka mpango wa BRN bila kujali mizania ya usawa wa mazingira kati ya shule na shule. Kukosekana kwa mafunzo kazini kwa walimu, kutopandishwa madaraja walimu na utolipwa kwa wakati stahiki za walimu wanaohamishwa/kustaafu mfano pesa ya usafiri.

Katika majadiliano washiriki walichangia juu Upotevu wa kodi nchini hususani katika sekta ya madini na viwanda ndio chanzo cha kukosa fedha za kutosha kugharimia sekta ya elimu nchini. 
Afisa Mradi wa Elimu kutoka TENMET, Bi. Alistidia Kamugisha akielezea juu ya uhusiano wa ukusanyaji kodi na maendeleo katika sekta ya elimu kwenye mafunzo ili kutafuta ufumbuzi wa changamoto za utoaji wa elimu bora hapa nchini mkutano huu umewakutanisha wanachama wa chama cha walimu Tanzania (CWT/TTU) na wadau wa elimu katika mkoa wa Singida.
Mkufunzi wa Mafunzo, Wakili Dominic Nduguru akitoa mada ya uhusiano wa Makusanyo ya Kodi Na Maendeleo ya Sekta ya Elimu kwa baadhi ya wadau na mbalimbali wa elimu mkoani Singida leo kwenye mkutano ulioandaliwa na TENMET wakishirikiana na ActionAid Tanzania.
Meneja Mradi Wa Elimu ActionAid Tanzania, Karoli Kadeghe akichangia mada wakati wa Mafunzo ya wanachama na viongozi wa Chama cha Walimu na Asasi za Kiraia waliokutana mkoani Singida leo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MAZOEZI CHACHU YA AFYA NA UHUSIANO MZURI KATIKA JAMII

0
0
Kituo cha utangazaji cha EFM redio kimecheza mechi ya kirafiki baina yao na madereva daladala siku ya leo ya tarehe 24/05/2017 katika Kiwanja cha Tanganyika Packers kuanzia saa kumi Jioni, ambapo watangazaji  wa Redio hiyo wamechuana vilivyo na wadau wao wakubwa.

Redio hii ya vijana na jamii kwa ujumla imezidi kutoa kipaumbele kwenye michezo hususani mpira wa miguu kwani imekua ikicheza mechi nyingi za kirafiki kila inapobidi ili kuhakikisha inajenga mahusiano mazuri na jamii inayoizunguka kama wadau wa taasisi mbalimbali ili kukuza vipaji vyao.

Mechi hizi za kirafiki ni kati ya michezo ambayo husaidia jamii kukutana kwa pamoja na kujenga mahusiano mazuri na vile vile husaidia kuhamasisha vijana kufanya mazoezi katika kuunga mkono kampeni ya serikali ya kufanya mazoezi  katika jamii ili kujiepusha na hatari ya kupata magonjwa yasioambukizwa.

RAIS ABBAS: UHURU WA PALESTINA NDIO UFUNGUO WA KUPATIKANA KWA AMANI NA UTULIVU

0
0

Rais Mahmuud Abbas wa Palestina amesema kwamba,Matakwa ya wafungwa wa kipalestina walio katika jela za Israeli ni ya haki na ni wajibu wa Israli kuyatekeleza, vilevile kupatikana kwa uhuru wa taifa lake ndio ufunguo wa amani na utulivu katika ukanda huo wa Mashariki ya Kati na Dunia nzima kwa ujumla.

Rais Abbas ameyasema hayo jana Jumanne Ikulu mjini Beit Lehem, alipokuwa na mkutano wa pamoja na mgeni wake Rais Donald Trump wa Marekani, huku akitilia mkazo dhamira yake ya kushirikiana nae katika kufanikisha mpango wa amani wa kihistoria na Waisraeli,pia kushirikiana nae Rais Trump kama washirika katika suala zima la kupiga vita Ugaidi duniani.

Mheshimiwa Rais Mahmuud Abbas pia ametilia mkazo msimamo wa Palestina unaotegemea utatuzi wa uwepo wa dola mbili chini ya mipaka ya mwaka 1967, ambazo ni dola ya Palestina ikiwa na mji mkuu wake Jerusalemu ya Mashariki na dola ya pili ni Israeli,huku ukipatikana utatuzi wa mwisho kabisa wa masuala yote husika, kwa misingi ya maazimio ya kisheria za kimataifa na makubaliano ya pande mbili za Palestina na Israeli.

Aidha Rais Abbas ametilia mkazo pia kwamba mzozo uliopo sio wa kidini,kwani kuheshimu dini zote na mitume yake ni sehemu ya imani ya taifa la Palestina, bali tatizo lililopo ni uvamizi, ujenzi wa makazi ya walowezi na kutokubali Israeli uwepo wa dola ya Palestina.

Rais Abbas pia amezungumzia usumbufu wanaoupata wafungwa wa kipalestina wanaoendelea na mgomo wa kula uliofikisha siku 37 mfululizo katika jela za Israeli,huku akitilia mkazo ya kwamba madai yao  ni ya kibinaadamu na ya haki,ni wajibu wa Israeli kuyatekeleza.

Kwa upande mwingine,Rais Abbas amelaani vikali shambulio baya  la kigaidi, lililotokea hivi karibuni mjini Manchester Uingereza lililopelekea vifo kadhaa na majeruhi,huku akitoa rambirambi zake za dhati kabisa kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo na familia za wahanga hao.

Rais mahmuud Abbas  na mwenzake Donald Trump,wakiwa katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mjini Beit Lehem.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA KAMATI MAALUM YA KWANZA ILIYOFANYA UCHUNGUZI WA MCHANGA WA MADINI ULIOTAKIWA KUSAFIRISHWA NJE YA NCHI KUTOKA KWENYE MACHIMBO YA MADINI NCHINI

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya uchunguzi wa mchanga wa madini mbalimbali uliotakiwa kusafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Abdulkarim Hamis Mruma Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiingalia Taarifa hiyo ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliotakiwa kusafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo mbalimbali  ya madini nchini mara baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Abdulkarim Hamis Mruma Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakwanza kulia wakishuhudia tukio hilo.
 Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Abdulkarim Hamis Mruma akisoma dondoo za Ripoti aliyoikabidhi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakisikiliza wakati mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Uchunguzi wa Mchanga wa Madini   Profesa Abdulkarim Hamis Mruma alipokuwa akiiwasilisha.
 Baadhi ya Mawaziri  pamoja na Wabunge wakifatilia kwa makini uwasilishwaji wa Ripoti hiyo ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliotakiwa kusafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo mbalimbali  ya madini nchini.
 Viongozi mbalimbali wa Dini na Siasa nao wakifatilia Ripoti hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Kamanda wa kikosi cha Trafiki mkoa wa Dar es salaaam mubashara na "Mshikaki" wa wanafunzi

0
0
 Mkuu wa Kikosi cha  Usalama Barabarani mkoa wa Dar es salaam Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP  Awadhi Haji akimhoji dereva wa bodaboda alipokuwa amewabeba watoto wa shule watatu,huku akijua kufanya hivyo ni kosa. Dereva huyo alikamatwa leo asubuhi maeneo ya Mbezi Makonde jijini Dar es salaam. Watanzania tuungane pamoja tupunguze ajali na kuokoa maisha ya watoto wetu wa shule na raia wengine, kwa kweli....Hii haikubaliki!

Balozi Seif Ali Iddi arejea kutoka Jukwaa la Dunia la Uchumi (World Economy Forum) Jordan

0
0
Na Othman Khamis, OMPR
 AmeMakamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewasili Zanzibar akitokea Mjini Amman, Jordan, alikohudhuria Jukwaa la tisa la Dunia la Uchumi (World Economy Forum) la Siku Tatu lililohudhuriwa na zaidi ya Wajumbe 2,000 kutoka Nchi 58 Duniani. 
Balozi Seif alimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kwenye Jukwaa hilo la Kanda ya Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika lililoshirikisha Viongozi Wakuu wa Nchi, Wafanyabiashara,wamiliki wa Makampunni ya Kimataifa, 
Wawakilishi wa Taasisi za Kiraia, Mashirikia ya Kimataifa, Wana Habari pamoja naVijana wapatao 2,000. 
 Katika Mkutano huo wa Jukwaa la Dunia la Uchumi Balozi Seif na Ujumbe wake alishiriki Washa ya Utalii iliyojikita zaidi katika masuala ya Kujenga Uchumi kwa Mataifa yaMashariki ya Kati na yale ya Kanda ya Afrika ili kuona njia gani zinaweza kutoa fursa za ajira kwa Vijana kwa kutumia Teknolojia ya Kisasa Mkutano huo wa Jukwaa la Uchumi Duniani ulifunguliwa na Kiongozi wa Jordan Mfalme wa Pili Abdullah Bin Al-Hussein kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa King Hussein Bin Talal katika Bahari Nyeusi. 
 Jukwaa la Uchumi la Dunia  limeasisiwa Mwaka 1971 chini ya Muanzilishi na Mwenyekiti wake Profesa Klaus Schwab huko Davos, Switzerland.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na baadhi ya Mawaziri na Watendaji Wakuu wa Serikali mara alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume akitokea Nchini Jordan kushiriki Mkutanowa Jukwaa la Dunia la Uchumi akimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Mauungano wa Tanzanmia Dr. John Pombe Magufuli.
Balozi Seif  Kushoto akibadilishana Mawazo na Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika chumba cha Watu Mashuhuri (VIP) kongwe. Picha na OMPR, ZNZ.

Wakuu wa Mikoa Zanzibar Wahimiza Uimarishaji Zao la Karafuu, Kuimarisha Uchumi

0
0

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dr. Idrisa Muslim Hija amelishauri Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC) na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kuangalia uwezekano wa kuanzisha taasisi maalum itakayoshughulikia tafiti za kitaalamu juu ya zao la karafuu.
Alitoa ushauri huo wakati akizungumza na Wakulima na Wadau wa zao la karafuu katika mkutano maalum ulioandaliwa na Shirika la ZSTC kwa Wakulima na wadau wa zao hilo Mkoa wa Kusini Unguja.
Alisema kutokana na zao la karafuu kuendelea kuwa uti wa mgongo wa uchumi wa nchi na wananchi wake ambapo wananchi wengi wanaonyesha nia na ari ya kulima zao hilo hivyo wanahitaji msaada mkubwa wa kitaalamu juu ya ukulima wa zao hilo.
 Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dr. Idrisa Muslim Hija akimkabidhi kitambulisho cha ukulima wa zao la karafuu Mmoja kati ya wakuliwa wa zao hilo.
Baadhi ya Wakulima wa zao la karafuu Mkoa wa Kusini Unguja wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mkoa huo. Habari kamili BOFYA HAPA

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

0
0
SIMU.TV: Tazama uchambuzi kidogo kutoka studio namba 2 kuhusu sakata la mchanga wenye madini na ripoti iliyokabidhiwa leo kwa mheshimiwa Rais Magufuli; https://youtu.be/pV0_GElRr0s

SIMU.TV: Baadhi ya wachimbaji wadogo mkoani Shinyanga wamepongeza uamuzi wa Rais Magufuli kupiga marufuku usafirishaji nje ya nchi mchanga wenye madini; https://youtu.be/JgaN2fYmIZg

SIMU.TV: Baadhi ya wananchi mkoani Iringa wamesema upotevu wa mapato hususani kwenye sekta ya madini unasababishwa na sheria zilizopitwa na wakati; https://youtu.be/m3XB0Xee66A

SIMU.TV: Baadhi ya wabunge mkoani Dodoma wamepongeza uamuzi wa Rais Magufuli kusimamia kikamilifu upotevu wa rasilimali za watanzania; https://youtu.be/oKIMnEwD90Q

SIMU.TV: Wananchi mkoani Mbeya wameitaka serikali kuangalia upya mikataba ya madini ili kuona kama ina manufaa kwa watanzania; https://youtu.be/lQO4sVP6K1M
SIMU.TV: Benki ya rasilimali nchini TIB kitengo cha biashara imeanza kutoa huduma kwa masaa 24 katika tawi lililoko kwenye bandari ya Dar Es salaam; https://youtu.be/4uYXWOlKbhE

SIMU.TV: Benki ya NMB imeanzisha akaunti maalumu ya biashara ndogo kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wajasiriamali wanaotaka kuanzisha viwanda; https://youtu.be/jKdF4Gj6HxE

SIMU.TV: Mamlaka ya mafunzo na ufundi stadi VETA na SIDO wamekubaliana kushirikiana kutoa mafunzo kwa wajasiriamali ili kuwaongezea uwezo; https://youtu.be/D83LkpFaDZM

SIMU.TV: Chama kikuu cha ushirika wilayani Masasi mkoani Mtwara kimefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 3.3 za wakulima wa Korosho; https://youtu.be/uTLorTble8Q  

SIMU.TV: Waziri wa habari na michezo Dkt Mwakyembe amesema serikali itaendelea kuunga mkono jitihada za kukuza soka la vijana; https://youtu.be/dcph22V3PZY

SIMU.TV: Kampuni ya SportPesa imezindua mashindano rasmi yatakayoshirikisha timu 8 zinazodhaminiwa na kampuni hiyo kutoka Tanzania na Kenya; https://youtu.be/dejhhV-IQNc

Shule ya Lucky Vicent yang’ara Juma la Elimu jijini Arusha

0
0
Na Nteghenjwa Hosseah - Arusha 
Shule ya msingi Lucky Vicent yaibuka na mshindi wa Jumla Kitaaluma kwa kushika nafasi ya kwanza Kimkoa katika maadimisho ya Juma la Elimu yaliyoadhimishwa katika viwanja vya Arusha School jijini hapa. Shule hiyo iliyopata na msiba wa wanafunzi 32, walimu 2 pamoja na dereva kutokana na ajali hivi karibuni imefanya vizur katika mitihani ya darasa la saba iliyofanyika mwaka 2016 katika ngazi ya Mkoa na Wilaya hivyo kujinyakulia Kombe pamoja na Cheti. 
Akipoka zawadi hizo za Ushindi Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bw. Innocent Mushi alisema wanafarijika kupata zawadi hizo ingawa bado simanzi na majonzi yametanda shuleni kwa wanafunzi pamoja na uongozi wa shule hiyo. 
“Tunamshkuru Mungu kwa Shule yetu kufanya vizuri na hizi ni jitihada za walimu kufanya kazi kwa bidii pamoja na wafunzi kuzingatia yale wanayofundishwa na walimu wao hakika zawadi hizi zimetupata faraja katika kipindi hiki kigumu tunachopitia.” Alisema Mwl. Mushi.
 Sehemu ya maonesho wakati wa Juma la Elimu lililofanyika katika viwanja wa Arusha School. 
Mgeni rasmi ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha Ndg. David Mwakiposa(kwanza kushoto) akitembelea maonesho wakati wa Juma la Elimu lililofanyika katika viwanja wa Arusha School. 

Wanafunzi wa shule mbalimbali pamoja na walimu wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa sherehe za Juma la Elimu

Katibu Tawala wa Wilaya Ndg. David Mwakiposa(kushoto) akikabidhi  Kombe la Ushindi kwa kuwa nafasi ya kwanza kimkoa  kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Lucky Vicent Bw. Innocent Mushi.

Katibu Tawala wa Wilaya Ndg. David Mwakiposa(kushoto) akikabidhi cheti cha Ushindi kwa kuwa nafasi ya kwanza kiwilaya  kwa Mwl. Mkuu wa Shule ya Lucky Vicent Bw. Innocent Mushi. 

WAZAZI NA VIONGOZI WATAKAO POKEA PESA KWA WALIOWAPA MIMBA WANAFUNZI WILAYANI KILOLO KUKIONA

0
0
Serikali Wilaya ya Kilolo  mkoani  Iringa  imetangaza  kuwachukulia  hatua kali  wazazi na  viongozi  wa  serikali  za   vijiji na vitongiji aambao  watasaidia kutorosha wanaume  wanaowapa mimba  wanafunzi katika maeneo  yao .

Agizo hilo  limetolewa na mkuu wa  wilaya ya  Kilolo Mhe. Asia Abdallah  wakati wa ziara  yake ya  kutembelea  shule  za msingi na  sekondari  katika kata ya  Ilula wilayani  humo  leo. Amesema kuwa  imekuwa ni kawaida ya  wazazi  kwa kushirikiana na baadhi ya  viongozi wa serikali za  vijiji na vitongoji  kupokea  pesa  kutoka kwa  wanaume  wanaowapa  mimba  wanafunzi  kisha kuwatorosha.

Mkuu  huyo wa  wilaya  alisema kuanzia  sasa mzazi ama kiongozi atakayebainika  kushiriki kupokea  pesa au  kumtorosha mtuhumiwa wa mimba   kwa  wanafunzi atakamatwa na kufikishwa mahakamani pasipo  huruma.

Hivyo alitaka  kila mzazi  na  kila mwananchi kuhakikisha  wanakuwa  sehemu ya  ulinzi wa watoto  hao wa kike na pale inapobainika  kuwa mwanaume ana mahusiano na  wanafunzi kuchukua hatua haraka ya kumfikisha kwenye  vyombo vya  sheria .Aidha  alisema kazi ya  viongozi wa  serikali  za  vitongoji na vijiji ni kuwalinda  watoto hao  wa  kike  dhidi ya  wabakaji kwa  kuwakamata na  kuwafikisha  polisi huku wazazi  hawana sababu ya  kukaa chini ya  watuhumiwa hao  wa mimba kwa lengo la  kumalizana nje ya vyombo  vya  sheria .
Mkuu wa  wilaya ya  Kilolo  mkoa wa Iringa Mhe. Asia  Abdallah akizungumza na wanafunzi wa kidato cha kwanza  shule ya  sekondari  Ilula leo
Walimu wa  shule ya  sekondari Ilula na  wanahabari  wakiwa katika kikao cha mkuu wa wilaya  ya Kilolo  leo
Mkuu wa  wilaya ya  Kilolo  mkoa wa Iringa Mhe. Asia  Abdallah akifurahia jambo na wanafunzi wa kidato cha kwanza  shule ya  sekondari  Ilula leo

TIB CORPORATE BANK TPA BRANCH WORKING 24 HOURS ABIDING TO HIS EXCELLENCY PRESIDENT JPM DIRECTIVES

0
0
The Bank has already commenced to offer 24 hours banking services through the TPA Mini Branch located within the Port Premises, in line with directives of H.E. President John Pombe Magufuli requiring all institutions responsible with Port activities to offer services for 24 hours every day.

The bank facilitates payments of all types of taxes as well as payments for all port charges.

The bank is well prepared and equipped following the recent initiative to embark on TAXBANK , a collection system whereby the tax payers are able to pay for their Taxes via TIB Corporate Bank Network to TRA account with an instant automatic update to TRA system.

Further, TIB Corporate Bank being main banker for Tanzania Port Authority (TPA) means that all port charges paid through the bank are instantly updated to TPA records enabling quick progress on other following processes. TIB Corporate Bank Ltd (TIB- CBL) is a fully fledged commercial bank, 100% owned by the Government of the United Republic of Tanzania.
 The Managing director  Frank Nyabundege (centre) explaining the issue to  journalists. Left  Theresia Soka- Head of Marketing and Corporate Affairs and right is  Mwallu Mwachang’a –Director of Corporate Banking
 Some of Directors of the Bank at the press conference. Seated from right are Fares Muganda-Director of Risk, Karoli Shayo-Director for Operations, Adolphina William- Director of Credit and Mwallu Mwachang’a –Director of Corporate Banking.


The Bank has a branch network in main cities of Tanzania, including three in Dar-Es-Salaam namely Samora , Mlimani City and TPA mini branch and three branches upcountry namely; Arusha, Mwanza, and Mbeya. The branches are strategically located to serve the Coast, Northern, Lake and Southern zones.The bank offers customized products including credit facilities, Trade products, cash management products and treasury products. All these embodied with state of the Art Premier banking lounge to our esteemed clients.

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 24.05.2017

Live: Tuzo zawacehzaji wa ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS MAY 25,2017


JIKO: TIBA YENYE NGUVU ZA AJABU!

0
0
Tiba hii inaitwa JIKO. Kila mwanaume anae itumia, INAMPONYESHA KABISA tatizo la UKOSEFU na UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME. Imethibitishwa na MKEMIA MKUU WA SERIKALI YA TANZANIA

Kufahamu jinsi tiba hii inavyo fanya kazi, bofya link hii hapa chini :


Kwa mahitaji yako ya tiba hii, wasiliana na duka la NEEMA HERBALIST & NUTRITIONAL FOODS CLINIC kwa simu namba 0766 53 83 84.

Tunapatikana UBUNGO jijini DAR ES SALAAM, jirani na SHULE YA MSINGI UBUNGO NATIONAL HOUSING nyuma ya jengo la UBUNGO PLAZA. · Kwa wateja waliopo DAR ES SALAAM, wasio na nafasi ya kufika ofisini kwetu, watapelekewa dawa mahali walipo ( HOME & OFFICE DELIVERY ).

· Kwa wateja waliopo mikoani, watatumiwa dawa kwa njia ya mabasi mbalimbali.

· Kwa wateja waliopo Zanzibar, watatumiwa dawa kwa njia ya usafiri wa boti.

· Kwa wateja wa Mombasa, watatumiwa dawa kwa basi la TAHMEED COACH.

· Kwa wateja wa NAIROBI watatumiwa dawa kwa basi la DAR EXPRESS.

· Na kwa wateja wa UGHAIBUNI ( DIASPORA), watatumiwa dawa kwa njia ya POSTA au DHL.

· Kwa taarifa zaidi kuhusu huduma zetu, tembelea kila siku website yetu www.neemaherbalist.com

AMSHA KIPAJI CHAKO NA MCHEZO WA KIATU KUTOKA KWA KIJANA COBRA WA MBEYA

MICHUZI TV: UPATIKANAJI WA SAMAKI KATIKA ZIWA VICTORIA, JIJINI MWANZA NA MIKOA YA JIRANI

MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI WALETA MABADILIKO CHANYA KWA WALENGWA KISIWANI ZANZIBAR

0
0

ESTOM SANGA-TASAF

Wadau wa maendeleo wanaochangia fedha za utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaotekelezwa na serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF nchini wameonyesha kuridhishwa na kasi ya kupambana na umaskini kupitia mpango huo ulioanza kutekelezwa takribani miaka minne iliyopita.

Wadau hao wa maendeleo kutoka nchi na mashirika kadhaa ya misaada ya kimataifa wameonyesha kuridhishwa na namna walengwa wa Mpango huo wa kunusuru kaya maskini wanavyotumia fedha za ruzuku katika kuanzisha miradi midogo midogo ya kiuchumi inayowaongezea kipato na kuwawezesha kuboresha maisha hususani katika sekta za elimu,afya na kuboresha makazi yao kwa kujenga nyumba za kudumu.

Wadau hao wa maendeleo ambao wako kisiwani Zanzibar kuona namna walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini wanavyonufaika na shughuli za Mpango huo,wametembelea shahia ya Potoa kaskazini Unguja ambako wamekutana na walengwa wa Mpango huo na kujionea shughuli walizozianzisha kwa kutumia fedha ya ruzuku inayotolewa na serikali kupitia TASAF ikiwemo uundaji wa vikundi vya ususi wa vikapu,mikeka na mapambo mbalimbali ya nyumbani .

Aidha wadau hao wa maendeleo wameshuhudia namna walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika shehia ya Potoa walivyoanzisha kitalu cha miche ya matunda na miti chenye jumla ya miche 40,000 chini ya utaratibu wa TASAF wa kuwapa fursa walengwa wake kuibua miradi na kuitekeleza wakati wa kipindi cha hari na kisha kuwalipa ujira ili kuwaongezea kipato.

Walengwa hao wamewaeleza wadau hao wa maendeleo kuwa licha ya kuiuza miche hiyo ,lakini pia huipanda kwenye maeneo yao kama njia mojawapo ya kutunza mazingira na kujiongezea kipato na pia kuongeza ujuzi wa namna ya kuotesha miche na kuitunza kitaalam kinyume na hali ilivyokuwa kabla ya kuanza kwa Mpango huo katika shehia yao.

Mwakilishi wa Shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia, Bwana Muderis Mohamed amesema kasi ya walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini nchini Tanzania ni ya kuvutia na kutia matumaini makubwa ya kupunguza umaskini miongoni mwa walengwa kutokana na mwitiko mzuri wanaouonyesha katika matumizi ya fedha na uanzishaji wa miradi midogo midogo ya kiuchumi kama ufugaji wa bata, kuku na hata mbuzi kwa kutumia fedha za ruzuku zinazotolewa na serikali kupitia TASAF. 
Wadau wa maendeleo wakiangalia baadhi ya vifaa vilivyotengenezwa na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini wa eneo la Potoa kisiwani Zanzibar.

Mmoja wa wadau wa maendeleo hakusita kununua kikapo kutoka kwa walengwa wa Mpango wa Kunusuru kaya maskini baada ya kuvutia na kazi hiyo ya mikono. Kikapo kimoja huuzwa kwa takribani shilingi 15,000 hadi 20,000.
 Mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini katika shehia ya Potoa  kisiwani Zanzibar bi. Munono Mohamed (wa pii kushoto) akizungumza na baadhi ya wadau wa maendeleo juu ya hatua yake ya kujenga nyumba kwa kutumia ruzuku ya fedha kutoka TASAF. Picha ya chini ni nyumba anayoendelea kuijenga Bi. Munono mama wa watoto  SABA.Aliyeshika daftari ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bwana Ladislaus Mwamanga. 
 Wadau wa Maendeleo wa TASAF, wakipata maelezo kutoka kwa mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika eneo la Potoa  Bi. Panga Makame juu ya mradi wa kufuga bata aliouanzisha baada ya kupata ya kupata ruzuku. Bata mmoja huuzwa kwa takribani shilingi elfu 30.

 Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini katika shehia ya Potoa wameanzisha kitalu cha miche ya matunda na miti kupitia utaratibu wa ajira ya muda ambao ni sehemu ya Mpango huo wenye lengo la kuongezea kipato hususani wakati wa kipindi cha hari.

HABARI ZAIDI SOMA HAPA

TADB YATOA ‘SAPOTI’ KAMPENI YA KITAIFA YA UNYWAJI WA MAZIWA

0
0
Katika kuhamasisha Watanzania wengi wanaongeza hamasa ya unywaji maziwa, Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeunga mkono juhudi za Serikali na Bodi ya Maziwa (TDB) nchini kwa kutoa vifaa vitakavyotumika katika Kampeni ya Kitaifa ya Unywaji Maziwa inayotarajia kufanyika Kitaifa mkoani Kagera kuanzia Mei 28 – Juni 1 mwaka huu.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo yaliyofanyika katika Ofisi za TADB jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga amesema kuwa Benki ya Kilimo imeunga mkono Kampeni hiyo kwa kutambua umuhimu wa kuchagiza unywaji wa maziwa nchini kama inavyopendekezwa na Shirika la Afya Duniani.

“Kwa kutambua umuhimu wa Kampeni hii, TADB kwa kushirikiana na TDB na wadau wengi tumeazimia kuhamasisha unywaji wa maziwa ili kufikia viwango vya kimataifa ya unywaji wa maziwa ambao unakadiriwa kufikia walau lita 200 kwa mwaka kutoka 47 za sasa,” alisema.

Aliongeza kwa kutambua umuhimu wa ufugaji wa ng’ombe wa maziwa TADB ilijumuisha mnyororo wa thamani wa Ufugaji wa ng’ombe wa nyama na maziwa kuwa ni miongoni mwa minyororo ya mwanzo inayopatiwa mikopo kwa ajili ya uongezaji wa thamani wa mifugo nchini.

Akasisitiza kuwa Benki yake imejipanga kuendeleza uongezaji wa thamani wa Ufugaji wa Ng’ombe wa Nyama na Maziwa ili kuchagiza juhudi mbalimbali za Serikali katika ustawi wa tasnia ya maziwa nchini.

“Benki inatoa mikopo na kusaidia uwekezaji kwa ajili ya ujenzi, ununuzi wa mitambo na ufungaji wa mitambo ya kuhudumia ng’ombe ikiwemo majosho na mabwawa ya kunyweshea na pamoja na usindikaji wa maziwa kwa ajili ya kuongeza thamani maziwa,” alisema Bw. Assenga.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (kushoto) akiwakaribisha maafisa kutoka Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) walipomtembelea Ofisini kwake kujadiliana juu ya Kampeni ya Kitaifa ya Unywaji Maziwa inayotarajia kufanyika Kitaifa mkoani Kagera kuanzia Mei 28 – Juni 1 mwaka huu. Katikati ni Kaimu Msajili wa Bodi, Dkt. Mayasa Simba na Afisa Habari na Mawasiliano wa TDB, Queenter Mawinda (kulia).
Menejimenti ya TADB ikifuatilia majadiliano hayo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (kushoto) na Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa, Dkt. Mayasa Simba (kulia) kuhusu nafasi ya wadau katika Kampeni ya Kitaifa ya Unywaji Maziwa inayotarajia kufanyika Kitaifa mkoani Kagera kuanzia Mei 28 – Juni 1 mwaka huu.

Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images